Simulizi : Roho Ya Giza
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jasho likamtoka mfululizo hofu ikazidi kuongezeka juu yake,,akazipiga hatua za uwoga kurudi nyuma,,,punde si punde ikasikika sauti ya roho ya giza ikimwambia safi umefanya kazi nzuri,,,usiogope wala usikimbie,,sauti hiyo ilisikika ikijirudia rudia kwenye masikio ya Fundikira ,,,akaufungua mlango na kutimua mbio kutoka ndani ya chumba hicho,,mtoto wa Fundikira aliendea kuzipiga hatua kuufuata mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho...akaikanyaga biblia,punde si punde ukazuka moto mkali,,ukaanza kumuunguza mtoto huyo,,akapiga kelele lakini sauti ya mtoto huyo ilikuwa inatisha, punde si punde akaonekana kiumbe wa ajabu akitokea ndani ya mwili wa mtoto huyo,,kiumbe huyo alikuwa na vichwa tisa na mikono tisa...akatoweka kimiujiza !!
mtoto wa Fundikira akanyanyuka na kujishangaa,,,
**************************
kule sebuleni alionekana Fundikira akiwa anataka kutoka nje ya mlango,,,ikasikika sauti ya mtoto wake ikiita kutokea kule chumbani,,Fundikira akasita kutoka nje ya nyumba yake,, akajisemea moyoni,, "mbona sielewi,, hivi hiyo ni sauti ya mtoto wangu!!?
akazipiga tua kukifuata chumba chake huku macho yake yakitazama kwa tahadhari... akaingia ndani ya chumba chake akamkuta mtoto wake kasimama kando ya kitanda!
alipoangaza angaza macho yake akaona ile biblia iko chini akaichukua haraka kisha akamsogelea mtoto wake huku akimtazama kwa macho ya mshangao!
Baada ya dakika kadhaa kupita,, Fundikira akaanza kusali kwa imani!! akimuomba Mungu amlinde yeye na familia yake,,
***********************
Upande mwingine alionekana Lucifer,,, akiwa kule kumzimu,,, akamuita kiongozi mkuu muwakilishi wa wafuasi wake duniani!! akasema,,,huyu mtu ni tatizo,, na kama akiendelea kubaki hai,, tutapoteza wanachama,, sass basi natoa amri,, lazima auwawe na endapo itashindikana basi uhai wako ni halali yangu! kiongozi mkuu akatii amri ya Lucifer akatoweka kimiujiza kurudi duniani!
****************************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine alionekana mke wa Fundikira akiendelea kutimua mbio pasipokujua ni wapi anaelekea, alikimbia umbali,giza lilikuwa totoro,,,akajikuta anatumbukia ndani ya shimo lililokuwa wazi,,shimo hilo lilikuwa refu na maji yenye kina kirefu kiasi,,, akapiga kelele kuomba msaada lakini hapakuwa na mtu yeyote eneo hilo,,, akajitahidi kufanya jitihada za kuokoa uhai wake,, punde si punde akahisi ameshikwa mguu wake mmoja anavutwa kuelekea chini ya maji hayo!
hofu ikazidi kuongezeka,, akaanza kupiga kelele,, wazo likamjia kuwa asali kwa imani,, bila kuchelewa akaanza kumtaja Mungu bila kuchoka huku akisali,, mara ghafla akahisi kaachiliwa mguu wake...
Upande mwingine alione manaume mmoja akiwa anaendesha pikipiki akapita kwenye lile eneo ambalo,,lipo lile shimo alilodumbukia mke wa Fundikira
akasikia sauti ya mwanamke akipiga kelele za kuomba msaada,, mwanaume huyo akaingiwa na roho ya huruma akaamua kusimamisha pikipiki yake,, akashuka na lil fuata shimo hilo! akamulika kwa kutumia tochi ya simu yake! akamuona mwanamke yumo ndani ya shimo hilo!
akasema,, "ondoa wasiwasi dada yangu.. wacha niangalie uwezekano wa kukutoa ndani ya shimo hili..
*********************
Kule nyumbani kwa Fundikira alionekana akimaliza. kusali... kisha akamsogelea mtoto wake na kumkumbatia.... ghafla wazo likamjia kuwa mkewe alikimbia,, akajisemea moyoni,, "sijui yuhali gani huko aliko!!? wacha nikamtafute usiku huu huu asije kupatwa na tatizo!!! Fundikira akamlaza mtot wake kitandani.. alipohakikisha kuwa kalala usingizi.. akatoka nje ya nyumba yake kwenda kumtafuta mkewe.. huko. mitaani.
wakati huo huo kule katika lile eneo alilokuwepo mke wa Fundikira alionekana mwanaume huyo akitafakari jinsi ya kumsaidia mwanamke huyo kumtoa ndani ya shimo hilo... akakumbuka kuwa nyuma ya kiti cha pikipiki yake,,, kuna kamba ndefu ambazo alizinunu mchana wa leo kwa ajili ya mifugo yake kadhaa kule nyumbani kwake....akachukua kamba hizo akaziunganisha kwa kuzifunga... ikapatikana kamba moja yenye urefu wa kutosha kufika ndani kabisa ya shimo hilo...
mke wa Fundikira akaishika kamba hiyo na kujifunga kiunoni,,, pia akaishikilia kwa nguvu.. yule mwanaume akaifunga kamba hiyo kwenye mti uliokuwa kando ya shimo hilo akaanza kuvuta kamba huku mke wa Fundikira akikanyaga kingo za shimo hilo... hatimae akafanikiwa kutoka ndani ya shimo hilo,,, punde si punde akajitokeza yule kiongozi mkuu muwakilishi wa wafuasi wa Lucifer hapa duniani... CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakuna aliyeweza kumuona kwa macho ya kawaida!! akagusa kichwa cha mwanaume huyo... ghafla akili ya mwanaume huyo ikabadilika,,, akaingiwa na roho ya kikatiri.. akasimama haraka kisha akamtazama mke wa Fundikira kwa macho ya msisitizo kufanya jambo fulani..akazipiga hatua kadhaa akaifungua ile kamba pale kwenye mti,, akaifunga kitanzi akaishikilia kikakamavu.. . kisha akazipiga hatua kumfuata mke wa Fundikira!!
mke wa Fundikira akaingiwa na hofu kupita kiasi,, akaona kuwa mtu huyo hana nia nzuri,, mtu huyo alipomkaribia mke wa Fundikira akamnasa na kumfunga kamba shingoni na kuanza kumnyonga!
wakati huo huo Fundikira katika pitapita zake kumtafuta mkewe akawa amefika eneo hilo akasikia sauti ya mwanamke akikoroma,,, aliposikiliza kwa makini sauti hiyo akahisi kuwa mwanamke huyo anahitaji msaada,, ingawa kwa wakati huo hakuweza kuitambua sauti hiyo,, akatimua mbio kuelekea kule inapotokeq sauti hiyo,,, alipoyltazama kwa makini akamuona mkewe akiwa anatapatapa kupigania pumzi huku akifanya jitihada za kujiokoa mwenyewe kwa nguvu zake zote... Fundikira akaokota jiwe na kumpiga kichwani yule mtu anayemnyonga mkewe kwa kamba!!
mtu huyo akadondoka chini na kupoteza fahamu, Fundikira akaifungua kamba hiyo shingoni kwa mkewe.. akafanikiwa kuokoa uhai wa mkewe,,
*************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa Fundikira,, alionekana mtoto wao akiwa amelala usingizi mzito pale juu ya kitanda... ajitokeza Lucifer ndani ya chumba hicho,, akazipiga hatua kukifuata kitanda hicho!! alipokikaribia,, akasita kufanya jambo lolote,, kwa sababu kulikuwa na biblia aliyoiacha Fundikira pale juu ya kitanda! Lucifer akakasirika kupita kiasi,, ni baada ya mpango wake kushindikana ,kumchukua mtoto huyo kumpeleka kuzimu! akatoweka kimiujiza.
wakati huohuo alionekana Fundikira na mkewe wakizipiga hatua kurudi nyumbani!
baada ya dakika kadhaa wakawa wamefika,, wakaingia ndani ya nyumba,, wakaelekea chumbani.. walipofika wakaanza kusali kisha wakapanda kitandani na kuutafuta usingizi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************************
Asubuhi palipokucha walidamka salama lakini,, Fundikira akamwambia mkewe kuwa waende kwa mchungaji! mkewe hakuwa na kipingamizi akakubali wazo la mumewe! wakajiandaa kisha wakaelekea kwa mchungaji.. huku wakiwa na mtoto wao wa pekee!
walipofika Fundikira akasema ukweli wa mambo yote aliyoyafanya wakati anamtumikia Lucifer! mkewe akaanza kumuogopa Fundikira baada ya kumsikia akisema kuwa amefanya mauwaji ya watu wengi wasiokuwa na hatia,, akasema,,"hata mabucha mengi ya kuuza nyama huwa wanauza nyama za binadamu pasipo wao kujua,, hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kuona jambo hilo,,
mchungaji akaanzisha maombi maalumu kwa Toba,, Fundikira akatubu kwa imani..
kisha mchungaji akasema jumapili mje kanisani!.
siku zilizidi kusonga hatimae jumapili ikawadia,, wakajiandaa kwenda kanisani!!! wakati mke wa Fundikira yumo bafuni anaoga,, ghafla bomba likaanza kutoa damu badala ya maji! mke wa Fundikira akapiga kelele akatimua mbio kutoka bafuni! Fundikira akashtuka kumuona mkewe anapiga kelele! akauliza kwa mshangao mbona mwili wako umetapakaa damu? umepetwa na nini?
mkewe akashindwa kujibu kitu chochote akabaki anatetemeka kwa hofu iliyokuw imetanda juu yake!
Fundikira akaamua kwenda kule bafuni kushuhudia nini kimetokea... alipofungua mlango wa bafu akashtuka kuona damu nyingi zimetapakaa kwenye marumaru!! alipotazama kwa makini akaona matone ya damu yakitokea ndani ya bomba!! punde si punde ikasikika sauti ya mkewe akilia kwa sauti kali,,
Fundikira akatimua mbio kurudi chumbani..akastaajabu hakumkuta mkewe,, alipoangaza angaza macho yake akaona alama za nyayo za miguu iliyokanyaga damu ikitokea chumbani akazifuata nyayo hizo huku macho yake yakitazama kwa tahadhari! akaona alama za nyayo hizo zimeelekea kwenye kile chumba chake cha siri alichokuwa akikitumia kuwasiliana na Lucifer kuomba chochote anachokitaka! akausukuma ulenukuta ambao ni mlango wa kuingia ndani ya chumba hicho!! alipoingia upande wa ndani akakuta mkewe kapoteza fahamu huku kazungukwa na jopo la watu tisa waliovalia majoho marefu yenye rangi nyeusi,, Fundikira akapaza sauti akasema,, "muacheni mke wangu! mimi sihitaji tena kuendelea kuwa mwanachama wenu!
punde si punde akaonekana mmoja kati ya watu hao tisa akichomoa kisu na kuchuchumaa pale alipokuwa amelala mke wa Fundikira!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
macho yakamtoka Fundikira!!! wazo likamjia kuwa arudi chumbani akachukue biblia akatimua mbio kukifuata chumba chake cha kulala,, ghafla akatereza na kudondoka chini akaangukia kisogo!! akatulia tuli!
wakati huo huo kule ndani ya kile chumba cha siri walionekana wale wafuasi wa Lucifer wakifanya ishara ya mikono yao.... kwa ajili ya kumchinja mke wa Fundikira!
Wakati huo huo akaonekana Fundikira akinyanyuka kutoka pale chini alipokuwa amedondoka! akahisi maumivu makali kisogoni mwake,, akajaribu kukumbika nini kilimtokea mpaka yeye kudondoka chini,,kumbukumbu zikajia,,akakumbuka kuwa mkewe yupo kweny hatari lakini hana uwezo wa kuwazuia wale wafuasi wa lucifer zaidi ya kusali kwa imani,,
Fundikira akatimua mbio kuelekea kwenye chumba chake,,akachukua biblia haraka,kisha akatimua mbio kukifuata kile chumba alichokuwemo mkewe,,akaingi akakuta yule mfuasi mmojawapo kati ya wale wafuasi wa Lucifer akiwa ameshikiria kile kisu kikiwa shingoni mwa mkewe!
Fundikira akaanza kusali kwa kukemea huku kashikilia biblia,,punde si punde wale wafuasi wa Lucifer wakaanza kupiga mayowe,,wakiashilia maumivu makali kwenye miili yao,,yani wanaunguzwa kwa moto,,Fundikira hakusita kuendelea kusali kwa imani,,hatimae wakatoweka kimiujiza na kutokomea kusikojulikana!
baada ya tukio hilo mke wa Fundikira akazinduka na kupata fahamu,akastaajabu kujikuta ndani ya chumba hicho akiwa uchi wa mnyama,akauliza kwa mshangao!,,"nini kimetokea?
Fundikira akajibu,,"walitaka kukuchukua kwa kuchinja shingo yako!
mke wa Fundikira akaingiwa na hofu kusikia maneno hayo,,akanyanyuka. kutoka hapo chini,, wakaongozana kuelekea chumbani,, wakamkuta mtoto wao kalala usingizizito pale juu ya kotanda!
Fundikira na mkewe wakaanza kusali,,kisha wakapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! baada ya dakika kadhaa kupita wakasinzia,,,
ilipofika majira ya saa moja za usiku,, wakashtuka kutoka usingizini,, wakastaajabu kuona wamelaal masaa mengi mfululizo! lakini cha kushangaza hawakumuona mtoto wao pale kitandani!! wakaingiwa na hofu,, Fundikira akatimua mnio kuelekea sebuleni! akamkuta mtoto wake akiwa kaketi kwenye sofa!! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Fundikira akasita kumfuata mtoto huyo,, akaanza kusali kwa kukemea akihisi huenda ni mtego wa Lucifar,,
kumbe mtoto huyo alidamka akaona wazazi wake bado wamelalal akaamua kutoka ndani ya chumba na kuelekea sebuleni!
Baada ya kumaliza kusali,, Fundikira akazipiga hatua kumfuata mtoto wake akamgusa,, akagundua kuwa hakuna jambo lolote baya mbele yao!
akaonekana mkewe akizipiga hatua kuja sebuleni,,kisha akaelekea jikoni kuandaa chakula angalau wapate mlo.
baada ya nusu saa chakula kikaiva wakaanza kula..
walipomaliza wakarudi chumbani hukunwameongozana na mtoto wao,,,wakapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi!
*************************
Asubuhi palipokucha,, Fundikira akadamka mapema akamuamsha mkewe, kisha akasema,,"yatupasa twende kule kanisani kwa mchungaji,,Mke wa Fundikira akadamka na kuandaa chai haraka.. kisha akamuandaa myoto wake kwa kumuogesha!
baada ya dakika kadhaa kupita wakanywa chai na kuondoka zao.
iliwalazimu kutembea kwa miguu kwa sababu,, gari alilokuwa analitumoa Fundikira katika matembezi yake lilichukuliwa na Lucifer kimiujiza kwa mara ya pili,,
walitembea mwendo wa dakika nyinginkiasi,, wakawa wamefika kanisani kwa mchungaji, alex,, wakaingia ndani ya kanisa wakamkuta mchungaji akiendelea kupanga vitu vilivyomo ndani ya kanisa vikae katika mpangilio.... mchungaji akafurahi sana kumuona Fundikira pamoja na familia yake kuja kanisani hapo,, akawakaribisha kisha wakaanzisha maombi ya muda mfupi,, baada ya kumaliza maombi, mchungaji akasema,, "mbona jana hamkuja kanisani kwenye misa takatifu!
Fundikira akaanza kueleza kilichotokea siku ya jana!
mchungaji akaingiwa na roho ya huruma kisha akasema,, "yawapasa mumrudie Mungu,, atawaonyesha njia sahihi pia atawaondolea mateso na misukosuko,, Fundikira na mkewe wakakubali kumchamungu kwa imani na matendo,,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA***
maisha ya Fundikira yakabadilika,, familia yake ikaishi kwa amani pasipo misukosuko,,Fundikira akawa mmoja kati ya viongozi wa kanisa hilo,, hatimae akawa mchungaji na kuanzisha kanisa lake,,, akapata waumini wengi sana,, kwa sababu,, alisimaam kiimani. kitendo hicho kilimchukiza sana Lucifer akaamua kuandaa mpango wa Fundikira kumtumikia yeye kwa namna nyingine...
siku moja majira ya mchana Fundikira akiwa njianinkuelekea kwenye kanisa lake kwa ajili ya ibaada takatifu,, ghafla simu yake ikaita,, alipoitazama akaona namba ngeni ambazo sizo za kawaida,, namba hizo zilisomeka 666, Fundikira akashtuka kuona namba hizo akakata simu hiyo kisha akaanza kusali kwa kukemea,, punde si punde simu ikaita tena! akaamua kuika kisha akazima simu yake,, akaendelea na safari yake ya kuelekea kanisani kwake,, baada ya mwendo wa dakika kadhaa simu yake ikaita tena!! akashtuka! akajisemea moyoni,, "mbona simu yangu nimeizima!? yawezekanaje inaita? akaamua kuizima kwa mara nyingine tena, akaendelea na safari yake,
************************
Upande mwingine kule kuzimu alionekana Lucifer,, akiandaa mpango kabambe wa kumrudisha Fundikira awe mfuasi wake,,,akaandaliwa mwanamke ambaye atakuwa maalu kumteka Kifikr la Fundikira! mwanamke huyo akatumwa duniani siku ya leo kwenda kufunya jitihada za kumnasa Fundikira kiimani na kimatendo ilimradi airudie kazi ya kumtumikia Lucifer ,,kwa, kuwasha wayu waache kumuabudu Mungu wamuabudu Lucifer.
*************************
wakati huohuo,, alionekana Fundikira akiingia ndani ya kanisa lake,, baada ya sekunde kadhaa akaonekana mwanamke mrembo kupita kiasi! wanamke huyo alikuwa na tumbo dogo,, na nyonga pana, kavalia gauni lililokuwa limeshikilia vyema mwili wake na kuonyesha umbo lwke la kuvutia,, mwanamke huyo akaingia ndani ya kanisa huku kashikilia kitabu kilichoonekana kuwa na kurasa nyingi,, kikafanana na biblia, akizipiga hatua mpaka kule mbele alipokuwepo Fundikira,,
Fundikira akastaajabu kumuona mwanamke huyo,, akamkaribisha kisha akamuuliza kwa ukarimu,, "nikusaidie nini dada?
mwanamke huyo akasema,, "nimekuja kwa ajili ya maombezi,, mimi jina langu naitwa SEVE ninatatizo la kushika mimba,, mpaka sasa sijawai kushika ujauzito kwa kipindi cha miaka tisa..naomba msaada wako,,
Fundikira akamtazama mwanamke huyo kwa macho ya huruma,, kisha akasema,, imani yako ndiyo itakayokuponya,, yakupasa umtumainie Mungu pekee,, atakuponya,, hakuna kinachoshindikana mbele yake kwa yeyote atakaye muita,, naye ataitika kwa kujibu maombi yako!.
Fundikira akastaajabu kumuona mwanamke huyo akirudi nyuma hatua chache,, ni baada ya kutaja jini MUNGU!(GOD).CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Fundikira hakujali akahisi huenda mwanamke huyo anajiandaa kupiga magoti kwa ajili ya maombi!
bila kuchelewa maomni yakaanza! Fundikira akafumba mqcho huku akisali kwa imani,, akimuomba Mungu afungue uzazi wa mwanamke huyo,,, akiwa katikati ya maombezi,, ghafla mwanamke huyo akaanza kuvua nguo,, akabaki uchi wa mnyama kama alivyozaliwa! akazipiga hatua kumeogelea Fundikira! akaanza kumpapasa nyeti zake! Fundikira hakusita kuendelea kusali! lakini kila akimtaja Mungu mwanamke huyo anatetemeka huku akirudi nyuma!! lakini hakukoma,, akaendelea kufanya kazi aliyotumwa na Lucifer!.. punde si punde Fundikira akajikuta anaingiwa na tamaa,, mwili wa Fundikira ukaingiwa na hisia za kutaka kujaamiana na mwanamke huyo! pasipokujitambua kuwa ni mtego wa Lucifer! akaacha kusali akaiweka biblia kando,, alipofumbua macho akamuona mwanamke huyo yupo uchi wa mnyama!
TAHARUKI!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment