Search This Blog

BINTI WA PILI WA MFALME - 1

 







    IMEANDIKWA NA : SALMA R. RAMADHANI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilianza kwa kuonekana mawingu makini yaliyokuwa juu ya anga likiling.arisha anga kwa rangi yake ya blue yenye kung.aa na jua lililoweza kuonekana liking.aa zaidi. Huku zikisikika sauti za ndege mbalimbali pamoja na mmiminiko wa maji katika mrefeji mdogo ulioweza kupita katika kijiji cha Isambala kuelekea mto mkubwa ulioko katika kijiji cha jirani.



    Ghafla utulivu ule uliweza kukatika baada ya mguu wa kike kuweza ukanyaga maji yaliyoko mahali pale Mara baada tu ya mguu ule kuweza kupita ilionekana miguu mingine ya kiume iliyokuwa ikikatiza katika eneo lile lile na wakionekana kumfuata binti huyo aliyekuwa akikimbia kwa kasi sana.



    Kishoka aliita mmoja kati ya vijana wale wanne.



    "Endapo hatutampata Sarafinah basi binti wa mfalme na mfalme mwenyewe hawez kutuacha hai"



    "Ni kweli kibonge cha kufanya ni kumpata Sarafinah na tumpeleke ngomeni kabla hajakimbilia kijiji cha jirani. Alijibu kishoka.



    " Nzanza na Nzenze aliita kishoka kwa kuwaita vijana wawili walioweza kubakia zaidi.



    "Ndyo shujaa" waliitika wote kwa pamoja.



    "Hatuwezi kurudi ngomeni bila Sarafinah hivyo atafutwe" alizungumza na wote walianza tena safari ya kumtafuta.







    ***** ***** ****



    Lilionekana kundi kubwa na wanakijiji wakijadiliana jambo huku wengi wakionekana kutikisa vichwa vyao ishara ya masikitiko.



    Ghafla alitoka binti mmoja ndani ya chumba kimoja katika ya vyumba vilivipo katika ngome ya mfalme na wote walikaa kwa kutulia na kutoa salamu kwa binti yule.



    "Wana Isambala hoyeee" alizungumza binti yule.



    "Hoyeee" waliitika wote kwa kuinamisha vichwa vyao chini huku mikono yao ikishika vifuani mwao.



    "Atukuzwe??



    " Binti wa mfalme Samela Iputo" walizungumza wanakijiji wote kwa pamoja.



    Sawa inueni vichwa vyenu....

    Wote walifanya kama walivyoweza kuagizwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kama mlivyoweza kutambua na kusikia kosa aliloweza kulifanya Sarafinah ndani ya ngome hii ya mfalme Iputo baba yangu Mimi, kwa mila na desturi za kijiji hichi hafai tena kuwa hai wala kuishi ndani ya kijiji hiki kwani amefanya kosa kubwa sana la kulala na mfalme mtaraji ambaye ni mume wangu Mimi katika kijiji hichi na hilo aliweza kulitambua kabisa hivyo basi........



    Kabla hajamaliza kuongea walionekana wakija mashujaa wa kijiji hichi wakiwa wamemkamata binti ambaye ndiye aliyekuwa akishtumiwa kwa kosa la kulala na mume wa Samela.



    Baada tu ya Samela kumuona alimfuata na kuanza kumpiga vibao mbele ya watu ambao walionekana kumtazama sana kwa hasira.



    Wakati huo alikuwapo mwanamke mmoja aliyekuwa ameishika nguo yake ya chini kwa nguvu sana na kung.ata meno yake.



    "Mpumbavu wewe unawezaje kulala na mwanaume ambaye si wa kwako kwani Kuna vijana wangapi hapa kijijini kwanini ukalala na mume wangu Nuhu alizungumza huku akiendelea kumpiga vibao Sarafinah.



    "Unastahili kufa.... Hustahili kubaki hai" alizungumza na kuchomoa panga lililokuwa kwa kijakazi wake na kutaka kumchoma nalo Sarafinah.

    Ulitokea Mkono wa kiume na kuzuia panga lile.



    "Nuhu" aliita Samela.



    Nuhu alimtizama kwa hasira sana Samela na kumtoa Sarafinah mikononi mwa mashujaa wale.



    "Atukuzwe.



    " atukuzwe mfalme mtaraji wa kijiji chetu Nuhu Noa " walijubu wanakijiji.



    "Inueni vichwa vyenu juu" alitoa amri hiyo na wote waliweza kufanya hivyo.



    "Unataka kufanya nin??? Alimuuliza Samela.



    " amekiuka kanuni na taratibu za kijiji hichi cha Isambala anastahiki kifo" alizungumza Samela



    "Kwa kuwa ana mimba yangu?? Aliuliza



    " Ndiyo"



    "Ulipokuwa na mimba yangu uliuwawa??



    " hpana... Lakini ameweza kulala na mume wa mtu tena kwa kukulazimish"



    "Hapana hajanilazimisha alizungumza Nuhu.



    " najua yeye ndiye aliyeweza kukulazimisha wewe ufanye hivyo huwezi kufanya hivyo"



    "Kama niliweza kufanya kwako kwanini nishindwe kufanya kwake, nililewa sana na nikajikuta nimelala naye kama nilivyoweza jikutaga nimelala na wewe miaka mitatu ya nyuma" alizungumza Nuhu.



    "Kwahiyo unamtetea?? Aliuliza Samela.



    " hapana "



    "Bali??



    " nataka nifanye kama vile nilivyoweza kufanya kwako baada ya kugundua kuwa nililala na wewe "



    "Unamaanisha nini?? Yani Unataka kumuowa?? Aliuliza kwa hamaki.



    Nuhu alitikisa kichwa.



    " hapana haiwezekani "



    "Inawezekana kwasababu Mimi tayri ni mfalme na ninauwezo wa kuowa wake hata zaidi ya wanne" alizungumza Nuhu na aliweza kuingia mtabiri wa kijiji hicho Mzee tambitambi.



    "Isambala hoyee"



    "Hoyeee"



    "Atukuzwe??



    " mtabiri tambitambi wa kijiji chetu"



    'Inueni vichwa vyenu.......ndugu wanakijiji wenzangu wa kijiji chetu hichi cha Isambala habari njema nilizonazo ni kwamba Nuhu tayri ameshaweza kutawazwa na mizimu imeweza kumkubali yeye ashike kiti hichi cha kifalme japo bado mfalme wetu yuko hai kwhiyo kwanzia sasa Mfalme wa kijiji hichi ni Nuhu

    Noa"



    Aishi maisha marefu mfalme" alizungumza Nzanza na wote waliweza kupiga magoti na kuvilaza vichwa vyao chini huku wakiitikia



    "Aishi maisha marefu mfalme Nuhu Noa.



    Nuhu alimtizama Sarafinah aliyekuwa akibugujikwa na machozi ya huzuni huku akiwa amemkumbatia Nuhu.



    ****** Baada ya miaka miwili *******



    Alionekana binti mdogo mwenye umri wa miaka mitano akiw na vijakazi katika mto mdogo au mrefeji wa kijiji cha Isambala akiwa anaogelea mahala hapo.



    Walikuwa wakija wasichana wawili walioweza kubeba mitungi yao ya maji kwaajili ya kwenda kuteka maji katika mto huo, walikuwa wakipiga stori zao na zilionekana kunoga kweli kwani walipoweza kufika tu waliinamisha mitungi yao na kuanza kuchota maji kwa kuendelea kupiga stori.



    Mmoja aliyekuwa anatizama upande alipokuwa akiogelea binti yule wa mfalme alisimama na kuachia mtungi ambao uliweza kupasuka.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " unashida gani mbona umepasua mtungi wa mama?? Aliuliza na kugeuka kutazama mwenzake anapoweza kutizama.



    Alishtuka na kujikuta mtungi wake umedondoka kisha akaanza kutetemeka wakati huo wote binti yule alikuwa akiwatizama kwa hasira sana.



    Zikisikika sauti zao wakilia kwa uchungu huku ikisikika milio ya fimbo juu ya miili ya watu. Baada ya dakika kadhaa alionekana mtot huyo akitengenezea shangaa zake vizuri kiunoni na kutembea huku wafuasi wake wakiwa nyuma yake na wakionekana mabinti wale wamevimba miili yao yote huku wakilia na kujikung.uta.



    ****** ****** ****



    Njee ya hapo kilioneka kijumba kimoja kidogo kando kando mwa mrefeji ule na aliweza kuonekena Sarafinah akiwa na binti wake mdogo aliyekuwa akimuimbia nyimbo kwaajili ya kum bembeleza na kumfanya alale.

    Aliingia Nuhu na alipotaka kusimama kwaajili ya kutoa heshima Nuhu alimzuia kwa ishara kisha akamsogelea mpaka pale alipo na kumbusu katika paji la uso alimtizama binti wake huyo mdogo na kutabasamu.



    'Mozah ameshakula? Alimuliza mkewe



    Sarafinah alitikisa kichwa.



    "Kwanini wewe uko hapa? Na unajua upaswi kuwa hapa hii ni sehemu iliyoweza kulaaniwa kwa sasa hupaswi......"



    "Shshshshsh.........najua hukuweza kuiba mali zile walizoweza kuziweka katika chumba chako, me najua na nina amini huna tabia ya uwizi kabisa..ila Samela alitaka wewe upoteze maisha kwa kufanya hivyo na Mimi ndiye niliyeweza kukuchagulia adhabu hii ya kuja huku..nisamehe Mimi kwasababu sijawa mume mzuri kwako , pamoja na baba mzuri kwa Mozah" alizungumza Nuhu na kumtazama binti yake ambaye alikuwa amelala.



    ***** ***** *****



    "Kibonge" aliita kwa sauti ya juu Samela baada tu ya kutaka katika chumba cha Mfalme.



    "Yuko wapi mfalme??



    "Alitoka malikia.



    "Akaelekea wapi??



    "Sifahamu malikia alijibu Kibonge.



    " Unasemaje hujui alipokwenda alizungumza na kumpiga kibao Kibonge.



    'Nikigundua alipoweza kwenda unapafahamu basi sitakuacha hai" alizungumza Samela na kutoka na wafanyakazi wake wawili wa kike.



    Wakati huo alionekana nuhu akiwa na mkewe Sarafinah pamoja na binti yao mdogo ambaye aliweza kuamka wakiwa pale pale wakicheza na maji ya mto ule waliweza kusikia michakacho na walipoweza kugeuka alionekana Mwanamke mmoja ambaye makamo yake yaliweza kwenda kidogo mwanamke huyu ndo yule ambaye aliweza kujizuia pindi Sarafinah alipoweza kukamatwa kwa Mara ya kwanza na kuanza kupigwa na Samela.



    Bi lunde! Aliita Nuhu na kusimama.



    "Isambala hoyee" alizungumza Bi Lunde



    "Hoyee"



    "Atukuzwe mfalme na malikia wa kijiji hichi cha Isambala" alizungumza Bi Lunde kwa kuinamisha kichwa chake chini.



    Nuhu na yeye alikilaza kichwa chake na kusema.



    "Atukuzwe pia mama wa malikia wa mfalme wa kijiji cha Isambala"



    "Atukuzwe" alijibu Sarafinah na wote waliweza kucheka.



    "Mbona leo umekuja huku huyo mke wako bado hajazipata taarifa hizi? Aliuliza Bi Lunde.



    " Yani hata najiuliza ilikuwaje eti nikalala naye alafu sijakuta hata matapishi asubuhi.



    "Kwanini?? Aliuliza Sarafinah



    " ww hukumbuki nilikuwa nikitapikaga kila nikimuona sasa nashangaa ilikuwaje au labda kisa alinilewesha alafu akanibaka" alizungumza.



    "Wewe Nuhu, kwanini Mara nyingi unapenda kusema hivyo wewe?? Aliuliza Sarafinah huku akimsukuma Nuhu.



    " Bi Lunde fikiria unajua siku hiyo me nikitoka zangu shambani nikakutana naye njiani akaniambia ya kuwa Sarafinah ni mgonjwa na kwa kuwa alikuwa ni rafiki wa Sarafinah nikaamini nikaanza mfuata akanipeleka kwa yule kijakazi wake Batuli baada tu ya kufka akanmbia kunywa maji haya kidogo nikamlete Sarafinah hapa umuone.....me ni kanywa ila nilihisigi ladha ni tofauti nikahisi kulala nikalala naamka nashngaa yuko Pembeni yangu akiwa hana nguo najitizama na Mimi sina nguo, alafu kanaanza kulia eti mara nashngaa baba yake ameshafika Mara kijiji kizima ndo nikapewa adhabu ya kumuowa kama sivyo Mimi ningemuuliaga mbali sana ila kwaajili yako ndo maana naendelea kuishi naye" alizungumza Nuhu akisonya na kuonesha kutokupendezwa na kile kilichoweza kutokea kipindi cha nyuma.



    Sarafinah pamoja na mama yake walibaki wakimtizama Nuhu aliyeweza kumuinua binti wake na kuondoka naye pale kwa kumpeleka ndani ya nyumba anayoishi Sarafinah.



    Wakati huo nao alionekana njiani malikia Samela akija kwa kasi sana maeneo Yale na kusema



    "Kama nitakukuta huko naapa nitamuuwa Sarafinah kwa mikono yangu mwenyewe na kumfanya binti wako huyo apoteee kabisa katika kijiji hiki" kiapo hicho aliweza kukiweka Samela aliyekuwa akieleka katika mto ule



    Miaka ilienda na siku zikazidi kusonga mbele huku bado kukiwa na mgogoro baina ya Sarafinah na Samela.



    Siku moja usiku wakati Sarafinah akiwa amejipumzisha kwenye chumba chake Aliweza kutoka njee kwaajili ya kupigwa na upepo. Ghafla alihisi hali ambayo haikuwa ya kawaida.



    "Sijisikii vizuri kabisa, au ni kwasababu Mozah Leo kaenda kulala na bibi yake? Alijiuliza na kutabasamu.



    " wala siyo kwa sababu mozah ameenda kulala na bibi Yake, bali ni kwasababu leo ni siku ya kifo chako, ilikuwa ni sauti ambayo iliweza kupenya katika masikio ya Sarafinah na kumfanya ageuke nyuma yake alikutana na Salome.



    "Salome" aliita kwa mshangao na ghafla alikamatwa na vijakazi wawili wa malikia Salome.



    "Hivi unajua nimeuchoka uwepo wak katika kijiji hichi, kwaajili ya wewe na binti yako Nuhu, hajali kuhusu Mimi wala binti yangu Sikinde, sasa ninakuuw kama ni laana iwe juu yngu" alizungumza na kutoa upanga kutoka kwa kijakazi wake kisha kumchoma nalo Sarafinah.



    "Ni Sawa wewe, ulikuwa rafiki yngu na mpenzi wa Nuhu lakini Mimi ni binti wa kifalme kila ninachoweza kukihitaji kutoka katika kijiji hichi lazima nikipate, ila kwa uwepo wako wewe unafanya Nuhu ananichukia mimi" alizungumza na kuchomoa panga kisha kumchomeka tena kwa Mara ya pili.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sarafinah alibaki akiguguma kwa maumivu huku akiwa amemshikilia tumbo lake ila kwa bahati aliweza kushika shingo ya Samela na kutoka na cheni iliyoko shingoni mwa Samela na kuikata.



    Ziliweza kudondoka shanga zile na Samela pamoja na wafanyakazi wake walianza kuziokota moja baada ya nyingine ili kuondoka ushahidi na baada ya kumaliza kufanya hivyo aliweza kuondoka yeye pamoja na vijakazi wake.



    Kulikucha asubuhi na alionekana Nuhu akiw na binti yake Mozah na kuelekea katika nyumba aliyokuwa akiishi Sarafinah.



    "Mama" aliita Mozah aliyekuwa ameshatizama miaka 9.



    ***** ***** ****.



    "Tayari alishaweza kulaaniwa na Ndiyo maana akawa anaishi njee ya kijiji chetu hivyo hawzi kufanyiwa maziko" alizungumza mganga wa kijiji cha Isambala jina lake walimuita Kipande.



    "Ni kweli kwa mila na desturi zetu lakini kwa mila na desturi zetu hizo hizo mtu ambaye amehusika na mauji anapaswa kuuwawa yeye pamoja na familia yake kwni tayari imeshalaaniwa kwa kufanya hivyo" alizungumza mtabiri tambitambi.



    "Sawa, mwili wa Sarafinah ukatupwe katika misitu ya Isambala na sitotaka achunguzwe mto yoyote yule juu ya mauaji yake kwani tayari alishaweza kulaaniwa" alizungumza mfalme Nuhu na kusimama.



    "Baba!! Aliitwa kwa mshangao Mozah na kusimama



    " kwanini maiti ya mama yangu itupwe? Na kwanini walioweza kuhusika na mauaji wasifuatiliwe Mimi nitawafuatilia mwenyewe. Alizungumza Mozah.



    "Mimi Ndiyo mfalme na Ndiyo mwenye kauli ya mwisho katika kijiji hiki, nimesema hakuna atakayeruhusiwa kufuatilia nani muuwaji na kwanzia Leo Stela utaishi na Mozah katika nyumba ile hutaruhusiwa kutoka wala kuingia katika ngome hii na yoyote atakayeweza kusogea karibu na nyumba ile basi atachinjwa kwa kukiuka amri ya mfalme" alizungumza Noah na kuingia katika kasiri yake ya kifalme.



    Mozah alimfuata ndani na ghafla ilisikika sauti ya Nuhu ikimuita mlinzi mkuu wa kasiri ya kifalme Kishoka.



    Aliingia ndani na kutoka na Mozah.



    "Kwa kosa la kuingia katika kasiri ya kifalme pasina ruksa achapwe viboko 20 na adhabu hiyo nitaitimiliza mimi" alizungumza Nuhu na Nzanza pamoja na Nzenze waliweza kumkamata mikono na miguu kisha kumlaza katika meza ya adhabu na hapo alianza kuchapwa fimbo. Kitendo hicho kiliweza kuwashtua wazee wa kijiji kile kwani kwa jinsi Nuhu alivyokuwa akimpenda binti yake huyo mdogo asingeweza kufanya hivyo. Wakati huo nao mganga kipande na malikia Samela walitizamana na kutabasamu.



    Baada ya kupokea adhabu hiyo mfalme alimuita Nzanza na Nzenze.



    "Ndiyo mfalme"



    "Ukajengwe uzio utakaoweza kufanya huyu asitoke wala mtu yoyote yule asiingie pale mpaka itakapopita miaka 10"



    "Hata ikipita miaka 20, sitakaa nikakanyaga tena katika kasiri hii" alizungumza Mozah na kufuata mwili wa mama yake alitoa vyeo vyote ambavyo viliweza kumfanya yeye aonekane malikia wa kijiji hicho pamoja na yeye akavivua vyeo vyote na kuvitupa chini.



    "Mama yangu hakuwahi kuwa malikia wala mimi sikuwahi kuwa binti wa mfalme, baba na mama yangu wote wamekufa siku ya leo" alizungumza kwa hasira na kuondoka katika kasiri ya kifalme.



    "Beba vyakula na upeleke huko hakikisha huruhusiwi kutoka katika eneo lile mpaka miaka 10 ipite na akikiuka basi atauwawa, au ataishi uko milele. Alizungumza na kuelekea ndani ya chumba chake na masaa ya jioni alionekena malikia Samela akiingia katika chumba cha mfalme akiwa ameshikilia kibuyu alichoweza kukiandalia togwa.



    "Karibu mfalme wangu" alizungumza Samela na kumpa tongwa ambayo aliipokea nuhu na kuinywa kwa pupa.



    Wakati akinywa Samela aliweza kukumbuka kitu kuwa baada ya kufanya mauji Yale aliweza kuelekea kwa mganga Kipande ambaye aliweza kumpatia dawa na kumwambia awe anamuwekea kwenye kinywaji chochote kile Nuhu na Nuhu atakuwa akimfikiria yeye katika Maisha yake yote "

    Alitabasamu na kumpapasa Nuhu kichwani aliyekuwa akiwaza jambo.



    ***** *****



    "Si ruhusiwi kwenda kumuona mjukuu wangu kwnini eti, kwanini Nuhu amebadilika hivyo?? Aliuliza Bi Lunde.



    " natumaini Kuna kitu malikia Samela na mganga Kipande wamefanye, kwani nilipokuwa nikimtizama mfalme niliweza kuuona moshi mweusi ukiwa unamzunguka" alizungumza mtabiri tambitambi.



    "Tunafanyaje sasa, kuhusu Mozah, tunafanyaje sasa kuhusu Nuhu pia? Aliuliza Bi Lunde.



    " Unajua nlimzindika kwa kiasi kikubwa Nuhu nashindwa kuelewa ni uchawi gani ulioweza kutumika ukawa na nguvu kuishinda mizimu yangu ya itongwe" alijiuliza mtabiri tambitambi.



    Hpo hapo waliweza kusikika michakacho na aliingia ndani Kishoka ambaye aliweza kuwapa ishara ya kuwa mfalme yuko njee na anataka kuingia ndani. Walisimam wote na kutoa heshima kabla ya mfalme kuingia ndani.



    "Kwahiyo mmekaa hapa mnanijadili Mimi, wote mnastahili adhabu, kishoka nahitaji vichwa vyao" alizungumza Nuhu kwa ukali.



    "Mfalme wangu.......

    Naomba utuhurumie kwa Tabia yetu mbaya tuliyoweza kuionyesha mbele yako,Tafadhali zihurumie shingo zetu " alizungumza Bi Lunde akiwa ameinamisha kichwa.



    "Haraka sana nimesemaaa.........ni utani" alizungumza na kucheka na hapo Bi Lunde aliweza kupumua pamoja na mtabiri tambitambi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haaaaaaaa alizungumza Bi Lunde na Nuhu alimkumbatia.



    "Umenishtua eti nikajua ya kuwa tayri Samela ameshakuloga na ma uchawi yake, umeniogopesha sana Nuhu"



    "Mama nimefanya hivyo kwaajili ya usalama wa Mozah, kwani ndiye mtu wa pekee aliyeweza kuniachia Sarafinah kutoka katika tumbo lake, nikikaa karibu naye naweza kumpoteza kama nilivyoweza kumpoteza Sarafinah na sitaki hali hiyo itokee, ndo maana nahitaji na wewe ukae mbali na Mimi pamoja na Mozah kwaajili pia ya usalama wako" alizungumza Nuhu na Mtabiri Tambitambi aliweza kumshika bega na kumwambia.



    "Umechukua maamuzi magumu sana unastahili pongezi"



    ***** ***** ****



    Paliweza kupambazuka asubuhi na malikia aliweza kutoka njee ya chumba chake Mara baada ya kusikia kelele za mtu akilia katika kasiri ile ya kifalme.



    Alipitoka njee alikutana na Kibonge akimchapa Bi Lunde fimbo za mgongoni huku Nuhu akimtizama kwa hali ya kawaida kabisa.



    Malikia Samela alimsogelea karibu kabia Nuhu.



    "Na utoe tangazo kwa yoyote yule atakayeweza hata kukaribia mpaka ule nilioweza kuuweka baina ya kijiji chetu na mahali alipoweza kuwekwa Mozah" alizungumza Nuhu na wafanyakazi wote waliweza kuitikia wito huo na Kuondoka kwa kuweza kuchukua NGOMA kisha kuanza kuzipinga na kutoa taarifa hiyo.



    Miaka 10 ilipita Hatimaye ikaongezeka miaka 2 tena katika kasiri aliyokuwa akiishi Mozah iliweza kuvamiwa na ngao iliyoweza kujengwa kwaajili ya kuzungushia nyumba ile iliweza kubomolewa hiyo ilikuwa ishara ya kuwa kwasasa yuko huru.



    Wakati huo nao binti wa Samela. Sikinde alikuwa akikatiza kuelekea katika mto kwaajili ya kuogelea na hapo aliweza kuwasikia wanakijiji walizungumza.



    "Siku ya Leo yule binti wa pili wa mfalme, anaachiwa huru natamani kwenda kumuona sijui atakuwa mzuri kiasi gani! Waliyazungumza bila kutambua ya kuwa Sikinde aliweza kuwasikia



    "Mozah nimeishi kwa Amani miaka yote 12, Tafadhali usije ukaiharibu furaha yangu, kwani sitaweza kukuruhusu" alizungumza Sikitu na kutabasamu.



    Miaka ilienda na siku zikazidi kusonga mbele huku bado kukiwa na mgogoro baina ya Sarafinah na Samela.



    Siku moja usiku wakati Sarafinah akiwa amejipumzisha kwenye chumba chake Aliweza kutoka njee kwaajili ya kupigwa na upepo.



    Sikitu aliweza kuongea akiwa na hasira sana na wafanyakazi wake wawili walibaki wakimtizama tu.



    "Tunaelekea huko huko alikoweza kuwekwaga Mozah" alizungumza na kuanza kuongoza njia.



    ******* *******



    "Mama, Kuna mtoto wa mfalme kutoka katika kijiji cha matajiri au kijiji kikuu katika nchi yetu, anatembelea kijiji hadi kijiji kwaajili ya kutafuta msichana wa kuowa, nataka amuowe Mozah ili aweze kwenda mbali na kijiji hichi kwani Ndiyo itakuwa njia pekee ya usalama wake zaidi" alizungumza mfalme Nuhu baada ya kuonana na Bi Lunde.



    "Kama hivyo Ndivyo itakavyotokea basi itasaidia sana, anakuja lini?? Aliuliza Bi Lunde.



    " nilipata maandishi ya kuwa atakuja siku ya Leo, ndo maana nimeruhusu Mozah aachiliwe siku ya Leo na avalishwe nguo zuri kama binti wa mfalme naamini hawezi kuukwepa uzuri wa Mozah" alizungumza MFALME Nuhu na Mtabiri Tambitambi alitikisa kichwa.



    ***** ***** *****



    "Yuko wapi Sikitu, Leo kijana wa mfalme kutoka katika kijiji tajiri anakuja hapa kijijini kwetu anatakiwa avae vizuri ili aweze kuonekana mbele ya kijana huyo na aweze kuolewa" alizungumza malikia Samela.



    ***** **** *****



    Wakati Sikitu akiwa anakaribia eneo lile aliloweza kufungiwa kwa muda mrefu Mozah alizisikia kelele za wanakijiji wakipiga vigelegele huku wengine wakisema.



    "Atukuzwe........ Binti wa pili wa kike wa mfalme Mozah Nuhu Noah"



    "Atukuzwe......



    " binti wa pili wa mfalme Mozah Nuhu Noah "



    Alitembea haraka haraka hadi kufika eneo lile na wanakijiji wote walinyamaza wakimtizama Sikitu aliyekuwa akihema kwa hasira.



    Wakati hayo yakiendelea katika upande mwingine wa walionekana vijana wawili wakiwa wamewasili na farasi wawili na wote wakiwa wamebeba baadhi ya vitu katika migongo ya farasi hao.



    "Oyah...... Me napumzika hapa kwanza" alizungumza kijana mmoja mtanashati n ambaye angeweza kuvutia machoni pa kila msichana.



    "Ndiyo mtoto wa mfalme" alizungumza kijakazi wake ambaye na yeye alikuwa siyo haba kwa uzuri.



    "Hiyo sitaki hiyo" alizungumza mtoto wa mfalme aliyejulika kwa jina la Hancy.



    "Ndiyo Hancy" alizungumza kijakazi wake na kucheka wote kwa pamoja.



    Hancy ni kijana ambaye alikuwa mkarimu sana wala hakutaka kuonyesha cheo alichoweza kuwa nacho mbele za watu, kwani hakupenda kupata mwanamke atakayeweza kumpenda yeye kutokana na mali au cheo alichonacho. Kijakazi wake Tomimo alikuwa ana undugu wa mbali kutoka katika familia hiyo ya kifalme hivyo alipenda kwenda naye kila mahali aendapo.



    ****** ***** ******

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliweza kufika katika kasiri ya kifalme na waliweza kupokelewa kwa shangwe na vigelegele kutoka kwa wanakijiji walioweza kufika katika eneo lile.



    Hancy aliweza kuvaa nguo za kawaida kabisa na kuweza kumtambulisha kama mfanyakazi na Tomimo akiwa amevaa nguo ambazo ziliweza kumfanya aonekane kama mtoto wa mfalme na huo ndiyo ulikuwa mchezo wao katika kila kijiji walivyoweza kupitia.



    Japo kuwa Tomimo aliweza kuja kwa cheo cha mtoto wa mfalme, lakini bado Hancy alipendeza machozi pa watu wengi haswa haswa wasichan.



    "Yani ni mzuri sana ila chaajabu ni kijakazi wa mtoto wa mfalme" alizungumza msichana mmoja na Hancy aliweza kuyasikia hayo maneno na kutabasamu.



    Baada ya kukaribishwa Hatimaye aliweza kuja mfalme Nuhu na kijakazi wake huku mkewe akiwa tayri ameshakaa mahali anapostahili kukaa.



    Mfalme alienda na aliweza kupewa heshima kutoka kwa Hancy pamoja na Tomimo na wanakijiji wake.



    Alikaa na kuwakaribisha.



    "Waiteni wanangu waje waonekane mbele ya mtoto wa mfalme" alizungumza mfalme Nuhu na vijakazi wakike wa Sikitu walielekea katk chumba cha Sikitu.



    Baada ya muda alikuja Sikitu akiwa amependeza kwa kiasi kikubwa sana tu huku akitembea kwa mwendo wa taratibu na wa madaha ulioweza kuwafanya wanakijiji wa kiume wakishangilia kwa kupiga miruzi na wanawake wakipiga vigelegele kwa fujo.



    Hancy na Tomimo walimtizama na Hancy alitabasamu baada tu ya kumuona Sikitu.



    Alielekea kukaa karibu kabisa na alipokaa Tomimo akiamini ndiye mtoto wa mfalme.



    "Yuko wapi Mozah? Aliuliza mfalme Nuhu.



    Stella alitoka ndani ya chumba ambacho alikabidhwa yeye na Mozah.



    " yuko wapi?? Aliuliza mfalme kwa hasira.



    "Nilimuacha ndani lakini nilipoweza kurudi sijamkuta tena" alizungumza Stela na kuinamisha kichwa chake chini.



    "Huyu mtoto huyu" alizungumza Nuhu na kutoa amri stella akamatwe mpaka pale Mozah atakapopatikana.



    "Muache mama yangu" ilisikika sauti ikizungumza na kuingia katika ngome ya mfalme alikuwa ni Mozah aliyeweza kuvalia nguo za kawaida kabisa na kuingia akiwa amefura kwa hasira alisogea mpaka pale walipokuwa wamemshika stela na kutoa mikono yao.



    "Iwe Mara ya mwanzo na mwisho kumshika Stella kwa nguvu nmna hii, mmenisikia? Aliuliza kwa hasira Mozah.



    " Ndiyo binti wa pili wa mfalme Mozah"



    Alimshika Stela na kumtizama mikononi mwake.



    "Mozah baba yako anakusubiria ni vizuri kama ungeenda kubadilisha nguo kisha uelekee pale walipo" alizungumza Stela na Mozah alienda akiwa na mavazi Yale Yale na alipofika alitoa heshima kwa malikia akatoa heshima kwa mfalme kisha akamgeukia Tomimo na kutoa heshima kisha akasimama na kumtizama.



    "Mimi siku..........



    Kabla hajamaliza kuzungumza mfalme alimuwahi na kumwambia.



    " usizungumze chochote kile kitakachoweza kunikera Mimi na ukae kimya katika mahala pako panapostahili kukaa" alizungumza na kumtazama Mozah ambaye alisogea mpaka alipoweza kukaa Hancy na kukalia kiti cha jirani.



    "Inamaana hujamsikia baba yako alivyoongea......amesema ukae mahali panapostahili kukaa wewe siyo kukaa katika viti vya vijakazi" alizungumza malikia Samela kwa kufoka.



    Mozah alimtizama bila kusema neno na kurudisha macho yake kwa baba yake aliyekuwa akimtizama tu.



    Hancy alimtizama kwa makini na kujikuta akitabasamu tu, hivyo Ndivyo ilivyokuwa hata kwa Tomimo.



    ****** ********



    Usiku uliingia na Hancy alikuwa Akicheka cheka tu.



    "Ni kipi kimekufurahisha mbona una raha sana leo? Aliuliza Tomimo.



    " Kati ya wale mabinti wawili wa mfalme, Mimi namfikiria mmoja" alizungumza Hancy.



    "Hata Mimi pia" alijibu Tomimo na kucheka.



    "Tomimo, katika Maisha yangu yote sijawahi kukuombaga kitu lakini nakuomba usije ukamfikiria msichana ambaye namfikiria Mimi" alizungumza Hancy.



    "Kwani wewe unamfikiria yupi???



    **** ***** *****



    Kukikucha asubuhi na alionekana Mozah akiwa njee ya chumba alichoweza kupatiwa na mfalme.



    Hancy alitoka akiwa na mswaki na aliweza kumuona Mozah.

    Alitembea kwa kutizama chini mpaka amfikie pale alipoweza kuketi ghafla naye Mozah aliweza kusimama na kujikuta wakipamiana na macho yao kutazamana huku mikono yao ikiweza kukishika kikombi kile kisiweze kudondoka na kujikuta wameshikama mikono, Hancy alitabasamu na kumtizama zaidi Mozah huku akimsogelea usoni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " we" alisema Mozah na kumsukuma kichwa Hancy.



    "Mjinga nini?? alizungumza na kuanza Kuondoka zake eneo lile.



    Hancy alizidi kutabasamu tu na kuishika vidole vyake.



    " dah!! Mlaini kweli, sijui kama anaweza hata kuchota maji kweli" alizungumza Hancy na kuendelea kucheka zaidi.



    Tomimo alikuja nyuma na kumshika bega Hancy.



    "Nakuona nakuona....... Huchezi mbali kabisa"



    Hancy Alicheka na kumpiga ngumi kidogo ya tumboni kisha akaenda mbele ila alipofika mbali kidogo Tomimo hakuonekana tena mwenye furaha usoni mwake.



    ***** ***** *****



    Alionekena Mtabiri Tambitambi akija katika eneo la ufalme tena akionekana mtu mwenye haraka.



    "Kuna shida gani mbona unakuja katika kasiri ya kifalme kwa haraka hivi?? Aliuliza malikia Samela.



    " atukuzwe malikia wa kijiji hichi cha Isambala........Kuna jambo nimeliona Leo limeweza kunishtua sana yuko wapi mfalme??



    "Njoo uingie ndani" alizungumza mfalme wa kijiji cha Isambala.



    Malikia Samela alienda katika chumba chake na kutoa kibakuli kikubwa kilichokuwa na maji alinyunyuzia dawa Flani kisha akainenea maneno Flani na hapo hapo aliweza kuonekena Mtabiri Tambitambi pamoja na mfalme Nuhu.



    "Endapo.....Mozah ataolewa na mtoto wa mfalme wa kijiji cha matajiri basi kijiji chetu kitaingia katika matatizo makubwa sana hivyo, hakikisha ndoa kati ya mtoto wa mfalme na binti yako haiwezi kutokea hata kama watapendana" alizungumza mtabiri tambitambi na ghafla alihisi kitu na kutizama sehemu ambayo macho yake yaligongana macho kwa macho na malikia Samela aliyekuwa ndani ya chumba chake alitemea mate maji Yale na sura zao ziliweza kupotea katika chombo kile.



    Samela alianza kucheka akiamini sasa binti yake huyo ndiye atakayeweza kuolewa na mtoto wa mfalme.



    Wakati huo alionekana Mozah akiwa katika mto ulioweza kupita katika kijiji chao akiwa anatupia tupia mawe lakinj ghafla aliweza kukumbuka jinsi Hancy alivyoweza kumshika mikono yake na kumuachia Tabasamu zito. Alijikuta akitabasamu na yeye.



    "Heeeeeee kwanini namfikiria huyo kijakazi" alizungumza Mozah na kusimama alipokuwa amekaa kwaajili ya kuondoka ghafla aliweza kukutana macho kwa macho na Hancy aliyekuwa nyuma yake alishtuk kwa kuogopa na kutaka kudondoka ila Hancy alimuwahi kwa kumshika kiuno na Mkono mwingine akiwa amemshikilia Mkono wake alioweza kubebea shanga zake.



    Wakati hilo likitokea alionekana Sikitu akiwa anaeleka uelekeo ule aliokuwepo Hancy pamoja na Mozah.



    Ni baada ya Hancy pamoja na Mozah kuwa katika hali ambayo mtu yoyote yule angewakuta ingeweza kuwashtua.



    Tomimo alikuwa wa kwanza kumuona Sikitu aliyekuwa akija eneo lile.



    Alipiga mruzi na farasi alianza kulia hivyo kumfanya Hancy kutambua ya kuwa kutakuwa na mtu ndani ya eneo lile.



    "Niachie alizungumza kwa hasira Mozah na Hancy alitizama alipomdakia ilibaki kidogo tu adondoke au afikie chini.



    " Sawa " alisema Hancy na kumuachia Mozah ambaye alidondokea katika mto ule.



    "We mpumbavuuuuuu alifoka Mozah kwa hasira na kwa sauti ya juu iliyoweza kupenya hadi masikioni mwa Hancy kwa nguvu na kumfanya Hancy aingize kidole chake masikioni na kutoa uchafu kisha kuupuliza.



    " muone huyu muone huyu...... Alilalama Mozah na kujitizama kwa kiasi alichoweza kulowa nguo zake Zote.



    Wakati huo nao aliingia Sikitu na baada ya kumuona Mozah akiwa ndani ya maji huku Hancy akiwa juu ya jabali Alicheka na kumtazama Mozah ambaye baada ya kuona anachekwa na Sikitu pamoj na wafanyakazi wake wote macho yake yalirudi tena kwa Hancy pamoja na hasira zake.



    Alisimama kutoka katika Yale maji na kumsukuma Hancy pembeni.



    Nguo zake ziliweza kulowana na zilikuwa nyepesi hivyo mwili wake uliweza kuonekana kwa kiasi flani.



    Hancy alivua koti lake ambalo lilikuwa lirefu na kubaki na nguo nyepesi sana juu ya kifua chake aliweza kumpita Sikitu na wafanyakazi wake ambao waliweza kubaki kuduwaa kwa kukitizama kifua chake na kumsindikiza kwa macho. Aliweza kumvisha nguo ya juu Mozah na kumsogelea kw mbele kish kuifunga mikanda miwili ya nguo iliyokuwa juu ya kofia ya nguo hiyo.



    Stela aliyekuwa mlezi wa Mozah aliweza kufika pale na kutoa mikono ya Hancy katika mwili wa binti yake.



    "Sitki kujua ni tabia zipi ulizoweza kutoka nazo huko kwenu, lakini kuwa na heshima huyu ni binti wa pili wa mfalme, anaweza akawa anaonekana kama mjinga katika ufahamu wako wa akili, ila huyu ndiye furaha ya mfalme Nuhu na wewe ni kijakazi tu, hivyo unapaswa kuwa na heshima mbele yake" alizungumza na kumshika mikono Mozah kisha Kuondoka naye eneo lile.



    Sikitu alimtizama sana Hancy na kujikuta anajishtukia baada ya Hancy kumtizama.



    Katika hali ya kujisahau Tomimo alivua nguo yake ya juu na kwenda kumvika Hancy kisha kutoka naye eneo lile, na kuweza kwenda kumpeleka mahali walipoweza kuacha farasi zao kisha kumpandisha na yeye akapanda farasi inayofuata na kuondoka zao.



    "Zawadi umeona?? Aliuliza mfanyakazi mmoja akimuuliza mwenzake

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Ndiyo Furaha nimeona" alijibu na waliweza kusikia sauti ya Sikitu akizungumza.



    "Huyu mfanyakazi ni mzuri sana kuliko mtoto wa mfalme, kwnini sasa yeye akawa mfanyakazi jamani?? Alijiuliza na kushika nguo yake kisha kung.atana mdomo wake kwa design ambayo aliweza kuitambua mwenyewe.



    Uliingia usiku na alionekana Hancy akiwa njee ya chumba alichokuwa akilala na Tomimo. Tomimo na yeye aliweza kutoka.



    " kaka, nini shida? Aliuliza Tomimo.



    "Tom, unajua mi nilifanya vile kwa kutania tu siyo kwamba nilimaanisha eti kumuuzi alafu pia yeye mwenyewe ndiye aliyeweza kunilazimisha Mimi kumuachilia lakini ona yule mama yake alikuja na kuanza kunigombeza Mimi lakini kama wangeweza kutambua wadhifa wangu basi sidhani kama angeweza kufanya hivyo, alafu Tom unajua me nampenda yule mwanamke eti, sitaki kabisa kumuumiza lakini sijui hata imekuwaje mpaka ikafikia hivi lakini...................."



    "Hancy.......tulia...... Tulia embu kwanza........usifikirie sana alizungumza na kumshika Hancy mikono.



    "We ni nani?? Aliuliza Tom.



    " Mtoto wa mfalme Hardati"



    "Mtoto wa mfalme Hardati huwaga hajutii chochote kile alichoweza kukifanya wala kukizungumza kwasababu huwa yuko sahihi kwa wakati wote" alizungumza na kumtuliza Hancy.



    "Unafanya nini usiku huu njee?? Aliuliza Stela.



    "Mama.......sidhani kama ulvyomwambia yule kijakazi ni sahihi, ni sawa ni kijakazi lakini hapana hukupaswa kumwambia hivyo kwani Mimi ndiye niliyoweza kumwambia aniachie na kudondoka mtoni na pale alikuja kunisitiri Mimi baada ya nguo zangu kulowa, lakini. . ........"



    "Unapaswa kuolewa na mtoto wa mfalme siyo kijakazi wa mtoto wa mfalme, hivyo hupaswi kuacha akajenga na wewe mazoea" alizungumza Stela na kuingia ndani



    "Ni sawa lakini siyo vizuri kwa vile ulivyoweza kumwambia we unafikiri anajisikiaje sasa hivi" alizungumza na kuingia ndani akimfuata Stela ambaye tayari alishamzoea kama mama yake.



    Wakati huo nao Hancy na Tom walikuwa eneo lile waliweza kuyasikia maneno Yale na Hancy alibaki akicheka.



    "Kumbe hana hasira na mimi, na ananitetea eti si umemsikia" alizungumza Hancy alizungumza huku akimpiga piga mgongoni Tom ambaye alimshika Mkono na kumwambia.



    "Hancy sasa unaniumiza" alizungumza Tom na kutoa Mkono wa Hancy.



    "Samahani.......... alizungumza na kuipiga piga mikono yake Hancy.



    " kweli umependa maana unaelekea kuwehuka" alizungumza na kumshika nguo ya juu ya Hancy kisha kuanza kumvuta na kutoka eneo lile, wakiwa wanatoka eneo lile waliweza kuonekana na Sikitu ambaye aliwatizama na kuanza kuangalia jinsi walivyokuwa wakiburuzana.



    "Hivi, huyu mfalme gani anakuwa na mahusiano na kijakazi wake namna hiyo" alijiuliza Sikitu na kuingia ndani ya chumba chake.



    ****** ***** ****



    "Mtoto wa mfalme Hardati njoo" alizungumza mfalme Nuhu na kumfanya Tomimo amfuate, huku Hancy akiwa nyuma yake walipofik waliweza kukaa na mfalme alimtizama Hancy.



    "Huwaga kila ninapoenda simuachi yeye nyuma kwasababu haonekani kama kijakazi kwangu, bali zaidi ya rafiki" alizungumza Tomimo.



    "Nilikuwa na maneno machache tu ya kuzungumza na wewe ni kuhusu binti yangu Mozah" alizungumza mfalme Nuhu na Hancy alitega sikio lake vizuri.



    "Binti yangu wa pili, ni mzuri kiumbo lakini siyo kiakili wala kimaarifa siyo kwamba nasema hana kabisa akili hapana bali kutokana na kwamba aliweza kukaa sehemu moja zaidi ya miaka12 pasina kutoka wala kwenda kokote pale ndo maana anaonekana mwenye kiburi, kwahiyo nakuomba usimpende binti yangu" alizungumza mfalme Nuhu.



    "Kwanini mfalme? Aliuliza kwa hamaki Hancy na Tomimo aliweza kulirudia lile swali.



    "Kwasababu ni mjinga, hajui kusoma, hajui kuandika, hajui kupika, hajui kuchota maji, hajui.........



    " me nitamfundisha vyote hivyo alizungumza Hancy na kumfanya mfalme Nuhu amshangae.



    "Namaanisha Tomimo anaweza akamfundisha vyote hivyo, hat kama itachukua miaka" alizungumza Hancy.



    "Lakini.......alizungumza mfalme Nuhu na Mozah alitokea pale hivyo maongezi hayo yaliyoweza kuishia pale.



    Alionekana Hancy akiwa juu ya farasi wake huku akiwa mwingi wa mawazo.



    " unafikiri kwanini mfalme hataki umuowe Mozah?? Aliuliza Tomimo.



    Hancy alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo na Tomimo alishusha pumzi ndefu.



    "Hata Mimi pia ili sifikiri sababu ni ya kuwa hajui kupika wala kuosha vyombo, lazima kuwe na sababu nyingine na Nahitaji wewe unitafutie hiyo sababu" alizungumza Hancy na alipotazama mbele aliweza kumuona Mozah akiwa juu ya farasi huku akionekana mwingi wa mawazo na farasi akiwa amesimama pale pale alipo.



    "Nafikiri tutaonana baadaye sana" alizungumza Hancy na kutabasamu kisha akaondoka.



    "Anaenda wapi huyu alijiuliza na kutazama mbele ambako aliweza kumuona Mozah.



    "Mungu wangu huyu Mozah huyu, atamfanya Hancy awe kichaa siku za karibuni alizungumza na kutaka kugeuza farasi wake na aondoke ila alihisi uwepo wa mtu nyuma yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Sikitu aliita kwa mshangao na kumtazama Sikitu aliyekuwa akijichekesha.



    "Ha-ha.....mambo alizungumza na kumtazama Hancy aliyekuwa akikaribia eneo lile alilokuwapo Mozah.



    Hancy alifika mpaka karibu na kumpita bila kumsemesha.



    " we.......wewe.......aliita Mozah na Hancy aligeuka na kumtizama.



    "Mimi!!!?



    " eeeehh njoo hapa" alizungumza Mozah.



    "Baba ake anasemaje siyo mjanja ilihali anataka kutumia cheo chake kuniomba msamaha bila mimi kutambua" alizungumza na kujisogeza karibu.



    "Huko kijijini kwenu, huwaga hamsalimii watu?? Aliuliza Mozah.



    " atukuzwe binti wa pili wa kike wa mfalme Nuhu " alizungumza Hancy na kugeuza farasi.



    "We kijakazi" aliita tena Mozah.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Samahani kwa kutoweza kuonyesha heshima mbele zako, alizungumza Hancy na kushuka juu ya farasi kisha akampiga magoti Mozah.



    " sikumaanisha nilivyokuwa nilivyokuita kijakazi alizungumza Mozah na kutaka kushuka juu ya farasi lakini alishuka pasina kutizama wapi pa kukanyaga na kujikuta akishuka mzima mzima na kumvaa Hancy aliyekuwa chini tayri.



    Hii iliweza kuwafanya wadondokeane Hancy akiwa chini kisha Mozah akapanda juu ya kifua cha Hancy. Wakati huo nao Sikitu aliwez kufika na Tomimo eneo lile na tukio lile aliweza kuliona lakini halikumpendeza Sikitu hata kidogo kwni tayari na yeye ndani ya moyo wake amekwisha mpenda Hancy.



    Wakati huo Sikitu aliweza kushuka kutoka kwa farasi na kwenda kumtoa Mozah juu ya mwili wa Hancy,



    "Unafanya nini hapa? Aliuliza kwa hasira na kumsukuma Mozah upande mwingine Hancy alisimama na kutaka kwenda mahali alipo Mozah kabla hajafika Sikitu alimshika Mkono na kumrudisha usawa wake kisha kumpiga kibao.



    Tomimo alishuka kutoka kwenye farasi wake na kwenda kutoa Mkono wa Sikitu katika Mkono wa Hancy.



    " huyu ni kijakazi wangu Mimi wala siyo wa kwako nitamuhadhibu mimi pindi nitakapo.....hii ni mara ya kwanza naya mwisho nisikuone tena ukifanya upumbavu ulioweza kuufanya kwa siku ya Leo.



    "Hancy, uko salama?? Aliuliza Tomimo na kumshika mahali alipopigwa kibao.



    Hancy alimtizama kwa macho ya hasira sana Sikitu na kuelekea mahali alipo Mozah.



    "Umeumia?? Aliuliza Hancy na kumsimamisha huku akimkung.uta kung.uta.



    " hapana, na wewe?? Aliuliza Mozah na kumshika Hancy shavu lake hali iliyomfanya Hancy ashindwe kuzungumza na kutabasamu.



    "Hancy, tunarudi ngomeni" alisema Tomimo na kwenda kumtoa Hancy Mkononi mwa Mozah.



    "Mozah.....alitaka kuzungumza jambo juu ya Mozah lakini alisita baada tu ya kupigwa jicho na Tomimo.



    Tomimo alimshika na kumfikisha kwenye farasi kisha akamuinua na kumpandisha na yeye akapanda farasi wake na kuondoka eneo lile.



    " haaaaaaaaaa...... Alizungumza Sikitu na kuanza kumtizama Mozah kisha macho yake yakarudi tena kwa Hancy na Tom waliokuwa wakipotelea eneo lile.



    ***** ****** *****



    Sikitu alipokuwa akirejea nyumbani alimkuta Tomimo akiwa na mfalme Nuhu huku akionekana kuvimba kwa hasira.



    "Yuko wapi huyo Mozah!? Aliuliza mfalme Nuhu na Mozah alitokea pale pale.



    " njooni mkae hapa" alizungumza mfalme na hapo hapo alikuja Hancy ambaye alipoweza kumuona tu Mozah aliachia Tabasamu.



    Wote walikaa na kubaki sasa wakitizamana.



    "Sikitu umemfanya nini kijakazi wa mtoto wa mfalme? Aliuliza mfalme Nuhu.



    " Muulize nilimkuta wapi??



    "Nilikuwa.......... Kabla Hancy hajaongea Tomimo alimdakia juu kwa juu



    "Kwanza naomba niwaweke wazi, huyu siyo kijakazi wangu kama mnavyodhania nyie.



    "We Tomimo Unataka kuzungumza nini?? Aliuliza Hancy kwa wasiwasi.



    "Usijali nataka kuwaambia pia huyu ni mmoja kati ya watu kutoka katika familia ya kifalme, na umuhimu wake ni mkubwa sana kunizidi Mimi hivyo ningependa mumpe heshima hata zaidi mnayonipa Mimi na Ndiyo maana simchukulii kama kijakazi" alizungumza Tomimo.



    "Sawa tumekuelewa, Sikitu na Mozah natumaini mtamchukulia huyu ndugu wa mtoto wa mfalme kama mnavyomchukulia mtoto wa mfalme.



    " ammmhhhh alitaka kuzungumza kitu Mozah lkini alijikuta anamtizama tu Hancy.



    "Naitwa Hancy alizungumza Hancy akijua ya kuwa Mozah anataka kutaja jina lake.



    " nilikuwa naomba samahani kwa siku ya Leo pamoja na zile zilizoweza kupita kwa kukukosea na kutokuonyesha heshima mbele yako....

    Mtoto wa mfalme.! Aliita Mozah



    "Unaweza ukaniita Tom, alizungumza Tomimo.



    " ninapenda kuomba samahani kwa kile kilichoweza kutokea kwa siku ya Leo na...."



    "Nimekuelewa Mozah, pia ulikuwa ufahamu hilo ndo maana" alizungumza Tom.



    "Vipi wewe Sikitu? Aliuliza mfalme Nuhu baada ya kuona hana hata dalili za kutaka radhi.



    "Ningependa kusema samahani tu" alizungumza kwa kifupi na kumtazama Tom.



    "Sawa yameisha" alizungumza Hancy na kusimama.



    "Kabla hamjaenda ningependa kuwakumbusha kitu kimoja, hawa ni mabinti wa kifalme hivyo ningependa muwaheshimu kama binti wa mfalme, Hancy hapa siyo mjini kwenu hivyo nakuomba upunguze mikono yako katika mwili wa binti yangu Mozah; kwani utajikuta umeowa bila kukusudia" alizungumza Mfalme Nuhu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Na je kama namaanisha kumuowa utaniruhusu?? Aliuliza Hancy na kumfanya Mozah asimame alipoweza kukaa.



    "We....alisema Mozah na kumshika Mkono Hancy, mfalme unaweza kuelekea ndani" alizungumza Mozah na mfalme Nuhu alitabasamu tu na kuondoka zake



    Alionekena Sikitu akiingia ndani ya chumba chake kwa hasira



    "Yani Hancy, a namwambia Mozah anataka kumuowa mbele ya baba?? Alijiuliza huku akitupa tupa vitu aliingia mama yake na kuokota baadhi ya vitu vilivyokuwa vimetupwa chini.



    "Unashida gani??



    " Mama Hancy anataka kumuowa Mozah "



    "Hancy ndo nani?? Aliuliza malikia Samela.



    " kijakazi wa Tomimo "



    "Unasema kijakazi wa yule mtoto wa mfalme wa Isadora.



    "Ndiyo huyo huyo".



    " Mungu wangu yani kweli huyu mtoto hana bahati; amekuja kudondokea mikononi mwa kijakazi na uzuri wake wote ule?? Alijiuliza malikia Samela....... Lakini ngoja sasa hiyo sindiyo nafasi nzuri ya wewe kuwa na yule mtoto wa mfalme sasa kinachokukera hapo ni nini?? Aliuliza malikia Samela.



    "Me nampenda Hancy"



    "We......Pumbavu wewe ......tena hiyo sauti yako hata isitoke njee una dhubutuje kumpenda kijakazi wewe ni mjinga nini sikutegemea kama ningezaa mtoto mpumbavu kama wewe, unafikiri ukiwa na mahusiano na huyo mjinga kipi utafaidi kutoka kwake; kama Unataka Mozah awe juu yako sasa ongea upumbavu na useme unamtaka kijakazi"



    "Lakini mama nimempenda eti ni mzuri hata kuliko Tom.



    "Ni sawa lakini ukishakuwa malikia utafanya yote hayo uyatakayo cha kwanza nataka uwe, malikia ukishakuwa malikia wa Isadora basi utaweza kuiendesha nchi nzima hii kwani Ndiyo kijiji chenye mali nyingi za utajiri kuliko vijiji vyetu" alizungumza malikia Samela aliyeonekana kuwa uchu na madaraka tu.



    "Pia nasikia vitu kutoka kwa watu weupe vinapatikana kwa wingi kwao, we hutaki vitu vizuri, tena unaweza ukapata na mtu mweupe huko huko ukaamua kuolewa naye na ukaachana tena na huyo Hancy unayemng.ang.ania"



    "Kwahiyo mama Unataka kusema kuwa naweza nikaolewa na mtu mweupe kupitia Tomimo"



    'Nashukuru kwa kunielewa"



    ***** ****** ****



    "Nimekuita hapa natak kujua kama kile ulichoweza kukiongea kina ukweli wowote"



    "Mfalme Nuhu, sikuwa natania kama utaweza kuniruhusu kufanya hivyo, basi nitamuowa Mozah"

    Alijibu Hancy.



    "Sawa, nmekuelewa" alizungumza mfalme Nuhu na kuinuka alipokuwa amekaa.



    "Lakini mfalme Nuhu samahani,nilitaka kuuliza, kwanini hutaki binti yako aolowe na mtoto wa mfalme wa kijiji cha Isadora??



    " siyo kwamba sitaki, bali ndoa itasababisha damu nyingi kumwagika na damu zilizoweza kumwagika kwaajili ya mapenzi katika kijiji hichi zinatosha" alizungumza mfalme Nuhu.



    "Hapo sijakuelewa" alizungumza Hancy kwa kusita sita.



    "Huwezi nielewa wala" alizungumza mfalme Nuhu na kutoka njee.



    "We Hancy...... Aliita Mozah baada ya kumuona Hancy, akitoka katika chumba cha mfalme Nuhu.



    Hancy alitabasamu na kumfuata Mozah ambaye alimshika Mkono na kuanza kumpeleka mahali anapopajua yeye.



    Hancy alikuwa akitabasamu tu na kutazama mkono wake uliokuwa Mkononi mwa Mozah.



    ****** ****** ******



    Katika mji au kijiji kikuu cha Isadora alionekana mfalme wa mahala hapo akiwa na mkewe Naligita.



    " Ila mume wangu,sifikiri kama mbinu anayoitumia Hancy, inafaa kwa jamiii na uhakika atakosa mwanamke na atarudi hapa nyumbani, tena nilitaka kukwambia mtoto wa yule governor wa kimarekani Sarah anakuja tena Tanzania unaonaje tukamuozesha kwa Hancy "



    "Natumaini sasa umemaliza kuongea ; Hancy atamuowa mwanamke kutoka katika nchi yetu hii hii na tena atamchagua mwenyewe kwa mapendekezo yake mwenyewe" alizungumza mfalme na kumpita malikia kwa kuongeza hatua za kutembea zaidi.



    "Mfalme wangu" aliita Naligita ila tayri mfalme alikwisha ondoka.



    Alikuja kijakazi mmoja na alitoa heshima kwa malikia kwa kuigusa sehemu ya juu ya paji lake la uso na kuinama mbele ya malikia ambaye alimgusa na unyayo mgongoni na kumfanya ainue kichwa chake.



    "Kijiji alichoko Hancy, nakitambua" alizungumza mfanyakazi yule na mama yake na Hancy alipiga atua za mbele na kutabasamu.



    ****** ***** *****.



    "Me sitki mazoea na wewe wala sitaki kuolewa na wewe" alizungumza Mozah.



    "Kwanini hutaki kuolewa na Mimi"



    "Mimi na wewe na watu wawili wa nafasi tofauti, wewe ni kijakazi tu japo kuwa lile li Tom limesema wewe sijui ni ndugu yake na Mimi ni binti wa pili wa mfalme, hata iwe vipi siwezi olewa na kijakazi" alizungumza Mozah.



    "Na ikiwa Mimi Ndiyo mtoto wa mfalme wa Isadora je utakubali nikuowe??? Aliuliza Hancy na kumsogelea Mozah kwa makini.



    " una...una....ongea nini wewe......kwanza sogea mbali na Mimi unanifanya mpka nashindwa kuzungumza alizungumza Mozah na kuanza kutazama chini.



    "Bado hujanijibu swali langu alizungumza Hancy.



    " sitaki kwenda mbali na kijiji chetu" alijibu Mozah.



    "Basi nitakuowa na nitaishi hapa na wewe" alizungumza Hancy.



    "Sitaki.....sitaki.....sasa kwanini unaning.ang.ania??

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Na wewe kwanini unanikataa?? Aliuliza Hancy na kumsogelea karibu zaidi.



    "Nyie wakaka wazuri huwaga mnapenda sana kutongoza kila mwanamke, kwhiyo nakuogopa, tena kama mfalme ndo atataka kuowa wanawake zaidi ya wanne, sitaki kupata shida Mimi juu ya mwanaume mmoja" alizungumza Mozah.



    Hancy aliishika mikono ya Mozah aliyekuwa akitetemeka kwa uwoga.



    "Mozah, nakuahidi ya kuwa sitaowa mwanamke mwingine tofauti na wewe, kama ilivyokuwa kwa baba yangu Mimi na baba yako wewe, tena nitakupenda wewe, mwenyewe tu kwa siku zote za maisha yangu na.......alizungumza Hancy na kusogea Karibu kabisa na mwili wa Mozah uliokuwa ukitetemeka.



    Alimshika mabega na kufanya Mozah kusisimuka mwili mzima na kujikuta akitoa sauti ambayo iliweza kufika katika kuta za ngome za masikio ya Hancy ambaye alishusha pumzi ndefu.



    " Tafadhali niruhusu nikuowe" alizungumza Hancy na kuteremsha macho yake chini ambayo yaliweza kukutana na uso wa Mozah aliweza kuuinua kwa kutumia Mkono wake mmoja.



    "Tafadhali Mozah olewa na mimi" alizungumza Hancy na Mozah alikiitikia tu.



    "Abeeee"



    "Nataka nikuowe, na nakuomba usikatae ombi langu" alizungumza tena Hancy.



    Kabla hajatoa jibu Mozah, Samela aliweza kufika pale na kusimama.



    "We kijana inavyoonekana adabu hauna kabisa" Alizungumza samela na kupita.



    "Me naenda alizungumza Mozah na kuondoka eneo alilokuwepo.



    " Mozah!!! Aliita lakini na yeye aliweza kuitwa na malikia Samela.



    Alimfuata malikia Samela.



    "Nataka kujua kitu kuhusu mtoto wa mfalme, embu nifuate" alizungumza na kuongoza njia .



    "Je alishakutamkia hata Mara moja juu ya mwanangu, Sikitu??



    " hata kuwaza hajawahi" alijibu Hancy.



    "Una uhakika gani kwani wewe ndo yeye, nataka kujua vitu gani anavipenda ili Sikitu aweze kuvifanya mbele yake??



    " hapendi mwanamke ambaye atampenda yeye kutokana na wadhifa alionao. Alijibu Hancy.



    "Huko mjini kwenu, nasikiaga watu weupe wanakujaga kweli??



    " Ndiyo"



    "Waooo mtoto wangu akiolewa katika familia ile, basi atapata bahati ya kuwaona watu weupe kila Mara na atakuwa malikia wa nchi nzima, Mimi nikiwa mama wa malikia, chochote nitakachotaka nitapewa tu nitaishi maisha ya raha sana jamni" alizungumza malikia na alipogeuka alikutana na macho makali ya Hancy.



    "Nini mbona unanitizama kwa macho mabaya hivyo??



    " Hamna; kama umemaliza maswali yako me naenda"



    "Sawa ila nina ombi la mwisho, alimpa ishara mfanyakazi wake ambaye alienda akafungua kiboksi kidogo na kutoa vito vya dhamani kisha akaitoa cheni moja na kumpatia Hancy.



    " chukua hiyo kwani ni kama ahsante kwa kunipa taarifa za mtoto wa mfalme, pia alikisogeza kiboksi kizima chenye vito vya samani na kusema



    "Ukinisaidia Sikitu, aolewe na Tomimo, basi nitakupa zaidi ya hizi, ila nachotaka sasa ni umshawishi Tomimo ampende Sikitu, kwasababu wewe tayari umeshampenda Mozah, na usipofanya hivyo basi Tomimo atamchukua Mozah na hutakuwa na uwezo wa kumuowa umpendaye"



    Alionekana baadaye Hancy akilalamika.



    'Mwanamke mpuuzi huyu, sijawahi onaga mwanamke mpumbavu, na mjinga kama huyu.....na kama siyo uwepo wake basi Mozah angekuwa ameshalijibu swali nililoweza kumuuliza , lakini kwasababu yake huyu mmama huyo aliendelea kulalama Hancy na Tom alibaki akimtizama tu huku akicheka.



    ***** ***** ***** ***



    "Natumaini sasa tumeweza kuvunja ule utabiri ambao ulisemekana ya kuwa lazima damu yangu iwe ndiyo mmiliki wa kijiji hichi kwasababu nimezaliwa kwenye koo ya kifalme.......ila mambo yote yameisha sasa mjukuu wangu, anampenda kijakzi wa mfalme na hapo hatoweza kugombana na Mozah juu ya mwanaume wake huyo anayempenda alizungumza Bi Lunde na kutabasamu mbele alimuona mjukuu wake.



    " ooohoooooo mjukuu wangu huyo, njoo mama yangu njoo, hay niambie shida ni nini mbona kam unaonyesha kuwa na wasiwasi"



    "Hamna, ila bibi nataka kujua kuhusu kitu, mama Stela aliniambia ya kuwa mwanzoni wewe ilikuwa uolewe na mfalme lakini bibi Yake Sikitu aliweza kuingilia ndoa yako na akaolewa yeye huku wewe ukionekana haufai mbele ya mfalme, alafu baadye kidogo ukaja kuolewa na kijakzi wa mfalme ambaye ni babu yangu Mimi, Je hukujisikia vibaya kuolewa na kijakazi??



    Bi Lunde Alicheka na kusema umenikumbusha zamani kweli.



    " Hapana sikuweza kujuta kuolewa na babu yako hapana, kwasababu niliweza kumpenda yeye na alinipa maisha ya kawaida sana ambayo nayapenda mpaka Leo hii"



    "Bibi eeeee nataka kuolewa na Mtoto wa mfalme ili niweze kuirudisha heshima yako, nataka ule na uvae vizuri, na watu waweze kukuheshimu wewe pamoja na Mimi, nataka Sikitu aone Furaha yangu na ninaamini furaha yangu ndiyo nguzo kubwa ya kumteketeza adui yangu" alizungumza Mozah



    "Usipende kufanya kile kitu kinachomuumiza adui yako kwa makusudi kwani vitu vingine vinaweza kukuumiza wewe Mara kumi ya zaidi vinavyomuumiza adui yako, kwahiyo we fanya tu vitu vyote ambavyo vinakupendeza wewe, kwa hakika lazima vitamuumiza tu, Hivyo nikuulize kitu??



    " Ndiyo "



    "Kati ya mtoto wa mfalme na kijakazi yule, unampenda nani??? Aliuliza Bi Lunde.



    " abee" aliitika Mozah.



    "Kwa upande wangu yule kijakazi ndo umzuri bhna ; kwanza nywele zak; macho yake mwili wake yani akiongea sasa"



    "We bibi unaongea ni wewe kwanini unamsifia hivyo; ni mzuri kweli lakini tabia yake ndo hatujaijua" alizungumza Mozah na maneno Yale baba yake mfalme Nuhu aliweza kuyasikia na Mtabiri Tambitambi aliyekuwa nyuma yake alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo.



    Baadye kidogo aliweza kuonekena mfalme; mtabiri pamoja na Bi Lunde.



    Huku akionekana mtabiri kufumba macho yake na kutikisa kibuyu kilichoweza kuwa pembeni yake.



    Aliyafumbua macho yake na kutabasamu.



    "Kila kitu kimeenda vizuri" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Basi itabidi tumuozeshe Mozah kama kila kitu kipo sawa" alizungumza mfalme Nuhu.



    ****** ****** *****



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo alionekana Hancy akiwa anamsubiria mtu maeneo ya mtoni.



    Huku akijitizama mtoni na kuweka nywele zake sawa.



    "Unaangalia nini?? Aliuliza Mozah na kuachia Tabasamu.





    Ilipoishia ni baada ya Hancy kuweza kumuona Mozah nyuma yake.



    "Hamna, alijibu Hancy na kumtazama Mozah nguo alizovaa.



    "Unanitizama je hivyo?? Aliuliza na kuanza kuziba kifua chake kwani nguo hiyo aliyoweza kuvaa kifua kiliweza kuonekana kwa kiasi kidogo..



    " ahaaaa, kwanini unajifunika huko?? Aliuliza Hancy



    "Hamna, alijibu na kuachia mikono kwenye kifua chake.



    Hancy alimtizama tena kifuani na kumfanya Mozah arudishe tena mikono yake kifuani mwake.



    "Umenitia nini?? Aliuliza Hancy.



    " aaaammmmhhhhhh nataka unifundishe kuendesha farasi" alizungumza Mozah



    "Sasa nitakufundishaje kama mikono yako utakuwa umeiweka hapo masaa yote? Aliuliza Hancy.



    "Nitarudi ngomeni kwenda kuvaa nguo nyingine, kisha nitarejea tena hapa" alizungumza Mozah na kuanza safari.



    Hancy alimshika Mkono na kumsogelea kwa karibu zaidi kisha akauachia Mkono wake na kuupitisha kiunoni mwa Mozah ambaye wakati Mkono ukipitishwa aliweza kuyafumba macho yake na kujikuta akihema mhemo ambao hajawahi kuutoaga katika Maisha yake.



    Baada ya kuhakikisha mikono yake imeweza kukutana aliegeshea kichwa chake katika bega la Mozah na kuanza kumpulizia upepo katika shingo yake.



    "Ha.....ha....Hancy" aliita Mozah japo kwa shida.



    Hancy alipeleka mdomo wake katika shingo ya Mozah na kumbusu wakati huo nao mikono ya Mozah iliweza kukamatia gauni lake kwa nguvu zake zote.



    Wakiwa katika hali hiyo. Ghafla iliweza kusikika michakacho ya watu na waliweza kufika wazee wa kijiji, Mtabiri Tambitambi, Mfalme Nuhu, Malikia Samela, Binti wa Mfalme Sikitu pamoja na baadhi ya vijakazi wao.



    "Kamkamateni haraka sana"



    Hiyo ndo kauli iliyoweza kuwashtua Hancy na Mozah.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Baba!!!!



    " Mfalme!! Aliita Hancy.



    "Mpumbavu wewe kijana, unakuja katika kasiri yetu alafu unafanya vitu kinyume na mila na desturi za kijiji chetu' alizungumza Mfalme Nuhu na Hancy alishawekwa mikononi mwa walinzi.



    " Mfalme aliita Tom na kuweza kujitokeza mbele ya Mfalme Nuhu.



    "Tafadhali naomba adhabu yake iwe juu yangu" alizungumza akiwa amepiga magoti na kufanya watu wamshangae.



    "Ikawaje tena mtoto wa mfalme akataka adhabu ya kijakazi iwe juu yake??



    Waliweza kufika katika eneo la adhabu huku Hancy na Mozah wakiwa katikati ya kiwanja hicho.



    " adhabu ninayoweza kuitoa juu yenu ambayo imeweza kutolewa na wazee wa kijiji hichi pamoja na washauri, lazima itimie haijalishi mtataka au hamtataka ila lazima muitimize...



    Hancy kwa kosa la kumshika, kumkumbatia na kumpiga busu binti wa pili wa mfalme, adhabu iliyoweza kutolewa juu yako ni ufunge naye ndoa" alizungumza mfalme Nuhu na Hancy aliinua kichaa chake na kuanza kucheka.



    "Yani unasema adhabu yangu ni kumuowa Mozah?? Aliuliza tena Hancy na mfalme alitikisa kichwa kwa furaha



    " Haaaaa hiyo wala siyo adhabu me nilikuwa natak hivyo pia" alizungumza Hancy na kumtazama Mozah ambaye hakuwa katika hali ya udhuni wala furaha.



    Wakati huo nao Sikitu alimtizama mama yake na kutabasamu huku akikumbuka ya kuwa mama yake na yeye ndiyo waliyoweza kupanga fumanizi hilo ili Hancy amuowe Mozah na yeye abakiwe na Tom ili aweze kuolewa bila kipingamizi chochote.



    Mfalme Nuhu aliweza kutoa ishara na waliweza kuja wafanyakazi wanne wake wawili na waume wawili wakiwa wamebeba mavazi ya harusi.



    Hancy aliweza kusimama na kuyafuata mavazi Yale.



    "Tafadhali naomba ruksa nikamvishe nguo hizi" alizungumza Tom na mfalme alimpa ishara mfanyakazi ampe nguo hizo Tom ambaye alimshika na Hancy na kuelekea katika chumba chao kwaajili ya maandalizi ya harusi.



    Stela na yeye aliweza kuomba ruhusa ya kwenda kumvika nguo Mozah.



    Wakiwa ndani ya chumba chao Mozah akionekana kuwa kimya



    "Vipi hutaki kuolewa naye??



    "Hapana siyo kwamba sitaki ila nadhani ni mapema sana eti mama, bado sijamjua vizuri alafu Leo nakimbilia tu kuolewa naye"



    "Me naamini Hancy ni mtu mzuri" alizngumza Stela.



    Huku nako Hancy alikuwa akimaliziwa kutengezewa nguo ya juu na Tom.



    "Unaonekana Leo unafuraha sana" alizungumza Tom.



    "Ndiyo, kwasabab nakwenda kumuowa mwanamke ambaye nampenda kuliko yani hata nashindwa kuelezea" alizungumza Hancy.



    "Lakini unajua kabisa Mozah hajafahamu wew ni nani, na hataki kuolewa na mtoto wa mfalme huoni kwamba utakuwa umemkosea kwa kiasi kikubwa sana" alizungumza Tom



    "Tom, katika Maisha yangu sijawahi fanyaga kosa hilo ndilo la kwanza nalifanya nani kwaajili ya furaha yangu na pia kwa ajili ya furaha ya Mozah pia, ila nitamwambia baada ya ndoa hii kama hatanitaka basi nitafanya chochote kile akitakacho yeye" alizungumza Hancy



    "Twende njee" alizungumza Tom na kumpulizia upepo machoni Hancy.



    Hancy alitabasamu na kutoka njee huku akivuta pumzi ndefu.



    ***** *** **



    Malikia yuko wapi aliuliza mfalme wa Isadora.



    Wafanyakazi walibaki wakitizama na kisha kutizama chini.



    "Swali halijibiki?? Aliuliza mfalme.



    "Hapana..........alijibu mlinzi mkuu wa Jumba lile la kifalme. Jina lake Samweli.



    " Samweli.. Aliita mfalme.



    "Ndiyo mfalme."



    "Malikia yuko wapi?? Aliuliza tena mfalme.



    " njiani kuelekea katika kijiji cha Isambala"



    "Unasema?? Aliuliza Mfalme kwa sauti ya juu na kuwafanya vijakazi wanaomuekeaga ulinzi malikia kupiga goti na kuweka mapanga yao mbele ya Mfalme.



    ***** ***** *****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog