Search This Blog

TAREHE 9 SEPTEMBER - 3







    Simulizi : Tarehe 9 September

    Sehemu Ya Tatu (3) 





    Asubuhi palipokucha Zack alidamka mapema,, akaenda kufungua maduka yake.. kisha akawaacha wafanyakazi wakiendelea na kazi,, yeye akaingia ndani ya gari lake akaelekea kwa lafiki yake kipenzi,, ili ampeleke kwa mganga! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipofika akamkuta rafiki yake anamsubiri!  bila kupoteza muda wakaongozana mpaka ndani ya gari la Zack na safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza!

    walitumia lisaa limoja njiani, hatimae wakafika kwa mganga aitwae MANYENYE,,Nyumba ya Manyenye ilionekana kujengwa kwa miti na kuzungushiwa nyasi kavu,, na nje ya nyumba hiyo,, kulikuwa na mawe mawili makubwa kiasi yakiwa kando ya mlqngo wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo,, lakini nyumba hiyo ilikuwa ni nyumba ya maajabu,, licha ya kuonekana ndogo kwa muonekano wa nje, lakini ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vyumba miamoja (100) vikubwa,,Zack akaongozana na rafiki yake kuingia ndani ya nyumba hiyo,, akastaajqbu kuona ukubwa wa nyumba hiyo!  tofauti ja inavyoonekana upande wa nje!!!  Zack akaeleza shida yake kwa mganga,, 

    Manyenye akasema,, "ni jambo rahisi sana, hakuna linaloshindikana mbele yangu, mimi ndiye Manyenye wa Manyenye. aliongea hivyo huku akitingisha vibuyu viwili alivyokuwa kavishikilia mikononi mwake!  kisha akasema,, "itabidi ufanye jambo la kijasiri,, Manyenye akasema chukua kisu hiki,,  andika hapo chini jina lako kamili pamoja na ubini wako kwa kutumia kisu hiki,, kisha andika Jina moja la huyo adui yako unayetaka kumuangamiza..

     Zack akaandika majina yake kamili pamoja na ubini wake. akiandika chini kwa kutumia ke kisu alichopewa na mganga!  kisha akasita akavuta kumbukumbu,, akakumbuka kuwa aliona jina la mtu huyo kwenye simu ya Shamy ,limeandikwa SHIRIMA,,  bila kuchelewa akaliandika jina hilo kwa kutumia kisu hicho!

    Makanya akasimama na kunyunyizia dawa,, ghafla akasita.. kisha akamtazama Zack akasema,, "mbona umedanganya ubini wako.. hili jina la ubini wako sio sahihi,, halionekani kwenye maono yangu ya kimizimu! hilo jina lingine Shirima mbona linaonyesha kuwa ndio ubini wako! halisi na ndio chimbuko la damu yako!  au umechanganya majina?  Zack akashtuka mqcho yakamtoka!







    zack akauliza kwa mshangao!  ,,"unamaanisha nini? mbona sielewi!  yani hili jina la huyu mshenzi unasema ndio ubini wangu?  mimi sijachanganya majina,, umesma niandike majina yangu pamoja na ubini wangu!  kisha ukasema niandoke jina moja la huyu adui yangu,, sasa yawezekana vipi jina la adui yangu liwe ubini wangu?

    Mganga ajaribu tena kupiga tunguli,, akasita kisha akasema,, "jina la adui yako linaonekana ndio ubini wako sahihi,, sasa kama wewe unadanganya,, nakuomba toka uondoke zako,, naona umekuja kunijaribu!!

    Zack pamoja na rafiki yake wakamuomba radhi manyenye kisha wakaondoka zao.



    ilipofika saa moja za usiku Zack akarejea nyumbani,, akamkuta Shamy anajiandaa kwenda kazini(night shift)

    Shamy akasema,, "pole na kazi kipenzi cha roho yangu,,

    Zack hakujibubkitu chochote akabaki kimya!  Shamy akastaajabu,, akauliza,, "kulikoni?  mbona kama unahasira! ? nani kakukwaza?

    Zack akasema,, "nahisi kama homa inaninyemelea..

    Shamy akafungua droo akatoa chupa ndogo yenye kioo chepesi sana,, (Test tube) kisha akachukua bomba la sindano likiwa na sindano,, akasema wacha nichukue damu yako nikaifanyie vipimo,, huenda unamaralia!

    Zack akasema,, "haina haja,, homa hii haiusiani na vipimo,,, kama kunavipimo vya mapenzi basi nahisi kipimo hicho ndio kitanifaa!  Shamy akastaajabu! akauliza,, "unamaanisha nini mpenzi? mbona sikuelewi!

    wakati shami anauliza hivyo,, simu yake ikaita,, alipoitazama akaona Shirima ndiye anampigia simu,, akaipokea kisha akasema,, samahani mkuu nipo najiandaa nitafika hapo muda mchache ujao.

    Zack akasema,, "hivi huyo Shirima mbona huwa anakupigia simu kila siku!  inamaana wewe ndiye daktari bora kuliko madaktari wengine wa hospotali hiyo!  Shamy akawa mnyonge,, akasema,, "mimi ni wako tu hakuna wa kubadilisha mawazo yangu juu yako.

    Zack akamtazama Shamy, kwa macho ya msisitizo.. Shamy akachukua mkoba wake akatoka nje ya nyumba akaingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuelekea kazini!

    baada ya dakika kadhaa Shamy akafika Muhimbili,,, akapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi yake,, punde si punde Shirima akaja ndani ya ofisi ya Shamy,, wakasalimiana,, kisha Shirima akanza kumchombeza Shamy akiulizia kuhusu jibu la ombi lake!  Shnamy akasema ,,"mimi nilikwambia kuwa ninamchumba na ninampenda kuliko mwanaume yeyote hapa duniani... kiukweli sina jibu zadi ya hilo,, samahani sana mkuu!



                               ***********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Baba yake Shamy akiwa chumbani na mkewe..

    baba shamy akasema,," kunajambo huwa nashindwa kulisahau,,jambo hilo lilinitokea miaka mingi iliyopita,, takribani miaka therathini na kadhaa,, Mama Shamy akauliza,, "jambo gani mume wangu!?  mbona unanitisha!  tafadhali ningependa kufahamu,.

    Baba Shamy akaanza kusimulia;

                                            ilikuwa hivi;  kqbla sijastaafu nilikuwa naendeshwa kwenye gari na dereva wangu. alikuwa ni kijana mstaarabu na mwenye adabu,, jina lake nalikumbuka anaitwa SHIRIMA,, nikawa naambiwa na majirani kuwa mimi napokwenda kazi,, mke wangu anaondoka nyumbani anakwenda kwenye starehe,, alioonekana sehemu mbalimbali za starehe mara kwa mara.... nikaamua kununua mtambo maalumu wa (UCCTV) kamera za kurekodi matukio masaa24 mfululizo... kamera hizo nikazitegesha kwa kuzificha chumbani mwangu...siku moja nikapata safari ya kwenda nchini India kwenye semina ya wiki moja,, tulichaguliwa madaktari watatu watatu kutoka hoptili zote za Rufaa....

    baada ya wiki moja kuisha nikarejea nchini.... nikaangalia video za matukio yaliyorekodiwa na zile kamera nilizozitegesha,,, mke wangu hakufahamu hilo,,kuhusu kamera hizo,, niliumia sana kuona anamshawishi Shirima afanyenae mapenzi,,ndani kwangu,, chumbqni kwangu mbaya zaidi kwenye kitanda ninachalala mimi na mke wangu.. nikaamua kumfukuza,,,kwa sababu alikuwa hana la kujitetea ushahidi kamili ulikuwa kwenye video zilizorekodiwa na kamera... akaamua kueleza ukweli kilichotokea akihisi huenda nikamsamehe,,, akasema,,"nilifanya hivi kwa sababu wewe hauna muda na mimi,, muda mwingi unakuwa kazini,, ukirudi unalala tu, hunipi haki yangu ya chumbani,,,sikufanya hivi kwa makusudi... mbaya zaidi ninaujauzito wake nisamehe mume wangu! Kiukweli niliumia kupita kiasi.. nikapoteza fahamu,, nikakimbizwa hospitali,, waliponifanyia vipimo nikagundulika nimepata ugonjwa wa msukumo wa damu ya kupanda,, (high blood pressure)

    Niliporudi nyumbani nikaamua kumfukuza mwanamke huyo,,

    mdogo wangu wa kike,, hakufurahia kitendo hicho cha mimi kumfukuza mke wangu.. akaamua kuishi nae nyumbani kwake... mimi nilifanya iwe siri yangu,, sikuwahi kumwambia mtu yeyote kuhusu hili.. mdogo wangu alinichukia sana,, akisema kuwa nimemfukuza mke wangu akiwa mjamzito.. na nimetelekeza ujauzito huo..aliishi hapo nyumbani kwa mdogo wangu,, mapaka siku ya lujifungua,, lakini baadae mwanamke huyo alikufa,, akabaki mtoto wake,, nahiso kama sikosei alimpa jina akamuita Zack...mdogo wangu aliendelea kunichukia huku akimwambia mtoto huyo kuwa mimi nilimtelekeza mama yake akiwa na mimba changa... mtoto huyo akaamini kuwa mimi ni baba yake,, lakini sivyo,,, pia nikajikuta namchukia sana mtoto huyo,, sikutaka hata kumuona,,,

    Shirima akakimbia,, tangu siku hiyo sijui yupo wapi,, pia sijui kama yupo hai au ameshakufa... sana kwa kuificha siri hii lakini leo nimeamua nikwambie..

    Mama Shamy akamtazama mumewe kwa macho ya huruma kisha akasema,, "pole sana kwa mkasa huu,, inahuzunisha sana....



    Siku zilizidi kusonga,,Shirima hakukoma kumsumbua Shamy,,akimtaka kimapenzi..

    simu za mara kwa mara zilizokuwa zinapigwa kwenye simu ya Shamy,, zilimfanya Zack,, aanze kuingiwa na mawazo ya kikatiri.. akaamua kuandaa mpango wa kumtafuta Shirima ili amfahamu kwa sura,, kisha aandae mpango wa kumuangamiza Shirima,,

    Siku moja Zack alionekana kaketi kwenye hotel fulani hivi,,, akinywa mvinyo..kwa mbali akaonekana Shirima akiingia ndani ya hotel hiyo akaketi kando ya Zack..  wakasalimiana na Zack..

    Zack hakuweza kutambua kuwa huyo ndiye Shirima adui yake. kwa sababu hakuwahi kumuona...  punde si punde simu ya Shirima ikaita.. akatabasamu na kuipokea simu hiyo.. akasema kwa sauti kubwa kiasi,, "HALLOW SHAMY..

    Zack akashtuka akajisemea moyoni,, "Shamy yupi?

    wazo likamjia kuwa ampigie simu Shamy.. akatoa simu yake haraka akapiga namba ya Shamy,,, akashtuka baada ya kuambiwa,, namba ya mteja unaempigia anaongea na simu nyingine!







    Zack akaingiwa na wasiwasi! punde si punde Shirima akamaliza kuongea na Shamy..

    Zack akaamua kumpigia tena simu Mchumba wake( Shamy) simu iliita bila kupokelewa!  Zack akahisi moyo wake unaripuka,, akajisemea moyoni,, "bila shaka yu alikuwa anaongea na Shamy wangu!  watu wengine sijui wanaakili gani,,, jitu zima linatongoza mabinti... sasa kwa umri wake akijilinganisha na Shamy ni sawa na mtoto wake wa kumzaa,, zaki alijisemea moyoni huku macho yake yakionyesha amejawa na jazba,, akanyanyuka kwa hasira akaparamia meza chupa iliyokuwa na sada ikadondoka na kupasuka,, wateja waliokuwepo kando yake wakawa wanamshangaa Zack,, akazipiga hatua mpaka kule alipokuwa amelipaki gari lake,, akaingia ndani ya gari na kuliondosha kwa kasi ya ajabu... kuelekea nyumbani,



                              *********************************



    Upande mwingine alionekana Shamy akiwa ndani ya gari lake,, akitokea kazini kuelekea nyumbani,, Shamy akajisemea moyoni,, "hii kazi ya kukesha usiku kucha,, inachosha sana mwili wangu hapa nilipo ninausingizi kupita kiasi,,

    baada ya dakika kadhaa kupita Shamy akafika nyumbani, akaegesha gari lake na kuingia ndani ya nyumba!  akapitiliza bafuni akaoga kisha akapanda kitandani kwa ajili ya kupumzisha mwili,



    wakati huo huo alionekana zaka akiliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu!,,,

    alipofika akamkuta Shamy kajilaza kitandani,,, hata bila salamu Zack akachukua simu ya Shamy akaangalia kuwa Shamy kaongea na nani mara ya mwisho!  macho yakamtoka akamtazama Shamy kwa hasira huku mwili wake unatetemeka... akasogelea na kuanza kumshushia kipigo kikali,, alimpiga bila huruma,, Shamy akapiga kelele za kuomba msaada huku akisema,, "JAMANI NAOMBENI MSAADA NAKUFAAA!

    kelele za Shamy zikazidi kumpandisha hasira zack akajikuta anaachia teke kali lililompata Shamy kifuani kwenye titi la kushoto,, Shamy akadondoka chini akatulia tuli!

    Zack akaingiwa na hofu,, jasho likamtoka huku anatetemeka,, akiamini huenda kauwa.

    akamsogelea Shamy akamuita huku akimtikisa, uso wa Shamy ulikuwa na majeraha yna damu ilitoka kwa wingi kwenye majeraha hayo,, Zack akaanza kulia huku, haja ndogo ikimtoka ikiambatana na vijampo vya mfululizo,, CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    punde si punde majirani wakafika,, ni baada ya kelele za Shamy kusikika vyema upande wa nje ya nyumba,, wasiwasi ukazidi kuongezeka Zack akatamani kukimbia lakini tayari alikuwa ameshachelewa..

    mmoja kati ya majirani hao waliokuja humo ndani,, alikuwepo afisa wa jeshi la polisi.. akaamua kumuweka Zack chini ya ulinzi.. kisha akapiga simu polisi akaamuru maaskari wawili waje akatoa anuani ya nyumba pamoja na mtaa..

    baada ya dakika kadhaa maaskari wakawa wamefika wakamchukua Zack na kumpeleka kwenye kituo cha polisi Chang'ombe.

    Shamy akakimbizwa haraka hospitali ya Muhimbili,,, manesi na madaktari walisikitishwa sana na hali aliyokuwanayo Shamy,, uso wake ulionekana kuvimba na majeraha ya mipasuko mikubwa... mbaya zaidi Shamy ni daktari tegemezi katika hospitali hiyo.. hivyo alipatiwa huduma ya kwanza kwa uangalifu wa hali ya juu!! Jopo la madaktari bingwa walihakikisha wanafanya jitihada za kuokoa maisha ya Shamy!

    Taarifa hizo zikamfikia daktari mkuu wa hospitali hiyo ambaye ni Shirima.. akafanya hima kuwahi hospitali,, akakuta Shamy kawekwa katika chumba maalumu cha msaada wa pumzi,, (I. C. U) Shamy hakuweza kuvuta na kutoa pumzi yeye mwenyewe hivyo akalazimika kuwekewa mipira maalu ya kusukuma hewa safi na kutoa hewa chafu,,mwilini(Oxigen machine)

    Shirima akauliza kapatwa na nini?  nesi akasema ,,"bado hatujapata taarifa kamili,lakini kaletwa na mtu huenda akawa ndugu yake,, Shirima akasema yuko wapi mtu huyo! nahitaji kuonana nae sasa hivi.

    nesi akaongozana na Shirima mpaka ke mapokezi,, wakamkuta mmoja kati ya wale majirani waliotoa msaada kwa Shamy,, Shirima akauliza,, "kapatwa na nini? 

    jirani huyo akasema,, "kapigwa na mume wake..

    Shirima akakasirika sana,, akajisemea moyoni,,"hii ndio? nafasi pekee ya kumiliki Shamy,,  nitahakikisha mtu huyo anafungwa miaka isiyopungua kumi,, kwanza huyu ndiye alikuwa anamchanganya Shamy mpaka asinipende mimi! sasa kaingia kwenye kumi na nane (18)zangu! ataisoma namba ya kirumi,,

    Shirima akaandaa mpango kabambe,, ili Zack afungwe zaidi ya miaka kumi gerezani.. wazo likamjia akakumbuka kuwa anaye rafiki ni kamishna wa jeshi la polisi.. hivyo aongee nae wambambikie kesi nyingine ikiambatana na kosa la kujaribu kuuwa kwa kukusudia...







    Baada ya kumaliza kuongea na kamishna wa jeshi la Polisi, Shirima akarudi ndani ya chumba maalumu cha msaada wa kusukuma hewa safi ndani ya mwili na kutoa hewa chafu mwilini(I.C.U) shirima alisikitika sana kumuona Shamy yupo kafika hali hiyo.



    Kesho yake,, kamishna akaandaa mpango wa kesi nzito ambayo haimuhusu Zack!

    wakati huo Zack aliwekwa maabusu,, pasipo mdhamana! 

    Siku zilizidi kusonga hatimae kesi ya Zack ikawadia,, akapandishwa kizimbani kusomewa mashtaka,,,

    akaonekana wakili mmoja aliyeandaliwa kwaajili ya kusema uwongo,,, hivyo kutokana na kazi yake ya kusimamia kesi mbalimbali,,aliaminika mbele ya mahakama hiyo,

    Hakimu akaanza kusoma mashtaka yanayomkabili Zack,,

    wakati huo Zack alikuwa kimya huku macho yamemtoka,, hakuamini alichokuwa anakisikia kutoka kwenye kinywa cha Hakimu! alistaajabu sana makosa yote yaliyosomwa akihusishwanayo,, hakuna hata moja alilolitenda,,

    akasimama wakili na kuanza kutoa ushahidi wa mashtaka yanayomkabili Zack,, wakili huyo akasema,, "Mnamo mwaka 2015 ndugu Zack alifanya tukio la ujambazi akishirikiana na wenzake,, wakavamia nyumbani kwa Daktari mkuu wa Muhimbi aitwae Shirima,,, wakapora madini ya dhahabu ambayo ni mali ya Shirima,, na baada ya kufanya tukio hilo la kuvamia na kupora kwa kutumia siraha za moto, wakatoweka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana!

    Wakili huyo,,baada ya kuongea uwongo uliotukuka,, akazipiga hatua kumsogelea Zack akauliza je unaweza kujitetea mbele ya mahakama? CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zack alibaki kimya pasipokuongea neno lolote,,huku macho yamemtoka kama mjusi kabanwa na mlango!

    kwa mbali alionekana Shirima akiwa kaketi akisikiliza kesi inavyokwenda,, uso wa Shirima ulionekana kujawa na tabasamu,,, akajisemea moyoni,, "tuvijana twingene tuving'ang'anizi,, sasa ngoja tuone jeuri yake iko wapi,, nani zaidi kati yangu mimi na yeye,,,



    Wakili akasema,, "siku kadhaa zilizopita ulijaribu kumuuwa mwanamke kwa kukusudia,, pia naomba uithibitishie mahakama,, kama huyo mwanamke ni mke wako halali wa ndoa,, onyesha cheti cha ndoa,



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog