Search This Blog

UFALME WA NUGUTU - 3

 







    Simulizi : Ufalme Wa Nugutu

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Huu ni upumbavu wa hali ya juu, Siwezi kuvumilia haya, haiwezekani watu wachache wawe na nguvu ya kupambana na watu elfu moja, waziri wa ulinzi linaingia kweli akilini" alifoka mfalme msongo alipopata taarifa kuwa jeshi lake lote limeteketezwa na baadhi kuwekwa mateka.

    "Kamanda Kayumba! Embu muelezee mfalme ilivyokuwa"

    "Mfalme mtukufu uishi miaka mingi" akainama na kusujudu kutoa heshima zake kwa mfalme,

    "Kiukweli mfalme mtukufu jeshi lako limeangamizwa na mtu mmoja tuu, ambaye ana nguvu zaidi ya simba, sauti kali mithiri ya radi na mwenye kwenda kwa haraka kama miale ya mwanga," alisema Kamanda Kayumba.

     Taarifa hiyo haikuvutia masikioni mwa Mfalme Msongo, akachomoa jambia na kukata kichwa cha kamanda kayumba pale pale.

    "Sipendi mniletee hadithi za kufikirika katika maisha ya kawaida, ninachotaka wale watu wote waangamizwe hadi hao mateka wote ueni kwa nguvu yeyote ile".

    Mfalme alichukia sana akutaka kusikia lolote toka kwa yeyote yule, Kengele ikagongwa na jeshi likajipanga sehemu ya gwaride kisha waziri mkuu akasogea na kuwaambia,

    "Mfalme amechukizwa na kitu kilichofanywa na wenzenu, kushindwa kutimiza agizo la mfalme adhabu yake ni kifo cha aibu, hivyo usiku wa kesho tutavamia kwenye ngome ile na kuangamiza kila kilichomo hadi watu wetu walio mateka wote chinjeni".

    "Uishi miaka mingi Nugutu........Ushindi kwa Nugutu..."

    "Uishi miaka mingi Nugutu............Sifa kwa mfalme mtukufu Msongo......"

    “Kitu kimoja zingatieni, shambulio hili ni la kimya kimya, hivyo kabla jua halijachomoza, tunatakiwa tuweke kambi katika milima ya videte, apo tutakuwa karibu na ngome ya maadui zetu, ivyo tutasubiri hadi jua litakapozama na kuvamia” lilikuwa ni agizo la mkuu wa jeshi kabla hawajaanza safari.

    Jeshi liliitikia kwa pamoja na kutawanyika kila mmoja kukusanya zana zake za kivita na kusubili amri ya kuanza safari kwa ajili ya mpambano.



    *********************



    Baada ya ushindi Mdidi akaenda alipomuacha mama yake na kumkumbatia kwa furaha isiyo na kifani,

     "Tumeshinda mama," Mdidi alisema.

    Balanoga akatoka na kuchemsha maji kisha akamwita Mdidi na taratibu akaanza kumkanda sehemu zile alizopata majeraha madogo madogo. Kwa macho ya bashasha Balanoga akazidi kumkoleza Mdidi ambaye muda mfupi uliopita alitoka kwenye shughuli nzito ya vita,

    "Mdidi nataka nikupongeze kwa mtindo wangu," alisema Balanoga.

    "Mtindo gani huo?"

    "Niruhusu utaufahamu nikishaufanya"

    Akili ya Mdidi ikazunguka kutaka kujua nini Balanoga anamaanisha hasa lakini hakupata jibu, akamtazama tena mrembo yule kisha akasema,

    "Sawa fanya lolote ujisikialo"



    Balanoga akatabasamu na kumsogelea zaidi Mdidi kisha kwa umakini mkubwa akamkumbata na kumbusu kwa bashasha. Bila kutarajia Mdidi akaanza kunyong'onyea na kuanza kupoteza nguvu, Balanoga hakushtuka zaidi sana aliendelea kumbusu na kumshika kila mahali. Ndani ya dakika chache Mdidi akawa tayari hajitambui ufahamu wake ukakata. Balanoga akaingiwa na hofu baada ya kuona hali hiyo na papo hapo akasikia mlango ukigongwa.

    “Aah! Mama”

    Balanoga akashtuka baada ya kufungua mlango na kumuona mama yake Mdidi ambaye kwa muda mrefu hakuwa na uwezo wa kutembea lakini leo amesimama na kusogea pale kilipo chumba cha Mdidi,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Balanoga, niambie nini kimemkuta mwanangu?” mama akauliza.

    “Umemfanya nini mwanangu niambie!”

    Balanoga akazidi kuchanganyikiwa, akajiuliza imekuaje mama akawa na hisia kali vile kwa mtoto wake, akashusha pumzi na kumwambia,

    “Mama sijamfanya chochote, ila nilimkanda tu majeraha yake kisha akaniambia kuwa anataka kupumzika, ndio nikamuacha alale”

    “Nipishe nipite”

    Mama akaingia na kumkuta kweli Mdidi amelala, akageuka na kumtazama Balanoga,

    “Una uhakika kweli ujamfanya chochote?”

    “Ndiyo mama,” alijibu Balanoga.

    “Usiku wa leo anahitaji kuwa peke yake, hivyo tumuache na sihitaji uniulize lolote kwa wakati huu”

    Balanoga akakubaliana na mama yake Mdidi, japo akawa na maswali mengi juu ya kilichotokea, akajikuta akijiuliza kwanini alivyomkumbatia na kumbusu, Mdidi nguvu zilimuishia, na kwanini kadri ya joto la mapenzi lilivyopanda ndivyo Mdidi alivyokuwa na hali mbaya hadi kufikia hatua ya kupoteza fahamu. Akatamani sana kujua Mdidi ni mtu wa aina gani hasa, muda wote akawa kimya huku akitafakari kilichotokea na kauli ya mama yake Mdidi.

    “Balanoga binti yangu najua utakuwa na maswali mengi juu ya Mdidi, lakini nipe muda ipo siku utajua kila kitu kuhusu yeye”.

    Asubuhu na mapema, Mdidi akaamka na kukuta mama yake pamoja na Balanoga wakiwa washaamka tayari, Kichwa kikawa kikimuuma sana, akasogea alipo mama yake na kumsabahi, kisha akamsabahi Balanoga ila binti yule akawa akimdadisi sana Mdidi kwa kila hatua anayoipiga.

    Akaja mzee aliyewakaribisha jana kisha akampongeza kwa kazi aliyoifanya jana, akamkabidhi jambia ambalo alilisahau jana wakati akipambana na wanajeshi wa Mfalme Msongo, Mdidi akalipokea na kuliweka mapajani pake.

    “Asante sana, mzee wangu”

    “Usijali simba wangu, na leo lazima tusherekee”

    Mzee akaaga na kuondoka, Mdidi akalishikilia vizuri jambia ili akaliifadhi, lakini ghafla hali ikabadilika, maumivu ya kichwa yakaongezeka maradufu, macho yakawa mazito sana, akaanguka chini na kuwa kama mtu mwenye kifafa.





    "Tusubiri hadi waanze kucheza na kujisahau ndipo tuwavamie"

    "Sawa mwaweza fanya hivyo ila kwa sasa wazungukeni na kuiweka katikati ngome yao, kisha nitapiga baruti juu na hapo wote kwa pamoja tutavamia na kuangamiza kila kilichomo"

    "Sawa mkuu"

    Jeshi likajipanga tayari kusubiri wakati muafaka wa mashambulizi ya kusthukiza,

    Sherehe za kujipongeza kwa ushindi wa jana zikashamiri na kupamba moto, Mvinyo wa kila aina na vyakula vya kila namna vikapikwa watu wakala na kuburudika, huku vikundi mbali mbali vya ngoma vikiendelea kutoa burudani ya namna yake.

    "Mdidi katika siku hii kubwa kwako naomba nikuambie jambo, tafadhari usilikatae"

    "Sawa zungumza nakusikiliza"

    "Niahidi utokataa"

    "Nakuahidi sitokataa"

    "Mdidi nimekuwa mfungwa na mtumwa ndani ya ngome yako ya huba, wewe ni mfalme wa moyo wangu sijutii kuwa kijakazi wako, naomba unifanye niendelee kuwa chini yako siku zote"

    "Eenh! Balanoga unamaanisha nini tena!?"

    "Mhm Mdidi inamaana bado akili zako hazijafunguka kujua nini hasa mimi nahitaji toka kwako" "bado sijaelewa Balanoga"

    "Mdidi nataka uwe mwanaume wa maisha yangu!" kauli iyo ilifanya mapigo ya moyo ya Mdidi kupiga mara kumi zaidi ya kawaida.

    "Hapana Balanoga siwezi!"

    "Toka lini umeenda kinyume na maneno uliyoyatoa mwenyewe, uliniahidi hutokataa tafadhari usinifanyie hivyo"

    Mdidi akajikuta akifadhaika sana kwani hata siku moja hakuwahi kwenda kinyume na neno alolitamka, akatafakari sana kisha akamtazama Balanoga ambaye tayari machozi yalishajenga mifereji midogo midogo kwenye mashavu yake, akamsogelea na kumkumbatia,

    "Nitatimiza hitaji la moyo wako" Balanoga akafurahi sana

    "Nakupenda sana Mdidi"

    "Nakupenda pia"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Balanoga ni mjanja sana kwenye mambo ya huba akampa nafasi ndogo ya kuongea mdidi kwa kumfanyia vituko vilivyoamsha hisia zao zote wawili, Balanoga akammbusu Mdidi kwa muda kama ilivyo kawaida kadri alivyo mbusu ndivyo nguvu zilivyozidi kumuisha.

    Wakati Balanoga akiendelea hivyo baruti ikapigwa juu na wote waliokwenye sherehe wakatahayaruki lakini kabala hawajakaa sawa mishale isiyo na idadi ikaingia ndani ya miili yao. Watu wote wakapiga yowe na kumuita Mdidi lakini mdidi hakuwa anajitambua, watu wote wakaangamizwa ndani ya muda mfupi Mdidi katika hali yake ile ile ya kutojitambua akawekwa chini ya ulinzi na mtu mmoja akatoa upanga tayari kwa kumchinja.

    "Wewe acha upumbavu utamchinjaje mtu aliye nusu mfu nusu hai, achana nae"

    "Hapana mkuu huyu si wakuachwa hai huyu ndiye yule mtu mwenye nguvu za ajabu"

    "Hahahahaha! Nguvu gani unazozungumzia wewe! Mbona hajafanya lolote, acha imani potofu chukua huyo mwanamke huyo mwache atakufa taratibu.



    Mdidi akaamka toka usingizi mzito uliomchukua baada ya kushika jambia lile, alivyofungua macho akashangaa kukuta amezingirwa karibu na watu wote wa eneo hilo. Shangwe na nderemo zikaanza kila mmoja alionesha kufurahishwa na Mdidi kurejewa na fahamu, Mdidi akamwita mzee pamoja na mama yake kando kisha akasema

    "Jamani maisha ya watu wa hapa yamo hatarini hamna atakayepona kama giza litaingia na kutukuta hapa"

    Mama yake Mdidi akashtuka zaidi Akakumbuka kuwa jambia lile lilikuwa na uwezo wa kuonesha mambo yajayo kwa yule aliyestahili kulimiliki,

    "Aah! Lazima tufanye jambo kubadilisha hatima ya watu hawa"

    "Lililopangwa limepangwa hamna atakayeweza kubadili hatima ya hayo yote, acha yatokee na yanasababu yakutokea"

    Mzee akaongea lakini Mdidi hakuridhika kabisa picha ya mauaji yakikatiri ikawa inatiririka kwenye ubongo wake, lazima tufanye jambo kubadili hatima ya yote haya.



    ******************************



    Jeshi la Mfalme msongo likajiandaa vilivyo kushambulia ngome ya maadaui zao, zana zote za maangamizi zikawa tayari kabisa. Wakati hayo yakiendelea Mdidi hakuwa na raha kwani alijua hatima ya watu wake ipo matatani, akaingia ndani na kufungua kifurushi kile alichokabidhiwa kipindi cha nyuma akakuta kuna kitabu chenye maelezo mbalimbali, akataka utulivu kukisoma hivyo ikabidi aende mbali kidogo na eneo hilo.

    Maandalizi ya kusherehekea ushindi yaliendelea kupamba moto vyakula viendelea kupikwa na vikundi mbali mbali vya ngoma, vikajiandaa kwa ajili ya tumbuizo. Mdidi yeye aliendelea kupekua kila kurasa kwa umakini ili aone kama kuna sehemu itakayomuwezesha kubadili hatima ya yale aliyoyaona lakini hakuambulia kitu, aliona vitu ambavyo kiukweli hakuvielewa.



    Kiza kikaanza kuingia yale ambayo mdidi aliyashuhudia kwenye maono yakaanza kuonekana moja baada ya jingine, machozi yakaanza kumtoka kwa kushindwa kufanya lolote juu ya yatakayotokea, akajikuta anachukua mvinyo uliopo katika eneo hilo la sherehe na kuanza kunywa, vikundi vya ngoma vikaanza kufanya mazuri na kutoa burudani kwa wote huku nyimbo za kulisifu jina la Mdidi zikitawala. Mdidi nae bila ajizi akaingia katikati na kuonesha ufundi wake wa kucheza, Balanoga akamfata na kumuita pembeni, Mvinyo ulimzidi nguvu na akawa anatembea kwa kuyumbayumba,



    "Mdidi katika siku yako hii kubwa naomba nikuambie jambo tafadhali usilikatae"

    "Sawa zungumza nakusikiliza",

    "Mdidi nimekuwa mfungwa na mtumwa ndani ya ngome yako ya huba, wewe ni mfalme wa moyo wangu sijutii kuwa kijakazi wako, naomba unifanye niendelee kuwa chini yako siku zote...."

    Mdidi aliposikia yale ikabidi ajipige makofi kidogo ili aone kama bado anaota au yupo katika mazingira halisi, moyo wake ukaenda kasi mno kwani ni wazi kile alichokiona ndicho kinaenda kufanyika Balanoga akaendelea kuongea lakini mawazo ya Mdidi hayakuwa pamoja nae, ikabidi amguse ndipo aliposhtuka na kusema,

    "Eenh! Balanoga unamaanisha nini tena!?"

    "Mhmh Mdidi inamaana bado akili zako hazijafunguka kujua nini hasa mimi nahitaji toka kwako",

    Mdidi akazidi changanyikiwa kwani kadri alivyojitahidi kubadili maongezi, ndivyo alivyojikuta akiingia katika maneno yale yale aliyoyasema kwenye maono, akabaki tuu ameshikwa na bumbuazi asijue atamke nini kwa kuhofia kuendelea kusema yale yale aliyoyaona,

    "Mdidi! Mdidi! Mdidi........!"

    "Naam!"

    "Mbona uongei!?"

    "Bado sijaelewa Balanoga"

    "Mdidi nataka uwe mwanaume wa maisha yangu!"

    Alivyosikia hayo alishtuka zaidi akajikuta anasimama na kusema,

    "Hapana Balanoga siwezi!"

    "Tafadhari Mdidi usinifanyie hivyo"



    Mdidi akajikuta akitoa machozi sababu aliamini muda si mrefu maisha ya wengi yanaenda kupotea, hatima akawa anaiona lakini hakujua ni vipi ataweza kuibadilisha, akahisi kuzidiwa na ushawishi wa Balanoga japo alijua fika huyo ndio chanzo cha yeye kushindwa kutoa msaada kwa watu wake, roho ilimuuma sana akaamua kutoka na kumuacha Balanoga peke yake. Balanoga alivyoona Mdidi ameondoka na kumuacha akamuita kisha akasema,

    "Ahsante kwa yote"

    Akaanza kurudi nyuma, Mdidi hakuelewa kile ambacho Balanoga anataka kukifanya lakini kadri Balanoga alivyokuwa akipiga hatua kurudi nyuma ndivyo kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake, kabla ya Mdidi kufanya lolote, Nkalo akawa amejiachia kuelekea kwenye mto ulio jaa majabali na ni wazi kama angefikia jabari lolote basi uhai wake ungekuwa mashakani. Mdidi akakimbia kwa haraka na kuingia mtoni akamfikia Balanoga kabla hata hajafikia jabari lolote, akamtoa hadi ukingoni mwa mto

    "Hivi unaakili gani wewe mwanamke...!"

    "Siwezi kuishi bila ya wewe Mdidi bora nife"

    Mdidi akahuzunika zaidi akamwangalia Balanoga ambaye alikuwa tayari kuangamiza maisha yake sababu tu ya penzi la dhati.

    "Sawa nitatimiza hitaji la moyo wako"







    Tabasamu likachanua na kuongeza uzuri zaidi kwa Balanoga pindi aliposikia kauli ya Mdidi

    "Nakupenda sana Mdidi"

    Daah Mdidi alitoa macho na wala hakutegemea kama kile alichokiona kinalazimisha kuendelea pamoja na jitihada zote zile alizozifanya,

    "Naku--pe-nda pia”

    Balanoga akamkumbatia Mdidi na kuanza kumbusu, hakuwa na ujanja wowote wa kufanya zaidi ya machozi kumtiririka, Balanoga akatumia kila njia kumkoleza Mdidi, akamshika kila mahali. Mdidi akaanza kuishiwa na nguvu, macho yakaanza kuwa mazito na hapo hapo akasikia Ukunga wa watu kuomba msaada kwa macho yake akashuhudia Balanoga akicheka kwa kebehi kisha akimtupa chini kama mzigo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama yake Mdidi akahisi hali ya tofauti akawa anaelekea kule alipokuwa Mdidi na Balanoga, pindi Balanoga alipoona mama Mdidi anakuja upande wake nae akachukua kitu chenye ncha kali kisha akajichanja na akajiangusha chini, mama Mdidi alipofika pale akachanganyikiwa kuona mwanae yupo katika hali ile, akaomba msaada wanajeshi kadhaa wakambeba na kumuweka sehemu nzuri kisha mama Mdidi akatoa kitabu na kuanza kukisoma kwa sauti ya chini huku akimtazama mwanae. Balanoga akashuhudia kile alichofanya mama Mdidi akamsogelea na kunyanganya kile kitabu, macho ya Balanoga yakabadirika na kuwa kama ya paka.

    "Huwezi kubadili hatima ambayo mwanao aliiona kwa macho yake, ulifikiri ni mtu mwema kwenu lakini la! Mimi ni kijakazi wa mfalme Msongo na lolote ninalofanya ni kwa ajili yake tuu!"

    Alivyosema hayo tuu mama Mdidi akakumbuka maneno aliyokwisha ambiwa apo awali na mumewe kuwa adui wa kwanza na wa mwisho wa Mdidi ni mwanamke ivyo asimruhusu kupenda kabla hajafika robo karne. Mama Mdidi akajiona ni mzembe wa kupindukia Balanoga akacheka sana na kuangamiza wale wanajeshi wote waliomzunguka, Kisha akamsogelea mama Mdidi na kumuwekea mkono kichwani, kisha akatazama juu na radi kali ikapiga apo apo mama Mdidi akaanguka chini na kutoelewa kinachoendelea.

    Ndani ya saa 3 kijiji chote kiliangamizwa hamna aliyepona nyumba zote zikachomwa moto.

    "Tafuteni kila kona angalieni kama kuna kiumbe chochote kinapumua kimalizeni"

    Jeshi la mfalme msongo likapita kila kona kuhakikisha kuwa hamna chochote chenye uhai, katika pita pita yao ndipo wakamuona Mdidi akiwa ajitambui kabisa, mmoja wa askari akachomoa jambia ili ammalizie lakini kabla hajafanya hayo, yule kamanda Mkuu akapiga mbiu na wanajeshi wote wakakusanyika pamoja wakawasha baruti na kushangilia, kisha safari ya kurudi Nugutu ikaanza.

    "Mkuu kuna Msichana tumemuacha"

    "Hawezi fanya lolote mwacheni atakufa taratibu kwa woga"

    Jeshi likaondoka na kumwacha Balanoga peke yake ambae akasogea hadi alipo Mdidi na Mama yake aka waweka sehemu nzuri.

    "Mdidi utanisamehe sana, japo si rahisi kwako kugundua ushetani wangu kwa sasa, pamoja na hayo yote nakupenda kwa dhati na kwa namna yeyote ile nitakufanya uendelee kuwa karibu yangu" Balanoga aliongea kwa sauti ya chini kisha akajiegeza pale alipolala Mdidi na mama yake.



    ***********************************



    Shamra shamra za ushindi zikarindima ndani ya jumba la kifalme, Mfalme Msongo alifurahi sana na kuwapongeza vijana wake kwa kazi walioifanya akawaamuru wapiga ramli waangalie nyota yake ili waone kama kuna kikwazo chochote kilichobaki, wapiga bao na wataalamu wa Nyota wakaangalia nyota ya mfalme Msongo lakini walichokiona hamna aliyeamini ikabidi warudie kupiga tena bao na wakaona tena kitu kile kile.

    Wingu zito lilionekana kutanda katika anga la Nugutu kiasi kwamba ata nyota ya mfalme Msongo haikuonekana vyema, wataalamu wa mambo yale ikabidi wakae waulizane wamwambie nini mfalme Msongo.

    "Mimi naona tumdanganye Mfalme juu ya hili sababu inaonekana huyo mrithi halali wa milki hii ya Nugutu ana nguvu kubwa sana ata miungu ya nugutu ipo pamoja naye" akasema mmoja kati ya wapiga bao,

    "Mimi naona tumvute kwanza huyo Mrithi ili tumuone ni mtu wa namna gani"

    Mwengine akatoa wazo hilo hivyo wote wakakubaliana na kuanza kufanya maombi yao, wakatumia beseni la maji kutazama sura yake wakafanya hivyo kwa muda mrefu sana lakini hawakufanikisha.

    "Nina njia moja ya mwisho ya kumleta hapa uyo mtu"

    Chaku mganga maarufu sana nchini Nugutu akasema huku akisogea kwenye kile beseni la maji na kuyapiga kwa usinga huku akitamka maneno yasiyoeleweka vizuri, maji yakaanza kuchemka kwa kasi mno na Chako akazidisha maombi, kivuli cha mtu kikaanza kuonekana kwenye maji yale, Chako akaanza kupunga usinga kwenye pande zote 4 za dunia picha ya yule mtu haikuonekana vizuri. Akachukua kitu chenye ncha kali kisha akajichoma kwenye kidole na kunyunyuzia damu yake kwenye beseni, maji yalichemka sana na moto mkubwa ukalipuka na kumuunguza usoni mganga Chako wale wengine walivyoona hayo wakajawa na hofu na kurudi nyuma.

    "Mhm huyu si mtu wa kawaida hatumuwezi hakika".

    Wakakubaliana wamfiche mfalme juu ya kile walichoshuhudia uku wakipeana kazi ya kuongeza nguvu zao na kuhakikisha wanaangamiza kile kikwazo cha mfalme Msongo.



    *******************************



    Mdidi akaamka na kukuta kijiji kizima kimeangamia, nyumba zimetekea na mali zimeharibiwa, akaangaza huku na huko kuangalia kama kuna dalili ya yeyote mwenye uhai lakini palikuwa kimya tuu, akamkumbuka mama yake kipenzi. Akaangaza alipokuwa, akamwona amelala chini huku akiwa na majeraha alipotazama pembeni akamkuta na Balanoga naye akiwa ameumizwa vibaya, akawasogelea wawili hao na akagundua kuwa bado wana uhai ikabidi awainue na kuwaweka katika sehemu salama, akaendelea kutafuta kila mahari ili aone kama kuna mtu mwenye kuhitaji msaada lakini hakuambua kitu zaidi ya kukuta majivu na mafuvu ya ndugu zake walioteketezwa kwa moto baada ya kuuawa na jeshi la mfalme Msongo. Mdidi akachimba shimo kubwa kwa ajili ya kuzika masalia ya miili ile kwa pamoja. Akafanikiwa na kuizika yote, wakati anafanya yote hayo Balanoga alikuwa akimtazama tu, alipomaliza shughuli akarudi alipowaacha mama yake na Balanoga na kukuta hali ya mama yake ni mbaya sana, akaingia msituni na kutafuta baadhi ya miti shamba kisha akarudi na kumpa mama yake. Baada ya muda hali ya mama yake ikaanza kuwa sawa.

    "Mwanangu kichwa kinaniuma sana, kuna kitu kilitokea ila sikumbuki ni kitu gani," alisema Mama.

    Balanoga alivyosikia ivyo akashtuka mno akajua mama yake Mdidi anazungumzia juu ya ushetani wake.

    "Mhm mama ni jambo gani hilo?"

    Mama akamtazama Balanoga kisha akamtazama Mdidi akavuta pumzi ndefu na kusema ,

    "Mwanangu nataka nikwambie kitu juu ya huyu msichana..."

    Moyo ukamlipuka Balanoga akahisi mama mdidi amekumbuka yale aliyomfanyia,

    "Nakusikiliza mama"

    Mama mdidi akamtazama tena Balanoga kisha akatabasamu na kusema,

    "Ishi naye vizuri"

    "Unamaana gani mama?"

    "Ni msichana mzuri mwenye kujali"

    "Mhmh mama ushaanza mambo yako, ila sawa nimekuelewa".

    Balanoga akashusha pumzi alivyosikia yale, hofu ikaisha na akawa katika hali ya kawaida.

    "Mama hapa hapatufai tena kuishi hivyo ni vyema tukaondoka na kutafuta sehemu nyingine"







    Mama akakubaliana na wazo la Mdidi hivyo bila kuchelewa safari ikaanza, sehemu ambayo Mdidi aliifikiria kwa haraka ni Kigomile kwa Chifu Mzovu, hivyo ikabidi waelekee huko baada ya kuhakikisha kila kiti chake cha muhimu anacho bila kusahau jambia lake.

    Walitembea taratibu hivyo kusababisha kutumia muda mrefu sana njiani, hatimaye wakakaribia milki ya chifu Mzovu pasi na kujua wakajikuta wamezingira na maaskari waliokuwa wakizunguka kuhakikisha usalama wa eneo hilo,

    "Nyie ni wakina nani na mnahitaji nini huku!"

    "Tunahitaji kuonana na Chifu Mzovu" Mdidi akajibu.

    "Mmetokea wapi?"

    Askari akauliza tena, Mdidi akababaika kusema sababu alijua akisema ametokea Nugutu wasingeruhusiwa kuingia humo,

    "Tumetokea mlima Videte" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askari akawaangalia kisha akawaamuru wenzie wampeleke kwa chifu,

     "Mkuu chifu hayupo nyumbani kwa sasa anaangaikia ndoa ya binti yake," akajibu Askari yule.

    "Nkalo anaolewa?" Mdidi akajikuta akiropoka kwa sauti kubwa hadi maaskari nao wakashtuka.

    "Unamjua vipi Nkalo?" Askari akamuuliza Mdidi

    "Niliishi hapa siku za nyuma kama kijakazi wake"

    Maaskari wakatazama kisha wakawachukua na kuongozana nao kwenye utawala huo wa chifu Mzovu, Mdidi akabadilika baada ya kupata habari za kuolewa kwa Nkalo hali ile ikamshtua zaidi Balanoga pia ikazua maswali zaidi kwa mama yake.

    "Mdidi ondoka na usifikirie tena kurudi hapa ila katika hali yeyote ile nitabaki nikikupenda"

    Maneno hayo yakajirudia katika akili ya Mdidi, moyo ukamuuma hadi akawa anajishangaa mwenyewe.

    "Mdidi umekutwa na nini?" Balanoga akauliza,

    "Hamna kitu nipo sawa tuu!"

    "Unaweza muongopea Balanoga ila si mimi mama yako, niambie mwanangu nini shida"

    Kabla hajasema lolote kwa mbali Nkalo akawa anakuja sehemu walipo, akaanza kuhisi kitu cha tofauti kwani moyo uliongeza kasi ya kudunda. Wote wakajikuta wakigeuka na kutazama kule Mdidi anapotazama. Nkalo Kabla hajafika walipo wa kina Mdidi akasikia akiitwa,

    "Nkalo! Nkalo......!"

    Akasimama na kugeuka kutazama nani anayemuita, alikuwa ni baba yake ikabidi asogee ili aweze kuongea nae.

    "Mwanangu unaenda wapi saa hizi?"

    "Baba nimepewa taarifa kuwa kuna watu wanaitaji kuonana nawe, wametokea mlima videte kwakuwa hukuepo nikaona si vibaya nikaenda kuwasikiliza wanashida gani," alisema Nkalo.

    "Sawa mwanangu acha tu niende nikawasikilize mwenyewe hupaswi kuangaika, siku mbili zimebaki tuu kwa ajili ya harusi yako"

    "Sawa baba"

    Nkalo akageuza na kurudi kwenye nyumba yake na Chifu Mzovu akaenda kule alipoelekezwa. Moyo wa Mdidi ukatulia sababu hakujua nini angezungumza endapo Nkalo angekuja na kuonana naye, Chifu alipofika wote wakainama na kusema.

    "Uishi miaka mingi eeh mtawala mtukufu"

    Chifu nae akainamisha kichwa ma kukiinua nao wakainua, Mdidi akamuelezea Chifu kila kilichowakuta, Chifu akawahurumia sana na akakubali kuwapa hifadhi, akaita kikao cha dhalura na watu wote wakakusanyika wakawatambulisha Mdidi, Balanoga na Mama yake, watu wakawapokea na wakakabidhiwa nyumba ya kuishi.

    "Mhm! hivi hiko kikao alichoitisha baba saa hizi ni cha nini?" Nkalo akamuuliza kijakazi wake.

    "Kuna wageni sijui wametoka wapi, Chifu amewapa hifadhi katika ardhi yetu, kuna mvulana mmoja, msichana na mama wa makamo, ila huyo mvulana inasemekana alishawahi kuwa hapa kama mfungwa"

    "Mfungwa! Jina lake ni nani??"

     "Sikumbuki vizuri jina ila ni kama Mdudu au sijui nini"

    "Mdidi!" Nkalo alishangaa sana.

    "Ndiyo dada anaitwa Mdidi, Vipi mboni umekuwa ivyo?" kijakazi akauliza.

    Nkalo hakujishughulisha kujibu akatoka ndani kwa haraka mno na kuelekea kwa baba yake.

    "Vipi mwanangu mboni Kama haupo sawa!?"

    "Baba nataka kujua wageni uliowapa hifadhi ni akina nani!?"

    "Aah! Nkalo ni yule kijana wa maajabu yupo na mama yake na msichana mmoja hivi, nahisi atakuwa mkewe"

    "Mkewe!" Nkalo akashtuka zaidi

    "Nahisi hivyo japo sina uhakika sana"

    Nkalo akatamani usiku huo huo aende kwa Mdidi, lakini hakuweza kufanya hivyo, akarudi chumbani kwake huku akiwa na mawazo tele.

    "Inamaana Mdidi ameoa! Sasa amekuja kuniumiza au, mboni sielewi?" Nkalo akajiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake.



    *************



    "Mama mwanao sijielewi kabisa!"

    "Unanini mwanangu?"

    "Mama nilivyomwona yule msichana nikahisi hali ya tofauti, moyo ulienda kasi na nilihisi kuumia na hasira kubwa niliposikia anaolewa"

    "Mhm Mdidi mwanangu umependa!"

    "Nimependa!"

    "Ndiyo mwanangu hayo ndiyo mapenzi!?"

    "Aaah! Mama mapenzi gani sasa haya, mboni nimesikia mapenzi ni raha sasa mbona mimi naumia"

     "Hahaha mwanangu! Raha pale unapokuwa na yule umpendaye”

    "Sasa mama nitafanyaje!" akauliza Mdidi.

    Mama akamtazama mwanae kisha akakumbuka kauli ya mumewe Makala kuwa adui wa mwisho wa Mdidi ni mwanamke ivyo amlinde asiingie kwenye ulimwengu wa mapenzi kabla ajafikisha robo karne.

    "Mdidi mwanangu wewe ni wapekee na upo tofauti na vijana wote wa Nugutu, Ivyo mwanangu nilikua nakuzuia sana kuanzisha uhusiano na watoto wakike hata leo nakwambia tena upaswi kupenda wala kupendwa kabla hukafikisha miaka 25"

    "Aah mama kwanini?"

    "Naomba ukalale kesho nitakwambia kila upasalo kulijua".



    **************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku ulikuwa mrefu sana kwa Mdidi mawazo yote yakawa kwa Nkalo, Nkalo naye tamaa ya kuolewa ikakata akatamani siku zisimame aepuke ndoa hiyo. Balanoga akaona tayari sasa kuna mpinzani anaetishia kupokonya tonge mdomoni.

    Usiku ukapita na siku mpya ikaanza, Kutokana na uchovu wa safari na misukosuko mingi Mdidi akachelewa kuamka siku hiyo.

    "Mama Mdidi bado hajaamka?"

    "Mhm na sijui ana nini huyu mtoto hadi saa hizi ngoja nikamwangalie Chumbani kwake"

    Mama akaenda chumbani kwa Mdidi lakini hakumkuta, akapatwa na wasiwasi na akarudi hadi alipo Baranoga.

    "Mdidi ndani hayupo sasa sijui ametoka saa ngapi na ameenda wapi"

    Wakati anaendelea kusema hayo Mdidi akaingia akiwa amebeba mbuzi pori,

    "Eenh! Mdidi umetoka saa ngapi humu ndani na huyo mnyama umemtoa wapi?" mama akauliza.

    "Mama Ilinilazimu kuamka asubuhi sana na kwenda kuwinda sababu tupo kwenye ardhi ya watu na si vyema tukawa ombaomba"

    Akamuweka mnyama yule sehemu salama kisha akaendelea na shughuli zake.

    "Hodi! hodi!"

    Mlango wa kwa kina Mdidi ukawa unagongwa, Balanoga akatoka na kufungua akakutana na Nkalo uso kwa uso, Balanoga akainamisha kichwa kutoa heshima zake kwa mtoto wa chifu naye Nkalo akafanya hivyo pia,

    "Naomba kuonana na Mdidi tafadhari"

    Balanoga akamuangalia Nkalo akatamani akatae lakini kukataa kitu alichoagiza mtoto wa chifu ni sawa na kupingana na chifu mwenyewe na lazima uadhibiwe kwa hilo.

    "Dakika moja tafadhali",

    "Hapana siwezi kuonana nae hapa, mfikishie ujumbe mwambie aje sehemu tuliyokuwa siku ya mwisho"

    "Sawa nitamwambia"

    "Uwe na siku njema" Nkalo akaaga na kuondoka,

    "Uwezi kumchukua Mdidi huku nikikutazama nitakufunza kitu ambacho hutoeza sahau maisha yako yote" Balanoga alisema maneno yale kwa sauti ya chini kisha akasonya na kuingia ndani.

    *********

    "Jamani kizuizi cha Mfalme msongo kipo kigomile, hatuitaji kutumia jeshi la damu kupambana, ila safari hii tutatumia jeshi la giza na tusimwambie mfalme lolote hadi tutakapo ikamilisha hii kazi"

    Mkuu wa wapiga bao wa Mfalme msongo akaongea na kuamuru jeshi la giza lifunguliwe na kunuiwa kuiangamiza Kigomile.



    ***********



    "Mwanangu! jana nilikwambia machache kukuhusu, ila kiufupi wewe ndiye mkombozi uliyeteuliwa na miungu ya Nugutu, kutetea amani na furaha kama ilivyokuwa enzi za utawala wa Babu yako Gaiya. Unatakiwa uende kwenye hazina ya Nugutu na ramani ni hii hapa, unatakiwa utumie siku 7 huko, kuna nguvu nyingine lazima uipate ndivyo tuweze kwenda Nugutu kuikamilisha kazi ya ukombozi. Hili jambia kazi yake unaijua na kile kitabu nilichokupa maelezo utayapata kwenye hazina".







    Mdidi akapokea ramani kisha akapokea na lile jambia, alivyolishika tuu akahisi kama amepigwa shoti na akawa kama mtu mwenye kifafa, kisha akaanza kuona.

    Ndege wakubwa na waajabu wakitanda eneo la kigomile huku wakitema moto na wengine wakiwashambulia wananchi wa sehemu iyo. Mdidi aliweweseka kisha akashtuka na kuketi moyo ukaenda kasi akaomba maji ya kunywa na kupewa kisha akatulia kwa muda bila kusema kitu, mama yake akawa anashauku la kutaka kujua nini mwanaye amekiona kabla hajauliza Balanoga akaja,

    "Mdidi samahani! Mtoto wa chifu alikuja na amesema anakusubili sehemu ya makutano"

    Mdidi aliposikia hivyo moyo ukalipuka na akajikuta akinyanyuka na kusahau yote aliyoyaona na kuanza kuondoka, mama yake akamtazama kisha akamuita,

    "Mdidi! Sitaki ukaonane na Nkalo"

    "Aaah! Mama kwa nini!?"

    "Sibadilishi kauli na sitaki maswali zaidi"

    "Mama hii si haki kabisa, nipe walau dakika chache nikaonane naye" Mdidi alilalamika mno kwa mama yake lakini mama hakuonesha kubadili msimamo wake.



     ****************************



    "Dada naona umesubili kwa muda mrefu na hajatokea, mi naona turudi nyumbani"

    "Hapana namjua vizuri Mdidi lazima atakuja"

    "Sasa utamsubili kwa muda gani?"

    "Tuendele kumsubili atakuja tuu..!"

    Yalikuwa maongezi kati ya kijakazi na Nkalo walisubili sana hatimaye wakakata tamaa,

    "Inawezekana kweli Mdidi ameoa, angekuja basi niongee nae mara ya mwisho kabla ya ndoa yangu, kwanini anifanyie hivi" Nkalo aliongea kwa sauti ya chini ambayo hakuna aliyemsikia, machozi yakaanza kumtoka, mwishoe akamwambia kijakazi wake waondoke

    "Laa! Dada hatuwezi kwenda ukiwa katika hali hiyo, lazima utaulizwa futa machozi na utulie"

    "Hapana siwezi acha kulia, moyo wangu unauma sana"

    "Dada tuliza akili yako na ufikiri juu ya ndoa yako na Chifu Magambi"

    "Mhm pamoja naenda kuolewa ila sitoacha kumpenda Mdidi.."

    Wakati wanaongea hayo Mdidi akawa anakuja huku akikimbia kuwahi.

    "Dada angalia nani anayekuja"

    Nkalo alipogeuka kutazama hakuamini kuona Mdidi anakuja nae akashindwa jizuia akajikuta akikimbia kuelekea upande alipo Mdidi, wakakutana kati na kukumbatiana, wakasahau kabisa kuwa kuna ukuta mkubwa kati yao ambao si rahisi kuvunjika. Nkalo akampiga makofi yasio na Idadi Mdidi

    "Kwanini umeoa na kuniacha mimi?"

    "Nkalo........!" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana Mdidi sitaki useme lolote, umenipa jeraha ambalo hamna anayeweza liponya, naolewa kesho, japo ni ngumu kuacha kukupenda ila nitahakikisha nakusahau kabisa"

    "Nkalo tafadhali nisikilize"

    "Sitaki kusikia lolote toka kwako"

    Nkalo akageuka na kuondoka kwa kasi bila kusikiliza lolote toka kwa Mdidi, roho ilimuuma zaidi akabaki akimtazama Nkalo anavyoenda, akashindwa vumilia akamfata huku akimwita.

    "Nkalo...! Nkalo...! Nkalo..." Nkalo akasimama na kumwangalia Mdidi.

    "Sema nakusikiliza"

    "Nkalo wewe uhujui ukweli naomba nikwambie"

    Nkalo akamtazama Mdidi kisha akamgeukia kijakazi wake na wakaanza kuondoka

    "Nkalo...!"

    Mdidi akaita tena safari hii hakugeuka, hakuwa na namna ya kufanya hakuwa na nguvu hata ya kurudi nyumbani akabaki amesimama akimwangalia Nkalo akitokomea, kabla hajaingia ndani Nkalo akageuka akakuta bado Mdidi akimtazama kwa huzuni.



    *****************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog