Search This Blog

USIKU WA KAFARA (ROAD TO 2017) - 2

 







    Simulizi : Usiku Wa Kafara (Road To 2017)

    Sehemu Ya Pili (2)





    NAAMU ! gadyson alihesabu kuwa amesha umaliza mwaka 2016 ! ama kweli usio lijua ni usiku wa giza mpenzi msomaji...



    Safari ya furaha ilizidi kusonga huku maongezi ya kiucheshi yakitawala ndani ya gari lile..



    Wakati baraka anaendelea kuendesha mara ghafla aliutambua muungurumo tofauti kwenye gari yake na hapo akakunja sura akilaani

    "Ah chuma kilishaanza kuchemsha acha niweke maji ili ipoe mdogo mdogo" baraka aliongea huku akifunga brek na kuchukua touchi na kushuka nayo akazunguka kwenye mlango wa mizigo akaufungua na kulitafuta dumu la maji lakini hakuliona..

    "ujinga huu hili dumu limeenda wapi" aliongea peke yake huku akizidi kupanga na kupangua mizigo lakini ilikuwa kazi bure...

    "wadau kidumu cha maji tume kitupa wapi" aliwauliza wenzake na wao hawakujua

    "kwani wale maafande walikirudisha kweli? maana walikishusha ule muda walipokuwa wana kagua" sarah aliwakumbusha wenzake..

    "aah pumbavu zao watakua hawakukipandisha" baraka aliwalaani wale askali wa barabarani... baraka akafunga mlango wa mizigo na kurudi kwenye uskani.

    "Hapa ina bidi niendeshe mwendo mdogo mdogo kwani gari inakaribia kuchemsha... ila kilo meta kazaa kutoka hapa kuna sehemu ina mashine ya walter wind hapo kuna kisima tutapata maji" baraka aliongea na wenzake wakaafiki na safari iliendelea kwa mwendo wa speed hamsini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila walipo zidi kutokomea ndipo gari nayo ilizidi kuchemsha na baraka nae akapunguza speed hatimae gari ikawa inatembea taratibu kabisa kana kwamba ilikuwa kwenye foleni za tanzara.



    Na mwishoe kabisa gari ile ilizima kabisa na baraka alijaribu kuwasha lakini haikuwaka hata kwa kujaribu...



    Wakawa wamekwama katikati ya msitu na hapakuwa mbali sana na lile pango la goroza!



    ******--*********;**************



    Malikia wa viumbe wale yule mzee kikongwe alikuwa ndani ya pango akisubiria kwa hamu muda ufike na kwenye taswila yake aliwaona jinsi kina baraka walivyo hangaika na gari lao ..!

    kikongwe yule aliwasha mshumaa mkubwa uliokuwa pembeni ya sanamu la goroza na kupunguza kiza ndani ya pango..



    "Sadaka imefika ..." aliongea na kuanza kutoka nje ya pango lile huku kichwani mwake akiliona lile gari la kina baraka linavyo jikokota kwa mwendo dhaifu...



    "Haya muda umefika mbweha mtaenda kuchukua sadaka sita zipo barabarani ....mzee juma njoo nikuoneshe ukawachukue tuje tufurahie damu zao" malikia kikongwe aliongea baada ya kutoka nje na mzee juma haraka akamsogelea mzee yule..



    Kwa hisia na maajabu malikia akamuelekeza mzee juma sehemu waliyo kwama akina baraka.. na mzee juma kwa muujiza mkubwa aliwaona wale marafiki sita waliokuwa ndani ya gari .



    "Haya chukua mbweha sita uwaongeze mkalete hiyo zawadi " malikia alimuamuru mzee juma...



    Wakatoka vijana sita kwenye kile kikundi cha washirikina wakiongozwa na mzee juma wengine wakiwa na mishale mashoka na wengine mikuki huku wengine mapanga ambayo hutumika na kikosi hiki cha mbweha kukutolea sadaka .

    jumla walikuwa saba wakaanza kuondoka kwa kukimbia wakielekea barabarani kuwachukua akina baraka ....huku mioyo yao ikiwa imetawaliwa natamaa ya kumwaga damu...



    "gola mchukue diana mrudishe kwao haraka kwanjia ulio itumia kumleta" mzee yule akamuamuru gola ambae hakupendezwa na amri ile kwani nia na matamanio yake ilikuwa kwa msichana diana usiku wa leo.



    Gola akamuinua diana ambae hakuwa na fahamu kabisa akamuweka begani kisha akamtazama mama diana kwa macho ya chuki.

    gola akageuka na kutikomea akiwa na diana begani...



    "Haya mliobakia anzenu ibada ya kukaribisha sadaka ya usiku huu wa kafara"..... yalikuwa maneno ta malikia....





    31December.

    Baraka alishuka na kwenda mbele ya gari na kufunua lile bati linayo ifunika injini na hapo macho yake yaka kutana na moshi kutokea kwenye injini.



    "Dah gari imechemsha tukisema tuisubiri ipoe inabidi tukae saa zima ....ila kutoka hapa hadi kwenye mashine ya wind walter ni kama dakika kumi na tano hivyo napendelea tukachukue maji huko ili tusichelewe sana" baraka aliongea huku akiliangalia gari lake lilio fuka moshi...

    baraka alikuwa mzoefu wa barabara hii mara nyingi alishawahi kuitumia na kutembea sana eneo la wind walter

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "dah hii ilishakuwa mbaya na mama nilimuahidi nitampigia jioni mpaka sasa hivi saa mbili usiku sijampigia na hapa naona mtandao haukamati" sarah alilaani maana alijua muda ule wazazi wake wanamtafuta kwenye simu...

    "Ah usijal chukua tablet yangu uwa pigie kwa namba yangu ya zantel maana zantel hapa ina kata kwa njia ya satelite" baraka alio ngea kisha akawageukia gadyson na john

    "oya wazee wa kazi tufanye maamuzi ya haraka" baraka aliwasihi

    "ok kama vipi hawa bibie tuwaache sisi tukachukue hayo maji haraka" john aliongea na muda huo baraka akafungua mlango wa mizigo na kuchukua dumu lisilo na kitu ndani kisha akamsogelea neema.

    "sasa jamani tunawaacha humu kwenye gari sisi tunakuja haraka" baraka aliongea na kumbusu neema kwenye paji la uso(neema na baraka walikuwa na mahusiano ya kimapenzi"



    John nae alimsogelea msichana dolla na kumbusu kwenye midomo yake..."kuwa na amani sawa mpenzi" john aliongea baada ya kumpiga busu na dolla alitikisa kichwa kuafiki. ..pia john na dolla walikuwa ni wapenzi



    Ni sarah pekee ndie alikuwa msichana asie kuwa na mpenzi kwenye safiri ile yeye mpenzi wake alikuwa akimsubiri kwenye ile hotel walio panga kwenda kushrehekea mwaka mpya pale bagamoyo.



    Gadyson nae hakuwa na mpenzi kwenye safari ile ila kuna wakati alijaribu kumchombeza sarah walipo kuwa mbugani mikumi, lakini sarah alionesha msimamo na gadyson akawa kalifutilia mbali lile swala.



    Baraka akachomoa ufunguo wa gari yake na kuutia mfukoni akiwa na kidumu aliwasha touch yake yenye mwanga mkali akaaanza kuongoza njia akiwaongoza john na gady kuelekea kwenye maji wakiwaacha wasichana watatu ndani ya gari.



    Tayari ilikuwa ni saa mbili usiku na upande wa magharibi mwezi mkubwa wa kuvutia ulikuwa una chomoza.



    Kile kikosi cha vijana mbweha kikiongozwa na mzee juma kilikuwa kime wasili eneo lile kwa usiri na ukimya wa hali ya juu na wao walikuwa upande wa pili wa barabara na waliwashuhudia akina baraka wakiwaacha wasichana ndani ya gari na wao wakitokomea ndani ya msitu.



    "sasa watu watatu wafuateni hao wa kiume sisi tunaenda kuwakamata hao wasichana wao tuna wapeleke kwa goroza" mzee juma aliongea na muda huo vijana watatu wakainuka na kuwafuata kina baraka ...vijana watatu hao walifuata kwa kuwazunguka na kwa mwendo wa ukimya mkubwa.



    "dalu wanyatie kimya kimya na wasikuone ukifika jaribu kuufungua mlango wa gari" mzee juma aliongea na kijana dalu akiwa na panga aliondoka akiwa kajikunja kuanzia kiunoni huku aki hama mti hadi mti akihofia ule mwanga wa mbala mwezi usije kumfanya aonekane.



    Ilimchukua dakika kumi na mbili kufika pale kwenye gari ali kokota kokota akiwa anatembele magoti aliufikia mlango na kujaribu kuvuta kile kitasa lakini haukufunguka akauwacha na kutambaa tena ili akajaribu kufungua mlango wa upande mwingine..



    Ndani ya gari wasichana hawakutambua lolote dolla na neema walikuwa wakisikiliza mziki kwenye ear phone na sarah alikuwa busy na tableti akihamisha namba za wazazi wake ili awapigie.....



    Baraka na wenzake walitembea kama dakika kumi kisha akasita kichwani kwake akiwa kuna kitu amekumbuka

    "ah nime fanya ujinga ujue humu ni mstuni na kuna wadudu wa na wanyama siku paswa kuiacha bunduki" baraka aliongea huku akisimama

    "ilo nalo neno" gadyson alijibuCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok ikimbilie sisi tuna kusubiri hapa" john aliongea na baraka akaweka dumu chini akaanza kukimbia kuirudia bunduki yake huku touch yake ikimulika msituni mule ipasavyo .



    Dalu wakati ule ana zunguka ghafla aliona mwanga wa touch kwa mbali ukija kueleke kwenye gari akahamaki na haraka akajua kina baraka wana kuja... haraka dalu akaingi uvunguni mwa gari...



    Sarah alijaribu kumpigia mama yake lakini mama yake alipo pokea simu sarah aliisikia sauti ya mama yake lakini mama yake hakumsikia sarah..

    "dah mtandao una sumbua kweli" sarah alisema na hapo akaona mwanga wa touch ukija upande wao "oh mara hii wamesha pata maji... ngoja nishuke nimpigie mama huenda nje ya gari nitaongea nae vizuri" sarah aliongea na kutoa lock ya mlango na kushuka akakifuata kisiki cha mti wa mbuyu akakipanda mara moja na kuanza zoezila kumpigia mama yake..



    na muda huo baraka nae alikuwa ameisha ifikia gari...





    31December



    "haloo nani mwenzangu" sauti ya mwanamke upande wa pili iliuliza na hapo moyo wa sarah ukachanua kwa furaha na akazidi kusimama imara juu ya kisiki kile

    "mama mimi ni sarah simu yangu imeisha chaji ila moyo wangu hujaridhika mwaka 2016 upinduke bila kusikia sauti yako" sarah aliongea kwa furaha

    "asante mwanangu tumekupigia sana ukawa hupatikani upo wapi muda huu" sauti ya mama sarah iliuliza kutokea upande wa pili

    "Ah nipo bwenini muda huu najisomea" sarah aliongea uongo kwani wazazi wake walijua yupo chuo hakuwashirikisha chochote kwenye safari hiii

    "haya mwanangu nimemtuma dereva wetu akuletee zawadi nilizo kuandalia kwa pongezi ya kuvuka mwaka 2016 salama ...ni zawadi nzuri sanaa mwanangu acha nimtumie na hii unayoitumia ili asipate tabu" mama sarah aliongea kwa wahka mkubwa na kukata simu.



    moyo wa mariamu ulipiga kwani alijua ataumbuka akiwa pale juu ya kisiki akashindwa afanye nini ili kumdanganya tena mama yake... na simu ilikuwa imekatwa!



    Baraka alisogea mpaka kwenye kioo cha gari walipo kuwepo neema dolla kisha akagonga na wasichana wale wakafungua

    "mbona upo peke yako " neema aliuliza

    "nilisahau bunduki si unajua njiani tunaweza kukutana na swala ...akawa bahati yetu" baraka aliongeakwa utani huku kumtupia sarah alie simama juu ya kisiki ..



    Ghafla yowe kubwa lilimtoka baraka kurunzi alioshika ikimdondoka huku akihisi kitu chenye ncha kali kikimcho kwenye paja lake...



    Naamu ulikuwa ni mshale ulio fyatuliwa ki ustandi ukitokea kwenye upinde wa mzee juma ndio mzee juma alikuwa ameamua kuanza kazi na hilo lilikuwa shambulizi lake la kwanza.



    Dolla na neeama walishtuka sana hawakujua nini kimemtokea baraka ambae alikuwa chini akigaagaa huku kilio cha maumivu kikimtoka.



    Yowe lile lilimshtua sana sarah hadi kufikia hatua ya kuichia ile tablet bila kujua akageuka kuangalia kule kwenye gari.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nini baraka" neema alipaza sauti huku akisukuma mlango



    "nimechomwa ..... ni mshale" baraka alilalama muda dolla alikuwa kwenye bumbu wazi ya aina yake..



    Neema alijaribu kushuka amuangalie mpenzi wake lakini hapo hapo kwa kihoro kikubwa alishuhudia watu watatu wakiwa na siraha za kienyeji wakija mbio kuelekea upande wao ikawa zamu ya neema kupiga yowe la kuhitaji msaada

    "mamaaa aaaa!" nema alijikuta akimuita mama yake huku akifanya jitihada za kurudi ndani ya gari wajifungie..



    Sarah alikuwa anapiga hatua kusogelea gari "kuna nini " alijiuliza moyoni huku fikira zake zikidhani alitamka kwa sauti na ghafla macho ya sarah yali mshuhudia dalu akitoka uvunguni mwa gari akiwa na panga ... na muda huo akasikia yowe la neema.



    Hapo sarah alihamanika na upeo wake ukatambua roho zao zilikuwa hatarini , sarah aligeuka na kuanza kutimua mbio akitokomea msituni huku akijaribu kuita ba kupiga kelele za kuomba msaada msaada na nyuma ya yake dalu alimkimbiza kwa mwendo wa ajabu...



    Upende wa gadyson na john********kabla ya yowe*********



    "Dah kimsitu kimetulia hadi raha" john aliongea wakati wakimsubiri baraka..



    "mazingira yapo poa simu yangu ingekuwa na flash light ninge.." gadyson alionge kisha akaacha huku macho yake yakiwa yame ona kitu kwa mbali kitu hicho kikiwa kama kimehama kutoka mti hadi mti mwingene na kisha haku kiona tena.



    "Ebwana nimehisi kama kuna kitu ama mtu alikuwa kule" gadyson aliongea

    "wapi...."john aliuliza na gady akamuonesha lakini wote hawakuona kitu...

    "hizo pombe ulizo kunywa mchana bado hazija kutoka kichwani"john aliongea huku akicheka



    "dah kweli acha nikakojoe huenda bado nipo kwenye hangover" gadyson aliongea huku akisogea kama hatua kumi na na akawa ana kojoa akimuacha john akibonyeza bonyeza simu yake....



    Nyuma ya john waliibuka watu wawili walio mnyatia kwa kumvizia na muda ule walikuwa nyuma kabisa ya mgogo wake ...

    Ghafla john akijikuta akikabwa kwa roba kali akahamanika vikali simu yake ikamdondoka akawa analeta purukushani akitupa mikono hovyo huku akikosa nafasi ya kupiga kelele kwani roba kali ilikuwa imebinya koromeo lake ipasavyo... na muda ule ule mikono yake ika kamatwa na kufungwa kamba ..



    Gadyson alihisi purukushani na alipo geuka alimuona john akiwa kakabwa na mtu mmoja huku mwingine akimfunga kamba mikononi....

    na muda huo huo macho mawili yalishudia mtu mwingine wa tatu akija upande wake akiwa na gongo mkono wa kulia huku mkono wa kushoto ukiwa na shoka ...



    wakati akiwa kwenye kihoro kikubwa hapo hapi akasikia yowe la baraka kwa mbali....



    Tume vamiwa. !!!neno hili lilipita kichwani na muda huo gady alipiga hatua kadhaa na kuanza kukimbia ..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini kabla hata ya kukimbia hatua ishirini gongo lilio rushwa na yule bweha wa goroza lilitua kichwani kwake na kumtupa chini kama mzigo huku akihisi kupoteza fahamu......



    Alijiinua tena na kukimbia safari hii alikimbia bila tahadhari na huku giza dogo ukichanganya na kupigwa kichwani na lile gongo hakuona vizuri mbele na hatimae aliuvaa mti na kuanguka chini na muda huo huo aliona mtu mwenye shoka akimsogelea sehemu ile aliyo anguka!

    "pumbavu usijitikise shoka hili litaka kata shingo yako" yule mtu alimfokea....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog