Search This Blog

SOSO - 2

 







    Simulizi : Soso

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mary alichanganyikiwa...waliendele kupiga kelele lakini haikusaidia yule mtu aliliongoza gari hilo kwa kuliendesha....walipokuwa njiani walikutana na watu wawili wanamvuruta mtu aliekufa kwa kuchinjwa maiti hiyo ilionekana kiwiliwili bila kuwa na kichwa... yule dereva alisimamisha gari hilo aina ya pikap double keben... kisha watu wale walirusha maiti ile yuma ya gari na kupanda wakaketi upande wa nyuma.... mary alifumba macho kwa uwoga kwa sababu watu hao nguo ziliwajaa damu pia walikuwa na sura mbaya sana za kutisha... meno yao ya mbele yalikuwa marefu...safari iliendelea na hatimae walifika kunako mapango ya SOSO... ghafla jamesi akataka kuleta utata mlango wa gari ulipofunfuliwa alishuka na kuanza kutimua mbio kuelekea kusikojulikana... alifanikiwa kutoweka eneo lile kisha wale wanawake wanne/lawi na sande walichukuliwa kupelekwa kunako ndani kabisa ya pango.... baada ya kuingizwa ndani ya pango hilo"" walifungwa mikono na miguu pamoja na kuzibwa midomo kwa gundi ya nailoni.... kisha yule mtu mmoja mwenye meno marefu na sura ya kutisha... yeye pamoja na dereva waliondoka wskamuacha yule mwenzao mmoja akiwachunga akinaSande wasitoroke..... kisha mtu huyo alikwenda upande mwingine mule ndani ya pango punde alirudi na meza iliyokuwa na mataili huku imefunikwa kitambaa kilichojaa damu... aliisukuma meza ile mpaka jirani kabisa na pale walipokuwa wamefungwa akinaSande...mary macho yalimtoka alipiga kelele lakini hakusikika kile alichokuwa anakiongea kutokana alizibwa mdomo kwa gundi ya nailoni... ghafla mtu yule alikifunua kile kitambaa kilichojaa damu... walichanganyikiwa baada ya kuona zana za kutisha juu ya meza ilee... kulikuwepo msumeno/nyundo/shoka/visu/misumari/plaizi na zana nyingine nyingi....

    zana hizo zilionekana kuenea damu iliyoganda..



    ***********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine James alikuwa anakimbia hata bila kujua ni wapi anaelekea mara ghafla alikoswakoswa na mshale ukapiga mti... alipo ona hivyo.. aliongeza kasi ya kukimbia mara ghafla alitokea yule dereva mbele yake... alipogeuka nyuma ili akimbilie upande mwingine alikutana na upanga ukazama moja kwa moja kwenye utosi.. damu ziliruka kama bomba la maji lililokatwa ghafla... kisha james alidondoka chini na kupoteza maisha..



    ************

    kule kwenye mapango ya SOSO yule mtu alichukua mkasi mkubwa"" ni ule mkasi unaotumika kukatia majani katika uzio wenye mauwa,, kisha akaenda moja kwa moja mpaka pale alipokuwa amefungwa lawi... mtu huyo alimsogelea usoni kabisa lawi aligeuka pembeni huku amefumba macho kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka mdomoni mwa mtu yule... kisha akamvua viatu..lawi aliogopa na mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi... alijadibu kumsihi yule mtu lakini maneno hayakusikika kwa sababu alikuwa amefungwa mdomo.... kisha mtu yule aliupeleka mkasi ule mkubwa kwenye kidole gumba cha mguu wa lawi alikata kidole hicho kisha akakitaduna kibichi.... lawi alipiga kelele huku haja ndogo ikimtoka... alihisi maumivu ya hali ya juu.. kisha mtu yule alipiga hatua kuelekea pale ilipokuwa meza akarudisha mkasi akachukua kisu kisha akazipiga hatua kuelekea pale alipofungwa mary... alichana blauzi aliyokuwa ameivaa mary kwa kutumia kisu hicho kikali.. kisha akashika ziwa moja la mary kwa lengo la kulikata ziwa hilo.... mara ghafla walirudi wale watu wawili,, ni yule dereva na yule mwenye sura mbaya ya kutisha wakiwa wanavuruta mtu aliyekufa. baada ya watu wale kurudi mtu yule aliacha kukata ziwa la mary....mary alihisi kupoteza fahamu uwoga wa hali ya juu ulitawala juu yake"""" yule dereva na yule mtu wa kutisha waliivuruta maiti ile mpaka pale walipokuwa wamefungwa akinaSande Sande macho yalimtoka baada ya kuona maiti hiyo ni ya mdogo wake james"""" sande alijitahidi kutoka pale lakini alishindwa alikuwa kafungwa kamba baraabara..

    watu wale waliendelea muivuruta maiti ya james kuelekea upande wa ndani zaidi ya pango la SOSO..... waliondokawote watatu.

    kumbe kipindi yule mtu anataka kukata ziwa la mary""""....maryalikuwa akifurukuta kwa uwoga wakati anafurukuta kamba aliyokuwa imefungwa kwenye mikono yake ilifunguka....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Mary alinyata kisha akawafungulia wenzake... wakaanza kutimua mbio kutoka ndani ya pango hilo.... lakini lawi hakuweza kukimbia kwa kasi kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kwenye mguu ni baada ya kukatwa kidole na yule mtu wa kutisha... walikimbi hatimae wakatokezea nje kabisa ya pango hilo... waliliona lile gari ambalo walilipanda baada ya kuomba lift... sande aliingia haraka upande wa dereva...kisha mary akamkongoja lawi wakaingia wote ndani ya gari... sande aliliwasha gari hilo... walitokomea porini wakiwa wanaitafuta barabara kubwa... punde walitokezea barabarani. walipokwenda umbali wa kilomita mbili.. gafla walikuta mawe yamepangwa barabarani...njia imezibwa sande alipobadilisha gia ili ageize gari na kurudi ule upande walipotoka alipotazama nyuma aliona watu wale wamesimama barabarani nyuma ya gari....huku wameshikilia mapanga makali na marefu....sande alipojaribu kuendelea kuendesha alitokea yule mtu moja akapasua kioo cha mbele kwa upanga.... kisha akaanza kumkatakata sande mapanga ya kichwani mpaka sande akapoteza maisha... wakati huo mary alikuwa akipiga kelele kuomba msaada lakini kelele hizo hazikusaidia kwa sababu walikuwa maili nyingi sana kutoka makazi ya watu... yule mtu mwingine alifungua mlango na kumto mary ndani ya gari kisha akamfunga kamba miguuni na mikononi... kisha wakamuuwa lawi... wakamchukua mary akiwa mzima pia walichukuwa.....maiti ya lawi na sande wakaondokanazo walitokomea kusiko julikana...



    ****BAADA YA MIAKA SABINI(70) KUPITA*****



    ilikuwa majira ya jioni yapata saa kumi na mbili(12) alionekana mtu mmoja anayeitwa JOHN akiwa ameketi kwenye sofa huku akiangalia Taarifa ya habari..

    ilisemekana kuwa kwenye mapango ya SOSO yamegunduliwa mafuvu mawili ya vichwa vya binadamu""" mafuvu hayo yalikuwa makubwa kuliko kichwa cha binadamu wa kawaida pia meno ya mbele yalikuwa marefu sana kuliko meno mengine... John alipata shauku ya kufika huko kwenye mapango ya SOSO....

    ilipofika asubuhi.. John alijiandaa kuelekea kwenye ofisi za maliasili kwa ajili ya kuomba kibali cha kwenda kwenye mapango ya SOSO kwa sababu eneo lile lililindwa kwa ulinzi wa hali ya juu.. hakuweza kuingia mtu yeyote bila ruhusa au kibali maalumu.. kumbe John alikuwa ni Daktari MTAFITI wa TABIA ZA MIMEA NA WANYAMA... kutikana na kazi yake hiyo ilimfanya apate kibali kwa urahisi sana bila mlolongo wowote...alirudi nyumbani kwake ikwa ajili ya kujiandaa na safari kesho asubuhi kuelekea mapango ya SOSO..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *************



    palipo kucha aliweka begi lake ndani ya gari lake aina ya LAND ROVER kisha akaliwasha gari na kianza safari.. alipofika mtwara aliamua kulala ili kesho yake aendelee na safari... na palipokucha alianza safari ua kuelekea kwenye mapango ya SOSO...ilipofika majira ya saa tisa alasili alifika wenye mapango hayo alionesha kibali cha kuingia humo.. kisha akafunguliwa geti akaingia kwenye mapango hayo aliingia mpaka ndani zaidi""" alifanikiwa kuona baadhi ya mifupa ya watu wale mifupa yao ilikuwa mikubwa minene mirefu kama ya mnyama.... john alichukua baadhi ya mifupa hiyo kwa lengo la kuipeleka katika maabara yake ili aifanyi uchunguzi...... baada ya kuchukua mifupa ile alitoka nje ya pango na kuzunguki baadhi ya maeneo ya mnje huenda akapata chochote kingine kitakachomsaidia katika utafiti wake..... mara ghafla alihisi kunamtu kapita kwa kasi kama upepo alipojaribu kuangaza angaza hakuona kitu chochote.... alizindi kusonga mbele kuingia ndani zaidi ya eneo lile... kwa mbali aliona kama kunamtoto kachuchumaa alipokwenda sehemu ile hakuweza kuona kile alichohisi kaona... aliona tu mnyama aina ya swala akiwa anavuta pumzi za mwisho mwisho bado hajakata roho vizuri....huku akiwa ametobolewa upande wa tumboni huku utombo wake ukiwa umekatwakatwa....kama kuna kitu au mtu alikuwa akila nyama ile mbichi... john hakujali alihisi kaona vibaya kuwa palikuwa na mtu pale kachuchumaa ile sehemu alipokuwa yule swala.... aliamua kuondoka pale na kuelekea upande mwingine... mara ghafla....





    Aliona tena kunakitu kimepita mbele yake kuelekea upande wa pili alisruka sana....alipojaribu kuangaza angaza hakuona kitu chochote... aliamua kurudi ule upande alipokuwa amelipaki gari lake lakini alistahajabu kukuta milango yote ya gari ipo wazi..... alijiuliza nani aliyefungua!!!! alianza kuzipiga hatua haraka alipokagua vitu vyake vilivyokuwemo ndani ya gari vitu vyote vilikuwepo isipokuwa ule mfuko aliokuwa ameweka mfupa na meno aliyoyakuta ndani ya pango..... john alichukia sana aliona kama utafiti wake hautaenda sawa kama akitoka huko bila kupata kitu chochote cha kufanyia utafiti... aliamua kurudi ndani ya pango..... kutokana ilikuwa ni jioni jua lilikuwa karibu kuzama hivyo palionekana kuwa na giza kiasi ndani ya pango lile... aliwasha tochi kabla hajaingia ndani zaidi alihisi vishindo kama mtu ananyata..... alistuka akatoa bastola kwa kujihami.... kisha akazidi kuingia ndani zaidi kunako pango punde aliuona ule mfuko.. aliuchukua na kuanza kurudi alipotoka ili atoke nje ya pango... wakati anamulika mulika huku na kule kwa kutumia tochi aliona damu alizipiga hatua za harakaharaka mpaka ile sehemu kulipokuwa na damu"""alipotazama vizuri aligundua kuwa damu hizo sio za muda mrefu kwani ilikuwa bado mbichi.... alitoa kijiko na kopo dogo alichota damu ile kisha akaitumbukiza ndani ya kikopo kile kisha akatoa kikopo kidogo zaidi kilichokuwa na maji ndani yake alimimina tone moja kisha akafunika...maji hayo ni maalumu aliweka tone hilo ili damu ile isigande....aliamua kuchukua damu hiyoili akaifanyie utafiti. kisha akaanza kizipiga hatua kuelekea upande wa nje... punde alitoka nje kabisa ya pango hilo... alipofika nje ya pango alikuta walinzi wawili wakimsubiri... ni walinzi waliowekwa na serikali ili kulilinda eneo hilo tangu jana baada ya kugundulika lile fuvu kubwa la binadamu.....ilisikika sauti ya mlinzi mmoja akimwambia john kuwa muda wa kuwepo humo imekwisha hivyo aondoke eneo lile.... john hakupinha kwa sababu kilichomleta kafanikiwa kukikamilisha.....

    alipanda ndani ya gari na kuliwasha akaanza kuondoka mara ghafla alisikia kelele za mlinzi akiomba msaada john aliwasha taa za gari aliona mlinzi mmoja akiwa chini katobolewa sehemu ya tumboni huku utumbo wake umemwagika chini.... alipoangalia upande wa pili alioma yule mlinzi mwingine anavirutwa kwa kasi ya ajabu...alipojaribu kutazama kwa makini aliona mtu akimvuruta mlinzi yule kumuingiza kunako pango...lakini hakufanikiwa kumuona vizuri mtu yule ni wa aina gani aliyekuwa akimvuruta mlinzi..

    john aliingiwa uwoga akaliondoa gari lake kwa kasi ya ajabu alifika getini akafunguliwa geti akaondoka zake.....



    ***************

     CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya john kufika dar aliingia moja kwa moja katika maabara yake ya kufanyia utafiti alianza kwanza uchunguzi wa mifupa ile na meno... aligundua kuwa meno mifupa hiyo haikuwa ya binadamu wa kawaida... john alistahajabu sana... lakini vipimo vyake vinaonesha kuwa mofupa ile ni ya binadamu.... tom alijiuliza sana inamaana binadamu huyu alikuwa anafananaje mbona meno yake maredu sana na mifupa yake ni mikubwa kuliko binadamu wa kawaida!!!!

    kisha akachukua damu ile na kuanza kuifanyia utafiti....aligundua damu hiyo ni ya binadamu lakini alistahajabu sana baada ya kuona chembechembe hai nyekundu na nyeupe hazifanani kabisa na chembechembe hai za damu ya binadamu..... chembechembe hizo zilionekana kuwa na nguvu za ajabu alipojaribu kuweka virusi kwenye damu hiyo havikuchukuwa muda vilikufa.....

    alitengeneza dawa kupitia damu hiyo kisha akaipa dawa hiyo jina la JDH Dawa hiyo ilitibu magonjwa yote yanayoshambulia kinga ya mwili... John alipata umaarufu barani Afrika na Duniani kwote kutokana na dawa aliyoigundua.... kabla ajaanza kuisambaza ili ianze kitumiwa ulimwenguni.. aliamua kuifanyia majaribio.....

    Alimchukuwa binadamu mwenye virusi aina ya PHV akmchoma sindano mti yule... kisha akamfungia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa ndani ya maabara yake...

    baada ya siku mbili kupita...

    john akiwa anaelekea kwenye maabara yake alistahajabu sana baada ya kufika jirani na maabara yake alikuta maabara imebombolewa alipojaribu kusogea hakumuona mtu yule aliyekuwa kamfungia kwaajili ya majaribio.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog