Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Tano (5)
Roda akabaki mdomo wazi,, akainamisha uso wake akalitazama tumbo lake,, akajisemea moyoni,, "Mungu wangu inamaana Tobi ni jini? pia alikuwa akiniingilia kimwili miaka yote hiyo? sasa nimepata jibu la swali nililokuwa najiuliza kila siku, kwa nini kila nikiamka usingizini nakuta sehemu zakungu za siri zimelowana,kumbe ni Tobi,
nini hatma yangu? CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roda alijisewmea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu...,kumbe tarehe za kujifungua zilikuwa zimetimia,,, punde si punde akaanza kuhisi maumivu makali chini ya kiuno, pamoja na mgongoni!! maumivu hayo yalikuwa makali kupita kiasi,, yakahamia tumboni Roda akajikuta anashindwa hata kusimama,
wakati huohuo,,upande mwingine, lilionekana gari likiendeshwa kwa mwendo wa taratibu,, ndani ya gari hilo walikuwemo watu wawili,, mke na mume! watu hao walikuwa wamepotea njia,, kwa sababu ni wageni maeneo hayo,, walikuwa wanamtafuta ndugu yao aliyekuwa anaumwa kwa kipindi kirefu,, punde si punde Tobi akajitokeza kimiujiza ndani ya gari hilo! akabadilisha mawazo ya dereva huyo pasipo yeye mwenyewe kujionyesha,
Tobi aliamua kufanya hivyo ili dereva huyo akamsaidie Roda,, kumpeleka hospitali,,kisha akatoweka kimiujiza,,, punde si punde dereva wa gari hilo akaamua kukatisha kona na kuifuata barabara ya vumbi!!
kwa mbali akaona nyumba,,,akaamua kuifuata nyumba hiyo,, alipofika akashuka na kugonga hodi,,
wakati huo Roda alikuwa anatambaa utadhani mtoto mdogo,, huku akihisi maumivu makali kupita kiasi, (uchungu wa mimba) Roda akasikia mlango unagongwa, akaingiwa na matumaini ya kupata msaada wa kupelekwa hospitali.. akajaribu kulaza sauti huku akisema,, "FUNGUA MLANGO UPO WAZI, yule dereva akastushwa na sauti hiyo!
akajisemea moyoni bila shaka mtu huyu ni mgonjwa,,
dereva huyo hakujali,, akafungua mlango alipoingia upande wa ndani ya nyumba akashtuka kumuona Roda akiwa anatambaa huku machozi yakimtoka,,
Roda akasema naomba msaada nipeleke hospitali tafadhali nahisi uchungu wa mimba!
Dereva huyo akamnyanyua Roda na kutoka nae nje ya nyumba,, akamuingiza ndani ya gari,, mke wa dereva huyo akaingiwa na roho ya huruma akasema,,"najua unapata maumivu kupita kiasi kwa sababu hata miminpia nina watoto.. uchungubwa mimba unatesa kupita kiasi.. jikaze.. wakati anaongea maneno hayo,, dereva alikuwa tayari ameshaliondosha gari,,
wakiwa njiani Tobi akajitokeza ndani ya gari,, Roda akamuona Tobi kaketi kando yake,, lakini dereva pamoja na mkewe hawakuweza kumuona Tobi, Roda akasema,, "haya yote umeyasababisha wewe,,, tazama ninavyoteseka! kwa nini umenitenda hivi?
yule dereva pamoja na mkewe wakastaajabu,, kila mmoja akabaki anajiuliza anaongea na nani?
wakati huo Tobi alikuwa anatabasamu,, huku kashika viganja vya mikono ya Roda,
Tobi akasema,, "usiogope,, mimi ndiye mwanaume ninayekupenda na wewe ndiye mama wa mtoto wangu,, Roda akajibu,, lakini wewe ni jini,
mke wa dereva akamwambia mume wake,, huyu anaongea peke yake,,ni mimba ndiyo imemchanganya,, huwa inatokea kwa mama mjamzito,
safari iliendelea,, hakuna aliyetambua Roda anaongea na nani,, walihisi ni uchungu wa mimba tu inamchanganya! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya dakika kumi kupita wakafika hospitali.. Roda akapokelewa haraka akaingizwa kenye wodi maalumu ya wazazi,,,
Roda akaandaliwa kwa ajili ya kusukuma mtoto atoke tumboni...
alisukuma kwa muda mrefu lakini ikashindikana,,
punde si punde Tobi akajitokeza ndani ya wodi hiyo,,Roda akashtuka kumuona Tobi.. alipojaribu kuongea na Tobi,, sauiti haikutoka Roda akawa kama bubu!
Tobi akafumba macho yake,, ishara ya kuwasiliana na mama yake,(Malkia wa bahari)
ili apewe maelekezo jinsi ya kumchukua mtoto,,, malkia wa bahari akasema,, usichelewe ndani ya sekunde tatu.. mtoto atakapotoka tumboni... endapo utachelewa basi mtoto huyo atakuwa binadamu wa kawaida,, hatoweza tena kuwa jini! hivyo tutakuwa tumepoteza aseti,, na mtoto huyo ni muhimu kwetu..
Tobi akafumbua macho baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Malkia wa Bahari.
wakati huo huo zikasikika sauti za manesi wakimuhimiza Roda asukume bila kubana miguu ili mtoto atoke akiwa hai.
punde si punde akaingia nesi mwingine.. nesi huyo alikuwa na uwezo wa kuona majini pasipo kudhurika na chochote,, pia majini walikuwa wanamuogopa sana mtu wa aina hiyo! nesi huyo alikuwa na pete maalumu aliyoachiwa na marehemu bibi yake,, pete hiyo ni adui mkubwa wa majini.. Tobi akashtuka kumuona nesi huyo!
Punde si punde,, ikasikika sauti ya mtu,, akimuita nesi,, aliyekuwa anaingia ndani ya wodi hiyo ya wamama wajawazito. nesi huyo akaamua kufunga mlango na kurudi upande wa nje! kumba daktari ndiye alimuita nesi huyo,, ampe maagizo juu ya jambo fulani.
kule ndani ya wodi,, Tobi akaanza kuwa na wasiwasi kupita kiasi! akajisemea moyoni,, "huyu nesi anakitu ambacho ni adui wa majini,, na kama akirudi humu basi mpango wangu utavurugika,, na sijui kama mama(Malikia wa majini )atanielewa!
wakati huo Roda alikuwa anafanya jitihada za kusukuma mtoto huku manesi wakimuhiziza,, asukume bila kukata tamaa,, endapo ataacha kusukuma atambana mtoto hivyo mtoto huyo atakufa! Roda alijitahidi kusukuma,,
Manesi waliokuwemo ndani ya wodi hiyo,, hawakuwa na uwezo wa kumuona Tobi,, pia sasahivi Tobi hakutaka kujionyesha machoni mwa Roda,, Tobi akajisemea moyoni,, "wacha nifanye jambo fulani,, ili mpango wangu ukamilike.,,,,baada ya kuwaza hivyo akatoweka kimiujiza! akajitokeza kwenye korido inayokwenda kwenye wodi!! akuona yule daktari aliyempa maagizo yule nesi mwenye uwezo wa kuona majini!
Tobi akamfuata daktari huyo,, alipomuongelesha tu,, akili ya daktari hiyo ikabadilika,, akazipiga harakaharaka kutoka kwenye kordo hiyo na kuezlekea nje kabisa,,, kwa mbali akamuona yule nesi anarudi,, ni baada ya kumuagiza akalete taarifa ya maendeleo ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi nyingine,, tofauti na wodi ya wamama wajawazito.... daktari huyo akaendelea kuzipiga hatua mpaka akamkaribia nesi huyo,, kisha akamuagiza kuwa aende kwenye maabara akalete test tube.
nesi huyo akaondoka zake kuelekea maabara.
wakati huo huo kule kwenye wodi ya wamama wajawazito,, alionekana Roda akiendelea kufanya jitihada za kusukuma ili mtoto atoke tumboni, wale manesi waliokuwa ndani ya wodi hiyo walostaajabu sana,, kwa sababu limepita lisaa limoja Roda anasukuma lakini hakuna dalili zozote za mtoto kutoka tumboni! nesi mmoja akatoka nje ya wodi hiyo kwenda kumuita daktari haraka,, ili wajue wanamsaidia vipi Roda! kabla nesi huyo hajatoka ndani ya wodi hiyo,, akasikia sauti ya manesi wenzake wakisema,, "jitaidi sukuma kwanguvu, mtoto ameanza kutokeza kichwa,, endelea kusukuma,, Roda akasukuma hatimae mabega ya mtoto yakaanza kuchomoza kikabaki kiuno na miguu vikiwa upande wa ndani ya tumbo la Roda,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kule nje ya wodi alionekana Tobi akimtazama yule nesi akiishilizia kuelekea maabara..
alipohakikisha nesi huyo kafika mbali,, Tobi akaanza kupata amani,, akatabasamu kisha akatoweka kimiujiza akajitokeza ndani ya wodi ya wamama wajawazito.. akashtuka!!! macho yakamtoka,,ni baada ya kukuta tayari Mtoto amekwishazaliwa,, hivyo amechelewa kulikamilisha jambo la kumchukua mtoto huyo ndani ya sekunde kumi ili mtoto huyo asiwe binadamu wa kawaida,awe jini!
Tobi akajisemea moyoni,,"nimechelewa! mama (Malikia wa bahari) hawezi kunielewa!
na sijui itakuaje? bila kuchelewa Tobi akatoweka kimiujiza! kuelekea kule ujinini.
kutokana na kutumia nguvu nyingi, kusukuma mtoto lisaa limoja mfululizo, Roda aliishiwa nguvu baada ya mtoto kutoka tumboni alipoteza fahamu... manesi wakampa huduma ya kwanza,,ili kunusuru maisha yake!
***************************************
Upande mwingine,kule katikati chini ya bahari ya hindi,,(ujinini), alionekana Tobi akijitokeza mbele ya mama yake(Malkia wa bahari) akaeleza yote yaliyotokea..
Malkia wa bahari akakasirika sana,, kutokana na hasira alizokuwa nazo akabadilika na kuonekana kutisha kupita kiasi.. macho yake yalibadilika na kuwa mekundu pasipokuonekana mboni kiini cha jicho.. masikio yake yakawa marefu kama mbwa mwitu! bahari ikachafuka,, upepo mkali ukavuma kwa kasi... upepo huo ulitengeneza mawimbi makubwa kupita kiasi.... hata manahodha waliokuwa wakiendesha meli zilizokuwa zikipita juu ya bahari, wakaingiwa na hofu kupita kiasi!
kule chini ya bahari, alionekana Tobi akiwa katika hali ya uwoga wa hali ya juu,, alitambua vyema kuwa mama yake kakasirika kupita kiasi!!! na akifikia hatua hiyo ya kubadilika na kuonekana hivyo,, huwa anaingiwa na roho ya kikatiri!!mama Tobi(Malkia wa bahari) akazipiga hatua kumsogelea Tobi,, punde si punde kucha zake za mikononi, zikawa ndefu mara kumi ya kucha zake za kawaida Tobi akazipiga hatua kurudi nyuma!!!!!
Malikia wa bahari akanyanyua mkono wake iliamuadhibu Tobi,,
kwa kiwango cha hasira alizokuwanazo Malkia wa bahari, ambaye ni mama mzazi wa Tobi,, hapo Tobi yupo kwenye hatari kubwa ya kuuwawa!
Tobi akaongea maneno ya lugha ya kijini,, maneno ya lugha hiyo yanashahbiana na maneno ya lugha ya kiarabu! akimaanisha kuomba msamaha wa dhati kwa kutubu kosa lake mbele ya Malkia wa bahari! punde si punde Malkia wa bahari akabadilika na kurudi kagika umbile lake la kawaida,, akaonekana vile vile alivyokuwa bibi kizee.
akamtazama Tobi kwa macho ya mshangao! kisha akasema,, "pole sana mwanangu wa pekee,, haikuwa dhamira yangu kukuangamiza, ni hasira tu,,, na nimejizuia kwa kiwango cha juu... lakini bado unayo nafasi,,,ingawa ni mlolongo mrefu ambao unaweza kugharimu maisha yako,, na siwezi kukubali mtoto huyo kuishi huko duniani..
ni lazima aletwe nyumbani kwa ujinini akiwa tayari ameshakuwa jini... mtoto huyo ni aseti ya Miungu wa bahari,, akwa sababu damu yake inamchanganyiko wa nusu binadamu na nusu jini,, hivyo anauwezo mkubwa kuliko majini wa kawaida... na asipoletwa huku ujinini basi atakuwa adui mkubwa na majini kwa sababu atakuwa anawaona na atatuangamiza bila huruma,, hivyo kutakuwa na hatari ya kizazi hiki kutoweka kabisa!
wakati huo Tobi alikuwa makini kumsikiliza mama yake(Malikia wa bahari) ili asije akarudia tena kufanya kosa kwa mara nyingine.kisha akauliza nifanye jambo gani ili niweze kuikamilisha kazi hii?
Malikia wa bahari akajibu,, "itabidi uende bahari ya saba(07)ukatafute gamba la konokono mwekundu aliyekufa,, gamba hilo ni maalumu kitalazwa kichwa cha mtoto huyo juu ya gamba hilo.. ni kinga kwa mtoto huyo,,ni muhimu sana.
bila kuchelewa Tobi akatoweka kimiujiza, kuelekea kwenye bahari ya saba(7)
****************************************
Upande mwingine, kule hospitali alionekana Roda akizinduka, na kupata fahamu,,akashangaa kuona tumbo lake likiwa dogo,, akajiuliza,, "inamaana nimeshajifungua? je? mtoto yuko wapi?
wakati Roda anasukuma mtoto,,alipotoka tumboni aliishiwa nguvu,, kwa sababu alitumia nguvu nyingi sana kusukuma mtoto,, hivyo hakujua kilichoendelea baada ya hapo kwa sababu alikuwa tayari kapoteza fahamu!
punde si punde nesi akaingia kwenye wodi hiyo huku kambeba mtoto,, akamkabidhi Roda mwanae,, kisha akasema mnyonyeshe sasahivi,,
Roda akampokea mtot huyo huku akimtazama kwa macho ya umakininwa hali ya juu,, akajisemea moyoni,, "asije kuwa ni jini!
alijisemea hivyo huku akiukagua mwili wa kichanga huyo.
akagundua kuwa ni mtoto wa kawaida na sio jini! akaanza kumnyonyesha.
Kesho yake Roda akaruhusiwa kurudi nyumbani,, wakati anatoka akakutana na yule dereva pamoja na mkewe waliompa msaada wa kumleta hapo hospitali.. Roda hakuweza kuwakumbuka kwa sababu wakati wanamleta hospitali,, ilikuwa ni nyakati za usiku,, pia Roda alikuwa amechanganywa na maumivu makali ya uchungu wa mimba,, hivyo hakuweza kuwatazama nyuso zao!
wakamsalimia Roda kisha yule mwanamke akasema,, "hongera wana,, unatukumbuka? Roda akamtazama mwanamke huyo kwa mshangao! kisha akauliza,, "nyinyi ni nani?
yule mwanamke akajibu,, "sisis ndio tulikuleta hapa hospitali jana usiku,, hivyo tulikuwa tumekuja kukujulia hali.
Roda akaingiwa na kumbukumbu,, akakumbuka kuwa aliletwa hospitali lakini hawafahamu watu hao... akasema,, "nimekumbuka asanteni sana kwa msaada wenu.. mimi nimeruhusiwa kurudi nyumbani! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule dereva akasema,, "wacha tukupeleke nyumbani, .
Roda akakubali,, wakaongozana mpaka nje kabisa ya jengo la hospitali hiyo.. wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa Roda ikaanza.
walipofika waka, Roda akashuka kutoka ndani ya gari akaingia ndani kwake... akashtuka kukuta madhari ya ndani ya nyumba imebadilika,, kila kitu kimebadilishwa na kuwekwa vitu vipya na nyumba ilikuwa safi kupita kiasi!
Roda akastaajabu akajisemea moyoni,, "bila shaka huyu ni tobi ndio kafanya haya yote,, Eee Mungu nisaidie niomdolee hili balaa la huyu jini Tobi..Roda akazipiga hatua akaingia ndani ya chumba chake,, akastaajabu kukuta kumewekwa kitanda cha kifahari na xhumba kimependeza kwa mapambo ya kila aina pamoja na nguo za mtoto,, zikiwa juu ya kitanda,, Roda akaingiwa na hofu akidhani huenda Tobi yumo mdani ya nyumba! akaita Tobi,, lakini Tobi hakuitika!
Roda akakisogelea kitanda akamlaza mtoto huku macho yake yakitazama huku na kule!
baada ya nusu saa kupita akaanza kuingiwa na amani,, hakuona dalili yoyote ya Tobi kujitokeza,
kumbe Tobi kabla hajaenda kule kwenye bahari ya saba,, alirudi duniani akaingia kwenye maduka kimiujiza na kuchukua vitu vyote hivyo ndani ya dakika moja.. kisha akaviweka ndani ya nyumba ya Roda,, akatoweka kimiujiza kuelekea kule kwenye bahari ya saba(7) Tobi alifanikiw kupata gamba la konokono mwekundu aliyekufa..
Siku zilizidi kusonga,, hatiimae mtoto akatimiza miezi miwili na nusu.
Roda alimpenda sana mwanae,, lakini akawa anaishi kwa wasiwasi kwa kuhofia huenda Tobi akamchukua mtoto wake!
upande mwingine kule ujinini,, alionekana Malkia wa bahari, akiandaa mpango kabambe,, jinsi ya kwenda kumchukua mtoto huyo siku ya leo,, kabla jua halijazama!
Akamuongezea Tobi nguvu za kimiujiza ili aende akamlete mtoto huyo kwa wakati unaotakiwa... Malkia bahari akasema,, "nenda huko duniani mimi nipo nyuma yako,, chochote utakachokifanya mimi nitakusaidia.
bila kupoteza muda Tobi akatoweka kimiujiza kuelekea Duniani.. pia Malkia wabahari akatoweka kimiujiza kwa ajili ya kumlinda Tobi,, ili waikamilishe kazi ya kumchukua mtoto na kumpeleka ujinini.
Nyumbani kwa kwa Roda, alionekana akimnyonyesha mwanae,, huku akimtazama usoni,, akatabasamu kisha akajisemea moyoni,, "hakika nimeza mtoto mzuri sana kafanana na Tobi,, lakini ninawasiwasi,, huenda Tobi akamchukua mtoto huyu,, yanipasa niende kwa mchungaji,, nimueleze jambo hili,, naamini atanisaidia.. huwa naona mahubiri yake kwenye kioindi cha Runinga akiwaomnea watu kwa imani na matatizo yao yanakwisha!!! mimi sitaki kumuona Tobi,, na siwezi kuishi na jini,,lakini naamini huu ni mpango wa Mungu kutenda haya yote,, mimi sijui sababu ni nini,, ajuaye ni yeye pekee!
Real da aliongea maneno hayo kwa dhati ya moyo! wakati huo alikuwa akimnyonyesha mtoto,, alipomtazama akagundua kuwa mtoto amesinzia akamlaza kitandani,,,
akaingia bafuni akaoga,,kisha akarudi chumbani akajilaza kando ya mtoto wake.. ghafla wazo likamjia akajisemea moyoni,, "kwa nini nisiende sasahivi.. kanisani kwake napajua.
****************************************
Upande mwingine alionekana Tobi pamoja na mama yake(Malkia wa bahari) wakijitokeza kimiujiza kando ya bahari! jirani na Cocobeach
wakazipiga hatua kuifuata barabara iliyokuwa jirani na bahari... Tobi akasema,, "kuna watu wawili mume na mke,, niliwaongoza waifuate nyumba ya Roda pasipo wenyewe kujijua... wakampa msaada wa kumpeleka hospitali,,unaonaje tukiwatumia watu hao ili iwe rahisi kumchukua mtoto?
Malkia wa bahari akasema ni jambo jema,, kwa sababu huwezi kumchukua hivi hivi,, ukiwa katika umbile lako halisi,, na ukiwa katika umbile la kijini pia huwezi kumchukua! kwa sababu damu yake ya yako zinamvutano,, ni damu moja.... hivyo ni lazima uingie katika kiwiliwili cha binadamu wa kawaida,, hapo ndipo utaweza kumchukua pasipo tatizo lolote!
Tobi akaangaza angaza macho yake huku na kule.. kwa kutumia uwezo wake wa kijini.. akaweza kujua ni wapi wanapoishi wale wanandoa waliompa msaada Roda kumpeleka hospitali.. kisha akasema,, "nimeshapajua ni wapi wanapoishi.. wakatoweka kimiujiza kuelekea kwenye nyumba hiyo! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo huo alionekana Roda akiwa amemaliza kujiandaa kwenda kanisani kwa mchungaji,,, akatazama saa ya ukutani ilikuwa ni saa kumi na dakika kadhaa. akamchukua mtoto wake,, akambeba kwa kumkumbata kisha akatoka nje ya nyumba yake... akaelekea kwenye kituo cha daladala... kabla hajafika huko,, akaonekana mwanamke akimsimamisha Roda,, Roda akasimama,, mwanamke huyo ni yule nesi mwenye pete yenye uwezo wa kupambana na majini.. pia pete hiyo ni adui mkubwa wa majini!
nesi huyo akasema najua huwezi kunikumbuka kwa sababu ulipoteza fahamu wakati unajifungua,, mimi ni nesi kwenye ile hospitali.
Roda akatabasam,kisha akasema,, "asante sana mimi naishi maeneo haya haya.......kama hautojali twende ukapafahamu pia nashukuru sana kwa msaada wenu nimejifungua salama,, bila kuchelew. a wakaongozana kurudi nyumbani kwa Roda.
walipofika Nesi huyo akambeba mtoto,, akashtuka akamtazama kwa makini mtoto huyo,,akaona anabadilikabadilika,, anakuwa mtoto wa kutisha mwenye manyoya na masikio marefu,!!!, pia anaonekana kurudi katika umbile la mtotonwa kawaida!
Roda akauliza,, unatumia kinywaji gani?
nesi huyo akainua uso wake na kumtazama Roda,, akasema,, "usijali kwa sasa sijisikii kunywa kitu chochote. kwani ulikuwa unaenda wapi?
Roda akajibu,, "nilikuwa naenda kanisani kwa mchungaji... lakini hakuna shaka nitakwenda tu kwa sababu hakuna umbali kutoka hapa nyumbani kwangu..
Nesi huyo akasema,, "inaonekana unatatizo na tatizo hilo sina uhakika kama unalijua!
Roda akashtuka,, akahisi huenda huyo ni Tobi kajibadilisha kwenye umbile la kike!
mqcho yakamtoka akauliza kwa mshangao! wewe umejuaje?
nesi huyo akasema,, "mumeo yuko wapi? namaanisha baba wa mtoto huyu!
Roda akazidi kuchanganyikiwa,, akabaki mdomo wazi!
Roda akasema,, "yupo lakini katoka atarejea baadae.
nesi huyo akasema,, "huyu mtoto wako anachembechembe za damu ya binadamu iliyochanganyikana na damu ya jini!
Roda akaingiwa na hofu kupita kiasi! akasema,, "najua wewe ni Tobi kwanini unaninyima furaha katika maisha yangu?
Nesi huyo akashtuka! akauliza,, "Tobi ni nani?
Roda akazidi kuchanganyikiwa.. akasema kama wewe sio Tobi ni nani? na umejuaje haya yote?
wati huo huo,,upande mwingine alionekana Tobi na mama yake wakijitokeza kwenye nyumba ya yulez mume na mke waliomsaidia Roda kumpeleka hospitali!
wakawakuta wanandoa hao wamejilaza chumbani wamepumzika! Tobi akaingia kwenye kiwiliwili cha mwanaume huyo huyo,, na Malkia wa bahari akaingia kwenye kiwilwili cha yule mwanamke...
pumde si punde wakashyuka kutoka usingizini kwa wakati mmoja,, wakawa na wazo la kwenda kumtembelea Roda ke nyumbani kwake!
bila kuchelewa wakajiandaa na kuingia ndani ya gari,, safari ya kwenda nyumbani kwa Roda ikaanza!
walipofika wakaingia wakashuka kutoka ndani ya gari na kugonga mlango wa Roda.
wakati huo Roda alikuwa anamsimulia nesi kila kitu kilichompata.. Roda akashtuka kusikia mlqngo unagongwa akajisemea moyoni,, "ni nani huyo anayegonga mlango?
kule nje Malkia wa bahari akaanza kuhisi hali ya hatari,, akasema,, "bila shaka sehemu hii kunaadui yetu!
pia Tobi akahisi harufu hiyo ya hatari... wakatoweka kimiujiza kutoka kwenye miili ya wana ndoa hao wawili!
punde si punde wanandoa hao wakajishangaa, kujikuta hapo!
wakaangaza angaza macho yao wakaliona gari lao! mwanamke huyo akamuuliza mumewe,, "tumefikaje hapa? mbonw kila nikivuta kumbukumbu sikumbuki kitu,, zadi ya kukumbuka kuwa tulikuwa nyumbani tumelala.
punde si punde Roda akafungua mlango,, akashtuka kuwaona watu hao.. kisha akasema,, "karibuni.
wanandoa hao wakatazamana usoni hawakuongea neno lolote wakaondoka zao na kuingia ndani ya gari kurudi nyumbani! huku wakiwa wametawaliwa na hofu kupita kiasi!
Malkia wa bahari pamoja na Tobi wakajitokeza kwenye ufukwe wa bahari!
pia jua lilikuwa tayari limeanza kuzama hivyo mpango wao ukashindikana.. wakatoweka kimiujiza kurudi ujinini kule chini ya bahari!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo huo kule nyumbani kwa Roda alionekana bado akiendelea kumsimulia,, yule nesi mkasa wote uliompata.. nesi huyo akamuonea huruma sana,, kisha akasema hili ni tatizo usipokuwa makini utampoteza mtoto,, kwa sababu ni lazima waje kumchukua mtoto wao!
kisha nesi huyo akanyanyuka na kumuaga Roda,, akamrudishia mtoto wake!
Roda hakuwa na kipingamizi,, akaongozana na nesi huyo mpaka nje ya nyumba..nesi akaondoka zake Roda akaelekea kanisani kwa mchungaji... kwa bahati nzuri akamkuta mchungaji,, anatoka kwenye ofisi iliyokando ya kanisa lake.
Roda akamsalimia mchungaji,, kisha akasimulia mkasa mzima..
bila kuchelewa mchungaji akasema,," tuingie kanisani,, wakaongozana mpaka ndani ya kanisa,, Mchungaji akasema,, "mlaze mtoto huyo hapo juu ya meza.. nianze maombi.
Roda akafanya kama alivyoagizwa na mchungaji, akamlaza mtoto pale juu ya meza.
Mchungaji akaanza kufanya maombi......akiwa katikati ya maombi.. mtoto akaanza kulia kwa sauti kali kupita kiasi akaanza kubadilika na kuwa mtoto wa kutisha... punde si punde ukatoka mwanga mkali ndani ya mwili wa mtoto huyo... akarudi katika umbile lake la kawaida.. mchungaji akaendelea kufanya maombi kwa imani kali nila kusita.
na baada ya dakika kadhaa kupita mchungaji akahitimisha kwa kusema,, "Amen.
Mtoto akanyamaza,, kisha mchungaji akasema,, "sasa waweza kwenda lakininusisahau kusali mara kwa mara,, usisahau kumkumbuka Mungu wako!.
wakati huo Roda alikuwa kabaki mdomo wazi juku macho yamemtoka akimtazama mtoto wake,, yani alikuwa aamini kile alichokishuhudia... mchungaji akasema,, "ondoa shaka Mungu yu pamoja nawe,, ukimuamini na kumtumikia yeye atakulinda kwa kila jambo..kisha mchungaji akazipiga hatua akachukua biblia moja na kumkabidhi Roda huku akisema,, "mara kwa mara jifunze kusoma maandiko ya kwenye biblia.....utajifunza mabo mengi ya kumtumainia Mungu muumba.
Roda akaipokea biblia hiyo kisha akamchukua mwanae.. na kuondoka zake kurudi nyumbani!
**************************************
Upande mwingine kule ujinini, alionekana,, Malkia wa bahari pamoja na Tobi...
Malkia wabahari akasema kwa lugha ya kijini akimaanisha,, " tumechelewa na jua limeshazama! kule duniani usiku umeanza kuingia ambavyo huku kwetu ndio panaanza kukucha,, hivyo tutaifanya kazi hii kesho,,
kama ilivyo kawaida viumbe wa kuzimu,, wanaishi tofauti na maisha ya binadamu!
huku duniani,,nyakati za mchana,, lakini huko kuzimu ni usiku wa manane..
na huko kuzimu nyakati za mchana,,,, huku duniani ni nyakati za usiku wa manane..
Kesho yake mipango ukaendelea wakajipanga kwenda duniani kumchukua mtoto wa Roda wampeleke ujinini.
Kule nyumbani kwa Roda alionekana yupo sebuleni akiwa anasali kwa imani huku kashikilia biblia.. alipomaliza akaingia jikoni kuandaa chakula wakati huo mtoto alikwa kalala usingizi juu ya sofa.
punde si punde Tobi na Mama yake(Malkia wa bahari akasema wakajitokeza ndani ya nyumba ya Roda upande wa sebuleni,, wakastaajabu kumuona mtoto haonekani kuwa na chembechembe zozote za ujini! Malkia wa bahari akasema bila shaka hapa kunajambo limetendeka! haiwezekani iwe hivi.. punde si punde mtoto akashtuka kutoka usingizini akaanza kulia,, Roda akatoka jikoni haraka kuelekea sebuleni.
akashtuka kumuona Tobi pamoja na Mwanamke mzee sana ambaye ndiye
mama Tobi(Malkia wa bahari) Roda akakumbuka maneno ya mchungaji,, kuwa afanye maombi kwa imani mara kwa mara,
bila kuchelewa Roda akaanza kusali huku akikemea kwa imani.. Tobi na Malkia wa bahari wakaanza kuhisi wanaunguzwa na moto mkali,, walipojaribu kutoweka kimiujiza ikashindikana.. wakaanza kupiga kelele za maumivu makali!
Roda akaendelea kusali bila kusita.. punde si punde wakaanza kuwaka moto.. hatimae wakateketea kabisa na kubaki majivu... ikawa ndio mwisho wa Tobi ma Malkia wa bahari.
Roda,,akamchukua mwanae haraka akambeba.. kisha akaichukua biblia na kuikumbatia.
akaamua kufanya mpango wa kuhama ndani ya nyumba hiyo siku hiyohiyo.. akahamia Temeke,,
siku zilizidi kusonga,, Roda hakuona mauzauza tena.. akaishi kwa amani na furahmiaka ikazidi kusonga hatimae mtoto akatimiza umri wa miaka kumi na nane(18) binti huyo anaitwa
SIMA. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roda akashindwa kuvumilia kuificha siri kwa mwanae.. kwa sababu kila kukicha binti huyo alimuuliza mama yake kuwa baba yake mzazi yuko wapi... Roda akamsimulia mkasa wote... binti huyo akastaajabu sana,, lakini akajipa moyo kwa kumtumainia Mungu... huku akijisemea moyoni,, "Mungu ndiye muweza wa yote,, amenileta duniani kwa namna hii,, MUNGU ndiye baba yangu pekee.
maisha yaliendelea,,wakaishi kwa amani na furaha.
******************MWISHO******************
0 comments:
Post a Comment