Search This Blog

DAMU YA MWANANGU - 1

 









    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Damu Ya Mwanangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Ilisikika sauti ya mtoto mchanga akilia,,,ndani ya nyumba moja iliyojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi kavu,,,wakati huo mama wa mtoto huyo alikuwa shambani,,akichuma matunda,,,angalau apate mlo kutokana na hali duni ya kimaisha iliyokuwa inamkabili.

    ilikuwa ni nyakati za masika,,,Wingu kiasi lilifunika anga,,pakawa na nuru hafifu,,utadhani ni Majira ya jioni,,mwanamke huyo akazipiga hatua,,za harakaharaka,,kuifuata nyumba  yake...

    kwenda kumtazama mtoto wake aliyekuwa akilia ndani ya nyumba..

    shamba halikuwa mbali, na nyumbani kwake,,hivyo aliisikia vyema sauti ya mwanae akilia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mwanamke huyo aitwae MUNA,,,alikuwa mlemavu wa akili,,,,alipata ugonjwa huo,,siku aliyojifungua,,,kutokana na huduma duni ya kiafya,,,kijijini kwao Muna hakuweza kuoata msaada wa kutibiwa kwa haraka...



                  ***************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muna akaingia ndani ya nyumba akamchukua mwanae akaanza kumnyonyesha,,,,,ghafla kunakumbukumbu ikamjia,,,akaanza kukumbuka matukio yaliyowahi kumtokea miaka mingi iliyopita..



    Muna alipata kichaa cha mimba,,wiki mbili kabla ya kujifungua...lakini cha kushangaza,,hata baada ya kujifungua,,,hali ya Muna iliendelea kuwa hivyohivyo,,,,hakuonyesha dalili zozote za kupona ugojwa wa akili,,,,

    Baada ya mwezi mmoja kupita,,,mume wa Muna akaamua kukimbia nyumba na kutelekeza familia yake,,,,

    Kwa sababu alifanya jitihada za kumtibu mkewe kwa kumleleka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji...lakinini ilishindikana.

    Muna hakuwa na ndugu....

    katika familia yao alizaliwa peke yake,,,na wazazi wake walifariki miaka mingi iliyopita,,,

    ndugu zake Muna wakagawana mali za wazazi wa Muna na kumfukuza muna nyumbani akiwa na umri wa miaka kumi na moja,,, Muna akakumbuka enzi za uhai wa wazazi wake,,waliwahi kumwambia kuwa,,Bibi na babu yake upande wa baba,walikuwa wanaishi katika kijiji kimoja kiitwacho UYOLE...ingawa hakuwahi kumuona bibi na babu,,kwa sababu wakati Muna anazaliwa,,,alikuta babu na bibi yake walishakufa miaka kadhaa iliyopita.....Muna akaona ni vyema aende UYOLE huenda kuna ndugu zake wengine huko kijijini......akaomba lifti ya gari,,akafanikiwa kupata lift katika roli moja la kubeba mizigo,kuelekea kijiji cha UYOLE,, akafika salama katika kijiji hicho,,,akaulizia kwa watu,,,akitaja jina la babu yake....akafanikiwa kupelekwa nyumbani kwa marehemu babu yake....alipofika akastaajabu sana kuona kwenye nyumba hiyo,,hakuna dalili za mtu kuishi ndani ya nyumba hiyo...akaamua kuingia ndani ndani ya nyumba hiyo,,,kulikuwa na tando za buibui,,pamoja na vumbi zito....akaanza kufanya usafi...hatimae nyumba hiyo ikawa safi,,,akawa anaishi hapo....



            *******************************



    Baada ya kumbukumbu hiyo,,Muna akaanza kucheka,,huku akiongea maneno yasiyoeleweka,,,,alipohakikisha mwanae kashiba,,akamfunga mgongoni,,na kutoka nje ya nyumba hiyo...

    akarudi kule shambani,kuendelea kuchuma matunda....ukimtazama Muna haonyeshi kama anaulemavu wa akili,,,lakini ukimuongelesha ndipoutagundua kuwa anatatizo la akili,,,,unaweza kumuuliza jambo,,akakujibu kitu kingine kabisa tofauti na ulivyomuuliza!!!,,,pamoja na hayo yote,,Muna alionekana kumpenda sana mwanae...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Mume wa Muna aitwae NYAMWELA....akiwa na wanakijiji wenzake wakinywa kahawa.....

    Nyamwela aliamua kwenda kuishi kijiji cha tatu kutoka kwenye kijiji alichokuwa anaishi na mkewe.....lakini watu waliokuwa wanamfahamu Nyamwela,,walimbeza kwa kusema kuwa si jambo jema kukimbia familia kwa sababu mkewe kapata ulemavu wa akili...

    maneno hayo yalimfanya Nyamwela akasirike,,,akaamua kuondoka zake akaelekea sehemu anayoishi kwa sasa...akiwa njiani akaingiwa na wazo,,,,,akaanza kutimua mbio,,,,,

    alikimbia mfululizo kwa muda wa dakika kumi,,akawa kafika nyumbani kwake akaingia ndani kwa pupa!!!...akachukua upanga akatoka nje na chuchumaa kando ya jiwe kubwa kiasi,,akaanza  kunoa upanga huo,,,kisha akarudi ndani ya nyumba akajisemea moyoni,,"nimechoka na hizi habari za Muna,,,kila mtu ananisema mpaka nakosa amani ya kuishi,,,,,,ningewezaje kuishi na mwanamke kichaa,,potelea mbali,,,,lazima nifanye jambo,,kuondoa mkosi huu....



              *****************************



    ilipofika nyakati za usiku,,,akaonekana akitoka nyumbani kwake,,akazipiga hatua kuelekea kijiji cha UYOLE,,, ni kile kijiji alichokuwa anaishi mwanzo....

    baada ya masaa mawili akafika katika kijiji hicho,,,,akaifuata njia inayoelekea kwenye ile nyumba aliyokuwa anaishi na mkewe MUNA...alipoikaribia nyumba hiyo,,akachomoa upanga kisha akaufuata mlango wa nyumba hiyo!

    akagonga hodi huku akiita jina la mkewe MUNA!

    ingawaje Muna na ulemavu wake wa akili aliweza kuitambua sauti hiyo kuwa ni ya mumewe Nyamwela,,,,

    ghafla akaanza kucheka peke yake huku akizipiga hatua kwenda kufungua mlango....

    alipoukaribia mlango,,kabla hajaufungua,,,

    punde si punde,, mtoto akaanza kulia,,,Muna akaacha kufungua mlango,,akatimua mbio kurudi chumbani,,,kumbembeleza mwanae,,



    Nyamwela,,, akawa anasisitiza kwa sauti kali,,MUNA FUNGUA MLANGO.......lakini muna hakumjali akaendelea kumbembeleza mwanae anyamaze kulia!

    Nyamwela akaamua kuzunguka nyuma ya nyumba,,katika dirisha la chumba alichokuwemo Muna na mwanae..

    akaanza kukata mbao za dirisha hilo kwa kutumia upanga aliokuwa kaushikilia mkononi.....

    Muna akashtuka!,,,akahisi huenda anataka kumnyang'anya mtoto......akaanza kulia,, mara anacheka,,huku akiongea maneno yasiyoeleweka!!!..alipoona dirisha linazidi kukatwa akaingiwa na hofu..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akamchukua mwanae akambeba mgongoni..kisha akazipiga hatua za kunyatia akafungua mlango na kutoka nje ya nyumba akatimua mbio..........

     wakati Muna anafungua mlango,,,aliurudishia kwa kuusukuma kwangu ukatoa sauti,,,

    Nyamwela akasikia ,,,akatimua mbio kuwahi mlangoni,,lakini akawa ameshachelewa,,

    tayari Muna alikuwa ameshatoka nje na anaendelea kutimua mbio....

    Nyamwela akasikia vishindo vya mtu anakimbia akagundua kuwa ni Muna,,,

     Nyamwela kaanza kutimua mbio huku kanyanyua upanga,, kuelekea ule upande aliokimbilia muna!!!

    TAFLANI!!!!





    Muna aliendelea kukimbia akiwa akambebe mwanae mgongoni,,

    Nyamwela hakufanikiwa kumuona Muna!  akaendelea kufanya jitiada za kumtafuta lakini pia hakuweza kumuona,,,kutokana na giza totoro lililokuwa limetanda,,,Muna hakuweza kuonekana kiurahisi,,



    baada ya masaa kadhaa kupita ,,,Muna akashindwa kuvumilia baridi kalili lililosababishwa na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi.

    akaamua kuzipiga hatua kurudi nyumbani,,lakini alikuwa kasahau kilichotokea masaa machache yaliyopita,,

    alipofika nyumbani kwake akaingia na kufunga mlango,,,akamlaza mwanae kitandani kisha naye akajilaza kando yake.



                                **************************



    asubuhi palipokucha Muna alidamka mapema,,,akazipiga hatua kuelekea shambani kutafuta chocho angalau apate mlo wa asubuhi....akamuacha mwanae akiwa chumbani,,,

    hakuwa na wasiwasi kwa sababu shamba halikuwa mbali kutoka usawa wa nyumba yake...akaangazaangaza macho yake huku na kule,,,akafanikiwa kuona uyoga uliokuwa umeota kandokando ya miti ya matunda.

    akachuma uyoga huo kisha akazipiga hatua kurudi nyumbani,,akakumbuka kuwa hakuna kuni za kupikia,,,akaamua kwenda kutafuta kuni kavu huko porini,,,ghafla akasita kuondoka,,,akaingia ndani ya nyumba akamchukua mwanae ambaye bado alikuwa kalala usingizi,,,akambeba mgongoni akaondoka zake!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Nyamwela,,akiwa nyumbani kwake,,,uso wake ulionyesha kutokuwa na furaha,,,kwa sababu kila kona anayopita watu wanaomfahamu wanamnyooshea vidole,,wakimsema kuwa ametelekeza familia yake kule kijiji cha tatu,,,mke pamoja na mtoto.

    siku zilizidi kusonga lakini Nyamwela bado alikuwa na mpango wa kumuua mkewe,,,kwa sababu ni kichaa,,hivyo hakutaka kuendelea kuishinae...kutokana na maneno ya watu kumsema,,akaona ni vyema aiangamize familia yake pamoja na mtoto mchanga,,ili yeye aanze kuishi maisha mapya,,

    punde si punde mlango ukagongwa,,,Nyamwela akauliza kwa sauti kali,,,wewe nani?

    ikasikika sauti ikitokea nje ya nyumba ikisema,,mimi rafiki yako Mabula,

    Nyamwela akanyanyuka na kufungua mlango akamkaribisha ndani.



    Rube akasema,,nimekuja hapa ninahitaji unisaidie baiskeli yako,,ninasafari kuelekea milima ya NZOKA,,

    Nyamwela akashtuka,,akauliza kwa mshangao,,unaenda kufanya nini huko? mbona hakuna makazi ya watu maeneo hayo?

    Rube akasema ,,"nakwenda kwa mganga kutafuta utajiri,nimechoka kuishi maisha haya ya umaskini,,nitazeeka hata sijanunua baskeli,,,

    Nyamwela akaanza kudadisi kiundani zaidi,,,lakini Rude akasema,,"mengi siyajui kuhusu upatikanaji wa utajiri,,lakini kuna mtu amenielekeza kwa mganga anayetoa utajiri,

    ndio sababu nimekuja hapa kwako uniazime baiskeli,,ilimradi safari yangu ya kwenda huko iwe rahisi.

    Nyamwela akajikuta naye anatamani kupata utajiri! akasema,,"hata mimi pia nahitaji,,hivyo ni vyema twende wote.



    bila kuchelewa safari ya kwenda kwa nganga ikaanza wakaelekea milima ya Nzoka...

    wakapakizana kwenye baiskeli,,kwa kupokezana kuendesha..

    baada ya lisaa limoja wakawa wamefika kwa mganga,,,wakaelezea sida yao,,,bila kuchelewa mganga akanza kupiga tunguli zake,,,,akaanza na Rube,,,akampa masharti magumu ambayo yalimfanya Rube akate tamaa yakuutaka utajiri,,,,aliambiwa  atoekafara la wazazi wake wote wawili,,ndipo apate utajiri..ikishindikana basi alete mchanga wa unyayo wa mguu wa mtu yeyote ampendae..kwa upendo ulioshibana.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog