Search This Blog

SHUHUDA - 1







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Shuhuda

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Usiponiambia ukweli nitatoboa macho yako... alisikika akiongea maneno hayo mpelelezi karimu... ni baada ya kukamatwa majambazi waliovamia benki lakini hawakufanikiwa kutoroka na pesa walizokuwa wameiba benki ya NMB... wakati wanatoka walijikuta wamezungukwa na mapolisi upande wa nje.. kutokana mapolisi walikuwa wengi... majambazi hao waliamua kusalimu amri.. na kuweka siraha zao chini walikuwa wawili... lakini mmoja alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kukimbia..."""yule jambazi mmoja aliyekuwa amebaki alikamatwa na kupelekwa kupelekwa polisi kwa upelelezi zaidi... akiwa kwenye chumba cha mateso....karimu alimpa mateso ya hali ya juu lakini jambazi yule aitwae Tito akusema chochote....ni kinanani anao shirikiananao.. karimu ariamuru jambazi yule arudishwe maabusu.....kisha akaondoka zake kwenda kufanya shughuli zingine..



    ************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana Mtu mmoja hatari sana anayeitwa Peter """"peter ndiye aliewatuma majambazi wale waende kuvamia benki... ghafla simu yake iliita na alipoipokea aligundua kuwa ni kamisna wa polisi alikuwa akimpigia.... alipoipokea simu ile alipewa taarifa kuwa kijana wake wa kazi kakamatwa... na kwa sasa yupo maabusu na siku ya kesho atapewa mateso ili aeleze ni kina nani anaoshirikiana nao hivyo tutakuwa matatani...

    Peter ni moto wa kuotea mbali aliandaa mpango u yule jambazi aliyekamatwa ili auwawe usiku huo huo asije akatoa siri... ilipofika majira ya saa tatu usiku... alionekena mtuhumiwa mmoja akiletwa mule sero.... mtuhumiwa huyo kumbe alikuja humo sero kwa kazi moja tu.. ya kumuuwa Tito... mtuhumiwa huyo alitumwa na Peter... na aliyefanya mpango wa mtuhumiwa huyo kuingizwa humo ni yule kamisna wa polisi....

    ilipofika majira ya saa sita alionekana kamanda wa zamu ya usiku huo akielekea kule sero aliyowekwa Tito pamoja na yule mtuhumiwa aliyeingizwa masaa machache yaliyopita... kisha kamanda yule alimuita mtuhumiwa yule na kusema kuwa anaitwa na kamanda kwenye ofisi ya mpelelezi.....mtuhumiwa yule alifunguliwa nakutoka nje kisha wakaanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye ofisi ya mpelelezi huku tito akiwa kabaki ndani ya sero.. baada ya dakika kadhaa mtuhumiwa yule alirudishwa mule ndani ya sero huku akiwa kashikiria mkate na chupa ya maji...kamanda wa zamu alifunga mlango wa sero na kuondoka zake... mtuhumiwa yule alimpa tito slesi nne za mkate..kwa sababu tito alikuwa na njaa hakula tangu jana alipokamatwa... alipokea mkate na kuanza kula.... wakati tito anakula mkate yule mtuhumiwa alikuwa akimtazama tito alivyokuwa akiishambulia mikate ile.. tito alipomaliza kula alipewa maji akanywa... walipiga stori na baada ya muda walilala..... mtuhumiwa yule alikuwa macho akisubiri kumuona tito akikata roho... kumbe mkate ule ulikuwa na sumu... hatari sana aina ya Thempiodical poison... sumu hii inauwa baada ya masaa matatu...na kifo chake huwa mtu anakufa ghafla..... baada ya masaa matatu kupita mtuhumiwa yule alinyanyuka pale alipokuwa amelala na kusogea alipokuwa amelala tito... alijaribu kumuamsha kwa kumtikisa... tito hakuamka wala hakuonekana kuvuta pumzi... mtuhumiwa yule aligunduwa kuwa tito kaishakata roho... aliichomoa simu aliyokuwa ameificha ndani ya suruali, na kumpigia peter kwamba kazi imeisha tayari. peter alifanya mawasiliano na kamisna wa polisi... baada ya dakika kadhaa kamanda wa zamu alikuja na kumchukua mtuhumiwa yule na kuondokanae..... walipotoka eneo zilipokuwepo sero mtuhumiwa yule aliachiwa na kuondokazake....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ************



    Asubuhi palipokucha mpelelezi karimu alijiandaana na kwenda kazini....alipofika alichukuwa faili la kesi ya yule jambazi na kuimgia ofisini kwake... kisha akaamuru jambazi yule aletwe.... alistahajabu baada ya kuambiwa kuwa jambazi yule amekufa ghafla usiku wa jana na maiti iko mochwari.... no kutakuwa kunamchezo unaendelea haiwezekani.. kabla ya kuzikwa lazima maiti hiyo ifanyiwe uchumguzi wa kina ili nijue nini kimemuuwa. alijisemea moyoni karimu""



    Karimu alifungua mlango wa ofisini kwake na kuondoka... alikwenda moja kwa moja mpaka hospitali ya Muhimbili.wakati anaingia ndani ya geti kuna mtu alikuwa akimfatilia nyuma yake..alipofika alijitambulisha kuwa yeye ni mpelelezi wa jeshi la polisi Tanzania... kisha akatoa kitambulisho chake cha kazi na kimthibitishia daktari anayeshughulika na maiti uoande wa mochwali...kisha karimu aliongozana na daktari yule mpaka kunako ndani kabisa ya mochwari... daktari aliuliza jina la marehemu kisha karimu akajibu Tito... daktari alielekea upande wa pili na kufungua jokofu... kisha akavuta maiti ile kuitoa nje ya jokofu.... na kuiweka kunako meza inayotumika kuanzaa maiti kabla ya kuwekwa ndani ya jokofu... kisha karimu alichukua grovs na kuzivaa kwenye viganja vyake... alizipiga hatua kuelekea pale maiti ilipokuwepo.... karimu alianza kufanya uchunguzi wake... kwa kuitazama kwa umakini mkubwa maiti ile.... hakuweza kuona jeraha lolote.... kisha alifungua macho ya maiti ile nakuyatazama kwa umakini wa hali ya juu.... karimu aligundua kuwa mtu huyu hakuuwawa kwa kunyongwa wala kupigwa.... alipotazama mwili wa maiti ile aligundua kuwa huenda marehemu alilishwa sumu.. kwa sababu ngozi yake ilibadilika na kuwa nyeusi zaidi huku vinyweleo vikitoa majimaji...

    karimu aliamua uchunguzi wa kidaktari uhusike... na kazi ya kuchunguza maiti hiyo ilianza....

    karimu alitoka nje ya mochwari na kumuacha daktari akiendelea na uchunguzi.... karimu alizipiga hatua na kuelekea alipokuwa amelipaki gari lake dogo aina ya IST... alifungua mlango na kuingia ndani ya gari lake huku akisubiri majibu ya daktari.



    ***********



    upande mwingine alionekana mtu akizipiga hatua kuelekea ule upande wa mochwari... mtu huyo alionekana kuvalia koti refu jeusi... na kofia ya soksi....mtu yule alipofika maeneo ya mochwari.. aliangaza angaza macho huku na kule.. kisha akafungua mlango wa mochwari na kuingia upande wa ndani...daktari alihisi kunamtu kaingia..nani huyo anayeingia bila ruhusa.!!! alijisemea moyoni... ghafla alisikia vishindo vya mtu akitembea... aliamua kusitisha kuendelea na uchunguzi akazipiga hatua kuelekea ulipokuwepo mlango ili aone ni nani kaingia bila ruhusa... alistahajabu hakuona mtu... kisha akaamua kurudi aendelee na kazi yake... ile anageuka akakutana uso kwa uso na yule mtu aliyeingia humo... kisha mtu yule alianza kumchoma visu vya tumbo mara nyingi bila idadi.. daktari alidondoka chini na kupoteza maisha....



    ***********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule upande wa nje karimu aliangalia saa yake ya mkononi na kuona kuwa zimepita dakika 45 hivyo daktari atakuwa kamaliza uchunguzi na kubaini nini chanzo cha kifo cha jambazi yule aitwae tito..

    aliamua kutoka nje ya gari lake na kufunga mlango wa gari..... alipogeuka aliona mtu akitokea ndani ya hospitali na kuelekea nje kabisa ya hospitali na kupanda pikipiki aina ya XXL BAJA na kutokomea kusikojulikana.....karimu hakumjali mtu yule kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea upande wa mochwari..alipofika kwenye mlango wa kuingia ndani ya mochwari aligonga mlango... kisha akaendelea kusubiri.... zilipopita dakika mbili aligonga tena..... lakini hakuona dalili zozote za mlango kufunguliwa.... aliamua kusogea na kusimama kando huenda labda daktari bado anafanya uchunguzi... alisubiri hapo mpaka lisaa limoja likapita... alistuka akaamua fufungua mlango na kuingia ndani yamochwari... alipoingia alistahajabu kukuta dakatari yule amelala chini huku damu nyingi zimetapakaa kwenye sakafu.... karimu alizipiga hatua za haraharaka na kusogea mpaka pale chini alipokuwa amelala daktari yule... alipomtazama aligundua daktari kafa... alipotazama mwili wake aligundua kauwawa kwa kuchomwa visu... karimu alijiuliza ni nani kafanya mauwaji haya!!!! ndipo alipokumbuka aliona mtu akitokea upande wa hospitali na kupanda pikipiki na kutokomea... akakumbuka uso wa mtu yule ulionesha wazi kuwa na wasiwasi....karimu alitoka mochwari na kukimbia kuelekea upande wa nje...



    Alipofika upande wa nje aliangaza angaza macho.. kisha akaingia ndani ya gari lake... kabla hajaliwasha simu yake iliita... alipoiangalia aligundua kamishna anampigia... akaipokea"" nakuhitaji ofisini kwangu muda huu.. ""alisema kamishna"" sawa bosi nakuja muda si mrefu" alijibu karim kisha akaliwasha gari lake na kuondoka kuelekea stesheni yalipo makao makuu ya jeshi la polisi..



    ****************



    upande mwingine alionekana peter akiendelea kupanga mipango ya kumuangamiza karim...peter aliingia ndani ya gari lake nakuelekea kwa mtu mmoja anaefahamika kwa jina la Gili"" mtu huyo alikuwa anashughulika na kuyengeneza vinyago vya kutisha walivyovitumia watu kuvivaa katika nyuso zao kwenye maonyesho au sherehe....kumbe gili alikuwa anatengeneza pia sira za bandia... kwa hiyo vinyago vilikuwa kama mwavuli wa kuficha kazi hiyo haramu.... punde peter alifika kwa gili...na kuitoa picha ya mwanamke kisha akamkabidhi gili""" ili atengeneze sura ya mwanamke kwa kutumia picha hiyo gili aliichukua picha na kuitazama kisha akasema kufikia jioni nitakuwa nimeimaliza kazi hii..... peter alizipiga hatua na kuondoka zake.. ilipofika majira ya jioni mida ya saa kumi na mbili... alionekana gili akiingia kwenye jumba la kifahari la peter.. alifunguliwa mlango na kuingia ndani kisha akafungua zipu ya begi lake dogo na kutoa sura ya mwanamke ya bandia na kumkabidhi peter..... kisha peter aliingia chumbani na kuchukua pesa... punde alitoka na kumkabidhi gili.....kisha gili aliondoka zake "" wakati gili anazipiga hatua kutoka nje......akatokimea kusikojulikana..



    ***********



    ule upande mwingine alionekana karim akishuka ndani ya gari lake na kuingia makao makuu ya polisi pale stesheni sentro....alizipiga hatua mpaka kwenye ofisi ya kamishna..aligonga hodi akaruhusiwa kuingia.... alipiga saluti kwa mkubwa wake wa kazi na kuketi.... kamishna aliuliza vipi kuhusu upelelezi wa kifo cha jambazi Tito???"'"

    kazi inakuwa ngumu kwa upande wangu kwa sababu kila muhusika anauwawa na bado sijabaini nini chanzo!!!! pia inaonekana muuwaji huyu ni mmoja na atakuwa na mtandao mkubwa wa kigaidi.. alijibu karim"""""

    kisha kamishna akasema ok nenda kaendelee na uchunguzi mimi nitalifanyia kazi swala hili.. """karim alinyanyuka na kutoka nje ya ofisi ya kamishna....



    karimu alipotoka...kamishna alichukua simu yake nakumpigia peter... kuwa makini... mtu huyu anaonekana kulifuatilia swalahili kwa undani zaidi... kamishna alisema kisha akakata simu...



    ****************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    siku iliyofuata peter alitafuta mwanamke mwenye umbo na urefu sawa na mke wa kamishna.... alifanikiwa kumpata kisha akampa maelekezo jinsi ya kuifanya kazi hiyo... na kumpa namba ya simu ya karim... mwanamke yule alikubali kifanya kazi hiyo"""kisha peter alimpa milioni moja na kumwambia hii ni utangulizi tu na baada ya kazi nitakulipa zaidi ya pesa hii.... peter aliondoka na mwanamke yule mpaka MOBI HOTEL.... walipofika peter alichukua chumba... aliingia ndani na mwanamke yule.... kisha peter akategesha kamera kila kona ya chumba kile...kamera hizo zilikuwa zikipiga picha kwa mfululizo kwa kuongozwa na kompyuta...... kisha peter alichukua sura ile ya bandia na kumvslisha mwanamke yule... huwezi kuamini mwanamke yule baada ya kuivaa sura ile alikuwa hana tofauti na mke wa kamishna........ kisha peter akamwambia mwanamke yule ampigie simu karimu... amshawishi aje katika chumba hicho.... mwanamke yule alifuata maelekezo aliyopewa na peter.... alifanikiwa kumshawishi karimu......

    karimu aliingia ndani ya gari lake na kuelekea MOBI HOTEL.. baada ya muda alifika... na kupanda ngazi kuelekea upande wa juu kilipokuwepo chumba hicho..... alipofika mlangoni alisita kugonga hodi... mara ghafla alihisi kama kunamtu anamfatilia kwa nyuma akimpiga picha.... alipogeuka hakuona mtu... aliamua kutazama kona zote hakuona mtu kwa mbali aliona mtu anaingia ndani ya gari huku akitazama upande wa juu ya MOBI HOTEL.. ile nazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba alichoelekezwa mara ghafla.



    Simu yake iliita alipoiangalia aliona ni yule mwanamke anampigia... aliipokea na kusema nimeshafika... kisha akakata simu.... alipoukaribia mlango alipiga hodi"" ingia mlango uko wazi" alisema mwanamke yule... karimu alifungua mlango na kuingia....alistahajabu kumkuta mwanamke ambaye hajawahi kumuona machoni mwake hata siku moja!!!! mwanamke yule alitabasamu na kusema karibu sana.... nimekuita hapa ninamazungumzo na wewe""ok haina shida karimu alisema hivyo... punde mwanamke yule alisoge kwa hatua za madaha kumfuata karimu pale alipokuwa ameketi..... na kumwambia unanikumbuka??? kuna siku tulikutana kwenye sherehe za maazimisho ya miaka 54 ya uhuru... ulinipatia namba yako""" karimu alipojaribu kuvuta kumbukumbu... hakuweza kumkumbuka...karimu akasema.. mbona sikukumbuki??? mmmh!! au ulikuwa unanijaribu??? alisema mwanamke huyo huku akimpapasapapasa karimu....



    ************



    ule upande mwingine alionekana peter akiwa anataza kwa makini kioo cha laptop yake aliweza kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya chumba kile kwa kupitia zile kamera alizozitegesha mule ndani.... alikuwa akipiga picha ya matukio yote yaliyokuwa yakiendelea mule ndani....



    **********



    kule MOBI HOTEL yule mwanamke alizidi kuifanya kazi aliyopewa..... aliendelea kumpapasa papasa karimu... karibu alistuka... bila shaka kutakuwa na kitu kinaendelea... alijisemea moyo... kisha akamsukuma mwanamke yule na kufungua mlango..... karimu alizipiga hatua kuelekea upande wa chini wa MOBI HOTEL....... aliingia moja kwa moja ndani ya gari lake na kuliwasha akaondoka zake.....

    kule chumbani yule mwanamke aliivua ile sura ya bandia.. kisha akavaa nguo zake na kuondoka zake.



    *************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine peter baada ya kupiga pocha za kutosha.... alichukuwa picha zile na kuziweka ndani ya bahasha.... kisha akachukuwa simu yake na kumpigia mtu... alikuwa akimpigia muosha magari ambaye alikuwa akiosha gari la kamishna......mtu yule alikuja mpaka nyumbani kwa peter... peter alimpa bahasha ile iliyokuwa na zile picha kisha akamwambia yule muosha magari kuwa kamishna akileta gari lake kuoshwa utaweka bahasha hiyo ndani ya droo ya gari.... kisha peter alimpa laki tano yule muosha magari..... akaondoka zake..



    ***********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog