Search This Blog

DAMU YA MWANANGU - 5

 







    Simulizi : Damu Ya Mwanangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    akatafakari nini cha kufanya,,wazo likamjia, akatimua mbio na kumuacha Matiku akiwa kasimama pale.

    Nyamwela akakimbia moja kwa moja mpaka kwenye eneo maalumu la kuegesha taxi,,akakodi taxi kisha akamsisitiza dereva aendeshe gari haraka kulifuata basi lililoondoka muda mchache uliopita...dereva huyo akafuata agizo la mteja wake....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kiukweli basi lile lilikwenda kwa mwendo wa kasi...hawakuweza kuliona kwa sababu lilikuwa umbali wa kilomita kadhaa.

    Dereva akaamua kuuliza,,"kunatatizo gani,,mbona unasisitiza niongeze mwendo hii ni hatari kwa usalama wa maisha yetu..

    Nyamwela akadakia na kusema,,"ni bora kufa kuliko nipoteze pesa zangu...

    Dereva huyo akashtuka akauliza kwa mshangao!! ,,"pesa? kwani ni kiasi gani cha pesa ulichokiacha ndani ya basi hilo?

    ambacho kinasababisha uhatariwhe uhai wako!

    Nyamwela akasema,,"ni bora hata zingekuwa milioni tano tatizo ni zaidi ya hizo!

    Dereva akamtazama Nyamwela kwa macho yq mshangao! kisha akauliza,,"ulikuwa umeketi kwenye kiti namba ngapi?

    Nyamwela.akatoa tiketi haraka mfukoni mwake..kisha akaitazama,,akasema,,"kiti namba 22....

    dereva akaendelea kuuliza maswali,,"uliziweka kwenye nini?

    Nyamwela akajibu haraka kwenye begi langu jeusi...mbaya zaidi begi hilo nililiweka juu ya kiti hicho!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ghafla wazo likamjia dereva huyo,,akajisemea moyoni,"ukisikia zali la mentali ndio hili,,,wacha nifanye jambo.

    akapunguza mwendo wa gari kisha akalisimamisha,,na kuliegesha kando ya barabara,,akashuka kutoka ndani ya gari!

    Nyamwela akahisi huenda dereva huyo anakwenda kujisaidia haja ndogo,,, lakini akastaajabu kumuona anaelekea upande wa mbele ya gari,,,punde si punde akafungua boneti ya gari hilo!

    akarudi ndani ya gari na kusema,,"gari limepata hitirafu..linahitaji matengenezo hivyo safari yetu imeishia hapa!

    Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa! akasema,,"sasa ndugu,,hapa nilipo sina hata shilingi...nilikuwa nategemea tukilipata basi hilo,,nichukue pesa zangu,,ili niweze kukulioa pesa zako...

    dereva huyo,,akajisemea moyoni,,"yani ungejua hata sina shida na nauli yako,,mimi nahitaji hizo milioni milioni...

    alijisemea maneno hayo huku akishuka kutoka ndani ya gari,,,

    Nyamwela akabaki akimtazama dereva huyo,,,ghafla wazo likamjia,,akajisemea moyoni,,"wacha nifungue mlango nitimue mbio,,naimani hatoweza kunikimbiza.....Nyamwela aliwaza hivyo..huku akiendelea kumtazama dereva huyo,,aliyekuwa upande wa nje ya gari.

    dereva huyo akajifanya anakwenda kujisaidia haja kubwa,,akazipiga hatua kukifuata kichaka kilichokuwa ndani ya pori dogo uoande wa pili wa barabara...

    akaingia ndani ya kichaka hicho!

    Nyamwela akaona huo mdio muda muafaka wa kutimua mbio...akafungua mlango taratibu akatimua mbio na kutokomea porini akajificha nyumba ya mti mkubwa,,akawa anachungulia kule barabarani,,akamuona ye dereva anatokea kichakani na kuingia ndani ya gari,,,,akaliwasha gari hilo akaliondosha kwa mwendo wa kasi!

    Nyamwela akaonekana akitimua mbio kutokea porini kuja upande wa barabara..alikimbia huki akipiga mayowe,,kuashilia dereva asimamishe gari hilo...lakini akastaajabu kuona dereva huyo anaendelea na safari,,badala ya kurudi alipotoka!

    Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa...akabaki kasimama katikati ya barabara huku kajishika kichwani! akaamua kuketi chini ya mti uliokuwepo kando ya barabara! akisubiri msaada wa lifti kwenye gari lolote litakalokatiza katika barabara hiyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Nyamwela.aliketi hapo chini ya mti kwa masaa mengi mfululizo..lakini hakuona dalili zozote za gari kupita katika barabara hiyo!

    akaamua kunyqnyuka na kuzipiga hatua akitembea katikati ya barabara.....alitembea umbali mrefu kiasi....



    wakati huohuo,,alionekana yule dereva wa taxi,,akiwa kalipata lile basi,,na kuchukua begi la Nyamwela,,akaingia nalo ndani ya taxi..akafunga milango na kufungua zipu ya begi hilo! akastaajabu kuona noti nyingi za shilingi elfu kumi kumi,,pamoja na nguo..akatoa nguo hizo na kuzitupa nje...akachukua pesa zote akazificha chini ya kiti alichokuwa amekalia!....

    akalitupa begi nje! akaliondosha gari lake kwa kasi ya ajabu...kuifuata njia ya kurudi.......



    Upande mwingine alionekana Nyamwela akiendelea kuzipiga hatua katikati ya barabara,,,akiwa kaweka mikono yake nyuma huku uwo wake ukionyesha kugubikwa na mawazo mazito!

    punde si punde akaona,ile taxi ikimpita kwa kasi ya ajabu,,akajisemea moyoni,,"nashukuru hajanitambua,,angenidai pesa yake ya nauli....Nyamwela alijisemea maneno hayo huku akiendelea kuzipiga hatua,,,

    alitembea umbali mrefu,,hatimae giza likaanza kutanda!

    akatazama huku na kule hakuona dalili zozote za mqkazi ya watu kuwepo jirani na eneo hilo!

    akaamua kupanda juu ya mti kwa lengo la kujihifadhi,,na kuepuka wanyama wakali,,kwa sababu eneo hilo limezungukwa na misitu yenye wanyama wakali!

    alikesha usiku kucha akiwa juu ya mti huo,,hatimae pakakucha...akatelemka kutokq juu ya mti huo,,na kuifuata barabara,,,akawa anatembea kando ya barabara hiyo,, huenda akapata msaada lift ya gari lolote litakalo katiza katika barabara hiyo! kwa mbali akaliona moja kati ya mabasi ya kampuni ya basi alilolipanda jana...akafurahi,,,akiamini huenda akapata msaada...

    akaingiza mkono wake mifukoni mwa suruali aliyokuwa ameivaa,,akatoa tiketi akaishikilia mkononi,,kisha akanyoosha mkono wake akiashilia dereva alisimamishe gari hilo!

    dereva akapunguza mwendo hatimae gari likasimama...Nyamwela akaingia ndani ya basi hilo akaonyesha tiketi yake,,kisha akatoa maelezo kuwa jana alisahau begi lake katika moja ya mabasi ya kampuni hiyo....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    dereva akamuonea huruma akasema nitakupa msaada wa lift ufike dar es salaam,,huenda begi lako limehifadhiwa katika ofisi zetu..

    Nyamwela akasimama na kusikilia bomba, safari ikaendelea...

    baada ya mwendo wa lisaa limoja kupita,,,Nyamwela akaona nguo zinazofanaan na nguo zake alizoziweka ndani ya lile begi!

    lakini akapuuza,,ghafla akaona lile begi likiwa limetupwa kando ya barabara,,na linqonyesha halina kitu ndani yake!

    Nyamwela akapaza.sauti na kusema,,"simamisha gari nimeliona begi langa tumelioita.

    abiria wakamshangaa,,,ghafla ikasikika sauti,ya abiria mmoja akisema,,"bila shaka mtu huyu karukwa na akili,,atakuwa kachanganyikiwa!

    abiria wengine wakadakia na kumuunga mkono abiria aliyesema hivyo!

    Nyamwela akaendelea kusisitiza jamani simamisha gari begi langu tumeshalipita na nimeliona kwa macho yangu...

    aliongea maneno hayo huku akimvuta dereva,,,

    dereva huyo akaamua kusimamisha gari na kumfukuza Nyamwela atoke ndani ya gari,,akisema,,"sina uhakika kama unaakili timamu,,yani unanivuta,,wakati naendesha gari,,huoni kuwa unaweza kusababisha ajali? haya toka haraka ndani ya gari.

    Nyamwela hakujali akashuka na kutimua mbio kurudi walipotoka...alikimbia kwa kasi,,hatimae akalikaribia lile begi! akaliokota!! macho yakamtoka,,begi hilo lilikuwa tupu,,halikuwa na kitu chochote ndani yake!,,Nyamwela akaanza kulia huku anacheka,,vyote kwa pamoja!!!! alipogeuza shingo yake kulitazama.lile basi,,kama bado limesimama,,,mara ghafla!!!!

    TAHARUKI!





    Nyamwela.akastaajabu kuona basi linatokomea....punde si punde akaona lile gari dogo likiwa linarudi....akasimama kando ya barabara na kupunga mkono ishara ya kumuomba dereva asimamishe gari hilo!

    lakini haikuwa kama alivyotegemea,,hakuamini gari hilo lilimpita na kutokomea,,

    Nyamwela akaamua kuzipiga hatua,, akalifuata jiwe lililokuwa kando ya barabara ,akapumzika! ghafla akahisi kamuona Muna anakatiza barabarani,,macho yakamtoka,,,alipotazama kwa makini hakumuona tena Muna,,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaingiwa na hofu,,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,hakuona mtu yeyote!

    Nyamwela akanyanyuka haraka na kuanza kutimua mbio! kadri alivyozidi kukimbia,,ndivyo harufu ya damu ilizidi kunuka kwenye pua zake,,,akahisi mikono yake imelowana,,akasita kukimbia akatazama mikono yake,,akaona damu zilizoganda kwenye mikono yake! punde si punde damu hizo zikatoweka kimiujiza,,akajisemea moyoni,,"hii ni ndoto au naona kweli??

    kqmq ni ndoto,,mbona nipo macho sijasinzia!?

    alijiuliza.maswali yasiyokuwa na majibu...



    Upande mwingine,,lilionekana gari kubwa aina ya SCANIA likiwa katika safari,,,gari hilo lilipita katika barabara aliyokuwepo Nyamwela,,ghafla mvua ikaanza kunyesha,,,Mvua hiyo ilizidi kuongezeka kila baada ya dakika kadhaa,,hatimae ikawa mvua kubwa,,ikiambatana na upepo mkali....baada ya dakika kadhaa kupita,,,gari hilo likawa linapita eneo alilokuwepo Nyamwela!

    Dereva huyo akastaajabu kumuona mtu akiwa kasimama chini ya mti mkubwa huku mvua ikimnyeshea,,,

    akaingiwa na huruma,,akapunguza mwendo wa gari,, hatimae likasimama,,akapiga honi,,akachomoza mkono wake nje akifanya ishara ya kumuita Nyamwela!

    Nyamwela hakuweza kusikia sauti ya honi,,wala kutazama upande wa barabarani,,,muda wote alikuwa kainamisha  uso wake

    chini,,

    dereva wa lile gari,,akajisemea moyoni,,"bila shaka mtu huyu yupo katika dimbwi zito la mawazo! akaamua kuliwasha gari na kuliondosha taratibu,,

    wakati gari hilo linaondoka,,Nyamwela akashtuka! akahisi kama kasikia mlio wa gari! akanyanyua uso wake! akaliona gari hilo likiondoka,,akakurupuka na kutimua mbio kuja barabarani,,akalikimbilia gari hilo kwa nyuma huku akiita kwa sauti kali na kunyoosha mkono wake kuomba msaada...

    yule dereva akamuona Nyamwela,,kupitia kioo cha pembeni!

    akaamua kusimamisha gari hilo! Nyamwela akalifuata kuomba msaada wa lifti.....lakini alipotazama upande wa dereva,,,akashtuka,macho yakamtoka! akashangaa kumuona Muna akiwa kaketi kando ya dereva huyo,,huku kashikilia tumbo,,na damu nyingi zikimtoka,,,Muna alikuwa akimtazama Nyamwela kwa macho ya masikitiko huku akilia kwa uchungu!

    Nyamwela akaogopa sana! akazipiga hatua kurudi nyuma,, alipotazama tena ule upande aliokuwa kaketi Muna,,akastaajabu kutokumuona Muna,, kiti kilikuwa tupu! Nyamwela akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana!

    Dereva akabaki na mshangao,,akijiuliza,,"mbona mtu huyu anaonekana kuwa na hofu kubwa,,kwani kaona nini ndani ya gari hili,,mbona kakimbia?

    baada ya sekunde kadhaa kupita dereva huyo akaliwasha gari na safari ikaendelea..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo, upande mwingine alionekana Nyamwela akiwa amejikunyata chini ya mti uliokuwa na matawi mengi,,maji ya mvua yalipita kiadi katika matawi hayo,,lakini baridi lilikuw akali kupita kiasi,,kutokqna na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi...mvua iliendelea kunyesha mfululizo ikiambatana na ngurumo za radi,,hatimae giza likaanza kutanda kabisa...hali hiyo ilimfanya Nyamwela azidi kuogopa....kwa mbali akamuona mtu akizipiga hatua kuja upande aliokuwa amesimama,,mtu huyo alipokaribia eneo hilo,,Nyamwela.akashtuka kumuona Muna akiwa akasiamam mbele yake,,punde si punde Muna akatoweka kimiujiza,,,Nyamwela akaanza kuoiga mayowe huku akitazama huku na kule,,,ghafla radi ikapiga kwenye ule mti aliokuwa amesimama chini yake,,mti huo ukapasuka katikati..na kumdondokea Nyamwela,,ukamkandamiza akafa papohapo!



                        ********MWISHO********





0 comments:

Post a Comment

Blog