Search This Blog

KOTI JEUSI - 3

 







    Simulizi : Koti Jeusi

    Sehemu Ya Tatu (3)



     CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Solo akalitazama koti hilo kwa makini,, kisha akakubali kuifanya kazi hiyo,,, lakini kishingo upande!  kisha akazipiga hatua kutoka nje ya ofisi hiyo! 

    alipoukaribia mlango,, ikasikika sauti ya mkuu wa jeshi akisema,, "nimekumbuka; pia kunakazi ndogo nahitaji uifanye muda huu huu!

    utaongozana na baadhi ya wanajeshi wangu  kuelekea mstuni.. kuzika maiti za watu fulani hivi!

    Solo akashtuka kisha akasema,, "hii ni kazi ya ziada malipo yake nayahitaji muda huu huu,, kabla sijaianza kazi hiyo!

    Mkuu wa jeshi akatabasamu!  kisha akasema,,"pesa sio tatizo.. akazipiga hatua kadhaa na kufungua kabati akatoa kibunda cha pesa na kumkabidhi Solo,,

    Solo akapokea pesa hizo,, na kusema,, " maiti hizo ziko wapi? 

    mkuu wa jeshi akasema,, "tayari zipo ndani ya gari!

    Solo akaongozana na mkuu wa jeshi mpaka kwenye gari hilo.. pia ndani ya gari hilo walikuwemo wanajeshi watatu!  Solo akakabidhiwa ufunguo kuwa yeye ndiye aendeshe gari hilo.. akazipokea funguo na kuingia ndani ya gari.. na safari ikaanza!



    mwanajeshi mmoja akasema,, "endesha gari mpaka kongowe....

    Solo akafuata maelekezo yote anayoelekezwa na mwanajeshi huyo!

    baada ya lisaa limoja wakafika kongowe... wakaufuata msitu uliokuwa na miti mingi midogomidogo!

    mpaka. katikati ya msitu huo!!  wakashuka kutoka ndani ya gari..



                         ***************************************



    wanajeshi hao watatu wakaanza kuzitoa maiti hizo ndani ya gari!!

    na kuziweka kando,, kisha wakachukua nyenzo za kuchimbia shimo wakaanza kuchimba shimo kwa kupokezana!! 

    iliwachukua masaa mawili mfululizo mpaka kumaliza kuchimba shimo hilo!!!

    kisha wakazivuruta maiti hizo kwa lengo la kuzikwa kwenye shimo moja!

    Solo akazisogelea maiti hizo zilizokuwa zimefungwa ndani ya mfuko wa plastiki!  akafungua...akashtuka macho yakamtoka baada ya kugundua kuwa maiti hizo ni za ndugu zake!!!  akaongea kwa sauti ya ukali akasema,, "ni nani aliyewauwa watu hawa?

    wale wanajeshi watatu wakamtazama kwa mshangao!!  kisha mmoja kati ya wanajeshi hao akasema bosi ndiye kawauwa,,

    mwanajeshi mwingine akadakia na kuongea maneno ya kejeri,,, kasema,, "fanya kazi iliyokuleta hapa,, unachunguza kujua,, ili iweje!!? 

    Solo akaingiwa na hasira,, akamsogelemwanajeshi huyo akachomoa kisu kilichokuwa kiunoni mwa mwanajeshi huyo!!  akamchinja papohapo!!!  wale wanajeshi wengine wakajiandaa kupambana na Solo!  kabla hawajatoa silaha,,

    Solo akawashushia kipigo kikali na kuwachinja!!!  kisha akalia kwa uchungu kuwapoteza ndugu aliokuwanao tangu utoto wao mpaka wamekuwa vijana wakubwa!!!  akaamua kuwazika wale wanajeshi pamoja ndani ya lile shimo...kisha akachukua maiti ya ndugu zake na kuziingiza ndani ya gari!  akaelekea nyumbani!

    alipofika akaeleza tukio zima!!  Bakari akasikitika sana kisha akajisemea moyoni kauwa watotowake kwa mikono yake mwenyewe!!!  Lakini haikuwa kusudio na lengo langu!!!  Eee Mungu

    walaze mahala pema peponi !!! pia Linda alisikitika sana,, ingawa hajui kuwa hao ni watoto wake wa kuwazaa! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taratibu za mazishi zikafanyika!  wakazika miili ya vijana hao watatu!



        **********BAADA YA WIKI MOJA KUPITA********



    Solo akamwambia Bakari kuwa anafahamu muuwaji aliyesababisha mauti ya ndugu zake! 

    Bakari akasema,, " ni lazima mtu huyo auwawe!

    Kisha akatoa koti jeusi!!! macho yakamtoka Bakari akajisemea moyoni,, "mbona hili koti linafanana na lile koti alilonionyesha mkuu wa jeshi kule kambini! inamaana huyu ndiye muuwaji ninayetakiwa kumuangamiza!!?







    Solo akamtazama Bakari,kwa macho ya mshangao kisha akauliza ,,"unamaana gani kunipa koti hili?

    Bakari akatabasamu kisha akajisemea moyoni hii ni zawadi tu,,,koti hili nililinunua miaka mingi iliyopita,,nililitunza kama mboni ya jicho langu! kwa sababu huwa nakumbuka tukio fulani ninapoliona koti hili!

    maneno ya Bakari yalizidi kumshangaza Solo,,akabaki mdomo wazi,,huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kuuliza kuhusu jambo fulani,,kuhusu koti hilo jeusi,,

    wakati Solo anatafakari,,Bakari akaonekana akizipiga hatua,akaliweka koti hilo juu ya bega la Solo na kuondoka zake,,akimuacha bakari akiwa bado yumo ndani ya chumba hicho,,Solo akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,,akatafakari,,kisha akapuuza kwa kujipa moyo akisema ,,"huenda hili ni koti tu alinunua kweli,,,sidhani kama huyu ndiye muusika wa mauwaji!,,akalitoa koti hilo kwenye bega lake na kulitazama kwa makini,kisha akalivaa,na kujitazama kwenye kioo!



                         *********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana mkuu wa jeshi akiwa anakunywa pombe kali aina ya CAPTAIN MORGAN,,punde si pude simu yake ikaita akashtuka! alipoitazama simu hiyo akasita kuipokea kwa sababu namba hiyo iliwahi kumpigia miaka kadhaa iliyopita,,na alipojaribu kutafuta mawasiliano hayo yanatokea eneo gani,,,kwa kutumia mtambo maalumu(GPS),hakuweza kupata mawasiliano hayo....pia leo namba hiyo imempigia!,,,akaogopa kupokea simu hiyo,,,akajaribu kutafuta mawasiliano hayo yanatokea eneo gani,,akastaajabu mtambo huo(GPS) ulionyesha kuwa mawasiliano hayo yanatokea mbeya,,

    kumbe Bakari alipitisha mawasiliano ya simu yake kwenye mtambo maalumu,,ambao unabadilisha eneo sahihi la mawasiliano yake,,na kuonyesha eneo tofauti ambalo sio sahihi...



    Bakari akapiga tena simu baada ya kuona simu haipokelewi! lakini sasa hivi simu ikapokelewa...kisha hakuongea neno lolote akacheka mfululizo! akasema,," KOTI JEUSI.

    kisha akakata simu.

    Mkuu wa jeshi akaingiwa na hofu! akatazama kushoto kulia lakini akawa bado hajiamini wakati yumo ndani ya ofisi yake,akanyanyuka haraka akazipiga hatua kuufuata mlango akaufunga kwa ufunguo kisha akazipiga hatua kurudi nyuma kwa kuhofia kuwa muuwaji hayupo mbali na eneo hilo! pombe zikamruka akabaki amesiama,,huku akijisemea moyoni,,"mbona huyu mtu anasababisha nakosa amani katika maisha yangu,,,hivi ni nani huyu,,na nikifanikiwa kumnasa nitamzika ndani ya chumba changu,kisha nitaweka kitanda juu yake...wakati anajisemea maneno hayo,,ghafla wazo likamjia,akachukua simu yake na kumpigia Solo,,kisha akamwambia kuwa waonane,,muda mchache ujao

    pasipo kujua kuwa sasahivi yeye ni adui wa Solo,,

    Solo akaitikia wito,,lakini moyoni mwake akafurahia ushindi akisema,,"huu ndio wakati wa kulipa kisasi juu ya vifo vya ndugu zake waliouwawa na huyu mwana haramu,,

    wakati huo Solo alikuwa bado ajalivua lile koti jeusi,,akazipiga hatua kutoka ndani ya chumba chake,,akalifuata gari la Bakari ambalo mara nyingi Solo hulitumia katika mizunguko yake.

    akaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea kwenye kambi ya jeshi,,,akiwa njiani kabla hajafika mbali,,mkuu wa jeshi akampigia simu,,na kusema wakutane kule kwenye maficho ya bihashara zake haramu...ni kwenye lile jumba ambalo linauzio wenye kuta ndefu na nene.



    solo akaliendesha gari lake mpaka eneo la maficho hayo...akaliegesha gari lake umbali mrefu kutoka eneo la jengo hilo! yeye akatembe kwa miguu akafanya jitihada za kuruka ukuta na kuingia ndani ya jengo hilo!akaketi mbali huku kageuzia mgongo wake kule kwenye geti la kuingilia ndani ya maficho hayo ya mkuu wa jeshi.!



                         **********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana mkuu wa jeshi akitokea ndani ya kambi ya jeshi huku kaongozana na wanajeshi wawili ambao na maafisa wa jeshi,,wakieleke kule mafichoni kufanya bihashara haramu ya kuuza silaha zilizokuwemo mafichoni humo,,silaha hizo wanataka kuziuza kwa maharamia/majasusi ambao watafika hapo masaa matatu mbele,,hivyo mkuu wa jeshi aliamua kumshirikisha Solo kama mlinzi endapo makubaliano yataenda tofauti baina yake na wale majasusi basi Solo amuwekee ulinzi,,kwa kupambana na majasusi hao.

    baada ya nusu saa kupita mkuu wa jeshi akafika eneo la maficho yake ya silaha pamoja na madawa ya kulevya....akabofya rimoti maalumu ya kufungulia geti hilo la umeme.

    akaliingiza gari lake kisha akafunga geti kwa kubofya ile rimoti maalumu....akashuka kutoka ndani ya gari huku akiwa kaongozana na wale maafisa wawili wa jeshi,,wakazipiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia ndani kabisa ya maficho hayo...baada ya dakika kadhaa kupita mkuu wajeshi akasema,,"mbona Solo anachelewa mpaka muda huu hajafika!

    akaamua kutoka nje kwa lengo la kupiga simu,,kwa sababu ndani ya maficho hayo aliweka mtambo maalumu wa kuharibu mawasiliano ya simu mpaka mutoke nje,,ndipo unaweza kupiga na kupokea simu!

    alipofika nje ya maficho hayo haramu..akatoa simu yake na kumpigia Solo,,,punde si punde ukasikika mlio wa simu ikiita kando...alipogeuza shingo yake akastaajabu kumuona mtu kaketi amevaa koti jeusi,,akionekana sehemu ya mgongoni tu...mkuu wa jeshi akaingiwa na hofu,,akatimua mbio kulifuata gari lake kwa lengo la kuchukua bastola...alipofungua mlango wa gari hilo mlango haukufunguka ,,kumbe alivyoshuka kutoka ndani ya gari,,aliacha ufunguo kwenye gari,,,wakati wameingia ndani ya maficho hayo,,,ndio muda ambao Solo alilifuata gari hilo na kuchukua ufunguo kisha akalifunga na kurudi kuketi pale pale...

    mkuu wa jeshi akahisi kuchanganyikiwa baada ya kugundua kuwa milango ya gari lake imefungwa ...akageuza shingo yake haraka kutazama kule alipomuona yule mtu aliyevalia koti jeusi,,lakini hakumona tena mtu huyo...hofu ikazidi kuongezeka akatimua mbio kurudi kuloe ndani ya maficho,,,alipofika akakuta wale maafisa wawili wa jeshi wameuwawa! wakati anatahamaki mara ghafla!!!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    wakati anatahamaki mara ghafla ukasikika mlio wa risasi ukitokea upande wa nje, mkuu wa jeshi akaingiwa na hofu kupita kiasi,,,akajikuta anatokwa na haja ndo mfululizo,,,akatimua mbio  kuelekea upande wa nje,,

    alipofika akashtuka kumuona Solo akiwa ameketi juu ya boneti la gari lake!huku kavalia lile koti jeusi!akajisemea moyoni,,"inamaa huyu ndiye muuwaji ninayemtafuta siku zote! mmh mbona kizaa zaa,,

    Solo akasema umefanya kosa kubwa sana ,,,kosa hilo litagharimu maisha yako siwezi  kukuacha ubaki hai!

    mkuu wa jeshi akauliza kwa mshangao! huku akiongea kwa sauti ya uwoga,,"kosa lipi hilo nililolifanya ?

    Solo akamtazama mkuu wa jeshi kwa macho ya msitizo kisha akasema,, "umeuwa ndugu zangu na ukanipa maiti zao nikazike kule porini! 

    hakika nakwambia wale wanajeshi watatu nilio ongozana nao nilichinja shingo zao nikawazika huko porini,,, sasa basi leo ni siku yako ya hukumu ya kifo!



               ************************



    Upande mwingine alionekana Bakari akiwa ameketi chumbani kwake akisikiliza maongezi yote na kuona kila kitu kinachoendelea! kumbe alitegesha lenzi ndogo sana,, ya jicho la kamera,, ambayo inanasa mawasiliano ya moja kwa moja na kuonyesha tukio zima alitegesha kamera hiyo maalumu kwenye lile koti jeusi alilompa Solo ,,,Bakari akachukua simu yake akapiga simu kwenye. vyombo vya dora,, akasema,, "tumevamiwa na muuwaji anayefanya tukio la mauwaji na kisha kufunika maiti kwa koti jeusi,, akataja eneo,, mtaa na anuani ya nyumba hiyo... kisha akakata simu huku akitabasamu,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo kule kwenye maficho ya mkuu wa jeshi,  alionekana Solo akichomoa kisu na kuzipiga hatua kumfuata mkuu wa jeshi,, kwa lengo la kumchinja,, Punde si punde ikasikika milio ya risasi kutokea nje ya uzio wa nyumba hiyo!  Solo akashtuka akajisemea moyoni,, "bila shaka. hawa ni maaskari,, ni nani aliyewaelekeza kuja eneo hili??  ghafla wazo likamjia kuwa akimbie kabla maaskari hao hawajaingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo!

    akatimua mbio akalivua lile koti jeusi akalitupa chini,, akaruka ukuta na kutokomea kusikojulikana!



    Mkuu wa jeshi akabaki kasimama kama sanamu!  punde si punde maaskari wakavamia na kuingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo,, wakamkuta mkuu wa jeshi akiwa kasimama palepale,, huku suruali aliyokuwa ameivaa imetapakaa mkojo!



    Maaskari walimtambua mkuu wa jeshi,, kisha wakamuwekea ulinzi,,, huku maaskari wengine wakiingia ndani ya maficho ya mkuu wa jeshi sham ficha silaha na madawa ya kulevya!! 

    mkuu wa jeshi akapaza sauti akisema,, "hajaingia humo kakimbilia huko nyuma ya nyumba hii...

    aliamua kusema hivyo ilimradi wale maaskari wasiingie kwenye maficho yake wakabaini kinachotendeka ndani ya maficho hayo!

    wale maaskari wakaacha kuingia ndani ya nyumba hiyo! wakatimua mbio kuelekea nyuma ya nyumba hiyo.. lakini hawakukuta mtu yeyote,, zaidi ya koti jeusi lililotupwa chini!

    mkuu wa jeshi akaingia ndani ya gari lake Ada ngozana na maaskari kumuwekea ulinzi mpaka kule kwenye kambi ya jeshi!! wakahakikisha wamemfikisha salama,



                                ********************



    upande mwingine alionekana Solo akiliingiza gari lake ndani ya geti la nyumba ya Bakari!  akashuka kutoka ndani ya gari na kuingia ndani ya nyumba!  punde si punde Bakari akaja sebuleni,, akamuuliza,, "umefanikisha jambo lako?

    Solo. akajibu,, "hapana mpango umeharibika,,,maaskari walikuja eneo la tukio.. nikashindwa kufanya chochote.. nikatimua mbio,,, lakini mpango wangu na msimamo. bado uko palepale!



    kumbe Bakari hakutaka Solo amuangamize mkuu wa jeshi siku hiyo... moyoni mwake alikuwa na jambo ambalo anataka kulifanya yeye mwenyewe,, nia na lengo lake anataka mkuu wa jeshi ajue ukweli kuwa wale vijan awatatu aliowapiga risasi ni watoto wake wa damu, pia alitaka mkuu wa jeshi ajue kuwa Solo pia ni mwanae!!  na mke wa mkuu wa jeshi ni mkewe kwa sasa,, na ameshamzalisha mtoto wa kike,,,

    mkuu wa jeshi akishajua ukweli wote huu,, ndipo. amuuwe kwa mikono yake!

       CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                    ************************



    siku zilizidi kusonga,, na maisha yakaendelea,,, lakini mkuu wa jeshi alikuwa na wasiwasi kuhusu maisha yake!!  mbaya zaidi anaamini kuwa muuwaji anayefanya mauwaji ni Solo!!  kumbe sivyo! 



    Siku ya leo alionekana Bakari pamoja na mkewe wakiwa matembezini,,, wakashuka kutoka ndani ya gari na kuingia,, kwenye jumba la kuonyesha SINEMA..pale Mlimani City..



    wakati huo huo huo alionekana mkuu wa jeshi akiwa kule kambini akitafakari nini cha kufanya!  mawazo yalikuwa yanasumnua ubongo wake... akaamua kumuita mlinzi wake wa karibu,,, aongozane nae kuelekea kwenye jumba la kuonyesha sinema.....



    kule kwenye jumba la kuonyeshea sinema all nekana mke wa Bakari(Linda) akijishika kichwa kisha akasema,, "kichwa kinaniuma sana, naomba turudi nyumbani tafadhali!  Bakari hakutaka kumkwaza Linda wakanyanyuka na kutoka nje ya jengo la kuonyeshea Sinema,, wakazipiga hatua kulifuata gari lao kule lilipokuwa limeegeshwa!!!  wakiwa wanazipiga hatua... likaonekana gari la mkuu wa jeshi likiingia ndani ya geti na kuelekea kule sehemu ya kuegesha magari,,,

    Linda na Bakqri wakaingia ndani ya gari,, Bakari akaliwasha gari na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza,,, wakati wanatoka eneo hilo.. mkuu wa jeshi akamuona Linda ameketi ndani ya gari hilo!  macho yakamtoka!!! akajisemea moyoni,, hivi  kweli au naota,, huyu ni Linda mama watoto wangu???  inamaana yupo hai!  mmh!  inamaana hata gari langu halijui!!  au nimemfananisha!?  mkuu wa jeshi alijiuliza maswali hayo mfululizo pasipo kupata majibu!!  alipotahamaki,, gari la Bakari lilikuwa tayari limeondoka eneo hilo...

    mkuu wa jeshi akaingia harakaharaka ndani ya gari lake akaliwasha na kuliondosha kwa kasi kulifatilia lile gari alilomuona mkewe yumo ndani ya gari hilo.

    PATASHIKA!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mkuu wa jeshi akaendelea kulifatilia gari hilo,kwa umakini mkubwa hakutaka limuache umbali mrefu! kumbe Bakari alikuwa kashtukia kuwa mkuu wa jeshi analifuatilia gari lake,,akatabasamu kisha akabadili njia ya kupita akapita njia nyingine,,,akamuacha umbali mrefu mkuu wa jeshi!hatimae akatokomea kabisa...mkuu wa jeshi akastaajabu sana hakuliona tena gari hilo,,akaangaza angaza macho yake kila pande lakini hakufanikiwa kuliona gari hilo! akakasirika kupita kiasi,,akaamua kurudi kambini,

    alipofika akaliegesha gari lake,,kisha akashuka kutoka ndani ya gari akazipiga hatua kuelekea kwenye nyumba anayoishi! akiwa kaongozana na mlinzi wake!



                     ***************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog