Search This Blog

CHOZI LA YATIMA - 5

 

    Simulizi : Chozi La Yatima

    Sehemu Ya Tano (5)





    Modesta hakuridhishwa kabisa kwa kitendo cha kuchukiwa na Safina, ikabidi afunge safari tena na kwenda kuwasalimia.

    Siku hiyo alifunguliwa na Safina mwenyewe, Safina alipomfungulia Modesta mlango tu, Safina akageuka na kutaka kukimbilia chumbani ila Modesta akawahi kumshika mkono Safina.

    MODESTA: Tafadhari Safina usinifanyie hivyo.

    SAFINA: Sioni sababu ya kuongea na wewe.

    MODESTA: Safina, niangalie Tafadhari.

    SAFINA: Ili iweje?

    MODESTA: Wee niangalie tu.

    SAFINA: (Akageuka na kumtazama), haya nishakuangalia.

    MODESTA: Je! Kuna lolote baya ambalo mimi nimewahi kukutenda?

    SAFINA: Hapana, ila ndugu zako wamenitenda vibaya.

    MODESTA: Je! Ni halali kumuhukumu mtu kwa kosa la ndugu zake?

    SAFINA: Si halali ila inategemea.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MODESTA: Safina, hakuna baya nililowahi kukutendea. Na si haki kunihukumu kwa kosa la ndugu zangu, nitazame mimi kama Modesta na si mtu mwingine kama unavyofikiria. Sina ubaya wowote na wewe Safina, tafadhari usinihukumu kwa kosa nisilotenda.

    Safina akafikiria sana maneno aliyoambiwa na Modesta kwani yalimwingia vilivyo kwenye akili yake. Ikabidi amkumbatie kwa kumuonyesha kuwa hana kinyongo nae tena.

    Na hapo akamkaribisha ndani vizuri na mazungumzo ya hapa na pale yakaendelea.

    SAFINA: Ni hasira tu ndio zinafanya niwe vile.

    MODESTA: Naelewa Safina, ila yote yataisha.

    SAFINA: Yataishaje?

    MODESTA: Cha muhimu hapa ifunguliwe kesi tu hata mimi nitakuwa shahidi.

    SAFINA: Kesi hiyo itahusu nini sasa?

    MODESTA: Ihusu kukunyang'anya mali na kukufukuza kwenu.

    Safina aliongea mengi sana na Modesta, kwakweli Modesta alipata faraja ya kusamehewa na Safina.



    Blenda na prof. Mike wakapanga safari ya kuja nchini.

    Siku ya safari wakiwa uwanja wa ndege, wakashangaa kuwakuta watu wawili nao wakiwa pale kuwangoja.



    Blenda na Prof. Mike wakapanga safari ya kuja nchini.

    Siku ya safari wakiwa uwanja wa ndege wakashangaa kuwaona watu wawili pale wakiwangoja.

    Wakawashangaa sana kwani hawakupanga nao safari, watu hao ni Joseph na Chuck.

    Watu hawa wakawaambia kuwa wameona vyema kuambatana nao, kwani bado wanahitaji kuwa nchini na pia wanahitaji kumuona tena Safina.

    Wazo kubwa la prof. Mike ni kumuona Safina tu, mtoto wa rafiki yake kipenzi mr. Sam. Kwanza hakuamini kabisa alichoambiwa na Blenda, alichotaka Mike ni kuyasikia kwa Safina mwenyewe.

    Muda ulipofika wakaingia kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda kumuona Safina.



    Ilikuwa siku ya Jumatatu ambapo Suzan aliwashangaa Musa na Safina kutokwenda shule.

    SUZAN: Mbona leo hamjaenda shule?

    MUSA: Tumefunga shule.

    SUZAN: Kumbe mmefunga! Nilikuwa sijui.

    SAFINA: Mmh! Mamdogo umesahau kuwa huu ni mwezi wa sita!!

    SUZAN: Mwenzenu nimesoma kipindi cha mkoloni halali yangu kusahau, kipindi kile cha muwa uliozamisha meli.

    Akawafanya Safina na Musa wacheke.

    SAFINA: Mamdogo nawe una vituko.

    SUZAN: Naomba niwatume basi.

    MUSA: Tutume tu mama.

    SUZAN: Naomba mniendee kwa Pendo kuna makaratasi atawapa mniletee.

    MUSA: Sawa hakuna tatizo.

    Basi Musa na Safina wakajiandaa na kwenda nyumbani kwa Pendo.



    Frank akiwa kwenye ofisi yake akashangaa kufikiwa na ugeni, nao wakajitambulisha kwake. Ikabidi Frank aanze nao safari ya kuwapeleka nyumbani kwake.

    Kitendo cha Safina kuwaelekeza wakina Blenda ofisi ya kamanda Frank ndio kilichowasaidia kwenda moja kwa moja na kumpata mahali hapo.

    Walipofika nyumbani kwa Frank, Suzan aliona sura moja ya tofauti nayo ilikuwa ya prof. Mike kwani Blend, Chuck na Joseph alishawaona kwa madam Lucy. Akawakaribisha sana nyumbani hapo.

    Wakaongea mengi ila walisononeka baada ya kuambiwa kuwa Safina hayupo, ila wakapewa uhakika wa kurudi muda sio mrefu.

    Frank akamuuliza Mike maswali ya hapa na pale na kupata mwangaza wa haki ya Safina kwani prof. Mike alimuelezea kuwa Sam alikuwa na wakili wake hapo nchini, wakaongea mengi na kushauriana mambo mengi.

    Wakina Blenda wakaamua kuaga ili waweze kwenda kumtembelea madam Lucy, kwahiyo wakaondoka na kumuacha Mike mahali hapo.



    SAFINA: Mamdogo Pendo sisi tunakwenda.

    PENDO: Loh jamani nishawazoea, kaeni basi kidogo hadi jioni.

    MUSA: Tulimuaga mama kuwa hatuta chelewa sana.

    PENDO: Basi sawa, mwambieni nitakuja kesho kutwa.

    Safina na Musa wakaanza safari ya kurudi, walipofika njiani wakakutana na mtoto wa jirani yao.

    MTOTO: Kaka Musa, nyumbani kwenu kuna mzungu kaja.

    SAFINA: Mzungu?

    MTOTO: Ndio mzungu nimemuona yupo nyumbani kwenu.

    SAFINA: Mmh!! Atakuwa nani jamani?

    MUSA: Twende tukajionee hukohuko Safina.

    Basi Safina na Musa wakaanza kutembea haraka ili wakamshuhudie huyo mzungu.

    Walipoingia ndani Safina hakuamini macho yake kwa alichokiona.

    SAFINA: Uncle Mike!!

    Basi Mike akainuka na kumkumbatia Safina kwa furaha.

    MIKE: How are you Safina?

    SAFINA: I am fine, and how are you doing?

    MIKE: Fine and very happy to see you again.

    SAFINA: I'm very happy too my uncle.

    Basi Mike na Safina wakaongea mengi. Safina akamueleza kila kitu kilichotokea tangu siku ambayo yeye na mama yake walipoingia hapo nchini, akamueleza na misukosuko yote aliyopitia, kwakweli Mike alimuonea huruma na kumsikitikia sana Safina.

    Wakapanga mikakati ya kuweza kumpata wakili wa Sam ili waweze kufungua kesi ya dhuluma na kudai haki vizuri.

    Prof. Mike akawapatia jina la wakili huyo ili waweze kwenda kumuulizia kwenye ofisi za mawakili.



    Pendo kama alivyowaambia wakina Musa, na siku hiyo akaenda kumtembelea Suzan.

    Kufika wakaongea mengi na Suzan akamweleza Pendo kila kitu kilichojiri kuhusu Safina.

    PENDO: Umesema wakili mnayemtafuta anaitwa nani?

    SUZAN: Prof. Mwambe.

    PENDO: Kama ndio huyo basi mimi napajua hadi kwake.

    SUZAN: Basi itakuwa vizuri kutupeleka.

    Suzan akampa habari hiyo Frank na akafurahi sana.

    Kesho yake wakafunga safari hadi nyumbani kwa prof. Mwambe.

    Wakamkuta nae ndio siku hiyo amerudi nchini kwani alikuwa nchi jirani. Kwakweli Mwambe alishangaa kuuona ugeni huo wa gafla.

    Baada ya salamu wakamueleza kilichowapeleka pale.

    MWAMBE: Kumbe mr. Sam alikufa?

    SUZAN: Ndio tena kifo cha gafla sana.

    MWAMBE: Maskini Sam!! Mawazo yangu nilijua bado yupo marekani jamani dah!!

    FRANK: Na tangia yeye na mkewe waiage dunia huu ni mwaka wa nane sasa.

    MWAMBE: Ooh!! Jamani, kumbe ni muda mrefu sana. Mr. Sam alikuwa rafiki yangu mkubwa sana hata kwenye harusi yake mimi nilikuwa bestman wake. Ningejua yote haya kabla wala binti yake asingeteseka kwani Sam alikuwa na mali nyingi sana, waliozichukia itakuwa wamefojisha tu.

    Basi Mwambe akaanza kuwaelezea kuhusu mali za Sam hapo nchini hadi wakabaki wanashangaa tu, wakakubaliana kuwa lazima ifunguliwe kesi ili waliomfanya Safina ateseke nao wapate fundisho.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Juta ambaye ndiye kaka mkubwa wa Sam, akapokea barua kuwa wanahitajika mahakamani. Ikabidi amuite Aisha na Jese azungumze nao.

    JUTA: Nashindwa kuelewa kabisa, eti twende mahakamani.

    AISHA: Kufanya nini tena kaka?

    JUTA: Eti kuhusu mali za Sam.

    AISHA: Mali za Sam? Mali gani wakati Sam alikufa kitambo!

    JUTA: Wanadai eti Safina ndiye aliyekuwa mrithi halali wa mali hizo.

    JESE: Jamani kaka si mlisema kuwa Safina alikufa?

    JUTA: Ndio, hata mi nashangaa hapa.

    AISHA: Kaka lazima kuna uzembe umefanyika mahali.

    JESE: Kama swala la uzembe atakuwa ni Peter tu, nimemuona akiwa pamoja sana na Modesta siku hizi.

    JUTA: Huu ni ujinga sasa, lazima tufanye kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.

    Mara kuna sauti ikasikika ikicheka nyuma yao.



    Wakiwa wanajadili mara ikasikika sauti ikicheka nyuma yao, kila mmoja alishtuka na kuwa na bumbuwazi. Ile sauti ilicheka tena ilicheka sana. Mara ile sauti iliyocheka wakasikia ikisema,

    "Huu ndio ule wakati nilioungoja kwa hamu"

    Mara kimya kirefu kikatanda hakuna aliyeweza kuongea hata kidogo, walijikuta wote wakikimbilia ndani.

    Kwavile hapo ilikuwa ni nje ya nyumba ya Juta kwahiyo wakaingia moja kwa moja ndani ya nyumba kwavile walikuwa nje.

    Baada ya kimya kifupi wakaanza kuulizana kuhusu ile sauti.

    JUTA: Hivi ile sauti inaweza kuwa ya nani?

    AISHA: Mmh!! Ile sauti ni kama ya marehemu wifi Latifa.

    JESE: Acha zako bhana Aisha, huyo Latifa alishakufa kitambo sasa sauti yake ifanye nini? Mi nahisi ni mtu tu alitaka kututisha.

    JUTA: Inawezekana, ila je mtu huyo wa kututisha ni nani?

    AISHA: Basi atakuwa Modesta jamani maana ana akili mbovu sana yule.

    Wakaamua kuuficha ukweli kwa fikra zao za uongo.

    Mke wa Juta akawa anawashangaa tu.

    SARAH: Mbona kama kuna mabishano hapa?

    AISHA: Wifi, kuna barua hapa inatutaka twende mahakamani, eti kesi ya kuhusu mali za Safina.

    SARAH: (Akashtuka), Safina?

    AISHA: Ndio Safina, wewe si ulimfukuza hapa!

    SARAH: Sikumfukuza wifi, aliondoka mwenyewe. Yule mtoto ana kiburi sana.

    AISHA: Mmh!! Wifi ulimfukuza wewe.

    JUTA: Jamani hapa tusirumbane, cha msingi tujue jinsi gani tutakabiliana na kesi hii.

    Ikabidi wajadiliane kwanza na kuona kwamba kuna ulazima wa kuweka kikao cha familia ili wajadili namna ya kukabiliana na hiyo kesi.



    Juta akaamua kuitisha kikao cha familia, na kuwaeleza wote kuhusu hiyo kesi.

    PETER: Hapo hakuna cha kufanya zaidi ya kwenda mahakamani tu.

    JESE: Upeo wako wa kufikiri ni mdogo sana Peter.

    PETER: Nakubali nina upeo mdogo na ndiomana mkakubaliana ninyi watatu kutengeneza hati feki na kuuza mali za marehemu.

    JUTA: Peter, unaongea vitu gani wewe? Umekuwa kama poyoyo!

    AISHA: Huyu Peter nae anakuwa mjinga kama Mode tu.

    MODESTA: Mimi sio mjinga ila nataka nisikie huo ujinga wenu wa leo.

    JESE: Hii miwatu mbili imevurugwa hii.

    Juta na Aisha wakawa wanacheka.

    JUTA: Tuacheni marumbano basi, cha msingi tujue tutafanya nini.

    JESE: Hivi kwanini Safina hakufa jamani?

    AISHA: Hata na mimi nashangaa.

    MODESTA: Kwanini msife nyie watu wazima? Mnataka afe mtoto kwa lipi? Kama kufa kufeni nyie.

    JUTA: Hata wewe kufa tu, maana maneno yako ni ya kufa kufa.

    JESE: Tumekaa na watu wasio na akili kabisa hapa, jamani twendeni tukasikilize mashtaka kwanza halafu tuamue cha kufanya. Ila cha muhimu ni kupinga mashtaka yote tutakayoambiwa.

    MODESTA: Hata kama mkipinga, ukweli utabaki pale pale.

    Halafu akainuka na kuondoka.

    JUTA: Huyu Mode hana akili kabisa na hafai kwenye ukoo ndiomana elimu yake ni ziro.

    PETER: Tafuteni na wakili wa kuwatetea kwanza.

    AISHA: Kwahiyo wewe unajitenga??

    PETER: Hakuna baya nililolitenda.

    JUTA: Tutaenda huko mahakamani kusikiliza jamani.

    Kwahiyo wakajipanga kwaajili ya kwenda mahakamani.



    Wakaamua kwenda kusikiliza mashtaka kwanza, na huko mahakamani wakamkuta Suzan na Frank.

    Wakasomewa mashtaka yao na kupinga yote, kwahiyo kesi ikapangwa siku nyingine kwaajili ya ushahidi.

    Walipotoka, Aisha akamfata Suzan.

    AISHA: Nilijua tu wewe kidudu mtu ndio umefanya yote haya.

    SUZAN: Maneno hayasaidii na lazima mtakuwa hatiani tu nyie.

    Aisha akaondoka na kuwafata ndugu zake ili wapate kujadili.

    JESE: Jamani hii kesi ni ngumu, wakili peke yake hatoshi lazima tutafute mganga wa kutusaidia.

    JUTA: Umesema vyema Jese, hilo ndio jambo la kufanya.

    Kumbe Modesta aliwasikia maneno yao, kwakweli alisikitika sana.

    AISHA: Jamani ishu ya mganga msiwashirikishe Modesta na Peter, hawa wataharibu tu mipango yetu.

    Wakakubaliana kwenda kwa mganga kumbe Modesta alishawasikia tayari.

    Walipoondoka ikabidi Modesta amfate Suzan na kumueleza.

    SUZAN: Sasa tufanyeje Mode?

    MODESTA: Cha muhimu ni maombi tu, kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana. Wale ni sawa na mfamaji kwahiyo wanatapatapa.

    SUZAN: Ila ndugu zako wana mambo sana.

    MODESTA: Wana mambo balaa ila nitachunguza tu, usiache kuomba juu ya Safina, Suzy.

    SUZAN: Sawa Mode nimekuelewa.

    Wazo kubwa la Modesta alitaka kwenda kwa yule binti wa kiarabu, Yusra ili ajue mambo ambayo ndugu zake wameyapanga kwa Safina safari hii.



    Siku ya kesi na ushahidi ilikuwa tayari, na prof. Mwambe akaweka tayari kila kitu kwaajili ya kesi hiyo.

    MWAMBE: Usijari Safina, kesho ndio siku yenyewe. Wewe jielezee tu bila uoga wowote.

    SAFINA: Sawa nimekuelewa.

    Basi Mwambe akawaaga na kuondoka. Wakabaki Safina na Musa pale nyumbani.

    SAFINA: Musa sijui kama nitaweza kujieleza.

    MUSA: Acha uoga Safina, utaweza tu. Jipe moyo utashinda, kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

    SAFINA: Naelewa Musa ila ndugu zangu ni wabaya sana jamani, yaani kuwaua wazazi wangu sababu ya mali!

    MUSA: Usiwaze sana Safina, ila ubaya ni kuwa serikali haitambui uchawi. Kama ingetambua, basi hata kesi ya mauaji ingewakabili hao jamaa. Ila cha msingi ni upate haki yako Safina.

    SAFINA: Ni kweli Musa ila napenda wale ndugu zangu na wao wateseke maisha.

    MUSA: Hukumu lazima iwakabili nduguzo Safina.

    Wakiwa wanajadili hayo, mara gafla Safina akaanguka sakafuni huku damu zikimtoka puani. Hofu kubwa ikamtanda Musa na kumpigia simu Suzan. Naye Suzan alihisi kuchanganyikiwa, akampigia simu Modesta.

    MODESTA: Suzy, nakuja hapo nyumbani sasa hivi. Msimpeleke hospitali.

    SUZAN: Sawa.

    Akakata simu haraka na kumpigia Musa.



    Musa akiwa kamuweka Safina begani ili ampeleke hospitali, anashangaa akipigiwa simu na Suzy na kukatazwa kufanya hiyo. Ikambidi amlaze kwenye kochi.

    Suzan aliharakisha na kurudi nyumbani, akamkuta Safina akiwa kwenye hali mbaya sana, hata na yeye wazo la kumpeleka hospitali likamjia.

    Wakati anataka kufanya hivyo mara Modesta akafika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SUZAN: Mode ona, tutafanyaje sasa?

    MODESTA: Tulia Suzy, ngoja nifanye nilichoambiwa kwanza.

    Modesta akachukua kipande cha mkaa na kukisaga halafu ule unga unga akachanganya na chumvi.

    Akachukua kidogo na kuchanganya na maji, halafu akaanza kumpaka Safina kwenye paji la uso.

    Na ule ung uliobaki akamnyunyizia puani, mara wakamuona Safina akijigeuza geuza na kupiga chafya mfululizo.

    Alipiga chafya kwa sana na mara akainuka na kukaa, akiwa haelewi chochote kilichotokea.

    SAFINA: Kwani kuna nini hapa?

    MODESTA: Hakuna kitu mama, usijari mwaya.

    Safina alikuwa anajishangaa tu kwani alipojigusa usoni alijiona ana vitu vyeusi vyeusi.

    SAFINA: Na hii ni nini?

    Ikabidi Musa amueleze Safina kilichotokea, kwakweli Safina alishangaa sana.

    Suzan nae alikuwa akishangaa yote.

    SUZAN: Mode, umejifunza wapi hiyo dawa?

    MODESTA: Suzy hayo ni mambo ya asili, yule Yusra ndio ameniambia nifanye hivi kwasababu nilienda kumuuliza.

    SUZAN: Mmh!! Walitaka kumpoteza Safina eeh!!

    MODESTA: Ndio, ila Mungu mkubwa Suzan. Hawatafanikiwa tena na hila zao mbaya, tena bora mmenisikiliza kutokwenda hospitali kwanza.

    MUSA: Kwani hospitali ingekuwaje?

    MODESTA: Mambo kama haya ukipeleka hospitali unammaliza mgonjwa sababu hospitali wangemchoma sindano na hapo ndipo pabaya.

    MUSA: Haiwezi kujirudia tena.

    MODESTA: Haiwezekani tena, kwani wenyewe watadhani Safina ameshakufa ila watashangaa kumuona kesho mahakamani.

    Wakasikitika sana, kwani ndugu hao walikuwa wabaya kwakweli bila hata huruma kabisa, ila siku zote mwisho wa ubaya aibu. Na ndiomana Mungu amewaaibisha.



    Juta, Aisha na Jese wakiwa kwa mganga wao, mganga huyu ndio yule yule aliyewasaidia kuwamaliza Sam na Latifa. Walihakikishiwa kuwa kila kitu tayari. Sasa kilichobaki ni kwenda kumzika Safina.

    Wakiwa wanajiandaa kuondoka mara hali ya hewa ikabadilika kwenye kile kibanda cha mganga, kwani yule mganga alianguka gafla na kuanza kutapatapa huku na kule.





    Wakiwa wanajiandaa kuondoka mara hali ya hewa ikabadilika kwenye kile kibanda cha mganga, kwani mganga alianguka gafla na kuanza kutapatapa.

    Wote watatu wakapatwa na bumbuwazi kwani mganga alikuwa akihangaika kama vile mtu anayekabwa.

    Gafla akatulia tuli, wakabaki wanaangaliana bila ya kujua cha kufanya.

    Mganga akiwa katulia pale chini, wakajaribu kumuamsha lakini hakuamka, walipomtazama vizuri wakagundua kuwa ameshakufa. Hofu kubwa ikatanda mioyoni mwao.

    AISHA: Jamani mbona sielewi kitu!!

    JUTA: Hata mimi sielewi kitu.

    JESE: Tutafanyaje sasa?

    AISHA: Tuite watu waje watusaidie.

    JESE: Halafu tutawaambia kuwa imekuwaje?

    Mara gafla mke wa mganga aliyeitwa Rhoda akaingia kwenye kile kibanda, akamuona mumewe kalala chini akiwa hajitambui.

    Akamkimbilia pale chini na kumtikisa akiwa kimya kabisa, Rhoda akaanza kulia huku akipiga kelele,

    "mmemfanya nini mume wanguuuuu?"

    Wakaona hapo itakuwa khatari, ikabidi wakubaliane kukimbia na kumuacha mke wa mganga na mganga akiwa pale chini.

    Rhoda aliendelea kupiga kelele iliyofanya watu kujaa kwenye kibanda hicho, kila mmoja alibaki kushangaa tu. Rhoda nae aliendelea kupiga kelele kuwa wamemuua mume wake.

    Watu wakambeba hadi hospitali ambako daktari alithibitisha kuwa yule mganga ameuwawa kwani inaonyesha kuwa kuna mtu amemnyonga.

    Rhoda akasema,

    "sikubali lazima watu waliohusika na kifo cha mume wangu washtakiwe"



    Juta, Aisha na Jese wakakimbilia moja kwa moja nyumbani kwa Aisha.

    JUTA: Mbona makubwa haya ya leo jamani!!

    AISHA: Makubwa tena makubwa haswaaa.

    JESE: Ila bora kazi ya Safina imeisha.

    JUTA: Ndio kazi ya Safina imeisha, ila je ni kitu gani kimemuua mganga?

    AISHA: Mmh!! Jamani labda ni uoga wetu tu. Usikute mganga hajafa, labda alienda kuongea na mizimu yake.

    JUTA: Inawezekana kweli hajafa, na bora iwe hivyo maana ndiye tegemeo letu yule.

    JESE: Ila kaka hakuna tatizo ilimradi Safina kafa unadhani kuna mtu atakaefika mahakamani hapo kesho? Ni moja kwa moja tutashinda kesi tu.

    JUTA: Ila mi nadhani hiyo kesho tutokee hapa hapa kwa Aisha. Sidhani kama ni salama kurudi kwangu.

    JESE: Kweli kabisa kaka, kwako pale wengi wanapajua. Hapa itakuwa rahisi hata kufanya dawa tulizopewa.

    AISHA: Ila jamani tuombee mganga asiwe amekufa maana mkewe chizi yule balaa.

    JESE: Jamani msilete mada za kufa tena, mshasema hajafa sasa hilo la kusema kama amekufa linatoka wapi tena? Halafu hata kama akifa sisi tutahusishwa vipi?

    JUTA: Hamna bhana Aisha amesemea tu. Ila kama akifa tunaweza kuhusishwa kwavile sisi ndio tulikuwa nae.

    AISHA: Sawa basi tufanye hajafa na hakuna chochote kilichotokea.

    Wakawa wanajipa moyo kuwa mganga hajafa.

    Wakaendelea kufanya dawa zao za kushinda kesi.



    Nyumbani kwa Frank wakawa wanajiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kesi.

    SUZAN: Hivi watakuwa na cha kujitetea kweli wale?

    FRANK: Watajiuma uma tu kama kawaida yao ila hawataweza chochote.

    SUZAN: Na wewe umejuaje kama watajiumauma?

    FRANK: Nilipata habari kuwa Aisha ni maneno mengi, ila leo atapatikana.

    Wakaingia kwenye gari pamoja na Safina na Musa, na safari ya kwenda mahakamani ikaanza.

    Kufika njiani, gari yao ikagongwa kwa nyuma kitu ambacho kiliwachelewesha kidogo mahakamani kwani walikuwa wakitatua kwanza lile tatizo la gari kugongwa.

    Walipofika, wakaingia mahakamani, na kukuta watu wote wameshafika.

    Hakimu alipoingia, ndipo kesi ikaanza kusomwa ikiwa kila upande kuna mashahidi na wakili wa kuwatetea.

    Wakili wakina Safina alikuwa Bwana Mwambe na wakili wakina Juta alikuwa

    Bwana Maneno.

    Kesi zilizowakabili washtakiwa zilikuwa nyingi, kwanza kudhurumu mali ya Yatima, pili kutengeneza hati feki na kuuza mali za marehemu na tatu kumfukuza mtoto wa marehemu na kumfanya ateseke mitaani.

    Kesi zote ziliwabana sana washtakiwa hata hawakujua ni wapi pa kupumulia.



    Baada ya kesi kusomwa, na mawakili kusema yao mbele ya mahakama. Mwendesha mashtaka akawataka mashahidi wa kesi hiyo waweze kueleza.

    Ndipo Bwana Mwambe alipomwambia Safina apande kizimbani na kujieleza.

    Kitendo cha Safina kupanda pale kortini, kiliwafanya wakina Juta kukosa amani na kushindwa kuelewa kuwa imekuwaje hadi Safina yupo hai hadi muda huo, hawakumuona kama kafika mahakamani kutokana na kwamba wakina Safina walifika nyuma yao.

    Safina akaelezea yote yaliyomtokea kwenye maisha yake tangu wazazi wake walipofariki, alielezea kwa uchungu sana, kila aliyekuwepo pale mahakamani alisikitika.

    Musa nae akaelezea jinsi alivyokuwa akiishi na Safina mitaani.

    Frank akaelezea hali halisi aliyomkuta nayo Safina.

    Suzan nae akaeleza mambo yaliyosibu hadi Safina kunyang'anywa mali zake.



    Basi na upande wa washtakiwa nao wakaanza kutoa maelezo yao.

    AISHA: Huyu mtoto ni wa kaka yetu kwahiyo mimi namuona kama mwanangu wa kumzaa, siwezi kumtenda vibaya kwani mimi na Sam ni ndugu tena wa damu. Kaka Juta alimchukua Safina na kumlea kama anavyolea watoto wake lakini Safina alitoroka.

    MWAMBE: Alitoroka au walimfukuza? Na si akaja kwao na kukukuta wewe na kaka yako halafu ukamfukuza pia!

    AISHA: Lakini........

    MWAMBE: Lakini nini? Aliwakuta na mkamfukuza siyo?

    AISHA: Unajua Safina......

    MWAMBE: Jibu swali nililokuuliza, mlimfukuza?

    AISHA: Hatukumfukuza bali aliondoka mwenyewe.

    MWAMBE: Kwahiyo Safina alijiamulia kwenda kupata shida na kuacha kwao?

    AISHA: Alikuwa na akili za kitoto enzi hizo.

    Kama kawaida ya kesi, ikahairishwa hadi kesho.



    Kesho yake kesi ikasomwa tena, shtaka ambalo waliamua kupingana nalo vilivyo ni swala la kumfukuza Safina kwani waliona kuwa hilo swala litawatia hatiani zaidi.

    Bila kutegemea, wakamuona Modesta nae akipanda kizimbani na kutoa ushahidi kuwa ndugu zake walimfukuza Safina.

    Na katika kulitia nguvu swala hilo, Modesta aliweza kumtafuta mtu aliyekuwa mlinzi wa nyumbani kwa Sam aje kutoa ushahidi kwani ndiye aliyeshuhudia.

    Mlinzi huyo aliitwa Juma. Naye akapanda kizimbani na kuapa kisha kuelezea ilivyokuwa.

    "Ilikuwa ni Jumamosi majira ya saa moja jioni, nilisikia mtu akigonga geti, nilipofungua alikuwa ni Safina. Kwakweli nilihudhunika kwa hali aliyokuwa nayo kwani alikuwa amekonda sana na alikuwa mchafu. Nilimkaribisha ndani na kuendelea na shughuli zangu, mara baada ya muda kidogo nikasikia dada Aisha akigomba mara nikamwona kamshika mkono Safina huku akisukumana nae hadi getini, akafungua geti na kumsukumia nje. Nikamsikia akimwambi kuwa "usirudi tena hapa na ukithubutu kukanyaga mguu wako tena mahali hapa nitakuchinja". Dada Aisha alisimama pale pale getini hadi Safina alipopotelea gizani kabisa ndipo akafunga geti na kuniambia "ole wako umkaribishe tena huyu mtoto ndani, nitakufunza adabu". Kwakweli niliumia sana moyoni ingawa sikuwa na la kufanya kwa wakati huo."

    Kila mmoja pale mahakamani alisikitika sana, jaji akaahirisha kesi hadi mchana wa siku hiyo ili ije kutolewa hukumu kwa wahusika.



    Wakiwa nje wanangoja hukumu ya kesi yao.

    JUTA: Jamani hivi Modesta ana akili kweli?

    JESE: Yule ni mlemavu wa akili, yani anaangamiza ndugu zake kwaajili ya watu baki dah!!

    AISHA: Ngoja tushinde halafu tuone atakimbilia wapi.

    Wakiwa wanazungumza mara wakamuona Rhoda akiwa na maaskari,

    RHODA: Hawa hapa ndio waliomuua mume wangu.



    Wakiwa wanazungumza mara wakamuona Rhoda na maaskari.

    RHODA: Hawa hapa ndio waliomuua mume wangu.

    Wale maaskari wakachukua pingu na kuwafunga watuhumiwa walioonyeshwa, kwahiyo Juta, Jese na Aisha wakafungwa pingu.

    AISHA: Jamani kosa letu ni nini??

    ASKARI: Nyie ni wauaji, mmemuua mume wa huyu mama.

    JESE: Lakini sisi hatumjui huyo mama.

    Wakaamua kumkana Rhoda pale kwa maaskari.

    RHODA: Kheee!! Kweli Wauaji ni wauaji tu yani leo hii Jese unanikana mimi!!

    JESE: Hatukujui bhana, tunakushangaa unamaana gani kusema sisi ni wauaji.

    RHODA: (Akamgeukia askari) Askari mimi nina mashahidi kabisa kuwa hawa ndio wahusika wa kifo cha mume wangu.

    Akatokea askari mwingine aliyeitwa Juma na kuwaambia.

    JUMA: Jamani hao watuhumiwa tayari kwani wana kesi yao inasomwa mchana kama vipi na hiyo ipelekeni kwa hakimu moja kwa moja wahukumiwe tu hawa.

    JUTA: Haiwezekani jamani, tena haiwezekani kabisa. Mnataka kutubambikizia kesi nyie.

    Modesta akaona nduguze wakiwa na pingu halafu wamezingirwa na maaskari, ikabidi aende kusikiliza. Akaambiwa kuwa nduguze wanashtakiwa kwa mauaji ya kumuua mganga.

    MODESTA: Vizuri sana, dhambi uliyofanya huwa haikimbiwi kirahisi hivyo. Mliwaua wale wengine kishirikina sasa imetokea aliyeuwawa kweli, amakweli hukumu ni hapahapa duniani, mbinguni kuhesabiwa tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    JUMA: Waliua kishirikina?

    MODESTA: Ndio, na bahati yao serikali haiamini uchawi.

    RHODA: Ila mume wangu hawajamuua kiuchawi, wamemkaba kiuhalisia kabisa hadi kufa.

    MODESTA: Kwani mume wako ni nani yao?

    RHODA: Mume wangu ni mganga wa jadi, wamemuua hawa halafu leo wananikana.

    MODESTA: Oooh!! Nimekuelewa mama, kama ndio hivyo basi watakuwa wamemuua kweli kwani niliwasikia kuwa wanaenda kwa mganga.

    JESE: Wee Mode wewe, acha maneno yako hayo. Nani wa kwenda kwa mganga kati yetu hapa? Sisi sio watu wa imani za kishirikina.

    ASKARI: Hapa sio pa marumbano, swala ni kwamba mmeua basi na hukumu lazima ihusike hapa.

    Juta, Jese na Aisha walikuwa ni watuhumiwa tayari ikawa ni ngumu kwenda kufanya mambo mengine kwani mchana walikuwa wanatakiwa kusomewa mashtaka.



    Basi mchana wa siku hiyo ulipofika, watu walijaa mahakamani hapo ili kujua hatma ya kesi hiyo, wengi walimuonea huruma Safina kwa maisha aliyopitia. Wengine waliwaza kuwa endapo wakinaJuta watashindwa kesi itakuwaje kwa mali walizonunua kwao.

    Kesi nyingine ikatajwa ikiwahusu Juta, Jese na Aisha ilikuwa ni kesi ya mauaji ila wakaikana kesi hiyo.

    Kesi ya mauaji ikapangwa kusomwa tena kesho wakati ushahidi kamili ukiletwa.

    Kwa hitimisho la kesi ya Safina, jaji akatoa hukumu ya kesi hiyo.

    "Kwakweli inasikitisha sana kwa mzazi kutafuta mali kwa shida kwaajili ya mtoto wako halafu mtoto huyo apate shida ambazo hukuzitegemea. Nbmini kuwa hata wazazi wa huyu binti watakuwa wamehudhunishwa sana kwa jambo hili. Watuhumiwa wamedhurumu jasho la mtu tena wamemtenda vibaya yatima wakati wanajua wazi yatima anapaswa kupewa upendo, watuhumiwa ndio walikuwa watu muhimu sana wa kumuendeleza huyu yatima kimaisha lakini kvokana na uroho wa mali wakatamani hata kumuua na hili ni kosa la jinai. Kutokana na hatia mliyokutwa nayo, mahakama hii inawahukumu kifungo cha miaka kumi na tano jela na adhabu kali. Na hili liwe fundisho kwenu na kwa wote wenye tabia kama za kwenu. Na Safina arudishiwe mali zake zote."

    Jaji alimaliza na kutoka, ikawa nderemo na furaha huku wakimpongeza Safina kwa ushindi.

    Wale walionunua mali za marehemu Sam, walisikitika sana kwani wengine waliuziwa bila vibali na wengine kwa hati feki.

    Na wao wakaamua kufungua madai ya pesa zao kwa watuhumiwa kwani walikuwa wametapeliwa.



    Ilikuwa ni furaha kweli kwa Safina na wengine wote walomuhurumia.

    Na kesho yake wakaamua kwenda tena mahakamani kusikilizia kesi ya mauaji.

    Kule mahakamani kesi ikasomwa tena, wakaipinga kabisa. Mashahidi wakatoa ushahidi wao kuwa waliwaona nyumbani kwa mganga, ubaya zaidi ni ushahidi alioutoa mtoto wa mganga kwani aliwapiga picha siku hiyo wakati wapo na baba yake. Kwahiyo wakakuta na hatia.

    Mahakama ikawahukumu kifungo cha maisha, na kuhusu kesi ya madai ya wale walionunua mali za marehemu Sam.

    Mahakama ikatoa tamko kuwa mali za Juta, Jese na Aisha zinadiwe halafu wanunuzi hao wapewe nusu hasara ili iwe fundisho kwao la kununua vitu bila ya vibali vinavyoeleweka.

    Kwakweli ilikuwa ni kilio kikubwa kwa Aisha, Juta na Jese. Walipokuwa wanapelekwa gerezani Peter na Modesta wakawafuata.

    JUTA: Tafadhari Peter nitunzie wanangu.

    PETER: Usijari kaka nitawatunza.

    MODESTA: Hata na mimi nitawatunza, sina roho mbaya kama mnavyodhani. Nimeshukuru kuwa mnaenda kuyalipia makosa yenu sasa. Na siku zote mkumbuke kuwa MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

    AISHA: Mode jamani, kweli tumeaibika. Hata hatutazamiki na watu tena. Najutia mimi, najutia yote niliyoyafanya ila yote nilishinikizwa na hawa kaka zangu.

    JESE: Hakuna cha kushinikizwa hapa, sema tujutie tu kwani aibu na fedheha vimetupata.

    Sarah na watoto wake wanne aliozaa na Juta, wote walikuwa wakilia na kuomboleza tu.

    Jese aliwahurumia watoto wake wawili aliokuwa anawalea.

    JESE: Na mimi nitunzieni wanangu.

    PETER: Usijari kaka, nitawatunza.

    Aisha hakuwa na mtoto ila alikuwa mjamzito, muda wote machozi yalimtoka kwani ameshajua kuwa mwanae atamzalia gerezani.



    Safina akakabidhiwa mali zake zote, kwakweli ilikuwa ni furaha sana. Na akamteua kamanda Frank na Suzan kuwa wasimamizi wa mali zake.

    Wakaamua kufanya sherehe kubwa sana ya kumpongeza Safina. Kwakweli Safina aliwashukuru sana, aliwashukuru wote.

    Akaamua kumkabidhi nyumba moja shangazi yake Modesta ili asihangaike.

    Maisha yalimuwia vigumu sana Sarah, akaenda kumuomba Safina kwani hakuwa na mahali pa kwenda na watoto wake.

    SAFINA: Wanao ni ndugu zangu, watakaa na shangazi. Ila wewe tafuta pa kwenda.

    SARAH: Nihurumie Safina, tafadhari nihurumie.

    SAFINA: Mbona wewe hukunihurumia?

    SARAH: Ni shetani tu alinipitia Safina.

    SAFINA: Ngoja nimuulize shangazi kama atakukubali wewe na roho mbaya yako.

    Safina akamuuliza Modesta, naye akasema ataishi nae ila Safina akamwambia Sarah kwamba ataishi kwa Modesta kama mfanyakazi wa ndani tu.



    Baada ya kukarabati nyumba yao, Safina akamuomba kamanda Frank kuwa wahamie huko na wote wakahamia pale kwenye nyumba ya marehemu Sam, ikawa ni furaha sana.

    Safina akamwambia kamanda Frank kuwa kiwanja kimoja kitumike kujengwa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wa mitaani, fedha iliyokuwa kwenye account ya baba yake ndio aliona kuwa itafanikisha shughuli hiyo.

    FRANK: Umeamua vyema Safina.

    SAFINA: Maisha ya mtaani ni magumu sana bamdogo, kuliko kupata shida ni bora wafurahie maisha kwa pamoja na mahali pazuri.

    FRANK: Sawa sawa Safina.

    Ikabidi Frank azianze hizo harakati.

    Siku Modesta akiwa amelala akatokewa na Latifa ndotoni na kumwambia.

    "kwaheri Mode, sasa mtu wangu atapumzika kwa amani"

    Halafu akampungua mkono kama ishara ya kumuaga.

    Modesta alishtuka na kusema, "Latifa"

    Modesta alifurahi moyoni kuona sasa ukweli na uongo umejitenga.



    Prof. Mike akapanga mipango ya kusafiri na Safina kwenda naye Marekani ili akamkabidhi vitu ambavyo wazazi wake waliviacha huko na kuendelea kuboresha maisha yake.

    Safina akaacha kila kitu chini ya Frank na Suzan.

    MUSA: Safina nitakumiss

    SAFINA: Hata na mimi nitakumiss Musa.

    MUSA: Ninachoomba usitusahau huko.

    SAFINA: Usijari kwa hilo Musa, nitawakumbuka siku zote. Tena nikiweza kule nitakualika na wewe uje Musa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUSA: Kweli Safina? Nitafurahi sana na mimi siku nitakayofika huko.

    SAFINA: Usijari, tuombeane uzima tu.

    MUSA: Nitakuombea daima.

    SAFINA: Asante Musa, machozi yetu yote yamekauka sasa.

    Safina na Musa wakakumbatiana kwa furaha.



    Ikafika siku ya safari, Safina na Prof. Mike wakajiandaa.

    Basi Suzan, Frank, Musa, Modesta na Peter wakawasindikiza hadi uwanja wa ndege. Wakaagana, halafu Safina na prof. Mike wakaenda kupanda ndege.

    Safina alifurahi sana kwani hakuamini kama maisha yake yanajirudia, ingawa aliwapoteza wazazi wake lakini aliamua kusonga mbele ili wazazi wake waendelee kujivunia kuwa nae hata huko walipo.

    Safina akajikuta akisema kwa furaha.

    "I can't believe that i'm going back to USA"



    ************************** MWISHO**************************

0 comments:

Post a Comment

Blog