Search This Blog

SUNDI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Sundi

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwambali alionekana mwanamke mzee sana akiwa anakatiza upande wa pili wa  barabara lilipokuwepo shamba lake..mwanamke huyo mzee anaitwa SUNDI,,akaingia shambani,,akaanza kuchuma mboga za majani alizozipanda shambani humo......ghafla akasita kuendelea kuchuma mboga hizo kumbukumbu ikajia akakumbuka enzi za usichana wake,,alibahatika kupata watoto  watatu..

    mumewe alikuwa ni mwanaharakati mmojawapo kati ya mashujaa waliopigania uhuru namo mwaka 1961....kwa bahati mbaya aliuwawa kwa kuchinjwa.....

    Sundi akabaki mjane,,akiwalea watoto wake hao watatu JUMBE na APOLO pamoja na mdogo wao wa kike aitwae NURU.

      baada ya miaka kadhaa kupita, Jumbe na Apolo wakaamua kwanda mjini kutafuta maisha, ni kutokana na hali ngumu ya kimaisha waliyokuwanayo...akajisemea moyoni,,"yani tangu hawa watoto walipoondoka hapa kijijini hawajawahi kurudi angaliu kujua hali yangu!

    bibi huyo aliwaza hayo yote huku usowake ukionyesha simanzi kubwa! akapiga moyo konde akiamini ipo siku watarudi kumjulia hali mama yao...



    Siku zilizidi kusonga hatimae,,

    Upande mwingine Jijini dar es salaam,,alionekana Apolo ambaye ni mdogo wake Jumbe...akiwa anajiandaa kulala....lakini akaonekana kifikra yupo ndani ya dimbwi zito la mawazo,,akajisemea moyoni,,"nimekukumbuka sana mama,, sijui uhali gani huko uliko..nitajitahidi wiki inayoanza niende kijijini angalau nikamjengee mama nyumba mpya....hizi ni baraka bila yeye kunizaa mimi,,leo hii nisingekuwa namiliki utajiri huu....baada ya kuzema maneno hayo....akajifunika shuka na kuanza kuutafuta usingizi.

    Apolo alifanikiwa kimaisha kwa sasa anamiliki kampuni ya safirisha wa mizigo nchi kavu....

    lakini Jumbe alikuwa bado hajafanikiwa kimaisha,,mara kwa mara alitegemea msaada kutoka kwa mdogo wake pia Apolo alimuajili kaka yake kama msimamizi mkuu katika kampuni hiyo..



    kadri siku zilivyozidi kusonga Jumbe akaanza kuingiwa na wivu,,kutokana na mafanikio makubwa ya mdogo wake,,,akaandaa mpango wa kumuuwa mdogo wake ili yeye arithi mali hizo...



         *****BAADA YA WIKI MOJA KUPITA******



    Safari ya Apolo,kwenda kijijini kwa mama yake ikawadia...akamuita kaka yake kisha akasema,,"mimi nakwenda kumsalimia mama kule kijijini,,nitakuwa huko kwa wiki mbili mbele,,pia nataka nimfungulie NURU bihashara naye aweze kupata pesa zake mwenyewe, natamani aje kuishi huku lakini si unajua yeye ndiye anayemuhudumia mama na kumsaidia shughuli za nyumbani.....hivyo naomba usimame ipasavyo katika utendaji wa kazi..

    Jumbe akacheka,,kisha akasema,,, inamaana leo hii uniamini kama nitasimamia ipasavyo? mbona siku zote kazi zinafanyika inamaana huwa unanifundisha kazi,,mdogo wangu punguza madoido...Apolo akacheka huku akisema,," kaka unamaneno,haya vipi wewe hauna mpango wa kwenda kumsalimia mama?

     Jumbe akajibu,,"wewe ukienda inatosha utakuja kunisimulia habari za huko,mimi na wewe ni damu moja ,hivyo ukienda wewe ni kama nimeenda mimi.

    ghafla uso wa Apolo ukaonekana kufadhaishwa na maneno hayo yaliyotoka kinywani mwa kaka yake....akamtazama Jumbe kwa macho ya msisitizo kisha akashusha pumzi...

    wakati huohuo walionekana vijakazi wa Apolo wakipakia mabegi yaliyokuwa na zawadi ndani yake,,,baada ya lisaa limoja safari ya kuelekea kijijini ikaanza....



    Jumbe akabaki,kuendelea kusimamia kampuni ya mdogo wake...wafanyakazi wa kampuni hiyo walikuwa hawampendi j

    Jumbe kutokana na kuwapelekesha katika kazi,,na kwasababu youye ndiye msimamizi mkuu wakati mwingine aliwafuta kazi wafanyakazi bila sababu za msingi....yote hayo Apolo hakuyajua.

    kutokana na majukumu mengi yaliyokuwa yanamkabili,,hakuwa na muda wa kuongea na wafanyakazi wake,,jukumu hilo alimuachia kaka yake kwa sababu anamuamini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

               ******************



    baada ya masaa mengi kupita,,,Apolo akiwa njiani anaendesha gari lake....akajisemea moyoni,,"sasahivi ni usiku, si vyema kundelea na safari wacha nitafute nyumba ya kulala wageni,,kisha asubuhi niendelee na safari..wakati anawazo hayo,,akaona kibao kinachongoza ilipo nyumba ya kulala wageni..akakatisha kona na kuifuata nyumba hiyo...akakodi chumba kimoja akapumzika hapo.



    Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema, na safari ikaendelea....

    baada ya masaa kadhaa kupita,,akafika kijijini kwao...akaliendesha gari mpaka nyumbani kwao...akamkuta mama yake amebeba mzigo wa kuni kichwani,,akitokea porini...

    Sundi akafurahi sana kumuona Apolo,,akampokea huku akiongea kilugha,,,akamkaribisha ndani....Apolo akauliza Nuru yuko wapi? nimemletea zawadi nahisi atafurahi sana.

    Bi'Sundi akainamisha kichwa chake huku akionesha furaha yake kupotea baada ya kuulizwa swali hilo....punde si punde akaangua kilio pasipo machozi kutoka,,kutokana na umri mkubwa aliokuwa nao...Apolo akashtuka! akauliza kwa mshangao! mama mbona unalia? nuru yuko wapi?

    Bi'Sundi akanyanyuka akamshika mkono Apolo akaongozananae kutoka nje wakaelekea nyuma ya nyumba!







    Bi'Sundi alilazimika kutembea hatua za taratibu,,huku kainamisha mgongo wake,,kutokana na umri mkubwa aliokuwanao! walipofika nyuma ya nyumba,,,Bi'Wundi akasema,,"hapa ndipo tulipomzika mdogo wenu Nuru....nyinyi tangu mlipotoa miguu yenu hapa nyumbani...hamjawahi kurudi hata kutujulia hali..

    Apolo akaanza kulia kwa uchungu huku akiwa akapiga magoti kando ya kaburi la Nuru...akasema,,"nisamehe sana mdogo wangu, sikutegemea kama mauti yangekupata,,,,natamani uamke angalau upokee zawadi nilizokuletea....

    wakati anaogea maneno hayo,,Bi'Sundi alikuwa akimtazama Apolo kwa macho ya mfadhaiko.

    Apolo akageuza shingo yake na kumtazama mama yake,,kisha akauliza,,"alipatwa na nini?

    Bi'Sundi,,akanyoosha mkono wake,,ishara ya kutaka Apolo amshike mkono...nae Apolo akafanya hivyo,,akashika mkono wa Mama yake,,kisha akanyanyuka...Bi'Sundi akamuongoza Apolo mpaka ndani ya nyumba akaweka mkewe wakaketi...kisha akaanza kusimulia kwa kilugha..ilikuwa hivi;



    Siku moja wakati natoka shambani nilimkuta Nuru akiwa yumgonjwa sana kalala huko chumbani kwake...nikaamua kumpa dawa za kienyeji,,,ilipofika nyakati za jioni,,hali ya Nuru ikawa njema,,lakini ilipofika saa nne za usiku...Nuru akazidiwa tena,,nikaamua kumpeleka kwenye kituo cha Afya nikiwa namajilani!

    tulipofi Nuru akafanyiwa vipimo,,ikagundulika kuwa snailmbe tumboni,,hivyo daktari akasema tumpeleke Hospitali ya wilaya..kiukweli nilichanganyikiwa,,kwa sababu sikuwa na pesa yoyote kwa muda huo,,hata majirani zangu walinionea huruma,,wakanichangia pesa,,lakini hata haikufikia robo ya pesa iliyokuwa inahitajika.....nikaamua kurudi nyumbani nikiwa na mego wenu(Nuru) kiukweli usiku wa siku hiyo Nuru hakupata usingizi,,alilia usiku kucha akilalamika tumbo linamuuma,,,

    Asubuhi palipokucha,,nikaamua kuuza lile shamba la kule bondeni.....nikapata pesa,,,nikiwa njiani kurudi nyumbani nikamchukue Nuru nimpeleke hospitali walitokea vibaka wakanipora pesa zote,,,nilisikitika sana,,,lakini sikuvunjika moyo..nikarudi nyumbani nikamchukua nuru....Ninangozana naye mpaka kwenye barabara kuu....tukapata lifti ya gari lililokuwa linaelekea mjini......dereva wa gari hilo aliamua kutupeleka hospitali......

    lakini tulipofika huko,,walikataa kumfanyia upasuaji,,mpaka pesa ilipwe......niliwasihi sana lakini walikataa..... baada ya lisaa limoj akupita Nuru alipoteza maisha kwa kukosa matibabu...ni miaka mitano sasa tangu mdogo wenu afariki.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maneno hayo yalimfanya Apolo aingiwe na uchungu wa hali ya juu....akalia sana,,huku akimuomba msamaha mama yake..Kwa kutokuja kuwajulia hali,,

    kama ilivyo kawaida mzazi ji mzazi tu...Bi'Sundi akawasamehe watoto wake Apolo nac kaka yake Jumbe..

    Kesho yake Apolo akatafuta mafundi ujenzi akalipia pesa taslimu..ijengwe nyumba ya kisasa kwa ajili ya mama yake...pia akamfungulia duka kubwa la kuuza nafaka na mahitaji mbalimbali ya nyumbani...Bi'Sundi akafurahi sana akampa baraka zote mtoto wake azidi kufanikiwa katika maisha...Apolo akaingia chumbani akatoka na simu mpya aliyoinunua kwa ajili ya mama yake,,iwe rahisi yeye kuwasiliana nae na kumjulia hali,,pindi akirudi dar es salaam.



    Baada ya wiki mbili kupita,,Apolo akarudi jijini Dar es salaam.

    Akafika salama,,akamsimulia kaka yake kuwa mdogo wao amekufa miaka mitano iliyopita hivyo ni vyema aende kijijini kumsalimia mama yao,,lakini Jumbe hakuonekana kuguswa au kushtushwa na kifo cha Nuru,,akasema,,"hiyo ni mipango ya mungu kwani wewe utaishi milele? Apolo akamshangaa kaka yake,,kuongea maneno hayo,,Jumbe akasema,,"mimi jatoka kidogo nitarejea baadae...

    siku zilizidi kusonga Apolo akaendelea na hughuli zake za kila siku.....



    Jumbe aliendelea kuandaa mpango wake wa kumuuwa Apolo ili arithi mali hizo za mdogo wake....Siku ya leo akaamua kwenda kwa mganga....alipofika akaeleza shida yake,,kisha mganga akasema hilo ni jambo rahisi sana.....lakini linamasharti magumu...inatakiwa aletwe kuku mweusi....pamoja na picha ya Apolo.....

    Jumbe akafanya hivyo,,akanunua kuku mweusi kisha akaiba picha ya Apolo na kuipeleka kwa mganga....alipofika akavikabidhi vitu hivyo,,,kisha mganga akatengeneza dawa ambayo inatakiwa imwagwe chini ya mlango wa kuingilia ndani ya nyumba...Apolo atakapovuka dawa hiyo basi atakufa ndani ya masaa machache...

    Jumbe akaipokea dawa hiyo kisha akarudi nyumbani haraka,,katika nyumba hiyo walikuwa wanaishi wao wawili,,hawakuwa na kijakazi wa ndani....hivyo Jumbe aliamini ni jambo rahisi saja kwa upande wake.....alipofika akaingia ndani ya nyumba kisha akanyunyizia dawa hiyo pale chini mlangoni.....alipomaliza akatabasamu huku akisema,, "utanisamehe mdogo wangu,,hizi ni dharau yani umekuwa  tajiri kablq yangu!!! hainiingii akilini...we kufa tu mimi jile raha za dunia,,alisema maneno hayo huku akifunga mlango....



    Ilipofika majira ya saa moja za usiku,,Apolo akarudi nyumbani,,akaliegesha gari lake,,kisha akashuka kutoka ndani ya gari,,akazipiga hatua kuufuata mpango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo!!!







    Alipoukaribia mlango huo,,akasita kuingia ndani,,akakumbuka kuwa kuna mizigo amekujanayo hivyo ameisahau kwenye gari,,akazipiga hatua kurudi kwenye gari.....mizigo hiyo ni Miche ya miti,,ambayo aliinunua,,akafungua buti na kushusha miche hiyo ya miti,,akaibeba na kuzunguka nyuma ya nyumba akaiweka huko,,,

    Apolo hakuona ulazima wa kurudi kupitia mlango wa mbele angali yupo huko nyuma ya nyumba na ufunguo wa kufungulia mlango wa nyuma qlikuwa nao..akafungua mlango wa nyuma na kuingia ndani...

    Wakati huo Jumbe alikuwemo chumbani mwake kapitiwa na usingizi...

    Apolo akafunga mlango huo,,akazipiga hatua kuelekea chumbani mwake.....

    baada ya dakika kadhaa akatoka na kuelekea sebuleni...akawasha Runinga akaketi kwenye sofa huku qkiwa kashikilia glasi yenye juisi ndani yake...



    Kule chumbani alionekana Jumbe akiwa bado kalala usingizi..akahisi sauti ya Runinga kule sebuleni,,akastaajabu! akajisemea moyoni,,"inamaana huyo ni Apolo? sasa mbona hajafa kama kavuka ile dawa pale mlangoni,,angekufa!

    Jumbe hakuweza kumuona Apolo wakati anaingia ndani ya nyumba,,,hakujua kuwa Apolo alipitia mlango wa nyuma hivyo hakuivuka ile dawa pale kwenye mlango wa mbele!

    Jumbe akazipiga hatua akatoka chumbani mwake akaelekea sebuleni,,akamkuta Apolo ameketi anatazama taarifa ya habari.

    Apolo akamsalimia kaka yake..kisha akaanzisha stori...

    lakini Jumbe akaonekana wazi kuwa hayupo hapo kifikra,,mawazo yake yalikuwa mbali..

    Apolo akaligundua hilo akauliza,,"mbona kama haupo sawa! unaumwa?

    Jumbe akajibu kwa kudanganya,,"siumwi,, ni uchovu tu niliokuwanao,,pia nimetoka usingizini muda mchache uliopita,,

    Apolo akabaki kimya huku akiendelea kutazama taarifa ya habari.



                   *************************



    Asubuhi palipokucha,,Apolo alidamka mapema kama ilivyokawaida yake...akajiandaa kwenda kazini,,alipomaliza akaingia jikoni akachukua jagi akachota maji kisha akazioiga hatua kuufuata mlango wa nyuma,,akaufungua akamwagilizia ile miche ya miti aliyoita jana....punde si punde simu yake ikaita..alipoitazama akaona mesdizi wake anampigia...akaipokea simu hiyo....kisha akasema,,"waambie wanisubiri dakika kadhaa...aliongea hivyo huku akiliweka jagi chini...akafunga mlango huo kwa funguo kisha akaondoka zake kulifuata gari kule mele ya nyumba,,,,akaingia ndani ya gari lake na safari ikaanza kuelekea kazini.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kadhaa kupita Jumbe ,,akajiandaa kuelekea kazi akajisemea moyoni,,"mbona Apolo anapitia mlango wa nyuma? hata jana yawezekana alipitia mlango huohuo! inamaana ameshtukia mpango wangu? Jumbe alijiuliza maswali hayo huku anaendelea kuvaa...alipomaliza akatoka chumbani akaelekea sebuleni,,akafungua mlango wa mbele lakini akasita kutoka nje akihofia huenda dawa hiyo ikamdhuru yeye kama akiivuka..akaamua kuufuata mlango wa nyuma,,,alipojaribu kuufungua akagundua kuwa umefungwa! Jumbe akahisi kuchanganyikiwa akasema,,"inamaana leo sitoki humu ndani?

    mbona huu ni mtihani! Jumbe akaamua kubaki nyumbani siku hiyo,,



                    ******************



    Upande mwingine kule kwenye kampuni ya Apolo,,alionekana akiwa kwenye kikao na wachina,,walikuwa wanajadili kuhusu magari mapya ambayo Kampuni hiyo ya kutengeneza magari hayo...imeomba kuingia ubia na Kampuni ya Apolo,,

    Ikalazimika Apolo asafiri kwenda china siku hiyohiyo...yeye pamoja na wawakilishi hao....walitumia ndege ya kukodi..

    kabla hawajafika uwanja wa ndege,,Apolo akaona ni vyema amtaarifu kaka yake kuwa yeye anasafiri...akaamua l'unegia simu.

    Jumbe akakasirika sana,,,akasema,,"sasa unamaana gani kusafiri na ufunguo wa mlango wa nyuma?

    Apolo akastaajabu kuulizwa swali hilo...hakujali akaamua kukata simu..wakaingia ndani ya uwanja wa ndege...na safari ya kuelekea china ikaanza....

    Baada ya masaa mengi kupita,,Jumbe akaanza kuhisi njaa,,,kwa sababu walikuwa hawapiki chakula,, sikuzote walikuwa wanakula kwenye hotel ya Apolo....hivyo hawakuwa hata na akiba ya chakula ndani ya nyumba,,,masa yalizidi kusonga Jumbe akashindwa kuvumilia njaa kali aliyokuwanayo...akajisemea moyoni,,"kwanza dawa hii ilitemgenezwa kwa ajili ya Apolo,,sidhani kama mimi nikiivuka itanidhuru!...polelea mbali,,dogo mwenyewe mjanjamjanja sijui kashtukia! manake simuelewi mara kanunu sijui vidubwasha gani,,,kaviweka huko nyuma ya nyumba akapitia huko huko....haya leo asubuhi kaamka  kapitia huko huko!!! huu ni ujinga nikiendelea kubaki humu njaa itaniuwa.

    Jumbe aliongea maneno hayo huku akizipiga hatua..kuufuata mlango wa mbele atoke nje aende kupata chakula....akaufungua mlango huo.....





    Akaufungua,,lakini akawa na hofu ,akasita kunyanyua mguu kuvuka dawa hiyo,,akafunga mlango na kurudi ndani,,

    masaa yalizidi kusonga ,,na njaa ikazidi kuwa kali...akarudi chumbani kwake akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi,,

    hakuweza kusinzia kutokana na njaa aliyokuwanayo,,akajisemea moyoni,,"kweli mchimba shimo hutumbukia mwenyewe...lakini mimi ni mjinga kiasi gani! akaamua kuvuja kitasa cha mlango wa nyuma,,akafanikiwa kuufungua mlango,,,akatabasamu huku akijipongeza kuwa yeye ni mjanja...akazipiga hatua kulifuata gari lake,,,akaliwasha na kuondoka zake...



    ilipofika nyakati za jioni,,akarudi nyumbani....akaingia ndani kupitia mlango wa nyuma...

    siku zilizidi kusonga,,,akawa anapitia mlango wa nyuma ,,kuingia na kutoka....baada ya wiki moja kupita Apolo akarudi nchini,,,,alipowasiri uwanja wa ndege akampigia simu Jumbe aje kumfata...

    Jumbe akaliwasha gari lake,,,na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza....akampokea Apolo,,,wakarudi nyumbani wakiwa pamoja.

    walipofika Jumbe akaliegesha gari kisha...akashuka kutoka ndani ya gari,,,akazipiga hatua kuzunguka nyuma ya nyumba...Apolo akauliza,,"kuna nini huko?

     Jumbe akasema,,"mlango wa mbele niliufunga ,,isitoshe funguo niliuwacha upande wa ndani...wacha nikakufungulie..

    Apolo akabaki kasimama hapo kando ya mlango wa mbele...

    wakati jumbe anaingia ndani,,,Apolo akaona anachelewa kufunguliwa mlango,akaamua kuzunguka nyuma ya nyumba naye akaingia kupitia mlango wa nyuma.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huohuo alionekana Jumbe akifungua mlango wa mbele huku uso wake ukiwa na tabasamu,,,akastaajabu kutokumuona Apolo pale nje..punde si punde ikasikika sauti ya Apolo,akisema,,"funga tu mlango,,mimi nimeshapitia huko kwenye mlango wa nyuma.

    Jumbe akaonekana kuchukizwa na kitendo hicho,,akaongea kwa ukali,,"sasa si ungesema kama unapitia huko,,umenipotezea sekunde zangu,,kufungua mlango!

    Apolo akastaajabu huku akimtazama kaka yake kwa macho ya mshangao..kisha akajisemea moyoni,,"siku hizi simuelewi kaka yangu..sijui kapatwa na nini,,yani jambo dogo anafoka bila sababu za msingi....

    alijisemea maneno hayo huku akizipiga hatua kuingia chumbani kwake,,akapitiliza bafuni akaoga kisha akapanda kitandani kujipumzisha..

    wakati huohuo,alionekana Jumbe akiwa kaketi sebuleni anatazama kipindi cha runinga,,,lakini kichwani mwake alikuwa akiwaza juu ya mpango wake wa kumuuwa Apolo.

    akajisemea moyoni,,"mimi sio kichaa,,,tena nina akili timamu na zinafanya kazi,,,ninauhakika asilimia mia ,,Apolo ameshtukia hili jambo,,itakuwa ameona dawa niliyoimwaga pale mlangoni,,,ndio sababu inayomfanya asipite kwenye mlango wa mbele...

    Jumbe akaamua kwenda kuhakikisha kama ile dawa ya ungaunga aliyoimwaga pale chini ya mlango,je? inaonekana?

    akafungua mlango akatazama kwa makini akagundua dawa hiyo haionekani,,,mpaka utazame kwa makini,,na si rahisi kugundua kama ni dawa ya kichawi.

    akafunga mlango akazipiga hatua kuelekea chumbani kwake.



    baada ya masaa kadhaa kupita,,Apolo akadamka,,akaamua kutoka chumbani na kuelekea sebuleni akiwa kashikilia kitabu cha hadithi za MAYA...mara nyingi Apolo alipenda kusoma vitabu vya hadithi,,hasa akiwa nyumbani..

    akaketi kwenye sofa akaanza kusoma kitabu hicho,

    punde si punde geti likagongwa,, Apolo akanyanyuka na kuchungulia dirishani,,,



    kumbe aliyekuwa anagonga geti ni mchumba wa kaka yake(Jumbe) kwa bahati nzuri geti halikufungwa kwa ndani,,hivyo mchumba wa Jumbe alipojaribu kusukuma geti likafunguka,akazipiga hatua kuifuata nyumba hiyo.

    wakati huo huo alionekana Jumbe akiwa chumbani kwake,,,,akazipiga hatua kuelekea sebuleni...hakujua kuwa mchumba wake yupo upande wa nje,

    Apolo akafungua mlango wa mbele akisubiri shemeji yake aingie ndani ya nyumba.

    kwa sababu mlango ulikuwa wazi,,jumbe akamuona mchumba wake akiwa kaukaribia mlango huo..macho yakamtoka! uzalendo ukamshinda akazipiga hatua za haraka!!!

    TAHARUKI!!!!!!





    Jumbe akaruka kama kipa,,,akafunga haraka mlango huo!

    Apolo akastaajabu kumuona kaka yake anamfungia mlango mchumba wake,,,Jumbe akaanza kufoka akiongea maneno makali,,akasema,,"kuanzia leo sitaki nikuone unakuja hapa ondoka zako....Apolo akabaki mdomo wazi akimtazama kaka yake kwa macho ya mshangao! kisha akauliza,,"kafanya kosa gani mpaka unamfukuza kama mbwa?

    Jumbe akajibu kwa kejeri,,"usiingilie mambo yasiyokuhusu fanya yako.

    aliongea maneno hayo huku akizipiga hatua kuelekea chumbani kwake.

    Apolo akabaki pale sebuleni akachungulia dirishani kutazama upande wa nje,,akamuona shemeji yake anaishilizia getini.



    wakati huo huo kule chumbani kwa Jumbe,alionekana akiwa kajilaza kitandani...akajisemea moyoni,,"ni bora nimefanya hivyo...lakini ni jambo gumu kumueleza mchumba wangu akanielewa...sijui nitumie uwongo gani kumwambia anielewe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana yule mganga,,aliyempa jumbe dawa hiyo ya kichawi...mganga huyo kumbe ni muongo.ile dawa aliyompa Jumbe sio dawa bali ni unga wa miti aliyoichoma na kusaga majivu yake...mganga huyo alikuwa ni tapeli si mganga wa kweli!

    siku ya leo akafungua sanduku kubwa kiasi lililotengezezwa kwa mbao...akatoa psa nyingi ndani ya sanduku hilo,,,akatabasamu kisha akasema,,"mjinga ndiye aliwaye,,hapa mjini,,hahahahaaha,,,

    aliongea maneno hayo huku akizitoa pesa hizo ndani ya sanduku.



                           ********************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog