Simulizi : Siku 100 Za Mateso Ya Kuzimu
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Swali kuu likawa Bastard ni nani? Kila kitu kwenye kijiji kile ilikuwa ni michoro isiyokuwa na maana yoyote.
Macho yake yaliendelea kugota kwenye simu ile ambayo neno ‘find the bastard’ liliendelea kusomeka kwenye kioo cha simu .
Akiwa amekodolea macho maandishi yale, akaona kitu kingine ambacho kilimsababishia taharuki kubwa.
Katika sehemu inayoonesha alama ya mnala wa mtandao kuwepo ama kutokuwepo ilionesha uwepo wa ‘bar’ mbili ambazo zilikuwa zinatoweka na kurejea.
Ubaridi ukamsambaa mauongoni mwake, shauku ya kurudi mahali alikotoka ikamjaa kifuani, lile neno ‘Find the bastard’ halikuwa kitu tena mbele ya kupata mawasiliano ambayo yatamwezesha kumrejesha alikotoka.
Upesi katika simu ile, akatafuta sehemu iliyoandikwa phonebook, kisha akawa anapekua majina mbalimbali.
Wala haikuchukua muda mrefu, akalifikia jina la kaka yake aitwaye Kiba, akaipiga namba ile na kuweka simu sikioni.
Muda mfupi badaye, mara simu ya upande wa pili ikaanza kuita, Amosi hakuamini. Jasho likamtoka. Furaha isiyo ya kawaida ikajitengeneza kifuani mwake.
Akaamini kwa kuwasiliana na ndugu yake yule ni mwanzo wa kupata msaada na kutolewa kwenye sehemu ile aliyoangukia na kukwama. Sehemu iliyokuwa na mauzauza na vingi vioja. Simu iliendelea kuita na haikupita muda mrefu ikapokelewa!!!.
*****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
GEITA TANZANIA-2010
Wiki moja ilikuwa imepita tangu taarifa za ajali ya ndege ya Panasonic Airline ipotee, duru mbalimbali za kichunguzi hazikuwa na majibu yenye kuwiana juu ya ni wapi ndege hiyo iliyokuwa na abiria takribani 201 imeangukia.
Kwa wiki nzima habari kuu katika vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC , Aljazeera, CNN na Globa Tv, ilikuwa ni juu ya ajali hiyo.
“Wataalamu wanaoendesha uchunguzi kuhusu ndege ya Panasonic Airlines iliyopotea siku sita zilizopita baada ya kupoteza mawasiliana wanasema hakuna dalili zozote za kutokea mlipuko ikiwa angani wakati huu Satalite za China zimegundua vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni kutoka katika ndege hiyo.” Mtangazaji mmoja wa Global Tv aitwaye Gladnes Malliya alilipoti.
Ni taarifa hiyo ndiyo iliyowasogeza familia ya marehemu mikidadi. Kiba na wadogo zake walisogea kando ya televisheni kufutilia habari hiyo ambayo ilikuwa ni muhimu kwao.
Kwa wakati huo walikuwa wamakeaa matanga baada ya kuwa tayari wamefanya mazishi yam zee Mikidadi aliyefariki kwa presha baada ya kupata taarifa juu ya mke wake Greta na mwanaye Amosi kuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye ndenge ile!.
“Wataalamu kutoka China wamesema moja kati ya satalite kumi walizotuma kutafuta mabaki ya ndege hiyo wamegunduwa vifaa ambavyo vimeokotwa chini ya bahari na vingine nchi kavu ambavyo, vinasadikiwa kuwa ni vya watu waliokuwemo katika ndege ya Panasonic iliyotoweka tangu siku ya Jumapili.
“Operesheni ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo zimepanuliwa zaidi katika bahari ya Andaman inayokaribina na bahari ya Pacific katika eneo la magharibi mwa Malaysia na bara la Amerika mbali kidogo na eneo ambalo ndege hiyo inashukiwa huenda ndiko iliko angukia ikiwa na abiria 201
“Tayari Marekani imetuma ndege zake katika eneo la anga ambalo satalite za China zimegunduwa mabaki ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya watu waliokuwemo katika ndege hiyo.
“Wakati huo huo wataalamu wa Marekani wamesema hakuna viashiria vyovyote vinavyoonyesha kuwa kulitokea mlipuko katika ndege hiyo wakati ikiwa angani kabla ya kuanguka.
“Ndege hiyo ya Marekani iliokuwa ikisafiri kutoka jijini Newyork city kuelekea jijini Pekin, landon, Honkong kisha Adis ababa nchini Ethiopia ilipotea kimiujiza ikiwa angani na watu 201. Zaidi ya nchi tisa ikiwemo Tanzania nchi pekee kutoka bara la Afrika, zinashiriki katika opereshani ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo ambapo hadi sasa juhudu hizo hazijazaa matunda.” Mtangazaji alimaliza kusoma taarifa ile
“Mungu wangu!” Kiba, alihamaki machozi yakimlenga, hapakuwa na chochote cha maana juu ya mustakabali wa wapendwa wao.
“Bado riwaya ni zile zile.” . mtu aliyekuwa pembeni yake alisema.
Bado, hakuna taarifa yeyote zaidi ya kutueleza wameokota sijui mizigo ya abiria. Kitu ambacho bado kinatuacha na jakamoyo ileile juu ya uhai wa wapendwa wetu”
“Tufanye nini?”
“Sasa wewe unadhani sisi tutafanya nini zaidi ya kusali kwa ajili ya watu wetu”
“Kweli kabisa…sasa?”
“Tufanyeni ibada”
“Sasa hivi?”
“Ndio”
Kwa pamoja Kiba na nduguze sambamba na watu wachache weingine walipiga magoti na kufanya maombi..
“Nkriii, nkrii, nkrii” wakiwa katika maombi simu ya Kiba ilikuwa ikiita kwa nguvu.
“Weka simu yako silent” mtu wa pembeni alimnong’ona sikioni mwa Kiba. Wakati anaweka silent simu ile, macho yake yalipotua kwenye kioo, hakuamini alichokiona, mpigaji wa simu ile alikuwa ni nduguye!.
Amosi Mikidadi. Moja ya watu walipotea kwenye ndege ya Panasonic Airlines, akiwa anasafirisha maiti ya mama yake mzazi.
******
Amosi simu ikiwa sikioni mwake akasikia ikipokelewa.
“Hellow,” alisema. Hata hivyo, hakujibiwa,kukawa kimya, akaitoa simu sikioni na kuitizama, akaona bado simu ile iko hewani, lakini mzungumzaji wa upande wa pili, hasikiki.
“Heloo!”akasema tena kwa nguvu.
“Ti, ti, ti” sauti ndogo ikatoka simuni, kisha ikakatika, halafu mtandao ukapoote!.
“Mungu wangu, nini hiki!!”
“Kwanini unanitupa mja wako kiasi hiki,” alizunghumza peke yake kwa kulalama huku macho yakiendeleakuwa kwenye simu ile.
Neno find the bastard likiendelea kujidai kwenye simu yake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mtamndao kwenye simu ile haukurudi, Amosi akahaha huku na kule, lakini wapi, neno ‘network error’ ndilo lililokuwa likitokea, likiwa na maana kuna tatizo la mtandao.
“Baba wa mbinguni nisaidie kiumbe wako, nipe majibu ya matatizo haya kama ulivyofanya kwa wanao Ayubu na Yohana .” Amosi alisali kimoyomoyo huku maneno yale yakibeba hisia kali hadi usoni. Machozi yalimbubujika
Kila kitu kwenye maisha yake kilikuwa ni michoro isiyokuwa na maana yoyote. Vitendawili na mafumbo yalikuwa yamemzingira kila kona.
Nafsi yake ikakiri wazi kwamba hakuwa katika dunia ya kawaida.
Alimini pale alipokuwa ilikuwa ni sehemu fulani kuzimu.
Swali kuu likawa, ni kwanini yupo sehemu ile? japo kuna wakati nafsi yake ilikiri alikuwa pale kwa makusudi lakini bado hakujua kusudio ni lipi na limeandaliwa na nani.
Kuna wakati alihisi pengine yupo ndotoni na yale yaliyokuwa yakimtokea yalikuwa ni matukio yanapita akiwa amelala usingizi wa pono.
Hata hivyo, wakati dhana hiyo alipingana nayo mwenyewe, maumivu na machungu aliyokuwa akiyapata alichelea kuamini kama yupo katika ndoto, alimini yale yalikuwa ni maisha ambayo aliishi. Mgogoro wa ndani kwa ndani ukaikoroga akili yake.
Siku nane tayari zilikuwa zimekatiwa, hakuwa ameweka chochote ndani ya tumbo lake, ajabu ni kwamba hakuwa ni mwenye njaa wala kiu!.
Hali hiyo, ikamfanya ajihisi pengeine yeye alikuwa amekufa, na pale alipokuwa alikuwa katika maisha ya roho.
Kadhalika, dhana hiyo ikapingana na utashi wake mwenyewe. Vipe awe ni roho ilihali ana mwili!.
Vipi awe ni roho ilihali anaishi na wanadamu kama yeye!.
“Kama mimi si mtu bali ni roho, basi hata hawa wawe ni roho pia!” akajiambia mwenyewe.
“Siko, kuzimu, lakini pia siko duniani!!” akawa anaongea peke yake.
“Kama siko kuzimu ama duniani nitakuwa wapi? Shimoni? Baharini? Mbinguni? ama wapi?”
Hakuna mtu aliyemwelewa Amosi, wengi walimwona kama mwendawazimu aliyetokea kusiko julikana, walimtizama kama mwehu aliyewahi kuwa na akili nyingi kabla ya kukumbwa na maradhi ya akili.
Naam! aliishi katika hali hiyo kwa siku nyingi sana.
Katika siku hizo nyingi. Simu yake ilindelea kuwa ‘off’. na hapakuwa na mahali pengine pa kupata nishati ya umeme ambayo ingemwezesha kuchaji kifaaa kile cha mawasiliano.
Katika kijiji kile maisha yalikuwa nyuma miaka takribani 50. Wao wakati ule kwao ilikuwa ni mwaka 1960.
“Nahitaji nipate sehemu yenye umeme, nichaji simu yangu” siku moja aliongea na mzee mmoja mlinzi.
“Simu na Umeme, ndio vitu gani”
“Hii hapa” alitoa simu ile mfukoni na kumwonesha mtu yule.
“Wooh ni nzuri inafanana na calculate, umeipata wapi hii?”
“Nitakueleza nioneshe mahali penye nishati ya umeme”
“Umeme ndio nini?” mzee yule alihoji. Amosi alichoka. Alishindwa hata kuendelea kuzungumza. Alichofanya ni kurejesha simu yake katika mfuko na kuendelea na maisha mengine.
Katika maisha yake ya kuhangaika na kulanda kama chizi, hakuwahi kusikia tena yale maajabu ya kuongea na mtu mawazoni, hakuwa kumwona yule mtoto mdogo ambaye alikuwa ni yeye mwenyewe, wala hakuwahi kujihusha na familia ile ambayo ilikuwa ni ya kwakwe mwenyewe.
Kadhalika, hakuwahi kula wala kunywa kama bidamu wa kawaida.
Ingawa hali ile haikuwa na athari kwakwe, ilimnyima raha, alijiona yupo tofauti na binadamu wa kawaida.
Kwa miezi miwili, sawa na siku 60 Maisha yake yalikuwa ni ya kutangatanga, malazi yake yalikuwa ni katika soko la kijiji kile, alikonda na kudhofu kwa mawazo.
Katika siku zote za maisha yake alichofanikiwa kujua kwenye kile kijiji ni jina la kijiji hicho! Kiliitwa Guem
Kila jioni ya siku imalizikapo, aliungana na walinzi wa soko la Guem na kuweka ubavu wake.
Hali ya kutazamwa kama mtu aliyedata, haikuwa kitu kwake, alimini siku moja angerudi kwenye maisha yake ya kawaida na mambo yote yangebaki kuwa hadithi.
****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ingawa watu wengi walimchukulia kama mwendawazimu lakini walinzi wachache wa soko la kijiji cha Guem walivutiwa na Amosi. utashi na akili alizo kuwa nazo katika kuchanganua mambo mbalimbali ilikuwa moja ya vitu vilivyo wavutia na kuwashangaza watu hao.
“Mimi nashindwa kuamini kama jamaa ni mwendawazimu,” siku moja wazee wawili walinzi wa soko walikuwa wakimteta Amosi wakidhani amelala.
“Ana akili nyingi sana, siamini kama jamaa ni kichaa.”
“Inawezekana ni mpelelezi”
“Wapelelezi ndio hujifanya vichaa?”
“Ndio. Mashushu wengi wakati mwingine hujifanya wendawazimu ili wasijulikane kwa maadui zao”
“Inawezekana.” mazungumzo yale yalisikika vizuri masikioni mwa Amosi, alijisikia vibaya kuona anavyoishi mithili ya mcheza filamu ambaye yupo katika igizo fulani.
“Naombeni niwaambie kitu?”Amosi aliongea kwa sauti. Jamaa wakastuka.
“Mimi sio kichaa, wala sio mpelelezi kama mnavyo dhani….
“Nataka mtambue jambo moja niko hapa kwakuwa nimenasa kurudi kwenye dunia yangu.”
“Dunia yako!!”
“Ndio, dunia yangu, dunia niliyokuwa naishi sio hii, huku ni kuzimu, niko mbali sana najihisi niko jela” Amosi alisema uchungu,
Maneno yale yalizidi kuwachanganya wale wazee walinzi.
Utata wa akili ya Amosi ulikuwa hapo.
“Duh” mtu mmoja aliguna.
“Ndio maana unadhaniwa huenda wewe sio mzima!” mzee mwingine akasema huku akionekana kufurahishwa na namna Amosi anavyojipambanua.
‘Lakini kijana kwanini usiende kwa the bastard.? anaweza kukusaidia” mzee mwiingine alisema.
Maeneno yale yalikua kama bomu masikioni mwa Amosi.
“Unasema!!” aliuliza kwa kiherehere.
“Kwanini usiende kwa the bastard.? anaweza kukusaidia,” mtu yule alirudia tena kumwambia.
Amosi ni kama vile alikuwa amemwagiwa maji ya baridi, kitu alichokuwa akiambiwa hakuamini kama ndicho kilichokuwa kikimsumbua kwa siku zote.
“Bastard!!” alisema kwa mshangao.
“Ndio. Jamaa ni bingwa sana wa matatizo kama yako.” Mtu yule akaendelea kumpasha.
“Mnaweza kunipeleka?”
“Ni wewe tu ukiamua”
“Lini?”
“Hata kesho asubuhi,” Mtu yule alimjibu.
Usiku huo ulikuwa mrefu kwa Amosi, alimini kabisa Bastard ni moja ya mtu anayeweza kuwa na majibu ya vitendawili vyote aliyokuwa akipitia maishani mwake.
Taswira ya matukio yote ya nyuma ikawa inajitengeneza kichwani mwake.
Tangu siku ya kwanza alipojikuta yupo mstuni akiwa ameangukia mbali na wenzake katika ajali mbaya ya ndege, muda mfupi badaye anakutana na majeruhi wale.
Kisha kutokewa na mauzauza yanayo ondoa uhai wa wenzake kadhaa.
Kama haitoshi, anatokewa na mama yake akiwa hai, ilihali alikuwa amemsafirisha kwenye ndege ile akiwa maiti. Mama huyo anmpa kipande cha ubao kilichoandikwa ‘find the bastard’ mambo yale yaliendelea kukisumbua mno kicha chake.
Akaendelea kukumbuka namna wenzake wote walivyokufa kwenye mazingira tata na kiumbe chenye umbo lenye kufanana na moshi.
Lakini pia, kumbukumbu zikaendelea kumpeleka hadi siku alipokuwa akiukimbizwa na moshi ule na kujikuta ametokeza kwenye kijiji cha Guem, ambapo pia, alikutana na mengi ya kustajabisha.
Akiwa katika bahari ya kumbukumbu hizo, alipitiwa na usingizi mzito hadi alipostuliwa alfajiri kukiwa tayari kumepambazuka.
“Oyaa kumekucha wewe,” Amosi alishitushwa na sauti ya jamaa aliyekuwa akizungumza naye usiku juu ya habari za kwenda kwa Bastard.
Alijinyanyua kivivu, akajinyoosha, fikra zake zikiwa katika msukumo mkubwa wa jambo moja tu. Kuonana na Bastard.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tunakwenda saa ngapi?” ndilo swali la kwanza alilohoji kabla ya salamu.
“Hata sasa hivi kama upo sawa.”
“Twende” Amosi aliitikia.
Hakuwa na cha kusubiri, alihitaji kuopata majibu na suluhu ya matatizo yale.
Mwanaume yule baba wa makamo, ambaye alijulikana kwa jina la Samsoni Magoma, aliongozana na Amosi.
Naye kama ilivyokuwa kwa watu wengine wa Guem waliamini akili za Amosi zilikuwa nusu fyatu nusu timamu. Alipitisha uamuzi wa kumsadia kijana yule aliyetokea kumpenda ingawa alikuwa na uchizi wa masaa.
“Itabidi tupite nyumbani kwangu…”
“Kuna nini?”
“Ili nipate kukoga, tupate kifungua kinywa, kabla ya kwenda huko,” Samsoni Magoma alimwambia.
“Haina neno”
“Lakini jambo moja bwana mdogo….” Aliendelea kuzungumza na Amosi.
“Jitulize,”
“Kivipi?” “Nisingependa uwe mwongeaji sana, maana maneno yako wakati mwingine ndio yanazidisha ugonjwa wa akili.” Samoni alimwonya, Amosi hakutia neno,ingawa hakuvutiwa na namna alivyochukuliwa kama mwendawazimu.
Walipita nyumbani kwa mtu yule, akaoga na kupata stafutahi ya chai na mihogo. safari ya kuelekea kwa Bastard ikaanza.
“Tumekaribia nyumbani kwa Bastard,” Samosoni aliongea, mapigo ya moyo ya Amosi yakaanza kumdunda.
Hakujua kwanini anakuwa kwenye hali ile, hata hivyo aliendelea kujikaza kiume.
Ndani ya nukta hizohizo, aliisikia simu yake iliyokuwa ndani ya mfuko wake wa suruali ikijiwasha!!
Alishangaa maaana simu ile iilikuwa imezima chaji muda mrefu.
Aliingiza mkono mfuko na kuitoa, akaona simu ikiwa inakamilisha mchakato wa kujiwasha, tena ikiwa imejaa chaji.
Aliendelea kuikodolea macho simu ile hadi ilipomaliza kuwaka.
Hakuamini macho yake kwa kile alichokiona punde baada ya simu kujiwasha.
Kwanza mtandao ulionekana kuwepo kwa asilimia miamoja, pili lile neno ‘find the Bastard’ halikuwepo, safari hii lilitokea neno jingine jipya.
Neno hilo lilisomeka hivi:
“Kill the bastard” Amosi alihisi mwili wake ukilowa jasho.
maneno yale yalikuwa ya Lugha ya Kingereza yakiwa na maana muue bastard!
“Mungu wangu!!” Amosi alichanganyikiwa. Kengele ya hatari iligonga kichwani mwake.
Akabaki akitizama simu ile kama vile kuna mtu ambaye yumo ndani ya simu ile, ambaye ndiye anayetoa mwongozo wa mambo yote yale.
“Ni nini?” Samsoni Magoma aliyekuwa hatua kadhaa mbele aliuliza baada ya kumwona Amosi akiwa amesimama huku akikodolea macho kifaa ambacho hakuwahi kukiona tangu azaliwe.
“Umekipata wapi hicho?” akauliza swali ambalo kwa Amosi lilikuwa ni la kipumbavu.
“Hivi Bastard ni nani haswaa?” Amosi akauliza akiwa amechanganyikiwa,
“Si ndio nakupeleka ukamfahamu na akusaidie mtatizo yako, ama?”
“Hujanijibu bado?”
“Sijajua mantiki ya swali lako.”
“Nijibu kwanza, nitakueleza mantiki badae”
“Unamtaka bastard humtaki?” Samsoni Magoma naye akauliza kwa ukali.
“Namtaka”
“Basi twende….kwanza tumekwisha fika, ni paleee…..pale kwenye kile kicha kile...” Akasema huku akisonta kichaka kikubwa kilichokuwa mita kama miambili kutoka mahali walipokuwa wamesimama.
****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kelele za taharuki alizozitoa Kiba baada ya kuiona simu ya Amosi, mtu waliyeamini amepotea na abiria wengine katika ndege ya Panasonic Airlines ilimshitua kila mtu.
“Amosi… Amosi… simu ya Amosi!!...Amosi anapiga” Kiba alipaza sauti.
Watu wote waliokuwa kwenye ibada kuomba uponyaji kwa ndugu wote walipotea na ndege ile. Walikurupuka na kukimbilia pale Kiba alipokuwepo.
“Mungu wangu!.. huyu ni Amosi” mtu mmoja aliuliza.
“Ni yeye”
“Bado anaishi!!!” mtu mwingine akadakiza.
Kiba alibofya kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni.
“Hellow…Hellow… Hellow!!”
“Weka Loud speker” mtu mwingine akalopoka, upesi Kiba akabofya sehemu ya kuweka sauti kubwa.
“Hellow” Kiba akaendelea kuita upande wa pili kwa nguvu. Watu wote walikuwa kimya. Kusikiliza kama mtu atakaye ongea simuni ni Amosi ama laa.
Simu ile ilikoroma, kisha muda mfupi kikasikika kimlio kikilia:
“Ti, ti, ti,” halafu ikakatika!
“Imekatika!”
“Mpigie” watu wakasema kwa sauti kubwa. Kiba hakuchelewa pale pale akaipiga ile namba.
“Namba unayopiga haipatikani” ndilo jibu walilolipata.
“Ayaaaa!!”
Sauti za mfadhaiko ziliwatoka watu wale. Wakaipiga ile namba mara nyingi zaidi, lakini jibu likabaki kuwa lilelile. Namba ilikuwa haipatikani.
“Sasa tufanye nini?” mtu mmoja alihoji
“Tupeleke taarifa polisi” mwingine akashauri.
“Lini?”
“Kesho asubuhi”
“Hapana twendeni sasa hivi” Kiba naye akasema. Naam muda mfupi badaye, taarifa juu ya kupata simu kutoka kwa moja ya wasafiri waliopotea na ndege ya Panasonic Airlines zilikua katika mikono ya jeshi la polisi mkoa wa Geita.
“Unauhakika namba hii ni ya Amosi?” kamanda wa mkoa Geita, Debora Majige alimuuliza Kiba.
“Nina uhakika hii ni namba yake afande”
“Sasa kwanini haipatikani?”
“Hilo hata sisi limetuchanganya” Kiba alisema.
Kamanda yule wa polisi, naye aliipiga namba ile. Jibu lilikuwa ni lilelile. Haikupatikana.Siku hiyohiyo taarifa hiyo ikatumwa makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini.
Masaa machache madaye wanausalama wa Tanzani na na kitengo cha CIA (Central Intelligence Agency) kutoka Merekani, ambao kazi yao kubwa duniani ni kuchunguza Vitisho, matukio ya kijasusi toka nje ya marekani, kwa pamoja walikuwa wakifuatilia sehemu simu ile ya Amosi ilipotokea.
Kazi ya kuchunguza simu ile mahali ilipotekea, haikuwa kitu kikubwa kwa CIA, muda mfupi badaye kila kitu kilikuwa kimekamilika.
Simu ile ilijulikana mahali alipokuwa imetokea. vikosi mbalimbali vya ukoaji, makomandoo wa kimataifa, wakishirikiana na CIA, walikuwa tayari kufika kisiwani Guem Kumpata Amosi, mtu aliyedaiwa kuwepo hai katika ndege ya Panasonic Arilines iliyokuwa imepotea.
“Inawezekana kweli kuna ugaidi katika jambo hili?”
“Sidhani, lakini ngoja tusubiri ripoti ya oparesheni ya askari waliokwenda huko.”
“Sasa kama huyo mtu aliyekuwa kwenye ndege anaonekana yupo Guem bila shaka hata ndege hiyo ipo mahali fulani kisiwani hapo, je inawezekana kweli setelite zote zilishindwa kubaini kama kuna kitu kinachohusiana na ndege ya Panasonic eneo lile?”
Watu wa usalama walikuwa wakizungumza.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila mtu alikuwa na shauku ya kujua matokeo ya uchunguzi ule.
******
Amosi aliendelea kutetemeka kadiri walivyokuwa wakikaribia kile kichaka, macho yake yalikuwa yakitua kwenye kioo cha simu yake, neno ‘Kill the Bastard’ liliendelea kung’aa kwa nguvu zaidi kadiri walivyokuwa wakikisogerea kichaka kile.
“Tumefika na bahati nzuri tumemkuta,” mtu aliyekuwa naye alimwambia.
Alisogea zaidi kwenye eneo lile lenye majani. Amosi alibaki akishangaa, hakuona kitu chochote kwenye kichaka kile japo mwenyeji wake alimwambi pale ndipo alipokuwa bastard na muda ule alikuwepo.
“Mbona sielewi?” Amosi alisema akiwa anangaza macho huku na kule.
“Huelewi nini?”
“Hapa ndipo anaishi huyo nani sijui!?”
“Ndio, ni hapa”
“Yuko wapi sasa?”
“Usiwe na haraka bwana mdogo” mtu yule akamjibu huku akisogelea sehemu ya majani chini ya ardhi. Amosi aliendelea kumfutilia mtu yule anachokifanya.
Magoma alipekenyua kwenye majani yale, kisha akakamata kitu. Kwa nguvu akakinyanyua kitu kile. Naam mfuniko wa chuma uliokuwa umezibwa kwa majani ulifunguka.
“Huu ndio mlango wa kuingia ndani kwa Bastard” Magoma alisema huku akimtizama Amosi kwa jicho lililomwashiria aingie kwenye tundu lile chini ya aradhi.
“Kumbe anaishi chini ya ardhi?”
“Ndio. Ingia sasa” Magoma alimwambia.
“Peke yangu?”
“Ndio”
“Kwanini tusiende wote?”
“Hatutakiwi kuongozana wote kijana, hebu kuwa mwelewa,” mtu yule alifoka.
“Naogopa kwenda peke yangu”
“Unaogopa nini wewe, hebu acha ujinga.” Magoma aliendelea kumkemea, Amosi hakuwa na jinsi, maji alishayavulia nguo, alikuwa hana budi kuyaoga.
Alisogea kwenye tundu lile pana, akachungulia, aliona ngazi za kienyeji zilizotengenezwa kiustadi ambazo zilikwenda chini kabisa na kupotelea kwenye giza zito ndani ya shimo lile.
“Ingia upesi” mtu yule akazidi kumsihi.
Amosi alishika zile ngazi na kutanguliza mguu, alipokanyaga tu, alihisi mwili wote ukimsisimka, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda kasi kuliko kawaida.
“Shika hii” jamaa aliyekuwa bado ameshikilia mfuniko ule alimpa tochi.
Amosi aliendelea kushuka taratibu ndani ya shimo lile refu kwenda chini. Muda mfupi badaye alikuwa akikaribia chini kabisa, giza lilikuwa kubwa, hata hewa ya mule shimoni ilikuwa nzito.
Alipotupa macho kule juu alikotoka, hakuona chochote zaidi ya giza, hofu ilizidi kutanda kifuani mwake, alitambua Magoma alikuwa amefunga ule mfuniko ndio maana hakuna alichoona.
“Kwanini kafunga!!” alinong’ona akwa hasira.
Hatimaye alifika chini kabisa ya shimo lile, aliwasha tochi, akamulika kulia na kushoto, hakuona chochote zaidi ya ukuta ulikuwa na unyevuvyevu wa maji.
Kulikuwa na ukimya wa kutisha, hakuna kilichosikika zaidi ya chakarachara za wadudu ndani ya shimo lile.
“Hellow” alisema kwa sauti ili kama kuna yeyote anayemsikia amwitikie. Lakini wapi, kulibaki kimya. Alishindwa kuelewa eneo alilokuwa ameletwa na mtu yule kama lilikuwa ni sahihi ama kulikuwa na dhamira mbaya. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mara ya kwanza akajilaumu mwenyewe moyoni kwa kumwamini mtu yule kirahisi.
Akiwa katika tafakauri mara akahisi akiguswa na kitu cha baridi begani kwake, alipiga yowe dogo la kuogofya huku akipangusa kitu kile kilichokuwa kimemgusa begani.
Alikuwa ni chura!!. Alishusha pumzi ndefu akajilaumu kwa kutokuwa jasiri kiasi cha kuogopa wadudu kama chura.
Muda huohuo akabaini kitu kisicho cha kawada kwenye sehemu ile ya shimo alipokuwa amesimama. Wakati akifurukuta na kurusha mikono yake kumswaga yule mdudu, kuna mahali aligusa na kuhisi kitu kisicho cha kawada.
Ulikuwa ni ukuta wa shimo lile, kuna mahali kulikuwa na kitu kama ubao.
Alipeleka mkono sehemu ile na kugusa.
Naam ulikuwa ni ubao wenye kufanana na ukuta.
Amosi aliposukuma ubao ule. Ukafungukia kwa ndani.
Chini ya shimo lile kulikuwa na sehemu nyingine ya ndani kwa ndani iliyokuwa na eneo pana mithili ya ukumbi wa disko.
Alipoangaza macho huku na kule, Amosi alikutana uso kwa uso na mtu akiwa anamtizama lkwa macho makali.
“Mungu wangu, kumbe Bastard ni huyu!!.” Amosi alinong’ona.
Akiwa wima, alihisi miguu inakosa nguvu, mwili wake ulikuwa ukitetememeka kwa nguvu, hofu ilikuwa kubwa kifuani mwake.
Mbele yake alikuwa akiangaliana na mtu ambaye hakumtegemea, ambaye nafsi yake iliamini ndiye bastard,
Mtu yule alikuwa amesimama wima, alikuwa amekunja uso, macho yake yake makubwa, mekundu. yalionekana kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na matumizi ya kilevi kama bangi.
Mwili wake ulikuwa mkakamavu, michirizi ya mishipa Ikiwa imetokeza kwenye mikono na uso wake, katika mwonekano huo, pia alikuwaa na mikwaruzo ya hapa na pale kwenye baadhi ya mwili wake.
Uso wa mtu huyo, mrefu mweusi, ulionekana ni kama ulikuwa ukitarajia ujio wa Amosi kwenye makazi yake mule shimoni.
Macho ya Amosi yalisaili mwonekano wa mwanaume yule na kuiona sura iliyojaa chuki na kisasi kikubwa. Kama mtu huyo aliwahi kuwa mwanaume mtanashati, mwenye haiba nzuri, hapakuwa na mvuto uliosalia kwa kiumbe yule
“Wewe si ni Boniphace Ngumije? Kumbe ndiye Bastard!!! Si ulikufa!!...” Amosi alipayuka, alikuwa amechanganyikiwa vibaya sana.
Hakutegemea kabisa kama Bastard anaweza kuwa ni moja ya watu anaowafahamu, fikra zilizokuwa zimejitengeneza kwenye kichwa cha mvulana huyo ni kwamba, Bastard kivyovyote vile hawezi kuwa kiumbe wa kawaida.
Lakini, kitendo cha kumkuta bastard ni mtu aitwaye Boniphace Ngumije, kilimchanganya, wakati akiwa kwenye taharuki hiyo, akakumbuka siku alipofahamiana na mtu huyo.
Alikumbuka siku ya pili tu tangu waanguke na ndege ya Panasonic Airlines na kupoteza mawasilino, wakiwa wanatafuta chakula katika msitu ndipo waliposikia sauti ya mtu anayeomba msaada, sauti hiyo ikiwa anatokea mstuni.
“Ni nani huyo?” alikumbuka wenzake walivyokuwa wakiulizana.
“Atakuwa mwenzetu.”
“Amekumbwa na nini?”
“Sijui” kumbukumbu ya namna walivyokuwa wanajadiliana juu ya mtu huyo anayeomba msaada ndani ya vichaka.
Akaendelea kukumbuka Ngumije alivyotokea akiwa anakimbia.
Wakati anakimbia kulikuwa na moshi wa ajabu uliokuwa ukimfuata nyuma. Na moshi huo ndio ulioua wenzake wote na Boniphace Ngumije mwenyewe akiwa ni mmoja wa watu walioawa kimauzauza.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Amosi akendelea kumkumbuka mtu yule kabla ya kuawa na moshi ule wa ajabu uliokuwa ukifuka kwa nguvu, alisema kwamba yeye pia alikuwa na wenzake waliopotea kwenye kisiwa kile wakiwa na ngalawa yao iliokumbwa na dhoruba.
“Kumbe ulituhadaa!!!” Amosi akasema tena kwa sauti iliyoonesha kuchanganyikiwa.
Aliongea akiwa amemkazia jicho yule mtu ambaye sasa alijidhirisha kwakwe kama Bastard.
Tabasamu baya likajitengeneza kinywani mwa Ngumije ama Bastard, kisha kwa sauti yenye mkoromo kama gari bovu likipandisha mlima akamjibu:
“Mambo yote hayo hayakuwa kwenye uhalisia wa mwili”
“Kivipi? unaongea nini? Sijakuelewa?” Amosi akamvulumushia maswali.
“Hakuna hata moja katika hayo yalipo kichani mwako yamefanyika katika uhalisia halisi”
“Unaongea mafumbo mengi, hebu zungumza vitu vya kuelewaka” Amosi akaunguruma kwa ukali.
Jambo hilo likamfanya Bastard angue kicheko kidogo cha dhihaka, kisha akasema:
“Hujatokewa na kitu chochote Amosi, mambo haya yote ni ndoto tu, unapita kwenye ndoto ukiwa kitandani.” Bastard akazungumza kwa sauti yake ileile yenye mkwaruzo mbaya.
Amosi alipiga kimya, akamtizima mtu yule, akaona uso wenye kuuliza una swali lolote.Naam naye bila ajizi akamhoji tena.
“Kwahiyo hapa niko ndotoni?”
“Ndio.”
“Na wewe uko ndani ya ndoto yangu?”
“Kabisa.”
“Na unaiona ndoto yangu inavyopita kwenye kichwa changu?”
“Ndivyo hivyohivyo Amosi” mtu yule akajibu, tabasamu lake likawa linapanda cheo taratibu na kuwa kakicheko kadogo.
“Ndio maana Soninapa aliinita Bastard, yanii mpumbavu ama mwanaharamu.”jamaa akaendelea kumpasha..
Amosi alichoka.
“Yanii mambo yoote haya yanayonitokea maishani ni ndoto!.... Nahitaji nirudi nyumbani, sihitaji kuendelea kuishi huku hiyo ndio shida yangu kubwa” hatimaye Amosi akaweka rai yake mezani.
“Unataka kwenda nyumbani bila kumuua bastard?” mtu yule akamwuliza.
“Whaat!!”Amosi alihamaki, moyo wake ulianza kupatwa tena na wasiwasi, ile dhana ya awali kwamba, huenda mtu yule alikuwa ni mzimu ikatawala zaidi.
Ndio. Nafsi yake ilikiri kwamba Bastard hakuwa binadamu wa kawaida.
“Kwa nini natakiwa nimuue huyo mtu?” akauliza
“Hii ni njia tu ilitumika kukuvuta ili ufike mahali hapa, hakuna mantiki yoyote katika hili” Bastard akaongea tena kwa mzaha.
Amosi akamwangalia kwa jicho lililosema endelea kuzungumza. Akaendelea.
“Sio sahihi mimi kukuleza, kwa nini uko hapa na kwa nini mambo yote haya yanapita katika ufahamu wako wa ikili ilihali ukiwa umelala usingizi huko maili nyingi sana.
Kazi unayotakiwa kufanya ni moja tu, kufikisha ujumbe wangu mahali fulani, ukifanya kazi hiyo kikamilifu, huko ndiko kwenye majibu ya kila kitu kilichokutokeakwenye maisha yako...”
“Kazi gani?” Amosi akamdakiza.
“Utakaporejea kwenye dunia yako hakikisha unamtafuta mtu aitwaye Soninapa narudia tena, huyu mtu anaitwa Soninapa mtafute huyu mtu mpe ujumbe huu..” Bastard alisema kisha akatoa kijipande chakavu cha karatasi na kumkabidhi mvulana yule.
Amosi alipokea kipande kile, akatupa jicho kwenye maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye karatasi ile, lakini wakati anafanya tendo hilo mara akahisi kama amepigwa na kitu kizito kichwani.
Palepale akahisi maumivu makali yakatambaa kichwani mwake, ndani ya nukta zilezile akahisi anakosa nguvu, akaanguka chini kama mzigo
“Puuuup” akajibamiza kichwa ardhini, macho yake yakakosa nguvu!!
“Nakufaaa!” aligumia maumivu
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NGUVU zilikuwa zikimwishia kwa kasi, fahamu nazo zikawa zinampotea.
“Na...ku...fa” maneno yenye kitetemeshi yalimtoka.
Alikuwa akigaragara pale chini, alishika kichwa chake kilichokuwa kwenye maumivu makali. Aliamini Bastard alikuwa amemshambulia na kitu kizito kichwani.
“Blood fool, Bastard ananiua!” Amosi alinong’ona kimoyomoyo. Alijuta kushuka chini ya shimo kumtafuta yule mwendawazimu.
“Nakurudisha kwenye dunia yako, sina mpango wa kukua,” kiajabu kabisa alisikia sauti ya yule mtu aitwe Bastard ikipita masikioni kama vile amevaa visikilizo vya masikioni ‘hearphone’.
Baada ya mauzauza yale kumtokea, akiwa katika hatua za mwisho kabisa kupotewa na fahamu, Amosi alianza kutapatapa mithili ya kuku aliyekatwa kichwa.
Muda mfupi badaye, akatulia tuli.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment