Sehemu Ya Pili (2)
Hatimae matokeo ya darasa la saba yakatoka miongoni mwa wanafunzi waliofauru Skola alikuwa mmoja wao Meyan akamtafutia shule ya kulipia nakumpeleka akaanza masomo apo.
Siku aliyoanza shule alikuwa kivutio kwa wengi kutokana na uzuri aliokuwa nao Skola wengi walimpenda.
Hakuwa na maringo wala majivuno ilo likamuongezea sifa nzuri kwa watu.
Mwaka wa kwanza ukaisha hatimae akaingia mwaka wa mwengine akiwa kidato cha pili.
Shuleni kuna mwanafunzi wa kiume alihamia alikuwa handsome sana wasichana wengi wakavutiwa nae, alikuwa serious sana kiasi kwamba hakuzoeleka muda wote anakaa pekeyake tu.
Mitihani ikitoka anashika namba moja kilasiku alikuwa na akili za ajabu adi walimu walimshangaa zaidi hakupenda kumuangalia mtu usoni alikuwa anainama chini ata akiwa darasani.
Siku moja Skola aliamua kumfata nakumsalimia kwa mara ya kwanza macho yao yaligongana nakutoa mn'garo wa ajabu.
"Skola wewe ni mwenzangu nipo hapa kwaajiri yako"
"Kivipi mbona sikuelewi"
"Meyan amekamatwa kafungwa chumba cha giza ujinini wewe ndie wakumuokoa mamayako"
"Mbona sikuelewi lakini wewe nani kwani?"
"Naitwa shabir ni mtoto wa Mfalme wa bahari ya dhahabu"
Aliongea nautoweka apo apo akamuacha Skola akiwa na mawazo sana asielewe aliyoambiwa.
Muda wakutoka shule ulifika akarudi nyumbani mnyonge sana nakujifungia ndani.
Usiku ulipofika aliota ndoto ya ajabu sana
Usiku ulipofika aliota ndoto ya ajabu sana, inayomuhusu Meyan yule mwanamke mzuri amefungiwa chumba cha giza kilichokuwa na joto sana kibaya zaidi hakuna aliempelekea ata maji ya kunywa amefungwa minyororo mwili mzima nakulazwa chini kwenye siafu wengi waliokuwa wakimtembea.
Ghafla Skola akashtuka nakuanza kuhema sana.
"Inamaana gani hii ndoto kwanini amefungiwa anateswa?"
Alijiuliza Skola lakini hakupata jibu, alipotizama ile pete ilikuwa ingara sana usiku huo ilikuwa saa nane usiku. Alizidi kushangaa ile pete, Mara akasikia sauti kubwa ikisema alistaajabu anaeongea hamuoni.
"Skolaaa wewe ni damu yetu unaitajika nyumbani uku duniani sio kwenu na lazima ufanye mauaji kumuokoa mamayako"
Ilisema iyo sauti mwisho ikapotea.
"Mimi mwenzao kivipi mbona siwaelewi ata Shabir alisema ivyo?"
Alikosa usingizi akabaki anamawazo sana akifikiria anayoambiwa.
Hatimae kulikucha akajiandaa nakuelekea shuleni, hakutaka ata kumsemesha Shabir sababu hakumuelewa.
Muda wakuondoka shule ilipofika Shabir alimfata Skola
"Unasiku tano tu zakuishi duniani! Unahitajika ujinini"
Alimwambia akiwa serious, pamoja nakujaaliwa sura yenye mvuto Shabir hakuwa mtu wakucheka ovyo mara zote yule makini zaidi akiongea akutizami usoni anaangalia chini.
Ilo likamtisha Skola aende ujinini kufanyaje wakati yeye ni binadamu.
"Shabir kwani wewe ni jini?"
"Ata wewe pia ni jini"
Alimwambia nakumfanya Skola atetemeke nakuogopa sana,
"Ukweli wote kuhusu wewe utaujua ukifika nyumbani, usisahau umepewa siku tano tu zakukaa duniani ukiwa tayari niambie twende nipo hapa kwaajiri yako"
Alisema Shabir nakuondoka.
Skola hakuelewa kabisa alijiisi anapagawa akili alijiuliza itawezekana vipi awe jini hakupata jibu.
Alirudi nyumbani mnyonge sana akiwa hana furaha.
"Ivi mama kwani mimi sio mtoto wenu au?"
Alimuuliza swali mamayake ambae alishangaa kwanini ameuliza ivyo.
"Kwasababu nimesikia Meyan ndo mamayangu sasa sielewi"
Alizidi kuongea uku akihudhunika.
"Skola mwanangu usijali ngoja babayako arudi jioni"
Alisema uyo mama na Skola akamuelewa aliingia chumbani kwake.
Bado mawazo hayakumuisha, alifikiria mengi sana.
Jioni ilifika uyo baba akarudi mkewe akamueleza kuhusu Skola
"Haina jinsi tumueleze ukweli sababu ameshakuwa mkubwa huyu"
Mwanaume alisema ambae ni Baba Samuel.
Baada ya apo Skola akaitwa nakukaa chini kuwasikiliza kwa makini sababu alitamani sana kujua ukweli wake.
"Skola mwanangu nataka nikueleze ukweli ujue. Miaka kumi na tano iliyopita kipindi iko tunaishi kwenye nyumba yetu ile ya mwanzo, siku moja Alfajiri nikiwa natoka nielekee kazini nje ya nyumba mlangoni nilipofungua nikaona mtoto mzuri amelala nilichokifanya nikumuita mkewangu kumuonyesha ambapo alimbeba nakumuingiza ndani, tulichoshauriana akatoe taharifa polisi.
Mimi nikaelekea kazini na mkewangu akajiandaa nakuelekea sitaki shari kituoni ambapo alijielezea lakini hao polisi walimwambia amchukue uyo mtoto nakumlea, sababu tulikuwa na mtoto wakiume Samuel pekeyako tukaona ni heri kwetu kupata mtoto wa kike ambae tulimpa jina Skola tukamlea kwa mapenzi yote mimi nikiwa Baba na mkewangu akiwa mama adi leo hii Skola wewe umekuwa mkubwa unajua baya nazuri lipi huo ndo ukweli sisi ni wazazi wako walezi, naisi Meyan ni mamayako kabisa sababu mnafanana sana"
Alimaliza kusema uyo mwanaume Skola hakuweza kujizuia alikuwa analia sana.
"Inauma sana mimi najua nyinyi ndo wazazi wangu"
Alisema akilia Skola akifikilia anakazi kubwa mbele yake alijikuta anaumia zaidi, ila hakutaka kusema ukweli yeye si binadamu akaamua kunyamaza tu.
Baada ya apo alikubali ukweli lakini aliwashukuru wamemlea kama mtoto wao bila kumtenga.
*****
Siku zilizidi kusonga kilasiku akienda shule anakutana na Shabir ambae anamkumbusha kuhusu iyo safari ya ujinini, Skola alikubali alitaka ajue ukweli kuhusu wazazi wake na ilikuwaje adi akatupwa nyumbani kwa Mama Samuel.
Siku ya nne ikafika sasa ambayo kesho yake ndio safari,
"Nataka niwaage wazazi wangu wasipate hofu kunitafuta"
Skola alimwambia Shabir ambae alikubali
"Utawaagaje sasa unaenda wapi?"
"Usijal kwailo"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema akarudi nyumbani nakuwaita wazazi wake
"Nataka kwenda kumuokoa mamayangu amefungiwa chumba cha mateso katumwa mtu aje kunichukua"
Alisema kwa majonzi Skola
"Pole sana mwanangu mungu atasaidia usitusahau lakini ukiwa uko uje ata kutusalimia wazazi wako"
"Hamna tatizo nawapenda sana siwezi kuwatenga"
Alisema akasogea nakuwakumbatia hakuongea kuhusu mambo yakijini alijua atawatisha, siku iyo walikula pamoja wakifurahi sana adi usiku ulipofika kila mtu akaingia kulala.
Saa nane usiku alisikia sauti ikimuita ahamke muda umefika wakuondoka alipofumbua macho alimuona Shabir
"Wewe umeingiaje humu?"
"Skola twende muda ndio huu"
"Lakini Shabir....
Kabla ajaendelea alishikwa mkono
"Fumba macho"
Sauti kali ilimuamuru, akajikuta anakubali nakufumba, baada ya muda mfupi wakatokea baharini kwenye daraja la salenda, bado alikuwa kashikwa mkono na Shabir ambae alitembea halaka halaka kuifata bahari adi walipofika akakanyaga maji nakuzidi kutembea, uoga ulimshika Skola akaisi anazama nakufa akajikuta anamkumbatia Shabir ambae wala hakuonyesha kuogopa kitu alizidi kusonga mbele adi maji yakawafika ya shingo.
"Tunakufa Shabir"
"Haufi Shaymaa naomba fumba macho"
Jina aliloita lilimfanya Skola ashangae kwanini kamuita Shaymaa alitaka kumuuliza lakini alichelewa akafumba macho.
"Tumefika fumbua"
Alisema Shabir, Skola hakuamini alipofumbua macho yake mji mzuri wenye kuvutia ambao ulijaa dhahabu tupu chini alibaki akishangaa nakustaajabu dunia aliyokuwepo
"Waooo kuzuri"
Alisema uoga ulimtoka akabaki anatabasamu.
Shabir alimshika mkono wakaanza kutembea njiani walipishana na watu warefu sana wanaotisha nakumuogopesha Skola lakini Shabir alimtoa hofu mwisho wakafika kwenye jumba kubwa kama hekaru lililonakshiwa dhahabu tupu, walinzi walifungua mlango wakaingia ndani ambapo walifika adi kwenye chumba kimoja kulikuwa na mwanaume na mwanamke ambao walikuwa watu wazima kidogo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shabir alisogea akasujudu Skola nayeye alifanya ivyo ni kama salamu kwao. Baada ya apo walikaa chini na maongezi yakaanza.
"Baba na mama nimefanikisha kazi nilipoifata duniani huyu ni binti wa Malkia Meyan"
Alisema Shabir
"Ni mrembo kama mamayake natamani awe mkwe wangu huyu"
Alijibu uyo mwanamke mwenye asili yakiarabu mweupe uku nywele zake ndefu ameziachia nakuburuzika chini uku zikiwaka waka nakun'gara.
"Mama tunakazi nzito yakufanya sio kuleta mapenzi"
Alijibu Shabir,
"Sawa fanyeni iyo kazi ikiisha ndoa ipite"
Alijibu uyo mwanamke Malkia samiray mumewe akaingilia Mfalme Jamal
"Uyu binti inatakiwa apewe nguvu kwanza awe kama sisi atoke kwenye umbo la binadamu"
Alisema na wote wakakubaliana akaingizwa chumba kingine akalazwa kitandani na hao watatu wakaungana kumwekea nguvu mwilini mwake waganga na wachawi wakubwa zaidi ya kumi waliitwa nao wakaungana kumuongeza nguvu Skola baada ya masaa sita Alishtuka
"Ha hahhhaa Shaymaaaaaaa"
Walishangilia kwa muonekano aliokuwa nao alibadirika nakuwa jini kabisa umbo la kibinadamu lilimtoka macho yake yalikuwa yanawaka kama ya paka makali sana uku mwili wake ukiwa mkubwa wenye nguvu sana
Waliandaa sherehe yakumkaribisha ujinini ilipoisha tu wakaanza safari yakuelekea bahari ya sahamu ambapo ni kwenye ufalme wa Zayuke ambapo anaishi Meyan
Zayuke ni Malkia wa kwanza kuimiliki sahamu, Baba yake Mfalme Abrahamu Al Amri alikuwa ni Mfalme wa sita kuimiliki sahamu!
Alibahatika kupata mtoto mmoja tu wa kike Zayuke alimua kumkabidhi huo Ufalme nakuimiliki Sahamu baada ya siku chache alifariki.
Zayuke alikuwa mwanamke jasiri mwenye nguvu zaidi aliwaongoza vizuri akifata mila zao bila kumuonea yeyote. Wengi walimpenda sababu hakuwa mwanamke wakumuingia ovyo aliwatetea sana taifa lake dhibi ya wabaya au maadui.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliolewa na mwanaume aitwae Ashraf saidi ambapo alibahatika kuzaa watoto wawili wa kwanza Zakhaki na wapili Meyan ambae alimpa hasira alipovunja miiko yao nakwenda kuzaa na binadamu aliahibisha sana ufalme wao, walipogundua walimchukua nakumfungia chumba cha giza akipata mateso adi kufa kwake.
****
Hatimae Shabir na Shaymaa walifika kwenye ufalme wa Zayuke ambapo waliruhusiwa kuingia ndani kuonana nae.
Walionyeshwa chumba nakukaa apo wakimngoja Malkia aje sababu alikuwa na mkutano na wazee wenye hekima wanaopatikana kwenye miliki iyo, Baada ya muda mfupi alitoka Malkia Zayuke wakamsogelea nakusujudu mbele yake
"Uishi miaka mingi ewe Malkia mtukufu"
Waliongea kwa pamoja.
Baada ya apo alikaa kwenye kiti chake, alikuwa mwanamke mzuri sana aliefanana na Meyan nywele zake ndefu zinazowaka nakumfanya an'gare sana alikuwa na macho makubwa kiasi yenye mvuto uku lips zake nene zikiwa kivutio kingine uyo ni Malkia Zayuke ni mrembo haswa utazani binti wa miaka ishirini kumbe ni mama mtu mzima mwenye miaka zaidi ya mia tatu, majini wanaishi umri mrefu sana tofauti na binadamu.
"Shaymaa karibu kwenye ufalme wa zayuke"
Alimwambia akitabasamu nakuongezeka urembo wake.
"Najua kuna mengi unitamani ujue kuhusu wewe na leo nitakueleza yote ilivyokuwa.
Aliongea Malkia Zayuke nakuanza kumuelezea kuhusu Meyan
"Nina watoto wawili wa kiume ambae ameoa kwenye ufalme wa dhahabu ambapo ametokea uyu Shabir naisi Zakhaki ndie aliemtuma Shabir akufuate duniani nakukueleza mamayako amefungwa chumba cha giza unahitaji kumsaidia.
Ni kweli msaada wa Meyan upo mikononi mwako, Meyan amenikosea sana! Kaukosea ufalme wa Zayuke anaanzaje kumpenda binaadamu zaidi akapata mimba nakuzaa mtoto akakuacha duniani alifanya kitendo kibaya sana ni bora angekuzaa nakukuleta uku kwanza.
Nakumbuka Meyan alitumwa vizazi duniani siku ambayo alitoka uku alipofika tu daraja la salenda alikutana na mwanaume mmoja mnyonge sana ambae alionekana anataka kujiua Meyan akaamua kumsaidia ambapo yule mwanaume alisema anamaisha magumu sana ndio maana alitaka afe, baada ya apo Meyan akaamua kumsaidia nakumpa utajiri.
Alisahau kazi iliyompeleka duniani akajikuta anampenda yule mwanaume nakushiriki nae mapenzi adi akapata ujauzito siku aliyojifungua alikuchukua nakwenda kukuacha nje ya nyumba ya baba na mama Samuel.
Baada ya apo akaanza kazi yakukusanya vizazi nakurudi uku.
Tukafanya sherehe kubwa kufurahia amekamilisha kazi yake.
Bahati nzuri alipata mwanaume alietaka kumuoa aitwae Jamaly ambae alifanikisha mipango yote ndoa ikapita na uyu mumewe ndie alijua kama Meyan amezaa na binadamu baada yakushiriki nae tendo aligundua mkewe anadalili za uzazi ndipo alipoamua kumbana mwanzo aligoma ila mwisho akaongea ukweli amezaa na binadamu ni jambo la aibu sana amefanya astahili kusamehewa uyu adhabu yake ni kifo tu.
Alimaliza kusema kwa uchungu Malkia Zayuke atamacho yake yalibadirika nakuwa mekundu kwa hasira alizonazo.
"Nahitaji kumsaidia Meyan atoke kifungoni"
Alisema Shaymaa Malkia akacheka sana nakumuangalia kwa huruma
"Utaweza masharti?"
Alimuuliza
"Ndio ninaweza"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sharti la kwanza ubadirishwe na kuwa jini upo tayari?"
"Ndio nipo tayari"
"Sharti la pili unapewa mwaka mmoja wakuishi duniani uku ukiwa muuaji wa kike upo tayari?
"Ndio nipo tayari"
"Sawa sharti la mwisho ambalo jepesi sana ni damu zinahitajika nyingi tutakazo jaza mapipa yetu sabini yatakayofanyika sadaka kwa mizimu ikubali kumfutia adhabu Meyan"
"Sawa nipo tayari kwa yote"
Alikubali Shaymaa nakumfanya Malkia acheke kwa furaha baada ya apo akachukuliwa nakuingizwa chumba cha maombi wakakutana majini wale wenye nguvu nyingi pamoja na wazee wachawi wenye uwezo wakamlaza kitandani Shaymaa nakuanza maombi yao yakumtoa ubinadamu mwilini awe jini kamili.
Kazi ilichukua masaa zaidi ya sita hatimae ikakamilika.
Baada ya apo walimuacha alale kidogo.
Baada ya nusu saa Shaymaa aliamka alitisha sana hao waliomfanyia maombi wote walikimbia kwa kumuogopa alikuwa kiumbe wa ajabu mwenye nguvu sana ambapo upepo ulivuma nakufanya vitu vigongane ndani ovyo alitisha ata Malkia aliogopa kumsogelea, Shabir akajitoa muhanga nakumfuata kuongea nae
"Shaymaa nakuomba punguza hasira na uwe kwenye umbo la kawaida"
Alimuomba akamuelewa nakurejea kuwa binti mrembo ajabu ambae aliutetemesha moyo wa Shabir nakujikuta anampenda sana
"Shabir najua kilicho moyoni mwako acha nimalize kazi ya mama nitakuwa wako"
Alimwambia, baada ya apo akaondoka kuelekea kule alipowekwa mamayake chumba cha mateso nje alimkuta mwanamke aitwae Nana ni mwembamba sana alafu anakichwa kikubwa tofauti na majini wengi warembo uyu Nana alikuwa ni m'baya sana alitisha na macho yake makubwa.
"Nataka kuonana na Meyan"
Alisema Shaymaa
"Haiwezekani haruhusiwi kutoka wala kuonekana"
"Mimi ndio nataka sasa kumuona"
Alijibu akitabasamu nakuongezeka uzuri wake, Nana aligoma kumruhusu kuingia Shaymaa alimwangalia kwa dharau apo apo akapotea hakujua alipoenda ila alisikia sauti ndani ikiongea ikabidi afungue mlango alipoingia hakuamini kumuona Shaymaa ndani amemkumbatia Meyan
"Ninakufa mwanangu"
Alisema kwa hudhuni
"Haufi mama nakusaidia niamini"
Alimjibu na apo apo akamtoa nakumfungua kilakitu akambeba adi kwa Malkia Zayuke
"Ewe mtukufu Malkia nakuomba mamayangu afungiwe chumbani kwake na sio kule kwenye mateso naahidi ndani ya siku tatu kilakitu kitatimia"
Alisema Shaymaa
"Na usipotimiza kichwa cha mamayako halali yangu"
Malkia alisema
Baada ya apo Meyan akaingizwa chumbani kwake na Shaymaa akamfuata Shabir kumuaga anarudi duniani kuchukua damu.
"Nahitaji kukusaidia"
Shabir alimwambia
"Hapana usijal anza maandalizi ya ndoa acha niende baada ya siku tatu nakamilisha kilakitu"
Alijiamini Shaymaa akaanza safari yakurudi duniani sasa.
Alitembea pembezoni mwa bahari adi alipotoka kabisa nakusimama barabarani kwenye daraja la Salenda, ilikuwa ni usiku saa nane kulikuwa na gari moja linakuja uku ndani kukiwa na wanaume wanne pamoja na wanawake zao wanne, walikuwa wamelewa sana sababu walitoka club usiku ule ilikuwa wikiendi, walipofika maeneo ya daraja la salenda, samir ambae alikuwa ni dereva anaendesha lile gari alishangaa kuona mtu kasimama katikati ya barabara alipojaribu kumkwepa alishindwa akajikuta anamgonga na gari lao kupinduka ajari ikatokea, wote walifariki apo apo kwakuvuja damu nyingi sana.
Kazi ya Shymaa ilianza alitoka apo nakutembea pembezoni mwa barabara taratibu kama asie na halaka.
"Habari yako dada?"
"Safi"
Akiwa anatembea aliona gari limemsogelea nakupunguza mwendo mwanaume mmoja akamsalimia
"Samahani unaelekea wapi?"
Aliuliza uyo mwanaume ambae alimuangalia kwa matamanio sana Shaymaa
"Naenda nyumbani"
"Oh sawa panda nikupeleke"
Akujifikilia wala nini alipanda na safari ikaanza mwendo wa nusu saa tu Shaymaa alibadirika nakumkaba yule mwanaume ambae alipoteza maisha apo apo nayeye akapotea.
Asubuhi kulikucha ambapo ile ajari iliyotokea daraja la salenda iliwahudhunisha watu sababu hakuna aliepona, maiti zikachukuliwa nakupelekwa mochwari uku ndugu wakitafuta nakuonyeshwa miili ya vijana wao ilikuwa huruma kwa wakina mama walilia sana watoto wao wamefariki.
Yule mwanaume alieuliwa kwenye gari alikuja kujulikana akapelekwa mochwari mkewe alilia sana kumpoteza mume wake kwani alikuwa njiani anasafiri kikazi ila huruma yake yakuwapa watu lift usiku imemponza nakupelekea mauti yake.
Shaymaa alikuwa stand ya mkoa Ubungo akiangalia magari yapi yamejaa sana ili asababishe ajari akaona gari moja la Arusha akalipanda ilo bila mtu kujua safari ikaanza walipotoka apo nakuelekea mataa ajari ya ajabu ikatokea ambapo gari lilitoka nje ya barabara nakuwasomba watembea kwa miguu watu wasiopungua mia moja walifariki apo chanzo cha ajari hakikufahamika wengi walioshuhudia wakausisha na mambo ya giza.
"Sio bure Freemasons hawa wanatoa sadaka"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema kijana mmoja muda huo Shaymaa ameshapotea kimaajabu.
"Kweli ata mimi naisi huu ushirikina maana gari tangu linatoka mule ndani naliona iweje lifike apa inatokea ajari isiyokuwa ata na chanzo shetani yupo kazini jamani"
Aliongea jamaa mwengine ilikuwa hudhuni vilio vilitawala ajari ya maajabu ata Trafki alipoitwa kupima hakuona chanzo cha ajari akabaki anashangaa maiti zote zikabebwa adi dereva alifariki wakaingizwa kwenye gari nakupelekwa hospital muhimbili.
Ni msiba uliogusa hisia za wengi sana, ndugu walifika nakuchukua miili ya watu zao nakwenda kuzika, ikiwa ajari hii bado watu hawajasahau ghafla inatokea nyingine ya treni inayoua watu zaidi ya mia tano ni treni mbili ziligongana uso kwa uso nakupinduka kuangukia chini kabisa, ilikuwa zaidi ya maajabu wengi walishangaa itakuwaje treni itoke kwenye barabara yake nakupinduka hakuna aliepata jibu.
"Dunia imefika mwisho tunaondoshwa taratibu"
Alisema mwanamke mmoja akilia.
Dar es salaam ilinuka damu kilakona, vilio, simanzi, majonzi vilitawala Taifa zima hakuna aliekuwa na furaha hudhuni iliwajaa watu wengi walioguswa na misiba iyo.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment