Search This Blog

MOCHWARI - 5

 







    Simulizi : Mochwari

    Sehemu Ya Tano (5)





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sehemu ya mwili wa mtu huyo upande mmoja,, ambao ni nusu,, alikuwa binadamu mzima,, na upande mwingine nusu alikuwa kaoza anatokwa na wadudu,,, mtu huyo wa kutisha alifungiwa ndani ya mto huo miaka mingi iliyopita.. inasadikika alitukana mizimu,,hivyo akapewa adhabu ya kufungiwa ndani ya mto huo!



    hivyo maiti zilizofufuka kule mochwari,, yeye ndiye alitumiwa na mizimu kuzifufua maiti hizo kimiujiza!!!  ni mganga pekee ndiye alikuwa anaijua siri hiyo!!!  hivyo damu ya mganga kuchanganyikana na maji hayo!!!  ilifa mtu huyo arudi duniani na kuvuta pumzi kama binadamu wa kawaida!!!

    kiumbe huyo akanguruma kwa sauti kali huku akizipiga hatua kutoka ndani ya mto,, cha kushangaza kiumbe huyo alitembea juu ya maji pasipo kuzama!! 



    Kagaruki akamfungua kamba Raisi wakaanza kutimua mbio!!    walikimbia pasipokujua ni wapi wanaelekea!!!  wakajikuta wametokezea barabarani!!  kwa mbali likaonekana gari likija upande huo!!!  Kagaruki akasimama katikati ya barabara,,akanyoosha mikono yake ishara ya kuomba msaada.. dereva wa gari hilo asimamishe gari lake...

    Dereva huyo akaonekana kustaajabu sana!  alipomuona Raisi wa nchi kuwepo mazingira hayo pasipo ulinzi wowote!!!!  akaamua kuliegesha gari lake kando kisha akashuka kutoka ndani ya gari!  

    Kagaruki akaomna msaada akisema,,"eneo hili sio salama yatupasa tuondoke,, tafadhali tunaomba msaada kutuondoa eneo hili!

    Dereva huyo akakubali akasema hakuna tatizo ingieni ndani ya gari!    Dereva huyo aliyaongea maneno hayo  huku akizipiga hatua kukifuata kichaka!

    kagaruki akauliza kwa mshangao! ,,"unaenda wapi huko? kunahatari.. tafadhali tuondoke!!

    dereva huyo akasisitiza kwa kusema ingieni,, ndani ya gari mimi nakwenda kujisaidia haja kubwa huko kichani!



    Kagaruki na Raisi wa nchi wakaingia ndani ya gari hilo..

    yule dereva akadizi kuzipiga hatua na kutokomea kichakani,,, akashusha suruali yake na kujisairia haja kubwa,, 



    Upande mwingine kule ndani ya gari,, alionekana Kagaruki pamoja na Raisi wa nchi wakiwa na nyuso za wasiwasi,,,mara ghafla ikasikika sauti kali ya mtu akilia kisha sauti hiyo ikanyamaza,,, Raisi akaingiwa na hofu,, akasema,, bila shaka dereva huyu kauwawa na yule kiumbe wa kutisha!

    wakati wakati wanatahamaki.. punde si punde akajitokeza Kiumbe huyo kutokea kule kichakani!! akiwa katapakaa damu kwenye mdomo wake!!!  Kagaruki akaingiwa na hofu,, akajisogeza haraka kwenye kiti cha dereva,,,kwa lengo la kuwasha gari waondoke eneo hilo haraka iwezekanavyo!!!  alifoshika sehemu ya ufunguo wa gari akagundua kuwa funguo haukuwepo hapo!!  macho yakamtoka,, akatazama upande wa nje,, akamuona kiumbe huyo wa kutisha akizipiga hatua kulifuata gari hilo!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kagaruki akaangaza angaza macho yake akaona funguo ukiwa umedondoka chini,, nje ya gari,, akafungua mlango haraka haraka akashuka kutoka nje ya gari akaufuata ufunguo huo!!!

    akauokota na kurudi ndani ya gari!!!  akaliwasha gari!! akaliondosha kwa kasi ya ajabu,, wakafanikiwa kutoka katika eneo hilo!

    Raisi akampongeza sana Kagaruki kwa kuokoa uhai wake!!  akamuahidi kuwa  Kagaruki atakuwa mlinzi mkuu wa ikuru....Kagaruki akatabasamu kisha akajisemea moyoni,, "maisha nimeyapatia...alijisemea maneno hayo huku akiendelea kuzipanga gia,,,, punde si punde ikasikika sauti ya kioo cha nyuma kupasuka,, walipogeuza shingo zao kutazama nini kimesababisha kioo kuvunjika,, macho ya kawatoka kumuona yule kiumbe wa kutisha akiwa kaning'inia nyuma ya gari hilo!

    KIZAA ZAA!!!







    Hofu ikazidi kuongezeka juu yao,, Rais akasema ongeza mwendo ,,endesha gari kwa kasi!

    Kagaruki akafanya kama alivyoagizwa na Raisi!

    akaliendesha gari hilo kwa kasi ya ajabu.... wakati huo yule kiumbe wa kutisha alikuwa anafanya jitihada za kung'oa mlango wa nyuma ya gari! Raisi akaangaza angaza macho yake akaona upanga kwenye kiti cha  nyuma ya gari!  akauchukua upanga huo,,,

    Kagaruki alizidi kuzipanga gia,, alipojaribu kugeuza shingo yake kutazama upande wa nyuma akashtuka,, yule kiumbe wa kutisha hakuonekana tena! hofu ikazidi kuongezeka... ghafla kikasikika kishindo juu ya gari, kitu kizito kutua.. punde si punde,, ikasikika sauti ya kitu kizito kikigonga juu ya gari hilo!  Kagaruki akajisemea moyoni,, "bila shaka huyu kiumbe wa kutisha ndiye anayegonga gonga!  wacha nifanye jambo! akakanyaga breki gari likasimama,,kutokana na mwendo wa kasi wa gari hilo na kusimama ghafla,,yule kiumbe wa kutisha akarushwa akadondoka mbele ya gari hilo akatokwa majeraha mengi kwenye sehemu ya mwili wake!! alipotaka kunyanyuka kagaruki akaliwasha gari na kuliondosha kwa kasi,,,

    gari hilo likamgonga kiumbe huyo na kumkanyaga kwa magurudumu!,, Kagaruki akafurahia ushindi.. ha a hawakuthubutu kutazama nyuma!! waliamini kuwa kiumbe huyo tayari kafa!!

    Safari ikaendelea hatimae wakafika ikuru!  Raisi akapokelewa na walinzi yeye pamoja na Kagaruki!!



                       ******************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumbe yule kiumbe hakufa!!  baada ya kugongwa na lile gari akaeodoka chini na gari likapita juu yake akashikilia kwa nguvu vyuma vilivyokuwa chini ya gari hilo!!

    kiumbe huyo wa kutisha,, mpaka muda huu alikuwa kule chini ya gari!  akajivuta taratibu na kutoka chini ya gari!

    akazipiga hatua za kikamamamavu,  kulifuata jengo la ikulu!,,  walinzi waliokuwa wanalinda upande wa nje!!  wakashtuka kumuona kiumbe huyo wa kutisha,, wakabaki wanatazamana wakitafakari nini cha kufanya! wakatoa bastola na kuanza kumshambulia kiumbe huyo wa kutisha!

    walifyatua risasi mfululizo lakini risasi hizo hazikumdhuru kiumbe huyo! bado aliendelea kulifuata jengo la ikulu!!  hatimae walinzi wakaanza kutimua mbio!



    kule ndani ya Ikulu,, alionekana Raisi akitazama yanayotendeka huko nje!  kwa kupitia mitambo maalumu iliyotegeshwa kuzunguka eneo lote la ikulu!  macho yakamtoka ,,akaingiwa na hofu,, akajisemea moyoni,, "hili ni jambo la kustaajabisha!  inamaana kumbe hakufa!,,, Raisi akaamuru kuwa milango yote ifungwe haraka!



    ke nje walionekana wale walinzi wakiendelea kutimua mbio walipoukaribia mlango wa kuingia ndani ya ikulu,, wakakuta milango imefungwa!!  punde si punde yule kiumbe akamnasa mmoja kati ya walinzi hao,, akamnyofoa kichwa,,kisha akawafuata wale walinzi wengine na kuwauwa kikatiri!

    kiumbe huyo alipohakikisha hakuna mtu yeyote aliyebaki hai huko nje!  akazipiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya ikuru!  alipoukaribia akaanza kuugonga mlango huo kwa kichwa na mikono yake halimae mlango huo ukaanza kuregea na kuvunjika... akazipiga hatua kuingia ndani zaidi,,,

    ukimya ulitawala,, 

    Wakati huohuo alionekana Raisi,,,pamoja na Kagaruki wakiwa ndani ya chumba maalumu kilichokuwa kimejengwa na kuzungushiwa vyuma imara! 

    wapishi,, pamoja na baadhi ya walinzi waliokuwemo ndani ya jengo hilo wakauwawa kikatiri,,,

    Kagaruki akasema yanipasa nifanye jambo!  Raisi akashtuka kisha akauliza,, "jambo gani hilo?

    Kagaruki akasema,, "mimi natoka nje ya chumba hiki nakwenda kupambana na kiumbe huyo!  aliongea maneno hayo kisha akafungua mlango na kutoka nje ya chumba hicho!  akazipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa umakini wa hali ya juu!!  akaona mtungi wa gesi,, akauchukua kisha akafungua koki gesi ikaanza kutoka!!  na kusambaa akachukua mtungi mwingine akafungua koki piq gesi ikaanza kuvuja kwa vingi!  CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo Raisi alikuwa anashuhudia yote hayo kupitia ule mtambo maalumu!  macho yakamtoka akajiuliza huyu mtu anataka kufanya jambo gani!!?  alijiuliza swali hilo huku akiendelea kutazama kwa makini kinachoendelea!!!  ghafla akaona kamera zilizokuwa upqnde mwingine zikionyesha yule kiumbe wa kutisha anakuja ule upande aliokuwepo Kagaruki!  Raisi akachukua kipaza sauti akaongea kwa sauti kali,, "rudi huku,,, huyonkiumbe anakuja eneo hilo muda mchache ujao!!

    Kagaruki aliisikia Sauti hiyo vyema,,akashtuka! wakati anatahamaki! punde si punde akamuona kiumbe huyo akizipiga hatua kumfuata hapo alipo!

    TAHARUKI!!!



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog