Search This Blog

SOSO - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Soso

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    HAPPY NEW YEAR....HAPPY NEW YEAR....HAPPY NEW YEAR???? ilikuwa ni majira ya usiku wa saa sita na dakika kadhaa zilisikika sauti hizo zikiimba ndani ya gari"""wanafamilia hao wanne(4) wakiwa na wanawake zako ndani ya gari aina ya

    TOYOTA V8"" waliimba wimbo huo wa mwaka mpya na kujipongeza kwa kuuwona mwaka mwingine wakiwa hai...walikunywa pombe ndani ya gari huku wengine wakiwabusu na kuwakumbatia wanawake zao kwa upendo(POMBE NI MBAYA UKIWA UNAENDESHA CHOMBO CHA MOTO).....Lakini MARY ambae ni mtoto wa waziri mkuu wa nchi alionekana kuwa nafuraha bila kunywa au kutumia kilevi chochote....alikuwa kamkumbatia mchumba wake aitwae Sande.....

    sande....Lawi....James na edga walikuwa ni ndugu wa familia moja....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari iliendelea..wanafamilia hao waliamua kwenda kutalii kwenye Maporomo ya maji huko mozambiki( MOZAMBIQUE) pia wafanye utafiti wa madini... lakini mary alianza kuingiwa na wasiwasi kwani huwa anaogopa sana kusafiri usiku...hivyo alimwambia Mchumba wake Sande kuwa watakapofika mtwara walale kisha waendelee na safari kesho yake Sande alikubali ombi la mchumba wake mary safari iliendelea""".....james..edga na lawi walikuwa wamesinzia kwenye viti vya upande wa nyuma wa gari hilo...kutokana na kuzidiwa na ulevi.....walikunywa pombe nyingi sana... kwa furaha ya kuuwona mwaka mpya...Sande aliendelea kuzipanga gia baraabara huku mchumba wake Mary kaketi kwenye kiti cha upande wa kushoto upande wa mbele....



    ***********



    Baada ya kufika mtwara Sande hakutaka kulala pale mtwara aliendelea kuzipanga gia....Mary hakufurahishwa na kitendo hicho cha sande kutomsikiliza....alichukia sana mary...sande aliendelea kuzipanga gia...huku akimbembeleza mary kwa maneno matamu... huku akiendelea kunywa bia.....aaaah baby mimi niko makini sana barabarani napokunywa pombe na kuendesha gari...usijali baby....Aliyasema maneno hayo sande aliyatamka kwa kilevi...mary hakutaka kuongea kitu chochote kutokana alikuwa kachukia sana....

    Tom aliendelea kuzipanga gia mpaka wakatoka kabisa nje ya makazi ya watu.. wakaanza kuingia kwenye barabara inayopita porini""" pori hilo lilioneka kubwa sana miti ilikuwa pande zote kusho na kulia hivyo barabara ilikuwa katikati ya msitu huo....sande aliendelea kuzipanga gia aliendesha gari kwa kasi ya ajabu...mary alimsihi sana sande apunguze mwendo....ghafla kunakitu kilitua juu ya gari..kisha kikadondoka chini mary aliogopa sana"" sande hakuweza kusikia kishindo kile juu ya gari kwa sababu alikuwa na ulevi kichwani mwake...mary alimuuliza sande kama kasikia kitu chochote..alijibu hapana hajasikia kitu....mary alinyamaza akabaki kimya huku akigeza shingo yake upande wa nyuma...hakuweza kuona kitu kutokana na giza lililokuwa limetanda...sande aliendelea kuzipanga gia....walikwenda umbali wa kilometa 20 mara ghafla kikasikika kishindo tena juu ya gari....ni kama kitu kinadondoka kutoka juu na kuangukia juu ya gari....mary aliogopa alihisi kama kuchanganyikiwa kisha akaanza kumlaumu sana sande unaona sasa nilikwambia tulale mtwara tuendelee na safari kesho ukawa mbishi!!!"",, sande alicheka kisha akasema punguza uwoga baby upo na mimi...ondoa sha kabisa...kisha akaongea maneno ya kejeri..

    ((mimi napiga ngumi za mfululizo hata jet lee haoni ndani)) kisha sande akacheka...mary alikasirishwa na maneno yale ya sande ya kejeriCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hivi sande mimi nakwambia jambo wewe unaleta utani...sidhani kama mtu anayekupenda akakahidi kile unachomwambia....kisha mary alichukua vidonge aina ya pirton akavimeza ili apate usingizi asishuhudie chochote kitakachotokea....sande alianza kum-bembeleza mary...

    mary alijibu kwa sauti ya ukali sitaki kusikia hizo nyimbo zako wakati mary anaingea hivyo mara ghafla alionekana mtu katikati ya barabara akiwa hatua tatu kutoka gari lilipo """",,kwa sababu sande

    alikuwa anaendesha gari kwa mwendo wa kasi alimgonga mtu yule...alikanyaga breki mpaka mwisho gari liliyumbayumba.....kisha likasimama...Hata sande aliogopa.....kisha akaaumua kushuka ili aone mtu huyo kafa au bado yupo hai!!!aliposhuka alistahajabu sana hakuona kitu chochote...alichungulia mpaka chini ua uvungu wa gari lakini hakuona chochote..wakati huo wadogo zake edga...james...na lawi walikuwa bado wamelala fofofo kutokana na ulevi mara ghafla..



    Mara ghafla sande alipogeuka nyuma alistahajabu kumuona yule mtu aliyemgonga....akiwa kasimama huku damu nyingi zikimtoka kama maji.. mtu yule alikuwa akimtazama sande.... sande aliogopa alihisi kupoteza fahamu pombe zilimruka akawa kama mtu ambaye hajatumia kilevi chochote.... aliingia ndani ya gari alipoliwasha gari halikuwaka alijaribu lakini ilishindikana.... alipotazama ule upande aliokuwa amesimama yule mtu hakuonekana tena... wakati huo mary alikuwa akilia kwa uwoga....baada ya sande kuona yule mtu hayupo aliamua kushuka akafungua boneti ya gari kuangalia tatizo kwa nini gari haliwaki... alihisi harufu ya petrol alipomulika kwa kutumia simu yake aliona mafuta yakimwagika chini alipotazama vizuri aliona tenki la kuhifadhi mafuta ya gari hilo limotobolewa na kishoka kidogo kikiwa hapohapo kwenye tundu... alichanganyikiwa... mara ghafla alisikia kitu kimepiga kwenye taili alipotazama aligundua ni mshale... aliamua kuwaamsha wadogo zake.. waliamka pamoja na wanawake zao mara ghafla kioo kilipasuliwa bila kuona mtu anayefanya hivyo...Edga... James... lawi pamoja na wanawake zao pombe ziliwaruka kila mtu aliamua kutoka ndani ya gari na kukimbia""" walikimbia bila kujua ni wapi wanaelekea... kutokana ilikuwa giza nene walijikuta wamo ndani ya pango""" waligundua hivyo baada ya mary kuwasha tochi ya simu yake na kumulika..... waliogopa sana.. waliendelea kuingia ndani zaidi ya pango hilo kwa ajili ya kujificha... mara ghafla mary alipomulika upande mwingine aliogopa akajiziba mdomo ili sauti isitoke... aliona kiganja cha mkono wa kinadamu..... mary alianza kulia huku akimlaumu sande.... CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ************

    Asubuhi palipokucha walistahajabu kuona miili ya binadamu waliouwawa ikiwemo ndani ya pango hilo... mara ghafla alisikia vishindo vya watu wakitembea kuingia ndani ya pango hilo....walijificha.... mary alichungulia aliona watu wawili wenye sura mbaya za kutisha meno yao ya mbele yalikuwa marefu na yenye ncha kali kama paka watu hao walikuwa wanavuruta mwili wa binadamu aliye katwa nusu kwa nusu kuanzia kichwani mpaka chini.. upande mmoja ulibaki mkono na mguu mmoja na upande mwingine hivyohivyo.... Mary alistuka kisha akawajulisha wenzake kile alichokiona.... waliamua kutimua mbio kuelekea upande mwingine.... walikimbia hata bila kujua ni wapi wanapoelekea...... ghafla sande aliona upenyo alipotazama vizuri aliona upande wa nje..... waliamua kutoka kwa kupitia upenyo huo.... walitoka wote kisha wakaanza kukimbia kuitafita barabara ili walitengeneze gari lao warudi nyumbani...... walipofika yale maeneo ambapo gari lao lilikuwepo walistahajabu kukuta gari limenyofolewa kila kitu limebaki bodi tu.... uwoga ukawaingia...... wakaanza kukimbia.... Edga ambaye ni mdogo wake sande alisema tusipite kwenye barabara tutaonekana kwa urahisi hivyo tupite njia za porini..... kabla hajamaliza kuongea alistukia kapigwa na mshale katikati ya paji la uso kisha mshale ukatokezea upande wa nyuma kisogoni""" Edga alidondoka chini na kupoteza maisha papo hapo. wenzake walipo ona hivyo walichanganyikiwa wakaanza kutimua mbio walikimbia umbali mrefu wakatokezea barabarani... waliamua kusimama kando ya barabara hiyo huenda wakapata msaada baada ya dakika kadhaa kupita....kwa mbali walisikia mngurumo wa gari... walifurahi sana...gari lile lilipokaribia sande alisimama barabarani kabisa huku akipunga mkono ishara ya kutaka dereva asimamishe gari...

    gari lilisimama wakaomba msaada kwa dereva yule awasaidie kuwatoa eneo lile dereva alikubali na kisha walianza safari.... huku sande akiwa kwenye mawazo juu ya kifo cha mdogo wake...baada ya umbali mrefu kidogo walistahajabu dereva yule ghafla kaloki milango.....kisha akakata kona kuelekea kule kwenye mapango ambapo mwanzo walikimbia kutoka huko.... walianza kupiga kelele....mary alipojaribu kufungua mlango wa nyuma wa gari hilo alistuka kukuta maiti ya edga....



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog