Search This Blog

TAREHE 9 SEPTEMBER - 2

 







    Simulizi : Tarehe 9 September

    Sehemu Ya Pili (2)





                    ******************************

    Asubuhi palipokucha Zack alidamka akakuta kijakazi wa nyumba hiyo ameshaandaa chai,,akanywa chai kisha akamuaga shangazi yake na kuondoka kuelekea kule kwenye nyumba anayoishi yeye na Shamy! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    baada ya siku moja kupita;  Shamy akarejea nyumbani akitokea Mwanza,, Zack akafurahi sana,,msiku zilizidi kusonga hatimae Shamy akapata kazi, akaajiliwa katika hospitali ya Muhimbili,, Maisha ya Shamy na Zack,,yakabadilika wakahama katika nyumba hiyo,, wakapanga nyumba nzima huko Mbezi,, Shamy akaamua kumpa Zack mtaji aanze kufanya bihashara kuliko kukaa tu nyumbani pasipo kujishughurisha kutafuta kipato!!

    Shamy akampa Zack mtaji wa milioni kumi(10) zlZack akafungua duka la vifaa vya umeme,, duka hilo lilimpa kipato kizuri kila siku zilivyozidi kwenda.. Zack akabadilika akawa kijana mtanashati kuliko,, maisha yao yakawa yenye amani na furaha kila kukicha! 

    Siku moja Shamy akamwambia Zack,, "jumapili hii tutakwenda nyumbani kwa shangazi yangu,, anaishi kigamboni,,, nataka nikakutambulishe kwake!  Zack akafurahi sana..kisha akasema hata mimi pia shangazi yangu anaishi kogamboni,, tukitoka huko tutapitia nyumbani kwake pia nikakutambulishe!

    jumapili ikafika,, siku hiyo wakadamka na kujiandaa kwenda nyumbani kwa shangazi yake Shamy! kutokana na elimu aliyokuwanayo Shamy,, alikuwa ni daktari maalumu kwa kufanya upasuaji wa Moyo... hivyo alikuwa ni mtu muhimu sana na tegemezi katika hospitali hiyo....

    Shamy na Zack wakaingia ndani ya gari la Shamy. na safari ikaanza..

    baada ya lisaa limoja walifika kigamboni!!  Shamy akaliongoza gari lake kukatisha kwenye barabara ya vumbi, akiiacha lami..  Zack akastaajabu!   akauliza,, "huku ndipo shangazi yako anapoishi?

    Shamy akatabasam kisha akajibu,, ndio,, kwa nini umeuliza hivyo?  hujayapenda mazingira haya?

    Zack akasema,, "barabara hii pia inaelekea nyumbani kwa shangazi yangu! yawezekana wakawa majirani!  Shamy akaendelea kuliendesha gari lake... Zack akazidi kustaajabu kuona wanakatisha kwenye njia inayoelekea kwa shangazi yake!  akauliza kwa mshangao,, "haa!  yani huku tunapoelekea ndipo nyumbani kwa shangazi yangu... nyumba ileee..wakati Shamy anatazama ile nyumba anayo onyeshwa na Zack,,, punde si punde,,, simu ya Shamy ikaita,akaacha kuendelea kutazama kule anapoonyeshwa na Zack.. akaitazama simu yake kisha akaipokea..simu hiyo ilikuwa inatokea Muhimbili.

    Shamy akaambiwa kuwa kunadharura, hivyo anahitajika Hospitali haraka kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo w mgonjwa aliyekuwa mahututi,, akageuza gari lake huku akimwambia Zack,, nahitajika kazini haraka iwezekanavyo..Zack hakuwa na kipingamizi!

    akabaki kimya,, Shamy akaliendesha gari lake kwa kasi kuelekea Muhimbili.



    walipofika Shamy akambusu shavuni Zack kisha akasema,, "samahani kipenzi naomba unisubiri hapa kwa dakika kadhaa wacha nikawajibike!  Zack akasema sawa mpenzi utanikuta... Shamy akashuka kutoka ndani ya gari,,,akazipiga hatua za haraka haraka. kuingia ndani ya jengo la hospitali..... wakati anazipiga hatua kuelekea kwenye chumba cha upasuaji akastaajabu kukutana na shangazi yake kwenye korido..akiwa kaongozana na mumewe akizipiga hatua za taratibu kupita kiasi kwa sababu alikuwa kapooza upande mmoja!  Shamy akawasalimia kisha akasema,, nilikuwa nije kukutembelea nyumbani kwako,,kumbe tungepishana?  hata hivyo niliishia njiani baada ya kupigiwa simu kuwa nahitajika kazini,, Shangazi yake akasema,, "kumbe unafanya kazi hapa?? hongera sana mwanangu!!  Mungubakutangulie kwenye kazi yako.. ghafla simu ya Shamy ikaita alipoitazama ilikuwa ni daktari mwenzake anampigia.. Shamy akamwambia shangazi yake,, "tutawasiliana,,  aliongea maneno hayo huku akazipiga hatua za haraka haraka kuufuata mlango wa chumba cha upasuaji!



    wakati huo huo kule nje ya hospitali alionekana Zack akiwa bado yumo ndani ya gari,, akimsubiri Shamy amalize kazi iliyomleta kisha waondoke... alipoangaza angaza macho yake akamuona Shangazi yake akiwa na mumewe!! akashuka kutoka ndani ya gari akawafuata.

    alipowakaribia akauliza,, "kulikoni nani mgonjwa?  Shangazi yake akajibu.. nilikuja kwenye mazoezi maalumu,, pia kunadawa nilikuja kuchukua....pia nimemuona dada yako,,ni daktari wa hospitali hii...

    Zack akasema,, "itabidi unipe namba zake za simu kama unazo"

    Shangazi yake akachukua simu yake ili ampe namba za simu za dada yake! alipobofya simu yake,, akagundua kuwa imezimika,, akasema,, "ooh kumbe simu imezimika chaji.. nitakutumia kwenye ujumbe wa maneno(sms) Zack akasema hakuna shaka,,pia mchumba wangu ni dakatari katika hospitali hii..

    kabla hajamalizia sentensi.... kwa mbali akamuona Shamy anakuja akitokea ndani ya jengo hospitali akija ulande wao.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati Shamy anazipiga hatua,,, simu yake ikaita,, akaipokea akaambiwa kuwa arudi kusaini(signature) ili alipe malipo ya ziada kwa ajili amefanya kazi wakati ni siku ya kupumzika!  Shamy akaamua kurudi ndani ya jengo la hospitali,,, akasaini.. kisha akazipiga hatua kuelekea kwenye ofisi ya muhasibu wa hospitali hiyo.. akapewa pesa.. kShamy hakutaka kupoteza muda,,akazipiga hatua kutoka  nje ya jengo la hospitali hiyo! kumbe wakati Shamy yupo kwenye ofisi ya muhasibu,, ndio wakati shangazi yake alikuwa anaagana na Zack kule nje. kisha akaingia ndani ya gari akiongozwa na mumewe.. wakaondoka kuelekea nyumbani!

    Shamy alipofika nje kabisa ya Jengo hilo,,akazipiga hatua za taratibu kulifuata gari lake kule alipoliegesha! akafungua mlango akaingia ndani ya gari.. akasema,, "samahani mpenzi kwa kuchelewa.

    Zack akajibu,, "usijali mpenzi mimi nipo kwa ajili yako! alafu umechelewa kidogo nimekutana na shangazi yangu dakika chache zilizopita!

    Shamy akasema,,"hata mimi pia nimekutana na shangazi yangu,wakati naingia kwenye chumba cha upasuaji!  lakini hatujaongea sana nilikuwa namuwahi mgonjwa.. kumbe tungeenda nyujmbani kwake muda ule tusingemkuta,, tungepishana.

    lakini usijali mpenzi tutakwenda siku nyingine.

    Shamy aliongea maneno hayo huku akiliwasha gari lake,, na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza...

    baada ya lisaa limoja kupita wakawa wamefika Mbezi.. Shamy akaliongoza gari lake mpaka nyumbani..



                           **********************************************



    Siku zilizidi kusonga na Maisha yakaendelea biashara ya Zack ilizidi kukua siku hadi siku akafungua duka la pili,,duka hilo likawa kubwa mara tatu ya lile la kwanza, Zack akawa ana muda mchache wa kupumzika na mchumba wake(busy). Kitendo hicho kilimfanya Shamy aanze kuhisi huenda Zack kapata mwanamke mwingine hivyo anamsaliti, siku moja Shamy akaamua kumuuliza Zack kwanini umebadilika? Zack akajibu, "hivyo unisikiliavyo sivyo ni msongo wa kazi wataki mwingine narudi nyubani usiku sana ,Shamy akakubali kishingo upade lakini bado akawa na wasi wasi kuhusu Zack.

    kadri siku zilivyozidi kusonga,,,mapenzi yao yalizidi kukuwa.. pia bihashara ya Zack ikazidi kuongeza kilato kadri siku zilivyozidi kusonga.. hatimae akaacha kuagiza mizigo,akawa anasafiri mwenyewe kwenda China na Dubai kufata bidhaa za kuuza kwenye maduka yake!

    Siku moja Zack alisafiri kwenda China, kufata bidhaa,, baada ya wiki moja,,akaunganisha safari akaelekea Dubai!



    siku aliyoondoka Zack kwenda China.. Usikubwa siku hiyo Shamy alipigiwa simu kuwa Shangazi yake ni mgonjwa mahututi.. kalazwa hospitali ya rufaa Muhimbili.. Shamy akawasha gari lake haraka akaelekea Muhimbili.. alipofika akawa amechelewa akakuta shangazi yake ameshakufa! Shamy akaangua kilio kwa uchungu wa hali ya juu.. akajitahidi kumpigia simu Zack ili ampe taarifa.. lakini Zack a

    akawa hapatikani kwenye simu! 

    Taratibu za mazishi zikafanyika wakazika kesho yake...

    Baada ya wiki moja kupita Zack akarejea nchini Tanzania..,,,alipofika nyumbani,, Shamy akampa taarifa kuwa shangazi yake amefariki, wiki iliyopita na tayari walishazika!

    Zack alisikitika sana akampa pole mchumba wake! 

    Zack alikuwa kamletea zawadi Shamy,, simu pamoja na viatu.. Shamy akafurahi sana.

    miongoni mwa zawadi alizoleta pia zilikuwemo zawadi za shnangazi yake....

    kesho yake akazichukua zawadi hizo ili ampelekee sahangazi yake kule kigamboni!

    alipofika akastaajabu kuambiwa kuwa shangazi yake amefariki, wiki moja iliyopita!  akasikitika sana,, akalia kwa uchungu! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akampogia simu Shamy, akamwambia,, "shangazi yangu pia kafariki,, wiki moja sasa imepita,, Shamy akampa pole mchumba wake,,kwa kumwambia maneno ya kumfariji!



    siku zilizidi kusonga... safari za Zack kwenda nje ya nchi.. zikazidi!  kitendo hicho kilimnyima Shamy furaha!  wakati mwingine akawa anahisi kuwa Zack atakuwa na mwanamke mwingine!



    Siku moja Shamy akiwa kazini,,, akaingia daktari mkuu, kwenye ofisi ya Shamy,, dakatari huyo,, mwenye umri wa makamo kiasi akaanza kumtongoza Shamy kwa kumrubuni kuwa atampandisha cheo.... Shamy akakataa kata kata akisema,, "mimi tayari ninamchumba,, tunatarajia kuoana hivi karibuni.. Daktari mkuu,, akaondoka huku akimwambia,,naomba uendelee kutafakari najua nimekushtukiza ndio maana unashindwa kunila jibu sahihi..

    Shamy akabaki na maswali mengi kupita kiasi,, akaanza kukumbuka matukio ya mchumba wake(Zack) zile safari za mara kwa mara tena za kushtukiza...pia hata akirudi nyumbani analala anasema amechoka!  Shamy akajisemea moyoni,, "wacha nifanye uchunguzi ili nibaini ni nani anayemchanganya mchumba wangu mpaka anashindwa kunipa haki yangu ya chumbani ipasavyo!

    Shamy aliporudi nyumbani akaandaa chakula cha usiku kisha akamkaribisha Zack,, wakaanza kula chakula... walipomaliza wakaenda kuoga kisha wakapanda kitandani.. shami akaanza kumdadisi Zack kwa kumuuliza maswali,, Zaki akaishia kusema hayo unayoniwazia hakuna hata mojawapo lenye chembe ya ukweli ndani yake,, mimi siwezi kukusaliti nakulenda sana,,, tatizo ni wingi wa majukumu ya kazi... Shamybakabaki kimya bola kuuliza swali lingine!  baada ya nusu saa kupita Zack akasinzia kabisa.. Shamy akanyanyuka kitandani akachukua simu ya Zack akaanza kukagua.. lakini hakupata ushahidi wowote.. punde si punde ukaingia ujumbe mfupi wa maneno(sms) ni mwanamke alikuwa amemtumia ujumbe huo Zack.. alipousoma.. akastaajabu ulikuwa ni ujumbe wa mapenzi!  akajisemea moyoni!  siamini hili ninachokiona! akaamua kuichukua namba hiyo akapiga simu kwa kutumia simu ya Zack... kumbe aliyetuma ujumbe huo alikuwa kakosea namba.. alikuwa anamtumia mtu mwingine!!  Shamy akakubali lakini akawa bado na wasiwasi kuhusu mwanamke huyo!

    Shamy akaitazama namba hiyo lakini hakuiona katika orodha ya namba zilizohifadhiwa kwenye simu ya Zack!

    akaamua kulala,,

    asubuhi palipokucha akaenda kazini,, akiwa ndani ya ofisi yake, daktari mkuu akaingia ofisini kwake.. kisha akaketi akamwambia Shamy kuwa anahitaji wale chakula cha mchana pamoja!

    Shamy akasema,, "bila shaka kama ni chakula usijali.

    Daktari mkuu akatabasamu kisha akafungua mlango na kuelekea kwenye ofisi yake.



    ilipofika mida ya saa saba za mchana Daktari mkuu akaongozana na Shamy mpaka ndani ya gari lake,, akaliwasha wakaelekea LEGENCY HOTEL kwa ajili ya kupata chakula cha mchana!  walipofika,,Daktari mkuu aitwae SHIRIMA akachukua begi dogo la plastiki(breefcase) akashuka kutoka ndani ya gari huku kalibebelea begi hilo... akaongozana na Shamy mpaka kwenye viti, kisha wakaagiza chakula cha aina moja!

    kabla chakula hakijaletwa.. Shirima akaanza kusimulia historia ya maisha yake!

    akasema,, "miaka ishirini na nane (28) iliyopita.. nilikuwa dereva wa daktari mkuu huko mwanza kwenye hospitali ya BUGANDO,, lakini mke wake alitokea kunolenda sana.. mimi nilikataa lakini alinilazimisha kisha akanitishia kuwa endapo nikiendelea kumkatalia atamwambia mumewe kuwa mimi ndiye nimemtongoza nivyo atanisimamisha kazi.. wakati huo nilikuwa kijana mdogo.. nikalazimika kukubali ili kulinda kazi yangu... sikumoja Daktari huyo alisafiri,,

    mkewe akaniita nymbani kwake... akanishawishi hatimae tukashirikiana kimwili... kumbe ndani ya chumba hicho kulikuwa na kamera(UCCTV) zikarekodi tukio zima... kamera hizo zilitegeshwa na mumewe kwa siri pasipo mke wake kujua...siku hiyo akapata ujauzito,,,

    Daktari huyo aliporudi akaona tukio zima kupitia video iliyorekodiwa na kamera hizo.. akaamua kumfukuza mkewe.. kiwha akasema ataniuwa... mimi nimatoroka na kukimbilia Kenya.. nikaishi huko kwa miaka mingi sana.... Shirima akasitisha kuongea kisha akafungua lile begi dogo la plastiki (breefcase)

    akatoa picha akamuonyesha Shamy, kisha akasema,, "hii ni picha ya mwanamke huyo na sijui yuko wapi? pia huyo mtoto wangu sijawahi kuiona hata sura yake Shamy akaitazama picha hiyo,, kisha akasema,, "pole sana kwa mkasa uliokupata.. hii ni kati ya sehemu ya maisha ya binadamu..

    kisha akaiweka picha hiyo juu ya meza,,, punde si punde chakula kikaletwa wakaanza kula huku wakibadilisha mawazo! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    walipomaliza kula,, Shamy akanyanyuka akasema,,"nisubiri kwa dakika kadhaa narejea..

    Shirima akauliza,, "unakwenda wapi Shamy akasema naenda chooni, aliongea hivyo huku macho yake yakionekana kuwa na aibu.

    Shirima akasema utanikuta ndani ya gari turudi kazini.

    Sahamy akazipiga hatua kuelekea chooni!

    Shirima akachukua begi lake akazipiga hatua kuelekea kwenye gari lake akaingia ndani ya gari akawa anamsubiri Shamy!

    baada ya dakika mbili kupita Shamy akarejea akastaajabu kuikuta ile picha bado ipo juu ya meza! kumbe Shirima aliisahau.. Shamy akaichukua na kuiweka ndani ya mkoba wake kisha akazipiga hatua kulifuata gari la Shirima.. akafungua mlango na kuingia ndani ya gari... Shirima akawa anaongea mfululizo mpaka Shamy akasahau kumpa Shirima ile picha..

    walipofika Muhimbili.. Shamy akashuka kutoka ndani ya gari kisha akalifuata gari lake.. na kuliwasha akaelekea nyumbani!

    alipofika akajilaza kitandani.. alipodamka ilikuwa ni majira ya saa moja za jioni.. akaandaa chakula cha usiku.. punde si punde Zack akarejea nyumbani!

    alipofika akamsalimia mchumba wake kwa furaha kisha akaingia chumbani... akakuta simu ya Shamy inaita ndani ya mkoba! akapaza sauti,, "SIMU YAKO INAITA.

    Shamy akasema,, "samahani kipenzi naomba uniletee,,, nitaunguza mboga opo jikoni..

    Zack akafungua mkoba akatoa simu!  akaona kunapicha akaichukua picha hiyo.. alipoitazama,, macho yakamtoka akashtuka kuona picha ya mama yake ipo ndani ya mkoba wa shamy!







    akajiulizaaswali mengi yasiyokuwa na majibu!! akazipiga hatua kulifuata begi lake,, akalifungua akazitoa picha za mama yake,, akazitazama kwa muda mrefu kiasi,,kisha akaitazama ile picha ya mama yake aliyoikuta kwenye mkoba wa Shamy!  akatabasamu kisha akajisemea moyoni,, "sasa mbona kaichagua picha hii!? bila shaka kaipenda kuliko picha hizi zote!  Zack akahisi huenda shami alofungua begi lake akatoa picha hiyo,, hakujua kuwa Shamy kaitoa wapi picha hiyo,, punde si punde simu  ya Shamy ikaita tena,, Zack akajisahau kuirudisha picha ile ndani ya mkoba wa Shamy akaichanganya kwenye picha nyingine za mama yake na kuzirudisha ndani ya begi lake!  kisha akalifunga na kuzipiga hatua kuufuata mlango akaufungua na kutoka chumbani akaelekea kule jikoni alipokuwepo Shamy,, akamkabidhi Shamy simu yake.. kisha yeye akaelekea sebuleni,, akawasha Runinga na kuanza mutazama vipindi!  ya kwenye Runinga.



    Baada ya lisaa limoja kupita Shamy alimaliza kuandaa chakula akakiweka kwenye meza ya chakula.. akamkaribisha Zack wakaanza kula...

    Zack hakuuliza kotu fhoxhote kuhusu ile picha kwa sababu aliamini Shamy hakuichukua kwa lengo baya!



    Siku zilizidi kusonga,, lakini simu Shamy ikawa inaita mara kwa mara,, tena ni namba moja pekee iliyokuwa ikimpigia mara nyingi, hata nyakati za usiku wakati Zack na Shamy wamepumzika!!! Zack akaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu namba hiyo lakini hakumwambia Shamy kitu chochote,, akawa anafanya uchunguzi kudadisi mawasiliano ha Shamy na pamoja na hiyo namba inayompogia mara kwa mara!

    Siku moja nyakati za usiku,, wakati Shamy yumo bafuni anaoga, ghafla ukaingia ujumbe mfupi wa maneno, kwenye simu ya Shamy! 

    Zack akaangaza macho yake ili aone kama Shamy anashuhudia anachotaka kukifanya.

    akaona hakuna dalili zozote za Shamy,, kuja muda huo kutokea bafuni.

    akaufungua ujumbe huo,, alipousoma akashtuka!  ujumbe huo ulisomeka hivi;  habari ya usiku huu!  nimekukumbuka,, na nomefurahi sana mchan wa leo tulivyokuwa pamoja!  pia nakutakia usiku mwema,, ewe mwanamke nikupendae!

    Zack akahisi kuishiwa nguvu,, jasho likamtoka! akajisemea moyoni,, " Shamy ananisaliti?  kosa langu ni lipi?  je!?  huyu ni nani anayetaka kuvuruga uchumba wangu mimi na Shamy? Zack akaamua kuufuta ujumbe huo Shamy asiuone..

    Shamy alipotoka bafuni akapanda kitandani,,lakini akamuona Zack akionekana hana furaha,akauliza,,"Mbona kama unamawazo!  nini kinakutatiza?

    Zack akaqmua kudanganya kwa kusema hakuna kitu,, nahisi uchovu tu.

    Shamy akazima taa wakaanza kuutafuta usingizi!



                            ********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zilizidi kusonga,,Shirima hakuacha kumsumbua Shamy,, kwa kuendelea kumchombeza maneno ya kimapenzi kila siku!

    Shirima akaamua kumbadilishia Shamy muda wa kufanya kazi,,akamuweka kwenye orodha ya madaktari wa zamu ya usiku (night shift) ..Shamy hakuwa na kipingamizi kwa sababu Mkuu wake wa kazi! 

    Shirima aliamja kufanya hivyo kwa lengo moja tu,, aweze kuwa na Shamy muda mwingi,, huenda Shamy akashawishika na kumkubalia!

    kitendo hicho kilimfanya Zack awe mnyonge sana,, akikumbuka na ule ujumbe mfupi wa maneno(sms) aliyouona kwenye simu Shamy,, anakuwa mnyonge kabisa..

    Sikumoja Zack akaomba ushauri kwa rafiki yake kipenzi,, akamueleza yote aliyoyasnhuhudia..

    Rafiki yake huyo akamshauri kuwa aende kwa mganga,, Zack akashawishika akaona ni ushauri mzuri na unafaa!

    Zack akamuaga rafiki yake kisha akaingia ndani ya gari na kurudi nyumbani.

    akiwa njiani,,wazo likamjia,,akajisemea moyoni,, "kwa nini nisimuangamize kabisa huyo kinyago anayetaka kuingilia mapenzi yangu!



                   *******************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog