Search This Blog

BAHARI YA HINDI - 4

 







    Simulizi : Bahari Ya Hindi

    Sehemu Ya Nne (4)





    Roda akashtuka akaingiwa na wasiwasi! Tobi akasema,,"jisikie huru mimi siwezi kikudhuru tatizo wewe ulienda kinyume na matakwa ya majini! katika safari yako uliyokuwa unasafiri kwenye meli...ulibeba kitu ndani ya begi lako..kitu hicho kilikuwa kinahabari kuhusu majini na viumbe wa kimiujiza!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akashtuka! akajaribu kuvuta kumbukumbu,ilikuwa hivi!

    Siku moja Roda alidamka asubuhi,,akajiandaa haraka haraka kwenda kazini....Siku hiyo alidamka kachelewa...... .alikuwa anahitajika aende kwenye jumba la makumbusho ya kale,,akaandike habari inayohusiana na mambo ya yanayosadikika ya kimiujiza!!

    alipofika katika jumba hilo la makumbusho aliendelea kuhoji wahusika wanaohusika na kutunza historia ya makumbusho hayo...

    akiwa ndani ya jumba hilo katika pitapita zake akaona kipande cha sanamu! kipande chicho cha sanamu..kilikuwa kimetengenezwa kwa madini ya Rubi nyekundu.  akakiokota kipande hicho akakiweka kwenye mfuko wa suruali yake ya jinsi(kitambaa kigumu) aliyokuwa ameivaa..

    akaendelea na utafiti wa kuchambua habari zinazohusiana na majini na viumbe wa kimiujiza!



    wiki moja baadae,,akiwa kazini katika kituo cha habari ambapo alipokuwa anafanyia kazi..akaletewa barua kuwa anatakiwa aende zanzibar kukamilisha taarifa ambazo anatakiwa aziwasilishe kazini zikiwa kamili.

    pia akakumbuka kuwa siku ambayo alisafiri...aliweka nguo zote ndani ya begi lake kwa sababu safari yake ya kwenda Zanzibar..angebaki huko kwa wiki nne(4) mwezi mzima..miongoni mwa nguo alizoziweka ndani ya begi,,,ni ile suruali ya jinsi ambayo inakipande cha sanamu iliyotengenezwa kwa madini ya Rubi! kipande hicho alisahau kukitoa ndani ya suruali hiyo....

    akashtuka akasema,,"nimefanya nini mimi? kosa langu ni lipi? au tatizo ni kile kidubwasha nilichokiokota kule kwenye jumba la makumbusho?

    kitendo cha Roda kuita Rubi kidubwasha! kilimkasirisha Tobi!!!! akabadilika na kuwa na sura ya kutisha!!! meno yake ya mbele yakarefuka ndani ya sekunde moja....

    Roda akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi! hakuwahi kumuona Tobi katika muonekano huo!...

    Tobi akamsogelea Roda akamwambia,,"unanikosea heshima mbele ya Malkia wa bahari..ambaye ni mama yangu mzazi!

    kutokana na hasira Tobi akajikuta anamkaba shingo Roda kwa mkono wake...

    Malkia wa bahari akagundua kuwa mwanae Tobi kakasirika kwa sababu Roda kadhalilisha Rubi!!

    akamzuia Tobi asifanye jambo lolote baya kwa kusema,,"huyu ni mpenzi wako,,chaguo langu mimi pamoja na miungu wa bahari.nakusihi mwanangu isimdhuru binti huyu!

    Ghafla Tobi akabadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida....akashtuka akamwambia Roda,,"samahani,haikuwa kusudio langu wewe ndiye amani ya moyo wangu....

    Roda alibaki kimya bila kujibu kitu chochote akimtazama Tobi kwa macho ya mshangao!

    Tobi akasema,,"nisamehe mpenzi..Roda akabaki akimshangaa Tobi!! kisha akamuuliza,,"kwa nini unaniita mimi mpenzi wako?

    Tobi akageuka nyuma na kuzipiga hatua kadhaa,kisha akajibu,,"nakuita mpenzi kwa sababu nakupenda na wewe ndiye chaguo langu..pia ni chaguo la Malkia wa bahari!

    Roda akashtuka akasema,,"mbona mimi sina hisia zozote za kimapenzi na wewe?

    Tobi akasema,,"kumbuka masaa kumi na sita yaliyopita tulikuwa kitandani ukasema kuwa umekubali kuwa wangu!

    Roda akaingiwa na wasiwasi akajilaumu kwa ule mpango wake aliodhani kwamba ni sahihi,,kwa kumkubalia Tobi ombi lake la yeye kuwa mpenzi wake!!!!



    Tobi akacheka kicheko cha sekunde tatu kisha uso wake ukawa kama mtu ambaye hajacheka!! akasema ,,"mimi siwezi kukudhuru bali wewe ndiye unataka kujiletea mauti.

    Macho yakamtoka Roda! baada ya kusikia kauli hiyo..akauliza kwa mshangao,,"Mauti?? mimi nimefanya kosa gani litakalosababisha uniuwe?

    Swali hilo lilimfadhaisha Tobi akajikuta amtazama Roda kwa macho ya huruma!

    Malkia wa bahari akatoweka kimiujiza! akamuacha Tobi na Roda wakiwa peke yao.

    Tobi akaongea kwa sauti ya chini,,"nakukupenda sana Roda..na sihitaji kukukosa..

    Tobi aliendelea kuongea maneno matamu yenye ushawishi wa asilimia mia moja(100%) Roda akajikuta anamuamini Tobi kwa asilimia zote!

    Roda akasema,,"nakupenda pia!...

    Tobi akafarijika na jibu la Roda lenye hamasa ya mahaba mubashara!!!! kisha akasema,,"haupo kwenye kifungo! mimi ndiye mkombozi wa maisha yako..Malkia wa bahari alitaka kuondoa uhai wako..kwa sababu ulibeba Rubi nyekundu ndani ya begi lako na ukapita juu ya himaya yake!!!

    lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu wewe ni mtu muhimu kwangu..adhabu amboyo ulitakiwa upate wewe  akaamua kuwapa abiria wenzako....kwa kunywa damu yao.

    Roda akauliza,,"mama yako anakunywa damu ya binadamu?

    Tobi hakutaka kuongea ukweli kuhusu hilo akajibu kwa kudanganya,,"hapana aliwapa adhabu tu ya kawaida..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akauliza kwa msisitizo,,!!"wewe umesema alikunywa damu ya abiria wenzangu!?

    Tobi akaamua kufanya miujiza ya nguvu za giza ilimradi Roda asiendelee kumuuliza maswali na asifahamu ukweli wowote kuhusu hilo!

    akatazama kando yake pakabadilika na kuonekana ni mbuga ya wanyama! kisha akamsogelea Roda na kumkumbatia..pumde si punde wakajikuta wamo ndani ya mbuga Ya wanyama! Roda akafurahi sana..mawazo yake yote yakatoweka yakahamia kutazama wanyama aliowaona mbele yake....

    Tobi akagumdua kuwa Roda amesahau kila kitu..akaamua kufanya jambo ili asije kukumbuka chochote..akamtazama machoni..ukatoka mwanga wenye rangi nyingi.ukaingia machoni mwa Roda...ukafuta kumbukumbu zote..

    Roda akawa hakumbuki kitu chochote alichokiona kabla.



    Tobi akamgusa Roda kichwani..pasipo Roda kujua kuwa Tobi analengo gani! Ghafla Roda akajikuta yupo nyumbani kwake akiwa chumbani.Roda hakuweza kugundua kitu chochote kilichotokea juu yake! kwa sababu Tobi alifuta kumbukumbu ya matukio yote yaliyotokea aliyoyashuhudia Roda machoni mwake..akanyanyuka kutoka kitandani,,akajiandaa kuelekea kazini...kabla hajatoka akasikia mlango wa sebuleni unagongwa!







    akaenda kuufungua...akamuona Tobi..Roda akatabadam na kusema,,"karibu.

    Tobi akajibu,,"asante nimekuja kukupitia twende kazini..

    Roda akasema,,"nilikuwa namalizia kujiandaa..

    Tobi akasema,,"sawa hakuna shaka wacha nikusubiri ndani ya gari...

    Roda akafunga mlango na kuendelea kuweka vitu vyake sawa.....



    Kule ndani ya gari alionekana Tobi,, uso wake ulikuwa umejaa tabasamu..punde si punde Roda akatoka ndani ya nyumba na kuufunga mlango wake..akazipiga hatua kulifuata gari la Tobi.

    safari ilaanza...walipofika kazini kazi zikaendelea kama kawaida,

    mmoja kati ya wafanyakazi wenzake akamfuata na kumuuliza jambo fulani...Roda akaonekana kishangaa baada ya mfanyakazi mwenzake kumuuliza mambo ambayo hayajui...

    Roda akasema mbona sikumbuki! kitu chochote kuhusu jambo uliloniuliza!

    yule mfanyakazi akaamua kuondoka kwa kuhisi kuwa Roda amemdharau!

    Roda akawasha kompyuta anayoitumia kuhifadhi kumbukumbu ya kazi zake! akastaajabu kuona ni mwaka 2017...akashtuka akahisi huenda kompyta yake imeharibu mpangilio(setting's)

    kumbe ni miaka kumi imepita tangu apelekwe kule ujinini..

    kumbe Tobi alifanya jambo la kimiujiza..miaka hiyo yote nafsi ya Roda ambayo ni kivuli chake ilikuwa inakwenda kazini kama kawaida..lakini ilikuwa ndani ya mwili wa mtu wingine...Roda halisi alikuwepo kule ujinini kwa kipindi cha miaka yote hiyo....

    Roda hakujali akaendelea kufanya kazi,bila kutambua yaliyotokea.



    siku zilizidi kusonga kusonga,,maishau yakaendelea...lakini Roda akilala nyakati za usiku.Tobi alikuwa anamtokea na kumuingilia kimwili,,pasipo Roda kujua chochote. Roda akawa anahisi ni ndoto,,lakini akajiuliza maswali mengi pasipokupata jibu,,"kwa nini  kila siku naota nafanya mapenzi na mtu ambaye siioni sura yake.na nikwanini ndoto hii ijirudie kila siku?



    siku zilizidi kusonga,,na miaka ikasogea.,,,,siku moja Tobi alikwenda nyumbani kwa Roda,,ilikuwa ni siku ya mapumziko ya kazi..

    Tobi akaanza kumchombeza Roda....

    Roda akaishia kutabasamh tu bila kujibu kitu chochote..wakaendelea kubadilisha mawazo kwa maingezi mbalimbali..

    Baada ya masaa mawili kipita Tobi akamuaga Roda na kuondoka zake.

    siku zilizidi kusonga..Tobi aliendelea kumtokea Roda nyakati za usiku na kifanyanae mapenzi pasipo Roda kufahamu...

    siku ya leo majira ya usiku wa manane..Tobi altokea Roda na kufanyanae Mapenzi...ghafla Roda akashtuka kutoka usingizini...akahisi kama kalowana sehemu zake za siri! akanyanyuka na kuwasha taa akashtuka kukuta kweli kalowana..alipojishika kwa mkono wake akagundua kuwa ni manii..macho yakamtoka akajisemea moyoni,,"ndoto gani ya namna hii...akaanza kuingiwa wasiwasi..akaamua kusali..kisha akaingia bafuni na kujisafisha mwili.

    alipomaliza akarudi chbani akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                           ************************



    Asubuhi palipokucha,Roda akadamka akajiandaa na kuelekea kazini ....alipofika akaingia ofisini..Tobi akamfuata wakasalimiana kisha akamuuliza ,,"umeamkaje?

    Roda akasema niko njema..lakini kunajambo linanitatiza,

    Tobi akatabasamu akajua kile ambacho Roda anataka kumwambia.

    Roda akaanza kumwambia Tobi kuhusu ndoto anayoiota  kila siku! Tobi akacheka kisha akasema,,"hiyo ni ndoto tu, yawezekana kunamwanaume unampenda sana...na kama hayupo basi inaonekana umeishi muda mrefu pasipo kushirikiana kimwili...mawazo yako ndio yanakufanya wewe uote ndoto kama hizo!

    wakati huo Roda alikuwa anamsikiliza Tobi kwa umakini...kisha akasema,,"labda ni kweli kwa sababu ninamida mrefu sana sijashirikiana kimwili..sikumbuki mara ya mwisho ilikuwa ni lini!     

    Tobi akauliza swali la kimitego,,"bafo hujafikiria kuolewa?

    Roda akatabasamu kisha akajibu,,"kwa sass bado sijampata mtu ninayempenda..

    Tobi akadakia! akasema lakini kumbuka nilishakuambia kuhusu mahusiano baina yangu mimi na wewe laki hukunijibu chochote..uliishia kitabasamu tu....kwanini usinipe nafasi hiyo..nikumiliki....Tobi aliongea maneno hayo huku akimtazama Roda machoni..

    Roda akauliza,,"tangu nimekufahamu sijawahi kukuona ukipiga kope! unatatizo gani machoni mwako?

    Tobi akashtuka kwa sababu alijua kuwa majini hawana uwezo wa kupiga kope kama walivyo binadamu wakawaida!! akajibu kwa kudanganya,,"mimi ndivyo nilivyozaliwa hivi..

    Roda akastaajabu lakini hakujali..



    Ilipofika jioni ,,muda wa kazi ulikwisha,Roda akaondoka na kuelekea nyumbani kwake....akajilaz akabaki anatafakali,,kuhusu yale maneno ya Tobi..akajikuta anapitiwa na usingizi akasinzia!

    baada ya masaa kadhaa kupita akashtuka usingizini..alipotazama saa ilikuwa ni saa tano za usiku..akanyanyuka na kuingia jikoni..akachulua mayaianne akayakaanga ...kisha akachukua juisi ndani ya friji..akaanza kula na kunywa juisi hiyo..akaingia bafuni akaoga kisha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi....

    ilipofika saa saba za usiku,,,Tobi akajitokeza mdani ya chumba cha Roda..akamtazama kwa macho ya matamanio akavua kofia yake aliyokuwa ameivaa kichwani..akafungua mkanda,,akapanda kitandani na kuanza kumuinhilia kimwili Roda....alipomaliza tu..Roda akashtuka kutoka usingizini..Tobi akatoweka kimiujiza....akasahau kofia yake juu ya meza iliyokuwemo ndani ya chumba cha Roda..

    Roda akajisemea moyoni,,"hivi ni kwanini huwa naota naingiliwa kimwili na mtu asiyeonekana sura yake? na nikwanini mdoto hii inajirudia kila siku?

    Roda akanyanyuka nabkuwasha taa...akashtuka kuona kofia ipo juu ya meza!!

    akaitambua kofia hiyo kuwa ni ya Tobi! akajiuliza moyoni,,"kofia hii imefikaje chumbani kwangu?

    nani kaileta humu..







    Roda akaingiwa na wasi wasi hofu ikazidi kuongezeka.. akatoka chumbani,, akaelekea bafuni,, akaoga kisha akarudi chumbani,, akashtuka,, macho yakamtoka alipotazama pale juu ya meza hakuiona tena ile kofia,, akajiuliza moyoni,, "hivi hii ilikuwa ni ndoto

    au niliona kwa macho yangu!!?  mbona akama niliona kofia hapa juu ya meza na nikaishika kwa mikono yangu! 

    basi kama ilikuwa ni ndoto,,,nahisi naanza kuchanganyikiwa.!

    Roda hakujali akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi..

    baada ya lisaa limoja kupita Roda alisinzia usingizi mzito.. Tobi akajitokeza chumbani kwa Roda,, akachukua shuka ndani ya kabati akamfunika Roda.. kisha akamvusu shavuni....

    Tobi akasimama wima,, akatoweka kiujiza. 



                      ************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi palipokucha,, Roda alidamka na kujiandaa kwenda kazini,,

    baada ya nusu saakupita Roda alimaliza kujiandaa, kisha akaondoka zake, kuelekea kazini.

    alipofika akamuona Tobi anaingia ofisini kwake,, wakasalimiana,, lakini Roda alikuwa anaitazama kofia ya Tobi aliyoivaa kichwani.

    Roda akasema,, "usiku wa kuamkia leo,nimeota kofia yako,, imo chumbani kwangu juu ya meza kisha sikuiona tena,, Tobi akacheka akasema,, "inaonekana kuna habari njema kuhusu ombi langu kwako.. Roda akatabasamu akabaki kimya pasipokuongea neno lolote! 

    Tobi akasema wacha nikaendelee na majukumu ya kazi Tutaonge baadae.



        ******BAADA YA WIKI MOJA KUPITA******



    Roda akaanza kujisikia tofauti.. akawa anapenda kulala pia mwili wake ulikuwa na uchovu muda wote,, akaanza kupoteza hamu ya kula!!

    siku zilivyozidi kusonga Roda akawa anatapika mara kwa mara,, akahisi huenda anamaralia, akaamua kwenda hospitali kufanyiwa vipimo vya damu! 

    lakini majibu ya vipimo vya damu yakathibitisha kuwa hana tatizo lolote mwilini mwake,,

    Roda akaamua kurudi nyumbani kwake,, lakini bqdo hali hiyo ilijitokeza mara kwa mara,, akawa anatamani kula vitu vyenye uchachu, kama maembe mabichi na ndimu...

    hali hiyo ilizidi kumtesa kila siku,, akaamua kurudi hospitali..

    akafanyiwa vipimo vya mkojo na haja kubwa... majibu yalipotoka yakathibitisha kuwa Roda ni mjamzito!  anamimba ya mwezi mmoja!



    Roda akasema,,"wahusika wa kitengo cha maabara hawapo makini na kazi yao! yawwzekana wamechanganya vipimo vyangu na vya mtu mwingine mimi wina ujauzito na ninamwaka mmoja sijashirikiana kimwili! daktari akabaki mdomo wazi... Roda akazipiga hatua na kuondoka zake..

    akarudi nyumbani....



                     ***********************



    ilipofika majira ya saa sita za usiku.. alionekana Tobi akijitokeza kule ujinini,,, akamwambia mama yake ,,"nina habari njema,, Mchumba wangu anaujauzito!  Malkia wa bahari akafurahi sana akampongeza kijana wake, kisha akasema,,, sasa fanya haraka iwezekanavyo siku atakayozaliwa mtoto huyo hakikisha haupotezi dakika wala sekunde,, kumleta huku ujinini,, vinginevyo hawezi kuwa mwenzetu kqma akivuta hewa ya duniani kwa sekunde kumi na mbili(12).

    Tobi akasema sawa nimekuelewa ewe Malkia wa bahari,  kisha akatoweka kimiujiza kurudi duniani..

    miezi ilizidi kusonga Roda akawa haoni mzunguko wa siku zake kila mwezi,, akaona tumbo lake linazidi kukuwa kadri miezi ilivyozidi kusonga,, Roda akaanza kuingiwa na wasiwasi akafanya iwe siri yake.. lakini tumbo la mimba halifichiki,, hatimae wafanyakazi wenzake wote wakajua kuwa Roda ni mjamzito!! 

    Tobi akawa na ukaribu wa hali ya juu kwa Roda..

    akawa anamuuliza maswali ambayo majibu yake anayajua,, "hivi baba wa mtoto aliye tumboni mwako yuko wapi?

    Roda alikosa jibu, kwa sababu kila akijaribu kukumbuka mahusiano yake,, ni mwaka mmoja uliopita,, akilinganisha na umri wa ujauzito wake hakuna uwiano!!  kitendo hicho kilimfanya roda awe na hofu pia wasiwasi,,



    Siku moja nyakati za usiku wa manane,, Roda alikuwa kalala chumbani mwake,,, ghafla Tobi akajitokeza akaanza kulipapasa tumbo la Roda,, kisha akalibusu akanyanyuka na kuzipiga hatua

    Punde si punde Roda akashtuka kutoka usingizini,, akashtuka kumuona mtu anaishirizia ukutani,,, mtu huyo alioneka kavaa viatu na nguo zinazofanana na nguo na viatu vya Tobi..

    Roda akanyanyuka haraka kutoka kitandani... akachukua simu yake na kumpigia Tobi.... ukasikika mlio wa simu ikiita sebuleni kwake,, Roda akakata simu haraka kisha akapiga tena... simu ya Tobi ikaita kule sebuleni,,, Roda akaingiwa na wasiwasi.. hofu kubwa ikatanda juu yake,, akafungua mlango taratibu akatoka nje ya chumba chake,,, akazipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa umakini mkubwa..... alipofika sebuleni,,  akahisi kamuona mtu anakatisha kuufuata mlango wa kutokea nje,,, hofu ikazidi kuongezeka... akachungulia,, hakuona mtu.. akaamua kurudi chumbani kwake.... alipogeuza shingo yake akaona tena miguu ya yule mtu inaishirizia kuingia chumbani kwake!!!!





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akaingiwa na wasiwasi,hofu ikazidi kuongezeka,, akazipiga hatua za kunyatia kuufuata mlango wa chumba chake !  akaufungua lakini hakuona mtu yeyote kuwemo ndani ya chumba chake. Roda akaingia akaketi kitandani.. akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,, akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi...

    lakini hakupata usingizi akabaki macho wazi mpaka pakakucha !!! akadamka na kujiandaa kwenda kazini......

    siku ya leo Tobi hakuja kumpitia Roda nyumbani kama ilivyo kawaida yake ! Roda akaamua kupanda daladala,,, alipoingia ndani ya daladala hilo akastaajabu kumkuta Tobi kaketi kwenye kiti ndani ya gari hilo,,,,akaamua kuketi kando yake kisha akamsalimia na kumuuliza,, "gari lako likowapi ? 

    Tobi akajibu,, "limepata hitirafu nimelipeleka kwa fundi...

    bqada ya nusu saa kupita wakafika mjini,, wakashuka kutoka ndani ya daladala na kuzipiga hatua kuelekea kazini ! wakiwa njiani Roda alimsimulia Tobi kuhusu matukio aliyoyaona usiku wa jana !

    Tobi akasema pole sana yawezekana unamawazo,, Roda akadakia na kusema,, "pia tumbo langu silielewi kadri miezi inavyozidi kusonga linakuwa kubwa !!

    nimeenda hospitali mara kadhaa,,vipimo vi. ethibitisha ninaujauzito !!  yani hata sielewi,, mimi sijashiriana kimwili takribani mwaka mzima ! 

    Tobi akacheka kisha akasema sio kweli kuhusu hilo ! mbona kila siku unashiriki kimwili,, pamoja na mwanaume unayemthamini na kumuheshimu !

    Roda akashtuka akamtazama Tobi kwa macho ya mshangao ! kisha akauliza,, "wewe umejuaje ?  kwa upande wangu mimi sijashirikiana kimwili mwaka mzima !!

    Tobi akasema siku ya leo ni siku maalumu kwangu,, nataka twende tukale chakula cha usiku pamoja ! Roda akauliza,, "mbona unakwepa swali langu ?

    Tobi akajibu,, "hapana nimeongea tu,, lakini ninauhakika na ulichokisikia,

    baada ya dakika kadhaa wakafika kazini..kila mmoja akaanza kufanya majukumu yake ya kazi !



    Ilipofika jioni,, muda wa kazi ukawa umekwisha, Roda akazipiga hatua kutoka nje ya jengo analofanyia kazi,, akakodi bodaboda impeleke nyumbani !

    akiwa njiani likaonekana gari la kubeba wagonjwa likiwa kwenye mwendo wa kasi.. gari hilo lilikuwa limewakaribia,, Roda akapiga kelele,," NAKUFAAA !!!

    punde si punde akaonekana Tobi akinyoosha mkono wake pikipiki ikainuka kama imebebwa ikatuwa kando ya barabara....watu wakatoka ndani ya magari yao wakatimua mbio,,,wakihisi pikipiki hiyo ni ya kichawi... Pia yule dereva bodaboda akashuka kutoka kwenye pikipiki akatimua mbio akihisi kuwa kabeba jini,, pia kitendo hicho kilimshua Roda.. akabaki mdomo wazi huku akiangaza angaza macho yake,,,kwa mbali akamuona Tobi anaishirizia kwenye ukuta wa jengo refu,, (ghorofa)

    Roda akatimua mbio kumfuqta Tobi.. alipolifikia jengo hilo hakumuona Tobi.. Roda akahisi kuchanganyikiwa !  akaamua kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kwake !  alipofika akajilaza kitandani,, akasikia mtu anagonga mlango,, akanyanyuka kwenda kufungua... alipoudungua mlango hakukuta mtu yeyote kuwepo hapo nje !

    akafunga mlango na kurudi chumbani... akajilaza kitandani... alilala usingizi mzito kupita kiasi.... mpaka saa nne za usiku Roda alikuwa bado kalala,, Tobi akajitokeza chumbani kwa Roda, akamvua nguo zote kisha akamuingilia kimwili alipomaliza akaamua kujionyesha mbele ya Roda... akamuamsha Roda !

    Roda akashtuka kutoka usingizini.. alipofumbua macho akamuona Tobi kalala kitandani kando yake... akauliza kwa mshangao !!  umefikaje humu ???

    wakati anauliza swali hilo akagundua kuwa yupo uchi wa mnyama akakurupuka kutoka kitandani akaficha maungo yake kwa kutumia shuka lililokuwa kitandani.

    akahisi kalowana sehemu zake za siri akamtazama Tobi kwa macho ya uwoga wahali ya juu.. kisha akauliza,,, wewe ni nani ?

    Tobi akasema,, "unamaanisha hunijui ?  mimi ndiye baba wa kiumbe kilichomo tumboni mwako ! kamq unakumbuka nilikwambia kuwa siku ya leo ni siku maalumu kwangu ?

    leo nimeamua ufahamu ukweli kuhusu mimi.. mimi sio binadamu wa kawaida kama ulivyozoea kuniona,, mimi ni JINI.. lakini sina nia mbaya na wewe mimi nimekupenda.. na nimekumiliki kwa kipindi cha miaka kumi na moja sasa,

    Roda akastaajabu sana akauliza kwa mshangao !  ,,"unamaanisha wewe ni jini na si binadamu ?  Tobi akacheka kisha akajibu,, "ndio ni kweli kabisa uyasemayo !

    Roda akataka kufungua mlango atimue mbio.. kabla hajagusa kitasa Tobi akajitokeza mbele yake !  ni kitendo cha sekunde..

    Tobi akasema,, "usiniogope,, mimi ndiye baba wa mtoto aliyetumboni mwako.. sina nia ya kukudhuru.. nimekulinda kwa miaka yote hiyo pia muda na wakati umewadia !!  utazaa mtoto wa kike,,,.kisha Tobi akatoweka kimiujiza !



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog