Search This Blog

MOCHWARI - 2

 







    Simulizi : Mochwari

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya mochwari alionekana Kagaruki akizipiga hatua huku macho yake yakiangaza huku na kule!  akaifikia meza ya kuoshea maiti akauchukua ufunguo haraka,,akaangaza mocho yake huku na kule hakuona ile maiti iliyofufuka!!  akatimua mbio kuufuata mlango! akachomeka ufunguo haraka akafungua,, kumbe kakosea! sio ufunguo sahihi, hivyo akauchomoa na kuchomeka ufunguo mwingine!  pia haukuwa funguo sahihi,, kutokana na hofu na uwoga aliokuwa nao,, hakuweza kuutambua ufungu sahihi wa kufungua mlango huo!

    akaanza kulia huku akiendelea kubadilisha badilisha funguo ili aupate ufunguo sahihi!

    hatimae akaufikia ufunguo wa mwisho kati ya funguo hizo zilizowekwa kwenye sehemu moja! akauchomeka haraka haraka,, kabla hajafungua akaisika sauti ya vishindo vya mtu akitembea nyuma yake!  akageuza shingo yake kutazama akashtuka kuiona ile maiti ikizipiga hatua kuja pale mlangoni! Kagaruki akajaribu kufungua kwanguvu ghafla ufunguo ukakatika!  akabaki na kipande,, huku kipande kingine kikiwa ndani ya tundu la ufunguo! Kagaruki akageuza shingo yake kutazama kule alipoiona maiti hiyo ikizioiga hatua kuja pale mlangoni.. akashtuka kuona maiti nyingine zikifungua milango ya majokofu na kutoka kwenye majokofu!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maiti hizo zilitoka mfululizo,, Kagaruki akaanza kupiga kelele,, wazo likajia akachukua mtungi wa gesi maalumu ya kuzima moto,,,akapiga mlango huo kwa nguvu pale kwenye kitasa,,,  mlango ukafunguka,, Kagaruki akatimua mbio huku akipiga kelele!

    alichanganyikiwa akasahau mlango wa kutokea nje ya hospitali uko wapi,, akayimua mbio kusonga juu zaidi ya hospitali hiyo,, manesi pamoja na madaktari wakastaajabu sana,, kumuona Kagaruki anatimua mbio huku macho yake yakionyesha kuwa na wasiwasi wa hali ya juu,,,



    Kule ndani ya Mochwari,, maiti ziliendelea kutoka kwenye majokofu... maiti hizo zikaanza kutoka nje kabisa ya chumba cha mochwari,,

    kwa mbali alionekana nes mmoja akizipiga hatua kuufuata mlango wa ngazi ya umeme(Lift) alipoukaribia mlango huo,, akaona lift ipo juu kwenye ghorofa ya sita(6)

    akaamua kusimama hapo nje kuisubiri ishuke chini,,

    punde si punde akahisi kama kunakitu kinatembe nyuma yake huku kikikoroma! akageuza shingo yake akatazama, akapiga kelele kuona kundi kubwa la maiti likija upande wake,, akapiga kelele,, lakini hakupata msaada,, maiti moja ikamnasa,,na kuchumbukuza vidole vyake kwenye macho ya nesi huyo ,,macho yakanyofoka,,kisha lile kundi la maiti likaanza kunyofoa viungo vya mwili wa nesi huyo na kumla nyama!

    punde si punde lift,, ikafika na mlango ukafunguka kulikuwa na nesi aliyekuwa anampeleka mgojwa kwenye chumba cha upasuaji,, mgonjwa huyo alikuwa kaketi kwenye kiti cha magurudumu huku akiwa hoi,, Baadhi ya maiti zikaingia ndani ya lifti, nesi akaanza kupiga kelele kwa hofu,,

    yule mgonjwa akapata mshtuko akafa papohapo,,mlango wa lift ukajifunga,, baadhi ya maiti zikabaki upande wa chini zikiranda randa na kutapakaa kila kona,

    zile baadhi ya maiti zilizoingia ndani ya lift hiyo zikaanza kumla nyama nesi huyo pamoja na yule mgonjwa aliyekata roho muda huohuo.



    Upande mwingine,,, walionekqna wanafunzi watano,, wa chuo cha utabibu.. kilichomo ndani ya hospitali hiyo,, waki, ipiga hatua kuufuata mlango wa lift... wakaona lifi ikiwa inatokea chini kuja upande wa juu,, mmoja kati ya wanafunzi hao akabofya kitufe, cha kuisimamisha lifti hiyo, endapo itafika kwenye hiyo ghorofa ya saba(7)

    wakaendelea kupiga stori huku wakicheka,,punde si punde mlqngo wa lift ukafunguka,,, macho ya kawatoka baada ya kuona maiti,, zimefufuka,, huku damu zimetapakaa ndani ya lifti, wanafunzi hao wakatimua mbio,,kila mmoja alipita njia yake huku wakipiga kelele,,

    kelele za wanafunzi hao ziliwashtua wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodini.. pamoja na manesi waliokuwa eneo hilo,, baadhi ya wagonjwa waliokuwa wanajiweza angalau kutembea,, wakatoka wodini na kuchungulia waone nini kinaendelea!  wakashtuka kuona maiti zikipiga hatua kutokea ndani ya lift,, huku midomo yao ikionekana kuzungukwa na damu!  maiti hizo zikaingia kwenye wodi,, na kuanza kufanya mauwaji ya kikatiri,,, kwa wagonjwa waliokuwemo ndani ya wodi hiyo!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                            ************************************



    Upande mwingine alionekana Kagaruki akiwa ndani ya ofisi moja ya manesi,, akiwasimulia kile alichokiona kule mochwari,,manesi wakastaajabu sana wakaanza kuingiwa na hofu,, kabla Kagaruki hajamaliza kusimulia,,zikasikika kelele za watu wakipiga moyowe ya kuomba msaada,, Kagaruki akasema,, tayari kimeshanuka huko,,tukimbieni,, Kagaruki akachomoza kichwa chake akachungulia akaona hali ya utulivu imetawala eneo hilo,,, akatimua mbio kuzifuata ngazi akaanza kushuka kuelekea upande wa chini.......



    wakati huo huo,, kule chini,, lilionekana lile kundi kubwa la maiti zilizofufuka kutokea kule mochwari. maiti hizo zilitembea kwa makundi makundi,,, likaonekana kundi moja likiingia ndani ya wodi ya uzazi,,wodi hiyo ni maalumu kwa wakinamama wajawazito na waliojifungua,,, kinamama hao wakaanza kupiga kelele,,,

    akaonekana mama mmoja kwenye kitanda cha mwisho akiwa anahangaika kwa uchungu,, akitarajia kujifungua muda mchache ujao!! 

    kundi hilo la maiti likaanza kufanya mauwaji,, kwa kinamama hao,,

    maiti moja ikamfuata mtoto mchanga aliyezaliwa masaa machache yaliyopita,, akamshika mtoto huyo akanyofoa kichwa na kuanza kumtafuna,,,

    maiti nyingine zikamfuata yule mama aleyekuwa anaumwa uchungu wa kujifungua,, mama huyo akajaribu kukimbia lakini alishindwa akadondoka chini,,, maiti moja ikamnasa,, ikatoboa tumbo la mama huyo na kutumbukiza mkono ndani ya tumbo akamnyofoa mtoto na kuanza kumtafuna huku maiti nyingine zikiendelea kunyofoa viungo vya mwili wa mama huyo na kuvitafuna...

    ndani ya dakika chache,, hakuna mtu aliyebaki hai ndani ya wodi hiyo,, na ukimya ukatawala..



                    *****************************************



    Upande mwingine alionekana Kagaruki akiendelea kushuka kwenye ngazi akielekea upande wa chini,, alipofika chini kabisa,, akashtuka kuona damu zimetapakaa kwenye sakafu,, akaingiwa na uwoga akatimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea!!  ghafla akakutana na kundi kubwa la maiti likiwa mbele yake,, alipogeza shingo yake akaona kundi lingine la maiti likija upande huo huo akawa katikati kazungukwa  kila upande!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kagaruki akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.. kundi hilo la maiti likaanza kumfuata pale alipokuwa amesimama! Kagaruki akaamua kutimua mbio akarudi kule juu ya hospitali akizipanda ngazi kwa kasi kama vile anashuka,



    Wakati huo huo kule nje ya hospitali hakuna aliyejua kinachoendelea ndani ya hospitali hiyo,,,

    masaa yalizidi kusonga,, hatimae giza likatanda!! mpaka muda huu haluna aliyefanikiwa kutoka ndani ya jengo la hospitali,, wala hakuna aliyeingia akafanikiwa kutoka... kelele zilizidi kusikika mfululizo!

    walinzi wahospitali hiyo waliamini huenda kelele hizo zinatokea kwenye wodi ya vichaa(C1)



    kule ndani ya hospitali bado hali ilizidi kuwa tete,, wagonjwa wengi walikufa kwa kutopatiwa matibabu kwa wakati,, wengine walikufa kwa mshtuko wa moyo,, mati hizo ziliendelea kurandaranda ndani ya hosptitali hiyo,, zilitapakaa sehemu zote..

    kwa mbali akaonekana Kagaruki akiingia ndani ya wodi moja iliyokuwa wazi,  akajifungia huku akirundika vidatanda mlangoni kwa kuvigusanisha! jasho lilimtoka mfululizo,, uwoga uliendelea kutawala juu yake...kumbe ndani ya chumba hicho kulikuwa na maiti tano(5) kati ya maiti zilizofufujka kule mochwari... miongoni mwa maitihizo ilikuwemo maiti ya yule mwanamke wa kiarabu... Kagaruki akahisi vishindo vya miguu vikitokea nyuma yake,, akageuza shingo yake,, hakuamini alichokiona! akaona maiti hizo tano zinaliga hatua kumfuata..

    Kagaruki akautazama mlango,, vitanda vilikuwa vimejaa pale mlangoni!  akajilaumu huku akivitoa kwa kuvisukumq haraka haraka. akafanikiwa kuvitoa vitanda vyote akafungua mlango haraka akatoka nje ya wodi hiyo akatimua mbio pasipokujua ni wapi anakoelekea!  Sasahivi ukimya ulitawala ndani ya hospitali hiyo, haikusikika hata sauti ya wadudu waliao usiku.

    Kagaruki akaamua kukifuata chumba cha ofisi ya madaktari..alipojaribu kufungua mlango akaona mlango umefungwa kwa ndani... wasi wasi ukazidi kuongezeka kila akijaribu kufungua milango ya wodi haikufunguka ilikuwa imefungwa kwa ndani.. akajikuta yeye peke yake yupo nje,, akaamua kutimua mbio kuelekea juu zaidi ghorofa ya mwisho. alipofika akavunja mlango akatokezea juu ya jengo hilo,,,



    kule nje ya hospitali,, walinzi wakaanza kuingiwa na wasiwasi,, hakuna hata daktari au nesi aliyekuja kusaini kutoka kazini... mlinzi mmoja akasema,, yawezekana leo kunakikao cha wafanyakazi wote wa hospitali hii,, yani mpaka sasahivi hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyetoka tangu walipoingia asubuhi! punde si punde ikasikika simu ikiita,, simu hiyo ilitokea ndani ya hospitali... mlinzi akaipokea simu hiyo... akastaajabu kusikia sauti ya nesi akionge kwa uwoga mpaka maneno yakawa hayasikiki vizuri! mlinzi huyo akauliza nini kimetokea mbona unaongea hivyo!??

    kabla hajamalizia kuongea sentensi,, ikasikika kelele ya nesi huyo,,simu ikabaki hewani.. mlinzi akawa anasikia sauti kama mtu anakula au anatafuna chakula kwa pupa,,mlinzi huyo akaamua kukata simu hiyo kisha akapiga tena kwenye namba hiyo, lakini simu iliita bila kupokelewa! mlinzi akaamua kuzipiga hatua kulifuata jengo la hospitali... alitembea harakaharaka nusu akimbie... akaingia ndani ya hospitali hiyo akaelekea kwenye gazi ya umeme(lift) akabofya kitufe cha kufungulia mlango... punde si punde mlango ukafunguka,, macho yakamtoka akaingiwa na hofu baada ya kuona damu nyingi zimetapakaa ndani ya lifti hiyo.. pia maiti za manes wawi pamoja na mgonjwa zikiwa hazina baadhi ya viungo.. matiti utumbo na viungo vyote vilivyomo ndani ya tumbo,, akageuka ili atimue mbio,, akakutana uso kwa uso na maiti moja imesimama nyuma yake!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo kule juu ya jengo hilo,alionekana Kagaruki akijaumu sana akasema,, "mimi ndiye chanzo cha haya yote,, tazama watu wasiokuwa na hatia wanaangamia pasipo kosa lolote,, alijisemea maneno hayo huku machozi yakimtoka... punde si punde akaona maiti moja inakuja upande huo,, kisha maiti zikaja mfululizo huku zimeongozana hatimae likawa kundi kubwa kiasi,,maiti hizo zikaanza kumfuata Kagaruki.!

    Kagaruki akaingiwa na uwoga wa hali ya juu,, akajikuta anacheka badala ya kulia.. akajisemea moyoni,, "ni bora nijirushe kutoka huku juu nife.. kuliko kuliwa nyama hivi hivi najiona..

    Maiti hizo zilizidi kusogea hatimae zikamkaribia,,akajirusha gorofani... kumbe wakati anajirusha alikuwa amekanyaga waya wa umeme waya huo ukajiviringisha kwenye mguu mmoja wa Kagaruki,, hivyo akabaki kaning'inia kichwa chini miguu juu! 





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog