Search This Blog

JINA LA URITHI - 4

 







    Simulizi : Jina La Urithi

    Sehemu Ya Nne (4)





    yule mwanamke akahisi kama kamuona mtu akitokea chumbani kwake na kuingia katika chumba kingine!! mtu huyo alikuwa kavalia mavazi yaliyochakaa na yenye kuchanika chanika!

    hofu ikazidi kuongezeka akapaza sauti, akauliza kwa mshangao!

    wewe ni nani? umeingiaje humu ndani?

    aliongea maneno hayo huku mwili wake ukitetemeka,na mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi ya ajabu!

    punde si punde tetemeko la ardhi likatoweka kimiujiza,,vile vitu vilivyodondoka chini,,na vyombo vilivyopasuka,,vilirudi katika hali ya kawaida kama vilivyokuwa mwanzo!

    macho yakamtoka,,tangu azaliwe hajawahi kuona maajabu ya namna hiyo! akaamua kutimua mbio kuelekea sebuleni,,akaparamia mlango akaufungua kwa pupa na kutoka nje ya Nyumba!

    kitendo hicho kilimfanya Laula naye aingiwe na hofu,,akatimua mbio na kutoka nje kwa sababu mlango ulikuwa wazi! alikimbia pasipokujua kinachoendelea,,ni kama alifuata mkumbo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo kule chumbani,,ulionekana ule mzimu! ukiendelea kumtafuta Laula,,lakini haukufanikiwa kumpata Laula.

    Laula aliendelea kukimbia,sasahivi hata njaa ilibaki stori!

    upande mwingini yule mwanamke akiwa njiani ghafla ule mzimu ukajitokeza mbele yake! ili amuangamize ,,kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha Laula kukimbia ndani ya nyumba ile! mwanamke yule akapatwa na mshtuko akadondoka chini na kupoteza fahamu..ghafla ule mzimu ukasita kumfuata mwanamke huyo pale chini alipodondoka! mzimu ukageuza shingo yake upande wa kushoto,,kwa kuhisi Laula yupo upande huo! punde si punde ukatoweka kimiujiza kumtafuta Laula amabaye ni mrithi wa jina lake!



    Upande mwingine,,kule kijijini,,ukimya ulitawala,,hakuonekana hata mwanakijiji mmoja akirandaranda,,wote walijifungia ndani ya nyumba zao,,sauti ya ndege warukao angani....hakuna aliyethubutu kutoka nje! baada ya masaa kadhaa kupita,baadha ya wanakijiji wakatoka nje ya Nyumba zao,,ni baada ya ukimya wa masaa kadhaa...sasahivi hapakuwepo na hali ya kutisha...ikapigwa mbiu,,wanakiji watoke ndani ya nyumba zao na kuendelea na shughuli zao kama kawaida...baada ya lisaa limoja kupita! wale walioshiriki kuchoma nyumba ya Njile,,wakaanza kufa moja baada ya mwingine! walikufa vifo vya kutatanisha katika nyakati tofauti tofauti..jambo hilo liliwashtua wanakijiji,haijawahi kutokea vifo vya watu zaidi ya kumi kufa kwa siku moja tena ni vijana shupavu na wachapakazi ndani ya kijiji hicho!hofu ikazidi kuongezeka kwa wanakijiji.



    masaa yalizidi kusonga,,hatimae giza likaanza kutanda,,Laula akonekana akiwa kwenye mkusanyiko wa watu wakitazama mpira wa miguu kwenye Runinga! akaona si haba naye ajumuike nao huenda akapata angalau msaada aweze kupata mlo...alisimama hapo kwa dakika kadhaa,,aliposogeza mguu wake akahisi kama kakanyaga kitu chini ya unyayo wake!! akainamisha uso wake kutazama ni kitu gani hicho! akaona ni pochi ndogo ya mfukoni..lakini akashindwa kuokota pochi hiyo kutokana na mkusanyiko wa watu wengi hivyo hapakuwa na nafasi ya kuinama.

    wakati Laula anafanya jitihada za kuinama,,akaonekana ni msumbufu..hivyo mtu aliyekuwa amesimama nyuma yake akahisi kama Laula anataka kumuibia,,

    kutokana na umri mdogo wa Laula akafukuzwa eneo hilo,,aende akalale,,huo sio muda wa watoto kuwepo maeneo hayo.

    Laula akaondoka zake kishingo upande huku akisononeka rohoni,,kwa sababu aliamini ile pochi inapesa ndani yake......

    baada ya Laula kuondoka,,ghafla ule mzimu ukajitokeza katika mkusanyiko wa watu hao,,ni baada ya kugundua kuwa mrithi wa jina lake yuko katika eneo hilo ,,kumbe Laula aliondoka dakika chache zilizopita!!! watu wote waliokuwepo katika eneo hilo wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,kila mtu alitimua mbio na kupita njia yake,,huku wengi wao wakipiga kelele za uwoga!

    Laula hakuwa mbali sana,,,akazisikia kelele hizo,,akageuza shingo yake kutazama kule kwenye mkusanyiko wa watu wengi...akaona wanatimua mbio,hakujua kinachoendelea akaona hiyo ndio nafasi pekee arudi kuichukua ile pochi pale chini!

    bila kuchelewa akatimua mbio kuelekea huko!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Laula aliendelea kukimbia kwa kasi,lakini alistaajabu kuona watu wakisamabaa kutoka eneo lile kuelekea upande mwingine......Laula akasita kuendelea kukimbia ,,akasimama aakageuza shingo yake huku na kule kutazama ,,huenda akaona chanzo na sababu ya watu kukimbia,,hakuweza kuona kitu chochote.........akaangaza macho yake kutazama ile sehemu aliyoona ile pochi ndogo...akafanikiwa kuiona pochi hiyo akazipiga hatua za haraka haraka,,kuifuata.

    alipokaribia eneo hilo...akasita akahisi kama kaona kitu lakini kitu hicho ni kama kimepita kwa kasi mbele yake! akainama kuokota ile pochi ndogo,,,ghafla ukajitokeza ule mzimu! Laula alilishuhudia hilo,mzimu huo ukatoweka kimiujiza,,ghafla Laula akahisi kunakitu  kimeingia ndani ya mwili wake! punde si punde Laula akasimama wima! akatoweka kimiujiza.



    upande mwingine kule kijijini,,alianeka mwanaume mmoja akizipiga hatua kutokea porini! mwanaume huyo alikuwa kavalia ngozi ya fisi ,huku upande wajuu akiwa kifua wazi! shingo yake ilionekana kujawa na kamba nyingi zilizoshikilia irizi! mkononi alikuwa kashikilia mkia wa mnyama NYATI, kwa kumtaza kwa haraka bila shaka ni mganga wa kienyeji.

    aliendelea kuzipiga hatua kuelekea katika kile kijiji kilichokumbwa na janga ambalo mpaka sasa halijafahamika chanzo chake.

    baada ya masaa kadhaa kupita akawa amefika katika kijiji hicho,,,wanakijiji walimshangaa sana mtu huyo,,wengi wao walimkumbuka,,kwa sababu mtu huyo anasadikika kuishi porini miaka mingi iliyopita! alikuwa na nguvu za ajabu zilizojaa mambo ya kimiujiza...kwa wazee au watu wazima waliozaliwa miaka ya 60. walimtambua mtu huyo alikuwa anauwezo wa kukutazama machioni na ukafa  papo hapo! mtu huyo aliogopeka kama aogopwavyo mnyama mkali.

    Wazee na watu wazima waliozaliwa miaka ya 60 ,,wakaanza kutimua mbio kwa kuhofia usalama wa uhai wao..

    kitendo hicho kikazua gumzo kwa wanakijiji ambao ni vijana,,wakaingiwa na hofu....pia na wao wakatimua mbio!

    gjafla ikasikika sauti ikisema,,"msikimbie,,nimekuja kwa nia njema,,kuwasaidia kwa sababu nami ni mzawa wa kijiji hiki...sauti hiyo ilisikika ndani ya masikio ya kila mwanakijiji hata ambaye hakuwepo katika eneo hilo! kwa muda huo!

    baadhi ya wanakijiji wakaanza kuingiwa na imani,,wakaamua kurudi kumsikiliza mtu huyo!

    baada ya dakika kadhaa wanakijiji wakawa wamekusanyika kwa wingi!

    bila kuchelewa mtu huyo akasema,,"nadhani baadhi yenu unanikumbuka,,lakini napenda kuwatoa hofu kuwa nimekuja kuondoa tatizo ndani ya kijiji hiki! kuna jambo ambalo hakuna anayefahamu ukweli wowote kuhusu hilo,,tatizo ni JINA.

    mtu huyo aliongea hivyo kwa msisitizo kisha akasita kuongea neno lingine,,

    mwana kijiji mmoja akauliza kwa mshangao,,"JINA!!?? limefanyaje?

    yule mtu akatabasamu kisha akageuza shingo yake kutazama upande wa pili,,akasema" ndio,,tatizo ni jina,,na jina hilo ni la urithi ndilo linalozua mabalaa katika kijiji hiki!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wanakijiji hawakuelewa anachokizungumza,,japokuwa wamesikia maneno aliyoyaongea! ikazuka minong'ono wanakijiji hao wakiongea chini chini!

    yule mtu akasema,,"mimi ninanguvu za kimiujiza,,na haya niliyaona kabla hayajatokea! nani kati yenu anamkumbuka mwanamke NJILE?

    wanakijiji wakashtuka! ghafla ikasikika sauti kutoka katikati ya mkusanyiko wa wanakijiji hao ikisema,,"mwanamke yule alizaa mtoto wa ajabu! bila shaka alikuwa ni mchawi,,na tulimfukuza katika kijiji hiki!

     kabla hajamaliza kuongea sentensi yake...ukasikika mvumo wa upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu...upepo huo ulitoa mlio wa kutisha ukitamka maneno haya,,"MIMI NDIYE.........







    ghafla sauti hiyo ikanyamaza kwa muda, na ukimya ukatawala!baada ya sekunde kadhaa sauti hiyo iliendelea kusema,,"hakuna atakayeweza kunizuia ,,nitarudi tena siku chache zijazo...ghafla sauti hiyo haikusikika tena na ukimya ukatawala...macho yakawatoka wana kijiji,,kwa sababu aliyekuwa akiongea maneno yale,,hakuonekana kwa macho ya kawaida,

    wakati huo yule mtu mwenye nguvu za kimiujiza alikuwa tayari ameshagundua kuwa si mwingine bali ni mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula,,,mbaya zaidi tayari mzimu huo umeshaingia ndani ya mwili wa Laula...hivyo ni hatari kubwa itatokea ndani ya kijiji hicho.

    wanakiji waliendelea kuwa na hofu kubwa,,kila mmoja alitamani kutimua mbio,,,,yule mtu mwenye nguvu za kimiujiza aitwae JOGOLO akasema,,"tatizo limeshakuwa kubwa kuliko nilivyotegemea,mambo haya yanasababishwa na mzimu wa Laula,,alifariki takribani miaka mia iliyopita,,tatizo ni jina,,na jina hilo alipewa mmoja kati ya watu wa ukoo wake,,,ni mtoto mdogo wa umri wa miaka kumi sasa naye anaitwa Laula,

    baaada ya kuongea maneno hayo,,wanakijiji wakashtuka! wakasema maneno yako yanaelekea kuna ukweli ndani yake kwa sababu,ni kweli,,mtoto wa Njile anaitwa Laula na inasadikika mtoto huyo anazo nguvu za kimiujiza...

    ikasikika sauti ya mwanamke akiongezea kwa kusema,,"tunaomba utusaidie tafadhali tutakupa chochote utakacho.

    Jogolo akatafakari kwa sekunde kadhaa kisha  akasema,,"yahitaji moyo wa ujasiri kuna jambo gumu ndani yake ili kuondoa tatizo hili..

    wanakijiji wakatazamana kwa macho ya taharuki..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ghafla akaonekana Jogolo akitazama huku na kule akamuita mmoja kati ya wanakijiji aje pale alipokuwa amesimama yeye...Jogolo akatoa kipande cha nguo nyeusi,,kitambaa hicho kilikuwa kimefungwa mizizi ya mti,,kisha akasema,,"umu ndani ya kitambaa hiki kuna mizizi ya mti maalumu,,,mti huo unaitwa Mfungilwa...mizizi yake huchimbwa usiku wa manane,,na mchimbaji hufanya hivyo akiwa uchi wa mnyama, ni dawa nzuri sana ya kunasa mizimu,,jinamizi na majini,pamoja na viumbe wasio onekana....unapomaliza kuchimba mizizi ya mti huo,,sharti uifunge ndani ya kitambaa cheusi...na siku ya kukifungua kitambaa hicho,,ni lazima binadamu afe ili dawa iweze kufanya kazi,,aliongew maneno hayo akiwa tayari kamkabidhi yule mwanakijiji ile dawa ya kichawi iliyofungwa ndani ya kitambaa cheusi! wanakijiji wakaingiwa na hofu,,ghafla ikasikika sauti ya mwanakijiji mmoja akisema,,"mbona dawa hiyo inamsharti magumu kiasi hicho! kwani hakuna dawa nyingine tofauti na hiyo?

    Jogolo akasema,,"hakuna namna nyingine,,,na dawa hiyo siruhusiwi kuigusa tena kwa sababu nimeshaitoa mikononi mwangu! mtu huyu niliyemkabidhi,ndiye mwenye jukumu la kuchagua ni nani afe ili kijiji kikombolewe katika janga hili...ukishamchagua mwanakijiji mmoja,,,simama mbele yake..vuo nguo zako zote..kisha fungua kitambaa hicho na ummwagie mtu huyo dawa hiyo.

    baada ya  Jogolo kuongea maneno hayo,wanakijiji wakaanza kurudi nyuma wakisukumana,,kila mmoja aliogopa kufa kwa ajili ya kumkomboa mtu mwingine!

    hata yule mwanakijiji aliyekabidhiwa dawa hiyo akaanza kuingiwa na hofu,,akajuta kwa nini alikubali kuipokea dawa hiyo kabla hajajua masharti yake!! jasho likaanza kumtoka mfululizo...mwili wake ukitetemeka kwa uwoga!

    Jogolo akasema,,"usiogope na huu ndio muda muafaka wa kukamilisha jambo hili,, dawa ianze kufanya kazi,,pasipo kufanya hivyo hakuna mwanakijiji atakayebaki hai,,mzimu wa Laula utawamaliza bila huruma! haya endelea kushikilia kitambaa hicho pasipo kukiachilia,,,kaza mikono yako kisha piga hatua kumfuata mtu mmoja yeyote kati ya watu waliokusanyika hapa,, na yeyote utakayemchagua basi atakufa papohapo na dawa itaanza kufanya kazi!

    wanakiji wakaogopa! ni baada ya kusikia maneno hayo...lakini cha kushangaza,,miguu yao ilikuwa mizito kama wamewekewa gundi,,hakuna aliyeweza kunyanyua mguu kuoneoka eneo hilo!



    yule mwanakijiji aliyekabidhiwa dawa,,akazipiga hatua huku akiangaza angaza macho yake kumchagua mwanakijiji mmoja!

    mkusanyiko wa wanakijiji ulikuwa mkubwa,,,kiasi kwamba Jogolo alikuwa amezungukwa na umati huo,,

    yule mwanakijiji akasita! kuendelea kutembea,,akageuka na kurudi ule upande aliokuwepo mwanzo,,Jogolo hakuwa na wasiwasi,,aliamini huenda ameamua kumchagua mtu kati ya waliokuwa amesimama nyuma ya Jogolo....

    lakini mwanakijiji huyo aka,ipiga hatua n akusimama mbele ya jogolo,,akaanza kuvua nguo na kuifungua dawa hiyo....macho yakamtoka Jogolo!!

    KIZAA ZAA!!!!!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Jogolo akaingiwa na hofu akajaribu kutoweka kimiujiza lakini ikashindikana,,,hii ni kwa sababu dawa ile ya kichawi inanguvu kuliko nguvu alizokuwanazo yeye mwenyewe,,na kwa sababu tayari alikuwa ameshamkabidhi mtu mwingine ile dawa,,,kwa sasa hawezi kufanya chochote.

    mwanakijiji akazipiga hatua mpaka karibu kabisa na Jogolo,,kisha akakifungua kile kitambaa cheusi kilichokuwa na dawa ndani yake,,, akaichukua dawa hiyo ili ammwagie Jogolo mwilini,, ghafla,,likatokea tetemeko la ardhi,,likiambatana na mvua kubwa,,,waanakijiji wakaingiwa na hofu ,,,punde si punde dawa ile ikaishiwa nguvu ni baada ya kunyeshewa na mvua.



                                       ************************************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog