Simulizi : Merisa Jini Mwitu
Sehemu Ya Nne (4)
“naam! Ni mimi Geb niko hai rafiki yangu na nina wiki ya tatu tangu nirudi nchini,ila matatizo tuu ndugu yangu yamenifanya nipoteze kila kitu”aliongea kwa huzuni huku akijitahidi kumsogerea Dav ambaye alikuwa akitokwa na kijasho chembamba cha uwoga “ usiniogope Dav mimi sikufa na wala sijafa kwani ni nani kati yenu aliishuhudia maiti yangu?” aliuliza swali Geb huku akijitetea iliawezekumuweka sawa Dav wa weze kusaidiana juu na namna ya kumwambia anna kuwa yeye bado yupo hai
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ni,,,ni kweli Geb sikupata kuona mwili wako pahali ukiwa mfu ila ishasemekana hivyo na kila mtu anajua umefariki”dav alijitetea huku akijitahidi kupunguza uwoga aliokuwa nao
“naelewa yote hayo Dav tangu siku ya kwanza nawasili nchi hii Roby ndiye alikuwa kimbilio langu kwa kila namna nilitamani sana kuondoka na kuenda kuanza maisha yangu mapya ughaibuni ila imeshindikana maana kuna vitoyangu ya thamani kubwa sana nimeiyacha Tanzania , Dav naomba unisaidie kuonana na anna najua wazi kwa hali aliyokuwa nayo sasa kupitia wewe ndo atanielewa mimi”
Lilikuwa niombi kutoka kwa Geb lakini pia lilikuwa amri katika akili ya Dav ijapo kuwa alitaka kujua ni wapi alikuwepokipindi chote hiko historia ile fupi aliyopewa Dav ilimsikitisha sana akajikuta naye akiamini juu ya uwepo wake Geb duniani kwani hakuwepo aliye shuhudia maiti yake ikiwa mfu ,walipanga siku ya kukutana na annana kumueleza ukweli juu ya yote yaliyotokea.
Kila mmoja alitahamaki baada ya kuambiwa juu ya ukweli kuhusu Geb,
“Masikini anna sasa itakuwa je?”Aliuliza marry ambaye naye alikuwa nyumbani kwa kina john wakilijadili swala hili
“tume panga baadaya Geb kesho kurejea hapa nyumbani atapigiwa simu anna na kuombwa aje mahali hapa ndio tutamueleza ukweli”alijibu Dav ambaye bado alikuwa haja amini juu ya kile alichokawa amekiona masaa machache yaliyopita .
Siku ilipowadia Geb alisindikizwa na Roby mpaka kwa kina Dav ambako ndiko aliko kawa akiishizamani kabla ya kwenda safari yake ya cannada, alipofika alipokelewa vizuri nawenzake kila mmoja alikuwa ananafsi ya uoga isipokuwa Dav peke yake kwani ndiye aliyekuwa wa kwanza kugundua kama Geb alikuwa hai baada ya nusu saa mlango uligongwa ambapo wote walikaa kimya na kusikiliza kwa mara ya pili mbapo mlango uligongwa tena Dav aliinuka na kuenda kuchungulia aliyekuwa akigonga hamadrasuli alikuwa anna ambaye alipigiwasiu muda mchache akiitwa kukiwana jambo muhimu alihitajika kulijua kuhusu Geb, Dav alifungua mlango na kumkaribisha anna mpaka ndani ambapo anna alipoingia tuu aligonganisha macho yake namtu aliyefanana zaidi na Geb alihisi uwenda alikuwa ndotoni ghafra akagonganisha macho yake na Roby alilikumbuka vyema lile tukio la kupewa msaada kule makaburini na pamoja na kulipiwa pesa ya bajaji na kaka huyo ambaye haku bahatika kumjua kwa jina hivyo ilimbidiasiwe na uhakika kwa ndo mwenyewe au amemfananisha aliyazungusha macho yake na kutua katika kila point ya kila mtu aliyekuwepo mahali pale mara Geb aliinuka na kumfata anna pale alipo anna ambaye alijawa na uwoga kw kushuhudia maiti aliyezikwa kwa kusadikika kuonekana tena hai mahai pale
“samahani mpenzi najua utajiuliza na kudhania mengi sana juu yakuniona mahali hapa mtu ambaye uliambiwa atakuwa amekwisha fariki baada ya kutafutwa sana ndani yam situ ule , ni kweli ilikuwa ngumu sana kwa yeyote Yule kuniona mahali nilipokawa nimehifadhiwa kwani himaya ya kifalme ya jinni mwitu iliyopo ndani yam situ ule walidhamiria kunipoteza ki kweli ndipo nilipojikuta nikiangukia mikononi mwa mwanamke wa kijini na kujikuta nikipewamasharti chungu nzima ikiwa nisioe mwanamke yoyote Yule duniani isipokuwa yeye na iwapo nitafanya tofauti sito ishi kwa raha ndani yandoa mpaka pale atakapo amua yeye, mbali na hilo alinitaka niwe mtunzaji wasiri hii juu ya utawala wa majini mwitu ndani yam situ ule, na leo nimeamua kuitoa siri hii anna mbele yako ilikuweza kujitetea ujue ni nini kilitokea mpnz wangu” alimaliza maneno hayo na kutaka kumshika mikono kipenzi chake anna ghafra alimponyoka akikimbia pasi na kujulikana alikuwa akienda wapi wakati anatoka kwa kina Geb alipitiliza moja kwa moja kuvuka barabara ghafra gari ndogo aina ya IST ilikuwa ikikatisha nayo barabarani hapo ikiwa spidi ikamgonga sehemu ya kiuno tukio lile lilishuhudiwa vyema na Geb ambaye alikuwaakimfatilia anna kwa nyuma walimchukua na kumtia katika gari na kwenda naye hospitali kwa wakati huo hakuna aliyekuwa akijua kilicho mpata Anna sio kwa mama yake wala baba yake baada ya masaa mawili daktari alitoka katika chumba cha emagence alichokawa amelazwa anna na Geb ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kunyanyuka na kumfata dktari na kumuuliza hali ya mgonjwa
“naam doktar hali ya mgonjwa wangu inaendelea je?” lilikuwa swali baada ya salamu na daktari Yule
“mgonjwa wako yu salama nabado anafanyiwa uchunguzi pamoja na kupewa huduma ya kwanza ila kuna jambo siwezi kukueleza mahali hapa tafadhali nifate ofisine “ aliongea hayo huku akiusukuma mlango wa chumba alichokawa akikaa nakufanya shughuri zake kisha nakuketi akiatiwa na Geb ambaye alitawaliwa na uwoga juu yamsichana Yule kwani bila shaka hakuwa akiaga kwao kuwa anakwenda wapi na mara zote alikuwa akizuiliwa kuondoka kutokana na kupenda kwake kutembelea makaburini,
“Naam Mr Geb umesema mgojwa ni nani yako?”Aliuliza daktari
“ ni mpenzi wangu ambaye natarajia kufunga naye ndoa siku za hivi karibuni “alijibu kwa kujiamini Geb
“Ok sio tatizo pia ila mpenzi wako anatakiwa kufanyiwa upasuaji katika sehemu yake ya nyonga ambayo kuna mfupa nabaadhi ya mishipa imeleta itirafu sasa tulikuwa tunahitaji saini ya wazazi wake katika hilo maana ni mawili either kumpoteza mpenzi wako pasi na sisi kufanya lolote au kumuokoa nakukipoteza kizazi chake “ hilo lilikuwa pigo jingine ndani ya moyo wa Geb kwanza alijiuliza ni wapi ataanza kujielezea iliwaweze kuamini kuwa yuko hai na waweze kuaminikila kilichotokea ni kiini macho tuu,pia aliliona gumu jingine ambalo kwa vyovyote alistahiki kujitwika kichwani na kutembea nalo na anna kuto zaa maisha yake yote iwapo atapona alishindwa kuipa ruhusa akili yake kuamua lolote alitoka katika chumba cha daktari akiwa amelowa jasho mithiri ya mtu aliyemwagiwa maji machozi yalimtililika kama motto ilikuwa kama ndoto kwake au hadithi aliyosimuliwa zamani kidogo juu ya pendo la kweli “Dah kwanini mimi lakini?” ndiyo kauli iliyosikika baada ya Geb kutoka ndani ya chumba cha daktari .
Alisogea karibu kabisa na walipoketi wenzie kisha naye akaketi
“ kulikoni Geb?” wote walimuuliza kwa pamoja wakiwa na shauku ya kutaka kujua ni kipi kilitokea.
“itabidi tuende kwa kina anna na tuwaeleze juu ya hali ya anna na kuwaeleza uwepo wangu na kuwatoa katika sayari ya ajabu ambayo imebeba historia juu ya kifo change katika msitu ule”
“Mmmh kwani kimetokea nini tena Geb?”alihoji john
“tafadhali nisaidieni juu ya hilo mengine tutaongea tuu nikiwa sawa”hakutaka kuongea chochote mpaka atakapo hakikisha amewatoa wazazi wa anna katika ulimwengu ule wa ajabu walitoka pamoja nakuelekea palipo maegesho ya gari wakimuacha marry na janneth wakimuangalia mgonjwa na wao kufunga safari mpaka kwa kina anna.
Walipofika walimkuta mama anna akitoka nje kumwaga maji machafu aliyokawa akifulia
“ Hodi mama?” kabla ya salamu Dav alibisha hodi ilikupewa ruhusa ya kuingia ndani ya nyumba ile, kwa kuwa mama anna alikuwa akiwajua vyema Dav na John hivyo hakumpashida mtu wa tatu kati yao ambaye hakuweza kumuona vyema sura yake baada ya kuvaa kofia iliyoziba nusu ya uso wake
“Aaah kina baba hao karibuni jamani leo mumemkumbuka mke wenu, karibuni mpaka ndani?”aliongea maneno hayo huku akijaribu kumtazama vizuri Yule aliyevalia kofia alianza kuhisi kumjua kutokana na mwendo wake ila jibu halikuja kwa haraka nahata hakuweza kukumbuka wapi alimuona, waliingia mpaka ndani na kuketi “ shikamoo mama ?” walisalimia wote isipo kuwa Yule aliyevaa kofia CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ marhabaa wanangu, karibuni mkewenu katoka kama kawaida yake bila hata kuaga kaenda kulia makaburini huko ikifika jioni ndo anarudi” alijieleza mama anna akijua bila shaka walikuja kumtembelea anna
“Duuh kumbe ajaacha tuu, ila hiko sicho kilichotuleta mama, sisi tuna habari mpya na za kuhuzunisha kiasi vipi baba yupo ilituweze kuwapatia kwa pamoja?” aliuliza Dav ambaye ndiye mtu aliyechaguliwa Geb kuwatoa watu wote waliokuwa katika ulimwengu wakifo chake
“ mmmh ndio yupo ngoja niwaitie” aliyasema maneno hayo na kuingia ndani akiita kwa kupaza sauti “ baba anna! Baba anna!” ghafra ikasikika sauti ya kiume ikiitika “ naamu mke wangu “
“kuna ugeni huku ?”
“ugeni! ugeni upi huo ?” huku akitoka alipokawa ameketi na kusogea sebuleni ambapo alikutana na mama anna katika varanda aliyokuwa ameketi.
“ni rafiki zake na Geb” walisogea pamoja na kuketi wakiwasikiliza
“ Habari zenu vijana?” aliwasalimu
“salama shikamoo mzee?” wote kwa pamoja waliitikia nakusalimia sauti ya Geb ilisikika vyema masikioni mwa mama na baba anna ila hawakutaka kuamini hilo ghafra Geb alivua kofia aliyokawa ameivaa na kufanya aonekane vyema uso wake
Haikuwa rahisi kama ilivyo dhaniwa maana mama anna alianguka pale pale na kupoteza fahamu walimpepea na kumnyunyizia maji mpaka akazinduka Geb aliwaeleza juu ya kila kilichotokea na kuwafanya wote warudi katika ulimwengu wazamani ambao waliishi wakijua Geb yuhai, hakuishia hapo tuu aliwaeleza na juu ya hali ya anna hospitali ambapo ilihitajika saini zao iliaweze kufanyiwa upasuaji, kwa kuwa wazazi wa anna walikuwa na imani juu ya dini na ndani ya ufufuo jambo lile alikuwa watia shaka sana moyoni mwao ila walimuombea Geb kisha wakajiandaa na kwenda hospital ambapo waliweka saini na anna kufanyiwa upasuaji na baada ya masaa kadhaa alitolewa katika chumba cha upasuaji akiwa ajielewi na kupelekwa katika chumba cha emergency ambacho hakustahili mtu yoyote kumuona kwa wakati huo na alikuwa chini ya uangalizi mkubwa wamadaktari wakati wame keti kwenye benchi wkisubiri kupewa majibu ya mgonjwa wa mara daktari mmoja alitoka katika kile chumba alicho kawa amelazwa anna , geb na baba anna walimkimbilia wakimuita “ Daktari,Daktari?”
Aligeuka na kuwatizama kisha akawapa ishara ya kumfata nyuma kule aendako walifika mpaka kunako mlango ulioandikwa Daktari Room no. 3 waliketi na kumsikiliza
***************************
“Naamu! Na zani ni ndugu wa anna magesa?”aliuliza daktari
“ bila shaka”alidakia mzee magesa aliyekawa na shahuku ya kutaka kujua hali ya binti yake
“Mmh!!!! Mgonjwa wenu anaendelea vizuri ila tumefanikiwa kuokoa maisha yake na kufeli kukirinda kizazi kisizurike mpaka hivi sasa ninavyo waambia anna hato zaa maisha yake yote”kisha akawatazama kisha kasema tena “ nina imani Mr gablier nilikueleza haya kabla ?”
“ndio ni kweli hilo nalielewa amna tatizo kwangu” baada ya Maelezo yale walipewa ruhusa ya kutoka nje iwapo hawana la ziada.
Walipotoka tuu mama anna ndiye aliyekuwa wa kwanza kumluck mumewe na kumuulizakulikoni ambapo akaelezwa hali iliyotokea kiasi ilimuumiza ila swali lilibaki mioyoni mwao kuwa je Geb atakubali kumuoa anna katika hali yoyote ataayo kuwa nayo?
Siku hii hawakupewa kabisa wasaa wakuonana na mgonjwa kwani bado alikuwa ajarejewa na fahamu zake mpaka baada ya muda wa siku tatu hivyo atakula ma kumywa kwa kutumia mibomba na kupumua kwa kutumia oxygen mashine, siku ya pili walihudhuria pia hospitali japo waliata nafasiya kumuona mgonjwa ila alikuwasi wakusema wala kufungua macho mpka siku ya tatu ambapo asubuhi na mapema baba na mama yake walifika hospitalini na kuingia moja kwa moja katika chumba ambacho alilazwa anna ambapo walikuta madaktari wakimuandaa vizuri na kumtoa mipira yote walizuiliwa kwa muda wasiweze kumuona kisha baada ya dakika zile waliruhusiwa
“Shikamoo mama?” aliongea kwa sauti ya tabu anna
“Marahabaa mwanangu unaendelea je?”aliitikia mama anna na kumjulia hali binti yake wapekee
“Naedelea vizuri , lakini mama nimefikaje mahali hapa kwani mi naumwa ?” aliuliza na kutaka kuinuka kitandani ghafra akajikuta akisikia maumivu makali sehemu ya chini ya kitovu na kupiga kelele “mamaaaaa!”
“Pole mwanangu usiinuke kwa kasi hivyo utaumia sawa ?”Alimtuliza mwanaye huku akimlaza tena taratibu
“Kwani mama kitu gani kimenifika katika tumbo langu”aliuliza anna
“Uligongwa na gari kiasi ikapelekea mifupa ya kiuno chako kusigana hivyo wameiweka sawa “
“Ooooh ok!” alisogea karibu baba anna pia na akawaomba wafumbe macho kwa ajili ya maombi kwa mola wao iliazidi kudumusha afya ya motto wao baada tu ya maombi alisikika mtu akiingia ndani ya kile chumba huku akisalimia
“Shikamoni wazee?”ilikuwa ni sauti ya Geb ambaye alikuwa ameshikilia mfuko katika mkono wake wa kushoto, baada ya kuitikiwa salamu yake alijisogeza panapo usawa wake anna na kumbusu katika paji lake la uso wakati huo anna hakuwa mwenye kukumbuka chochote kilichotokea wala kumkumbuka yoyote hapo awali isipo kuwa baba na mama yake pekee hivyo hakuweza kumtambua Geb alikuwa ninani yake walakumkumbuka alikuwa kama yupo ndani ya sayari mpya, picha nyingi za zamani zilijificha.
Zilipita siku kadhaa na sasa Anna aliruhusiwa kutoka hospitali na kurejea nyumbani kubwa walilo ambiwa amepoteza kumbukumbu kwa muda ila pia atakuwa ni mtu wakuuliza maswali sana ninyema akajibiwa kweli iwapo kama mtu atakayekuwa akiulizwa atakuwa anajua ukweli juu yajambo atakalokuwa akiulizwa na hiyo pekee ndio itakuwa njia pekee ya kurejesha fahamu zake, maishayaliendelea na anna alikuwa akiishi na Geb kama mpenzi wake huku akiwa amesahau kipindi kifupi kilicho muumiza hapo nyuma hakuna aliyetamani anna ajue tena ule ukweli wa zamani na hasa Geb alihofia kuliondoa tabasamu ambalo kila leo liliongezeka katika uso wa anna.
Wakiwa chumbani wamepumzika anna alianza kumwambia Geb” hivi mpenzi mbona mimi nimejikuta tuu nakupenda wewe na nikijaribu kufikiri ni wapi tulikutana huwa jibu na kosa kabisa “
“kwani we unakumbuka mara y kwanzauliniona wapi?” aliuliza Geb ilikuhakikisha kumbukumbu za anna
“Mimi nakumbuka tu siku ile naumwa ulikuja hospitali kunitazama ndo mara ya kwanza kuonana na wewe”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Geb alitabasamu kisha akamshika anna mkono wake wa kushoto na kumtazama machoni “ mimi ni Geb anna Geb wako Yule wa kipindi kile unasoma ambaye nilikuwa nikisafiri kila kukicha na mara ya mwisho nilisafiri huku nikiwa nimeshakuvarisha pete ya uchumba “aliyasema hayo huku akiichezea pete ilipendeza vizur kidoleni kwa anna na kuibusu” pete hii nilikuvalisha siku moja kabla ya wewe kunitambulisha kwenu kisha nikasfiri na kwenda cannada kikazi kwa muda wa miezi sita sikuwa nchini na hatimaye nikapotelea huko na kuzaniwa nimefariki dunia”alimtazama anna usoni ambaye alikuwa yupo makini kuisikiliza hadithi ile ambayo ilikuwa na picha ya ajabu kichwani mwake ambayo ilikuwa ikikumbuka kila kilichojiri, wakati Geb anataka kuendelea kuelezea ilivyokuwa alishtuka kumuona anna akifumba macho na kulegea mithiri ya mtu aliyepoteza fahamu au kuaga dunia kabisa, alimtikisa bila mafanikio alimuita hakuamka alichukua maji pia haiku saidia alimpigia simu mama anna ambaye alikuwa nje akipika pikakwa ajili ya mkwe we.
Aliacha kila kitu na kuja kuangalia hali ya binti yake ambapo walipata wazo la kumchukua na kumpeleka hospitali ambapo walipewa jibu kuwa ni hali ambayo huwa inamtokea mtu aliyepoteza kumbu kumbu hasa siku atakayo fikiria sana juu ya jambo ambalo lilimfurahisha sana maishani au kumuumiza sana nahivyo ndivyo ilivyokuwa kwa anna kiasi daktari aliwatoa hofu ila aliwaomba warudi siku ya pili ilikuwezakuona hali yake inavyoendelea na wao walifanya hivyo ambapo siku ya pili walivyofika walimkuta anna akiwa na fahamu zake na akilia
“Kulikoni mama mbona kilio tena?”aliuliza baba yake anna huku akimsogelea binti yake na kumuweka sawa mara Geb naye aliwasili ile kuingia tuu akakutana na anna macho kwa macho anna alishtuka na kuanza kujivuta pembezoni mwa kitanda kila Geb alipokaribia na kutaka kumshika anna alitetemeka sana
“anna mama mbona unaniogopa hivyo?” alinungunika baada ya kuwa kafanikiwakumshika mkono
“Geb we siumekufa ni kipi kimekufanyauwe hapa leo?” maneno ya anna yaliuchoma vilivyo moyo wa Geb kiasi akajikuta akimkumbuka merisa mwanamke ambaye anaamini hakuwa mwema kwake na kumfanya aishi maisha ya ajabu tofauti na awali haikuwa kazi ngumu kumuelekeza anna juu ya yale yaliyotokea na kwa kuwa tayari wazazi wa anna walishalielewa hilo naye alimuelewa vyema Geb.
Baada ya masiku kadhaa annaaliruhusiwakutoka hospital na kurejea nyumbani mipango ya harusi ilifanywa upya ilikuhakikisha ndoto za wawili wale zinafikiwa ,siku hii Geb na anna walitoka pamoja kwa ajili ya kwenda kuangalia nguo za harusi watakazo zipenda pia kukodisha ukumbi wa sherehe za harusi hiyo vikao vya harusi vilifanywa kwa muda wa mwezi sasa na ndovilikuwa vipo mwishoni tarehe ya kharusi ilikaribia na watu kujipanga kushuhudia harusi ile iliyotikisa jiji la Dar es salaam kabla hata ya kufanyika kwaka kwake.
“Sikia Geb unastahiki adhabu kali kwa kila kosa ulilonitendea, nitakuadhibu kukaambali na mkeo kwa muda wa takribani miaka mitatu napo ndipo hasira zangu zitakapo fanikiwa kwisha nitamuadhibu mkeo pia kumfanya kijakazi wa himaya yangu”aliongea kwa ukali msichana mrembo aliyekawa amesimama mbele ya mboni za Geb na anna
“Jaman kwaninimekukosea jambo gani?”aliuliza Geb huku akimkumbatia vilivyo anna wake iliasije kuchukuliwa kimiujiza
“sikia Geb nilikuambia kwa mali nilizo kupa hupaswi kuishi na mwanamke yoyote isipo kuwa wakijini ila ninazo taharifa zako kuwa kesho ni kharusi yako,nilikuambia Geb iwapo utafanyajambo bila kunishirikisha utapotea na kupoteza ndoto zako zote “ alituli akacheka kwa dharau kishaakamsogelea tena Geb ambaye alimuogopa sana Yule msichana pili umefanya kosa ambalo unastahikihata kifo ,umetoa siri za himaya ya jinni mwitu kwa viumbe wenzio basi na wewe huu ndo mwisho wako” Ghafra alipotea na anna
“Merisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!”alipiga kelele geb kiasi nyumba nzima waliamka na kwenda kuangalia anatatizo gani kumbe alikuwa akiota
*******************************
“Vipi Geb?” alimuuliza anna huku akimuweka sawa
“ni ndoto tu mpenzi wangu tulale “ alijibu huku akijiweka sawa kulala tena ghafra mlango uligongwa
“ nani ?” aliuliza anna
“Mimi hapa fungua mlango kulikoni?” ilikuwa ni sauti ya mama ake na anna
“amna kitu mamailikuwa ndoto mbaya tuu”
“ndoto ndo makelele yote hayo?”aliuliza mama anna wakati tayari amekwishaingia ndani
“Eti baba kulikoni?”alimgeukia Geb na kumuuliza
“nikama alivyosema mwenzangu mama ni ndoto tuu”alijibu Geb akimtoa hofu mama anna kiasi mama anna akarudi zake kupumzika akimuacha anna na Geb mule chumbani.
“Mpenzi ni ndoto gani hiyo mbona umeshituka sana na kupiga makelele hukitaja jina la merisa ?”alihoji anna ilikuweza kujua ni kitu gani hasa kilimtisha geb ndotoni
“tulale anna kesho asubuh nitakuhadithia kila kitu”walivuta shuka zao vizuri na kukumbatiana mpka usingizi ulipo wachukua mwanga wa jua ulipita pembezoni kidogo mwa dilisha ambalo halikufunikwa vizuri na panzia kiasi mwanga uliwamulika usoni anna alikuwa wa kwanza kushtuka na kuitazama saa ya mezani ilikuwa ya pata saa mbili kasoro asubuhi
“we Geb tuna darasa leo kanisani la ndoa saa tatu kasoro na saizi saambili amka tujiandae” aliongea anna huku akimtikisa Geb,Baada ya muda mfupi walikwisha amka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kanisani walipotoka nje walikuta tayari mama anna amekwisha pika chai wakanywa na kumuaga mama anna wakaelekea kanisani sala ya ndoa ilisomwa na wanandoa wa tarajiwa anna na Geb walibarikiwa na mzee wakanisa kisha wakaombewa,Ilikuwa furahi isiyo na kifani kwa upande wa wapendanao hao wawili kabla ya kurudi nyumbani walipendelea kwenda beach kupanga familia yao na maisha yao baada ya ndoa waliongea mengi juu ya harusi yao , na familia ambayo wanatarajia kuijenga
“ILA Geb wenimwanaume wa ajabu sanasijawahi ona?”aliongea anna kwa sauti ya chini
“Kwanini?” aliuliza Geb
“ni dhahiri umeridhia kunioa hali ya kuwa sito kupatia motto ?” lilikuwa ni swali zito ambalo anna kwa kipindi chote hiko tangu kutolewa kwake kizazi alikuwa akilifikiria sana na kudhani awez kuolewa na mwanaume yoyote Yule
“sikia anna hata kama ungelikuwa na kizazi kama nimeandikiwa sito itwa baba na mtoto wa damu yangu mwenyewe basi sitoitwa tuu hata nikatambikemizimu ya kwetu” alimjibu anna kwa masihara ila alikuwa akikimaanisha walijikuta wakitabasamu baada ya jibu la Geb kumlidhisha anna
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“hivi hukuniambia uliota ndoto gani usiku ule wamanane?” aliuliza swali jingine anna ambaye alitamani kujua kilichomshitua Geb kiasi akamtaja mwanamke Yule wakishetani (merisa)ambaye anna alimuelewa vyema kutokana na historia nzima ilivyokuwa naalivyohadithiwa ni kweli merisa alikuwa msaada mkubwa sana kwa Geb tangu aliporudi kutoka cannada kwani tayari nafasi yake ya kazi ilikuwa imeshachukuliwa na mtu mwingine na hata mali zake zingine ziliandikwa kamamtu aliyefariki sasa zilihitaji kurithiwa na kwa kuwa Geb hakuwa na ndugu mali zile zilitawanyika bila kujulikana zimekwenda wapi lakini merisa alimpati kila kitu kwa sasa Geb alikuwa na nyumba yake mwenyewe,gari la kutembelea zuri kabisa na mbali na hayo geb alikuwa na biashara ambazo zilimsaidia pia kumuweka mjini kwa muda wote huo ambao yeye hakuwa na kazi ya kufanya .
“Merisa alinijia ndotoni kunamaneno aliniambia yalinitisha ghafra nikashuhudia akiondoka na wewe katika mazingira ya ajabu”
“Mmh na mm tena?” aliuliza anna huku akiwa na hofu kubwa moyoni
“ndio, ila usijali ndoa yetu imezungukwa na maombi mengi awezi kufanya lolote lile ila inabidi tuwe imara sana juu ya chochote kitakacho tokea mbele yetu”alisisi tisha Geb ambaye alikuwa akiihofia zaidi siku hiyo ikifika na namna ya kuziepuka harisa za merisa ilikuwa ni kwa kupitia maombi pekee, jioni walirejea nyumbani ambapo anna ilibidi akaendani siku kadhaa kabla ya kharusi mnamo tar 23 july yamwaka huo ndiyo ilikuwa siku rasmi ya wanandoa hawa kutambulika katika ulimwengu kuwa wao sasa ni tayari wanandoa.
Siku hii ilikuwa ya shamla shamla kubwa ndani ya jiji la dar es salaam kwa kila aliyeifahamu vyema historia ya wapenzi hawa wawili alitamani kuona siku hii wakiwa mke na mume tayari majira ya asubuhi anna aliamka na kujiandaa ilikuweza kwenda saluni akiongozana na wapambe wake na bila kukosa betha rafiki yake wa kipindi kirefu kwa upande wa Geb pia alikuwa sambamba na bestman wake Dav akifatiwa na Roby wakimsindikiza Geb saluni iliaweze kuwekwa ndevu nanywele sawa.saa tano kamili walihitajika kanisani kwa ajili ya kufungishwa ndoa. Geb ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasili akimsubiri anna baada ya muda kidogo anna alipokea simu akiwa saluni “baby kulikoni mbona mpaka saizi?” aliuliza Geb kwa sauti nzuri ya upole
“Nakuja mpenzi kuna vitu ninamalizia kuviweka sawa”
“Ok usichelewe basi maana tunakusubiria wewetu hapa”
“Ok mpenzi nakuja “alikata simu na kuitumbukiza katika pochi baada ya muda alikuwa tayari amekwisha wekwa sawa na kutoka saluni na wapambe wake
“Sikia kaka nakuomba usimamishe gari mara moja”aliomba anna baada ya kugundua ameisahau pochi yake kule saluni
“Kulikoni tena jamani?” alihoji betha
“Pochi yangu naomba turudi saluni nimeisahau pochi yangu”
“Mmh inakitu gani cha muhimu hivyo wacha miniwasiliane na Yule dada wa pale saluni atuhifadhie”
“Hapana betha wacha tukaichukue kuna simu yangu kule nitamtia hofu Geb iwapo atapiga alfu simu isipokelewe “
“Sawa basi we nenda na dereva sisi tutafute taxi ilitukawatie moyo unakuja au?”Betha alitoa wazo ambalo hakuwa na yakini juu ya kukubaliwa kwa wazo lile hatimaye anna alikubali nay eye akarejea saluni akiwa na dereva.
Yapata saa sita na nusu sasa anna hakuonekana kanisani kila mmoja alianza ingiwa na hofu simu yake iliita mpaka na haiku pokelewa na hakuna aliyekawa na taharifa zozote zile Geb alimtafuta betha na kumuuliza kulikoni
“Vipi shem yupo wapi mwenzio?”aliuliza Geb huku akiwa na hofu kubwa juu ya usalama wa anna siku ile kwani alijua vyema hasira za adui wake siku ilendio zilikuwa ziki zidi mara dufu
“Mmh mimi mwenyewe sielewi shemu tuliachana naye njiani ambako aliombakuifatilia pochi yake aliyoisahau saluni”
“we shemu inakuja kweli unamuacha bi harusi mwe….”kabla ajamalizia simu yake ya mkononi iliita ilikuwa namba ya anna
“Hellow?” ilisikika sauti ya mwanaume shababi upande wa pili wa simu ile iliyomfanya Geb ashindwe kuelewa jambo lolote kabla ya Yule jamaa kujitambulisha “hellow” alijibu Geb kwa unyonge huku akitumia busara kubwa
“Samahani naongea na Mr Gabriel?”alihoji kuhakiki
“Naam ndo mwenyewe sijui naongea na nani na mwenyesimu yuko wapi?”alijibu huku akimporomoshea maswali mengine mawili mfululizo
“am..mimi ni daktari nilikuwa nakuhitaji hapa mwananyamala hospitali mara moja huyu binti kapatwa na matatizo kidogo”
***********************************
Baada ya maelezo ya daktari kumthibitishia kuwa anna alikuwa amepatwa na matatizo Geb alikata simu na kumfata baba yake na anna ambaye hakuwa na stori naye zaidi ya kumshika mkono na kuongozana naye mpaka katika maegeshoya gari na kuondoka wakiongoza kuelekea mwananyamala ndani ya gari mzee magesa ambaye ndiye baba mzazi wa anna alijaribu kuhoji kutaka kujua kilicho jili ila ilikuwa ngumu sana kwa Geb ambaye aliwaza adhabu atakayo kuwa amechaguliwa anna kwa ajili yake aliwaza kupotezwa na kubaki mwili pekee ambao baada ya muda ungezikwa kwa kusemekana amekufa na baadae roho iachwe huru itange tange tange ila pia aliwaza juu ya harusi yake aliyoifanya kwa gharama kubwa iwapo itavunjika aliwawaza watu wa heshima aliowahalika ndani ya hafla ile kwa jinsi watakavyo mchukulia aliikumbuka ahadi aliyopewa na merisa kupewa adhabu ya kutoishi na anna kwa miaka kadhaa macho yalikuwa yakimtiririka kila kona na kujikuta akijutia safari yake ya kwenda cannada, safari ambayo aliitilia shaka kabla hata ya kuondoka kwake ,safari iliyomuhalibia ndoto zake na siku hii iliyokuwa maalum kwake pia aliwaza uwenda yote ni juu ya hasira za mwanamke Yule wakishetani ( merisa) aliyekutana naye kipindi hicho wakati akiwa safarini cannada.
Baada ya dakika kadhaa walikuwa katika maegesho ya magari ambapo Geb alisimamisha gari na kupiga simu “nimefika nijechumba namba ngapi”alihoji kisha kukaa kimya akifatisha maelekezo kisha wakashuka na kuelekea kule ambapo Geb alielekezwa,walifika mahali nakuhesabu vyumba kutoka kulia cha kwanza mpaka cha nne ambacho kiliandikwa Emegence room yaani chumba cha dharura,wakati anaingia Geb alikutana uso kwa uso na sura iliyojawa damu kiasi ilikuwa ngumu kuelewa zaidi juu ya kilichotokea msichana aliyekavalia gauni jeupe la bibi kharusi gauni lote lilichafuka kwa damu alibaki akilalama kwa mauivu juu ya kitanda alicho lazwa alisogea moja kwa moja na kumshika anna kichwani”masikini anna wangu kulikoni mpenzi?” aliuliza Geb huku matone ya machozi yakimdondokea anna juu ya kifua chake ilimuuma Geb kwa kumuona anna katika hali kama ile ambayo alijua dhahiri ni adhabu za merisa ambayo alikuwa akimuadhibu mtu ambaye akustahili kupewaadhabu hiyo.
“naam” aliitika mzee magesa ambaye sasa ndiye ilibidi asimame kama mwanaume juu ya kusikiliza tatizo la mwanaye baada ya Geb kukosa kabisa nguvu ya kufanya lolote ila kulia tuu na kufikilia mwisho wa hukumu ya mateso ya merisa kwake ni lini/
“hali ya binti yako ni kama hvyo unavyoiyona,binti yako amefikishwa mahali hapa na wasamalia wema baada ya gari alilokawa amepanda msichana huyu kuacha njia na kugonga mti hali ambayo imepelekea vipisi vidogo vidogo vya vioo kuingia ndani ya mboni za binti yako na kuziba kabisa nuru iliyopelekea kuto kuona chochote tangu hapo”
“Daaah kwa maana hiyo mwanangu nikipofu tangu sasa?” aliuliza tena mzee magesa iliaweze kupata uhakika ila halikutoka jibu tofauti na la kwanza ni kweli anna alikuwa amekwisha nyang’anywa uwezo wake wa kuona
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“masikini mwanangu”aliongea kwa masikitiko makubwa akionyesha kuumizwa na hali iliyomfika anna kwawakati ule ila daktari hakuishia hapo tuu “na ila dereva aliyekuwa akimuongoza binti yenu amefanikiwa kutoka akiwa salama ila amechanika kidogo sehemu ya mkono wake na kioo cha gari hilo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment