Simulizi : Wakala Wa Shetani
Sehemu Ya Tatu (3)
"Turudini, muda huu ni mbaya mvua inaweza kushuka si mnakumbuka kuna wingu lilitoweka kiajabu huenda likatuulia mbali. Kwanza sehemu hii haina
maeneo ya kujificha na kama mvua itashuka kama ya juzi basi sote tutakufa tunajiona."
SASA ENDELEA...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Basi turudini, maana tumekwenda sana bado kidogo tutaingia kijiji cha jirani, mnakumbuka wale ni mahasimu wetu wakubwa?"
"Haya jamani turudini, lakini bado nina uhakika tumewaacha nyuma."
"Lazima tutawapata kwani hawana sehemu ya kukimbilia."
Walikubaliana kwa pamoja kugeuza, ilikuwa ni ajabu ya Mungu kushindwa kuuvuka ule mti ambao ndipo alipokuwa wamejilaza Ngw'ana Bupilipili na
mwanaye.
Wakati wakijadiliana, Ngw'ana Bupilipili huku akitetemeka, alifumba macho na kumuomba Mungu amuokoe na kikombe kile akiwa amemkumbatia mtoto wake
na kuomba asilie. Kwani kama angelia angeharibu kila kitu, wakati akiomba huku amemkumbatia mwanaye alijisaidia haja ndogo.
Aliamini kwa kujisaidia kule lazima mikojo ingemuwasha na kumfanya alie na kutoa sauti na kuharibu kila kitu. Aliuweka mkono mdomoni kwa mtoto wake ili
akitaka kutoa sauti basi amzibe.
Aliendelea kumlilia Mungu huku akijikabidhi mikononi mwake. Baada ya maombi yaliyochukua zaidi nusu saa alipofumbua macho hakukuta mtu yeyote.
Aliamini kwa mara nyingine tena Mungu amemtendea muujiza.
Siku zote aliamini Mungu hutenda muujiza kwa kila amtegemeaye, watu wale kuishia nyuma ya mti aliokuwa amejilaza ulikuwa muujiza mwingine.
Alinyanyuka alipokuwa amejilaza na kumbadili nguo mtoto.
Ajabu kubwa baada ya hali ya utulivu mtoto alianza kulia, kila kitu kilichomtokea kilikuwa kikimuonesha maajabu mengine. Mungu alizidi kudhihirisha uwezo
wake kwa kumziba kauli mtoto wakati wa matatizo na kumuachia wakati wa hali ilipokuwa shwari.
Alimnyonyesha mtoto wake mpaka akashiba, baada ya kumaliza kumnyonyesha, naye alifungua mzigo wake na kutoa kipande cha muhogo wa kuchemsha
kutokana na njaa kali iliyokuwa ikimuuma.
Baada ya kudanganya tumbo, alijikuta akiwa njia panda asijue aende wapi. Alisimama kwa muda akiwa hajui hatima ya maisha yake ya mbele.
Aliamini kilichokuwa kikifuata mbele yake kilikuwa mtihani mzito kuliko uliokuwa umekwisha muda mfupi wa kuokoka katika kinywa cha mauti. Alijiuliza
ataishi wapi, atakula nini na nini hatima ya maisha ya mwanaye?
Kichwa kilikuwa kizito kupata jibu na kujikuta akitokwa na machozi huku akizungumza na Mungu wake amuoneshe njia.
Muda ulizidi kukatika asijue nini hatima yake katika mbuga ile ambayo kila muda ilizidi kutisha.
***
Usiku ulipoingia Ngw'ana Bupilipili na mwanaye walijilaza pembeni ya mti ule mkubwa huku akiendelea kumuomba Mungu asishushe mvua kwa vile
hawakuwa na sehemu ya kujikinga, pia awalinde na wanyama wakali wapitao usiku.
Mungu aliwalinda na kulala bila tatizo mpaka asubuhi. Siku ya pili Ngw'ana Bupilipili alijinyanyua toka alipokuwa amelala na kumchukua mwanaye aliyekuwa
bado yupo kwenye usingizi. Ilibidi waamke alfajiri kutokana na baridi kali na hali ya hewa bado ilikuwa haijapambazuka vizuri kwa wingu kuwa jeusi.
Alimfunga vizuri mwanaye na kuanza safari ya kuelekea kusikojulikana, alivuka mpaka wa kijiji na kuingia kijiji cha jirani. Aliamini huenda jamaa waliokuwa
wakimtafuta wakadamka alfajiri kuanza msako upya na kumkuta, kwa hasira ya kupoteza ndugu zao, lazima wangewaua wote.
Baada ya kuamini mwanaye amekaa vizuri kifuani alianza safari ya kuelekea kusikojulikana. Moyoni aliapa kurudi kijijini alipokimbia kwa ajili ya kulipa kisasi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitembea mwendo wa saa saba bila kupumzika huku akikwepana na wanyama wakali kama simba, chui na baadhi ya wanyama waliokuwa katika pori lile la
kutisha.
Baada ya mwendo mrefu huku akisumbuliwa na njaa na kiu kikali, alijikuta akiishiwa na nguvu na kuamua kujipumzisha chini ya mti mkubwa. Mtoto wake
alianza kulia akionesha njaa inamsumbua. Alitoa titi nje na kumuwekea mtoto mdomoni na yeye kujilaza pembeni yake.
Kila mtoto alivyokuwa akiyavuta maziwa ya mama yake kwa nguvu kutokana na njaa ndivyo naye nguvu zilivyokuwa zikimuishia na kumfanya ahisi
kizunguzungu kizito. Kiza kinene kilitanda mbele yake, hakujua chochote kilichoendelea.
***
Ngw'ana Bupilipili aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kitanda cha chuma kilichokuwa kimetandikwa vizuri. Mkononi kulikuwa na mrija wa kuingizia maji
mwilini mwake. Alitulia na kutafakari kwa muda huku akipepesa macho. Baada ya akili yake kutulia aligundua pale ni hospitali.
Alishtuka na kuamini mtoto wake anaweza kuwa ameuawa na yeye yupo pale anasubiri kupona ili wanakijiji wakamfungulie mashitaka ya mauaji ya wanakijiji
ambao waliuawa na marehemu mumewe.
Aliamini hata kama atajitetea vipi kuwa hakuhusika na mauaji ya wale wanakijiji waliomuua mume wake, bado wasingemwelewa kwa kuamini alishirikiana na
mumewe kufanya mauaji.
Alitamani kunyanyuka, ikiwezekana atoroke japo hakujua pale yupo wapi. Alijaribu kujinyanyua alipokuwa amelala lakini mwili nao haukuwa na nguvu,
alijirudisha chini na kujilaza. Moyoni hakukubali kushikwa kirahisi namna ile. Lakini bado alikuwa katika kitendawili kizito mwanaye alikuwa wapi.
Alijitahidi kunyanyuka huku moyoni akiapa kupambana na yeyote atakayejitokeza mbele yake. Alijitahidi kujinyanyua na kukaa kitako kisikilizia hali yake.
Wazo lake kubwa ni kutafuta upenyo atoroke hospitalini ili kuikimbia kesi nzito ya mauaji iliyokuwa ikimkabili marehemu mume wake. Kuhusu mwanaye
alikuwa amekata tamaa kwa kuamini lazima atakuwa amekwishakufa. Alikaa kitandani mawazo yakiwa mengi huku akivuta pumzi kwa ajili ya kupata nguvu
zitakazomfanya atembee peke yake.
Wakati akitaka kuteremka kitandani, alisikia mlango wa chumba alicholala ukifunguliwa. Alirudi kitandani kwa haraka na kujifanya bado hajarudiwa fahamu.
Akiwa amefumba macho na kupumua taratibu ili mtu asijue kama ameshaamka, alisikia nyayo za viatu zikisogea alipokuwa amejilaza.
Hakujitikisa, woga ulimjaa na kuanza kutetemeka kwa kuamini wamekuja kumwangalia kama karudiwa na fahamu ili wamkamate. Akiwa bado amefumba
macho, alisikia wakizungumza:
"Dokta ina maana hadi sasa atakuwa bado hajarudiwa na fahamu?" Sauti ya kike iliuliza.
"Noo, lazima atakuwa amerudiwa na fahamu, hakuwa na tatizo kubwa, ni njaa na uchovu ndivyo vilivyomfanya awe vile," ilikuwa sauti ya dokta mwenye
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lafudhi ya kizungu.
"Mbona bado yupo vilevile?"
"Inawezekana kalala, dawa tulizomchanganyia kwenye dripu zina nguvu sana lazima atajisikia vizuri tu, huenda kulala huku ni usingizi na si kupoteza fahamu."
"Sasa dokta kama atapata fahamu ataweza kumnyonyesha mwanaye, maana mtoto yule kila tulichompa amekataa."
Kauli ile ilimshtua Ngw'ana Bupilipili na kuamini kumbe mwanaye bado yupo hai lakini bado alijawa na maswali pale ni wapi na watu wale ni akina nani. Na
nini shida yao kwake, lakini kusikia kuwa mwanaye mzima na anahitaji ziwa la mama, aliamini sehemu ile ni salama na kuwa tayari kwa lolote.
Alijipindua na kujifanya kama mtu anayetoka usingizini, kabla hajafumbua macho, alisikia sauti ya kike ikisema.
"Dokta kweli ameamka."
"Hakuwa na tatizo kubwa sana."
"Kwa hiyo dokta?"
"Mpaka sasa hatujajua anatoka wapi na anaelekea wapi, ngoja apate nguvu tutaweza kumuhoji."
Ngw'ana Bupilipili alizidi kutoka mashaka kwa kuamini sehemu ile ni salama ambayo ilimuhifadhi baada ya kumuokota porini. Alifumbua macho na kumuona
daktari mzungu aliyekuwa amevaa shati la rangi ya bluu bahari shingoni, alikuwa na kipimo cha mwenendo wa mzunguko wa damu.
Pembeni yake alikuwepo binti mmoja mrembo aliyekuwa ameshikilia faili na kalamu mkononi. Walipomuona amefumbua macho, wote walisogea mpaka
kitandani. Daktari alimshika kichwani na kumwambia kwa sauti ya upole.
"Unajisikiaje sasa?"
"Sijambo," alijibu kwa sauti ya chini.
"Pole."
"Asante."
"Unaitwa nani?"
"Salome," alidanganya jina.
"Andika jina hilo," daktari mzungu alimgeukia msaidizi wake na kumweleza aandike jina la mgonjwa.
"Hali ya mwili unaisikiaje?"
"Mmh, uchovu tu na mwili kuishiwa nguvu."
"Okay, nafikiri ukipata chakula utapona kabisa."
"Nitashukuru, mwanangu yupo wapi?"
"Yupo, utaweza kumnyonyesha?" walimuuliza.
"Ndiyo."
"Okay, kamleteni mwanaye."
Baada ya kusema vile, msaidizi alitoka kumfuata mtoto na kubakia daktari mzungu ambaye aliendeleza kumdodosa mgonjwa.
"Eti mama umetokea sehemu gani?"
"Kabla sijakujibu naomba unieleze hapa ni wapi na nimefikaje?"
"Ooh vizuri mama, hapa ni kituo cha watumishi wa kiroho, tupo kwa ajili ya kutoa misaada kwa watu wa maeneo ya karibu kielimu na kiafya.
Baada ya kusema vile, msaidizi alitoka kumfuata mtoto na kubakia daktari Mzungu ambaye aliendelea kumdodosa mgonjwa.
Eti mama umetokea sehemu gani?
Kabla sijakujibu naomba unieleze hapa ni wapi na nimefikaje?
Ooh vizuri mama, hapa ni kituo cha watumishi wa kiroho, tupo kwa ajili ya kutoa misaada kwa watu wa maeneo ya karibu kielimu na kiafya. Taarifa zako
tumezipata kutoka kwa wasamaria wema waliokuwa wakipita porini na kukuta ukiwa umepoteza fahamu, ilibidi tuwatume vijana wetu ambao walikuchukua na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kukuleta hapa.
Baada ya kukufanyia uchunguzi haukuwa na tatizo kubwa zaidi ya njaa na uchovu wa kuonekana umetembea kwa muda mrefu bila kupumzika na pia ulikuwa
hajapata chakula cha kutosha, kitu kilichofanya mwili ukose nguvu na kukufanya upoteze fahamu.
Nina imani umenielewa vizuri, una swali lingine? daktari alimuuliza kwa sauti ya faraja.
Ooh, asanteni sana Mungu aendelee kuwabariki.
Amen, mh! Nini kimekusibu mpaka kuwa katika hali hii?
Ngwana Bupilipili kabla ya kujibu alivuta kumbukumbu jinsi alivyonyanyasika kwa ajili ya kujifungua mtoto albino na kifo cha mumewe huku akishangaa jinsi
mwanaye alivyopewa huduma nzuri bila kubaguliwa kwa jinsia au rangi yake.
Bila kutegemea machozi yalianza kumtoka, mdomo ulikuwa mzito kutoa matamshi. Daktari alishtushwa na hali ile na kumfanya aamini lazima yule mama
atakuwa na tatizo zito. Kabla hajanyanyua mdomo wake kutamka kitu. Mara mlango ulifunguliwa, akaingia yule msaidizi akiwa amempakatia mtoto.
Ngwana Bupilipili alitaka kunyanyuka kitandani baada ya kumuona mwanaye akiwa hai. Baada ya kupewa mwanaye alijikuta akimtazama mara mbilimbili huku
akimgeuza kwa kumuangalia kama yupo sawa.
Baada ya kupata uhakika yupo sawa alimnyonyesha, mtoto akalidaka ziwa la mama yake na kunyonya kwa fujo kutokana na njaa kali.
Daktari na msaidizi wake walitabasamu kwa pamoja huku wakifurahia mtoto alivyofurahia ziwa la mama yake. Daktari hakutaka kumsumbua sana, alimwacha
amnyonyeshe mtoto na kumuachia maagizo msaidizi wake.
Pamela, baada ya kumaliza kunyonyesha mgonjwa apewe chakula, apate maji ya kuoga kisha apumzike, jioni nitakuwa na mazungumzo naye, anaonekana ana
kitu kizito moyoni mwake.
Sawa dokta.
Daktari alitoka na kumuacha msaidizi wake ameketi kwenye kiti kusubiri amalize kunyonyesha mtoto na kumpa huduma alizopangiwa.
***
Ngwana Bupilipili aliishi pale kwenye kituo cha kiroho na mtoto wake ambaye alikutana na watoto wengine wenye ulemavu wa ngozi. Hali ile ilimpa faraja
kubwa na kuamini kijijini kwao imani za ushirikina ndizo zilizotawala na kuwafanya kila kukicha wamkosee Mungu.
Pamoja na kukaa pale kwa amani, moyo wake ulikuwa ukiumia kila alivyofikiria kifo cha mumewe na mali walizoziacha kijijini. Alijikuta akiapa lazima alipe
kisasi cha kifo cha mumewe na mtoto wao wa kwanza albino aliyeuawa kwa imani za kishirikina.
Kila kukicha alikuwa akibuni njia ya kulipa kisasi kwa wanakijiji waliosababisha yote yale. Siku moja akiwa anafanya usafi kwenye stoo aliona pakiti ndogo
iliyokuwa imeanguka chini na kumwaga unga mweupe chini.
Aliiokota na kutafuta sehemu ya kuiweka, wakati huo Sister Lucy alikuwa akiingia stoo na kushtuka kumuona Ngwana Bupilipili ameshika pakiti ile tena bila
gloves mkononi. Alionekana kushtuka sana.
Mama Kusekwa kwa nini unashika dawa hiyo bila gloves?
Nimeikuta hapa chini ndio nilikuwa natafuta sehemu ya kuiweka.
Hii ni sumu, ukiiweka mdomoni utakufa dada yangu.
Sumu?
Eeh.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mungu wangu, kama ni sumu inafanya nini humu ndani?
Si sumu kwa maana imetengenezwa kuua watu, ni dawa ya kuua wadudu katika mitaro, mashimo ya maji hata wadudu warukao na watambaao.
Sasa inakuwaje unasema sumu kumbe dawa ya kuulia wadudu?
Mama Kusekwa, hii ni dawa lakini ukiitia mdomoni inageuka sumu na kukudhuru.
Mmh, sawa.
Tena dawa hii kama utakumbuka kuna mwaka mtu mmoja aliiweka kwenye tanki la maji na kuua familia nzima.
Mmh! Sasa inakuwaje mtu aweke kwenye tanki la maji wafe watu wengi, kwani ina nguvu gani isiyopungua katika maji mengi?
Hii ni sumu kali sana ndio maana nikashangaa kukuona umeishika kwa mkono. Unatakiwa kunawa vizuri na sabuni mikono yote na kuhakikisha unakuwa msafi
kabla ya kumshika mtoto wako.
Nashukuru Sister Lucy. Basi ningetoka hapa ningepewa embe mimi ningekula tu bila kujua kama nina sumu mkononi.
Basi kuanzia leo unatakiwa kuvaa gloves kabla ya kupanga vitu vya humu ndani.
Nitafanya hivyo, hivi kama ukiitia dawa hii kwenye lambo la kijijini si unaweza kuua watu wengi?
Tena usiombe kufanya kitu kama hicho, na dawa hizi hupatikana sehemu kama hizi madukani hazipo kwani ni kali sana, zinaua mara moja.
Baada ya maelezo yale Ngwana Bupilipili alikwenda kunawa kwa sabuni na kisha aliendelea na kazi yake.
***
Jioni ya siku ile akiwa amejilaza kitandani kwake, wakati huo mwanaye akiwa anaendelea kufaidi ziwa tamu la mama yake, alijikuta akikumbuka maneno
aliyokuwa akizungumza na Sister Lucy kuhusu ukali wa ile dawa ya kuulia wadudu kuwa ni sumu kali kama mwanadamu atainywa.
Aliamini kupitia sumu ile itakuwa njia nyepesi ya kulipa kisasi, alijua akienda kuiweka katika chanzo cha maji ambayo hutumiwa na wana kijiji lazima ataua
watu wengi.
Alijikuta akiwachukia watu wote wa kijiji cha Nyasha kwa kuamini kila aliyetoka katika dawa ya wauaji nao walitakiwa kuipata hukumu ile kwa kuamini kama
wao walifurahia vifo vya watoto wenye ulemavu wa ngozi basi nao watoto hao nao watafurahi kusikia mauti yao.
Alijikuta akiapa lazima alipe kisasi tena kikubwa na kuacha historia ya vifo vya watu wengi. Alipanga siku ya pili akiingia kufanya usafi achukue paketi nne za
sumu ambazo zote ataziweka katika vyanzo vya maji ya Kijiji cha Nyasha.
***
Siku ya pili akiwa anafanya usafi stoo alichukua paketi nne za dawa ya kuulia wadudu na kuificha kwenye kanga. Baada ya usafi alitoka nayo na kwenda kuificha
chumbani kwake.
Baada ya kuipata ile dawa alipanga siku moja ataondoka kwenye kambi ile saa kumi za usiku kwenda Kijiji cha Nyasha.
Baada ya kujipanga na kuipanga siku ya kwenda kulipa kisasi, alimtaarifu shoga yake wa karibu kuhusu safari yake lakini alimdanganya kuwa anafuata vitu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
vyake.
Baada ya kukubaliana siku ya pili majira ya saa kumi za usiku Ngwana Bupilipili aliamka na kwenda kumuamsha shoga yake ambaye alikuwa amelala.
Vipi, safari imeiva?
Eeh, shoga, niangalizie mwanangu, alimpa mtoto wake aliyekuwa bado na usingizi.
Shoga yake alimchukua na kumuingiza ndani na kumlaza kitandani kisha alitoka ili amuage.
Basi shoga safari njema.
Nashukuru shoga, Mungu akijalia tutaonana.
Ngwana Bupilipili kabla ya kuondoka aliingia chumbani kwa shoga yake na kumnyanyua mtoto wake kitandani na kumkumbatia kwa uchungu huku machozi
yakimtoka. Hali ile ilimshtua shoga yake na kuhoji kulikoni.
Vipi mbona unalia?
Basi acha tu, nimekumbuka vitu vingi hasa baada ya kukumbuka kifo cha mume wangu na leo narudi hukohuko.
Kama ni hivyo kwa nini unakwenda tena?
Hapana kuna vitu vyangu vingi na vya muhimu sana lazima niende.
Sasa utaingiaje pale kijijini?
Hapana siendi nyumbani nitaishia shambani kwetu.
Unajuaje kama shamba bado lipo mikononi kwenu?
Yote nitayajua huko huko.
Basi bwana akutangulie safari yako yote.
Amen.
Alimrudisha mtoto kitandani baada ya kumbusu, alimgeukia shoga yake na kumkumbatia kabla ya kugeuka na kuondoka kuwahi safari yake ambayo aliamini
mpaka saa mbili asubuhi atakuwa Kijiji cha Nyasha.
Hakutokea mlango wa mbele, aliruka ukuta kuogopa kuulizwa na mlinzi anakwenda wapi. Baada ya kufanikiwa kutoka salama nje ya kambi alianza safari
kuelekea Kijiji cha Nyasha moyoni akiwa na dhamira nzito ya kuwa tayari kupambana na lolote litakalotokea mbele yake.
Katika kijiji cha Nyasha ilikuwa siku ambayo iliwachanganya watu wengi baada ya kila nyumba kulalamikia tatizo la tumbo. Hospitali zilijaa wagonjwa ambapo
wengi walipoteza maisha. Ilibidi taarifa zifike haraka mkoani na kutumwa timu ya wataalamu kuja kufanya uchunguzi.
Ilionesha watu wa kijiji kile wamekunywa sumu iliyokuwa kwenye maji, mifugo yote ilikufa na kufanya kijiji kiwe katika janga zito la maafa ya watu na mifugo.
Ilibidi wagonjwa wote wahamishiwe mjini lakini wengi walifia njiani.
KaYA nyingine zilipoteza familia nzima na nyingine zilipoteza zaidi ya watu watatu.
Mara moja watu wa Kijiji cha Nyasha walipigwa marufuku kunywa maji yote, uchunguzi ukaanza kufanywa ambapo ilibainika kuwa vyanzo vyote vya maji
vilikuwa na sumu.
Ilibidi iletwe dawa na kuondoa sumu katika sehemu zote zenye vyanzo vya maji lakini wakati huo Kijiji cha Nyasha kilikuwa na msiba mzito wa kupoteza nusu
ya wanakijiji.
Taarifa za msiba mzito uliowakuta wanakijiji wa Nyasha zilimfikia Ngwana Bupilipili ambaye alijawa na furaha kuamini mpango wake umefanikiwa. Pamoja na
kufanikiwa kuua watu wengi, bado dhamira yake ilikuwa haijatimia. Alipanga kukifanya kijiji kile kiwe cha historia kwa kuwamaliza wanakijiji wote na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kubakiza magofu.
***
Baada ya kufanikisha zoezi la awali la kukiteketeza Kijiji cha Nyasha, Ngwana Bupilipili aliendelea na mchezo wake ule, kila hali ilipotulia alikwenda kuweka
sumu kwenye maji. Hali ile ilikiweka Kijiji cha Nyasha kwenye mashaka na kuamua kufanya uchunguzi wa kina juu ya nani anayefanya mchezo huo.
Makachero toka serikalini walianza uchunguzi wa siri bila mtu yeyote kujua. Walilinda kwa saa 24 vyanzo vyote vya maji kwa kubadilishana kufuatilia mtu
aliyekuwa akisababisha mauaji ya wanakijiji cha Nyasha.
Ngwana Bupilipili kama kawaida yake baada ya mambo kutulia alirudi tena kwenye Kijiji cha Nyasha kuendeleza hukumu yake ya kuhakikisha anakisafisha kijiji
chote.
Kurudi kijiji pale ilikuwa mara ya nne, kama kawaida alimuaga shoga yake na kumuachia mwanaye Kusekwa aliyekuwa ametimiza miaka miwili.
Alitembea katika mbuga kama ilivyo kawaida yake, kwa vile alikuwa ameshakuwa mzoefu, hakuwa na hofu tena ya kutembea mbugani peke yake. Kutokana na
uzoefu alikuwa akitoka usiku zaidi ili alfajiri imkute ameshamaliza kazi yake.
Baada ya mwendo wa saa tatu bila kupumzika, aliingia Kijiji cha Nyasha kukiwa bado na giza, hakukuwa na mtu yeyote. Alijisifu kuondoka mapema kwa
kuamini atamaliza kazi zake bila mtu yeyote kumuona.
Baada ya kuangalia usalama wa eneo lile na kuona hakuna tatizo, aliifungua ile sumu na kuitia kwenye chanzo cha maji kisha aliifunga na kuelekea kwenye
kisima cha akina mama. Wakati akifanya vile walinzi wa eneo lile walikuwa bado hawajamuona.
Wakati anataka kuondoka eneo lile askari mmoja alishangaa kumuona mwanamke akitokea kwenye chanzo cha maji.
Hey, wee mama unafanya nini alfajiri hii?
Nakwenda shamba, Ngwana Bupilipili japo alikuwa katika mshtuko mkubwa lakini alijitahidi kujibu kwa kujiamini.
Shamba, mbona majibu yako yana utata, unakwenda shamba gani ikiwa mashamba hayapo eneo hili?
Achana naye bwana, si unajua tumemaliza lindo salama, alisema mlinzi mwingine.
Haya potea hapa.
Ngwna Bupilipili alimshukuru Mungu kumuepusha na watu wale, ndipo alipofumbuka macho kuwa sehemu ile ina ulinzi. Aliteremka kuelekea bondeni kwa
kuhofia kugeuza lazima wangemtilia wasiwasi.
Aliamua kutafuta njia nyingine ya kumuokoa kwa kuondoka eneo lile ambalo aliamini limezungukwa na ulinzi mzito. Alitembea kwa tahadhari akipita pembeni
kutafuta njia ya kutokea nje ya Kijiji cha Nyasha.
Askari mmoja alimuona Ngwana Bupilipili akitembea kwa mashaka na kuamua kumfuatilia taratibu. Baada ya mwendo mfupi alikutana na sehemu kubwa
iliyokuwa imetengeneza kama bwawa.
Alipoiangalia sehemu ile ilimuonesha kabisa watu huchota maji. Akili yake ilimtuma sehemu ile vilevile inatakiwa kuwekwa sumu. Kwa tahadhari kubwa alitoa
paketi ya dawa ya kuulia wadudu na kuanza kuinyunyizia kwenye maji yake.
Askari aliyekuwa akimfuatilia alimshangaa na kujiuliza yule mwanamke ananyunyiza nini kwenye yale maji.
Hakutaka kumshtua alimsogelea taratibu mpaka alipokuwa na kusimama nyuma yake bila Ngwana Bupilipili kumuona. Baada ya kuimiminia ile dawa iliyobaki
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
aliirudisha kwenye paketi yake kisha aliifunga kwenye mfuko wa plastiki na kuiweka katika mfuko wa kaptura aliyokuwa amevaa.
Wakati anavua gloves ndipo yule askari alipomshtua.
Unafanya nini?
Ngwana Bupilipili alishtuka na kuanza kutimua mbio, lakini hakufika mbali alikamatwa.
Daktari Father Joe alipoingia ndani alimkuta Ngwana Bupilipili akiwa amejilaza kitandani. Lakini aliamini kabisa mlalo ule si wa mtu kupoteza fahamu bali wa
usingizi wa kawaida. Akiwa bado hajapata jibu juu ya kuwa katika hali ile alimgeukia msaidizi wake Sister Marry.
Eti sister nini kilichomtisha na kumfanya akimbie na kuanguka kisha kupoteza fahamu?
Kwa kweli mpaka sasa hatujajua ila niliambiwa alitoka mara moja.
Alikuwa amekwenda wapi?
Mmh, hapo sijui ngoja tutamuuliza mwenyewe akipata fahamu.
Ngwana Bupilipili alizifahamu vizuri sauti za Father Joe na Sister Marry hali iliyomfanya ashushe pumzi kwa kuamini yupo sehemu salama. Alijifanya kujigeuza
kitu kilichowafanya wasogee kitandani. Sister Marry akamwita:
Mama Kusekwa... Mama Kusekwa.
Abee, aliitika na kujinyoosha.
Vipi unajisikiaje? Sister Marry alimuuliza kwa sauti ya upole.
Mmh, sijambo kiasi, alijibu huku akifumbua macho.
Eti tatizo nini?
Nilikuwa natoka kutafuta baadhi ya vitu vyangu nilivyoviacha porini wakati nakuja, ndipo nilipokutana na mnyama mkali aliyeanza kunifukuza, kwa kweli
nilikimbia kwa nguvu zangu zote.
Sikumbuki kilichoendelea na kujikuta nipo hapa, Ngwana Bupilipili alitengeneza uongo unaofanana na ukweli.
Ooh, pole sana.
Asante.
Hakukujeruhi? Father Joe aliuliza.
Sidhani najiona nipo salama ni maumivu madogomadogo ambayo sijui ni ya nini.
Unaweza kwenda chumbani kwako, kama utasikia tatizo lolote mwilini mwako utatujulisha.
Ngwana Bupilipili alinyanyuka kitandani na kutembea kwa kuchechemea kwa muda kisha alitembea kawaida. Alikwenda hadi chumbani kwake na kujilaza bila
kumfuata mtoto kwani hakuwa na mawazo ya mwanaye zaidi ya kujifikiria jinsi alivyookoka katika mikono ya askari waliokuwa wakilinda chanzo cha maji.
Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa huenda wakafanya msako na kwa vile askari yule ameshaiona sura yake, lazima angemtafuta na kumpata. Aliamini katika
msako wao lazima wangefika kwenye ile kambi na lazima angemtambua na kumkamata.
Ngwana Bupilipili aliamini kabisa kwa upande wake muda ule kwake kuwepo pale kambini hakufai, kwa kuamini wakimkosa porini lazima watamtafuta kwenye
kambi ile.
Wazo lake kubwa lilikuwa ikifika usiku atoroke na mwanaye na kutimkia sehemu asiyoijua japokuwa alijua ni hatari, lakini aliamini bora akafie mbele kuliko
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kukamatwa na kuhukumiwa kifo.
Hata shoga yake alipoingia hakumuona kwa vile alikuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo.
Shoga nakuona upo mbali vipi umeumia sana?
Walaa, kawaida tu.
Mh! Za huko?
Shoga mbona yamenikuta leo makubwa.
Yapi hayo?
Kidogo leo nishikwe na askari waliokuwa wakilinda vyanzo vya maji.
Vyanzo vya maji?
Eeh, japokuwa nilikuwa sijakueleza ukweli wa safari yangu, kwa vile wewe umekuwa mtu wangu wa karibu na muhimu sana lazima nikueleze ukweli hata
nikishikwa ujue tatizo langu.
Ushikwe kwa kosa gani tena? shoga yake alishtuka.
Tulia basi nikueleze usiwe na pupa na nitakachokueleza naomba ibakie siri yako.
Hakuna tatizo shoga.
Ngwana Bupilipili alimueleza yote aliyoyafanya baada ya kufiwa na mume wake na ahadi ya kisasi aliyoiweka ya kukisambaratisha Kijiji cha Nyasha, siku ile
jinsi alivyokamatwa na askari na kufanikiwa kumtoroka. Shoga yake Bupe hakuamini alichoelezwa na Ngwana Bupilipili na ujasiri aliouonesha wa kutimiza
dhamira yake.
"Mmh, nimekusikia, nakupa hongera, wewe ni mwanamke wa shoka kwa yote uliyofanya. Huna kosa shoga kwani ulichokifanya ni sawasawa, kuwatia adabu
mashetani wale.
"Sijui kwa nini hukuniambia na mimi nikusindikize, hata mimi nina kisa changu kizito sikuwahi kukueleza na sababu ya mimi kufika hapa."
"Kisa gani hicho shoga?"
"Kwa vile wewe umeniamini na kunipa siri yako nzito, nami sina budi kujiweka wazi kwako. Mimi nilikuwa nimeolewa katika Kijiji cha Ng'wana Nsimba,
Shinyanga vijijini na mume aliyekuwa na mali ya wastani.
"Kwa bahati mbaya mume wangu alifariki, ndugu walinidhulumu mali zote na kuonekana sina thamani mbele ya watu. Kwa kweli roho iliniuma kwa vile tangu
nilipoolewa nilikuta ng'ombe ishirini tu, kwa vile sikutaka mume wangu apate shida, katika ng'ombe zangu sabini za mahari nilichukua 40 na kuzichanganya na
za mume wangu.
"Kwa miaka minane zizi lilikuwa na ngombe mia nne ishirini. Kwa bahati mbaya mume wangu alifariki, ndugu wakanifukuza kama mbwa, hata nilipoomba
ng'ombe zangu 40 walininyima. Sikutaka kubishana nao, niliondoka na kurudi nyumbani na wanangu wawili.
"Nikaapa kuwashikisha adabu japokuwa walinidhihaki na kuniona siwezi kufanya kitu chochote kwa vile waliamini wanawake ni viumbe dhaifu.
"Moyoni nilipanga pigo zito, ndipo siku moja niliwavizia wamelala na kutia moto nyumba zao za nyasi kwa kuanzia milangoni. Kwa vile nyumba nyingi za
vijijini za nyasi madirisha yake ni madogo, walikosa pa kutokea, nikaiteketeza familia yote ya marehemu mume wangu.
"Siku ya pili taarifa zilizagaa juu ya vifo vya familia ya mume wangu, sikutaka kuitwa kutoa ushahidi kutokana na kutoa maneno makali siku waliyonidhulumu
mali zangu.
"Niliamini mtu wa kwanza nitakuwa mimi, basi nilitoroka bila mtu yeyote kujua na kutembea kwa miguu kwa muda wa siku tatu, usiku nililala na asubuhi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
niliendelea na safari zangu.
"Ndipo siku moja nilipotokea mbele ya kambi hii nikiwa nimevimba miguu kwa kutembea. Kwa kweli watu wa hapa kwa ukarimu waliniokota na kunitibu kisha
walinitunza mpaka leo hii.
"Najua walinitafuta nami nilijificha huku, sijui nitatoka lini kwa vile najua nikionekana kijijini kwetu nina kesi ya mauaji. Basi mdogo wangu matatizo yetu
yanafanana na kisasi chetu kinafanana japo wewe ulidhamiria kufyeka kijiji kizima na mimi nilitimiza nadhiri yangu ya kuipoteza familia yote.
"Japo ni dhambi lakini namshukuru Mungu kuniwezesha kulipa kisasi, hata leo nikifa nitakuwa nimekufa bila kinyongo. Kwa kweli sikushangai kwa hatua
uliyochukua, kisasi ni hapahapa dunia kwa Mungu hesabu, naamini hata uliowaua umelipa kisasi kwa kiasi kikubwa," Bupe alisema kwa hisia kali
zilizomkumbusha donda na maumivu ya moyo.
"Mmh! Umeona dada watu walivyo na roho za kikatili kuliko wanyama? Ni kweli kabisa kisasi duniani kwa Mungu hesabu."
"Umeona eeh!"
"Ila shoga kuna kitu kinanichanganya sana akili yangu."
"Kitu gani tena?"
"Wasiwasi wangu huenda wale askari wakaendesha msako mkali, wakinikosa porini lazima watafika huku. Heri ningekuwa nimewaua wanakijiji tu msako wake
usingekuwa mkali lakini nimewaua baadhi ya askari waliopiga mswaki asubuhi kwenye mto ule.
"Hawawezi kukubali kirahisi, lazima watanisaka kwa udi na uvumba, wakinikosa porini watakuja kunitafuta hapa na lazima watanikamata."
"Sasa ulikuwa na wazo gani?"
"Nitoroke."
"Uende wapi?"
"Nitokemee zangu mbele kwa mbele huku nikimlinda mwanangu na wanyama wakali."
"Kwa nini usibakie ili siku wakija ujifiche usijitokeze?"
"Mmh, hiyo itakuwa yamkini, hujui wana ujuzi gani katika kusaka wahalifu, wanaweza kunikamata kama kuku wa mdondo, shoga niache nitokomee zangu
Mungu anajua majaliwa yangu na mwanangu."
"Sema tu wasiwasi wako, basi wakipita hao watu urudi sidhani kama watarudi mara mbili."
"Sawa shoga."
"Sasa kwa nini usimuache Kusekwa ili uende peke yako? Si unajua jinsi pori linavyotisha hasa usiku huu."
"Hapana shoga huenda hii ni safari yangu ya mwisho, hivyo siwezi kumuacha mwanangu japokuwa kiza cha nje kinatisha pia hatufahamu tunakwenda wapi. Ila
tuombee kwa Mungu atulinde ili tuonane tena."
"Yaani huwezi amini moyo wangu umekuwa mzito kwa nini usiahirishe kuondoka usiku huu, uondoke asubuhi?"
"Hapana shoga, niamuapo kitu siwezi kukisitisha, niache niondoke nitarudi baada ya siku mbili. Nina imani huenda asubuhi ya kesho wakaingia hapa."
"Mmh sawa, nakuombea safari njema na Mungu akutangulie kwa jambo lolote."
"Amen."
Bupe alimuacha Ng'wana Bupilipili apumzike kwa ajili ya safari yake ya usiku wa manane.
***
Baada ya tukio la kushtukiza la vifo vya askari watatu waliokuwa wakilinda na kutoroka kwa mtuhumiwa, jeshi lilijipanga upya kumsaka mtuhumiwa kwa
kuagizwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kumsaka muuaji ambaye alionekana ni mzoefu tena mtu hatari.
Baada ya kupatikana silaha na askari wa kutosha, msako mkali ulipangwa kuanza siku ya pili alfajiri kwa kusaka pori lote na maeneo ya karibu. Kila kitu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kilikwenda kama kilivyopangwa watu nao walijipanga kwa kuamini adui yao ni mzoefu wa kutumia silaha za moto.
Msako ulianza saa kumi na moja alfajiri wakiwa wamepishana robo saa na muda aliopanga Ng'wana Bupilipili kutoka kambini. Wao walikuwa nyuma kwa nusu
saa Ng'wana Bupilipili aliondoka majira ya saa kumi na nusu.
Ng'wana Bupilipili aliondoka kambini majira ya saa kumi na nusu akiwa amembeba mwanaye mgongoni kwa kumfunga madhubuti na kitenge.
Kwa ujasiri mkubwa, aliingia ndani ya pori lenye kiza kinene. Akiwa amejitolea kwa lolote litakalotokea mbele yake, alianza safari yake kwa kupita kwenye
mbuga iliyokuwa ikitisha huku milio ya wanyama na wadudu watembeao usiku ikitawala.
Hali ya hewa ilikuwa ya baridi kali lakini hiyo haikumsumbua. Alitembea huku akimuomba Mungu amfikishe salama na kumlinda na vitu vibaya japokuwa
hakujua anakwenda wapi usiku mnene kama ule.
Baada ya mwendo wa robo saa wingu zito lilitanda na kuongeza kuimeza nuru ndogo ya nyota na kuongeza hofu kwa Ng'wana Bupilipili.
Alimuomba Mungu amuokoe na mvua ile kwa vile sehemu aliyokuwa akienda hakukuwa na sehemu ya kujikinga asilowane.
Dua yake haikufua dafu kwani baada ya dakika tano mvua nzito ilishuka.
Alijikuta akipata wazo la kurudi kambini, kwani sehemu aliyokuwa akielekea ilikuwa haionekani vizuri kutokana na kiza kizito.
Hakujua ajifiche wapi, alisimama akiwa amemkumbatia mwanaye aliyemtoa mgongoni na kumweka kifuani. Alijikuta yupo kwenye uamuzi mzito.
Mvua iliendelea kuwanyeshea ikiambatana na upepo mkali. Aliamini kabisa kurudi ni kujitia ndani ya kitanzi, akapiga moyo konde na kuamua kuendelea na
safari.
Lakini kwa upande mwingine aliona kama ataendelea na safari itakuwa sawa na kuhatarisha maisha ya mwanaye kwa mvua na baridi kali ya usiku huo.
Hakuwa akijua mvua itakatika saa ngapi, hivyo lazima mwanaye angepata matatizo ya baridi ambayo yangemfanya awe katika wakati mgumu wa kumhudumia
mtoto pia kujificha na maadui zake.
Alijikuta akipiga moyo konde na kuamua kuendelea na safari yake kwa kuamini haitanyesha muda wote uliobakia kufika asubuhi. Alitembea huku
amemkumbatia mwanaye.
Alitembea bila kupumzika kwa zaidi ya saa moja huku mvua ikipungua na kumfanya aendelee na safari yake kwa kuingia ndani ya vidimbwi vya maji bila kujua
kwa vile kiza kilikuwa kizito hasa kutokana na wingu zito lililokuwa limetanda.
Baada ya mwendo mfupi alijikuta akipita kwenye njia ambayo ilikuwa na shimo na kumfanya ateleze na kutumbukia kwenye shimo lililokuwa limejaa maji.
Alipiga kelele za woga na kujikuta akizama mpaka chini na mwanaye, alianza kuhangaika ndani ya maji kuokoa maisha yake na ya mwanaye.
Alibahatika kushika mzizi uliokuwa ndani ya maji, kwa nguvu zake zote aliufuata ule mzizi hadi kufanikiwa kutoa kichwa chake nje na cha mwanaye.
Aliung'ang'ania ule mzizi huku akichezesha miguu na kufanikiwa kukanyaga jiwe lililokuwa pembeni ndani ya maji mle shimoni.
Alijisogeza hadi juu ya jiwe na kusimama juu yake. Mikono yake ikiwa bado imeshikilia ule mzizi ambao ulikuwa kama nguzo yake mle ndani ya maji.
Baada ya kusimama ndani ya maji aliweza kujitoa mpaka sehemu za kifua, sehemu iliyobaki ilibakia ndani ya maji. Bado hakuona nje wala kujua urefu wa shimo
lile. Alimuomba Mungu amuokoe mwanaye kama kifo basi kimkute yeye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikosi maalum kiliendelea na msako wa nguvu katika pori lile kwa kumtafuta Ngwana Bupilipili kila kona bila mafanikio, kwa kupita pori kwa pori.
Watu wote walitawanyika na kuziba njia zote za kutokea kusubiri kupambazuke ili msako kamili uanze.
Wakati kunapambazuka Ngwana Bupilipili alijikuta yupo ndani ya shimo ambalo pembeni yake kulikuwa na mti mkubwa ulioingiza mizizi yake ndani ya shimo.
Ilikuwa ajabu muda wote wa misukosuko mwanaye hakupiga kelele, alikuwa kimya na kutulia kwa mama yake.
Ilifika hatua ya Ngwana Bupilipili kufikiri mwanaye huenda amefariki kutokana na ukimya wake. Alipomuita aliitikia kumuonesha mama yake yupo salama.
Baada ya kuhakikisha mwanaye yupo salama alishika mizizi ya ule mti na kupanda hadi juu. Alifanikiwa kutoka ndani ya shimo salama, kwa vile alikuwa
amechoka na maji ya mvua alijilaza pembeni ya mti na mwanaye ambaye alimuachia ziwa anyonye.
Akiwa katikati ya usingizi alisikia sauti za watu wakibishana.
Sidhani kama atakuwa amefika huku.
Bwana wee kwani nani alikuambia adui huwa ana mpaka wa sehemu ya kukimbilia?
Kwa hiyo tuendelee kumtafuta, nina uhakika tutampata.
Haya jamani safari iendelee mvua ya leo inatisha tumekesha nayo na kuamka nayo, nguo zote zimetota maji.
Hii ndiyo kazi ya jeshi.
Haya jamani nataka mpaka saa sita mchana tuwe na jibu tumempata au la.
Haya jamani tunaweza kuendelea tumepumzika vya kutosha.
Ngwana Bupilipili alijua amekwisha, lazima wangemuona hakuwa na sehemu ya kukimbilia. Sauti za askari zilizidi kumsogelea, hakuwa na ujanja zaidi ya
kumchukua mwanaye bila kufikiria anafanya kitu gani na kujitupa naye ndani ya shimo la maji ili kujificha.
Kama mwanzo aliporomoka ndani ya maji na kwenda hadi chini ya maji kisha alirudi juu na kufanikiwa kuishika mizizi ya mti ambayo ilimsaidia kumpandisha
juu.
Aliwasikia watu wale wakizungumza huku wakisogea kwenye lile shimo. Ngwana Bupilipili alizama chini ya maji na mwanaye kwa muda ili watu wale
wasimuone.
Baada ya muda alitokeza kwa juu kuvuta hewa. Aliwaona wakiwa wamempa mgongo, aliweza kuwaona askari waliokuwa wamebeba silaha kali za kisasa kama
walikuwa wakimsaka Osama.
Moyoni alijiuliza kama watamkamata watamfanya nini. Pembeni ya shimo lile kulikuwa na majani ambayo angeweza kusimama chini yake na mtu wa juu
asimuone.
Alijisogeza chini ya yale majani ambayo yalimficha. Aliendelea kumuomba Mungu wale watu waondoke haraka kwani maji ya mle shimoni yalikuwa ya baridi
tena machafu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wasiwasi wake mkubwa uchafu na baridi lile ni hatari kwa afya ya mwanaye. Akiwa bado anamuomba Mungu alimsikia mtu mmoja akisema.
Ngoja nikojoe shimoni.
Haikupita muda mkojo ulitua kichwani kwa Ngwana Bupilipili. Ilibidi atulie na kuuacha mkojo ule umwagikie kichwani. Baada ya jamaa kumaliza aliwasikia
wakishauriana kuhusiana na msako uliokuwa ukiendelea bila mafanikio.
Jamani kwa nini tuendelee kumtafuta porini kwa nini tusiende hata kwenye kile kituo cha kiroho labda atakuwa amekimbilia kule? mmoja alitoa wazo.
Wazo zuri, wengine watakwenda kule na tuliobaki tutaendelea kumtafuta.
Kwa hiyo?
Muda huu tupumzikeni kidogo kama nusu saa kisha tutaendelea na msako, tuhakikishe mpaka jioni kila kitu kiwe kimeeleweka, aliagiza mkuu wa msako ule.
Hakuna tatizo.
Baada ya muda Ngwana Bupilipili alisikia kimya sehemu ile, hakuwa na haraka aliongeza dakika tano kuthibitisha kweli wameondoka.
Baada ya dakika tano kupita alishika mizizi na kujipandisha juu, alipofika juu alishukuru Mungu hakukuwa na mtu yoyote.
Taratibu kama komandoo wa kivita aliyekuwa akiwatoroka maadui, alifanikiwa kuwatoroka baada ya kuwaona kwa mbali.
Alielekea upande wa Mashariki kuwakimbia adui zake. Baada ya mwendo mfupi aliamua kupumzika kwani mwanaye alianza kutetemeka kwa baridi.
Alijitahidi kumkumbatia lakini haikusaidia kwa vile naye mwili wake kwa baridi la muda ule na ubaridi wa maji uliufanya mwili wake uanze kufa ganzi.
Kila dakika hali ya mwanaye ilibadilika na kuonesha kupoteza uwezo wake wa kawaida. Hali ile ilimfanya Ng'wana Bupilipili kuchanganyikiwa na kuona jinsi
alivyokuwa akimpoteza mwanaye huku akimuona.
Baada ya kuanza kuhema kwa shida, alijilaumu kwa kukaidi ombi la shoga yake Bupe la kumuacha mtoto kambini. Aliamini kama mwanaye atakufa yeye ndiye
atakayebeba lawama kwa vile hali ile isingemtokea kama angemuacha mtoto kambini.
Moyoni alijuta na kuona kama mwanaye atakufa, basi kwake yeye hakuwa na sababu yoyote ya kupoteza maisha ya mume wake, kupoteza maisha ya wanakijiji
na sababu ya yeye kuteseka vile.
Hali ya mwanaye ilizidi kuwa mbaya hata akawa haoneshi kupumua. Aliamini kabisa njia iliyokuwepo ya kumsaidia mtoto wake ni kujisalimisha kwa wale
askari ambao wangeweza kuokoa maisha ya mwanaye kama wakifanikiwa.
Kwake hakuona hatari yoyote kama atafungwa au kunyongwa na mwanaye kubakia salama japokuwa hakujua mtoto wake ataishi maisha gani.
Alimchukua mtoto wake na kumuweka begani na kuwafuata wale askari waliokuwa wakimsaka huku akitokwa na machozi kwa uchungu wa mwanaye. Askari
waliokuwa wamejipumzisha walishtuka kumuona mwanamke akiwa amembeba mtoto begani huku akionekana ametota kwa maji.
Wote walimtazama na kujiuliza anatoka wapi. Alipofika mbele yao alimbwaga mtoto wake mbele yao huku akisema:
"Haya mleni nyama sasa," alisema huku akifoka kwa sauti ya kilio.
"Mbona hatukuelewi, tumle nyama kivipi?" askari mmoja alimshangaa.
"Si mlikuwa mnataka kuona mwanangu anakufa? Haya amekufa furahini, haya nipelekeni mkaninyonge sasa."
Mkuu wa oparesheni hiyo alimchukua haraka yule mtoto na kugundua tatizo lake ni baridi yabisi, kwa haraka walitengeneza joto ambalo lilimsaidia mtoto
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kurudi katika hali ya kawaida kisha alichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo chao cha huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
Wakati huo Ng'wana Bupilipili alikuwa ame wekwa chini ya ulinzi baada ya kugundulika ndiye adui aliyekuwa akitafutwa. Hakutaka kuwabishia.
Walimshangaa mtu ambaye walikuwa na wasiwasi huenda ni mkakamavu tena mwenye mafunzo ya kijasusi, kumbe ni mwanamke. Mkuu wa oparesheni ile
alishtuka na kuuliza mara mbili.
"Ndiye huyu?"
"Ndiyo mkuu," alijibu askari aliyekimbiwa na Ng'wana Bupilipili.
"Sasa mbona anaonekana tofauti na sifa nilizosikia, nilijua ni mkakamavu mwenye mwili wa mazoezi."
"Mkuu usimtazame kwa macho, ni zaidi ya gaidi, mwanamke huyu kama alivyoniahidi alipania kukimaliza kijiji kizima."
"Eti mama ni kweli?" Mkuu alimuuliza kwa upole.
"Maswali ya nini, si mmeshanikamata? Ninyongeni basi au niueni kwa risasi si mmekuja na bunduki kuniua?" Ng'wana Bupilipili alisema huku akilia kwa
hasira.
"Hatuwezi kukunyonga kwa vile sisi si mahakama, la muhimu maelezo yako yanaweza kusababisha tukuache huru."
"Hayatasaidia kitu kwa vile maelezo ya awali nimueleza huyu kaka, lakini mliamua kunisaka kama gaidi. Mmefanikiwa kunikamata nipelekeni nikanyongwe ili
mfurahi. Lakini naapa Mungu atalipa kwa kila roho isiyo na hatia," Ng'wana Bupilipili alizungumza kwa uchungu huku akimwaga machozi.
"Serikali haipo kwa ajili ya kumuonea mtu bali kuhakikisha kila mwanadamu anaishi kwa uhuru na amani bila kuvunja sheria," mkuu alionesha ustaarabu kwa
kujibu kwa upole.
"Kwa vile wao wamekufa ndiyo serikali imeliona hilo, na sisi tuliopoteza roho za watoto wetu na waume zetu serikali yetu ni ipi?"
"Mmepotezaje hizo roho?"
Ng'wana Bupilipili alirudia maelezo ya mauaji ya albino Kijiji cha Nyasha na kifo cha mumewe, ikiwemo kuporwa mali zao na wanakijiji cha Nyasha.
Baada ya kumsikiliza mkuu alisema:
"Bado hukutakiwa kuchukua sheria mkononi kwa vile kuna vyombo vya sheria."
"Mmh! Vyombo vya sheria kwa vile wamekufa wao, mbona vifo vya watoto albino hamkuwahi kuja hata siku moja ila hivi ndiyo mmetengeneza mtego wa
kuninasa, ndiyo maana nikasema nipelekeni mkani.ni..ni..ni.. Haaa!"
Ng'wana Bupilipili alishika chini ya titi la mkono wa kushoto baada ya kusikia mchomo mkali kwa ndani kama kumepasuka.
Maumivu yalikuwa makali na kuhisi kama mbavu zinagusana. Alipiga kelele za maumivu na kuanguka chini akiwa amepoteza fahamu.
***
Ng'wana Bupilipili baada ya kurudiwa na fahamu, alipofumbua macho alijiona yupo ndani ya hema amelazwa chini kwenye turubai lililokuwa limetandikwa na
pembeni yake alikuwepo mwanaye Kusekwa ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi.
Alijikuta akijiuliza pale ni wapi na amefikaje, alimuangalia mwanaye ambaye alikuwa amelala huku akionekana yupo katika hali ya kawaida. Ili kuhakikisha
mwanaye ni mzima aliweka sikio kifuani ambako alimsikia akihema vizuri.
Akiwa bado anamuangalia vizuri mwanaye, alishtushwa na sauti za watu waliokuwa wakisogea kwenye hema lile huku wakizungumza.
"Huenda amesharejewa na fahamu, ngoja tukamuangalie, yule mwanamke simuamini kabisa."
"Lakini mbona sifa za yule mwanamke hazilingani naye? Huenda kuna wahusika wakuu na yeye ni mtu wa kutumwa tu," askari mmoja alisikika akisema.
Ng'wana Bupilipili alipowasikia wamekaribia alirudi sehemu aliyokuwa amelala na kujilaza kana kwamba hajarudiwa na fahamu kwa kujitahidi kuhema kwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
taratibu sana. Askari wale waliingia hadi ndani na kumkuta amelala, hata kuhema kwake hakukuwa kwa kawaida.
"Bado hajaamka twende zetu," alisema mmoja baada kuwa na uhakika mtuhumiwa bado amelala.
"Sasa tutaondoka saa ngapi?"
"Mkuu amesema tumsikilizie kwa muda zaidi ya hapo tutambeba na kuondoka naye."
"Unajua bado siamini kama ni yeye ambaye katupa taabu ya miezi zaidi ya sita."
"John anasema yule mama kwa macho haoneshi hatari yake kwani alisema alifanya vile kulipa kisasi cha mume na mtoto wake aliyeuawa na wanakijiji kwa
imani za kishirikina."
"Mmh! Basi ni kiboko, ni wanawake wachache wenye moyo wa ujasiri kama yeye."
"Ndiyo maana mkuu amesema ulinzi uwe mkali."
"Sasa unataka kuniambia huyu mwanamke na mtoto wake walikuwa wanaishi wapi na hii mvua?"
"Kutokana na maelezo ya John alisema anaishi porini kama mnyama."
"Utani huo, kwa muda gani?"
"Huu ni mwezi wa saba sasa."
"Mungu wangu, alikuwa anakula nini na kulala wapi?"
"Hapo ndipo unatakiwa ujiulize juu ya uwezo wa kikomandoo wa huyu mwanamke."
"Au amewahi kupitia jeshini?"
"Hilo kwa kweli sijui, ila mwanamke huyu kama ni kweli ni zaidi ya mwanajeshi wa kawaida."
"Ina maana yupo peke yake?"
"Kutokana na maelezo inaonekana aliondoka kijiji pale baada ya kuuawa mtoto na mumewe na kuamua kulipa kisasi kwa mkono wake."
"Lakini mkuu si amesema lazima aseme ukweli au ateswe sana, kwa mateso ya bosi hata awe komandoo lazima atasema."
"Ngoja tuone."
"Mmh, twende tupeleke taarifa."
Ng'wana Bupilipili aliwasikia wakiondoka, alitulia kwa muda kisha alinyanyuka taratibu alipolala na kunyata hadi kwenye mlango wa kutokea. Alichungulia kwa
chati nje, aliwaona askari wawili waliokuwa wamekaa juu ya gogo la mti wakicheza karata wakiwa wamempa mgongo.
Aliangalia upande mwingine ambapo aliwaona wengine kwa mbali wakinywa pombe kali kukata baridi. Upande wa pili kulikuwa na mbuga ambayo ilikuwa ni
vigumu mtu kutoka nje ya hema bila kuonekana.
Akawa na wazo la kutoroka kwa kuamini akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria lazima hukumu itamuumiza yeye. Aliamini anaweza kupita kwa mwendo wa
kunyata nyuma ya wale askari. Lakini wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kama ataonekana basi atajiweka katika wakati mgumu sana.
Aliamini ukweli wowote hautaaminiwa zaidi ya kuteswa ili kulazimishwa aseme asichokijua. Aliamini njia nyepesi ni kutoroka na kupania kama atafanikiwa
kutoroka asingesimama kwa siku mbili kutembea pori kwa pori mpaka atakapotoka nje.
Akiwa bado anatafakari jinsi ya kutoka ndani ya hema lile, macho yake yalitua kwenye uwazi uliokuwa upande wa chini ya hema. Wazo la haraka lilikuwa kupitia
katika upenyo ule ambao hakukuwa na ulinzi wowote, wazo la kumbeba mtoto wake aliliweka pembeni kwani aliamini kutokana na kauli za wale watu
mwanaye yupo salama.
Alimchukua mtoto wake na kumkumbatia kwa muda huku machozi yakimtoka, kwa sauti ya chini alimueleza mtoto wake:
"Kusekwa baba, nakupenda sana mtoto wangu, nina imani mpaka sasa upo katika mikono salama ila mama yako hatari nzito ipo mbele yangu. Nakuacha baba ili
nami niokoe maisha yangu kwani bila hivyo kitanzi kipo shingoni kwangu.
"Kusekwa baba, mama yako sijui niendako, japo wewe ni mtoto usiyejua lolote lakini niombee mama yako nitoke salama, safari yangu iwe yenye muongozo
mwema na Mungu aniongoze nifike kwenye mikono salama.
"Nakupenda mwanangu, nakupenda sana na Mungu akulinde kwa jambo lolote baya, Mungu akipenda tutaonana siku yoyote kama bado tunaishi na kama siyo
duniani basi kwenye ufalme wake wa milele."
Baada ya maombi yaliyomtoa machozi huku moyo ukimuuma kutengana na mwanaye kipenzi kama angefanikiwa kuwatoroka, alimrudisha kwenye turubai na
kusimama kwa muda akimuangalia mwanaye huku moyo ukizidi kumuuma.
Alishika mikono kifuani huku akilia, akageuka na kupiga magoti kupekenyua sehemu iliyokuwa na uwazi kwa chini na kutoka kwa kutambaa. Baada ya
kufanikiwa kutoka bila kuonekana, aliingia porini kwa mwendo wa kuinama na kunyata.
Ilifikia hatua ya kutembelea tumbo kama komandoo aliyekuwa akivamia kambi, baada ya kufanikiwa kufika mbali kidogo ambako aliamini kabisa hawezi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuonekana, alitimua mbio kukata pori bila kujua hatari atakayokutana nayo mbele.
Alikimbia kwa mwendo wa mbio za marathoni bila kupumzika kwa kuamini uwezo wake wa kukimbia bila kupumzika ndiyo utakaookoa maisha yake.
Alikimbia kwa saa tatu bila kupumzika na kujikuta ametokea kwenye barabara kubwa ya lami. Alisimama na kuanza kuhema kwa kasi, hali iliyomfanya ahisi
kizunguzungu. Bila kupenda alianguka chini na kupoteza fahamu.
***
Baada ya muda kukatika, mkuu wa kikosi maalumu cha kumsaka muuaji wa Kijiji cha Nyasha alimtuma askari akamuangalie tena Ng'wana Bupilipili kama
ameamka ili kama bado amelala wambebe na kuondoka naye. Askari alikwenda hadi kwenye hema kuangalia kama mtuhumiwa wao ameamka.
Alikwenda hadi ndani ya hema lakini katika hali ya kustaajabisha, ndani ya hema hakukuwa na mtu yeyote zaidi ya mtoto aliyekuwa bado amelala. Ilibidi
awaulize wenzake waliokuwa wanaendelea kucheza karata.
"Oyaa washikaji yule mwanamke yupo wapi?"
"Si amelala humo ndani."
"Mbona simuoni?"
"Sele hebu acha utani, yupo humo ndani."
"Kweli washikaji yupo mtoto peke yake."
Wale askari waliokuwa wakicheza karata walinyanyuka na kwenda hadi ndani ambako hawakumkuta. Walijikuta wakichanganyikiwa na kuanza msako kuzungaka
hema lakini hakukuwa na mtu yeyote eneo hilo.
Walijikuta wakipagawa na kujiuliza watamwambia nini mkuu wao aliyewapa jukumu la kumlinda yule mwanamke aliyeonekana dhaifu mbele ya macho ya watu
lakini ni hatari kwa vitendo.
Waliotumwa walirudisha taarifa za kutoweka kwa Ng'wana Bupilipili na kumtelekeza mtoto. Sherehe yote ya kumpata mtuhumiwa iliyeyuka na kuamuliwa
ufanywe msako wa haraka. Kila askari alitawanyika kwenda anapopajua ili mradi arudi na mtuhumiwa.
Askari wote walitawanyika huku waliofanya makosa ya kizembe wakichanganyikiwa zaidi kwa kukimbia ovyo bila kujua wanakwenda wapi.
Askari wengine walibakia pamoja na mkuu wao kwa ajili ya kulinda usalama wa mtoto.
Msako ulifanyika mpaka usiku wa manane lakini hawakupata chochote, mkuu wa oparesheni ile aliwaeleza waliofanya uzembe wahakikishe
mtuhumiwa anapatikana la sivyo wasirudi. Hawakupata muda wa kupumzika, walirudi kufanya msako.
Waliona hawawezi kukaa na yule mtoto aliyeanza kumlilia mama yake. Kwa vile kituo cha kulea watu wanaoishi katika mazingira magumu kilikuwa
karibu, siku ya pili walimchukua na kumpeleka katika kituo kile. Walipofika mkuu wa kikosi cha kumsaka muuaji alijitambulisha kwa Father Joe, baada ya
kujitambulisha walimueleza sababu ya kuwepo pale.
Father alikubali kumpokea mtoto yule na kumlea, lakini alishangaa kumuona ni mtoto wanayemfahamu.
"Ha! Huyu mtoto si wa hapahapa kambini?"
"Hapana Father huyu tumemuokota porini na mama yake," alijibu mkuu wa oparesheni.
"Huyu wa hapahapa kambini na mama yake anakaa hapahapa, jina lake anaitwa Kusekwa."
"Hapana huyu mama yake ni muuaji tena amekimbia baada ya kumkamata na kumtelekeza huyu mtoto," mkuu wa oparesheni alizidi kubisha.
"Hapana, mama yake ni mkimbizi wa Kijiji cha Nyasa, si muuaji," Father Joe alimtetea Ng'wana Bupilipili.
"Father hebu tuitie huyo mwanamke tumuone na amtambue mtoto wake," mkuu wa oparesheni alimuomba Father Joe.
Father Joe alinyanyua simu na kumwita sister mmoja, baada ya muda mfupi Sister Mary aliingia.
"Sister Mary naomba uniitie Ng'wana Bupilipili."
"Sawa Father," sister aligeuka na kuondoka.
Baada ya muda alirudi akiwa peke yake.
"Vipi yupo wapi?"
"Hayupo father."
"Atakuwa amekwenda wapi?"
"Kwa kweli jirani zake hawana taarifa zozote mpaka jana usiku wanakwenda kulala walikuwa wote."
"Chumba chake kina vitu vyake?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ngoja nikahakikishe," sister alisema huku akiondoka.
Sister alitoka tena na kwenda chumba cha Ng'wana Bupilipili ambako hakukuwa na mabadiliko yoyote. Alirudi na kutoa taarifa, baada ya kusikia vile mkuu wa
oparesheni aliuliza.
"Kwani huyo mnayemsema mnayo picha yake?"
"Ndiyo."
"Basi tupeni tuiangalie kama siyo yeye tuondoke tukaendelee na msako wetu."
Father Joe alifunua faili lililokuwa na picha za watu wote waliokuwa kwenye kambi ile. Alichambua picha mojamoja kwa umakini mpaka akaipata picha ya
Ng'wana Bupilipili.
"Picha yake hii hapa," Father Joe alisema huku akiwakabidhi.
Waliichukua ile picha na kuitazama kwa muda na kugundua kumbe mbaya wao hakuwa akikaa porini kama alivyojinadi bali alikuwa anakaa kwenye kambi ile.
"Father ndiye huyu!"
"Mna uhakika?" Father Joe aliuliza macho yakiwa yamemtoka pima.
"Kwa asilimia mia moja."
"Mmh! Mnataka kuniambia huyu mwanamke ni muuaji?" father alishtuka.
"Ndiyo father, ameua watu wengi Kijiji cha Nyasha na askari wenzetu wawili."
"Lakini si ndiyo kijiji alichokuwa akiishia zamani kabla ya kukimbia kuokoa maisha ya mwanaye huyu mlemavu wa ngozi na kujikuta akimpoteza mumewe
aliyeuawa na wanakijiji na kufanikiwa kukimbilia hapa tulipowahifadhi siku zote za maisha yao?"
"Ni kweli father, maelezo yako na ya huyo mwanamke yapo sawa, aliahidi mbele yangu kuwa analipa kisasi na kama asiponyongwa baada ya
kumkamata, atahakikisha Kijiji cha Nyasha kinabakia historia, atakifagia chote," alisema askari aliyemkamata Ng'wana Bupilipili.
"Mmh, kumbe ndiyo hivyo, mbona mimi nilikuwa sijui!" father alishtuka huku Sister Mary naye akisikia habari ya kumshangaza.
"Basi father yule mwanamke ni zaidi ya gaidi, ameua watu wengi kwa sumu ya dawa ya kuulia wadudu katika maji."
"Dawa ya kuua wadudu ni dawa gani hiyo?"
"Kwa kauli yao nakubaliana nao, Ng'wana Bupilipili anahusika, chumbani kwake chini ya godoro nimeikuta hiyo dawa zaidi ya paketi tatu," Sister Mary
aliwaunga mkono.
"Mmh, kama ni hivyo yule mwanamke ni mbaya sana, nilikaa naye na kumueleza awasamehe na kumuachia Mungu na kunikubalia. Kumbe alikuwa na siri yake
nzito moyoni ambayo sote humu ndani tulikuwa hatujui," Father Joe alisema kwa masikitiko.
"Kwa kuonesha huyu mwanamke ni mzoefu hii ni mara ya pili tunamkamata na kutoroka juzi tulimkamata lakini alifanikiwa kututoroka."
"Mmh, sasa napata picha inawezekana siku hiyo ndiyo aliyokimbia na kuangukia mlango wa kuingilia getini na kudanganya alikimbizwa na mnyama mkali,"
Father alitoa ushuhuda.
"Kwa usemi huo ni kweli kabisa, mmh! Mwanamke yule basi ni mzoefu kama ameweza kukaa hapa na kufanya mauaji bila mtu yeyote hapa kambini kujua ni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mzoefu wa hali ya juu," Sister Mary alisema kwa masikitiko makubwa.
"Sasa atakuwa wapi?" Father Joe aliwauliza wale askari.
"Kwa kweli mpaka sasa hatufahamu kakimbilia wapi, kwa sababu mazingira ya kututoroka ni ya hali ya juu. Inawezekana alishapitia mafunzo fulani ya jeshi, si
rahisi mtu wa kawaida akawa na uwezo wa kufanya vile hata kuweza kutembea porini peke yake na kukimbia kwa umbali mrefu."
"Sasa mtafanya nini?"
"Tutaondoka na picha hii ambayo tutaiweka katika vyombo vya habari, lazima atakamatwa tu."
"Lakini nina imani kama ni tabia yake ya kurudi kambini basi lazima atarudi na sisi tutawajulisha mara moja," Father Joe alitoa wazo.
"Mtatusaidia sana."
Walikubaliana wamuache mtoto Kusekwa ambaye ni mlemavu wa ngozi na kuamua kuendelea kumsaka Ng'wana Bupilipili.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment