Simulizi : Utajiri Wa Damu
Sehemu Ya Pili (2)
Niliwaza, ni nini anataka kuniambia mzee huyo, lakini akili ikagonga kuwa ni lazima itakuwa kuhusu mbwa-mtu.
Katika maisha yangu sijawahi kuona mbwa akiwa na sura ya binadamu. Niliwahi kusoma katika vitabu kitu kama hicho na nilikuwa nadhani ni mambo ya utunzi tu lakini sasa nimejionea laivu.
Mzee Mitimingi aliingia ndani na kutoka na begi jeusi, aliketi kisha akalifungua.
Alitoa noti nyekundunyekundu na kuzihesabu kisha kunipa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chepriska, shika hizi ni fedha zako, alisema. Niliona kama amechanganyikiwa kwa sababu alikwishanipa shilingi laki moja na shilingi elfu thelathini za kinyozi aliyekuwa akinikusanyia nywele za watoto wadogo.
Mzee ulishanipa fedha zangu na za kinyozi, sikudai chochote, nilimkumbusha.
Hapana, si nimekuambia kuwa nataka kukuambia jambo gumu na zito? Chukua kwanza huu mzigo.
***
Katika kituo cha polisi, Inspekta Ado alikuwa amejifungia akichambua majalada lakini yote yalihusiana na vifo vya watu mbalimbali.
Huyu Josefu Kumusi, alinyongwa kwa kuninginizwa mtini, Paulo Gunia naye hivyohivyo lakini Hamisi Mpepechere yeye kifo chake siyo cha kunyongwa kwa kuninginizwa bali aliuawa huko alikokuwa na kuninginizwa mtini ili ionekane alinyongwa, alijisemea Inspekta Ado kama vile kulikuwa na mtu aliyezungumzanaye.
Kifupi mezani kwake kulikuwa na majalada tisa na yote yalikuwa yakihusu watu kuuawa na watu wasiojulikana.
Mbaya zaidi ni kwamba hakuna hata mtuhumiwa aliyetiwa mbaroni.
Hili ni tatizo sana. Kwa nini wahusika hawapatikani? Ina maana wapelelezi wangu wana walakini? aliendelea kujihoji.
Baadaye alichukua jalada la mauaji ya Mpepechere na kuanza kulisoma.
Huyu Chepriska anaweza kujua kitu, kwa nini hawa wapelelezi wamemuachia? alijiuliza na kuamua kupiga simu chumba cha wapelelezi.
Haloo. Inspekta Ado hapa. Naomba mpelelezi anayeshughulikia kesi ya kifo cha Mpepechere aje ofisini kwangu, aliamuru.
Baada ya dakika tatu hivi, askari mpelelezi aliingia katika ofisi yake na kunyooka huku akiwa amekakamaa.
Jambo afande? akasalimia.
Jambo. Keti.
Askari yule aliketi na kusubiri bosi wake atampa maelekezo gani.
Nilikuwa napitia hili jalada la kesi unayoipeleleza nikaaona yule binti Chepriska umemuachia.
Ndiyo afande.
Kigezo gani kilikufanya umuachie?
Kama umesoma vizuri afande maelezo yake, sijagundua lolote la kumhusisha ndiyo maana siku iliyofuata tukaamua kumuachia lakini tulimuambia kuwa tukimhitaji tutamuita.
Kwani hukufanya uamuzi huu peke yako?
Ndiyo afande tulikaa jopo la wapelelezi na tukagundua kuwa huyu binti alikuwa mlevi tu ambaye alikuwa akikutana na marehemu baa lakini alikuwa hakujui nyumbani wala kazini kwake.
Mlifuatilia huko baa?
Nilifuatilia usiku uleule na mwenye baa ya Chambilecho alinihakikishia kuwa wote hao ni wateja wake ambao hawana uhusiano wowote.
Uliaminije hilo?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliamini kwa sababu mwenye baa alisema marehemu siku nyingine alikuwa akija na mkewe au mpenzi wake na kukutana na msichana Chepriska na kukawa hakuna malumbano wala ugomvi na binti huyo naye kwa siku kadhaa alikuwa akija na boifrendi wake na marehemu hakuwa akionesha kuchukia.
Inspekta Ado aliuma kalamu yake akawa anamuangalia yule askari wake wa upelelezi kisha akafunua jalada la kesi na kutoa simu yake ya kiganjani. Akabofya namba kadhaa, simu ikawa inaita kwani aliitegesha kwenye spika ya nje.
Akiipokea mwambie anahitajika hapa polisi.
Sawa afande.
Haloo, ni Chepriska anayeongea?
Ndiyo.
Tafadhali sana unahitajika hapa kituoni.
Sawa nakuja lakini nipe dakika ishirini kwa kuwa siko nyumbani na ni lazima nifike nyumbani kufunga mlango maana nyinyi polisi hamuaminiki.
Hatuaminiki kwani sisi wezi?
Hapana. Naweza kuja hapo mkanishikilia.
***
Chepriska baada ya kupokea simu akajiona ni mnyonge sana hali iliyomfanya mzee Mitimingi kuwa na wasiwasi.
Kwani hiyo simu imetoka wapi? Maana baada ya kuipokea umekuwa mnyonge sana, kulikoni?, akamuuliza.
Hii simu imetoka polisi. Wananiita .
Polisi wanakuita? Tafadhali sana usiwaambie kuhusu huyu mbwa mtu, ukiwaeleza tu, umeniiua, umeelewa? Mzee Mitimingi alisema hayo huku akiwa ametoa macho.
"Lakini mzee umeniambia kuwa utaniambia jambo zito, kabla ya hujasema simu imeingia, kwani huwezi kuniambia kwa kifupi?"
Aliniangalia akiwa amekunja sura kisha akasimama.
"Nilichokuambia hukielewi, kwamba nimekuongezea shilingi laki moja kwa ajili ya kuficha siri hii. Mbwa huyu hajawahi kuonwa na mtu yeyote isipokuwa wewe na mimi."
"Ni hilo tu?"
"Wee mtoto, kwani katika maisha yako umewahi kumuona mbwa kama huyu?"
"Sijawahi, kwani huyu ni mbwa au jini?"
"Swali gani hilo unauliza? Nilichokueleza umeelewa?" Alifoka huku akifuta jasho usoni.
"Samahani mzee."
"Nimepata wazo jipya. Hebu wapigie hao polisi na uwaambie kuwa leo huna nafasi kwa kuwa kuna dharura, waombe uende kesho."
"Lakini mzee nikifanya hivyo wanaweza kudhani kuwa nataka kutoroka?"
"Wewe waombe kama watakataa basi, nitakupeleka mimi."
"Sawa."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilichukua simu na kuipiga namba ya yule mpelelezi, baada ya kuita ikapokelewa.
"Inspekta Ado hapa."
"Aaah, nilifikiri ni simu ya mpelelezi wa kesi ya marehemu Mpepechere."
"Nani anaongea?"
"Ni mimi Chepriska."
"Aaah binti, ni mimi niliagiza wakuite, nahitaji kukuona."
"Nilikuwa nampigia mpelelezi wangu ili kumuomba nije kesho kwa sababu saa hizi nampeleka mzee wangu hospitali anaumwa," nilimdanganya.
"Kwani sasa hivi upo wapi?"
"Nipo Mtaa wa Mizambarauni nyumba namba kumi na mbili."
"Sawa lakini mpelelezi atakuja kukuona jioni nyumbani kwako."
"Sawa mzee na nashukuru kwa kuniruhusu."
Nilikata simu na kumuangalia mzee Mitimingi.
"Wanasemaje? Wamekuruhusu?" aliuliza mzee Mitimingi huku akinikodolea macho.
"Wameniruhusu. Nimeongea na bosi wao."
"Mbona umeitaja namba ya nyumba yangu?"
"Nimewaambia wewe mzee wangu unaumwa, nakupeleka hospitali."
"Una akili sana binti wewe na ndiyo maana napenda sana uwe unafanya kazi zangu na safari hii ni lazima nibadili maisha yako yawe ya kifahari."
Alifikiri kwa dakika kama moja hivi kisha akachukua juisi na kuinywa, akaniangalia, akasema:
"Kumbe ulikuwa na namba ya bosi wa wale wapelelezi?"
"Nilikuwa sina kumbe yule mpelelezi alitumia simu ya bosi wake kunipigia."
Wakati wanaendelea na mazungumzo yao walipigwa butwaa baada ya kuliona gari la polisi Defender' likipiga honi kwenye geti.
Bahati nzuri mlinzi ambaye sikujua awali alikuwa wapi, alifungua geti na taratibu gari likaingia ndani.
"Jifanye mgonjwa," nilimnong'oneza mzee Mitimingi.
Naye kisanii akawa ameegesha shingo yake upande pale kwenye kiti cha sofa alichokuwa amekalia.
Lile gari lilisimama hatua chache kutoka pale tulipokuwa tumeketi na mzee Mitimingi.
"Karibuni sana," nilisema huku nikijifanya sina hofu nao. Askari watatu walishuka, miongoni mwao alikuwepo askari wa kike. Nilihisi kwamba wamekuja kunikamata kwa sababu kwa sheria za polisi mwanamke hukamatwa na askari wa jinsia yake.
"Huyu ni mzee wangu, lakini siyo baba yangu mzazi ni wa kunilea."
"Sawa. Mimi ni Sajenti Mbegu na hawa ni wapelelezi bila shaka huyu wa kike unamkumbuka."
"Namkumbuka, ndiye aliyekuwa akinihoji pale kituo cha polisi."
"Huyu mzee wako anaitwa nani?"
"Ni mzee Mitimingi."
"Haah kumbe mzee Mitimingi ndiye huyu? Ni maarufu sana kwa sababu huwa naona mabasi na malori yake sehemu mbalimbali hapa mjini yakiwa yameandikwa jina lake."
"Bahati mbaya mmekuta anaumwa."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siyo mbaya kwa sababu yote ni mipango ya Mungu."
"Karibuni, sijui mnatumia kinywaji gani?"
"Wewe tuletee juisi tu, hakuna mnywaji wa pombe hapa."
Niliingia katika nyumba ya mzee Mitimingi japokuwa sikuwa mwenyeji mle ndani lakini nilikwenda moja kwa moja jikoni nikakuta friji.
"Khaaaa" nilisema kwa sauti. Nikafunga mdomo kwa mikono yangu kushangaa kile nilichokiona ndani ya friji.Niliona kuna kiganja cha mtu!!
Nilitaka kutimua mbio kurudi walipo askari lakini nikaona nikifanya hivyo tutakuwa tumejipalia mkaa maana hata mimi nitajiingiza katika matatizo.
Nilishika boksi moja la juisi nikaipasua na kumwaga kiasi chini kisha nyingine nikaweka kwenye trei na kuwaletea wageni.
"Vipi mbona tumesikia ukisema khaa?" aliniuliza yule askari wa kike.
Kabla sijajibu chochote nilimuona mzee Mitimingi akitetemeka, bila shaka alijua polisi wakikagua wataona maajabu ya mbwa-mtu na kiganja kwenye friji.
"Naona mzee amezidiwa, tumuwahishe hospitali," alisema askari mmoja.
"Nilifungua friji kwa nguvu nikaangusha boksi la juisi, likapasuka. Nitakunywa mimi hii, hizi juisi zingine ni zenu." Nilidanganya.
Kila mmoja nilimpa pakiti lake na glasi na wakaketi wakawa wanakunywa nami nikaenda alipoketi mzee Mitimingi nikawa namgusa shabu kuona kama ana homa kali (nilikuwa naekti') .
"Vipi mzee ana homa kali?" aliuliza yule askari.
"Siyo sana."
"Bila shaka Afande Ado alikueleza kuwa tutakuja kwako."
"Ni kweli, lakini kwani hapa ni nyumbani kwangu?"
"Tulitumia akili za kipelelezi tukaona kuwa kabla ya kuja kwako tuanze kwanza kuja hapa kwa mzee maana ulisema upo hapa."
"Mmefanya vizuri maana mtanisaidia hili janga."
"Janga gani?"
"Hili la kuugua mzee wangu."
Askari hao walikunywa juisi yao haraka haraka kisha kunipa pole kwa kuuguliwa na mzee.
"Sasa tukupe lifti ya kumkimbiza mzee hospitali?"
"Hapana, sasa hivi ataingia dereva wake na tutatumia hilo gari."
"Basi kama ni hivyo ni sawa."
"Lakini ningeomba basi nije kituo cha polisi kesho asubuhi kwani sijui hospitali madaktari watasemaje au watachukua muda gani kumtibia."
"Subiri nimjulishe Afande Ado kwa sababu yeye ndiye aliyetutuma."
Baada ya kusema hayo askari aliyekuwa kiongozi wao alichukua redio yake ya upepo na kumpigia afande wake.
"Halooo deka mbili."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nakusoma, sema."
"Tumefika kwa huyu binti Chepriska."
"Mmefika nyumbani kwake?"
"Hapana tumefika kwa mzee wake. Si alikuambia kuwa mzee wake ni mgonjwa?"
"Ndiyo."
"Baada ya kusema hivyo tulitumia akili yetu tukaamua kuja moja kwa moja hapa kwa mzee wake, mzee Mitimingi."
"Ehee endelea."
"Ni kweli tumemkuta huyu mzee wake ana hali mbaya sana, ni mgonjwa."
"Anaumwa nini?"
"Anatetemeka mwili wote, hawajui hasa anasumbuliwa na nini?"
"Kwa hiyo mmekubalianaje?"
"Hatujakubaliana chochote isipokuwa ameniomba aje hapo kituoni kesho nami nikamuambia kuwa siwezi kutoa uamuzi ndiyo maana nikaona ni vyema tuongee humu kwenye redio nisikie ushauri wako."
"Kama mmehakikisha baba yake ni mgonjwa ni vyema mkamkubalia. Asije akafa mzee wake akatusingizia polisi, sawa?"
"Sawa afande."
Wakati anazungumza na kiongozi wake nilikuwa nikimuangalia mzee Mitimingi aliyekuwa amekaa kwenye kochi akiwa amejilegeza.
Wakati hayo yakiendelea, kule nyuma yule mbwa mwenye sura ya mtu akawa analia kwa sauti ya juu.
Uliaji wa mbwa huyo ulimfanya mzee Mitimingi azidi kutokwa na machozi. Bila shaka alikuwa anadhani kwamba polisi wanaweza kwenda kibandani na kumuona mbwa huyo wa ajabu ambaye dunia nzima hakuna.
"Huyo mbwa kwa nini analia?" aliuliza yule askari wa kike.
"Ngoja nikamuangalie," nikasema.
Nilizunguka nyumba na kwenda kibandani. Nilikuta amejifunga kamba shingoni, hivyo kushindwa kugeuka na ndiyo maana alikuwa akilia kuomba msaada.
Nilijitahidi kuikunjua kamba aliyokuwa amefungwa shingoni na kuiweka sawasawa. Aliniangalia kwa huruma mno na kuachia tabasabu.
"Usiwe na wasiwasi nitakusaidia." Nilisema polepole bila kusikia mtu mwingine yeyote isipokuwa mbwa huyo.
Ajabu ni kwamba mbwa mtu yule aliitikia kwa kutikisa kichwa huku akitokwa na machozi. Nilijisikia vibaya sana.
Kwa jinsi alivyokuwa na sura ya binadamu, nilihisi kwamba inawezekana huyu mzee amemgeuza mtu kuwa katika hali ile.
"Chepriska, huyo mbwa ana nini?" aliuliza yule askari polisi wa kike.
"Ahaa, alikuwa amejifungafunga shingoni na kamba, hivyo akawa anashindwa kugeuka." Nilijibu.
"Hajapata madhara makubwa?"
"Hajapata," nilimjibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tuje kukusaidia kumfungua?" alizidi kuhoji askari yule wa kike huku akiangalia kwa mbali.
NILIMUAMBIA kuwa hakuna haja ya kuja kunisaidia kwa sababu nilikuwa nimeshamfungua na nikamdanganya kuwa mbwa mwenyewe ni mkali.
Mbwa mtu yule nilimuahidi kwamba nitamsaidia japokuwa nilikuwa sina uhakika kama nilichokuwa nakisema alikuwa akikielewa au la.
Baadaye nilichota maji kwenye kisufuria nilichokikuta ndani ya banda lake na kumuwekea. Mkononi nilikuwa na juisi ile iliyopasuka. Niliona akiiangalia kama vile anataka kusema, nitilie kidogo.
Nilichukua sinia dogo ambalo linatumika kumuwekea chakula na nikamimina ile juisi pale, haraka sana aliiendea na kuanza kuilamba.
Mbwa mtu yule alitabasamu tabasamu ambalo lilinifanya niamini kwamba yule hakuwa mbwa hawa wa kawaida tuliowazoea, nikawa sina shaka yoyote kwamba huyu ni mtu aliyegeuzwa kuwa mnyama huyo.
Kwa nini huyu mzee amefanya ukatili huu? nilijiuliza kimoyomoyo bila kupata jibu lolote.
Nilirudi kwa wale askari na kuwaomba waondoke ili nimpeleke mzee Mitimingi hospitali kwani wakati huo dereva wake alikuwa tayari amefika na gari lake aina ya Range Rover 5.2 .
Sawa, kwa kuwa afande kasema tukupe ruhusa tunafanya hivyo lakini uje ofisini kesho saa mbili asubuhi bila kukosa, alisema yule askari wa kike.
Japokuwa hakuwa amevaa sare za kipolisi nilihisi kwamba ndiye mkubwa wao wa kazi kati ya wale askari watatu waliofika kunichukua. Wangekuwa na sare ingekuwa rahisi kuwatambua kwa kuwa vyeo vya askari polisi mwenye magwanda huwa hadharani kwani huvaliwa mkononi au mabegani.
Chepriska uguza pole, akasema askari yule.
Alimgeukia mzee Mitimingi ambaye alikuwa anaekti ugonjwa akamuaga. Mzee pole sana, Mungu atakusaidia na kukuponya.
Mzee Mitimingi anafaa kuwa msanii kwani aliitikia kwa kichwa huku akiachia mdomo, hali iliyomfanya atokwe na udenda.
Nilichukua kitambaa nikawa namfuta udenda uliokuwa ukimtoka na wakati huo huo mlinzi ambaye alikuwa Mmakonde wa kuchanja alifungua mlango wa geti na gari la polisi likatoka.
Baada ya difenda hilo la polisi kutoka mlinzi huyo alifunga geti na kuja haraka sana pale nilipokuwa na mzee Mitimingi.
Kwani huyu nzee anachumbuliwa na nini? aliniuliza.
Anasumbuliwa sana na malaria na kichomi, nilimdanganya.
Dawa ya kichomi ninayo. Nilikuwa nimempelekea ntu mmoja lakini chikumkuta. Ni hii, chungu nitakupa kidogo meza tu uchimungunye, uminielewa?
Mzee Mitimingi alimkubalia kwa kuitikia kwa kichwa na baada ya dakika mbili aliinuka na kuingia ndani na ile dawa aliyopewa na mlinzi wa Kimakonde aliiacha pale alipokuwa ameketi.
Alipoingia ndani aliwaza mazungumzo kati ya polisi na Cheprisca.
Chepriska, huyo mbwa ana nini? aliuliza yule askari polisi wa kike.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ahaa, alikuwa amejifungafunga shingoni na kamba, hivyo akawa anashindwa kugeuka. alijibu.
Hajapata madhara makubwa?
Hajapata.
Sasa tuje kukusaidia kumfungua?
Hapana.
Mzee Mitimingi akawa anashangaa jinsi msichana huyo alivyofanya ujanja hadi akafanikiwa kuwalainisha polisi. Hakika huyu msichana ni mwerevu sana na ameniokoa, alijisemea kimoyomoyo.
Chepriska, aliita.
Bee baba, nilimuitikia.
Njoo ndani mwanangu, uje na hiyo dawa ya Mmakonde.
Wakati nainuka niliichukua ile dawa na kuifutika kiganjani. Mmakonde ambaye alikuwa getini aliposikia sauti ya mzee akaja mbio.
Unaona ile dawa inafanya kashi haraka chana. Umechikia ameanza kuchema, mwambie dozi haijakamilika, chacha kesho nitamletea nyingine atapona kabicha, alijisifu yule Mmakonde bila kujua kuwa dawa zake mzee Mitimingi hakuzinywa.
Sikumjibu lolote nikamuacha kwa sababu angejua lengo letu asingetuletea habari zake hizo.
Uchimfiche nzee, akasisitiza.
Sawa nitamueleza, nilimjibu huku nikiingia ndani.
Anasemaje huyo Mmakonde? aliniuliza.
Anazungumzia dawa aliyokupa.
Achananaye, nitakupa zawadi kubwa sana kwa kunifichia siri kwa polisi.. kuhusu mbwa na mkono wa mtu kwenye friji, alisema Mwzee Mitimingi huku akiniangalia.
Kimya kilitawala kwa dakika kadhaa kisha akaingia ndani na kutoka na bunda.
Cheprisca, hizi ni shilingi milioni tano. Ni zako. Umetumia akili sana kuficha siri zangu. Kwanza kwa kuwadanganya polisi kwamba mimi naumwa wakati siumwi chochote.
Nakushukuru sana mzee Mitimingi lakini na wewe ulikuwa unatetemeka, ilikuwa unavunga au?
Hapana. Nilikuwa natetemeka kweli kwa woga. Kulikuwa na mambo mengi sana ambayo umenisaidia leo, ungekuwa na roho ya kuniangamiza leo ningekwisha.
Sawa. Pamoja na kukushukuru lakini jambo moja kubwa ukumbuke kwamba natakiwa kwenda polisi kesho asubuhi.Nilimuambia huku nikipokea mzigo wangu.
Hilo nakumbuka.
Sasa kabla ya hilo ni lazima twende hospitali ili niwe na vyeti vyako kuonesha kuwa hukuwa unawadanganya polisi kwa ugonjwa wako.
Ushauri wako ni mzuri sana lakini kabla ya kwenda huko kuna mambo ya kukuambia ambayo utapaswa kuyazingatia,
Nilimsikiliza, nikawa namtazama usoni. Alikunja sura na kuniangalia. Aliangalia kwenye geti lake na kuona mlinzi wake yule wa Kimakonde yupo palepale getini.
Tuingie ndani kwanza maana kuna mambo ya siri sana nataka kukumegea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tuliinua na kuingia ndani huku nikiwa nimeshika shilingi zangu milioni tano. Kwangu mimi ilikuwa kama ni ndoto kushika fedha nyingi kiasi kile, tena kwa wakati mmoja.
Nilipoingia ndani niliketi kwenye sofa kubwa na mzee Mitimingi aliamua kukaa karibu na mimi.
Sikiliza kwa makini habari hii ninayokupa na nakuomba sana hii ni siri kubwa. Sijawahi kumuambia mtu yeyote na kama utathubutu kuitoa nje basi kichwa chako ni halali yangu.
Baada ya kusema maneno hayo alikaa kimya huku akiniangalia usoni ili asikie ningemjibu nini. Nami kichwa kilifanya kazi haraka nikapangusa uso wangu kwa kitambaa cheupe kisha nikamuambia.
Sikiliza mzee Mitimingi. Mimi nimesoma hadi chuo kikuu. Kama unaona kuwa hiyo siri yako mimi nitaivujisha, ya nini kuniambia?
Ni lazima nikuambie. Unamuona yule mlinzi wa Kimakonde? Hajawahi kumuona yule mbwa mtu hata mara moja. Wewe pia ulikiona kiganja cha mtu kwenye friji, jambo ambalo hakuna mtu aliyewahi kuona kitu kama hicho.
Alitulia kwa sekunde kama kumi hivi, akazidi kuniangalia machoni nami nikainamisha kichwa kisha akasimama.
Ngoja kidogo, nakuja.
Aliinuka kuelekea kwenye friji, nilidhani anakwenda kuniongezea kinywaji kwa sababu juisi niliyokuwa nakunywa ilikuwa imekwisha.
Badala yake alichukua mfuko akaweka kitu. Nilifikiri haraka nikagundua kuwa alikuwa akihamisha kile kiganja na kukipeleka chumbani kwake baada ya sekunde chache akaja kuketi palepale alipokuwa amekaa awali.
Sikiliza Cheprispa. Nilikwenda kukihamisha kiganja kile kutoka kwenye friji na kukiweka chumbani kwa sababu sikutegemea hata siku moja kuwa kuna mtu angefungua friji leo lakini wewe ulifungua. Ulifungua kwa nia nzuri ya kuwapa wageni, yaani wale polisi vinywaji.
Kwani mzee nilikosea?
Hapana. Hujafanya kosa kabisa tena mimi nakusifu sana kwa jinsi ulivyotumia akili na kuwazubaisha polisi. Ilikuwa ni hatari sana.
Alichukua bilauri yake iliyokuwa na juisi akainywa.
Nataka kukusimulia kuhusu yule mbwa mtu. Umemuona jinsi alivyofanana na sura ya mtu? Yule ni mtu. Nilimpa masharti akayakosea akajikuta anageuka mbwa.
Masharti gani hayo?
Ni kwamba nilimuambia kama ninavyokuambia wewe leo kwamba usitoe siri, yeye akatoa siri kwa mpenzi wake kwamba mimi utajiri wangu unapatikana kwa njia ya damu.
Ina maana wewe umemfanya binadamu awe vile?
Siyo mimi ni masharti ya mganga ndiyo yamemfanya awe vile! Mimi nilimuonya kuwa jambo hili usiliseme kwa watu yeye akamwaga mchele kwenye kuku wengi, yakampata yale.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa kwani huyo mganga hana dawa ya kumfanya arejee awe binadamu?
Kwanza mimi aliniudhi sana na sikuwa na mpango wa kumrejesha kabisa katika hali ya kawaida kwani alichokuwa akinifanyia ni sawa na kuniua. Wewe unaweza kumsamehe mtu anayekuua?
Hapana mzee Mitimingi, kama ni mateso umemtesa sana. Naomba chondechonde msamehe na mrejeshee ubinadamu wake.
Naweza kumrejeshea lakini hadithi ya jambo hili ni ndefu na nzito siyo kama unavyofikiri. Kwanza ni lazima nimpige viboko kila siku vitano. Ndiyo masharti yenyewe la sivyo mimi nitakuwa kama yeye.
Mzee Mitimingi baada ya kuyasema hayo aliniambia kwa kuwa hadithi ya mbwa mtu ni ndefu aliona ni vema kama nitakwenda kwanza polisi kuripoti kisha nirudi anisimulie kwa urefu.
"Chepriska hadithi hii inahitaji muda mrefu ili uelewe na usiwe na maswali."
"Lakini mzee nimekuambia kuwa twende kwanza hospitali ukapate vyeti kwa sababu wale polisi wakijua kuwa hatukwenda hospitali wanaweza kudhani tulikuwa na jambo tulikuwa tumelificha."
"Sawa. Mimi nitakwenda hospitali peke yangu, wewe nenda polisi."
"Hapana twende sote polisi."
Mzee Mitimingi hakuwa na la kufanya isipokuwa kukubaliana na Chepriska hasa kwa kuwa alijua kwamba ana upeo au uwezo wa kutabiri kitakachotokea.
"Chambilecho," aliita mzee Mitimingi.
Mara aliingia ndani kijana mmoja ambaye alikuwa amevaa Kaunda suti.
"Ndiyo mzee."
"Gari lako lina mafuta ya kutosha?"
"Ndiyo mzee. Jana jioni niliweka ya shilingi elfu hamsini na hatukuzunguka sana."
"Sawa. Tungoje tunatoka."
Mzee Mitimingi alichukua begi na kunipa.
"Huo mzigo wako tumbukiza humo."
Nilichukua ule mfuko wa nailoni uliokuwa na shilingi milioni tano na kuziweka kwenye lile begi. Baadaye tuliinuka na kuingia kwenye gari aina ya GMC la Kimarekani.
"Tupitie Hospitali ya Misheni kwa Buruda John."
Ndani ya gari hakuna hata mtu mmoja aliyezungumza na hatukuchukua muda mrefu tukawa tumefika kwa Buruda John.
"Nisubirini, nakuja," alisema mzee Mitimingi akaingia hospitali huku mimi na dereva Chambilecho tukimsindikiza kwa macho.
Alikaa ndani ya hospitali hiyo kwa dakika kumi na mbili kisha alitoka akiwa na rundo la makaratasi.
"Nimeandikiwa ED 3 (mapumziko ya siku tatu)."
"ED ya nini kwani wewe unafanya kazi ya mtu?"
"Napita kulekule kwenye ushauri wako kwamba hii ni kuonesha kuwa naumwa sana. Wakija wale jamaa wakiona hii, watajua naugua kweli."
"Sawa."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Chambilecho sasa elekea polisi."
"Lakini kama hujali si ni bora tungeenda kukushusha wewe nyumbani kisha polisi niende na dereva?"
"Hapana , polisi ni polisi, unaweza kwenda wakakung'ang'ania."
"Sasa wakining'ang'ania wewe utafanyaje? Si wanajua kwamba wewe upo taabani?"
""Hapana, nitatumia ujanja kwa kuwaambia kuwa nimepata nafuu lakini nimeambiwa nisifanye kazi yoyote na ndiyo maana nina ED."
Niliona kuwa wazo lake ni zuri, nikaamua twende naye polisi. Kutoka pale hospitali ya Buruda hadi polisi ilituchukua dakika kumi na tano.
Nilikwenda moja kwa moja kwa Inspekta Ado ambaye nilimkuta akisoma majalada yaliyokuwa juu ya meza yake.
"Karibu Chepriska."
"Ahsante."
Niliingia na kuketi kwenye kiti kilichokuwa kando ya meza yake kubwa. Nilitulia kusubiri ataniambia nini lakini badala yake akawa anaendelea kupekua yale majalada.
Mara moja akachukua alilokuwa akilitafuta.
"Nimekuita nilitaka kuongeza mambo kadhaa humu kwenye jalada lako."
"Sawa."
"Kwanza pole kwa kuuguza maana askari waliokuja kwako jana waliambiwa upo kwa mzee wako Mitimingi. Kwani yule ni baba yako mzazi?"
"Hapana, ni baba wa kunilea tu."
"Oke."
"Kuna habari kwamba mzee yule anapenda sana ushirikina. Hiyo ni kweli?"
"Hilo mimi silijui."
"Wewe umewahi kuishi pale kwake?"
"Hapana. Mimi huwa namtembelea tu, sijawahi kuishi pale."
"Kwa nini?"
"Kwa sababu mimi nilipoingia hapa mjini kwa nauli ya yule mzee niliamua kuwa nijitegemee. Nikapanmga chumba. Siku za kwanza alinilazimisha sana niishi pale kwake nikakataa katakata."
"Ulikataa kwa kuwa ulikuwa unajua kuwa huyo mzee ni mshirikina siyo?"
"Hapana, nilipenda niwe huru."
"Kwani ulipofika hapa mjini alikuambia atakupa kazi gani?
"Aliniambia kazi yangu ni kusimamia magari yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment