Search This Blog

DAMU YA MWANANGU - 4

 







    Simulizi : Damu Ya Mwanangu

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyamwela akajikuta ametokezea sehem ya kutisha,,akaangaza angaza macho yake,,lakini hakuitambua sehemu hiyo!

    hofu ikazidi kuongezeka,,,akazipigq hatua za kunyatia,,akajificha nyuma ya jiwe kubwa...ghafla akahisi kudondokewa na kitu chq kimiminika akanyanyua uso wake kutazama upande wa juu ya jiwe....akaona damu nyingi zinamwagika kutoka juu ya jiwe kuja upande wa chini,,,akatimua mbio,,,,

    alikimbia pasipokujua ni wapi anaelekea! kwa mbali akamuona yule mwanamke aliyemuona kule nyumbani kwake muda mfupi uliopita! lakini mwanamke huyo aonekani sura alikuwa kavalia mavazi meupe,,huku kambeba mtoto mchanga,,aliyekuwa anchuruzika damu yingi upande wa shingoni!

    mbaya zaidi,,mwanamke huyo alikuwa anaonekana akiishilizia mguu wa mwisho kuingia katika chumba kilichokuwa na mlango!

    punde si punde giza likatawala neo hilo! hofu ikazidi kuongezeka!

    Nyamwela akaangaza macho yake kutazama huku na kule,

    hakuweza kuona chochote kwa sababu giza lilikuwa totoro!

    kwa mbali akaona nuru ya mwanga ukimulika kuja upanda wake,,

    macho yakamtoka ! ghafla akamuona yule mganga akiwa kashikilia moyo,,,mganga huyo alikuwa anapumua kwa haraka haraka,,kisha akasema,,umeniponza,,hakika hata wewe huwezi kubaki hai!

    baada ya kusema maneno hayo mganga akadondoka chini na kupoteza uhai!

    punde si punde ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia mfululizo!

    sauti hiyo ilijirudia rudia kutokana na mwangwi...

    ghafla giza likatoweka,,na mwanga ukatawala! Nyamwela akashtuka kumuona yule rafiki yake akiwa ameshikilia upanga mkali,,ni yule rafiki yakealiyemchinja kule porini!

    wakati anataamaki,,kwa mbali akaonekana Muna akiwa anazipiga hatua kuja upande huo,,,,

    ghafla akajitokeza mtoto wa Nyamwela akiwa hana kichwa...mtoto huyo alikuwa kalala chini,,mbele ya Nyamwela!

    akatimua mbio!! kabla hajafika mbali,,akahisi harufu kali ya damu inanuka kwenye pua zake! akanyanyua ukono wake kuguza pua zake! akashtuka kuona damu zikimtoka puani,,,punde si punde yule mwanamke,,aliyekuwa kavalia mavazi meupe,akajitokeza kando ya Nyamwela, akiwa kashikilia upanga ,,,akanyanyua upanga huo na kufyeka shingo ya Nyamwela..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyamwela akashtuka kutoka usingizini,,kumbe alikuwa anaota ndoto,,usingizini,,,akagusa shingo yake kuhakikisha kama yupo salama! kumbe matukio yote,,ilikuwa ni ndoto!

    akanyanyuka haraka kutoka kitandani,,akachukua kiberiti na kuwasha koroboi!akageuza shingo yake kutazama kitandani,,akamuona mkewe akiwa kalala usingizi huku mikono yake akiwa kaiweka juu ya tumbo lake lenye ujauzito!

    Nyamwela.akajisemea moyoni,,"ndoto hii inamaanisha nini? mbona sielewi! punde si punde mkewe akadamka,,akastaajabu kumuona mumewe akiwa kasimama kando ya kitanda akimtazama kwa mshangao!

    akaamua kumuuliza,,"mbona umesimama hapo?

    usiku wote huu!

    kabla hajamaliza kuongea, Nyamwela akasema,nimeota ndoto mbaya sana!



    wakati huohuo upande mwingine walionekana vijana wawili wakiwa wanatembe barabarani huku wakiimba nyimbo...sauti za vijana hao zilisikika kama sauti ya watu waliozidiwa na ulevi!

    mmoja kati ya vijana hao wawili,,akasema,,"huyu bwege analala na pesa ndani wakati sisi tunashida na pesa.

    kumbe vijana hao waliiba pesa zilizokuwa Nyumbani kwa Nyamwela! mcha wa leo....hapakuwepo mtu yeyote hivyo waliweza kuingia ndani ya nyumba ya Nyamwela na kuiba pesa hizo.



    Ke nyumbani kwa Nyamwela,,alionekana mke wa Nyamwela akisema,,"hiyo ni ndoto tu mume wangu,,cha msingi sali kwa kukemea,,kisha lala..

    Nyamwela akamtazama mkewe,,kisha akasema ni jambo jema mke wangu,,wacha nichukue biblia,,,,

    akazipiga hatua kuifuata kabati ndogo,,akaifungua ili achukue biblia ,ghafla akashtuka! akauliza kwa sauti ya kukali,,"pesa zangu niliziweka humu ndani ya droo,, ziko wapi?

    Muna akamtazama mumewe kwa macho ya mshangao!

    kisha akasema,,"ni siku kumi sasa sijafungua hiyo droo,ebu tazama kwa makini,

    Nyamwela akasema kwa ukali,,"pesa hizo sio za kwangu,,nilikopa kwa ajili ya kuandaa shamba,,nataka pesa zangu..

    Muna akabaki kimya,,

    Nyamwela akaingiwa na hasira,,akafungua mlango na kutoka nje ya chumba,,akachukua kisu,,akarudi chumbani,,akamkuta muna kasimama kando ya droo akizitafuta pesa hizo..

    alipogeuza shingo yake ,,,mara ghafla!!!!!!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nyamwela akanyanyua mkono wake uliokuwa umeshikilia kisu, Muna akastaajabu akauliza kwa msangao! ,,"mbona wataka.kuniumiza pasipo kosa?

    kabla hajamaliza kuongea,,

    Nyamwela akamdunga kisu upande wa tumboni! macho yakamtoka Muna,,akashindwa hata kupiga kelele akabaki kshikilia tumbo lake,,kwenye ile sehemu aliyodungwa kisu!

    damu nyingi zikamtoka,,akadondoka chini na kupoteza maisha! akiwa na ujauzito wa kukaribia kujifungua!

    Nyamwela akatahamaki,,kuona mkewe kadondoka chini!

    akahisi kuchanganyikiwa akajiwemea moyoni,,"jamani nimeuwa! kwa nini nikefanya hivi!

    akatafakari nini cha kufanya,,,wazo likamjia,,"nisipofanya jambo la kupoteza ushahidi nitaozea gerezani..

    akazipiga hatua za haraka haraka akatoka chumbani na kuelekea kwenye stoo,,akachukua jembe ,,sululu na koleo,,akarudi ndani ya nyumba,, akaanza kuchimba shimo ndani ya chumba chake cha kulala,,,

    alichimba shimo hilo kwa masaa kadhaa mfululizo,,alipohakikisha shimo hilo linafaa ,,akatumbukiza maiti ya Muna,,na kuanza kufukia shimo hilo,,,alipomaliza akaweka kitqnda juu ya shimo hilo!

    kiwha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi!

    hakuweza kupata usingizi usiku kucha,,kutokana na mawazo aliyokuwanayo!



    Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema,,na kuondoka zake,,

    Wakati huohuo,,alionekana mama yake Muna,,akijiandaa na safari ya kwenda kuwatembelea kwa lengo la kuwajulia hali,,,

    akatoka na kuzipiga hatua kuelekea nyumbani kwa Nyamwela...

    baada ya lisaa limoja akawa amefika Nyumbani kwa Nyamwela,,hapakuwa na umbali mrefu,,ni kijiji cha jirani.

    akastaajabu kuona mlango umefungwa!

    akalazimika kuketi kando ya nyumba hiyo katika mti uliokuwa na matawi mengi na kutengeneza kivuli tulivu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    masaa yakazidi kusonga,,na hakuna dalili yoyote ya mtu kurudi nyumbani,,,akajiuliza,,"inamaana watakuwa wamekwenda wapi?

    mbona muda wa kujifungua umekaribia,,sasa kwa nini anazurura!

    mama Muna alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu...

    akakata tamaa akaamua kurudi nyumbani kwake!



    ilipofika majira ya saa nne za usiku,,akaonekana Nyamwela akizipiga hatua kuusogelea mlango wa nyumba yake!

    akafungu mlango na kuingia ndani ya nyumba!

    lakini alikuwa na hofu,,kutokana na kitendo cha ukatiri alioufanya

    jana.

    akasukuma mlango wa chumbani na kuingia ndani,,,punde si punde akahisi kunamtu anatembea nje ya nyumba yake,,vishindo vya mtu huyo vilisikika jirani na dirisha la chumbani kwake!

    Nyamwela akaingiwa na wasiwasi,,akatoka nje ya nyumba kwenda kutazama ni nani anayetembea nje ya dirisha la nyumba yake!

    alipozipiga hatua kuzunguka nyuma ya nyumba,,,alipoangaza angaza macho hakuona kitu chochote akalisogelea dirisha la upande wa chumba chake,,,alipolikaribia,,akasikia sauti ya mwanamke akilia kwa uchungu ndani ya chumba!

    macho yakamtoka Nyamwela,,akazipiga hatua za kunyatia akachungulia uoande wa ndani kupitia matundu yaliyokuwa kwenye mbao za dirisha hilo,,punde si punde,,

    kikasikika kiwhindo cha mtu akitembe nyuma yake,,,akageuza shingo yake kutazama!!!!lakini hakuona kitu chochote....

    akahisi kuchanganyikiwa,,hofu ikazidi kuongezeka....akaamua kuondoka eneoz hilo la nyuma ya nyumba huku macho yake yakitazama huku na kule!

    alipoukaribia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba,,ikasikika sauti ikiita jina lake!

    sauti hiyo ilitokea nyuma yake,,akageuza shingo kutazama ni nani anayemuita!

    akamuona muna,,akiwa kasimama kando,,, akinyoosha mkono wake ishara ya kumuita asogee karibu zaidi,,Punde si punde...zikasikika sauti za majibizano,,sauti hizo zilitokea ndani ya nyumba! Nyamwela alipogeuza shingo yake kutazama ule upande aliokuwa kasiamama Muna,,hakumuona tena,,ghafla ikasikika sauti nyingine ikiita jina lake,,,akageuza shingo yake haraka kutazama,,,akashtuka !!!macho yakamtoka,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi!!!!!! akazipiga hatua kurudi nyuma, akajikwaa na kudondoka chini! akaanza kupiga kelele huku kafunika uso wake kwa viganja vya mikono yake,,,mara ghafla!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    akasikia tena sauti ya mtu akiita jina lake! akaitambua sauti hiyo!!

    akafunua uso wake kutazama,,akamuona rafiki yake kipenzi aitwae Mtiku.

    macho yakamtoka! akabaki mdomo wazi huku kapigwa na bumbuwazi!

    Matiku akauliza,,"mbona upo katika hali hiyo! umepatwa na nini?

    Nyamwela hakujibu kitu!! uso wake ulionyesha kuwa na wasiwasi na hofu ya hali ya juu! macho yake yalitazama huku na kule,,,hasa ile sehemu aliyomuona Muna kasimama!

    baada ya sekunde kadhaa ufahamu ukarudi...akajisemea moyoni,,"hivi haya niliyoyaona ni kweli au maruwe ruwe tu?

    Nyamwela alijiuliza maswali mengi pasipokupata majibu!

    Matiku akabaki kasimama huku akimtazama Nyamwela kwa mshangao,,,

    Nyamwela akasema,,"naomba uniache tutaonana kesho,,sijisikii vyema.

    Matiku akaondoka zake!

    Nyamwela akanyanyuka kutoka pale chini alipodondoka,,akazipiga hatua kuingia ndani ya nyumba!



    akaogopa kukisogelea kitanda,,akajisemea moyoni,,"nimepoteza mtoto wangu kwa ujinga wangu mwenyewe! na mke wangu pia...hasira gani hizi,,

    Nyamwela aliwaza hayo,,huku machozi yakimtoka!

    akajipa moyo ,,akakisogelea kitanda na kuketi juu yake,,,baada ya sekunde kadhaa kupita akaamua kujilaza,,,akapitiwa na usingizi,,akiwa ndotoni ,ghafla akasikia sauti ya mtoto mchanga akilia,,pumde si punde akamuona Muna,,katika ndoto,,akiwa kaweka mkono wake juu ya tumbo,,huku damu nyingi zikimtoka!

    Nyamwela akashtuka kutoka usingizini! akaandaa mpango wa kuhama katika kijiji hicho.



    Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema,,na kuipiga nyumba yake mnada,akafanikiwa kupata mteja,,akauza nyumba hiyo kwa shilingi,,mitioni saba,,,

    akachukua pesa hizo na kuziweka ndani ya begi!,,akaelekea kwenye kituo cha mabasi yanayokwenda jijini Dar es salaam,,

    baada ya lisaa limoja akawa kafika mjini,,akakata tiketi,,,kisha akaingia ndani ya basi hilo! akalipakata begi lake...akisubiri safari ianze!

    Baada ya dakika kadhaa kupita,,, akaangaza macho yake kutazama upande wa nje kupitia dirishani..

    kwa mbali akamuona rafiki yake kipenzi ni yule Matiku...akaamua kuliweka begi lake lililokuwa na zile pesa zote pamoja na nguo zake....akazipiga hatua kutoka ndani ya gari. kumfuata Matiku,,angalau ampe taarifa kuwa ameamua kuhama na kwenda kuanzisha maisha mapya jijini Dar es salaam.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyamwela akaamua kutimua mbio amuwahi Matiku kabla hajafika mbali! akaamua kupaza sauti kumuita Matiku!

    Matiku akaitambua sauti ya Nyamwela akageuza shingo yake na kusimama...

    Nyamwela alipomkaribia Matiku,,,akasikia mngurumo wa gari likiondoka,,,alipogeuza shingo yake kutaza kule lilipokuwepo basi....akashtuka kuona basi hilo likitokomea kwenye barabara ya kuelekea Dar es salaam!

    Macho yakamtoka!







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog