Search This Blog

TAMBIKO - 2

 







    Simulizi : Tambiko

    Sehemu Ya Pili (2)







    Asubuhi palipokucha Bibi Maliwa alidamkaapema..akaingia shambani na kuchimba viazi vitamu..akaandaa chai..

    Conso akadamka na kuanza kumsaidia mama mkwe wake kazi ndogondogo...

    Bibi maliwa akasema itabidi mjukuu wangu afanyiwe tambiko la kimila..ka ilivyokawaida katika ukoo wao.....

    Shinje na Conso hawakuwa na pimgamizi...



    ilipofika majira ya saa kumi za jioni...Bibi Maliwa akamuita Shinje pamoja na Conso kwa ajili ya tambiko la mjukuu wake...akachukuwa maji kiasi akayaweka ndani ya beseni,,akachukua kitovu cha Shinje ambacho alilitunza tangu Shinje alipozaliwa....akakidumbukiza ndani ya beseni akachukua kitambaa akachovya kitambaa hicho  kwenye maji hayo na kumfuta Maliwa mwilini..

    alipomaliza akamuosha Maliwa kwa maji hayo. kisha  akasema,,"sasa tambiko limekamilika.

    katika mila zetu ni lazima mjukuu aoshwe maji yaliyotumbukizwa kitovu cha baba yake..ili kumlinda na mizimu na mapepo wabaya...



       ******BAADA YA WIKI MOJA KUPITA******



    Shinje na Conso wakapanga safari  wakarudi nyumbani...bibi Maliwa akawasindikiza mpaka kwenye kituo cha mabasi.na safari ikaanza..

    baada ya masaa mengi kupita waliwasili jijini Dar es salaam..

    maisha yaliendelea kama kawaida...miezi ilisonga hatimae Maliwa akaanza kusimama mwenyewe bila kushikiliwa na mtu..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********BAADA YA MIAKA 15 KUPITA********



    Maliwa alitimiza umri wa miaka kumi na mitano(15)

    Siku moja akiwa amelala katika chumba chake usiku wa manane..ghafla akabadilika na kuwa binadamu mwenye kichwa cha ndege aliyefanana na  kuku...punde si punde kichwa chake kikarudi katika hali yake ya kawaida.....hali hiyo Maliwa hakuitambua kwa sababu ilimtokea yeye akiwa usingizini...

    kumbe lile tambiko lililofanywa na yule mganga pamoja na mumewe sasa limeanza kuleta matatizo...ni baada ya kuzika baadhi ya nywele za Maliwa poja na kuku aliyechinjwa ndani ya shimo moja..na kuwekwa dawa ya kichawi ndani ya shimo hilo....ili Maliwa afe Tambiko likamilike..lakini ilishindikana kwa sababu ya kipande cha nyuzi ya nguo ya Maliwa kilihitajika ili Tambiko likamilike...

    Siku moja Maliwa alidamka na kwenda shuleni..siku ya leo aliamua kupita njia ya mkato..njia hiyo inatokezea kwenye ule uwanja wa mpira uliozungukwa na miti ya mikaratusi..palipozikwa nywele zake pamoja na kuku...alipofikaaeneo hayo akahisi kichwa kinauma kupita kiasia ghafla kichwa chake kikabadilika na kuwa kichwa cha ndege anayefanana na kuku..Maliwa akaingiwa na hofu..alipotaka kutimua mbio ghafla ule mzimu wa ye bibi aliyeshiriku kufukia nywele za Maliwa akahitokeza..huku kavalia sanda nyeupe..





    Maliwa akaingiwa na hofu kupita kiasi! akatimua mbio..

    alikimbia umbali mrefu kiasi huku anapiga mayowe kwa uwoga!! akajikura ametokezea kwenye makazi ya watu! akakimbia kwenye nyumba ambayo ilikuwa na watu ndani yake..watu hao walipomuona Maliwa wakatimua mbio kutoka nje ya nyumba huku wakipiga kelele za uwoga na kusema,,"JINI,,JINI..

    Maliwa akazidi kuogopa,,akageuza shingo yake na kutazama nyuma,lakini hakuona kiti chochote! hata ule mzimu u yule bibi hakuuona tena..akatoka ndani ya nyumba hiyo huku akizipiga hatua za haraka haraka kurudi nyumbani kwao...akiwa njiani anatembea alistaajabu kuona kila mtu anayekutananaye anatimua mbio huku akipiga kelele! lakini Maliwa kila akitazama nyuma yake akuweza kuona kitu chochote,,kitendo hicho kilizidi kumuogopesha Maliwa akaanza kulia....

    akaamua kutua mbio kuelekea nyumbani kwao.

    akaparamia geti na kuingia ndani..akapitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni.Conso akastaajabu kumuona mwanae anakichwa cha ndege anayefanana na kuku! akaingiwa na hofu akatimua mbio kuelekea chimbani huku akipiga kelele..hali hiyo ilimfanya Maliwa azidi kuchanganyikiwa...akasema,,"mama mbona unanikimbia? kwa nini kila mtu ananikimbia yani hata wewe mama yangu? Maliwa alisema maneno hayo huku akilia kwa uchungu..akazipiga hatua za harakaharaka akaingia chumbani kwake!! akajitazama kwenye kioo akaona anakichwa cha ndege!! Maliwa hakuamini alichokiona..akaanza kulia kwa sauti kali...akafunga mlango kwa ndani!



    ********************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kule chumbani kwa Conso,,alionekana akimpigia simu Shinje na kumueleza alichokiona kwa mtoto wao.Shinje akashtuka sana! hakuamini alichoambiwa na mkewe..akahisi huenda Conso kachanganyiliwa!!

    Shinje akaamua kurudi nyumbani haraka....

    alipofika hakukuta mtu yeyote sebuleni..akaamua kwenda chumbani kwale akafungua mlango..lakini haukufunguka ,,Conso alikuwa kaufunga kea ndani!

    Shinje akapaza sauti,,"FUNGUA MLANGO MIMI MUMEO..

    Conso akafungua mlango haraka,Shinje akaingia ndani ua chumba.akauliza,,"Maliwa yuko wapi? kwani hajaenda shule leo?

    Conso hakujibu kitu,, aliendelea kulia!

    Shinje akauliza tena,,"kumetokea nini? ebu nyamaza uniambie.

    Cinso akasema,,"mtoto wangu...aliongea hivyo huku akifuta machozi.

    Shinje akazidi kuchanganyikiwa..akawa na shauku ya kutaka kujua nini kinaendelea!!

    Conso akasema ,,"Maliwa anakichwa kama cha kuku...

    Shinje akacheka sana! kisha akasema,,"yani mke wangu haujaacha tu,utani wako...mimi najua tu ulikuwa umenikumbuka..na hiyo ni janja yako ili nirudi nyumbani..Conso akamtazama Shinje kwa macho ya hasira..akajikuta anampiga kofi mumewe..kisha akasema ,,"yani mimi nakwambia kuhusu tatizo lililotokea wewe unaleta utani.Shinje akashtuka...tangu amuoe Conso hajawahi kumfokea wala kumkatisha kauli..lakini kitendo cha Conso kumoiga kofi! kilimfanya ahisi huenda taarifa hizo ni za kweli....



    wakati huo huo,kule chumbani kwa Maliwa, alisikia sauti ya baba yake akicheka akaamini kuwa baba yake anaweza kumsaidia,,akafungua mlango na kutoka nje..akazioiga hatua za haraka haraka akasahau hata kugonga hodi akapitiliza moja kwa moja mpaka ndani ya chumba cha wazazi wake!!

    Shinje akageuza shingo yake..akashtuka kumuona Maliwa anakichwa cha kuku! Conso akaanza kupiga kelele..akatimua mbio akatoka nje  ya chumba hicho!.

    Shinje pia akatimua mbio..akatoka nje kabisa ya nyumba yake..Conso na Shinje wakakimbilia kwa jirani ambaye ni yule babu aliyeshiriki kufanya Tambiko kwa kufukia nywele za Maliwa pamoja na kuku aliyechinjwa katika shimo moja!



    **************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule ndani ya nyumba alibaki Maliwa,,akilia kwa uchungu! akakata tamaa..akajisemea moyoni,,"sioni sababu ya kuendelea kuishi humu ndani..ni bora nikafie huko mbali nisiwape tabu wazazi wangu...nimeshajua kwa nini watu wananiogopa! lakini nini chanzo cha haya yote?? Maliwa alijiuliza maswali hayo bila kupata jibu lolote..akaamua kuondoka na kutokomea kusikojulikana!



    *************************



    Upande mwingine kule kwa jirani.Conso na Shinje wakamsimulia jirani yao..yele waliyoyaona kwa mtoto wao..

    Yule babu akawatazama na kuwapa pole ya kinafki..wakati yeye ndio muhusika wa hayo yote.

    Shinje na Conso wakaomba ushauri wafanyaje ili kumsaidia mtoto wao..Babu huyo akasema,,"bila shaka kunamtu anaichezea familia yenu..Conso akauliza kwa mshangao!! anaichezea kivipi?

    babu huyo akajibu,"itakuwa kuna mtu anawaroga,,lakini msiende kwa mganga yeyote tafuteni njia mbadala.Conso na Shinje wakatazamana usoni..  Shinje akajibu,," sawa tunashukuru asante kwa ushauri wako....wakabaki hapi kwa lisaa limoja mfululizo..

    (uchungu wa mwana aujuae mzazi) Conso akaingiwa na roho ya ujasiri akasema,,"tafadhali mume wangu turudi nyumbani tukamtazame mtoto..hata tukibaki hapa haitasaidia chochote..Shinje na Conso wakaongozana mpaka nyumbani..walipofika,,hawakumuona Maliwa..walimtaduta kwenye vyumba vyote lakini hawakufanikiwa kumpata...Conso akasema,,"ninamashaka na huyu jirani yetu..kwanini amesema tusiende kwa mganga yeyote,,bali tutafute njia mbadala!!? haiwezekani,,akili yangu yote inaniambia kuwa huyu babu atakuwa anafahamu kinachoendelea.Sinje akakubaliana na mkewe..wakaamua kwenda kwa mganga.....muda huo huo..



    ************************



    Upande mwingine ke nyumbani kwa jirani,,aliomekana yule babu akiwa ndani yachumba chake cha kulala..akachukua kioo..cha kichawi akatazama ili aone ni nini kinaendelea ndani ya nyumba ya jilani yake..pia ajue ni mipango ipi wanaipanga Conso pamoja na Shinje..akashtuka kioo chake cha kichawi kilionyesha Conso na Sinje wanaelekea kwa mganga..akajisemea moyoni,,"nisipofanya jambo fulani,nitaumbuka na watajua kuwa mimi ndiye muhusika..akajigeuza na kuwa paka...akatoweka kimiujiza!!!



    wakati huo huo kule njiani alionekana Conso pamoja na Shinje wakiwa wamekaribia kufika kwa mganga......ghafla wakamuona Paka weusi akitokea kwenye majani na kusimama mbele yao katikati ya njia waliyokuwa wanapita!.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Conso akashtuka akamwambia Shinje," mtizame paka huyo macho yake yanatisha Conso aliyaongea maneno hayo huku akajificha nyuma ya mgogo wa Shinje.....Shije akasema," mke wangu wewe ni muoga sana yaani unawaogopa paka ,huyu ni jamii ya paka pori kwa lugha yetu tunawaita kimbulu ....usiogope mke wangu tuendelee na safari yetu, wajaendelea kuzipiga hatua lakini Conso akaendelea kuwa na wasiwasi.....lakini cha kushangaza kila walipozidi kusonga mbele paka huyo alijitokeza mara kwa mara kama alivyojitokeza mwanzo Conso na Shinje wakaanza kupata wasiwasi,Conso akasema,"bila shaka huyu si paka wakawaida Shinje akasema,"hata mimi nimeanza kupatwa na wasiwasi huyu si paka wa kawaida na kwa nini ajitokeze mara kwa mara mbele yetu?? takribani  mara tatu mfululizo..........

    Wakasita kutembea wakabaki wamesimama kutizama nini hatima ya paka huyo,ikasikika sauti ya kicheko cha mwanaume mzee Shije na Conso waligeuza shingo kutazama sauti hiyo inatokea wapi lakini hawakuweza kumuona mtu anaetoa sauti hiyo, walipotazama mbele yao hawakumuona tena yule paka......hofu ikazidi kuongezeka juu yao Conso akasema," mume wangu mimi naogopa ni bora turudi nyumbani Shinje akasema," tatizo lako wewe mke wangu ni mwepesi wa kukata tamaa mapema tumeshamla ng'ombe mzima basi tumalizie mkia , twende tukalikamilishe jambo lililotuleta huku ,.....Conso hakuwa na namna ikabidi akubaliane na maneno ya mumewe. Wakaendelea kuzipiga hatua kusonga mbele lakini Conso alionekana kuwa na uwoga wa hali ya juu alitembea huku akigeuza geuza shingo yake kutazama upande wa nyuma.



    ************************



    Upande mwingine....alionekana mganga akiwa katika himaya yake....wakati anatengeneza dawa kwa ajili ya wateja wake...akahisi harufu ya hali ya hatari!! akajisemea moyoni,,"bila shaka kunajambo baya litatokea muda si mrefu...Mganha huyo alitambua hivyo kupitia mitego yake ya kimiujiza aliyoitegesha katika himaya yake..ili kubaini maadui wanaoimgia katika imaya yake!!! wakati anatafakari nini cha kufanya....Paka mweusi akajitokeza mbele yake...pumde si punde paka huyo akabadilika na kuwa binadamu...kumbe ni yule babu!! akarusha nguvu za giza zikampiga yule mganga akadondoka chini na kupoteza maisha papo hapo.

    Kisha babu huyo akajibadilisha umbile akafanana na mganga huyo aliyekufa! kisha akaificha kichawi maiti ya mganga huyo...

    kisha akaketi chini kwenye mkeka uliozungukwa na vibuyu.



    kwa mbali alionekana Shinje na Conso wakizipiga hatua kuja hapo kwa mganga...walipofika wakaeleza tatizo lao! kwa mganga huyo pasipokujua kuwa huyo sio mganga bali ni yule babu mchawi....Mganga huyo wa bandia akasema,,"itabidi wewe mama wa mtoto huyo ubaki hapa  siku mzima..itakapofika asubuhi dawa itakuwa imekamilika ili kumuokoa mwanao! Shinje na Conso wakatazamana usoni...Shinje akapinga jambo hilo.akasema kama mke wangu kubaki hapa haiwezekani labda na mimi nibaki!

    Mganga akasema,,"ni mwiko kushuhudia dawa hii ikiwa inatengenezwa,,anatakiwa mama wa mtoto huyo,ndiye abaki hapa....mganga huyo bandia alisema maneno hayo huku akitingisha tingisha tunguri...

    Conso akamsihi sana mumewe ili akubali,,,alimsihi sana hatimae Shinje akakubali....kisha akaondoka zake kurudi nyumbani na kumuacha mkewe kabaki hapo kwenye himaya ya mganga....



    ************************



    ilipofika majira ya saa moja za usiku..mganga huyo bandia akamwambia Conso kuwa avue nguo zake zote..kisha alale kwenye mkeka huku akiwa uchi...Conso akashtuka akasema,,"dawa gani ya namna hiyo mpaka nivue nguo?

    mganga akasema,,"bila kufanya hivyo mtoto wako atakufa siku chache zijazo!

    Conso aliposikia maneno hayo akalazimika kukubali alichoambiwa na mganga....akavua nguo na kulala juu ya mkeka...kisha mganga akasema usifumbue macho mpaka nitakapokwambia...na ukikosea masharti..utaharibu dawa!

    Conso alafumba macho..punde si punde mganga akavua nguo na kuanza kula uroda...Conso alitamani amtoe mganga huyo lakini kila akikumbuka yele maneno..akajikuta anakuwa nyonge ilimradi atimize masharti ipatikane dawa ya kumsaidia Maliwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog