Search This Blog

TAREHE 9 SEPTEMBER - 5







      Simulizi : Tarehe 9 September

      Sehemu Ya Tano (5) 





      Shirima akapoteza fahamu,,, pasipo kupata msaada wowote....

      baada ya dakika kadhaa Shamy na Zack wakafika nyumbani kwa Shirima... wakaliegesha gari ,,wakazipiga hatua kuufuata mlango wa nyumba ya Shirima... Zack akagonga mlango,, lakini mlango haukufunguliwa! akasema,, "au katoka?

      Shamy akafungua mkoba wake akatoa simu,, na kumpigia Shirima,,,

      simu iliita bila kupokelewa,, Zack akasema mbona nasikia mlio wa simu ikiita ndani ya nyumba hii au atakuwa amelala?

      Shamy akazungusha kitasa cha mlango ukafunguka akashtuka kumuona Shirima kalala kwenye sakafu! akaingia ndani haraka,,pia Zack naye akaingia,,

      Shamy alipomtazama Shirima akagundua kuwa Shirima,, amepoteza fahamu,, akampa huduma ya kwanza kwa kumpepea mfululizo.. punde si punde Shirima akazinduka,, na kupata fahamu!!  akastaajabu kumuona Shamy!  alipogeuza shingo yake akamuona Zack!

      Shirima akanyanyuka pale chini akazipiga hatua kulifuata jokofu,, akafungua na kutoa chupa ya maji,, akaanza kunywa,, kisha akaketi kwenye sofa,,

      Zack na Shamy nao wakaketi kwenye moja ya masofa yaliyokuwemo ndani ya sebule ya nyumba ya Shirima!

      wakasalimiana,, kisha Zack akatoa picha ya mama yake na kuzipiga hatua kumsogelea Shirima,, akasema,, "unamfahamu huyu? Zack aliongea huku akimkabidhi Shirima ile picha!  Shirima akaipokea,,alipoitazama akasema ndio namfahamu,, huyu ni mzazi mwenzangu,, na sijui yuko wapi?

      Macho yakamtoka Zack! akajisemea moyoni,, "mama yangu hakuwahi kuwa na mtoto mwingine zaidi yangu... inamaana huyu ndiye baba yangu?  mbona hii ni kama sinema! sasa yule aliyenitambulisha mama kabla hajafariki kuwa ndiye baba yangu,, aghhh!!! 

      wakati Zack anajiuliza maswali hayo,, Shamy na Shirima walikuwa wakimtazama Zack,,alionekana yumo ndani ya dimbwi zito la mawazo pia yupo mbali kifikra!

      Zack akauliza,, "unamaanisha wewe ni baba yangu?  kwa sababu mama yangu hakuwahi kuzaa mtoto mwingine zaidi yangu..

      Shirima akakohoa kwa sekumde kadhaa kisha akasema,, " mnamo miaka 29 au 30 iliyopita niliwahi kuwa na mahusiano na Bi'Eliza Mushi..

      Zack akazidi kuchanganyikiwa baada ya kumsikia Shirima kataja Jina kamili la mama yake pamoja na Ubini!

      Shirima akaendelea kusimulia,, "Bi'Eliza alikuwa ni mke wa bosi wangu aitwae RICH.

      richi alikuwa ni daktari mkuu wa hospitali ya Rufa Bugando huko Mwanza... haikuwa dhamira yangu mi; i kushirikiana kimwili na mke wa bosi wangu,, lakini Bi'Eliza alinilazimisha pia akanitishia kuwa endapo nitakataa kumtimizia haja yake.. atasema maneno ya uwongo kwa bosi wangu ambaye ni mumewe ili anifukuze kazi,,, kiukweli nilisikitika sana nikiangalia mimi ndiye tegemezi la kumlea mama yangu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mgonjwa sana.. pia mimi nilikuwa mtoto wake wa pekee... na hakuna ndugu wa kutupa msaada..

      nilitafakari kwa kina,, nikaamua kukubali ili niendelee kufanya kazi nipate pesa ya kumuhudumia mama yangu....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      siku moja Bosi Rich alisafiri kikazi.. mke wa Rich akaniita nyumbani kwake.. nilipofika akanishawishi nishirikiane nae kimwili,, nikajikuta nashindwa kuwa mvumilivu.. akaniongoza mpaka chumbani anapolala yeyw na mumewe... kumbe Rich alitegesha kamera ndani ya chumba chake pamoja na maeneo yanayoizunguka nyumba yake!!

      mimi na Bi'Eliza hatukuweza kutambua kuwa kumakamera zinaturekodi...

      siku zilizidi kusonga,,na baada ya wiki mbili kupita,, Bi'Eliza akaniambia kuwa anaujauzito wangu, niliogopa sana kwa sababu nilijua hii ni hatari endapo Rich atagundua!!  wiki moja baadae hatimae bosi Rich akarejea nyumbani kwake...akagundua kuwa mkewe kamsaliti tena kwa kulazimisha yeye mwenyewe.. aliona tukio zima lililorekodiwa na kamera(UCCTV) akachukia kupita kiasi akamfukuza mkewe...

      mimi nikaogopa  kuendelea kuishi Mwanza nikaamua kuhama mimi na mama yangu nikakimbili huku dar es salaam! tangu miaka ya 80...kwa sababu nilikuwa nimesomea mambo ya uuguzi.. nikaamua kujiendeleza kielimu zaidi.. nikapata stashahada ya udaktari... serikari ikanipa mkopo wa kujiendeleza zaidi.. hatimae nikamaliza masomo yangu nikawa daktari maalumu!  ndipo nikaajiliwa hospitali ya Muhimbili kama daktari mkuu... kiukweli sikuwahi kumuona tena Bi'Eliza na sijui alijifungua mtoto wa jinsia gani! kumbe wewe ni mwanangu! eee Mungu asante kwa kunikutanisha na mtoto wangu kwa namna hii!  pia samahani sana Shamy!  haya yote yametokea kwa sababu sikujua,, kuwa wewe ni mchumba wa mwanangu... Shamy akatabasamu pasipokuongea neno lolote!

      Zack akabaki mdomo wazi huku akimtazama Shirima!,, akanyanyuka na kumkumbatia baba yake.



      Siku zilizidi kusonga,,Zack akawa na furaha kumjua baba yake mzazi,, pia Shamy akafurahi mkuu wake wa kazi ni baba mkwe wake.

      maisha yalikuwa mazuri kupita kiasi... waliishi kwa amani siku zote!

      Siku moja Zack akaongea na baba yake(shirima) kuwa ni vyema waende kupeleka barua ya Posa nyumbani kwao Shamy,, ili ndoa ifungwe.. Shirima hakuwa na kipingamizi.. mipango na taratibu zikafanyika na safari ya kwenda mwanza nyumbani kwao Shamy ikawadia!





      Shirima akalazimika kuongozana na Zack pamoja na Shamy kwenda nyumbani kwao Shamy,,huko Mwanza... Shirima akalipia usafiri wa ndege,, akapatiwa tiketi tatu....

      Shamy akawajulisha wazazi wake kuwa anakuja huko nyumbani kumleta mchumba wake amtambulishe kwao!

      wazazi wa shamy wakafurahi sana,, wakafanya maandalizi kwaajili ya wageni hao.

      Shamy Zack pamoja na Shirima wakaelekea uwanja wa ndege(Air poart) tayari kwa safari.,,,,,

      baada yaasaa kadhaa wakawa wamefika mwanza,,, wakakodi taxii kutoka kwenye kiwanja cha ndege Mwanza mpaka Nyakato nyumbani kwao Shamy..... walipofika wakapokelewa,,, Mama Shamy akafurahi sana kumuona mwanae pia akafurahi kumuona mchumba wa Shamy pamoja na baba wa mchumba wa Shamy.. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      wakati huo Baba Shamy hakuwepo nyumbani... alikuwa katika shughuri zake.

      Chakula pamoja na madikodiko yakaandaliwa... tayari kwa chakula cha mchana.

      walipomaliza kula,Shamy akaandaa Sehemu ya kulala wageni wake...

      ilipofika majira ya saa mbili za usiku......Shirima akaenda kupumzika katika moja ya chumba cha wageni katika nyumba yao Shamy!

      Akabaki Shamy Zack pamoja na Mama Shamy wakiwa sebuleninwakitazama taarifa ya habari..... Shamy akasema,, "mama wacha sisis tukapumzike,, naona leo baba kachelewa kurudi,,, hivyo wageni wangubwataongea nae kesho Mungubakipenda,

      Maam Shamy hakuwa na kipingamizi,, akasema,, "hakuna tatizo mwnangu..

      Shamy akamuongoza Zack mpaka chumbani... wakapumzika...

      ilipofika saa nne za usiku Baba Shamy akarejea nyumbani... lakini akakuta wageni tayari wamelala vyumbani....



                               **************************************



      Asubuhi palipokucha Baab Shamy alidamka mapema kama kawaida yake.. akajiandaa kuelekea kwenye shughuri zake.... kabla hajatoka akamwambia mkewe,, "wacha mimi niwahi kusimamia miradi yangu,,lakini nitawahi kirudi japo nisalimiane na wageni..



      Mama Shamy hakuwa na kipingamizi,, Baba Shamy akatoka nje ya nyumba akaingia ndani ya gari,,, na kuondoka zake.

      Whamy akadamka akaandaa Chai kwa ajilibya wageni wake...

      kisha akawakaribisha katika meza ya chakula...

      Bnaada ya masaa sita lupita Baba Shamy alirejea nyumbani... alipoingia sebuleni akastaajabu kumuona adui yake yumo mdani ya nyumba yake!  ambaye ni Shirima

      Baba Shamy akapigwa na butwaa... lakini akawa mvumilivu,,, wakati huo Shirima macho yalimtoka hakuamini anachoshuhudia mbele ya macho yake!

      Baba Shamy akaketi kwenye Sofa....punde si punde Shamy akaja sebuleni akitokea chumbani..... akamsalimia baba yake na kumkumbatia kwa upendo.

      kisha Shamy akaanza kutoa utambulisho kwa baba yake.

      akasema,, "baba hawa ndio wageni wangu.. huyu anaitwa Zack ni mchumba wangu.

      na huyu anaitwa Shirima ni baba mzazi wa Zack... nimechukua jukumu jili kuwaleta nyumnani kwa lengo la kufahamiana pande zote mbili. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Macho yakamtoka baba shamy.. akabaki mdomo wazi! wakati hio Shirima alikuwa akimtazama bana Shamy kwa macho ya aibu,, huku akijisemea moyoni,, "hii ni fedheha laiti kama ningejua nakuja kwenye nyumna ya huyu mzee nisinge thubutu lakini hakuna namna,, hayo yalishatokea na yamepita,, lakini sijui atachukua maamuzi gani juu ya jambo hili!

      Shamy aliendelea kutoa utambulisho kisha akaketi kando ya baba yake..

      Maam Shamy akasema, kwa ulande wangu mimi sina kipingamizi.... kwa sababu wao wamependana na wameamua kulifikisha swala hili kwa wazazi mimi sioni tatizo lolote.. labda baba Shamy,, unalo la kuongea??

      Baba Shamy akabaki kimya huku kainamisha uso wake chini..... ajambo hilo lilimfanya Shamy akose furaha ghafla,, akahisi huenda baba yake akakataa ndoa isifungwe!

      pia watu wote wakastaajabu!

      Baba Shamy akanyanyuka pasipokuongea neno lolote akazipiga hatua kuelekea chumbani....Shamy na Zack wakatazamana!

      utu uzima dawa, Shirima akahisi jambo baya litatolea muda mchache ujao.. akaketi kwa taadhari huku mkono wake mmoja kauegesha kiunoni... kumbe Shirima alikuwa na bastola....

      punde si punde Bana Shamy akaonekana akitokea chumbani huku kaweka mikono yake nyuma... alipofika sebuleni akachomoa bastola akamnyooshea Shirima,, wakati huohuo pia Shirima akachomoa bastora kumnyooshe Baba Shamy!

      Watu wote waliokuwepo pale sebuleni wakapigwa na butwaa!!! wakabaki wanajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu... punde si punde ukasikika mlio wa risasi!!!!







      Baba Shamy akaamua kupiga risasi juu ya dari.. kutokana na hasira alizo kuwanazo.. kisha akaitupa bastola juu ya sofa.. akaketi kando, akasema,, "hivi wewe shirima unatafuta nini katika maisha yangu? wewe uliharibu ndoa yangu miaka ya 80,,kwa kushirikiana kimwili na mke wangu wa kwanza,,ukaona haitoshi ukaamua kumpa ujauzito,, mshukuru mungu wako ulikimbia,, bila hivyo ningeondoa uhai wako kwa mikono yangu mwenyewe... haya leo umekuja kuivuruga tena familia yangu... hivi wewe unahitaji roho yangu ndio uridhike?



      Shirima akahisi fedheha,, akamtazama Baba Shamy kwa macho ya aibu...kisha akasema,, "haikuwa kusudio langu,,, Mungu pekee ndiye shahidi wa hilo... mkeo alinilazimisha nifanye hivyo... akanitishia kuwa nisipomtimizia haja yake atasema uwongo kuwa mimi namtaka kimapenzi... ili wewe unifukuze kazi.... na kwa kipindi hicho mama yangu alikuwa mgonjwa sana,, anahitaji matunzo pamoja na mahitaji kama dawa na chakula,,niliamua kukubali ombi la mkeo kwa sababu moja tu... niendelee kufanya kazi nipate fedha za kumtunza mama yangu... lakini haikuwa kusudio langu... pia ilikuwa ni siku moja tu... na kwa mipango ya Mungu,, mkeo akapata ujauzito!! na mtoto mwenyewe ni huyu Zack... samahani sana,,naomba haya mambo yaishe... kwa sababu tayari wewe unafamilia nyingine.



      Shamy akashtuka akahisi kuchanganyikiwa,,, macho yakamtoka!

      Pia Zack akabaki mdomo wazi!



      Mama Shamy akasema,, "kwa upande wangu mimi sioni kama kunatatizo... huwezi jua kusudio la Mungu,,punguza hasira Baba Shamy!

      Baba Shamy akamtazama mkewe,,, kisha akashusha pumzi; akasema,, "kiukweli Shirima wewe sijui nikuweke katika historia ipi ya maisha yangu.... umekuwa gumzo kwenye ubongo wangu... SITOSAHAU KAMWE..

      Shamy akazipiga hatua za taratibu akamsogelea baba yake,, akapiga magoti kisha akasema,, "tafadhali baba yangu kipenzi naomba umsamehe,, ameshakwambia ukweli.

      pia nampenda sana Zack,,yeye ndiye mwanaume wa maisha yangu... naomba baraka zako baba yangu... Shamy aliongea maneno hayo huku machozi yakimtoka.

      maneno ya Shamy yalimfanya baba yake aingiwe na roho ya huruma,, akamkumbatia binti yake(Shamy) akasema,, "ondoa shaka mwanangu,, nawatakia kila la heri wewe na mchumba wako.

      Shamy akafueahi sana..

      baba Shamy akazipiga hatua akamsogelea Shirima akashikana mkono na Shieima ishara ya amani.



      *****************************

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      baada ya siku nne kupita.. Shirima,, Zack pamoja na Shamy wakarudi dar..

      mipango ya harusi ikafanyika na ndoa ikafungwa.



      Maisha ya Shamy na Zack yakawa na amani na furaha,,,kutokana na furaha na amani aliyokuwanayo Shamy,.,utendaji wake wa kazi ukaongezeka hatimae akapata tuzo ya daktari bora katika sherehe za tuzo za hospitali hiyo... daktari mkuu(shirima)

      akaamua kumpandisha cheo..na mshahara wa Shamy ukaongezwa kwa aslimia kumi ya mshahara wake aliokuwa analipwa mwanzo.

      baada ya miezi mitano(5) kupita,,Shamy akapata ujauzito.

      Zack akafurahi sana,, upendo ukazidi kuongezeka kila kukicha,,

      baada ya miezi tisa (9) kupita Shamy akajifungua mtoto wa kike,, mtoto huyo alikuwa mrembo kama mama yake,,, hatimae Zack akawa na familia.... alihakikisha familia yake inakuwa na amani siku zote.... pia Shirima alifurahi sana kumpata mwanae wa pekee(Zack) pamoja na mjukuu wake...

      Familia hiyo inaishi kwa amani na upendo mpaka leo.





      ****************************MWISHO**********************************



0 comments:

Post a Comment

Blog