Search This Blog

BINTI WA PILI WA MFALME - 5

 







    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Embu toka hapa maana sikuelewi unachokizungumza" alisema Hancy na kuondoka zake.



    Alionekana Fancy, akicheka pembeni na kusema Hancy sasa itabidi uanze kuamini maneno niliyoweza kumwambia Sikitu akwambie... Mpaka sasa mchezo wangu unaendelea vizuri nataka kujua sasa utaishiaje? alizungumza na kumtazama Kipande ambaye aliishia tu kutabasamu.



    Malikia aliweza kutoka na hapo hapo Hancy alitokea katika kordo nyingine kwaajili ya kuelekea chumbani mwake na Mozah ndani aliweza kuifungua kabati yake na kuitafuta ile cheni hatimaye aliweza kuiona na kuiokota baada ya kuiona aligeuka na kusema nimeipata.



    Macho yake yaliweza kukutana uso kwa uso na Hancy ambaye aliweza kuiona ile cheni Mozah aliwahi kuificha akiamini ya kuwa Hancy hajaiona.



    "Hancy" aliita kwa kujichekesha.



    Hancy na yeye aliweza kucheka na kujifanya ajaona kitu



    "Unafanya nini ?? Aliuliza Hancy akimsogelea.



    " Hamna alijibu Mozah na kuweza kuirudishia ile cheni katika kabati kisha akageuka na kulifunga.



    "Nilikuwa napanga panga nguo" alizungumza Mozah na kumfuta Hancy.



    "Mbona uliniambia utachelewa kurudi" aliuliza Mozah na kuweka mikono yake katika kiuno cha Hancy.



    Hancy alimshika katika shavu na kumuuliza.



    "Kwani umeuchukia uwepo wangu kwasasa?? Aliuliza Hancy na kumsogeza Mozah zaidi.



    " au kuna jambo ambalo ulilitaka kulifanya pasina uwepo wangu?? Aliuliza Hancy na Mozah Alicheka tu.



    "Hapana.....hakuna ambacho nitaweza kukifanya pasina uwepo wako" alizungumza Mozah na Hancy aliitoa mikono ya Mozah kisha kuanza kulisogelea lile kabati kwaajili ya kwenda kulifungua.



    "Hancy" aliita Mozah na kujitokeza mbele yake.



    "Nini??



    " Unataka kuchukua nini kwenye kabati?



    "Nataka kubadilisha shati" alizungumza Hancy na kuanza kusogeza hatua.



    "Ngoja Mimi ndiye mke wako uniambie Unataka shati lipi nikuchukulie" alizungumza Mozah.



    "Hapana nataka kuchukua mwenyewe" alizungumza Hancy na kumpita Mozah.



    Mozah alimuwahi mdomoni na kumpiga busu Hancy kisha kuanza kumsogeza mbali na kabati lile.



    "Mozah unashida gani wewe?? Aliuliza Hancy na kujitoa mwilini mwa Mozah.



    Mozah aliweza kukumbuka ya kuwa Fancy alimwambia ahakikishe Hancy hatoweza kuiona hiyo cheni kwani ingeweza kuleta shida.



    " hapana siwezi kumfanya Malikia Maua aweze kugundulika" alizungumza Mozah na hatimaye alimuita Hancy.



    "Nini aliuliza Hancy na kugeuka nyuma ambako aliweza kumuona Mozah akifungua kamba za gauni lake na kuweza kulidondosha chini.



    " Mozah!! Aliita Hancy kwa kigugumizi na Mozah aliweza kumsogelea taratibu kabisa kisha akaanza kumfungua vifungo vya shati na kumpiga mabusu.



    "Mozah" aliita Hancy na kumtoa katika mwili wake.



    "Ni nini Unataka kufanya eti?? Aliuliza Hancy na kumpisha Mozah kisha kwenda kuokota gauni la Mozah na kumvisha.



    Hancy alitoka njee na kuondoka zake. Mozah alibaki kitandani akiwa ameshika kichwa chake na kujiuliza " kwanini alitumia njia ile"



    Lazima Hancy atakuwa amenifikiria vibaya alizungumza na kuanza kutoka njee kwaajili ya kwenda kuzungumza



    Alipofungua mlango tu aliweza kukutana na Hancy akirudi kwa speed ndani.



    Hancy aliita Mozah na Hancy alimrudisha ndani kisha akaanza haraka haraka kumvua nguo na kumtupia kitandani.



    "Bora tumalizie kile ulichoweza kukianzisha" alizungumza Hancy na kuanza kuvua nguo zake .



    Wakati huo Fancy alikuwa njee, sawa sawa ila nakuhakikishia ya kuwa hii ni mara ya mwisho kuushika mwili wa Hancy, kwani itabaki kama kumbukumbu tu alicheka sana na kuyafuta machzo yake.



    Ni baada ya Fancy kula kiapo ya kuwa hiyo ni mara ya mwisho Mozah kuushika mwili wa Hancy.



    Waliweza kufanya kile ambacho walihisi ni sahihi kwa upande wao.



    Usiku ulikuwa mwingi na Mozah alikuwa wa kwanza kuamka kutoka kitandani alielekea moja kwa moja hadi kwenye kabati aliloweza kuficha Cheni ile kisha akaitoa.



    Aliitizama na kumtizama Hancy ambye alikuwa amelala.



    Alijisikia vibaya sana jinsi anavyoweza kumdanganya Hancy lakini hakutaka Malikia Maua aingie kwenye matatizo kwani Furaha ya Hancy ni mama yake, hivyo asingependa kuona Hancy akiingia katika huzuni.



    Aliichukua cheni ile kisha akafungua kisanduku chake kidogo na kuweza kuiweka cheni ile. Akimini ya kuwa hakuna mtu aliyeweza kumuona basi alielekea bafuni.



    Hancy aliyafumbua macho yake na kuelekea moja kwa moja hadi sehemu ambayo aliweza kuihifadhi ile cheni aliifungua na kuitizama ile cheni.



    Aliirudishia na kuelekea kitandani huku akiwa mwingi wa mawazo.



    Palipambazuka asubuhi na Mozah alikuwa wa mwisho kuamka kitandani. Hakuweza kumuona Hancy kama kawaida yake kwani Mara nyingi Hancy humuamsha na kumtaka aende akaoge.



    Alihisi Hancy atakuwa ameelekea bafuni alisimama na kwenda kugonga bafuni mlango uliweza kufunguka na hakukuwa na uwepo wa Hancy mahali pale.



    "Ameelekea wapi?? Alijiuliza na baada ya muda kidogo alitoka ndani ya chumba chake na kwenda kumtafuta Fancy.



    Akiwa anamtafuta Fancy aliweza kumuona akiwa amekaa na Hancy huku akiwa amemshikilia Mkono na wakiwa wanacheka.



    Alikuja Sikitu na kusimama pembeni yake.



    " hivi unafikiria nini eti, kwamba Hancy na Mozah ni mtu na dada yake; labda wewe Ndiyo unafikiri hivyo, lakini wewe ni ndugu yangu Mimi hata kama nakuchukia vipi kwakuwa umeolewa na Hancy ila nataka nikwambie ukweli ya kuwa Fancy na Hancy siyo ndugu na kuwa makini sana na Fancy kwani siyo mtu mzuri kwa upande wako"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unajua sijaweza kukuelewa" alizungumza Mozah na Sikitu alimsogelea na kumwambia.



    "Fancy anamahusiano ya Siri sana na Hancy na Fancy siyo Dada wa damu wa Hancy" aliondoka Sikitu na alikumbuka ya kuwa Fancy alimtaka aseme maneno yao ili kuharibu ndoa baina yake na Hancy na Hancy hatoweza kukubali kuona ya kuwa Kuna ugomvi baina yake na Mozah hivyo atamfukuza mozah na atachukua muda huo kumshawishi amuowe yeye. Sikitu akiwa anaamini kbisa ya kuwa anafanya yote kwaajili ya kuisaidia nafsi yake lakini lah hakuwa hakijisaidia bali kuharibu ndoa ya ndugu yake na kujitengenezea Kaa la moto.



    Mozah alibaki akiwa amesimama pale na akiwatizama wakati huo nao Fancy aliweza kumuona na aliendelea kumshika Mkono Hancy huku wakicheka.



    Hancy alipokuwa akicheka aliweza kumuona Mozah



    Aliutoa Mkono wa Fancy kisha kuelekea mahali alipo Mozah na kumshika Mkono.



    "Hii ni mara ya mwisho Hancy nakuapia ya kuwa hutauacha tena Mkono wangu kwaajili ya kwenda kuushika Mkono wa Mozah.



    Hancy alienda na kutabasamu.



    "Ndo umeamka? Aliuliza Hancy.



    Mozah alitikisa kichwa na kumtazama Fancy aliyekuwa akiwatizama.



    "Leo niliona nisikuamshe kwani inaonekana Jana usiku ulichoka sana" alizungumza Hancy na Mozah hakuwa akimjibu kitu.



    Aliweza kukumbuka maneno ya Sikitu lakini aliona ni upuuzi tu.



    "Huu ni upuuzi nafikiria nini" alizungumza na Hancy aliweza kumsikia akinung.unika.



    "Nini??



    " Hamna alijibu Mozah na kuanza Kuondoka na Hancy.



    Tom akiwa katika pita pita zake aliweza kumuona Fancy akizungumza jambo na Sikitu tena likionekana la Siri sana



    "Hawa wameanza lini kuzungumza?? Alijiuliza Tom na ghafla kwa mbele aliweza kumuona Zawadi.



    " Zawadi?? Aliita Tom na kuacha kuwafuatilia Fancy na Sikitu kisha akaanza kumfuata Zawadi.



    Alipofika alimgeuza na kumuuliza.



    "Wewe" aliita Tom na kumgeuza lakini aliweza kuona aliyeweza kumgeuza siyo Zawadi.



    "Samahani alizungumza Tom na kusema kwanini namfikiria huyu mwanamk alijiuliza na aliweza kupata wazo la kurudi alipofika hakuweza kumuona yoyote yule.



    " Kwanini Leo naona naona vibaya, nafikiri mfalme ataweza kumsamehe Zawadi kwa kumpitishia adhabu ndogo juu yake. Alijiaminisha kihivyo Tom na kuondoka zake.



    "Mozah hicho unachoweza kukifanya usifikiri ya kuwa unamsaidia huyo mtu asigundulike lakini fikiria kuhusu nafsi yako na nafsi ya Hancy hivi unafikiri Hancy atajisikiaje pindi atakapoweza kuusikia ukweli kutoka kwa mtu mwingine tofauti na wewe; ilihali alikubali kupata adhabu zote ili aweze kukuokowa wewe, kama huwezi kuniambia Mimi ukwli basi mwambie hata Hancy ili ajue atakusaidiaje kwani kutaja watu ambao siyo sahihi hakukufanyi wewe uaminike katika ufalme huu na ukumbuke kila mahali Kuna sheria na kanuni zake; nakuomba uzungumze ukweli nani kaweza kukupatia ile cheni" alizungumza Stela na kuondoka zake huku akiweza kumuacha Mozah katika mawazo tele.



    Muda ulikwenda na Hancy alikuwa akirudi ndani, huku akiweza kukumbuka ya kuwa alimuuliza Fancy kuhusu cheni yake.



    "Fancy ile cheni niliyoweza kukukabidhi siku ya kuzaliwa iko wapi??



    " kaka Hancy, ile cheni niliogopa kukwambia ila iliweza kupotea pamoja na ile cheni ya kifalme, nilijua utakasirika Ndiyo maana sikuweza kukwambia" alizungumza Fancy



    Hancy aliacha kuwaza na aliweza kuingia ndani ya chumba chake na kumkuta Mozah akiwa mwingi wa mawazo Hancy aliweza kwenda kukaa upande wa pili kisha akajilaza kitandni na yeye mawazo yakiwa yanamzonga hakutaka kuamini ya kuwa Mozah anaweza akawa anahusikia na tukio lile la kuiba cheni ya kifalme, katika upande wa pili Mozah alikuwa akiwaza atawezaje kumwambia Hancy ya kuwa mama yake anahusika na hilo.



    "Hancy"



    "Mozah"



    Waliweza kuitana kwa pamoja na kila mmoja akionyesha kutaka kusema jambo.



    "Unataka kusema nini?? Aliuliza Hancy.



    " Kuna jambo nataka kukwambia .... Na wewe??? Aliuliza Mozah.



    "Kuna swali nataka kukuuliza" alizungumza Hancy na kusema ila wewe anza kuzungumza.



    Mozah alivuta pumzi ndefu kisha akamgeukia Hancy vizuri na kuvut tena pumzi.



    "Malikia Maua........



    Kabla hajaongeza neno mlango ulifunguliwa na aliingia Malikia Maua aliyeonekana kutoka kwa jasho



    " Mozah binti yangu,alizungumza na kuanza kujichekesha hali iyoweza kumfanya Mozah ashindwe kuzungumza zaidi.



    "Mama unashida gani?? Aliuliza Hancy na kusimama kisha akamfuata mama yake.



    " Hamna; Mozah tunaweza tukaenda kuongea kidogo katika chumba changu sasa hivi" alizungumza Malikia Maua na kuanza safari huku akimtizama Mozah nyuma.



    "Mozah" aliita Malikia Maua na Mozah aliweza kutoka kitandani akiwa anatetemeka baada tu ya kushuka alipiga hatua Tatu lakini kutokana na hofu iliyoko moyoni mwake alijikuta anajikanyaga na kutaka kudondoka.



    "Mozah kuwa makini" alizungumza Hancy na kushindwa kuelewa kitu gani kinaendelea baina yao.



    "Wanashida gani hawa?? Alijiuliza lakini hakutaka kuwaza sana.



    Baada ya muda alionekana Mozah akitoka katika chumba cha Malikia Maua akiwa amepoza sana.



    Aliyakumbuka maneno ya Malikia Maua.



    " Mozah Tafadhali nipe muda kidogo zaidi na nitasema na kuuweka ukweli wazi mwenyewe "



    "Lakini Malikia Maua kwanini unafanya hivi??



    " Mozah yote haya niyafanyayo ni kwaajili ya kuilinda ndoa yangu pamoja na mtoto wangu na heshima ya falme hii hata wewe Kuna wakati utafika na utaweka kila kitu pembeni kisha uipiganie ndoa yako; na Mozah nataka nikwambie ya kuwa wewe ndiye furaha ya mwanangu Hancy; hakikisha uipotezi furaha yake kwani akosapo furaha na Mimi huudhunika zaidi "



    Baada ya Mozah kuweza kuyakumbuka maneno hayo tayri alishafika ndani na Hancy alikuwa akimsubiria.



    "Nilitak kuondoka lakini nilikumbuka Kuna jambo wahitaji kuniambia hivyo nikasema nikusubirie.



    " Ammmhhhh nilikuwa nataka kukwambia tu ya kuwa ukienda huko uendako uniletee chochote kitu' alizungumza Mozah na Hancy alimtizama tu.



    "Una uhakika?? Aliuliza Hancy na kumsogelea Mozah.



    " Ndiyo" alijibu Mozah akiweweseka.



    "La Ndiyo hivyo, kwanini unatetemeka mikono?? Aliuliza Hancy na Mozah alibaki akimtizama tu.





    "Aaauuhh unashida gani wewe?? Aliuliza Tom pasina kumtizma usoni



    " Fancy!! Samahani alizungumza Tom na kumuinua.



    Hancy aliweza kurejesha kumbukumbu zake juu ya alivyoweza kuambiwa na Fancy kuhusu cheni ile.



    Mozah akiwa ndani aliweza kulia sana kwani alijua anafanya makosa kwa kutoweza kumwambia mumewe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa katika hali ile aliweza kuingia Fancy na kumkuta akilia.



    "Fancy., nashindwa kwanini nashindwa kumwambia Hancy ukweli najiona mdhulumaji mbele ya Hancy siwezi hata simama nikamtizama kwa zaidi ya Mara mbili usoni mwake; nahitaji kumwambia juu ya Malikia.



    " hapana huwezi kufanya hivyo " alizungumza Fancy kwa ukali na hatimaye alijishtukia.



    "Namaanisha hupaswi kufanya hivyo kwani hata Mimi mambo yote Yale Malikia aliyoweza kunifanyia sijamwambia chochote kile nipe siku ya Leo na kesho Utamwambia Hancy kila kitu. Alizungumza Fancy akimkumbatia Mozah aliyekuwa analia na kusema leo tu nitasababisha dhoruba na hakuna kati ya wewe na Hancy atakayeweza kuhitaji kumuona mwenzake wala kumsemesha hiyo ni ahadi yangu.



    Hancy alikuwa amechukua vito vya dhamani zikiwemo cheni hereni na bngili za kike kwaajili ya kwenda kumpatia Mozah akiamini ya kuwa Mozah anatamaa na vitu vya thamani.



    Akiwa anaviweka ndani ya kimkoba chake aliweza kutokea Sikitu ambaye alimshika bega na kumlalia katika bega hilo kisha kumwambia.



    "Mozah hawezi ridhika na hivi, kwani atatamani zaidi na zaidi na atajifanya hataki hivi ili asionekane ni mwenye tamaa juu yako, na Kama aliweza kukupa wewe mwili wake ili tu usiweze kuiona ile cheni embu fikiria amewapa wanaume wangapi mwili wake kwa kuficha uhalifu wake usiweze kufika kwa mfalme, tena alianza na Tom.



    Hancy aligeuka na kumshika shingoni Sikitu.



    " unafikiri nitmuacha Mozah na kukufuata wewe, unafikiri nitayaamini maneno yako ?? Aliuliza Hancy na kumwambia.



    "Hii ni mara ya mwisho ukijaribu tena kuongea vibaya juu ya Malikia mtaraji wa Isadora nitakurudisha nyumbani kwenu Isambala ukiwa marehemu.



    Alizungumza Hancy na kuanza Kuondoka.



    " Mozah siyo mtu mzuri kwako na anamahusiano ya Siri na Tom; wote wale wanakufanya tu mjinga " aliropoka Sikitu na Hancy alitupa vitu vile chini kwa hasira kisha akamgeukia Sikitu na kumnyooshea Mkono kwa hasira sana.



    Sikitu aliogopa na kurudi nyuma baada ya kuona Hancy amevimba kwa hasira.



    Aliinama chini na kuokota vitu vyake baadhi kisha akaondoka zake.



    Huku nako alionekana Tom akiwa anatembelea katika kasiri ile ya kifalme huku akiwa mwingi wa mawazo aliweza kugongana na Fancy.



    "Oohh fancy samahani" alizungumza Tom na kumuinua Fancy kisha kutaka kuendelea na safari zake.



    Fancy alijifanya hawezi kutembea na kudondoka chini.



    "Nahisi mguu wangu umeshtuka nenda chumbani kwa Hancy utamkuta Mozah akupe dawa uniletee.



    Tom aliwahi haraka haraka kwaajili ya kwenda kuleta dawa pasina kufikiria wakati huo nao Fancy aliinuka na kujikung.uta kisha akatabasamu na kuondoka zake.



    " huyu siyo mtu mzuri" alizungumza Nzenze na kuwaz kitu gani kinaweza kutokea juu ya Tom na Mozah wakati huo nao aliweza kumuona Hancy akipita na kuelekea chumbani kwake akiwa amejawa na hasira sana.







    "Kipi kinaenda kutokea huko" alizungumza Nzenze na kuanza kumfuata nyuma nyuma Hancy.



    Tom alifika na Mozah alishngaa.



    "Dawa huku ndani??



    "Ndiyo ameniagizia huku"



    "Hapana Hamna dawa mbona huku ila subiri kidogo nina dawa yangu huwa nimeihifadhi cjui kama itaweza msaidia" alizungumza Mozah kisha akasogeza stulli na kupanda kabla hajaweka mguu wa pili vizuri aliweza kuweweseka na kujikuta anataka kudondoka Tom aliweza kumuwahi kwa kumdaka sehemu ya kiuno na kumfanya Mozah alaze kichwa chake katika kifua cha Tom.



    Hapo hapo Hancy aliweza kuingia na kuwaona katika hali ile.



    Baada ya Tom kumuona Hancy aliweza kushtuka na kumuachia Mozah ambaye aliweza kumshukuru ila alishngaa wapi anapoweza kushangaa aligeuka na alikutana uso kwa uso na Hancy.



    "Hancy" aliita Mozah na Tom alishaweza kujua kabisa ya kuwa Hancy ameshikwa na hasira na hawezi kujicontrol tena.



    "Hancy; hatujafanya chochote namaanisha Mozah hajafanya chochote" alizungumza na kumshika Mkono Mozah akimuweka nyuma yake kitendo kile kiliweza mkumbusha Maneno ya Sikitu na kujikuta akitupa kile kimkoba alichoweza kuja nacho na kudondoka chini.



    Alimtizama Tom kwa hasira aliyekuwa amemshikilia Mkono Mozah



    "Unadhubutuje kumshika Mwanamke wangu Mkono mbele yangu?? Aliuliza Hancy na Tom aliuachia kisha akamwambia Mozah kimbia.



    " Hancy!! Aliita Mozah na ghafla Hancy alichukua chupa ya Maua na kuirusha ukutani.



    "Hancy usiwaze chochote cha kijinga na unatambua ugonjwa ulionao usitake urejee katika hali ya mwanzo zi control hasira zako"



    Hancy alizidi kutupa vitu ndani na kumuelekea Tom.



    Alimpiga Tom ngumi na kumfanya adondoke chini.



    "Tom" aliita Mozah na jina lile liliweza kujirudia zaidi ya Mara 7 katika kichwa cha Hancy.



    "Mume wako niko mbele yako na unadhubutuje kumtaje mwanaume mwingine mbele yangu?? Aliuliza Hancy na kumchapa kibao Mozah.



    Mozah alidondokea kitandani na Hancy alianza kumfuata.



    " kitu gani ambacho sikupi au sikuridhishi tukiwa kitandani haya Leo nitakuridhisha alizungumza Hancy na kuvua shati lake la juu.



    "Hancy unashida gani wewe?? Aliuliza Mozah



    " Unaniogopesha eti?? Alizungumza Mozah huku akilia.



    Tom aliamka na kumshika Hancy kwa nyuma.



    "Mozah kimbia nenda kaite walinzi waje wanisaidie Hancy amerudia hali yake ya ukichaa"



    "Ukichaaa!!! Aliuliza Mozah kwa hamaki na Hancy alimsukuma Tom kule kisha akachukua chungu cha uwa na kumpasulia Kichwani.



    Alimgeukia Mozah ambaye alishindwa kupiga hta hatua moja baada ya kuyasikia maneno kutoka kwa Tom ambaye tayari ameshalowa damu.



    " Mimi na kuweka kitandani ili nikuridhishe wewe unatoka na kutaka kwenda kutafuta mwanaume mwingine wa kukuridhisha. Inamaana Mimi sikutoshelezi?? Aliuliza Hancy na kutupa meza karibu na mozah alitizama pembeni na kuona upanga aliuvuta na kuanza kumsogelea Mozah.



    "Ha....ha....Hancy umekuwaje!? Alibaki kuuliza Mozah ambaye hakuwahi kuiona hali hiyo kwa Hancy. Watu walishafika mlangoni na kuanza kugonga wakimtaka Hancy afungue mlango.



    " Mozah aliita Malikia Maua.



    "Kaa mbali naye" alizungumza Mfalme Kantala na kutaka walinzi wafungue mlango.



    "Mozah" aliita Hancy akitaka kumsogelea kwa ukaribu zaidi.



    Mozah alianza kukimbia ndani na kumfanya Hancy apatwe na hasira zaidi.



    "Msizungumze wala kupiga kelele; mtamchanganya Hancy ndani alizungumza Mfalme na wote walikaa kimya.



    Fancy alitabasamu na kusema sasa Mfalme hawzi vumilia kwa ulichoweza kukifanya Mozah wala Hancy hatokutambua tena kwasasa kwani tayari amesharejewa na ugonjwa wake na huwa hapatani na mtu tofauti na Mimi na hiyo itakuwa nafasi yangu Mimi kuingiliwa kimwili na Hancy kisha kuwa mke wa Hancy wakati huo wewe na dada yako mtakuwa kijijini kwenu"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mozah kwanini unanikimbia eti?? Hunitaki Mimi sindiyo unamtaka huyu hapa chini?? Aliuliza Hancy na kuanza kumpiga Tom.



    " Hancy aliita Mozah na kutizama mlangoni ambako palikuwa pamefungwa na Hancy.



    "Hancy aliita Mozah kwa sauti ya utaratibu Sana.



    "Unaniogopesha" alizungumza Mozah akionekana mwenye wasiwasi.



    Hancy aliushika ule upanga na kuutupa chini kisha akaenda kuokota cheni alizoweza kuingia nazo.



    "Mozah nimekuletea vito hivi vya thamani ili usiweze kwenda kumuibia tena Fancy vito vyake; na Fancy ameweza kuniambia Mimi ukweli wote sitopenda tena uende ukachukuwe vito vyake nikaenda kukuletea wewe vito vya thamani lakini umeona havina maana na unakumbatiani na Tom ndani ya chumba changu. Alizungumza Hancy na kugeuka akiwa na sura nyingine alivirusha vile vito vya thamani na kumpiga Mozah sehemu za bega na kumchubua kwa kiasi kidogo kisha damu kuanza kumtoka.



    " ohhh damu; aliuliza Hancy na kuendelea kuyasikia makelele ya mlango.



    "Sitaki kelele alizungumza Hancy na kukamata tena panga lake na kuanza kupiga piga kila mahali huku akionekana kama kichaa.



    Mlango ulifunguliwa na mwanga ulimpiga machoni.



    Hancy alipiga kelele na kuonekana kuzidi kuwa kichaa kwa kuendelea kupiga kelele na kukata kata vitu ndani.



    Walinzi kadhaa waliweza kufika kwaajili ya kupambana naye lakini hawakuweza kumkabili.



    Timo aliinuka nyuma yake na kuweza kuokota kitu kizito.



    " Hancy aliita Mozah lakini tayari alishaweza kuchelew alipigwa na kitu kizito kichwani na aliweza kudondoka chini.



    "Hancy!! Aliita Mozah kwa sauti na kumfuata Hancy aliyekuwa amedondoka chini.



    Malikia alianza kufunga madirisha ya ndani pale.



    " funga madirisha na milango rudishia pazia Hancy asipigwe na mwanga"



    "Ni nani huyo anahusika na huu ujinga namtaka huyo aliyesababisha yote haya" alizungumza Mfalme Kantala kwa hasira sana.



    Baada ya muda kidogo kilionekana chumba kikigungwa na Mfalme Kantala huku kila mtu akiwa njee.



    "Mozah upo salama??



    " kwanini Hancy amekuwa hivyo?? Aliuliza Mozah na Malikia Maua alimtaka waende kuzungumza ndani ya chumba chake.



    "Kwanza tungependa kukutaka radhi kwani hatukuweza kujua ya kuwa Hancy hali yake hii itaweza kumrudia tena. Nilijifungua Hancy akiwa mzima kabisa na mwenye afya nzuri alikuwa vizuri na baada ya kufikisha miaka7 Hancy alikuwa kila akiona mwanga basi huwa anauogopa sana hivyo alikuwa akitoka njee ya kasiri kipindi cha mvua tu siku moja akiwa ametoka njee tulimtafuta sana na tulishindwa kujua wapi kaweza kuelekea, tulimtafuta kwa takribni siku 2 na siku ya Tatu tuliweza kumkuta Hancy akiwa amejificha na kujifunika na majani mengi ili asipatwe na jua lakini Mara hii hali yake ilizidi kuwa mbaya kwani hakutaka hata kelele na alikuwa akipiga kelele akisema wtu waweze kunyamaza tu ilituchukua muda mpaka tukaweza kumrudisha ngomeni tulimfungia katika kile chumba na alikaa huko kwa miaka 4 na alitimiza miaka 10 akiwa hapatani na mwanga wala Sauti yoyote.



    Fancy aliweza kuingia katika chumba kile na Hancy aliweza kuanza kurejea katika hali yake......niliamini amepona kbisa kwani hakuwa akiogopa tena mwanga wajua wala hakuwahi akiogopa kelele, ilipita miaka kadhaa na Hancy aliweza kufungua sungura wake katika banda lake siku moja asubuhi aliweza kutoka katika chumba chake na kutaka kumletea sungura chakula chake lakini hakuweza kumkuta sungura bali alimkuta mbwa akimalizia kumla sungura wake Hancy aliweza kushikwa na hasira na alimuuwa yule mbwa kwa kutumia mikono yake damu ilimtapakaa mwili mzima niliogopa sana na hapo watu walikuja na kuanza kuzungumza tena kwa sauti, sauti zile ziliweza kumdhuru Hancy na alianza kupiga kelele na kuanza kuyaficha macho yake ilituchukua muda kuweza kumkamata na kumrudisha katika chumba kile tena, Fancy aliweza kuingia na hakuweza kuletewa shida yoyote na Hancy japokuwa kwa Mara ya kwanza ilikuwa ngumu kufanya hivyo; sasa nawaza ni kipi umemfanyia Hancy mpaka akawa katika hali ile?? Aliuliza Malikia Maua.



    "Fancy!!!!!! Aliita jina lile na aliweza kukumbuka ya kuwa Hancy alimwambia " Fancy amenambia wewe ndiye uliyechukua vito vyake,pia akakumbuka Tom aliingia ndani ya chumba chake na aliweza kumwambia "Fancy kamuagizia dawa; lakini akakumbuka pia alimuona Fancy akitembea kwa kawaida kabisa"



    "Fancy!!!! Aliita Malikia Maua na kusema.



    " huyu shetani huyu

    Sintamvumilia kwa michezo yake michafu" alizungumza na kuondoka katika chumba chake

    Mozah alisimama na kutaka kumfuata lakini alishangaa baada ya kumuona mtu aliyeweza kusimama mbele yake.



    "Nzenze???? Aliita kwa hamaki



    " atukuzwe binti wa pili wa mfalme wa kijiji cha Isambala "



    "Wewe" alirudia tena kwa mshangao.



    ***** ***** *****



    "Sina imani na Nzenze nina uhakika Kuna jambo aliweza kulificha mbele yangu, kurudi andaaa safari ya kurudi Isadora" alizungumza Mfalme Nuhu na Nzanza aliweza kutikisa kichwa ishara ya sawa.







    Mtabiri Tambitambi aliweza kutazama na kusema wakati umefika sasa ila kwa maombi ya Bi Lunde miungu yetu imeweza kumsikia na imerudisha majibu Mtabiri Tambitambi alitupa kete zake chini na kutabasamu akiwa katika nyumba yake



    Huku nako aliweza kuonekena Bi lunde akiwa katika sehemu wanazoweza kuabudu huku akitaka miungu yao iweze kumlinda mjukuu wake.



    Kwa upande wa Malikia Samela alionekana akijitengenezea nguo zake vizuri.



    "Malikia wangu kila siku unazidi kuwa mzuri tu kitandani"



    Malikia Samela aligeuke na kumtizama Mganga Kipande.



    "Kama haujaweza kumpa Sikitu umalikia kule Isadora basi muuwe Mozah naamini Mozah akifa hakuna msichana mwingne mzuri kumzidi Sikitu"



    "Malikia Samela tukifanya hivyo lazima itahitaji kafara kubwa sana upo tayri kulipia?? Aliuliza mganga kipande na Malikia Samela alikubali akisema hata kama ni kwa kifo chake.



    ****** ******* ******.



    Alionekena Sikitu akipanga nguo zake na Fancy aliweza kumfuata



    " unafanya nini??

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kilichoweza kunileta hapa ni Hancy kama Hancy mwenyewe ndo huyo kichaa nakaa hapa kufanya nini?? Aliuliza Sikitu.



    " kwahiyo Unataka kuondoka zako?? Aliuliza Fancy.



    "Ndiyo naondoka"



    "Unafikiri nani anaweza kukuruhusu wewe uondoke!?



    " hakuna aliyeweza kuniambia Mimi nije hapa wala hakuna mtu atakayeweza kuniambia Mimi nisiondoke hapa"

    Alizungumza Sikitu na ghafla alihisi Kuna kitu kimeweza kuingia katika mgongo wake.



    Aligeuka na alikutana na Fancy Akicheka.



    "ukiondoka ukiwa hai sina uhakika kama utaweza kutunz Siri yangu, nanikwambie tu nilikuwa nakutumia wewe ili uweze kuwaweka mbali Hancy na mozah kisha Mimi niwe na mahusiano naye"

    Alitoa kisu na kumchoma tena Sikitu huku akiwa anacheka.



    Aligeuka nyuma na macho yake yaliweza kukutana uso kwa uso na Baba yake Kisude aliyeweza kumwambia



    "Huku umefika mbali sana huyo unayemuuwa ni binti wa kwanza wa mfalme wa kijiji cha Isambala sidhani kama kesi yake inaweza isifuatiliwe kwa umakini kama jinsi ulivyoweza kumuuwa mdogo wake na Zawadi, na kumdanganya Zawadi kwamba upo na mdogo wake na siku akitambua ulishamuuwa basi itakuwa mbaya sana kwani Zawadi anasiri zko nyingi sana nani mbaya kwa upande wako Zawadi kuwa adui wako



    "Usijali kuhusu hilo kwani baada ya siku mbili utakuwa Mfalme na Mimi nitakuwa mtoto wa mfalme na Hancy ataendelea kuwa Mfalme mtaraji tu"



    "Kivipi" aliuliza Kisude.



    Na Fancy alimuuliza.



    "Huwezi nisaidia kuja kuibeba hii maiti tukaitupe au mpaka nikamatwe"



    Wakiwa pale waliweza kusikia vishindo nani Malikia Maua alikuwa akija eneo lile.



    Kuna mtu anakuja huku walianza kumficha Sikitu lakini kabla hawajaweza kumficha vizur tayari alishaingia Malikia Maua



    "Umemuuwa Sikitu?? Aliuliza kwa hamaki na kabla hajamka pale alipokuwa akimtizama Sikitu aliweza kupigwa na kitu kizito kichwani mwake àlidondoka na damu zilianza kumtoka ghafla alitulia kabisa



    Fancy aliinama na kumpima pumzi.



    " hii ni mbaya kwani huyu ni Malikia wa hapa na mke kipenzi wa Mfalme Kantala"



    Walibaki wakitizamana tu na muda kidogo alionekana Mozah akiwa anamtafuta Malikia.



    "Mmenionea wapi Malikia Maua?? Aliuliza Mozah na wafanyakazi wote waliweza kusema hawajamuona.



    " alisema anaelekea kwa Fancy, mbona Hamna mtu katika chumba kile?? Alijiuliza na hatimaye alimuona Fancy mbele yake



    "Fancy Malikia Maua yuko wapi???



    Fancy alishtuka sana na akamuuliza kwa wasiwasi.



    " Sijakuelewa "



    "Nimekuuliza Malikia yuko wapi, kwamaana aliniaga anakuja chumbani kwako"



    "Hapana sijapata kumuona kabisa wala hajaja chumbani kwangu" Alizungumza Fancy na kuondoka akiwa anawasiwasi.



    "Fancy" aliita Mozah na kumsogelea Fancy akionekana mwingi wa hasira.



    "Kuna jambo aliloweza kuniambia Hancy na nimeshindwa kumuelewa; alikuuliza swali lolote lile juu ya ile cheni uliyosema Malikia Maua alikuwa anakutaka wewe uilete chumbani kwangu?? Aliuliza Mozah na Fancy alijibu kwa wasiwasi.



    " hapana" aliongea kwa harak na kurudi zake ndani.



    "Sawa endelea kujifanya ya kuwa wewe ni mtakatifu na ninakuonyesha kwanza nimpate mahali ulipoweza kumpeleka Malikia Maua.



    Ilipoishia ni baada ya Mozah kula kiapo ya kuwa atapambana na Fancy pale atakapoweza kumpata Malikia Maua.



    Nzenze sijapata kumuona Malikia Maua lakini nakumbuka ya kuwa mara ya mwisho alisema lazima aelekee kwa Fancy, na pia nimeongea na Fancy anaonekana mwenye wasiwasi sana hapa nawaza atakuwa amempeleka wapi Malikia Maua??



    "Mnaongelea nini hapa?? Aliuliza Tom ambaye hakuweza kuelewa kinachoongelewa pale.



    Mozah alimtizama tu bila kusema neno.



    Baada ya muda alionekana akilitaja jina la Fancy kwa hasira.



    " kumbe yeye ndo chanzo cha yote haya yeye ndiye chanzo cha kila kitu; sitamuacha mzima naapa"



    "Tom, hata Mimi natamni kumpoteza kwa haraka zaidi lakini nahofia kwasababu bado hatujaweza kutambua mahali alipoweza kuwepo Malikia hivyo kitu cha kwanza ni tumpate kwanza Malikia Maua.



    Nzenze alikubaliana na Mozah na sasa akabaki Tom tu aliyekuwa na mashaka.



    " nawaza sana juu ya Hancy sasa, ameshaweza kugeuka na kuwa kichaa nafikiri hata hili nalo liko juu ya mpango wa Mozah na Mfalme anamuamini sana Mozah hata tukiongea lipi hawezi kutuafiki kwasababu hataweza kutuamini afadhali Hancy angekuwa katika hali yake ya kawaida.



    "Mimi nitamrudisha Hancy katika hali yake" alizungumza Mozah



    "Mozah si kirahisi hivyo kama uongeavyo akishashikwa na hali hiyo huchukuwa miezi hata 9 kuweza kupona na ninahofu kubwa sana kwani siku zake za kukaribia kutawadhwa na kuwa Mfalme ni siku baada ya kesho sidhani kama itawezekana hilo, ila nahisi naye huyu Mjomba wake Kipande kuna jinsi anahusika kwani mara nyingi anaonekana kuwa kama mtu mwenye tamaa za madaraka. Alizungumza Tom.



    " Kipande siyo Mjomba wake bali Baba yake mzazi na hilo ndilo kosa pekee lililoweza kumfanya Malikia Maua atumikishwe katika kuiharibu ndoa ya Hancy na Mozah" Wote waligeuka na walikutana uso kwa uso na Zawadi.



    Zawadi aliitoa heshima yake kwa Mozah pamoja na Tom. Aliyekuwa akitabasamu tu na kusema.



    "Zawadi, aliendelea kutabasamu na Nzenze ndiye aliyebaki akishangaa



    " we... We......we si umeshakufa nilishuhudia kabisa ukizikwa na Fancy "



    "Eeeeeeeee" alizungumza Mozah na kumtazama Zawadi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Amezikwa aliuliza Tom kwa mshangao.



    " nimezikwa aliuliza hata Zawadi ambaye hakumuelewa nzenze.



    "Ndiye Nina uhakika ni wewe, ila mbona kule ulikuwa mdogo mdogo na hapa umekuwa mkubwa?? Aliuliza Nzenze.



    " Zawadina"!! Alizungumza Zawadi na Tom alimdakia.



    "Unamaanisha yule pacha wako???



    " pacha??????!!!! Aliuliza Nzenze na Mozah.



    Zawadi miguu ilimuishia nguvu na aliweza kudondoka chini.



    "Mbona Mimi sielewi" alizungumza Nzenze na Tom alisema



    "Inamaana Fancy alimkuwa na mdogo wako kwa muda wote huo ndo maana ulikuwa ukifanya kazi chini yake kama ndiyo hivyo kwnini sasa akamuuwa pacha wako hiyo inamaanisha hata wewe huna dhamani tena kwake sasa kabla hajamteketeza mtu mwingine yoyote yule basi nitamteketeza yeye" alizungumza Tom na kuchomoa panga kiunoni mwa Nzenze kisha akaanza safari.



    "Tom" aliita Mozah na kumkimbilia lakini tayari Tom alishaweza kuzamiria jambo lile akiwa karibuni kuingia katika chumba cha Fancy aliweza kuzuiliwa na Zawadi aliyeweza kuja mbele yake na kulala katika kifua chake.



    "Endapo nitakupoteza wewe tena katika maisha yangu basi nitajiuwa mwenyewe baada ya kumuuwa Fancy" alizungumza na kujilaza vizuri katika kifua cha Tom.



    Tom aliutupa upanga wake chini na aliweza kumkumbatia Zawadi huku na yeye alitokwa na machozi.



    Mozah aliweza kujisikia vibaya sana kwa kumuamini Fancy ambaye ndiye chanzo cha mambo yote mabaya katika kasiri ile ya kifalme. Aliweza kuifikiria hali ya mumewe Hancy na kujikuta akilia tu.



    Nzenze yeye alibaki kustaajabu tu inawezekanaje mtu aliyeweza kumuona akizikwa yuko hai tena?



    ***** ****



    Huku nako alionekana Fancy akiwa anazungumza na Mfalme Nuhu ambaye alionekana mwingi wa mawazo na aliyeshindwa kujua afanye maamuzi yapi sahihi.



    "Bab kesho kutwa unatakiwa uachie kiti cha kifalme na umfanye Hancy awe Mfalme najua ndicho kinachoweza kukuhuzunisha kutokana na hali ya Hancy ila Baba nakuhakikishia nitafanya kwa haraka zaidi na upesi mpaka apone Hancy ndani ya siku ya kesho.



    "Yuko wapi Malikia Maua?? Aliuliza Mfalme na kumtolea macho makali sana Fancy ambaye alianza kujing.atang.ata.



    " Mfalme nani amekwambia Mimi nilikuwa na Malikia Maua Leo Mimi sijamtia hata machoni" alizungumza Fancy na Mfalme alimuuita Mfanyakazi aliyekuwa akipita eneo lile.



    "Yuko wapi Malikia Maua?? Aliuliza Mfalme na Fancy alishusha pumzi ndefu sana akijua kuwa Mfalme hakuwa akifahamu jambo lolote lile wala kujua kipi kinachowez kuendelea.





    Ni baada ya Fancy kuweza kutambua ya kuwa Mfalme hajui chochote kile.



    Sasa aliamini amebakiza siku moja tu kabla ya mipango yake kutimia.



    Wakati huo nao shida iligeuka kwa Mozah, Zawadi; Nzenze pamoja na Tom waliokuwa wakimtafuta Malikia Maua katika kasiri ya kifalme mwishoni walikutana katikati na kila mmoja hakuwa anajua mahali Malikia Maua alipo.



    "Tufanyaje sasa?? Aliuliza Mozah akiwa hajui kipi cha kufanya.



    Wakiwa eneo lile wakiwa wanajadili juu ya Malikia Maua aliweza kupita Fancy na aliwaona.



    " wameweka kikao chanini hawa?? Alijiuliza na kusogea mbele pale walipo



    "Zawadi!! Aliita kwa mshangao baada tu ya kumuona kwani aliamini ya kuwa Zawadi hakuwa na uwezekano wa kutoka katika gereza aliloweza kufungiwa.



    " imekuaje uko hapa??? Aliuliza na Zawadi alibaki akijiishika nguo yake kwa nguvu ili asiweze kuharibu mipango yao.



    "Nakusalimu binti wa Mfalme alizungumza na kuweza kukilaza kichwa chake chini.



    " mbona uko hapa?? Umetokaje kule???



    "Malikia Maua ameweza kunitoa Leo, baada ya kugundua ya kuwa sina hatia" alizungumza Zawadi na kumfanya Fancy ashtuke kidogo.



    "Malikia??? Aliuliza kwa kurudia



    " ndiyo "



    "Yuko wapi?? Aliuliza baada ya kutoweza kumuelewa Zawadi.



    " ameondoka hapa na kuelekea katika chumba chake " alizungumza Zawadi na watu wote walibaki wakimshangaa.



    "Unasema?? Aliuliza kwa hamaki na kwasauti ya juu.



    "Mbona umeshtuka hivyo, kun tatizo kwani?? Aliuliza Mozah na Fancy alibaki kinywa wazi.



    " ammmhh hata na hivyo; embu wewe kijana twende nikupeleke kwa Malikia kwani kuna kazi anahitaji umfanyie" alizungumza Mozah na kuondoka na Nzenze.



    Hali hiyo ilimchanganya sana Fancy na alikumbuka yeye ndiye aliyeweza kumpima na kugundua ya kuwa apumui.



    "Au alijifanya ya kuwa hahemi?? Alijikuta akijiuliza kwa sauti na Zawadi aliweza kulinasa neno hilo.



    " mbona unazungumza mwenyewe aliuliza Zawadi akiwa anamtizama kwa hasira sana Fancy.



    "Hapana" alijibu Fancy na kutoka eneo lile haraka haraka.



    Baada tu ya kuondoka Zawadi aliweza kuachilia kilio cha kwikwi na Tom alijisogeza karibu na kumkumbatia kisha kumlaza katika kifua chake.



    "Jizuie hivyo hivyo, mpaka tufahamu wapi alipoweza kumpeleka Malikia Maua; pia umetumia njia nzuri sana kwani Fancy ataelekea hiyo sehemu aliyoweza kumpeleka Malikia Maua.



    " Nzenze inabidi tufanye kazi ya ziada na kwa haraka sana kwanza kamtafute mama Stela yeye pia anaweza kutusaidia kwa hili" alizungumza Mozah na Nzenze alitikis kichwa.



    "Lakini kwanini ukasema ya kuwa Malikia Maua ananitaka Mimi wakati wote hatui mahali Malikia Maua alipo?? Aliuliza Nzenze



    "Na ndiyo maana nakwambia tunamuhitaji Mama Samela" alizungumza Mozah na Nzenze alitoa heshima kisha akaondoka.



    ******* ******** ********



    Uku nako katika kijiji cha isambala alionekana Mganga kipande akiendelea kufanya yake kwaajili ya kuweza kumtoa uhai Mozah.



    "Malikia Samela sidhani kama tunaweza tukafanikiwa nahisi kabisa kwahili tutashindwa"



    "Na ndiyo neno ambalo silitaki kutoka kwako wewe ni Baba yake kwanini unashindwa kumsaidia mwanao??



    "Sawa ila inabidi tukubaliane na matokea yatakayoweza kutokea" alizungumza Mganga kipande na kuendelea kufanya shughuli zake ila wakati akifanya hivyo Kibonge aliweza kumuona na aliweza kupeleka taarifa hivyo kwa mtabiri Tambitambi.



    "Hivyo wanataka sasa kumuuwa Mozah?? Aliuliza mtabiri na Kibonge aliweza kukubali kwa kutikisa kichwa.



    " tufanyaje sasa?? Aliuliza Mfalme na mtabiri Tambitambi alisema.



    "Katika mji wa Isadora wewe ndiye unayeweza kutegemewa kwani mji huo mkuu ukiingia matatizo basi yataadhiri na vijiji vya karibu, na hiyo itakuwa hata rahisi kwa Mganga kipande kumuuwa Mozah pasina mtu kumuhisi kama ni yeye" alizungumza Mtabiri Tambitambi na Mfalme Nuhu aligeuka na kulitizama jeshi lake la maaskari alioweza kuwaaandaa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa, ila pia nakukabidhi maisha ya binti yangu Tafadhali, muweke katika hali ya usalama alizungumza Mfalme nuhu na kuanza safari ya kuelekea katika mji wa Isadora.



    Wakati wakiwa njiani Malikia Samela aliweza kuwaona



    Kwani huyu Mfalme anaelekea wapi na jeshi kubwa hivi, au kuna vita?? Lakini mbona hajapata weza kuniambia?? Lazima nifuatilie mpaka niweze kutambua ya kuwa ni wapi anapoweza kuelekea.alizungumza Malikia Samela na kuamua kulifuata jeshi lile nyuma nyuma.



    ***** ****** ********



    " Nashindwa kuelewa hata Mimi hapo" alizungumza Fancy akiwa na Baba yake Kisude.



    Itawezekanaje na Malikia tuliweza kwenda kumtupa mbali sana na kijiji hichi?? Amewezaje kurudi pasina kuwa na farasi kwanza tayari tulishamuuwa" alizungumza Kisude na Fancy alimdakia kwa juu.



    "Siyo tulisha wewe ndiye uliyeweza kumuuwa " alizungumza Fancy na Kisude alimtizama kisha akasem.



    "Kama atanitaja mimi basi hawezi kukuacha na wewe; kwani tulikuwa wote kwa pamoja"



    Fancy alitizamana na Kisude na Kisude akasema.



    "Na je kama hii ni trick wanataka kujua mahali alipo Malikia Maua"



    "Kivipi???



    " nahisi ya kuwa labda tumeshaweza kugundulika ya kuwa sisi siyo watu wazuri katika kasiri hii"



    "Ingelikuwa hivyo basi tungeshakuwa hatuna ulimi sasa"



    "Sidhani kama wanaweza kufanya hivyo shida yao ni Malikia Maua endapo watafanya hivyo juu yetu basi watashindwa kutambua wapi alipo Malikia Maua" alizungumza Kisude ambaye alianza kuhisi kitu.



    Ghafla wakiwa pale waliweza kusikia sauti za wafanyakzi wakitoa heshima kwa Malikia.



    Wote waliweza kukimbilia dirishani na kutaka kutizama kama ni kweli ni Malikia Maua.



    Waliweza kushangaa kwani mavazi aliyoweza kuyavaa ni ya Malikia.



    "Haiwezekani' alisema Fancy na kutaka kutoka njee.



    " unaakili wewe, unatakaje kutoka Njee?? Mimi sitaki matatizo tena?? Alizungumza Kisude kwa haraka haraka.



    "Nataka kwenda kudhibitisha kama ni Malikia Maua kweli?? Nilihakikisha hakuwa akihema alikuwa amekufa itawezekanaje akawa yuko hai tena" alizungumza Fancy akionekana mwenye stress nyingi.



    "Je ukienda na ukikuta ndiye,utafanya nini?? Aliuliza Kisude na kutizama njee ambako Malikia hakuwepo tena.



    Lazima nikamuone na kama ndiye basi nitamuuea kabla hajaweza kufikisha habari hii kwa Mfalme kantala na kila anayejua kuhusu mimi, kwani ni kesho tu kesho ndiyo unatakiwa kuwa Mfalme wa Isadora na Mimi kuwa mtoto wa Mfalme halali wa Isadora mpaka pale Hancy atakapoweza kupona na kuwa Mume wangu na Mfalme" alizungumza Fancy na kutoka ndani ya chumba chake akimtafuta Malikia Maua.



    Akiwa anaendelea kamtafuta alionekana mtu akiwa nyuma yake na akiwa ameshika kisu kwaajili ya kumteketeza.



    Fancy alihisi kitu na aliweza kusimama akiwa katika hali ya uwoga ila wakati anageuka tu tayari mtu yule alishaweza kushikwa na mtu mwingine na kufichwa katika kordo moja ili asipate kuonekana.



    Fancy alivuta pumzi ndefu na kuondoka eneo lile.



    Wakati huo alionekana katika kordo moja Tom akiwa amemshikilia Zawadi na kuushika mkono uliokuwa na kisu.



    Alimshika Zawadi kwa nguvu na kuanza kumvuta huku akiwa amekishika kile kisu.



    "Unataka kufanya upumbavu gani kila kitu tumekipanga vizuri lakini wewe unataka kuharibu mipango yetu, unawezaje kufanya hivyo?? Aliuliza Tom na Zawadi alijitoa mikononi mwake.



    "Kamuuwa mdogo wangu Mimi; kaniulia Zawadina wangu, kamfanya nini mdogo wangu mpaka akamuuwa sitamuacha mzima" alizungumza na kuanza kuondoka

    .

    Tom alifika na kumzuia kwa kuufunga mlango wa chumba chake.



    "Unajua ukifanya hivyo hakutakuwa na tofaut baina yako na yeye; Zawadi hata Mimi Fancy kanifanya mengi mabaya sana lakini navuta subra kwaajili ya kufikia lengo, Tafadhali kuwa na subra" alizungumza Tom na kwenda kumkumbatia Zawadi aliyekuwa analia.



    Wakiwa ndani ya kile chumba kwa njee waliweza kumuona Fancy akihangaika na kuhaha ha-ha.



    "Zawadi husikii raha ukimuona Fancy anavyoyangaika huku na kule" aliuliza Tom akiamini ya kuwa Zawadi aliweza kumuelewa ghafla alisikia mlango ukijigongeza na mbele ya macho yake aliweza kumuona Zawadi akimfuata kwa kisu Fancy.



    Alimkaribia na kutaka kumchoma kisu lakini nyuma yake aliweza kuja Mozah na kumshika mkono ule wenye kisu Fancy aligeuka nyuma na aliweza kuwaona wote wawili.



    Kuna shida gani mbona Zawadi yupo katika hali hii?? Alizungumza Fancy akimtizama Zawadi aliyekuwa amejawa na hasira.



    Zawadi alitaka kuzungumza lakini alizibwa mdomo na Tom aliyekuwa ameshafika eneo lile.





    "Kuna nini? Aliuliza Fancy na Tom alimjibu.



    "Malikia Maua anakuitaji katika chumba chake cha kimalikia"



    "Mimi?? Aliuliza Fancy kwa hamaki na wakati huo kisu sasa kilikuwa mkononi mwa Tom na Zawadi.



    " ahaaaaaaa kelele hizo zilitoka kwa Tom na hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kuzielewa kelele hizo zimetoka wapi.



    Fancy nitakupeleka Kwa Malikia Maua " alizungumza Mozah na kuanza kuonyesha wapi pa kuelekea.



    Tom alimshika kwa nguvu Zawadi na kumrudisha tena chumbani kwake.



    "Zawadi acha ujinga eti" alizungumza Tom na Zawadi alisema.



    "Hata iwaje lazima nitumie hiki kisu....... Alizungumza na kukivuta akiamini kipo mikononi mwa Tom lakini alishangaa baada ya kuona kisu kile tayari kina damu alishusha macho yake chini na hapo alikuta damu zikimtoka Tom tumboni mwake.



    'Tomimo" alijikuta akishngaa na kumuita Tom jina lake kabisa kwa kulirefusha huku nako Mozah akiwa njiani alikuwa anaomba litokee jambo lolote la kumzuia Fancy asiende naye kwani alimtumia mama yake kujifanya ndiye Malikia Maua.



    Ghafla mbele ya macho yake alimuona Mfalme na yeye akielekea katika chumba kilekile cha Malikia Maua.





    Mfalme aliita Mozah kwa mshangao.



    Mnaelekea kwa Malikia Maua?? Aliuliza Mfalme na Mozah alijibu kwa wasiwasi.



    "Ndiyo"



    "Unaumwa au, mbona unatetemeka?? Aliuliza Mfalme kantala akimtizama Fancy aliyekuwa anatetemeka.



    " ha....ha.....hamna" alijibu akiwa anatetemeka.



    "Sawa twende" alizungumza Mfalme kantala na kuanza safari yake tena.



    Ikiwa imebaki hatua kadhaa kabla ya kuingia katika chumba cha Malikia Maua alichokuwapo Samela.



    Alibakisha hatua kadhaa lakini ghafla zilianza kusikika kelele za Hancy.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kuna nini tena?? Aliuliza Mfalme kantala na kuanza kukimbia mbio mbio.



    " Hancy " aliita Mozah na kuanza safari wakati huo nao Fancy alitaka kwenda mahali alipo Hancy lakini aligeuka na kuutizama ule mlango tena.



    Alisimama na kuanza kurudi kwa utaratibu kabisa ili kuweza kutizama kama ndiye Malikia Maua au lah.



    Alisogelea mpaka mlango na kuanza kuufungua taratibu kabisa aliufungua mpaka alipoweza kuumaliza alivuta pumzi ndefu na kuanza kusogeza hatua zake kidogo kidogo.



    Fancy" ilisikika sauti ikiita na Fancy aliogopa sana kwa uwoga kisha akaanza kugeuka nyuma kwa uwoga zaidi



    'Ma.. Ma....Malikia?? Aliita kwa mshangao na mbele yake alimuona Malikia Maua akiwa na damu mwili mzima.



    "Kwanini umeniuwa"



    'Hapana hapana ...hapana " alisema Fancy na kuanza kupiga kelel ghafla alisikia tena anaitwa nyuma alipogeuka alimuona tena Malikia Maua.



    "Ha....ha....pana....... Hapana" alizungumza Fancy na kuanza kupiga kelele.



    Yote Yale yalikuwa ni mawenge hakukuwa na mtu yoyote mbele yake aligeuza safari na kuanza kurudi ndani aliingia ndani ya chumba chake na kuanza kusema hapana hapana hawezi kuwa Malikia Maua lazima nikadhibitishe kesho kama ndiye au lah! Alizungumza Fancy na kujilaza kitandani pake.



    Palikucha asubuhi na maandalizi yalianza kwaajili ya kuweza kumfanya Hancy Mfalme mtaraji.



    "Kuna nini?? Aliuliza Mozah baada ya kuona watu wakipamba maeneo Yale.



    " nini kinaendelea?? Aliuliza Mfalme kantala na mfanyakazi mmoja aliweza kumjibu.



    "Tumepewa maagizo ya kupamba kasiri nzima"



    "Na nani??



    "Na mimi" alizungumza Kisude.



    "Mfalme wangu umesahau ya kuwa Leo ni siku ya kumvika Ufalme Hancy?? Aliuliza Kisude na Mfalme alimjibu.



    "Na unatambua hali ya Hancy ya kuwa hana uwezo wa kuliona jua kwa wakati huu itakuwaje ufanye sherehe hiyo Leo?? Aliuliza Mfalme kantala na Kisude alimtizama na kusema.



    " lazima Hancy hasimikwe Leo kwani ndiyo siku ambayo anatakiwa kupatiwa Ufalme akipewa siku tofauti na Leo basi hatakuwa Mfalme bora "



    Mfalme alikosa cha kuzungumza na kuhema tu



    "Malikia Maua yuko wapi?? Aliuliza Mfalme kantala na Kisude alishangaa.



    " Kwanzia Jana hatujapata kumuona" alizungumza mfanyakazi mmoja na Kisude alianza kuwaza inamaana Jana walipata kumuona nani.



    Alimtizama Mozah na Mozah alimtizama pasina kusema neno lolote



    "Huu ni mtego huu" alizungumza kimoyo moyo na kuanza safari wakati huo nao Fancy alikuwa akikata msitu mdogo uliokuwa karibu na mji wa Isadora na kutizama mbele na nyuma kama kuna uwezekano wa mtu kuwa anamfuata.



    Alidhibitisha hamna mtu na aliendelea na shughuli zake



    Ila nyuma yake alikuwapo Nzenze.



    Katika chumba cha Tom alionekana Tom akiwa amejilaza kitandani huku chumba kikiwa na moshi wa kushoto pamoja na vyungu vilivyokuwa vikitoa moshi huo. Pembeni yake aliluwa Zawadi aliyekuwa akimtizama tu na kujiuliza saa ngapi anaweza akaamka.



    "Tom aliita Zawadi na bado hakupata jibu lolote lile kutoka kwa Tom.



    " Tom; unajua nitajisikia vibaya San kama utaendelea kulala hapa chini kwaajili yangu....... Najisikia kuumia sana Tom........ Tafadhali amka" alizungumza Zawadi na kuendelea kulia wakati huo nao alionekana Tom akiyafumbua macho yake.



    "Nakupenda Tom, sitaki ulale hapa kama unavyolala hivyo Tafadhali fungua macho yako" aliendelea kulalama Zawadi ambaye hakuweza kutambua kama tayari Tom alishaweza kuamka na anamsikia kwa kila jambo analoliongea.



    "Tom; endapo ukiamka basi nitakwambia ukweli ya kwamba nakupenda na sitako nikupoteze kwaajili ya ujinga wangu tena,na kama hautaamka alizungumza na kusimama wakati huo nao Tom aliyafunga macho yake.



    " Nitaenda kumuuwa Fancy mara moja" alizungumza na kuanza kuondoka.



    "Zawadi" aliita Tom na Zawadi aliweza kuisikia sauti hiyo .



    "Nimeshaamka usiende tena mahali" alizungumza Tom na kuanza kujiinua.



    "Tom" aliita Zawadi na kumrudia Tomimo.



    "Tom" aliita tena na kuendelea kumpapasa papasa mwili wake.



    "Ahhhhh we vipi, hauoni aibu kunishika shika hivyo Mimi mtoto wa kiume" aliuliza Tom na kutaka kujiinua.



    "Unataka kwenda wapi lala kwanza"



    "Hapana hatuwezi kumuachia vita hivi Mozah mwenyewe lazima tupambane wote" alizungumza Tom na alishngaa baada ya kuona wafanyakazi wengi wakihangaika huku na kule.



    "Kuna nini Leo??



    " Hancy ndiyo siku ya kusimikwa na kuwa Mfalme"



    "Itawezekanaje iwe Leo na wakati hali ya Hancy bado ipo matatani"



    "Nafikiri mchezo mzima huu ilikuwa ni juu ya Ufalme huu Fancy na Baba yake wanataka wamiliki Ufalme"



    "Baba yake??? Aliuliza Tom kwa mshangao.



    Muda kidogo ulienda na alionekana Kisude akiwa na wafanyakazi wachache.



    " kabla hajaweza kunitaja jina langu hakikisha ya kuwa mnautoa uhai wake" alizungumza Kisude na vijana wale walitoa ishara ya sawa kisha wakaweza kuondoka



    "Fancy, siwezi kukubali kukikosa kiti hichi cha kifalme kwaajili yako kwani nimekipambania sana takribani miaka 19, nilipomteka Hancy na kumpa mateso ili tu kusiwe na Mfalme tena na nije niiuchukue Mimi lakini ilishindikana baada ya Hancy kupona ila kwa mara hii hata kama ni kumuuwa Hancy Leo lazima nikichukue kiti hiki cha kifalme" alizungumza Kisude na kujitizama katika kioo kikubwa.



    "Hatimaye nimebakiza masaa machache sana kabla ya kuwa Mfalme wa mji wa Isadora" alizungumza Kisude na kuanza kucheka sana akimini ya kuwa ushindi ni wake na hakuna atakayeweza kumzuia.



    "Mnachokiongea ni nini mbona Mimi sielewi" alizungumza Mfalme kantala na hapo alirudi Nzenze.



    "Wapi amempeleka Malikia Maua?? Aliuliza Mozah.



    Nzenze alikumbuka ya kuwa baada tu ya kufika mahali alipoweza kufika Fancy; basi Fancy alianza kushangaa na kusema ya kuwa haiwezekani wakawa hai nahakika walikufa wote wawili.



    " wawili??? Aliuliza Tom na kushangaa.



    "Huyo wa pili ni nani??? Aliuliza Mozah.



    " ngoja mbona siwaelewi nani kafa?? Aliuliza Mfalme kantala ambaye alishindwa kuelewa ni kipi kinaendelea.



    "Inamaana mtu wa pili lazima awe Sikitu" alizungumza Zawadi na wote walimgeukia.



    Muda ulifika na alionekana Mfalme kantala akiwa amekaa katika kiti chake cha Kifalme huku akiishika mikono yake kwa hasira pembeni yake alikaa Kisude na upande mwingine alikaa Fancy.



    "Ndugu wana kijiji wa mji huu wa Isadora Leo ninafuraha kubwa sana kwani ni siku ya kuweza kumsimika mwanangu Hancy kuwa Mfalme wa mji huu; hivyo basi naomba tule na tunywe kabla hatujaanza utaratibu huo. Alizungumza Mfalme kantala na kukaa chini.



    Wakati huo nao Kisude alikuwa akicheka tu akiamini Ufalme ni wake.



    Alimtizama Fancy na kumpa ishara ya amfuate.



    Walitoka pembeni na Kisude alimuuliza



    " ulienda wapi?? Aliuliza Kisude.



    "Malikia wala Sikitu pale tulipoweza kuwaficha hawapo hivyo kabla mambo hayajaweza kuharibika basi tuharakishe kuuchukua huu ufalme" alizungumza Fancy na Kisude alimwambia.



    "Unauhakika ya kuwa hawajamchukua hao waliokuwa wakikufuatulia nyuma??



    " wakina nani hao??



    "Huu ulikuwa ni mtego wala siyo kweli ya kuwa Jana tulimuona Malikia Maua hakuwa yey"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unamaanisha wameshaweza kunitambua?? Aliuliza Fancy kwa hamaki.



    " kabisa" alijibu Kisude na kumwambia.



    "Sihitaji kuukosa Ufalme huu kwaajili yako hivyo hakikisha huniletei madhara katika hili" alizungumza Kisude na kuondoka zake



    "Wamenionaje"



    Wakati huo nao alionekana Mozah akiikifungua chumba anachokaa Hancy kwasasa kwaajili ya kwenda kuzungumza naye"



    Alivua viatu na kutembea taratibu pasina kupiga kelele na pia alihakikisha ya kuwa hakuna mwanga wowote ule utakaoweza kupenya na kuingia ndani.



    "Hancy". Aliita kwa utaratibu na kukaa pembeni ya Hancy aliyekuwa amejikunyat zake



    " Hancy " aliita tena na kutaka kuzungumza naye jambo lakini kabla hajasema lolote lile mlango uliweza kufunguliwa kwa nguvu na kuingiza mwanga kule ndani .



    Hancy alianza kuweweseka kwa kupiga kelele za huku na kule.



    Njee alionekana Fancy ambaye alitabasamu na kuondoka zake.



    Fancy aliita kwa hasira Mozah huku akiendelea kupambana na Hancy aliyekuwa analeta shida kwaajili ya ule mwanga.



    Ghafla Hancy aliweza kumsukuma Mozah na Mozah alidondoka chini kisha kimya kikatawala.



    Huku nako katika kiti cha kifalme Mfalme aliweza kufuatwa na Kisude kisha kumtaka amtangaze yeye kama Mfalme kwani Hancy hana uwezo wa kupona tena.



    "Siwezi kukupa Ufalme wangu" alijibu Mfalme kantala



    "Sawa basi hutaweza kuuona mwili wa mke wako wala huyu mtoto wako" alizungumza Kisude na Mfalme kantala alimtizama.



    Alipewa ishara ya kukaa kwenye kiti kisha akakaa tena na kumtizama Kisude.



    Kisude alimpa ishara ya aongee.



    Mfalme alinyoosha mkono na NGOMA Zote ziliweza kuachwa kupigwa.



    "Umefika muda wa kumtawadha atakayekuwa Mfalme baada yangu" alizungumza Mfalme na Kisude aliendelea kutabasamu huku akimtizama Fancy aliyekuwa amefika eneo lile.



    Mfalme alitoa kofia lake la kifalme na kuanza kwa kusema



    "Kwa kuwa mwanangu hali yake siyo nzuri basi nitampa Ufalme kwa muda kwanza Mjomba wake Kisude na hali yamwanangu itakapo tengamaa basi Ufalme huu utarudi tena kwake" alizungumza Mfalme kantala akiwa na hasira juu ya Kisude



    "Haaaaa" wanakijiji ndiyo waliyobaki wakishangaa.



    Mfalme alianza kupiga hatua za kusogea mbele lakini mzee mmoja aliweza kukataa.



    "Siku ya Leo ilikuwa kwaajili ya Hancy kama atavikwa mtu mwingine Ufalme kwa siku ya Leo basi mji huu utatapaka damu"



    "Lakini Hancy anaumwa" alizungumza Kisude na alisikia sauti nyuma Yake.



    "Ila pia ameshapona" alizungumza Hancy ambaye alitokea nyuma ya Kisude na kumpita alitoa heshima kwa Baba yake na kuweza kupokea kofia ile ya kifalme.



    Aliivaa kisha akageuka na kumtizama Kisude



    "Kwanzia sasa Mimi ndiye Mfalme wa Isadora. Kisude pamoja na mwanao Fancy mnahukumiwa kunyonga walinzi kamateni hao na mkawanyonge"



    Kisude alicheka na kumwambia.



    Walinzi wote wapo chini yangu Leo ni siku yangu tu lazima niwe Mfalme.



    "Sidhani kama hilo litawezekan" alizungumza Mfalm Nuhu aliyekuja na maaskari zake walikwisha washindwa walinzi wote wapinzani na kuwabeba baadhi yao.



    "Mimi sijafanya chochote alizungumza Fancy na ghafla alisikia sauti ikimtaka anyamaze.



    Alikuwa akija Sikitu huku akiwa amembeba Malikia mgongoni mwake aliyekuwa tayari amekwisha fariki.



    Wewe na Baba yako ndiye mliyeweza kumfanya Malikia Maua hivi" alizungumza Sikitu na kuudondosha mwili wa Malikia akiwa anajikongoja taratibu kabisa wakati huo nao alionekana Mganga kipande akituma kombora lake la kumfuata Mozah.



    Wakati huo nao Mozah alikuwa amesimama pembeni ya Fancy na Zawadi aliyekuwa amemshikilia



    "Kombora lilienda moja kwa moja na kabla halijaweza kumfika Mozah tayari Sikitu alikuwa amesimama mbele ya Mozah na kumbora lile liliweza kumpata Sikitu aliyemdondokea Fancy na kuchomoa kisu alichokuwa amekificha kisha kumchoma nacho



    Wakati huo nao Kisude alitaka kukimbia lakini alipigwa mshale na aliweza kufia pale pale hivyo habari ya Fancy, Sikitu na Kisude zikawa zimeishia hapo



    Huku nyuma nako alionekana Mganga kipande kupigwa na kitu na kuweza kudondoka huku damu zikimtoka naye Malikia Samela baada ya kuona hivyo alianza kukimbia lakini na yeye hakufika mbali alijikwaa na kudondokea kwenye kiski kilichomchoma tumboni



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    MWISHO



BINTI WA PILI WA MFALME - 4

 







    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nitaondokaje na kumuacha Mozah nyuma?? Inamaana sitaweza tena kumpata Hancy?? Hapana siwezi kufanya hivyo lazima nijifiche na nisiweze kuonekana.



    " Kwasabab unampenda Hancy ndo maana hutaki kumuacha sindiyo? Aliuliza Fancy na kupita mbele yake.



    "Fancy" aliita Sikitu kwa mshangao.



    "Nitakusaidia usiende nyumbani kwenu lakini na wewe utanisaidia Mimi kitu kimoja"



    "Kitu gani hicho?? Aliuliza Sikitu



    "Hujanijibu kwanza kama umekubaliana na kile nilichoweza kukwambia? Alizungumza Fancy na Sikitu alionekana kumtizama tu huku Zawadi akishuhudia tukio lile.



    Hancy akiwa chumbani kwake na kuweza kuelekea bafuni huku nyuma alionekana Mozah na yeye akija baada tu ya kuzungumza na baba yake



    " Mozah" aliita Zawadi na kumfuata huku akitizama kulia na kushoto kama Kuna mtu anayeweza kumuona.



    "Usimruhusu Sikitu abaki hapa namaanisha fanya kila njia ila Sikitu aondokee katika ufalme huu"



    "Kwanini?? Aliuliza Mozah lakini Zawadi alishaweza kuondoka.



    "Unamtafuta nani?? Aliuliza Tom.



    " Zawadi lakini......... Basi tu alijibu Mozah na kuondoka zake



    Tom alimshika Mkono na kumuuliza



    "Amekwambia nini??

    " Hamna" alijibu Mozah na kuondoka huku akionekana ni mwenye mawazo kwa kiasi.



    Tom aliweza kumuona Zawadi akiishilia kwa mbali na akaamua kumfuata.



    Huku nako Mozah aliingia chumbani akiwa na mawazo alitaka kwenda kubadilisha nguo uwani lakini alihisi Hamna mtu hivyo alienda na kufunga tu mlango wa ndani kisha akavua nguo zake na kuweza kubeba taulo kisha kuingia bafuni pasina kutizama kama Kuna mtu au lah kisha akaufunga mlango wakati wote huo Hancy alikuwa na mawazo juu ya kile alichoweza kukiona juu ya Tom na Mozah masaa machache tu yaliyoweza kupita. Hivyo hakuweza kumuona kama Mozah ameingia ndani.



    Mozah aliweza kugeuka akiwa amefungua taulo lake huku nako Hancy aliinuka kutoka katika sehemu ya kuogea na kugeuka na hapo ndipo walipoweza kuonana wote kwa pamoja na kupiga makelele huku Hancy akirudi katika pool lake na Mozah akirudishia taulo lake alijitahid kuvuta mlango lakini haukufunguka.



    "Sijaona kitu" alisema Hancy akitabasamu wakati huo Mozah alikuwa akipiga piga miguu yake chini kwa aibu

    "Hata mimi sijaona" alizungumza Mozah na kuendelea kuvuta mlango.



    "Ngoja nikusaidie"



    "Hapana usiinuke sitaki kuona tena"



    "Hu....hu.....hutaki kuona tena inamaana umeshaona" alizungumza Hancy na kuanza kulia pasina kutoa machozi.



    "Hapana sijamaanisha hivyo Mimi" alizungumza Mozah na kugeuka .



    "Koma wewe angalia huko huko usigeuke" alizungumza Hancy na kuanza kuvuta taulo ambalo hakuweza kulifikia.



    "Ni vutie hilo taulo hapo, na usigeuke kwasababu nimesimama" alizungumza Hancy na Mozah alianza kusogea Karibu yake.



    Na Hancy alilivuta taulo na Mozah lote na kuweza kumuacha katika hali tatanishi kidogo



    Hancyyyyyy...... Aliita Mozah na kufumba macho yake kupitia viganja vyake vya Mkono



    "We umeweza kuniona utaondokaje na Mimi sijakuona? Alizungumza Hancy na kuanza kuzungumza.



    Wakati wote huo Hancy macho yake yaliweza kuwa juu wala siyo kweli kwamba alikuwa akimtizama Mozah



    "Kumbe hapo ndo uko hivyo?? Aliuliza Hancy kwa kucheka na Mozah hakuweza kumuona kutokana na kwamba hata yeye aliyafumba macho yake.



    " Hancyyyyy........ Aliita Mozah na kwenda katika kifua cha Hancy kwaajili ya kujificha.



    Hali hiyo iliweza kumshtua Hancy na kumfanya maneno yote na kicheko kiishe.



    "Mo....... Mo....... Mozah mama" aliita Hancy kwa shida San na Mozah aliweza kumtazama Hancy kisha akagundua hamtazami.



    Mozah aliingia sehemu ya kuogea kisha akasema.



    "Hancy njoo ndani"



    "Ndani wapi??



    " ndani ya sink la maji; tuoge wote"



    "Hapana nimeshamaliza kuoga" alizungumza na kutaka kuondoka Mozah alimshika kisha akamwambia



    "Basi njoo nisugue mgongo" alizungumza na kumvuta Hancy ambaye muda wote alikuwa akitizama juu



    Alikaa katika sink huku moyo wake ukiweza kumuenda mbio.



    "Lakini Mozah...... Aliita Hancy lakini kauli yake iliweza kuishia hapo na kubaki kumtizama Mozah ambaye alikuwa akitabasamu tu.



    "Tafadhali mguu wako toa, namaanisha umekaa sehemu mbaya" alizungumza Hancy na Mozah aliuinua mguu wake mpaka Katika kifua cha Hancy na kuanza kuushusha tena.



    "Mozah.. ...... Tafadhali usiirudishe tena huko" alizungumza Hancy kwa tabu sana kwani tayari ulishaweza kufika mahali ambako hakutaka uendee "



    "Mozah me sipendi hii" alizungumza Hancy na kuinuka.



    Mozah alisimama kisha akamuuliza



    "Vipi kuhusu hii?? Aliuliza na kuanza kumbusu Hancy sehemu za kifua huku akimngata kidogo kupitia meno yake.



    " Na vipi tena kuhusu hii" aliuliza na kuanza kumpiga busu mdomoni Hancy.



    "Au nifanye hivi?? Aliuliza Mozah na kupandisha mikono yake juu akimuonyeshea na kutabasamu kisha kuanza kuishusha chini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Mozah huko usishike nitashindwa kuvumilia tena" alizungumza Hancy na Mozah alimshika kisha akatabasamu kilichoweza kusikika ni kelele tu za Hancy na kuweza kumrukia Mozah mdomoni kwa pupa kisha kuendelea na sehemu Zingine.



    Wakati huko yakiendelea hayo kwa upande huo alionekana mtu akimkamata Zawadi na kumfunga mdomo.



    "Zawadi alifurukuta na kuweza kumng.ata Mkono lakini alishikwa tena



    " Zawadi tulia" ilikuwa ni sauti ya Tom.



    Na akiwa pale aliweza kumuona Fancy anapita hivyo aliweza kumvuta na kuegemea nguzo moja ya nyumba ili wacweze kuonekana.



    Baada ya Fancy kupita Mozah aliweza kuutizama mkono wa Tom ulioweza kumshika sehemu ya kifua wakati huo nao Tom na yeye aliyahis mapigo ya moyo wake yanaenda kasi sana na mahali alipoweza kushika Kuna joto sana hivyo aliweza kutizama na kumtizama Zawadi ambye macho yao yaliweza kukutan na Tom alianza kuachia taratibu kabisa sehemu aliyoweza kuishika na baada ya Mkono wake wote kuweza kutoka aliondoka pasina kusema jambo lolote lile.



    "Uuuwwwhhhh alipiga ukunga mdogo Zawadi na kuweza kujishika kifua chake.



    Palikucha asubuhi sana na Hancy alitoka kwaajili y kwenda kuzungumza na mfalme Nuhu aliyekuwa akitoka katika chumba chake.



    " ahaaaaa Hancy umeshaweza kufika??



    "Ndiyo Mfalme" alizungumza Hancy na Mfalme Nuhu aliweza kumuuliza.



    "Mahali wapi patakuwa salama pa sisi kuweza kuzungumza??



    "Njia ni hii Mfalme" alizungumza na kuongoza njia.



    Wakati huo nao Fancy alikuwa nyuma yao akiweza kuwafuatilia kwaajili ya kuweza kuyasikiliza mazungumzo yao.



    "Nahitaji kujua kama umeshaweza kumfahamu mtu ambaye alihitaji kumuuwa Mozah"



    "Ndiyo nilishaweza kumpata na tayari ameshaweza kurudi kwao; kwahiyo kwanzia sasa Mozah yupo katika hali ya usalama" alijibu Hancy.



    "Una uhakika lakini ya kuwa uliyeweza kumpata ndiye aliyeweza kutenda hayo?? Aliuliza Mfalme Nuhu.



    " Ndiyo; kwamaana kile kisu tuliweza kukikuta katika begi lake na pia mfanyakazi mmoja alikiri ya kuwa usiku ule aliweza kumuona nacho"



    "Lakini Sarah aliweza kukataa na kusema siyo yeye wala hausikii kabisa .......... Hancy nilikuja na cheni yangu na hatimaye siwezi kuiona je umenionea??



    " hapana "



    Mfalme Nuhu alitabasamu na kutoa cheni katika mfuko wa shati wa Hancy.



    "Je hii ni ya kwako??



    " hapana sijachukua" alizungumza Hancy.



    "Lakini nimeitoa ndani ya shati lako



    "Ni kweli lakini sijaiweka Mimi cheni yako Mfalme"



    "Basi utambue ya kuwa aliyeweza kufanya hivyo siyo Sarah bali ni mtu wa karibu sana na Sarah ndiye aliyeweza kufanya hivyo" alizungumza Mfalme Nuhu na kusema



    "Ukiweza kumpata huyu anayesikiliza kile tunachoweza kuzungumza hapa basi huyo ndiye aliyeweza kuhusika" alizungumza Mfalme Nuhu na Fancy alishtuka sana na kuanza kukimbia ili kuweza kutoka katika eneo lile lakini aliweza kupamia kitu na kiliweza kudondoka chini.



    Hancy alitaka kumfuata lakini Mfalme Nuhu alimzuia kisha akamwambia



    "Kati ya wale wote walioweza kuwa Jana mezani na kuweza kunisikia Mimi nikikwambia nahitaji kuzungumza nawe mmoja wao lazima ndiye aliyefika hapa, na huyo ndiye muhusika" alizungumza Mfalme Nuhu na kuendelea kuzungumza



    "Na hutaweza kumlinda mke wako kama hutaweza kuutumia moyo wako na akili yako katika hili"



    Mfalme Nuhu aliondoka na Hancy aliweza kutaja Mozah kisha kuanza kuelekea katika chumba cha Mozah kwa haraka wakati huo nao Mozah alikuwa amelala ili aliweza kuonekena Fancy akiwa ameshika kisu na kusema lazima ufe Leo huna pa kukimbilia.



    Fancy alikuwa amejificha mahali na kumtazama Mfalme Nuhu ambaye aliweza kugeuka alipoweza kujificha Fancy na kusema.



    "Ni vizuri kama utajitokeza kisha tuzungumze kwni najua ujaondoka; ila nimemtoa Hancy tuzungumze wawili" alizungumza Mfalme na kuanza kumfuata eneo alilokuwa Fancy.



    "Hapana siwezi kumuulia hapa, italeta shida katika ufalme huu" alizungumza Fancy na kuweza kutupia kisu chake katika upande mwingine na kutupa chupa upande mwingine hali hiyo iliweza kumchanganya Mfalme na akashindwa kujua wapi mahali sahihi alipo Fancy.



    Fancy aliondoka na mfalme Nuhu alishindwa kumtambua wakati huo nao Hancy aliweza kufika katika chumba chake na Mozah.



    Baada tu ya kufika hakuweza kumuona Mozah kitandani.



    "Mozah......Mozah...... Mozah" alianza kuita Hancy na Mozah alitoka akiwa bafuni.



    "Unashida gani?? Aliuliza Mozah na Hancy aliweza kuja kumkumbatia tu.



    " Hancy nashindwa kuhema eti" alizungumza Mozah na kuchomoa kichwa chake katika kifua cha Hancy.



    "Samahani alisema Hancy na kumtoa Mozah kifuani mwake.



    " Mbona kama machozi?? Aliuliza Fancy na kuanza kumfuta machozi Hancy.



    "Hamna" alijibu Hancy na kumchukua Mozah kisha kwenda kumkalisha kitandani.



    "Mozah aliita Hancy na kumshika mabega.



    "Abeee"



    "Nataka uwe makini na maisha yako na kama Kuna mtu yoyote yule unayehisi ni mbaya katika Maisha yako au atahitaji kukuzuru basi utaniambia" alizungumza Hancy na Fancy Alicheka tu.



    "Unaongea nn wewe eti?? Alizungumza Mozah.



    " Mozah" aliita Hancy na kumshika Mkono tena.



    "Namaanisha eti, Tafadhali wekea makini katika mwili wako na maisha yako,na kama Kuna mtu yoyote............"



    "Sawa sawa sawa........... Nikwambie" alizungumza Mozah na kutabasamu.



    "Lakini Hancy.....unaweza kunambia una shida gani?? Aliuliza Mozah kwa kumtazama Hancy aliyekuwa na mawazo kibao.



    " Hamna" alijibu Hancy na kumtaka Mozah arudi kulala.



    "We unaenda wapi?? Aliuliza Mozah.



    "Nitamsindikiza Mfalme Nuhu mpaka njee kabisa ya mipaka yetu ili lisiweze kumkuta lolote jambo" alizungumza Hancy.



    "Siwezi kwenda na wewe" alizungumza Hancy.



    "Kwanini???



    " Mozah..... Ukiamka asubuhi Tom atakuwa karibu nawe mpaka pale nitakapoweza kurudi"



    "Kwanini?? Aliweza kuinuka Mozah na Hancy alimrudisha tena kitandani.



    Mozah unaweza ukafuata kwanza kile ninachoweza kukwambia na kama kutakuwa na shida yoyote au unahitaji chochote na huwezi kuzungumza na Tomimo basi Utamwambia Fancy akusaidie.



    " Ila Hancy...........CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Lala kwanza, inamaana hujachoka mbona unauliza maswali sana eti" alizungumza Hancy na Mozah alitabasamu tu.



    "Nimechoka lakini baada ya kutokuona kitandani nikaogopa ndo maana niliweza kuamka" alizungumza Mozah na kujifunika na shuka vizuri.



    Hancy aliondoka na kuweza kumuacha Tomimo njee ya chumba cha Mozah.



    Mfalme Nuhu aliweza kutoa amri aitwe Sikitu kwaajili ya kuweza Kuondoka katika falme ile.



    Aliyeweza kutumwa alirudi pasina Sikitu.



    "Yuko wapi?? Aliuliza Mfalme Nuhu na Hancy alifika pale.



    Kisha akazungumza mambo machache na Mfalme Nuhu ambaye alionekana kupanda katika farasi yake.



    " Hancy nakuamini ndo maana nakuachia Sikitu katika mikono yako" alizungumza Mfalme na kuweza Kuondoka zake.



    *** **** ***** ****



    Mozah aliamka na kutoka njee akiwa bado hayuko vizuri.



    Stela aliweza kumuona na kumfuata Mozah kisha akamrudisha ndani.



    "Kwnini unatoka njee?? Alimuuliza na kuweza kumketisha kitandani.



    "Shuka liko wapi?? Aliuliza Stela huku akitizama kulia na kushoto



    " shu....shu.....shuka lipi?? Aliuliza Mozah kwa wasiwasi.



    Stela aliingia bafuni na kutoa shuka ndani ya bafu.



    'Mama unapeleka wapi?? Aliuliza Mozah.



    "Umetumia nini tangu uamke??



    "Sijala chochote lakini kwanini umechukua......... Kabla hajamaliza kuzungumza Stela tayari alishaweza kuondoka na alirudi akiwa na Malikia Maua ambaye alionekana kubeba chakula katika Mkono wake pamoja na baadhi ya vitu ambavyo aliweza kuja navyo katika chumba cha Mozah akiwa na wanawake wawili wa makamo.



    Waliweza kutandika mkeka chini kisha wakamfunika Mozah na kanga aliyoweza kuileta Malikia Maua.



    Baada ya hapo alichukua baadhi ya bangili chache alizoweza kuja nazo kisha akamvisha Mozah pamoja na cheni baada ya hapo alichukua Maua Maua Flani kisha akamwagia baada ya hapo aliweza kupatiwa chakula na kisha akakitoa kijiko kimoja na kumlisha Mozah baada ya hapo waliweza kupiga vigelegele na wote walioweza kubakia waliweza kumrushia Maua yaliyoweza kubaki



    Vigelegele vile viliweza kusikika na Fancy aliweza kuingia ndani ya chumba kile.



    "Kuna nini?? Aliuliza na hakuna aliyeweza kumjibu kwani wote walikuwa busy wakimshughulilia Mozah.



    " Kuna nini?? Aliuliza tena na wakati huu alimuuliza Zawadi.



    "Mozah ameshahalalishwa kuwa mke sahihi wa Hancy, kwahiyo Hancy atatawazwa sasa na kuwa Mfalme siku hizi za Karibuni" alizungumza Zawadi na Fancy alisema.



    "Hapana"



    Wote waliweza kugeuka na kumtazama Fancy aliyeweeza kujishtukia.



    "Hapana usinambie ya kuwa tayari umelala na Hancy... Haaaaaaaa alizungumza Fancy na kuachia kicheko cha umbea.



    "Siamini kweli" alizungumza Fancy kisha akatoa kidani kimoja katika shingo yake na kumvisha Mozah.



    "Mozah inabidi baadye uniambie ya kuwa ilikuwaje mpaka ukalala ulianzaje nataka kujifunza kutoka kwako" alizungumza Fancy na Malikia Maua aliguna kidogo kisha akazungumza



    "Unahakika ya kuwa hujui chochote kama usemavyo, natamani uolewe hapa ili nije nitoe shuka lako"



    Fancy aligeuza macho na kumtazama lakini Malikia Maua aliishia tu kumtazama vile vile.



    "Ammmmhh Malikia kwa kuwa tumemaliza sasa........ Tunaweza tukamtoa hapa Mozah" alizungumza Stela na Malikia Maua alizungumza .



    "Ni kweli maumivu bado atakuwa anayasikia, mkwe wangu Mozah mpandisheni kitandani kisha nitamlisha chakula hichi mpaka kiweze kuisha. Alizungumza Malikia Maua na kutabasamu Fancy alishikwa na hasira na kuweza kusimama kisha akaondoka eneo lile.



    Zawadi Alicheka kimya kimya baada ya kumuona Fancy akiondoka eneo lile.



    "Sawa, nitashughulika na wewe baada tu ya kumaliza kushughulila na Mfalme Nuhu, subiri uone nitakufanya upige magoti na kuniomba msamaha kwa kile ulichoweza kukifanya juu yangu" alizungumza Fancy na mbele aliweza kumuona baba yake kipande lakini kila mtu katika kasiri hiyo walitambua ya kuwa ni Mjomba wake na kuamini ya kuwa ni kaka yake na Malikia wa mji wa Isadora.



    "Nahitaji kuwa Malikia Je unaweza kunisaidia?? Aliuliza Fancy na kipande aliweza kucheka tu.





    "Hatimaye Leo umeweza kujua ya kuwa nina umuhimu katika kukusaidia wewe uwe Malikia wa Isadora" alizungumza kipande na kucheka akimtizama Fancy aliyekuwa akimtizama tu.



    Muda ulienda na masaa yaliweza kupita Hatimaye aliweza kurudi Hancy akiwa na baadhi ya watumishi wake.



    Alipofika tu alikuta Kuna sherehe ambazo alishindwa kuzielewa zilikuwa ni sherehe zanini.



    "Kuna nini huku?? Alijiuliza na kuanza kutembea kwa wasiwasi kwani kila alipokuwa akitembea heshima ziliweza kutolewa zaidi.



    "Ni nini hii?? Aliuliza Hancy na aliweza kuyaona matone ya damu yakielekea katika kordo zinazoweza kuelekea katika chumba chake na Mozah



    " Mozah" alilitaja jina hilo na kuanza kukimbia kuelekea katika chumba akaacho na Mozah



    Aliendelea kukimbia zaidi na zaidi na hapo ndipo alipozidi kuchnganyikiwa kwani damu zilielekea kabisa chumbani mwake na hakuwepo Tom kama alivyoweza kumuacha alipoondoka.



    "Mozah aliita na kwenda kufuungua mlango kwa kasi na hapo ndipo alipobaki akitizama sehemu moja hadi upanga wake kuweza kumdondoka mikononi mwake.



    " Mozah aliweza kuita kwa sauti ya chini kabisa na kuanza kutazama kwanzia chini hapo lilionekana gauni zuri la kitambaa lililoweza kufunika miguu na sakafu ya nyumba ile kwa kiasi kikubwa mkanda kidogo sehemu ya tumboni ulioweza kuli cover tumbo lake. Mikono meupe iliyoweza kupambwa na aina mbli mbali za bangili pamoja na Pete za asili huku shingoni pia kukiwa na vidani vilivyoweza kufanana na baadhi ya bangili za Mkononi hereni zilizoweza kupamba sikio na kitambaa kilichoweza kufungwa kichwani kilichoweza kuendana na gauni lake alikuwa ni Mozah aliyeweza kupmbwa vizuri sana na kupendeza zaidi machoni pa Hancy.



    "Mozah"



    "Ishia hapo hapo n hatua zako

    ....... Alizungumza mama yake Hancy, Malikia Maua na kutabasamu.....huku akimshika Mozah kidevuni.



    "We ni mrembo kweli mwali wangu"



    "Mozah" aliita kwa utaratibu Hancy na kabla hajazungumza alichokuwa akihitaji kukizungumza aliweza kufika Mfalme Kantala.



    "Mwanao amekwisha mtizama mwali wangu, kimila na desturi anapaswa kufanya chochote kile nitakachomuagiza kufanya" alizungumza Mama Hancy.



    "Mila gani hizo?? Aliuliza Hancy.



    'Lakini kama unavyoweza kutambua ya kuwa huyu ni Mfalme mtaraji hakikisha sharti unalotaka kumpa lisiwe ligumu" alizungumza Mfalme Nuhu.



    "Sawa" alijibu Malikia na kumtizama Stela ambaye alisema

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ninampa dakika 20 tu aweze kuoga na kuvaa nguo hizi akiwa katika chumba hichi na mkewe"



    Malikia Maua alimtiza na kusema.



    "Sidhani kama hiyo ni adhabu au ni nafasi ya upendeleo" alizungumza Malikia Maua.



    "Ni mkwe wangu siwezi kumpa adhabu kubwa" Alizungumza Stela na wakaanza kucheka na Malikia Maua kwambalia aliweza kumuona Fancy akiwa amesimama na kuwatizama huku akiwa ni mtu mwenye hasira kali sana.



    "Ni vizuri kama tukiondoka njee alizungumza Stela na wote walitoka njee.



    Stela aliweza kutizama upande ambao aliweza kumuona Fancy lakini hakuweza kumuona tena.



    " itakuwa nimeota au nini?? Alijiuliza lakini hakuweza kupata jibu kabisa aliondoka akiwa na mfalme pamoja na Malikia huku nako Hancy aliweza kujivuta hatua za kivivu mpaka mahali alipo Mozah.



    Altizama kwa ukaribu zaidi na kusema.



    "Mozah,kwa kweli wewe ni mwanamke mzuri sana" aliweza kumpapasa katika sehemu ya kiuno kisha kumgeuza Mozah na kumfanya ampatie mgongo wake.



    Aliweza kuupapasa mgongo wa Mozah ulioweza kuwa wazi na kuanza kuinusa harufu inayotoka katika mgongo huo.



    "Hancy....... Aliita Mozah na kutaka kujitoa katika mikono ya Hancy lakini Hancy aliweza kumzuia na hatimaye aliweza kumgeuzia usoni pake. Alimtizama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kupeleka mdomo wake katika lipsi za Mozah.



    " Hancy Unataka nini?? aliuliza Mozah na kuanza kurudi nyuma.



    "Dakika 20 ni nyingi San kwangu, hivyo naomba tutumie wote dakika 10 alizungumza Hancy na kuendelea kujisogeza karibu zaidi na zaidi.



    " Hancy....... Nimeshapakwa rangi mdomoni utajichafua" alizungumza Mozah.



    "Haina shida alizungumza na kumsogelea karibu zaid.



    " Hancy....... Utaifuta rangi ya mdomo" alizungumza na kumzuia Hancy kwamikono yake.



    "We Mozah kwanini unaniwekea vikwazo vingi hivyo?? Aliuliza Hancy na kumtazama Mozah.



    " Hamna lakini muda unakaribia kuisha jiandae tuondoke " alizungumza Mozah na Hancy alikaa kitandani.



    "Siendi mahali"



    "Kwanini?????



    Hancy alinyoosha mdomo wake akimaanisha ya kuwa anahitaji busu.



    " Hancy lakini"



    "Basi siendi mahali" alizungumza Hancy na kujilaza kitandani.



    "Haya amka" alizungumza Mozah na kutizama kulia na kushoto kama Kuna mtu kisha akambusu Hancy mdomoni kisha kuanza kujitoa Hancy aliweza kusimama na kuendelea kumpiga mabusu mazito na baada ya dakika moja kupita Hancy aliweza kujitoa kisha akatabasamu baada tu ya kumtizama Mozah usoni.



    "Mozah"



    "Abeeee"



    "Ingekuwa hatutoki kwenda njee basi ningemaliza hamu niliyonayo juu yako"



    "Hancy........... Tutafanya hivyo pale sherehe itakopoweza kuisha cha kufanya kwanza ni ujiandae kwani wanatungoja



    Hancy alimbusu tena Mozah kisha akaingia bafuni.



    Sherehe zilianzaa sasa na zilibaki dakika chache sana kabla ya Mozah na Hancy kuingia katika hafla hiyo.



    Fancy alimtizama baba yake na kutabasamu huku akionekana Zawadi akiwa aliyeweza kukosa furaha.



    " Ni Jan tu mliweza kulala pamoja lakini siku ya Leo hamtaweza kufanya kile mlichoweza kukifany kwa siku ya Jana, kwani Mozah Hancy hatokuhitaji tena katika kitanda chake. Alizungumza Fancy na kucheka San na hapo hapo aliweza kutokea Mozah akiwa ameshikwa mkono na Hancy.



    Alijenga Tabasamu la kinafiki usoni mwake kisha akaenda kuwapokea wote kwa pamoja baada tu ya kuingia katika katika yao



    "Kama nilivyoweza kuitenganisha hii mikono na bado wote mkawa na furaha juu yangu Ndivyo nitakavyoweza kufanya na wote hamtaweza kunitilia shaka Mimi " alizungumza Fancy na kumtazama baba yake kisha kuendelea kucheka tu.



    Hatimaye muda ulifika na watu walikunywa na kusaza na sasa muda uliweza kwisha na ukawa ndo mwisho mwisho wa sherehe hiyo.



    Huku nako katika kijiji cha Isambala alionekana Mtabiri Tambitambi akitizama chungu chake na kusema.



    "Sasa utabiri unaenda kukamilika"



    Mozah akiwa anapiga stori mbili Tatu na Tom, Sikitu aliweza kwenda kwa Hancy aliyekuwa akipiga stori na watu wengine.



    Hancy aliweza kukumbuka ya kuwa asubuh ya siku hiyo aliweza kufuatwa na Fancy na Fancy aliweza kumwambia ya kuwa ambembeleze Mfalme Nuhu aweze kumuacha Sikitu katika kasiri yao ili kama Sikitu ndiye aliyeweza kutaka kumuuwa Mozah basi Itakuwa rahisi tena na kwa kipindi hiki kuweza kumkamata..



    Wakati hayo yote yakiendelea Zawadi alibaki kama muonaji tu na hakuweza kupata ujasiri wa kumwambia Mtu yoyote yule.



    "Hancy" aliita Sikitu na kumpatia kinywaji alichoweza kuja nacho.



    Hancy aliweza kukipokea.



    "Kuna jambo nahitaji kukwambia

    ..................... " Mozah anaonekana mtaratibu na mstaarabu machoni pa watu wengi lakini Mimi ndiye ninayeweza kuifahamu tabia yake kwani mm ni Dada yake na nimekuwa naye pamoja"



    "Kwa madai yako?? Aliuliza Hancy.



    " Mozah si mtu sahihi kwa upande wako na ninataka kukwambia ya kuwa amekupatia wewe usichana wake ili uendelee kumuamini zaidi lakini anatoka na wanaume zaidi ya wawili" alizungumza Sikitu na Hancy aligeuza macho yake kumtizama Mozah kisha akayarudisha kumtizama Sikitu na kumwambia.



    "Kwahiyo Unataka nakuamini ya kuwa hata Tom, anamahusino na Mozah???



    " Sitaki huamini kwasasa ili fuatilia kwa ukaribu hata wewe mwenyewe utaweza kugundua hilo " alizungumza Sikitu na kuondoka.



    Huyu mwanamke mshenzi sana anafikiri ya kuwa mm naweza kumuamini yeye. Akiwa anazungumza alikuja Fancy.



    Una shida gani mbona unazungumza mwenyewe???



    "Huyu kichaa aliyetoka hapa ananiambia Mimi ya kuwa Mozah anamahusiano na Tomimo.



    " Na wewe umefikiriaje???



    "Siwezi kufikiria upumbavu kama huo ikiwa Jana tu niliweza kushare mwili mmoja na mke wangu Mozah, siwezi amini upumbavu kama huo wakati mm ndiye niliyoweza kuutoa usichana wake; nikwambie kitu Fancy...... Tomimo namuamini sana labda angemtaja mwanaume mwingine tofauti na Tomimo ndo ningeweza kumfikiria lakini Tom hawezi" alizungumza Hancy na kwa mbali alimuona Tom akija na Mozah eneo lile alilokuwapo kwa kumshika Mkono kiistarabu kabisa.



    "Saa Zingine rafiki yako ndiye adui yako" alizungumza Fancy.



    'Ni kweli lakini mke wangu siyo adui yangu, hivyo hat kama ni kweli siwezi kuachana na Mozah kwaajili ya Tom " Alizungumza na kuweza kumpokea Mozah kutoka kwa Tom.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tomimo......., kama unampango wa kutaka kuniibia Mozah kutoka kwangu basi nakwambia mapema ya kuwa Mozah ni Malikia mtarajiwa hivyo, hupaswi hata kum kumtamani kwa macho" alizungumza Hancy na Tom alijibu



    "Nitaweka tamaa kwa wasichana wengine wote lakini siwezi kuweka tamaa juu ya Mozah kwani ni Sawa na kujiibia mwenyewe" alijibu Tomimo.



    "Umesikia alizungumza Hancy kwa kumtazama Fancy



    " Hancy...... Kwanini umemwambia Tomimo maneno hayo ina maana huniamini Mimi??? Aliuliza Mozah na Hancy aliweza kuupeleka Mkono wake Mozah mdomoni mwake aliiubusu na kitendo kile kiliweza kumuuma roho Fancy.



    "Hapana nakuamini sana tu ila Tom simuamini zaidi kwasabab hata baba yangu mwenyewe anachanganyikiwa na uzuri wako" alizungumza Hancy na Mozah alimtizama tu.



    "Mbona huchek? Alizungumza Hancy na Mozah alimtizama tu.



    " inamaana huniamini Mimi??? Aliuliza tena Mozah



    "Mozah aliita Hancy na kumsogeza karibu zaidi.



    " mke wangu" aliita tena jina jingine kisha akamsogeza nywele zake zilizokuwa zimefika machoni baada tu ya kufungua lemba aliloweza kufungwa.



    "Katika duniani hii mtu gani wa kwanza unamuamini??? Aliuliza Hancy.



    " wewe"



    Basi amini ya kuwa Mimi katika hii dunia mtu wa kwanza ninayemuamini ni wewe kwasababu wewe ndiye unayenijua zaidi hata kuliko mma yangu aliyeweza kunilea kwa miaka 23 siwezi kuacha kukuamini wewe kwani katika mahusiano, jambo la kwanza la muhimi ni uaminifu, pasina uaminifu basi mapenzi yetu hayawezi kufika mbali" alizungumza Hancy na Mozah aliweza kutabasamu.



    "Waooooo hapo tu ndo unaponiuwaga" alizungumza Hancy na Tom na yeye aliweza kudakia.



    "Mimi hapo ndo anaponimalizaga"



    "We Tom wewe, hupaswi kumtazama mke wangu alafu akakufurahisha"



    "Sasa nitafanyaje kama yeye ndo furaha yangu"



    "Unamsikia huyu eeeeeeeee,nitampiga ngumi sasa hivi alizungumza na kumtishia Tom.



    "Acheni utoto bhna" alizungumza Mozah na Fancy alibaki tu akiwatizama.



    Alifika muhudumu akiwa na baadhi ya vinywaji alichukuliwa vinywaji viwili kisha akampatia Tom na Fancy.



    "Hancy unahamu na nini?? Aliuliza Mozah na Hancy alimpa ishara mtumishi yule aondoke.



    Alimsogelea karibu na kumwambia.



    "Nina hamu na wewe" kauli ile hata Tom aliweza kuisikia na kumfanya ateme kinywaji alichokuwa akikinywa.



    "Unashida gani kwani nmekwambia wewe, tena Tom inabidi utafute ka mwanamke kazuri kazuri kama Fancy uweke naye mahusiano ili usije ukaaa hata utamu wa mtu hauufahamu"



    "We kichaa umelewa nini?? Aliita Tom na kumsukuma Hancy.



    " Embu twende ndani" alizungumza Mozah na kumchukua Hancy kisha kuanza kumpeleka katika chumba wanachoweza kulala.



    Fancy alitaka kumfuata lakini aliweza kuzuiliwa na Tom.



    "Kati ya wewe na Sikitu nani kamwambia Hancy ya kuwa Mimi ninamtaka Mozah" aliuliza akiwa hana sauti ya utani ndani yake na akiwa amemshikilia Mkono kwa nguvu Fancy.





    "Sijazungumza kitu chochote kile juu yako" alizungumza Fancy na kutaka kujitoa mikononi mwa Tom.



    "Bora uwe unasema ukweli kwamaana kama utakuwa unazungumza uongo basi sitakuacha usambaratishe furaha ya Mozah na Hancy; hivyo nitakukata kichwa chako pasina mtu yoyote kutambua, baada ya kuzungumza hayo aliweza kumuachia Mkono kisha akanyooka moja kwa moja hadi sehemu aliyopo Sikitu alimshika Mkono na kumvuta karibu na yeye baada ya kuzungumza maneno machache alimuacha na kuondoka.



    Palikucha Asubuhi na alionekana Mozah akijinyoosha kutoka kitandani aligeuza Macho yake na aliweza kumuona Hancy aliweza kutabasamu tu na kuweza kuinuka na shuka kutoka kitandani kisha akaelekea bafuni akiwa amekaa ndani ya sinki la kuogea huku akifurahia mambo ambayo aliweza kuyakumbuka mwenyewe.



    "Unafurahia nini?? Aliuliza Hancy na kuingia ndani ya sinki la maji.



    " Hancy, sijamaliza bhna kuoga" alizungumza Mozah akificha sehemu yake ya juu ya kifua"



    "Embu acha ujingaa kwamaana nilichoweza nilivyo viona jana na juzi siwezi kukisahau hata kimoja. Alizungumza Hancy na kumsogelea karibu Mozah kisha kuitoa mikono yake kifuani.



    Alivuta brash kisha akalipaka sabuni na kuushika Mkono wa Mozah huku akiusugua taratibu taratibu sana.



    " aaaaauuuhhhhhhh" alipiga kelele Mozah na ziliweza kumfikia Fancy aliyekuwa njee ya mlango wa bafu akiwasikiliza.



    "Hancy uko nitajisafisha mwenyewe" alizungumza Mozah na Hancy alianza kucheka.



    "Hancy........ Aliita Mozah kwa sauti na kupiga kelele.



    "Cheza, cheza sana na cheka uwezavyo lakini nakuhakikishia ya kuwa hichi Ndicho kitakuwa kicheko chako cha mwisho Mozah ; sitakuruhusu ucheke zaidi ya hapa" alitoka akiwa na hasira na amevimba sana Stela alimtizama na kushindwa kuelewa ametoka kufanya nini katika chumba hicho hivyo aliamua kuelekea huko aliifungua mlango na alisikia kelele za Mozah pamoja na Hancy wakiwa wanacheka kwa pamoja



    "Sasa mbona huyu ametoka kama vile alikuwa anagombana na mtu huku ndani" alijiuliza lakini hakuweza kujipatia jibu



    Njee ya kasiri ya kifalme alionekana Tom akiwa anamsubiria mtu aweze kupita maeneo aliyoweza kuwapo yeye; kweli punde si punde alionekana Zawadi akipita huku akiwa ameshikilia sinia ikiwa imefunikwa na kitambaa chekundu.



    Tom aliweza kumvuta hadi kwenye kichochoro alichoweza kajificha yeye.



    "Nataka uniambie ukweli jambo gani linaliweza kuendelea katika kasiri hii?? Aliuliza Tom na Zawadi alikuwa akihitaji kujichomoa katika mikono ya Tom



    " nimekwambia sifahamu, kama jinsi wewe hufahamu chochote basi na Mimi sifahamu chochote. Alizungumza Zawadi na kuanza Kuondoka



    "Wewe mm nakusemesha ww unao........."



    Kabla hajamaliza kuzungumza Zawadi aliweza kumrukia mdomoni mwake ili asiweze kuzungumza zaidi kwani kwa wakati huo Fancy alikuwa akipita huku akiwa amefura kwa hasira"



    Tom alibaki akikodoa macho tu kwani hata maneno hayakuweza kumtoka.



    Baada ya Fancy kupita pasina kuwatambua Zawadi alijitoa mdomoni mwa Tom na kuondoka zake.



    "Mungu wng; Mungu wangu; huyu mwanamke kanifanya nini eti yani busu langu la kwanza" alikuwa akijizungumzia Tom moyoni huku akiwa ameshika mdomo wake



    "Siamini kama busu langu la kwanza limepotea kirahisi namna hii" alikuwa akizungumza Zawadi huku akishikilia vizuri sinia lile lisiweze kudondoka.



    Mozah akiwa anazunguka katika kasiri ya kifalme Malikia Maua aliweza kumuita na Mozah aliweza kumfuata kisha akaingia katika chumba alichoweza kuitwa.



    Alifika na kukaa kisha Malikia alitoa moja kati ya cheni zake za dhahabu na kuweza kumvisha Mozah shingoni.



    "Unaonaje hii cheni imekupendeza siyo? Aliuliza Malikia na Mozah aliweza kuitika ishara ya Ndiyo na kutaka kuivua



    " hapana Haina haja nimekununulia wewe" alizungumza Malikia



    "Ahsante mama" alijibu Mozah na Malikia alimwambia unaweza kwenda sasa.



    Mozah aliondoka na kufunga mlango hapo hapo Malikia aliweza kudondoka chini na kuanza kulia pasina kutoa sauti huku akisema Mozah nisamehe sina jinsi siwezi kumpoteza mume wangu pamoja na mwanangu, kwani nisipofanya hivi Kipande atamwambia ukweli wote mume Wang " alizungumza Malikia Maua



    Wakati Mozah anaondoka tu Fancy Alicheka sana kisha akasema mchezo ndo unaanza.



    Baada ya dakika kadhaa kupita Mozah aliweza kutoka katika chumba chake na hapo aliweza kuona watu wengi wakiwa eneo linaloweza kufanyikaga mkutano.



    .Hancy aliweza kumfuata na kumshika Mkono kisha kumuelekeza mpaka mahali alipohisi ni sahihi kwa yeye kusimama na Mozah.



    "Samahani kwa kuweza kuwaita hapa ni kwamba nimeweza kupotelewa na cheni yangu na nimejaribu kuitafuta katika kila chumba cha kasiri hii lakini bado sijapata na Cheni yenyewe ni Babu Mfalme aliyeweza kumkabidhi mkewe"





    "Ngoja unaongelea cheni gani wewe?? Aliuliza Mfalme na kusimama.



    " cheni niliyoweza kukupatia?? Aliuliza mfalme Kantala



    Fancy alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo.



    'Mpumbavu wewe, haraka sana cheni hiyo iweze kutafutwa na atakayeweza kupatikana nayo inafahamika ni ipi adhabu, atakatwa Mkono kama mila na desturi zinavyosema" alizungumza Mfalme Kantala na Mozah akiwa anapepesa pepesa macho aliweza kukuta macho ya Malikia yakimtizana kwa huzuni kabla hajafumbua chochote kile Fancy aliweza kuita



    "Mozah"



    Watu wote waliweza kugeuza macho yao kwa Mozah



    "Wewe ndo umeiba cheni yangu????



    "Nimeiba?? Aliuliza Mozah na kutazama shingoni pake alipoweza kumtizama Malikia Maua hakuweza tena kumtizama usoni.



    " Mozah nani kakupa hiyo cheni??? Aliuliza Mfalme Kantala.



    "Cheni?? Aliuliza Mozah na kuishika ile cheni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Mozah nani kakupaa hii cheni, najua huna uwezo wa kuichukua, nani kakupatia hii cheni?? Aliuliza Hancy na Fancy na yeye aliingilia kati.



    "Nani kakupa hii cheni Mozah?? Aliuliza Fancy



    " najua huna uwezo wa kuiba; nambie nani kakupa cheni hii?? Aliuliza tena Fancy.



    Mozah alimtizama Malikia Maua pasina kusema neno lolote lile.



    "Mimi ndo niliweza kuiokota hivyo sikudhani kama inadhamani namna hiyo, Ndiyo nikampatia Mozah, kwahiyo kama Kuna adhabu naomba iwe juu yangu binti yangu hausiki" alizungumza Stela na Fancy aligeuka kisha akamtizama kwa hasira sana.



    "Hapana" alizungumza Mozah na kusema.



    "Mama yngu hausiki kwa hilo muhusika wa hilo ni Mimi mwenyewe"



    "Mozah" aliita Hancy kwa mshangao na alijikuta tu Mkono alioweza kumshika nao Mozah ukidondoka.



    Hakuna mtu katika kasiri ile aliyoweza kuyaamini maneno ya Mozah



    "Hivyo naomba adhabu iwe juu yangu" alizungumza Mozah na kumtazama Malikia Maua ambaye alishindwa kuzungumza kitu na kubaki machozi tu yakimtoka.



    "Mfalme wangu, naomba umsamehe Mozah kwani hkuweza kufahamu ya kuwa atendalo ni kosa alizungumza Fancy huku akichekelea moyoni.



    " Naweza nikawa mjinga lakini siyo mpumbavu, Mozah hafahamu mahali zinapokaa Hadhina za kifalme, hivyo Hancy...... Kwnini umeweza kuchukua cheni hiyo pasina ruhusa na kumpatia Mozah?? Aliuliza Mfalme Kantala na kumgeuzia upande Hancy.



    "Hapana Hancy ahusiki na chochote kile" alizungumza Mozah.



    "Mozah, ni sawa acha tu watu watambue ya kuwa Mimi ndiye niliyefanya hivi huna haja ya kunifichia haya" alizungumza Hancy.



    "Hapana mm Ndiyo muhusika"



    "Hapana huusikii kwasababu kama ungekuwa umeiiba basi usngeweza kuivaa hadharani.......Mfalme nisamehe Mimi kwasabab niliweza kuifuata amri ya Hancy na kwenda kuchukua mkufu huo pasina kufikiria dhamani ya mkufu huo" alizungumza Tom na kuomba adhabu iwe juu yake.



    Fancy alishikwa na hasira sana kwani mpaka hapo sasa hat iweje Mozah hawezi kuwekwa tena katika makosa.



    "Wote ambao hamuuhisiki na familia ya kifalme mnaweza mkaondoka Hancy na Tom mtapata adhabu kutokana na hiki mlichoweza kukifanya; wote nifuateni katika chumba cha Siri"



    Mfalme Kantala aliongoza mwendo na Hancy aliweza kushikwa na Maaskari wawili pamoja na Tom kisha kupelekwa katika chumba cha Siri ambacho huweza kutolewa adhabu.



    "Mozah" aliita Stela na kumshika Mkono kisha Kuondoka naye.



    Malikia Maua aliondoka akiwa mnyonge sana huku akimtizama kwa hasira sana Fancy pamoja na Kipande



    "Aaaaahhhh alipiga kelele Fancy na kutupa glassi.



    Hili umelikwepa lakini nahakika nitapoteza furaha yako mazima hata kama ni kwa kuchukua maisha yako



    Ni baada ya Fancy kuweza kukasirika baada ya kuona mitego yake yote juu ya Mozah imeweza kuteguka.



    Mozah akiwa ndni ha chumba chake Malikia Maua aliweza kuingia na kumtizama tu Mozah.



    "Mozah itakuwa vizuri kama utarudi nyumbani kwenu kwamuda kwanza kisha baada ya muda kadhaa mambo yakiwa sawa nakuahidi ya kuwa nitakuj kukuchukua lakini kwa sasa rudi" alizungumza Malikia Maua na kuanza Kuondoka.



    "Kwanini ulinipatia cheni ambayo ulifahamu kabisa ya kuwa nikiwa nayo lazima iniletee matatizo?? Aliuliza Mozah na Malikia Maua alisit kupiga hatua lakini baada ya kuvuta pumzi ndefu aliongeza hatua.



    "Unajua kwaajili yako Hancy pamoja na Tom wameingia kwenye matatizo na ikitokea Hancy pamoja na Mfalme Kantala wakigundua ya kuwa ww ndiye umeweza kuniptia cheni ile basi wataghafilika juu yako, cyo wewe tu bali hata ufalme mzima"



    "Sawa fanya vile utakavyo" alizungumza Malikia Maua na kutoka njee.



    Baada ya Kuondoka tu alionekana Fancy akizungumza.



    "Endapo Mozah atamwambia Hancy basi mchezo wangu hautaweza kufika mbali. Aliingia ndani na kumkuta Mozah akiwa na mawazo.



    " Mozah, hivi nimesikia vizuri ulichoweza kuzungumza kwamba Malikia Maua ndiye aliyeweza kuiba ile cheni ya kifalme Kisha akakupatia wewe?? Aliuliza Fancy



    "Ha....ha....hapana" alizungumza Mozah n kwenda kumshika Fancy Mkono.



    "Hapana nimesikia Malikia Maua anawezaje kufanya hivyo, lazima nikamwambie Hancy" alizungumza Fancy na kuanza Kuondoka



    Mozah alimuwahi na kumshika Mkono.



    "Fancy, sitopenda niweke ugomvi juu ya Hancy na mama yake, hivyo sitopenda Hancy atambue chochote kile.



    " lakini........



    "Fancy, wifi yako anakuomba umsaidie kwahili"



    Fancy alimtizama Mozah kwa macho makali sana baada tu ya kumuita Wifi.



    "Lakini lazima kuwe na chanzo mpaka akafanya hivyo; embu niambie amekwambia sababu"



    "Hapana hata Mimi nataka kuifahamu hiyo sababu kwani Malikia Maua hawezi fanya kitu kama hicho pasina sababu hivyo lazima nipate sababu na baada ya kupata ndipi nitakapomwambia Hancy kwani yeye ni mume wangu ni lazima atambue" alizungumza Mozah.



    "Sawa.....na kabla haujaweza kunitambua basi nitaweka kikwazo kikubwa ambacho hata ukiongea ukweli hakuna atakayeweza kukuamini tena" alizungumza Fancy na kucheka kimoyomoyo.



    Aliweza kutoka na Mozah akiwa anafikiria kuhusu Hancy aliweza kuingia Stela na kumuuliza.



    "Nani kakupa hiyo cheni?? Aliuliza Stela.



    Katika chumba cha adhabu alikuwapo Mfalme Kantala, Tom pamoja na Hancy, walikuwa wakitizamana tu pasina kuongea neno lolote lile huku Mfalme akiwa amekaa katika kiti kimojawapo kilichopo pale ndani.



    " Nataka kumfahamu nani kampa Mozah ile cheni, kati ya Fancy na Malikia Maua" alizungumza Mfalme na Hancy alimuuliza Tom.



    "Unafikiri kati ya Malikia Maua na Fancy nani atakuwa amefanya hivyo???



    " inakuwa ngumu kubashiri nani kahusika " alisema Tom.



    Wakiwa katika hali ya majadiliano aliweza kuingia Nzanza ambaye aliweza kuyasikia yote waliyoweza kuzungumza.



    "Baba" aliita Hancy.



    "Mi namuhusi Fancy, na nataka kujua kwanini kaamua kufanya hivyo??



    " Lakini sidhani kama Fancy atakuwa amehusika na hili?? Alizungumza Mfalme.



    "Nafikiri kun mtu mmoja tumeweza kumsahau" alizungumza Tom na wote walimgeukia.



    Katika upande mwingine alionekana Sikitu akiwa anafikiria tukio lile lililoweza kutokea



    Aliweza kukumban na Fancy.



    "Hii ni kazi yako sindiyo???



    " Kazi gani??? Aliuliza Fancy akijitia hafahamu chochote kitu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Wewe ndiye uliyeweza kumpatia Mozah ile cheni kisha ukajifanya ya kuwa huioni sindiyo; hivi unafikiri ya kuwa Mozah akikumbwa na kashfa ya Uwizi Mimi nitaweza kuolewa tena?? Aliuliza Sikitu aliyeonyesha kujali kuhusu kuolewa kwake.



    " Sikitu Mimi sijaweza kuhusika na hili, na kama ningelikuwa ni Mimi kwanini niitafute cheni ambayo tayari najua kabisa mahali ilipo" alizungumza Fancy.



    "Kama siyo wewe je ni nani?? Aliuliza Sikitu.



    "Sifahamu labda ni kweli Hancy ndiye aliyeweza kumpatia Ndiyo maana hakuweza kusema lolote lile" alizungumza Fancy.



    "Haya yote ni makosa ya Mozah yeye ndiye sababu ya Hancy kwenda kuiba cheni na kumletea kama Kuna lolote litakalomtokea Hancy huko alikopelekwa basi sitaweza kumsamehe Mozah kwahili" alizungumza Sikitu na Fancy aliachia tu Tabasamu akiamini ya kuwa Sikitu ameweza kudanganyika.



    Aliweza kuonekana Nzanza akizungumza na mtu na kumpa maelekezo yote ya Yale aliyoweza kuyasikia akiwa ndani katika chumba alichoweza kupelekwa Hancy na Tom.



    Baada ya kutoa maelezo hayo aliweza kutoa heshima na kuondoka zake.



    Mozah akiwa ndani huku akipiga hatua za kwenda kulia na kushoto akimsubiria Hancy. Mlango uliweza kufunguliwa na Mozah alijua ni Hancy.



    "Hancy!!!! Aliita Mozah lakini aliingia ndani Sikitu ambaye alimtizama kwa macho ya chuki.



    "Sikitu" aliita Mozah na Sikitu aliweza kumfuata



    "Hancy yuko wapi??



    " bado hajaja"



    "Hancy ndiye aliyeweza kukupatia ile cheni au ni Fancy?? Aliuliza Sikitu na Mozah alimtizama kwa mshangao.



    Sikitu alimfuata na kumkaba shingo.



    " Ni mchezo gani unaonichezea wewe na Fancy?? Eeeeeeee Kuna kitu mnakicheza juu yangu sindiyo??



    Sikitu aliita Mozah na kujitahidi kutoa Mkono wa Sikitu katika shingo yake.



    "Nakuuliza kwanini Fancy alikupatia cheni yake alafu akajifanya kukutetea mbele ya mfalme na Hancy, niambie ni mchezo gani unaoweza kuucheza wewe na Fancy??? Alienda kuzungumza Sikitu pasina kujua ya kuwa anamchanganya tu Mozah ambaye hakuwa anafahamu kitu chochote kile kati ya hivyo alivyokuwa akivizungumza.



    Aliweza kuingia Tom akiwa na Hancy na Hancy aliweza kwenda na kumsukuma Sikitu kwa kumtoa Mkono katika mwili wa Mozah.



    "Mozah" aliita Hancy na kumtizama Mozah ambaye alikuwa akikohoa huku akimtizama Sikitu katika hali ya kutoweza kumuelewa.



    "Mozah" aliita Hancy na kwenda kuchukua maji kisha akampatia Mozah.



    Hancy aligeuka na kukumbana uso kwa uso na Sikitu ambaye aliweza kuogopa. Hancy alianza kumfuata lakini Mozah aliweza kumzuia



    "Hancy"



    "Hancy achana naye" alizungumza Tom na kumtoa Sikitu ndani ya chumba cha Hancy na Mozah.



    "Hancy aliita Mozah baada ya kuona katika mwili wa Hancy Kuna mabaka ya damu.



    " Hancy aliita na kwenda kumshika katika mgongo



    "Aaaaahhhh alipiga kelele Hancy akimaanisha ya kuwa anaumia.



    " Pole ....pole.....pole" alizungumza Mozah na kutoa mikono yake katika mwili wa Hancy



    "Nifanyaje sasa, kunywa kwanza haya maji.....hapana kakae kwanza kitandani kisha nikakuandalie dawa" alizungumza Mozah na Hancy alimshika Mkono



    "Kwnini Sikitu alikuwa akikunyonga au yeye ndiye aliyekupatia ile cheni?? Aliuliza Hancy



    " Hancy unatoa damu katika mwili wako, ngoja kwanza tulishughulikie hilo" alizungumza Mozah na kutaka kuondoka



    "Mozah kama hutaweza kusema ukweli ya kuw nani ameweza kukupatia hii cheni basi adhabu hii itanipata ndani ya miezi 7 ndilo niweze kusamehewa"



    "Miezi 7 ??? Alihamaki Mozah



    " Ndiyo "



    Hancy aliweza kukumbuka ya kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyeweza kuchukua mjeledi na kujichapa kwaajili ya kuweza kumsababisha Mozah azungumze ukweli.



    Muda ulienda na masaa yakapita Hatimaye ziliweza kupita siku Tatu pasina Mozah kuzungumza ukweli wowote ule kwa Hancy



    "Kuna njia moja ya kumforce Mozah aseme ukwel"



    "Njia gani?? Aliuliza Mfalme Kantala.



    " nipewe adhabu mbele yake najua lazima aseme ukweli" alizungumza Hancy



    "Hancy kama umeweza kujipa adhabu kwa muda wa siku Tatu nzima na hajaweza kuzungumza unafikiri atazungumza tena? aliuliza Tom



    " Mozah hataweza kuvumilia pindi atakapoweza kuona napata adhabu mbele yake"



    "Hancy!!!



    " baba nakuomba Tafadhali na Tom naomba uniadhibu wewe na usiweze kuacha mpaka pale atakapoweza kusema ukweli, hii Ndiyo njia pekee ya kuweza kumtambua adui wa Mozah pamoja na kile anachoweza kukitaka" alizungumza Hancy na wote walionekana kutoweza kuridhka na wasemacho.



    Watu wote waliweza kutokeza katika ukumbi ambao Mara nyingi wanakijiji wote huweza kukusanyiki pindi linapoweza kutokea jambo kubwa na inahitajika adhabu.



    "Hapana sitaweza kumuacha Hancy apate adhabu lazima nimsaidie" alizungumza Fancy akiongeza mwendo.



    "Hancy, Hancy......... Siwezi endelea kukuona unateseka zaidi lazima nimtaje Malikia Maua tu" alizungumza Mozah huku akiyafuta machzi yake na kuendelea kupiga hatua kwaajili ya kuelekea mbele zaidi.



    Malikia Maua naye aliweza kutoka katika chumba chake na kuzungumza, "Sidhani kama nilichoweza kukifanya kimeweza kuisaidia familia yangu bali kumuingiza katika matatizo mwanangu" alizungumza na kutaka kutoka katika chumba chake lakini aliweza kusimama na kutizama mbele baada ya kukutana uso kwa uso na Kipande.



    "Usitake kuniambia ya kuwa hichi ninachoweza kukifikiria hapa ndicho unachoenda kukifanya, kwahiyo huogopi ya kuwa utakufa na ukishakufa wewe hakutamfanya mwanangu Fancy aache kuwa Malikia wa mji huu wa Isadora, na bado Mfalme atabaki kumuamini tu ya kuwa Mimi na wewe tulikuwa kaka na dada na tutaweza kuuchukua ufalme huu kwa kumtumia Hancy" alizungumza kipande na Malikia Maua alibaki akimtizama tu pasina kusema neno.



    Hancy alianza kupatiwa adhabu baada ya watu wote kuweza kufika na adhabu yenyewe ilikuwa ya kupigwa na mjeledi mgongoni Mara 70.



    Fancy alijitahid kuvumilia akiwa na Mozah.



    Lakini Mozah alishindwa kujizuia zaid.



    "Mfalme" aliita Mozah na kupiga hatua za kuelekea mbele na hapo Mfalme aliweza kuzuia Hancy asipigwe tena kwa upande wa pembeni kidogo alionekana mtu aliyekuwa amejigubika gubigubi na akizungumza.



    "Mtaje mtaje huyu mpumbavu aliyeweza kukufanya wewe na mumeo mkateseka mpaka kufikia hatua hii" alizungumza mtu huyo ambaye hakuweza kuonekana sura yake ila pembeni yake alionekana Nzanza na yeye aliyekuwa amejisitiri ili asiweze kufahamika.



    "Mfalme Kantala Tafadhali Hancy hausikii na hili, Tafadhali naomba muachie huru" alizungumza Mozah akiwa amepiga magoti na akilia kwa uchungu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kama siyo yeye je ni nani?? Aliuliza Mfalme na hapo Mozah alitulia.



    " binti wa pili wa mfalme Nuhu nakuuliza tena kama siyo Hancy ni nani??? Aliuliza Mfalme Kantala na Mozah alibaki akiweweseka tu.



    "Huwezi kuongea adhabu iendelee" alizungumza Mfalme huku akishika mikono yake katika kiti chake kwa nguvu na Malikia Maua akiwa amekaa pembeni yake.



    Mfalme aliiita tena Mozah na kumsogelea karibu zaidi.



    Mfalme alinyoosha Mkono Mkono na Tom aliacha kumpa adhabu Hancy.



    "Ni nani?! Aliuliza Mfalme Kantala na kwa Mara hii macho ya Mozah yaliyokuwa yamejaa machozi yaliweza kutazama sehemu aliyokaa Malikia Maua na kuinua Mkono wake taratibu kumuelekezea.



    Watu wote waliweza kukitazama kidole cha Mozah na macho yake yalipoweza kuelekea wakati huo nao Malikia Maua alikuwa akihema kwa nguvu na kutaka kuinuka katika kiti chake lakini mdomo wa Mozah ulimfanya aache kusimama.



    " Zawadi.... Zawadi..... Zawadi!!!!! Jina hilo lilipata kujirudia kupitia masikio ya watu wengi na wengi walibaki mdomo wazi na kushangaa.



    "Zawadi!!!! Watu wengine waliweza kushangaaa kwani Zawadi ni mfanyakazi muaminifu kabisa katika kasiri hiyo ya kifalme.



    Zawadi aliweza kupiga magoti na kusema.



    "Nisamehe Mfalme wangu, yote haya niliweza kuyafanya juu ya kwmba nampenda Hancy na ninahitaji aachane na Mozah kwaajili ya kuweza kuniowa mimi" alizungumza Zawadi na Hancy alitizamana na Tom na kubaki katika hali ya mshangao.



    Muda ulipita na Hancy alikuwa akitembea na Tom huku kila mmoja wao akionekana mwenye mawazo.



    Tom aliweza kukumbuka yakuwa wakati Mozah ananyoosha kidole pamoja na macho yake kwa uhakika yalikuwa yakimuelekea Malikia Maua na hapo anadhibitisha kwani Malikia Maua alikuwa akisimama lakini baada ya kusikia jina Zawadi aliyeweza kuwa nyuma yake basi alishangaa sana na aliweza kuketi cheni.



    "Tom" alimshtua Hancy kutoka katika mawazo unawaza nini eti?? Aliuliza Hancy na Tom alisema.



    "Nafikiri Mozah anadanganya"



    "Hata Mimi nafikiri hivyo, kwani sijawahi kumuonaga Zawadi hata siku moja akionyesha dalili zozote za kunitaka kimapenzi" Alizungumza Hancy na Tom alikumbuka ya kuw tayri alishaweza kupigwa busu na Zawadi.



    "Embu subiri nakuja" alizungumza Tom na kuondoka wakati huo nao alionekana Nzanza pamoja na Nzenze wakitoa heshima na mtu yule ambaye aliweza kujifunika kila siku aliweza kuifunua sura yake alikuwa Mfalme Nuhu.



    "Nafikiri sasa ni salama kwasababu mwanamke aliyekuwa akimsumbua binti yangu sasa tayari yuko mikononi mwa sehemu ambayo hataweza kumgusa tena, naweza kurudi nyumbani sasa"



    "Mfalme aliita Nzanza na kuendelea kuzungumza.....



    " Nahitaji kubaki hapa kwa muda kisha nitaweza kuja kijijini"



    "Sawa ila uhakikishe ya kuwa uko salama na wasiweze kutambua ya kuwa uko hapa" alizungumza Mfalme Nuhu ambaye kwa wakati huo alikuwa juu ya farasi pamoja na vijakazi wake wawili Nzanza na Nzenze.



    Aliweza kuondoka na Nzenze na Nzanza alitoa heshima kisha akarudi katika njia ya kuelekea tena katika mji wa Isadora.



    Aliweza kukumbuka ya kuwa kabla ya Mozah kuingia katika ukumbi ule wa adhabu basi aliweza kukutana na Zawadi na Kuna jambo walikuwa wakizozana na Mozah.



    "Nahitaji kufahamu ni kipi walichokuwa wakikizungumza" alisema Nzanza na kumtazama Mfalme Nuhu kwa mbali.



    "Mfalme nimeshindwa kukwambia hili kwani nahitaji kufuatilia Mimi mwenyewe kwa makini.



    ***** ***** *****



    Ulikuwa muda wa usiku na Mozah alionekana mwingi wa mawazo huku Hancy akiwa ameingia chumbani na kuweza kumkuta katika hali hiyo.



    " Mozah " aliita Hancy na Mozah aliweza kushtuka.



    Hancy alimsogelea na kukaa kitandani.



    "Mimi ni nani wako?? Aliuliza Hancy.



    " mume wangu"



    "Tafadhali naomba uniambie ukweli ni nani aliyeweza kukupatia ile cheni?



    " Hancy!! Aliita Mozah



    "Najua kabisa Zawadi hawezi kutoa kitu chochote kile bila amri ya Fancy; kama Fancy ndiye muhusika basi unapaswa kuniambia "



    "Hapana Fancy hausiki na chochote kile wala Fancy hawezi kufanya hivyo, Je ni adhabu gani anaweza kupatiwa Zawad??



    " katika falme yetu hukumu ya mwizi ni kukatwa mkono"



    "Mkono?? Aliuliza Mozah kw hamaki kisha akaweza kukumbuka ya kuwa Zawadi alitaka amtaje yeye jina ili kuweza kukwepesha aibu hiyo katika familia ya kifalme.



    Mozah niambie ukweli ni nani kahusika tena?? Aliuliza Hancy.



    Mozah hakuongea kitu zaidi ya kujitizama vidole vyake



    " Mozah nakuuliza kwa Mara ya mwisho na wala sitakuuliza tena, Tafadhali niambie hiyo cheni ilifikaje katika shingo yako" aliuliza Hancy kwa kumshika Mkono Mozah.



    Mozah alivuta pumzi ndefu kisha akasema



    "Zawadi"



    Hancy alimtizama na kumwambia huu Ndiyo ukweli nilioweza kuubeba kwa sasa na sitakuuliza tena kwani nimeamini kile usemacho alizungumza Hancy na kisha kumkumbatia Mozah.



    "Hancy!! Aliita moza kwa utaratibu



    " naam"



    "Naweza kumuona Zawadi kwa siku ya Leo?? Aliuliza na Hancy aliweza kutoa jibu.





    "Ndiyo unaweza ila Mfalme asitambue kwani nikwasiri sana haruhusiwi kuonana na mtu yoyote mpka siku itakapoweza kutolewa hukumu kwaajili yake.



    **** **** ****



    "Kipande sikudhani kama unaweza ukatumia njia hii kwaajili ya kuhakikisha ya kuwa ukweli haufahamiki kwasasa, sasa nimeamini ya kuwa Zawadi ni mtumishi muhimu na mtiifu sana katika upande wangu hivyo lazima nimtumie na yeye ili kukifikia kiti cha ufalme"



    Wakati huo nao alionekana Zawadi akiwa ndani ya gereza huku akikumbuka ya kuwa aliweza kuambiwa na Kipande amshawishi Mozah akubali kumtaje yeye lasihivyo basi angeweza kubashiri kipi kitakachotokea kama atashindwa kufanya hivyo.



    "Najua mtajua ya kuwa nimefanya kwaajili yenu lakini si hivyo nimefanya kwaajili ya ........" Kabla hajamjata aliyemfanya akafanya hivyo Tom aliweza kuingia na kumfanya aache kuwaza.



    "Zawadi nataka kujua kwanini uliichukua cheni pasina ruhusa au ni Fancy niambie au ni Malikia alikuamuru" Alizungumza Tom na Zawadi alisema



    "Nimefanya yote hayo kwasababu nampenda Hancy, na Nahitaji kuolewa naye"



    "Zawadi" aliita Tom na kumvuta karibu kabisa na sehemu aliyoweza kusimama



    "Natambua ya kuwa humpendi Hancy, unanidanganya najua kabisa ya kuwa unanipenda Mimi na hii ni tangia siku ile nikusaidie wewe pamoja na mdogo wako wa kike, huwezi nidanganya Mimi na hata siku ile uliweza kunibusu Mimi najua na ninauhakika ya kuwa Mimi ndiye mwanaume wa kwanza kukubusu wewe, hivyo usinidanganye bora uniambie ukweli na ukiongopa utanifanya nikuchukie wowote kuliko mwanamke yoyote yule duniani"



    Tom aliita Zawadi na kutoa mikono ya Tom kwa mwili wake.



    "We....we....wewe ndo unawaza vibaya sijawahi kukupenda mm wewe, Mimi nampenda Hancy"



    "Ahaaaa kweli eeee, alizungumza Tom kisha akamvuta Zawadi na kuanza kumpiga mabusu ya kumlazimisha kwa mdomo.



    Zawadi aliweza kujichomoa kwa Tom na kumpiga kibao.



    Tom alimshika tena na kumpiga mabusu mengine Zaidi.



    Zawadi alirudi nyuma na kutaka kumpiga kibao.



    " Nipige tena kama Unataka tena nikubusu" alizungumza Tom na Zawadi alibaki akiutizama Mkono wake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa tuone" alizungumza Zawadi na kuanza kupiga kelele za kuita walinzi.



    Hapo hapo aliweza kuingia Mozah na Hancy.



    "Zawadi" aliita Hancy na walianza kusikia walinzi wakija.



    'Ni hatari kupatikana hapa" alizungumza Hancy na kumshika Mozah Mkono huku akimtaka Tom na yeye aweze kuondoka.



    Tom alimnyooshea Mkono Zawadi na kuondoka akiwa mwingi wa hasira



    Muda ulipita na alionekana Tom akiwa na hasira sana.



    "Unajua kwamara ya kwanza katika Maisha yangu hatimaye Leo nakuona ukiwa katika hali ya hasira" alizungumza Hancy.



    "Yule msichana yule. ...... Nitamuonyesha tu" alizungumza na Hancy Alicheka.



    "Au umempenda Zawadi?? Aliuliza Hancy



    " Nini Pumbavu kabisa Mimi nimpende yule wanawake wameisha nini! Alizungumza Tom na kusimama.



    "Hapana Mimi sijasema ya kuwa unampenda bali nimekuuliza je unampenda lakini naona umechukia au ni ukweli??



    " Hancy aliita Tom kwa sauti ya juu na Hancy alisimama kisha akatoa heshima mbele ya Tom na kuondoka zake.



    Tom aliweza kujishtukia na kusema



    "Mungu wangu nimewezaje kuzungumza hivi mbele ya mfalme mtaraji??



    ****** ****** ********



    Wakati huo alionekana Malikia Maua akiwa na Fancy huku akiwa amemshikilia kitu Mkononi mwake.



    " usinitizame inabidi ufanye hivyo au kama hutaki nitatoa udhibitisho ya kuwa wewe ndiye unayehusika na kumpa cheni Mozah



    "Lakini wewe ndiye uliyenipa alizungumza Malikia Maua.



    " Ni sawa lakini Mozah hatambui hilo yeye anajua ya kuwa wewe ndiye uliyeweza kumpa " alizungumza Fancy.



    "Na usijali sana kwani hii Ndiyo kazi yako ya mwisho wala hutafanya tena baada ya kufanya hii"



    "Nitakuwa na uhakika gani?? Aliuliza Malikia Maua.



    " Mama mbona ulikuwa unaniamini sana Mimi tangu mwanzo niamini ya kuwa hii Ndiyo kazi ya mwisho na hutafanya tena kazi hiyo"



    Malikia Maua alimtizama na kuondoka .



    Wakati anaondoka Fancy Alicheka na kuweza Kuondoka kuelekea katika chumba cha Mozah.



    "Mozah........ Aliita Fancy na kuanza kulia.



    " unashida gani?? Aliuliza Mozah.



    "Ma.....Ma...Malikia Maua amenilazimisha kuja kukuwekea wewe hii cheni yake katika nguo zako na amesema nisipofanya hivyo basi atakuja kuweka mwenyewe"



    "Malikia Maua?? Aliuliza Mozah kwa mshangao na kushindwa kuelewa.



    " Fancy wifi yangu usijali kuhusu hilo, na nashukuru sana kwa kuweza kuniambia ukweli wote huu" alizungumza Mozah bila kutambua ya kuwa anayeweza kumkumbatia ndiye joka kubwa katika ndoa yake.



    Fancy Alicheka tu na baada ya hapo alionekana akiufunga mlango wa Mozah kwa Tabasamu kubwa sana.



    Mozah akiwa ndani aliweza kuwaza juu ya yale maneno aliyoweza kuambiwa na Fancy na alishindwa kuelewa kwanini Malikia Maua anataka kumfanya yeye aonekane mwizi katika kasiri hiyo ya kifalme ilihali mwanzo kabisa yeye ndiye aliyeweza kumpokea kwa mikono yote miwili.



    Akiwa anajiuliza hapo aliweza kuingia Malikia Maua na Mozah alisimama akimtizama na kujifanya haelewi chochote kile kama alivyoweza kushauriwa na Fancy.



    "Karibu Malikia Maua" alizungumza Mozah na kutoa heshima.



    Malikia maua alionekana mwingi wa wasiwasi na aliweza kuficha kitu katika Mkono wake. Alianza kumsogelea Mozah taratibu kabisa na hali hiyo ilimshtua Mozah na kuanza kurudi nyuma lakini mwishoni aliweza kufika katika kabati na hapakuwa na pa kuelekea tena.



    "Mozah nimekuja kukutaka radhi kwa kile nilichoweza kukifanya juu yako pia nakushukuru kwasababu hukuweza kunitaja Mimi na pia uliweza kunifichia Siri yangu wakati akiyazungumza hayo aliweza kufungua kabati kidogo sana na kuweza kuachia ile cheni aliyoweza kuwa ameishika katika Mkono wake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mozah alimuona lakini hakuzungumza lolote lile.



    Huku nako alionekana Sikitu akimsimamisha Hancy aliyekuwa akieleka chumbani mwake.



    "Nakwambia na nitakwambia tena na tena kwaajili ya usalama wa maisha yako na ufalme wako ni kwamba Mozah siye binti mzuri kwa upande wako na Mozah anatamaa sana ya mali na ile cheni nakwambia ukweli kabisa ya kuwa Mozah ndiye aliyeweza kuichukua na kumsingizia Zawadi"

    ITAENDELEA

Blog