Search This Blog

ROHO YA GIZA - 2

 







    Simulizi : Roho Ya Giza

    Sehemu Ya Pili (2)





    Asubuhi palipokucha Fundikila alidamka mapema. akaingia bafuni akaoga kisha akatoka nje ya nyumna yake akaingia ndani ya gari na kuondoka zake kwenda kutafuta mtu wa kumtoa kafara....akiwa njiani akamuona fukara(ombaomba)

    fukara huyo ni mlemavu wa miguu hajiwezi,,

    Fundikila akaliegesha gari lake kando ya barabara akachukua chupa ya juisi akaifungua akaweka sumu maalumu inayouwa ndani ya masaa 12.. kisha akashuka kutoka mdani ya gari akazipiga hatua mpaka pale alipokuwepo mlemavu huyo. ombaomba... alipomkaribia akamkabidhi ile chupa ya juisi kisha akarudi zake ndani ya gari....

    mlemavu huyo akaifungua chupa ya juisi hiyo,,kutokana na njaa kali pamoja na kiu,, akainywa kwa pupa...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fundikila akatabasamu kisha akaliwasha gari lake na kurudi zake nyumbani!

    ilipofika majira ya saa tisa za usiku,,, Fundikila akiwa usingizini ikasikika sauti ikimwambia umefanikisha jambo lako... sasa waweza kufunga ndoa. Fundikila akashituka kutoka usingizini.. akaona pete mbili za dhahabu kwa ajili ya ndoa... ni lazima azitumie pete hizo kumvisha mkewe pamoja na yeye mwenyewe.



    Siku zilizidi kusonga Fundikila akamptafuta yule mwanamke aliyekutana nae sikuile wakabadilishana namba za simu... wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi... hatimae Fundikila akaenda nyumbani kwao mwanamke huyo aitwae DORA...

    wazazi wa Dora wakafurahi sana binti yao kuolewa na tajiri...

    Dora pia alifurahi kwa sababu kila akipata mchumba na kumpeleka kumtambulisha,, wazazi wake walikataa wakidai kuwa hawawezi kukubali aolewe na masikini fukara.

    mipango ya harusi ikafanyika na ndoa ikafungwa.



                ******BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA*********



    Fundikila akapewa masharti kuwa asimpe ujauzito mkewe vinginevyo atapata matatizo makubwa katika maisha yake,, huenda akafa kabisa..  anatakiwa aishi pasipo kupata mtoto!

    jambo hilo lilimnyima furaha Fundikila,,akajisemea moyoni,, "sasa huu sio ufahari ni adhabu,, nani atakuwa mrithi wangu..... je mke wangu atanielewa kuishi nae pasipo mtoto!

    Fundikila akaitikia kwa shingo upande......baada ya kikao kuisha akajitokeza nyumbani.. wakati huo mkewe alikuwa kalala usingizi mzito hakuweza kujua mumewe hakuwemo ndani ya nyumba...kwa sababu alifumbwa kimiujiza na ni mwiko kwa ambaye sio mwanachama kuona jambo hilo!

    siku zilizidi kusonga,,hatimae mke wake akashika ujauzito! Hilo ni kosa kubwa amelifanya Fundikila!

    baada ya siku kadhaa kupita mauzauza yakaanza kuiandama nyumba yake....

    siku moja nyakati za usiku Fundikila pamoja na mkewe wakiwa wamelala...

    kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer akajitokeza chumbani kwa Fundikila..





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fundikila akashtuka usingizini,, kumbe alikiwa anaota! akaanza kuingiwa na wasiwasi,,,akajisemea moyoni,, hili ni tatizo.. naamini haikuwa ndoto bali ni kweli....kanitokea usingizini.. hii inaashiria hali ya hatari!!  sijui nifanye nini kujiondoa kwenye chama hiki,, hii ni adhabu,, yani mali nilizonazo na heshma kila kona ya mtaa eti nikose mtoto!!  haiwezekani..liwalo na liwe,, nipo tayari hata kupoteza uhai wangu lakini si kukosa mtoto....

    Fundikila akadamka akazipika hatua kuufuata mlango akatoka nje ya chumba chake.... akazipiga hatua kadhaa akausogelea ukuta unaotenganisha korido katikati.... akasimama kisha akatazama kushoto kulia,,, aakaugusa ukuta huo... akausukuma kwa nguvu.. ukafunguka..... kumbe ukuta huo ni mlango maalumu wa chumba chake chasiri... chumba hicho hakuna anayekijua zaidi yake.... hata fundi aliyetengeneza mlango huo ukafanana na ukuta..... aliuwawa usiku huohuo baada ya kumaliza kutengeneza....

    Fundikila aliamua kumuangamiza fundi huyo ili asije akatoa siri.. kwa kuwasimulia mafundi wenzake huko mitaani kuwa nyumba ya Tajiri Fundikila inachumba cha siri ndani yake....



    Fundikila akaingia ndani ya chumba hicho.. akaufunga mlango,,kisha akasimama katikati ya chumba hicho....

    mara nyingi alikitumia kwa kuomba chochote anachokitaka na kinakuja kimiujiza wakati huohuo..... lakini usiku wa leo Fundikila aliingia ndani ya chumba hicho kwa lengo tofauti!!!

    akanyoosha mkono wake likajitokeza joho lenye rangi nyeusi na rangi nyekundu.....kisha akanyoosha mkono mwingine ikajitokeza ile fimbo ya dhahabu.. akavua pete yake ya dhahabu... vitu vyote hivyo hajavipata duniani... alilewa huko kuzimu kutoka kwa Lucifer!  akavitupa chini kisha akatazama kando kikajitokeza kiberiti..

    Fundikila alikuwa na uwezo wa kuomba chochote kile atakacho kwa sababu tayari ni mtumwa/mfuasi wa Lucifer!  akaamua kuvichoma moto vitu hivyo kisha akatoka kwenye chumba hicho na kurudi kule chumbani kwa mke wake!  akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! 



                                ********************



    Asubuhi lalipokucha,, mke wa Fundikila alidamka mapema kama kawaida yake.. akaingia jikoni na kuandaa chai kwa ajili ya mumewe.. alipomaliza akaweka chai na chapati,,maya, matunda,, juisi kwenye meza ya chakula,,kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani.... akamkuta Fundikila akitoka bafuni... akamuandalia mavazi,,

    Fundikila alipomaliza kuvaa akatoka chumbani akaelekea sebuleni kwa ajili ya kupata chai...

    baada ya dakika kadhaa alimaliza.. kisha akamuaga mkewe kwa kumbusu shavuni! akazioiga hatua kutoka nje.... macho yakamtoka!! hakuliona gari lake.. akajisemea moyoni,, "huyu mwizi kaingiaje humu,,pasipo mimi kusikia!

    wacha niwahi kutoa taarifa kwenye vyombo vya dora... haiwezekani gari langu la kifahari liibiwe hivi hivi..... CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akatimua mbio mpaka barabarani.. akakodi taxi..

    akaelekea kwenye kituo cha polisi kutoa taarifa..

    alipofika.. akaandikisha maelezo..

    yule askari akaanza kumuhoji,, akasema,, "nitajie namba ya gari lako!

    Fumdikila akataja.

    yue askari akatazama namba ya gari aliyoitaja Fundikila.. lakini haikuwemo katika kitabu cha ofodha. ....askari huyo akasema,, "mbona hakuna namba hiyo... inaonesha kuwa haijawahi kutumika,, yaani kusajiliwa......akaendelea kusema,, "ebu kalete kadi ya gari lako...

    Fundikila akaomdoka akarudi ndani ya taxi na kuelekea nyumbani kwake..

    alipofika akapitiliza mpaka chumbani kwake.. akafungua droo anayoitumia kuweka vitu vyake vya thamani... zikiwemo nyaraka zake muhimu.

    macho yakamtoka hakuona kitu chochote!  droo hiyo ilikuwa tupu!

    akamuita mkewe.... akamuuliza,, "vitu vilivyokuwa humu kwenye droo umeviweka wapi?

    mkewe akastaajabu.. akasema,, "tangu umenioa,sijawahi kufungua hiyo droo..wacha nikusaidie kutafuta. huenda uliweka sehemu nyingine... wakaanza kutafuta kila pande ya chumba hicho.. lakini hawakuona chochote.. akazipiga hatua.. akatoka mpaka nje ya geti..

    Fundikila alitembea kwa haraka nusu akimbie...akafungua geti kisha akamfuata yule dereva tax.. alipomkaribia akatoa pochi ya mfukoni(warlet) alipoifungua macho yakamtoka!! haikuwa na pesa hata shilingi.. pia kadi yake ya benki haikuwemo.. akazidi kuchanganyikiwa.. akaingia ndani ya taxi,, akasema nipeleke CRDB BANK,,

    bila kuchelewa dereva akaliwasha gari lake akafuata maelekezo ya mteja wake.

    bada ya dakika kadhaa walifika.. Fundika akashuka kutoka ndani ya gari hilo.. akazipiga hatua za harakaharaka huku akijikwaa... akahisi tai aliyokuwa kaifunga shingoni mwake inaongeza uzito akaamua kuivua na kuiweka mfukoni..... akaingia ndani ya benki hiyo... akamfuata muhudumu wa benki na kutoa taarifa za upotevu wa kadi yake ya benki... yule muhudumu akatazama kwenye kitabu cha orodha.. lakini halikuonekana jina la Fundikila..

    Fundikila akasema, "mimi ni mteja wenu na mara ya mwisho kutoa pesa ni jana mchana.... iweje mniambie sina akaunti kwenye benki yenu... ebu acheni utani...

    wale wahudumu wakatazamana.... wakahisi huenda Fundikila kapatwa na ugonjwa wa akili!!! kisha wakabaki wakimtazama... Fundikila akaamua kutoka nje ya benkk hiyo.. akaingka ndank ya taxi.. akasema,, "nileleke posta ya zamani..

    baada ya nusu saa wakawa wamefika.. Fundikila akashuka kutoka ndani ya gari.. akazipiga hatua kuelekea kwenye kampuni  yake angalau akachukue pesa amlilpe yule dereva taxi... alipolikaribia jengo la kampuni hiyo... likatoweka mimiujiza!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fundikila akahisi kuchanganyikiwa,,akaamua kurudi kule lilipokuwa limepaki gari(taxi) akafungua mlangto ana kuingia ndania ya gari hilo,, kisha akasema,,"nipeleke nyumbani kwangu.



       *******************



    upande mwingine kule nyumbani kwa fundikila, alionekana mkewe akiwa amejilaza kitandani,,ni baada ya kumaliza shughuli ndogo ndogo za nyumbani...akiwa usingizini akahisi mgongano wa vyombo,, kule jikoni! akashtuka kutoka usingizini akanyanyuka kutoka kitandani akaufuata mlango akaufungua na kutoka chumbani,,,,akaelekea jikoni..alipofika akastaajabu kukuta chumba cha jiko kipo tupu hakuna kitu hata kimoja!!! macho yakamtoka akaingiwaq na hofu.

    akatoka haraka jikoni akazipiga hatua kuelekea sebuleni,kwa lengo la nkutoka nje ya nyumba....alipoangaza macho yake akastaajabu kuona sebule ipo tupu hakuna kitu hata kimoja! akapikicha macho yake,huku akijisemea moyoni,,"hivi naota au nashuhudia kwa macho yangu? mbona maajabu haya!?

    hofu ikazidi kuongezeka akatimua mbio kuufuata mlango akatoka nje ya nyumba...akabaki hapo nje akimsubiria mumewe!



    wakati huohuo alionekana Fundikila akiwa ndani ya taxi,,,akielekea nyumbani huku akimsisitiza dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi...

    baqada ya nusu saa kupita Fundikila alifika nyumbani...akashuka kutoka ndani ya taxi,,akaparamia geti na kuingia upande wa ndani!akastaajabu kukuta mlango wa kuingilia ndani ya nyumba upo wazi pia mkewe yupo nje kaketi huku machozi yakimtoka!

    akajisemea moyoni,,"bila shaka hali sio shwari! alijisemea maneno hayo huku akizipiga hatua kumfuata mkewe pale alipokuwa ameketi,akamuuliza,,"mbona umeketi hapa nje?

    mkewe akajibu,,"nashindwa kuelewa hii nyumba yetu yani nilichokiona siku ya leo!!!!!!!!

    akasita kuendelea kusimulia kisha nakasema ingia ndani ukajionee mwenyewe.

    Bila kuchelewa Fundikila akazipiga hatua za harakaharaka akaingia ndani ya nyumba...

    macho yakamtoka kuona hakuna kitu chochote sebulen! akashtuka akaamua kuifuata korido inayoelekea vyumbani..akasukuma ukuta uliokuwa na mlango wa siri wa kuingia katika kile chumba alichokuwa akikitumia kumuomba Lucifer ampe anachokitaka!

    akashtuka kukuta watu watatu..wamevalia majoho meusi wakiwa wameketi chini wameizunguka mishumaa mingi iliyokuwa ikiwaka!na

    upande wa kichwani walikua wamefunika nyuso zao kwa kofia pana zilizokuwa zimeungana na majoho waliyokuwa wamevaa!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    moshi mkubwa ulikuwa umetanda ndani ya chumba hicho! punde si punde ikasikika sauti ya mke wa Fundikila akipiga kelele kule nje ya nyumba.



    Fundikila akatimua mbio kuelekea nje kutazama nini kimempata mkewe!

    kabla hajaufikia mlango wa sebuleni...ukasikika mngurumo wa kutisha na sauti za watu wengi wakiongea kwa kujibishana!

    Fundikila akaingiwa na hofu kupita kiasi!akapaza sauti kwa uwoga akisema,,"najua hamjaja kwa nia nzuri...lakini ninaombi,

    nipo tayari kupoteza uhai wangu lakini naomba muache kiumbe aliyomo tumboni mwa mke wangu...sipo taya kumpoteza mwanangu wa pekee...



    baada ya kuongea maneno hayo akafungua mlango na kutoka nje haraka...akashtuka kukuta mkewe kazungukwa na moto ulio waka kutokea kwenye ardhi,,moto huo uliwaka huku umechora alama ya pembe tatu! mke wa Fundikila akiwa katikati ya moto huo...yeye hakuweza kuona moto huo kwa macho ya kawaida..lakini alikuwa anahisi joto kali kupita kiasi ,,lililosababisha maumivu kwenye mwili wake!

    Fundikila akajisemea moyoni ,,"bila shaka wanataka kumuangamiza mtoto aliye tumboni mwa mke wangu!!!



    yanipasa nifaye jambo.wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla...akajitokeza Lucifer akiwa ameongozana na watu wawili wenye mbawa zilizofanana na popo!

    Lucifer akazipiga hatua kuwafuata wale watu waliokuwa wamemzunguka mke wa Fundikila,,miongoni mwa watu hao alikuwemo kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer duniani...

    Lucifera akasema,,"muacheni,,muda na wakati bado haujawadia,,hakuna haja ya kumuangamiza kiumbe huyo aliye tumboni mwa mwanamke huyo.. yawapasa muhakikishe Fundikila anapata mateso na fedhea ndipo mauti yamfuate...

    baada yaLucifer kuongea maneno hayo akatoweka kimiujiza na wale wafuasi wake wakatoweka muda huohuo..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mke wa Fundikila hakuwa na uwendo wa kuona yale yote yaliyotendeka muda mchache uliopita!

    .sasahivi ile hali ya joto kali mwilini mwake ilitoweka!

    Fundikila akatimua mbio kumfuata mkewe akaanza kumkagua kama kaumizwa na wale wafuasi wa Lucifer!

    alipogusa mwili wa mke wake,, Fundikila akaanza kutokwa na damu kwenye kucha za mikono yake! wakati anatahamaki...akahisi maumivu makali kwenye paji la uso..punde si punde akadondoka chini akapoteza fahamu!!

    PATASHIKA!!!!!!





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog