Search This Blog

NZITA - 3

 







    Simulizi : Nzita

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    palipokucha zanida alitoka chumbani...akaelekea jikoni huku akiwa kamuacha nzita bado kalala... aliandaa uji kwa ajili ya nzita.... ili akiamka anywe... kama ilivyokuwa kawaida..... baada ya muda nzita aliamka...zanida alingia chumbani...lakini alikuwa akimtazama nzita usoni.... zanida alianza kumuogopa nzita... lakini

    (DAMU NZITO KULIKO MAJI HATA KULIKO KARINYA) mama ni mama tu... zanida alimnyanyua nzita kutoka kitandanina kumuandaa ili amuogeshe kisha ampe uji....

    wakati huohuo.. mama yake zanida alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwa zanida...baada ya muda kidogo alifika kwa zanida.....

    zanida alimkaribisha mama yake... bora mama umekuja... mmh!! yani mjukuu wako simuelewielewi kabisa.. alisema zanida"""

    misha akamsimulia mama yake mambo yote aliyoyaona... mama zanida alistahajabu sana... pole sana mwanangu bila shaka kuna watu wabaya wanamuandama mwanao!!!! alisema mama zanida""

    waliendelea kupiga stori...zanida aliandaa chakula kisha wakala.... na ilipofika saa kumi na moja jioni mama zanida aliondoka kurudi kwake....

    zanida alianza kucheza na mwanae nzita.. walicheza michezo ya kitoto kabisa..... ghafla jasimin alimpigia simu zanida... wakati zanida akiongea na simu.. nzita alizipiga hatua akaelekea kunako meza alivuta uwa lililokuwa limewekwa mezani kama pambo... uwa lile lilidondoka... kwa kuwa lilikuwa ndani ya chombo cha kioo.. kilipasuka... wewe achaaa!!! "zanida aliongea kwa kufoka.... nzita aligeuka na kumuangalia mama yake.....kisha macho ya nzita yalianza kubadilika na kuwa mekundu huku uso wa nzita ukionesha kukasilishwa na kitendo cha mama yake kumfokea.... nzita alianza kuzipiga hatua huku akielekea pale alipokuwa ameketi mama yake....

    zanida aliogopa sana.... oooh mwanangu nisamehe sikukusudia kufanya hivyo nakupenda mwanangu..... ghafla nzita alirudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuambiwa maneno hayo na mama yake... lakini zanida alionekana kuwa na wasiwasi na uwoga wa hali ya juu.... aliogopa hata kumuangalia nzita usoni. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika saa mbili kasoro usiku.. zanida alimpa nzita chakula...nzita aliposhiba zanida alimbembeleza nzita huku akimuimbia nyimbo ili nzita alale... hazikupira dakika nyingi nzita alisinzia.. kisha zanida alimuweka nzita kitandani... alimfunika shuka kisha na yeye akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.... punde alisinzia.... akiwa usingizini"' alihisi kama kuna mtu anagusa gusa vitu upande wa sebuleni... nzita aliamka.. alipoangalia kando!!! hakumuona nzita hivyo alijua wazi kuwa nzita ndiye atskuwepo huko sebuleni.... zanida aliamua kunyanyuka ili akaone nzita anachokifanya.... zanida alizipiga hatua za kunyatia... alipofika upande wa sebule..hakumuona nzita.... zanida aliogopa sana... alisikia kama mtu anagusagusa vitu upande wa jikoni... zanida alinyata na kuchungulia upande wa jikoni... kwa kupitia tungu la ufunguo lililopo kwenye kitasa... alistahajabu kumuona nzita kafungua friji huku akila nyama mbichi... zanida aliogopa alihisi kuishiwa nguvu... ghafla alidondoka na kupoteza fahamu... alipozinduka ilikuwa ni Asubuhi..... akiwa kitandani... ghafla kumbukumbu ikamuijia alikumbuka kile alichokiona jana... alipotaza kando ya kitanda hakumuona nzita.... zanida alinyanyuka haraka kutoka kitandani ili aelekee sebuleni kumuangalia nzita.... alipojaribu kufungua mlango haukufunguka!!!! mlango ulikuwa umefungwa na funguo haikuwepo pale kwenye kitasa..... mara ghafla....





    Mara ghafla alihisi vishindo mtu anatembea nyuma yake... zanida aliogopa sana alihisi kuchanganyikiwa... mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio.... aliogopa hata kugeuka nyuma... alisita kwa sekunde alipogekuka nyuma hakuona mtu mara ghafla mlango ulifunguka wenyewe na kubaki wazi...zanida alishindwa kuvumilia aliamua kutoka mbio..kuelekea upande wa sebuleni.... alikimbia akafungua mlango na kutoka nje.... alistahajabu kumkuta nzita akiwa amemkamata na kumnyanyua juu mtoto wa nyumba ya jirani aliyekuja kucheza na nzita...zanida aliogopa... alijiuliza mtoto mdogo huyu ananguvu za humyanyua mtoto mwenzie tena kwa mkono mmoja... kisha akaona nzita anasogeza mdomo wake katika shingo ya mtoto yule... ghafla zanida alipaza sauti ""ACHA NZITA!!!!"" nzita alimuachia mtoto yule akadondoka chini..mtoto yule alinyanyuka na kutimua mbio huku akilia... . nzita alipogeuza shingo kumtazama mama yake,, macho ya nzita yalikuwa mekundu kama mboni imepakwa rangi nyekundu... kisha nzita akaanza kuzipiga hatua kuelekea ule upande aliokuwa amesimama mama yake.... zanida aliogopa akaanza kuzipiga hatua kurudi nyuma ghafla zanida alijikwaa kwenye ngazi na kudondoka...PUU!!! nzita hakuwa na huruma hata chembe!!!! alizidi kuzipoga hatua kuelekea pale mama yake alipodondoka.. alipomkaribia alinyanyua mama yake kwa mkono mmoja... zanida aliogopa sana haja ndogo na kubwa zilimtoka kwa wakati mmoja... jasmini alifika ghafla nzita alimuachia mama yake...na kurudi katika hali yake ya kawaida.... jasmini hakuweza kuona kitendo kile.. kisha nzita akamkumbatia miguuni mama yake huku akionesha kuwa na sura ya uwoga.... zanida alitulia tuli huku macho yamemtoka akimuangalia nzita anataka kufanya nini.... CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    jasmin alishuka kutoka mdani ya gari... alistahajabu kumkuta zanida kasimama kama sanamu huku mwanae nzita kamkumbatia miguuni. mmh!! shosti ulikuwa unacheza na mwanao? aliuliza jasmin"" kumbe wakati jasmin anakuja...zanida akili yake yote ilikuwa kwa nzita hivyo hakuona kipindi jasmin akija... ghafla zanida fahamu zilirudi alichuchumaa na kumuangalia nzita usoni kwa umakini... pia nzita alimtazama mama yake kwa sura ya upole na huruma.. jasmin alistahajabu sana""" shost kunanini kimetokea!!!! mbona wamtazama nzita kwa umakini?? aliuliza jasmin

    zanida hakujibu kitu... kisha akasema karibu ndani.. jasmin alisema hata sikai shosti nilikuwa napita tu nikaona ni vyema nije kukujulia hali.. nimetokea mtaa wa pili.. kumuona bosi wangu Yumgonjwa.... kisha wakaagana jasmin akaingia ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake...



    **************



    zanida aliogopa kulala nyumbani kwake siku hiyo

    hivyo alimchukua nzita na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao kwa baba na mama..

    baada ya lisaa limoja kupita zanida alifika nyumbani kwao akiwa na mwanae nzita.. zanida ilibidi amsimulie mama yake mambo yanayomtokea"" kuhusu maajabu na vimbwanga vya mwanae Nzita... hata mama zanida aliogopa baada ya kusimuliwa mambo hayo... mama zanida alimuangalia nzita..lakini nzita alionekana ni mwenye furaha alikuwa upande wa nje akicheza na babu yake... mama zanida alimwambia zanida yakupasa umrudie Mungu anza kusali sana siku zote bila kuchoka yawezekana kuna watu wabaya wanawafanyi hila wewe na mwanao nzita""" zanida aliupokea vyema ushauri wa mama yake... utakula nini leo? aliuliza mama zanida.... aaah chochote tu mama...alijibu zanida""" kuna maharage nimechemsha asubuhi yapo jikoni kayaunge... adlisema mama zanida"" aaah mama twende wote tupige stori hu mimi napika""alisema zanida huku akitabasamu""""hahahaha mwanangu hujaacha tu kudeka!!! haya twende""" wakanyanyuka kutoka sebuleni wakazipiga hatua kuelekea upande wa jikoni....



    *********



    kule nje nzita aliendelea kucheza na kucheka na babu yake,,, huku babu yake akiendelea kulitengeneza gari alikuwa anakaza nati za nyaya zinazotoka kwenye betri...mara ghafla babu yake nzita alijiugonga na spana...kwenye kidole punde damu zikaanza kutoka kwenye ile sehemu aliyojigonga... alitoka kwenye boneti nakuchukuwa kitambaa azifite damu zile....ni kosa kubwa nzita alipo ona damu alianza kutamani kunywa damu ile...macho ya nzita yalibadilika na kuwa mekundu... akaanza kuzipiga hatu kumfata babu yake... babu yake nzita alistahajabu kumuona mjukuu wake kabadilika ghafla... aliogopa akaanza kurudi nyuma... zita aliongeza kasi ya kuzipiga hatua babu yake alipo ona hivyo aliamua kutimua mbio kuelekea upande wa ndani... mara ghafla..



    Mara ghafla nzita alianza kuzipiga hatua za haraka haraka... babu yake alikimbia akaingia ndani.. nzita alibaki nje huku akitazama nyumba..baba zanida alimuita mkewe pamoja na zanida. kisha akawaambia wachungulie upande wa nje kupitia dirishani... walipochungulia waliona nzita yupo kawaida... mbona hamna kitu?? mama zanida aliuliza" babu yake nzita alibidi na yeye achungulie... alistahajabu kumuona nzita akiwa katika hali yake ya kawaida!!!! jamani nimeshuhudia kwa macho yangu nzita kabadilika na macho yake ualikuwa mekundu.... zanida alifungua mlango haraka na kutoka nje.. akamuita nzita.. kisha nzita akaanza kuzimpiga hatua kuelekea ule upande alipokuwepo mama yake"" zanida alimbeba nzita na kuingia nae ndani,,, baba zanida alimuangalia nzita kwa macho ya uwoga... hakutaka hata nzita asogee karibu yake..

    zanida alimshika mkono nzita na kuingianae jikoni..



    **********CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ilipofika majira ya saa mbili za usiku.. zanida aliandaa chakula mezani... wakaanza kula... na walipomaliza kula.. zanida alimuogesha nzita na kumuandaa alale... kisha naye akalala. hazikupita dakika nyingi nzita na zanida walisinzia...

    ilipofika usiku wa manane zanida aliamka ghafla hakumuona nzita.. zanida alistuka akajua ni kawaida ya nzita kuamka usiku na kwenda sebuleni.. hivyo zanida alinyanyuka kutoka kitandani na kuanza kuzipiga hatua kuelekea sebuleni.. alipowasha taa alistahajabu...nzita hakuwepo sevuleni... zanida alihisi kuchanganyikiwa... alipochungulia nje... alimuona nzita kaketi chini.. huku kazungukwa na watu watatu... waliovalia mavazi meusi marefu kama kanzu... zanida aliogopa sana ghafla alijitokeza..yule mtu wa ajabu ambaye ndiye baba yake nzita... alimshika mkono nzita na kuanza kuzipiga hatua kuondoka nae... zanida akapaza sauti akimuita mama yake.. MAMA NJOO UONE.. ghafla watu wale walitoweka na nzita.. mama zanida alikuja haraka sebuleni.. kuna nini!!mama zanida aliuliza......mama mwanangu nzita""zanida alisema"

    kafanyaje??, "mama zanida aliuliza""

    wamemchukua mwanangu wameondoka nae...

    kabla hajamaliza kuongea alimuona nzita akizipiga hatua kutokea chumbani.. zanida aliogopa akajificha nyuma ya mama yake^ nzita alizipiga hatua mpaka alipokuwa amesimama bibi yake akamkumbatia miguuni.. bibi alimnyanyua mjukuu wake na kumbeba... wakati huo zanida alikuwa akitazama kwa makini nini kitatokea... au ulikuwa unaota?? mama zanida aliuliza""

    zanida hakujibu kitu... alibaki kimya... kisha mama zanida aliondoka na mjukuu wake kuelekea chumbani kwake huku akisema...nenda kalale mimi na babu yako tutalala na nzita... zanida alizipiga hatua kurudi chumbani kwake... lakini alikuwa na uwoga wa hali ya juu..... mama zanida alimuweka nzita kitandani na kusema lala mjukuu wangu"".. nzita alijilaza..... punde babu yake nzita aliamka alistuka kumkuta nzita kitandani.. alinyanyuka haraka na kuwasha taa.. ghafla hakumuona tena nzita kitandani... alipotazama mlangoni alimuona nzita kasimama mlangoni.. huku akimuangalia babu yake kwa sura ya huruma na macho ya umakini..... baba zanida alimuamsha mkewe.. kwa kumvuta nywele... nini tena mbona unanivuta nywele angalia usije ukamlalia mtoto...mama zanida alisema hivyo""" kabla hajaongea neno lingine... alipogeuza shingo alistahajabu kumuona nzita kasimama mlangoni... njoo mjukuu wangu"" mama zanida alimuita nzita... kisha nzita akazipiga hatua kuja kitandani.. alipanda kitandani.... na kujilaza.

    baba zanida aliogopa kulala chumbani humo... huyu si mtoto ni jini" baba zanida alimwambia hivyo mkewe huku akifungua mlango kuelekea sebuleni.... alipowasha taa ya sebuleni aliogopa sana... alimuona nzita akiwa kasimama hewani... jesus huyu mtoto si nimemuacha chumbani!!!

    baba zanida alitimua mbia kurudi chumbani... alistahajabu kumkuta nzita kalala kando ya bibi yake.... baba nzita alihisi kuchanganyikiwa aliiona nyumba inawasha kama pilipili.. aliamua kupanda kusimama hapo mpaka pakuche... lakini baada ya lisaa limoja uzalendo ulimshinda .. alijisogeza kitandani kwa hatua za kunyatia.... akalala.

    mara ghafla.



    Mara ghafla bubu yake nzita alihisi vishindo vya watu wakitembea upande wa sebuleni....akaingiwa na woga... iliamka akaanza kuzipiga hatua za kunyatia kuelekea upande wa sebuleni... alipowasha taa hakuona kitu...kisha akaona kimvuli cha mtu akitembea nyuma yake,,, akageuza shingo yake haraka...hakuona mtu yeyote... alipotazama kwa makini..aliona mguu ukiishlia ni kama mtu alikuwa akitembea kuelekea upande wa jikoni... alistuka sana macho yakamtoka... aliamua kuzipiga hatua za polepole kuelekea upande wa jikoni... alipokaribia mlango wa jikoni... aliuliza wewe ni nani??? lakini hakujibiwa...alipochungulia hakuona mtu akawasha taa jikoni.. hapakuwa na mtu mule jikoni...aliamua kurudi chumbani.. alipofungua mlango alimuona nzita akielea hewani.. akawasha taa haraka.. alistahajabu kumuona nzita kalala kando ya bibi yake... baba zanida alitamani kuikimbia nyumba......alisimama kwa sekunde kadhaa huku macho yake yakitazama pale alipokuwa kalala nzita.. kisha akaamua kupanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******BAADA YA MIAKA MINNE(4)KUPITA*******



    nzita alitimiza umri wa kwenda shule alikuwa na miaka saba(7) Zanida alimpeleka nzita kumuandikisha darasa la kwanza katika shule ya msingi iitwayo ADEN PRIMARY SCHOOL...shule hiyo ilikuwa ni ya bweni. (boarding) kisha nzita alianza masomo wiki hiyohiyo.. nzita alikuwa na uwezo wa kipekee katika uwelewa wa masomo... walimu na wanafunzi wenzake walimpenda sana nzita.. siku moja nzita akiwa darasani wakati mwalimu akifundisha somo la hesabu... alianza kuwauliza maswali wanafunzi wake.. kwa kumchagua mmoja mmoja.. mwalimu alimsimamisha nzita na kumuuliza swali... kabla mwalimu hajamaliza swali nzita alikuwa tayari ameshajibu... mwalimu alistahajabu.. kisha akamuuliza swali lingine.... kabla mwalimu hajauliza swali nzita akajibu...mwalimu alistahajabu zaidi... mmh!!! amejuaje kuwa nataka kuuliza swali hilo mbona kajibu kabla sijauliza swali.... mwalimu alijisemea moyoni...viruzi sana waweza kuketi.. nzita aliketi...muda wa masomo ulipokwisha.. wanafunzi wote walitoka darasani na kuelekea mabwenini..



    ************



    Hatimae walifanya mtihani wa kumaliza muhula wa kwanza"".nzita alifanya mitihani yake kwa dakika mbili tu...kwa kila mtihani mmoja... walimu walistahajabu nzita aliongoza kwa nafasi ya kwanza... hakupoteza hata alama moja kwa kila mtihani.. utadhani katunga yeye.. walifunga shule wanafunzi wote wakarudi majumbani kwao..zanida na jasmin walimfata nzita shuleni...na kuondokazao



    ***********

    nzita akiwa nyumbani alikuwa akimsaidia mama yake kazi za nyumbani... zanida alistahajabu sana"" kila akiamka anakuta nzita kafanya kazi zote kwa wakati mmoja na kwa muda mchache"zanida alishangazwa na kitendo hicho..kwani yeye huwa hufanya kazi hizo siku nzima mpaka jioni.. lakini nzita yeye hufanya kwa dakika chache bila yeye kuona... sikumoja zanida alidamka mapema ili ashuhudie nzita huwa anazifanya kazi hizo kwa namna gani.. alisikia nzita akiwa jikoni"" zanida alizipiga hatua za kunyata akachungulia.. alistahajabu hakumuona nzita mule jikoni.... kisha akaona vyombo vinajiosha vyenyewe bila mtu kuonekana. kisha aliona vitu vingine vikijiweka vyenyewe katika sehemu yake.... aliogopa sana.. akazipiga hatua kuelekea sebuleni... aliona tambala la deki likisafisha vigae bila mtu kuonekana.... alisikia mtu anafagia uoande wa nje.. alipochungulia aliona ufagio unafagia wenyewe bila mtu kuonekana!!!!!

    zanida alistuka sana aliangaza angaza sehemu zote hakumuona nzita... alitaka kupaza sauti ili amuite nzita... lakini akasita.. akaamua kuacha kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani kwa nzita.... alipo fungua mlango wa chumba cha nzita mara ghafla..



    Alipofungua mlango wa chumba cha nzita mara ghafla alistuka sana aliona nzita akiwa amelala... akaamua kurudi jikoni aone kinachoendelea... alipofunga mlanga ile anageuka kuzipiga hatua kurudi upande wa jikoni.... ghafla alimuona nzita akitokea upande wa jikoni na kuelekea nje"" zanida alitamani kukimbia lakini alishindwa....aliamua kuingia jikoni ili aone nzita alikuwa anafanya nini... alistahajabu kukuta vyombo vimeshaoshwa na kupangwa kabatini.. kisha chakula kimepikwa na kimeshaiva tayari.... zanida alitoka jiko akaelekea upande wa nje... alistahajabu sana mazingira yalikiwa masafi... aliamua kumuita nzita..... NZITA"" nzita aliitika na sauti ilikuwa ikitokea upande wa ndani... zanida alirudi haraka ndani... alimuona nzita akitokea chumbani kwake... huku uso wa nzita ukionesha wazi kuwa ametoka usingizini... zanida alibaki mdomo wazi... macho yalimtoka... alibaki kasimama kama sanamu huku akimtazama nzita.... nzita hakuonesha kuwa na wasiwasi.... nzita alisema abee mama nimesikia umeniita"" zanida alibaki kimya hakuongea kitu.. nzita alipo ona mama yake kabaki kimya aliamua kuondoka na kuelekea bafuni. zanida aliogopa sana... najuta kukuzaa utaniuwa na presha mwanangu... zanida alijisemea moyoni. kisha akazipiga hatua za kunyatia mpaka kwenye mlango wa bafu... akaanza kuchungulia kwa kupitia tumdu la ufunguo kwenye kitasa ili aone je nzita anaoga kweli au anafanya nini!!!!! alimuona nzita anaoga.... zanida aliendelea kuchungulia nzita alimaliza kuoga na kujifuta maji na taulo... zanida aliamua kutoka mlangoni hapo... ile anageuka akamuona nzita anatokea chumbani kwake huku akiwa kabadilisha nguo na kuvaa nguo zingine... zanida aliogopa sana... akataka kukimbia... nzita akasikika akimwambia mama yake""" hata usikimbie mama... zanida alianza kulia....huku akijilaumu kwa nini alienda kwa mganga.



    ************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    baada ya wiki moja kupita iliwadia krismasi (christmas) siku hiyo zanida alimpigia simu jasmin nakumuomba awapeleke bichi (beach) kwa sababu jasmin alikuwa na usafiri zanida aliamua kumtoa out mwanae nzita.... na kumpeleka akaogelee na kucheza na watoto wenzake...

    wakiwa bichi(beach) zanida na jasmin waliamua kukaa peke yao wakinywa vinywaji.... nzita alijichanganya na watoto wenzake na kuanza kuchezanao... baada ya muda watoto wale waliamua kwenda kucheza kwenye maji.... walipoelekea kunako maji... watu wslistahajabu kumuona nzita akiwa anatembea juu ya bahari itadhani anatembea nchi kavu.... watu wote waliokiwepo hapo bichi walianza kuogopa na kutimua mbio kila mtu alipitia njia yake.... zanida alistahajabu kuona watu wanakimbia huku wakipiga kelele... jini jini!!!! zilisika sauti zikisema hivyo.... zanida alijisemea moyoni... bila shaka atakuwa ni nzita na vimbwanga vyake... alipotazama upande wa baharini alistahajabu kumuona nzita akiwa anazipiga hatu juu ya bahari... jamani mwanangu.....alisema kwa sauti zanida..... jasmin macho yalimtoka... akatimua mbio kwa uwoga.... zanida alipaza sauti na kumuiya nzita... NZITA""" nzita aligeuka na kumtazama mama yake.... kisha akaanza kutimua mbio kurudi nchi kavu.....watu walivyo ona nzita anarudi tena kwa kukimbia... walitimua mbio wote hakubaki mtu zaidi ya zanida neke yake...



    **********



    kule nje jasmin alionekana anatimua mbio kuelekea alipolipaki gari lake... alipofika alifungua mlango haraka na kuingia ndani ya gari...

    mara ghafla.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    mara ghafla alistuka kusikia sauti ya nzita ikisema.. mbona umetukimbia na kutuacha wakati tulikuja wote.... jasmin alipogeuka nyuma alikutasha macho na nzita... macho yalimtika jasmin akafungua mlango wa gari akataka kutoka nje... ghafla mbele yake... alimuona zanida akija ule upande lilipokuwa limepaki. gari la jasmin huju kamshIka nzita mkono... jasmin alistahajabu!!! akageuza shingo yake haraka kuangalia mule ndani ya gari hakumuona nzita!!!!! jasmin alichanganyikiwa alitamani kutimua mbio.... zanida na nzita walifika mpaka pale lilipokuwa limepaki gari la jasmin.. watu wengine walioshuhudia nzita akitembea juu ya bahari waliamua kumpiga picha kwa kutumia simu zao pamoja na kamera za kawa kawaida.. lakini kila aliyempiga nzita picha"" picha hazikulnekana...kwenye kamera zaawaida wala kamera za simu.... kisha nzita na zanida wakaingia ndani ya gari"" jasmin aliingia pia lakini alikuwa na uwoga wa hali ya juu... alitamani zanida aendeshe gari lake,,, alafu yeye apande usafiri mwingine...jasmin allijipa moyo akaliwasha gari na kuondoka...



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog