Search This Blog

MOCHWARI - 4

 







    Simulizi : Mochwari

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kagaruki akawa kiumbe wa kutisha! akawa na nguvu kuliko kiumbe yeyote duniani!

    akazipiga hatua kulifuata jemgo la ikulu........

    wakati huohuo alionekana Rais akiamuru walinzi wa ikulu wamshambulie Kagaruki kwa siraha nzito nzito!amri ya Raisi ikatekelezwa walinzi hao wakaanza kumshambulia lakini cha kushangaza makombola hayo yalimshambalatisha Kagaruki vipande vipande na ndani ya dakika moja vipande hivyo vilijikusanya na kujiunga, walinzi hao walistaajabu wakabaki mdomo wazi., Kagarauki aliendelea kuzipiga hatua kulifuata lile jengo la ikuru....Kagarauki alikua na nguvu kupita kiasi akavunja mlango na kuingia ndani ya Ikulu,,mambo yakaanza kuwa magumu ndani ya ikulu.....



    wakati huo huo walionekana walinzi wakimuingiza Raisi kwenye chumba maalumu cha maficho.....walinzi hao walipohakikisha Raisi yupo katika sehemu salama, wakatoka kwenda kfanya mpango wa kumuangamiza Kagaruki!



    upande mwingine alionekana mganga akiongea na mizimu yake ya kichawi,,punde si punde giza likaanza kutanda hatimae likawa giza totoro! macho yakamtoka mganga..akajisemea moyoni,,"haya ni zaidi ya maajabu,,,sijawahi kuona mchana umegeuka kuwa usiku!

    mganga huyo akaanza kuingiwa na hofu,,akaona vile vibuyu vyake vya kichawi havimsaidii kichu chochote,akaamua kuvitupa chini akatimua mbio huku macho yake yakitazama huku na kule,,akaonamlango uliokuwa nyuma ya jengo la ikulu,,akaufuata mlango huo alipojaribu kuusukuma,,mlango ukafunguka akaigia ndani...kisha akaufunga mlango huo...akazipiga hatua,,punde si punde wale walinzi wakaanza kufyatua risasi mfululizo,,kuelekea kule alipokuwa amesimama mganga!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mganga huyo akanyoosha mkono wake ,,ghafla zile silaha walizokuwa wamezishikilia wale walinzi zikabadilika na kuwa nyoka! wakaingiwa na hofu ,,wakazitupa chini,,,ikasikika sauti ya mganga kisema,,"kwa nini mnajaribu kuniangamiza?

    sauti hiyo ilisikika masikioni mwa kila mlinzi...macho yakawatoka! wakati wanatahamaki,,,vikasikika vishindo vizito vya miguu ikitembea!hofu ikazidi kkuongezeka,,wakatimua mbio,,kila mtu alipitia njia yake kwenda kujificha ,,mganga akabaki kasimama hapo!

    akaonekana Kaawi,,garuki akizipiga hatua kumfuata mganga pale alipokuwa amesimama!

    mganga huyo akaanza kurusha mashambulizi kwa nguvu za kichawi lakini kagaruki alizidi kumfuata mganga mpaka pale alipokuwepo mganga huyo,

    kagaruki akamshika mganga kwenye koo akanmnyanyua juu kisha akamrusha mbali...mganga akaanguka...akahisi maumivu makali sehemu ya mgongo na kiuno...

    muuwa kagaruki hakuishia hapo aliendendelea kushusha kipigo kikali kwa mganga na sasa anataka kumuangamiza kabisa,,yani kuondoa uhai wa mnganga huyoa kichawi.

    mganga akakumbuka jambo fulani,,,kipindi anafundishwa mambo ya kichawi,,miaka arobaini iliyopiyota! akakumbuka kuwa aliambiwa akikutana na kiumbe wa nguvu za giza aongee maneno fulani...wakati anayakumbuka maneno hayo ili ayaseme....kagaruki akamshika mkono nakuunyofoa ukatoka ,,,,,mganga huyo akapiga kelele za maumivu makali kupita kiasi...akaongea yale maneno ya kichawi.....punde si punde Kagaruki akaanza kupiga kelele akadondoka chini...ukazuka moshi mkuba akabadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida...akajishangaa...pia makashtuka kumuona mganga akiwa kalala chini damu nyingi zikimtoka huku akiwa hana mkono mmoja!

    Kagaruki akamsogelea mganga huku nmacho yake yakitazama huku na kule...akionyesha kuingiwa na uwoga wa hali ya juu,,alipomkribia mgnga akamnyanyua kutoka pale chini...



    upande wa nje hali ikaanza kubadilika.. giza likatoweka na pakaonekana ni mchana kama kawaida.....

    wakati huo huo alionekana Raisi akiwa bado yumo ndani ya ke chumba maalumu amejificha kulinda uhai wake...

    walinzi wakaonekana wakifungua mlango huo na kuingia ndani.. wakamwambia Raisi kuwa hali ya amani imerudi....hivyo aondoe wasiwasi...

    Raisi hakuamini maneno hayo... akaomba aonyeshwe video zilizorekodiwa nana kamera maalimu za ulinzi wa ikuru... akaonyeshwa....

    kidogo Raisi akaanza kuingiwa na amani....akatoka nje ya ikuru kushuhudia nini kilichotokea....

    akaonekana Kagaruki akiwa anamkokota mganga kutokea nyuma ya jengo la ikuru.......

    Raisi akaamuru mganga apewe huduma ya kwanza haraka sana..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya lisaa limoja kupita....... mganga akaonekana akiwa kalazwa kwenye wodi maalumu... iliyopo hapo ikulu..... hali yakenilionyesha kuwa njema kiasi ingawa hakuwa na mkono mmoja.......akahisi harufu ya hatari.... punde si punde ikasikika sauti masikioni mwake ikisema....,,"inahitajika damu ya mtu mwenye upara asiyekuwa na nyele kwenye kisogo...

    imwagwe damu yake kwenye mto.......

    na mtu ambaye amechaguliwa n aMizimu yumo miongoni mwenu......... mganga akashtuka... punde si punde akaingia Raisi ndani ya wodi hiyo kumjulia hali mganga..... ghafla ikasikika sauti.. ikisema huyu ni.

                   







    sauti hiyo iliendelea kusisitiza kuwa damu ya mtu inayohitajika kumwagwa kwenye mto,,,umo miongoni mwa watu waliopo ikuru.

    lakini sauti hiyo aliisikia mganga pekee,,,akajaribu afakari ni nani aliyekuwa na upara,,,yani hana nywele kichwani.

    akashtuka kumuona Raisi ndiye mtu pekee mwenye upara!,,,

    mganga akabaki kuifanya iwe siri yake,,,mtu yeyote asijue,,

    wakati huo Kagaruki alikuwa chini ya uangalizi wa walinzi wa ikuru,,



    baada ya siku kadhaa kupita ,,mganga alipona,,kisha akasema tatizo bado halijakwisha! inahitajika niende kwenye mto kushukuru mizimu ili amani iendelee kuwepo,,nitaongozana na Kagaruki!

    Raisi akadakia na kusema,,"mimi pia nitaongozana na nyinyi ,,mganga akashtuka! macho yakamtoka,akajisemea moyoni,,"laiti kama angejua kuwa yeye ndiye anahitajika kumwagwa damu yake,,asingethubutu kuongozana na sisi!



          ***********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi palipokucha ikaandaliwa ndege maalumu,,wakaingia ndani ya ndege hiyo, na safari ikaanza,,ndani ya dakika kadhaaq wakawa wamefika kwenye mto huo uliopo nje ya mji,,wakashuka kutoka ndani ya ndege hiyo ndogo yenye uwezo wa kubeba watu wanne(4)

    wakazipiga hatua kuufuata mto huo,,,walipofika mganga akausogelea mto huo akanyoosha mikono yake akaongea maneno ya kichawi! punde si punde, ukasikika mvumo wa upepo mkali ulioambatana na moshi mkubwa...ghafla maji ya mto yakabadilika yakawa na rangi ya bluu,,ikasikika sauti ikisema,,bila shaka ujio wenu ni kwa dhumuni la kuleta shukrani kwa mizimu...haya kazi ianze ndani ya dakika kumi,,,vinginevayo hakuna mtu atakayetoka akiwa hai ndani ya eneo hili.

    Raisi na kagaruki wakatazamana ,,,kagaruki akauliza kwa mshangao! mbona sielewi ,,ni shukrani gani hiyo!?

    ikasikika sauti ikisema ,,"ni lazima imwagwe damu ya mtu mwenye upara kati yenu!

    Raisi akashtuka kusikia hivyo akatimua mbio kwa sbabu yeye pekee ndiye aliyejuwa na upara,,,yani kichwa chake hakina nywele sehemu ya katikati!

    pia Kagaruki akatimua mbio,,akabaki mganga pekee kasimama pale kando ya mto,,,yeye pamoja na rubani wa ndege waliyokujanayo...punde si punde kikaonekana kiumbe kikipita mbele yao,,kwa kasi ya ajabu ,hawakuweza kukitambua kiumbe hicho! wakati wanatafakari nini cha kufanya ,,,kiumbe huyo akamfyeka shingo rubani na kutoweka kimiujiza! mganga akabaki amekodoa macho,,,akaanza kuongea maneno ya kichawi,,,akimaanisha kuomba msamaha kwa mizimu,

    ghafla akajitokeza kiumbe huyo mbele ya mganga!,,,kiumbe huyo alionekana kutisha! akazipiga hatua kumfuata mganga alipomkaribia akasema,,mimi sijaribiwi,,,nahitaji damu hiyo haraka,,vinginevyo wewe utakuwa wa pili kufa,,

    mganga akaingiwa na hofu baada ya kuyasikia maneno hayo,,,akaangaza angaza macho yake kichawi..akafanikiwa kumuona Raisi akuwa kajificha kwenye kichaka...

    akaamua kumfuata.. alipofika kwenye kichaka hicho...

    Raisi akafurahi akiamini kapata msaada kwa mganga... lakini ikawa ndivyo sivyo!!!  mganga akamgeuka Raisi akamnasa na kumfunga kamba,, akamshurutisha kinguvu kumpeleka kule kwenye mto... ili amchinje Raisi na kumwaga damu yake kwenye mto huo! 



               *********************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    upande mwingine alionekana kagaruki akiendelea kutimua mbio.. pasipokujua ni wapi anaelekea!  akajikuta anazunguka na kutokezea kule kwenye uleule mto!!! akashtuka kumuona mganga kamfunga kamba Raisi mikononi,, huku akimshurutisha kwa kumsukuma kumpeleka kwenye ule mto..

    Kagaruki akazipiga hatua za kunyatia akazunguka na kutokezea nyuma ya yao!!!  akaokota kipqnde cha mti mnene kiasi. ..kumbe kipande cha mti huo ukikigusa au kushikilia... basi hautaweza kuonekana kwenye macho ya viumbe wenye nguvu za giza!!

    wakati huo mganga hakufahamu chochote kinachoendelea!

    akamchoma mganga upande wa ugavuni.... kwa kutumia kipande cha mti huo!

    kwa sababu mganga alikuwa amesimama kando ya mto huo!  akadondoka na kutumbukia ndani yamto..... damu yake ikachanganyikana na yale maji ya mto... hilo ni kosa kubwa!!!

    punde si punde.... akaonekana mtu wa kutisha akitokea ndani ya mto huo!!!

    PATASHIKA...            





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog