Search This Blog

KOTI JEUSI - 4

 







    Simulizi : Koti Jeusi

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana Solo akiwa nyumbani,,akijiandaa kutoka kuelekea katika mizunguko yake! ghafla simu yake ikaita ,alipoitazama akagundua kuwa mkuu wa jeshi ndiye anampigia,,akaipokea simu hiyo! maongezi ya mkuu wa jeshi,,yalikuwa hivi:

    yani kumbe muuwaji ninayemtfutamiaka yote ni wewe! kwa nini unafanya mauwaji kisha unafunika maiti kwa koti jeusi,,nini dhamira yako! embu niambie sababu ya kufanya mauwaji hayo na nikwanini unauwa maafisa wa jeshi na viongozi wa serikarini pekee!?

    Solo akabaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema,,"muuwaji sio mimi,,lakini hayupo mbali,utamuona hivi karibuni ,lakini kuhusu kifo chako,,nitakuuwa mimi mwenyewe kwa mikono yangu, kish akakata simu.



    punde si punde Bakari na Linda wakafika nyumbani,,,Bakari akaliegesha gari lake,,wakashuka kutoka ndani ya gari wakaingia ndani ya nyumba,,,wakamkuta Solo anatoka ndani ya nyumba kuelekea upande wa nje,,, Bakari akamfuata Solo kwa nyuma kisha akasema,, "unakwenda wapi? 

    Solo akamtazama Bakari kisha akajibu,, "sifiki mbali dady nakwenda kununua kitu fulani dukani lakini kwenye maduka ya mjini! 



    Bakari akasema,, "kuwa makini huko uendako.. lakini kunajambo nataka nikueleze! 

    Solo akawa na shaukubya kutaka kujua jambo hilo! 

    Bakari akasema,, "muuwaji anayetafutwa miaka mingi iliyopita,, anayefanya mauwaji na kisha kufunika maiti kwa koti jeusi,,, si mwingine muuwaji huyo ni mimi mwenyewe...

    Solo. akashtuka kusikia maneno ya Bakari,, akauliza kwa mshangao,, "kwa nini uliamua kufanya hivyo?  Bakari akaanza kusimulia kuwa,, alikuwa mwanajeshi miaka mingi iliyopita,, kisha mkuu wa jeshi akampa kazi ya kuwauwa watu watatu ndani ya wiki moja,, miongoni mwa watu hao alikuwemo Raisi wa nchi.. nikakataa kufanya mauwaji hayo,, mkuu wa jeshi akaamua kunisingizia kesi ya kuiba silaha za kivita katika kambi ya kijeshi niliyokuwa nafanyia kazi!  nikahukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani!

    akasita kuendelea kusimulia,,hakutaka Solo ajue kuwa mkuu wa jeshi aliiangamiza familia ya Bakari,, pia hakutaka ajue kuwa Solo ni mtoto wa mkuu wa jeshi,,  kisha akasema,, "ndipo nikaamua kufanya mauwaji kwa maafisa wa jeshi na viongozi wa serikarinwalikuwa wanashirikiana na mkuu wa jeshi kwenye bihashara haramu! 



                              *************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine kule kwenye kambi ya jeshi alionekana mkuu wa jeshi akiwa  chumbani kwake akajaribu kufanya uchunguzi wa mawasiliano ya Solo yanatokea eneo gani,, akagundua kuwa Solo yipo Tabata muda huo.. akaamuru wanajeshi waende kumteka Solo kwa sababu amemwambia kuwa muuwaji anayefanya mauwaji na kufunika maiti kwa koti jeusi anamjua!! hivyo Solo akinaswa atasema ni wapi muuwaji huyo alipo!

    Amri ya mkuu wa jeshi ikatekelezwa baadhi ya wanajeshi wakaelekea tabata wakiongozwa na kifaa maalumu (GPS) kwenda kumnasa Solo,,



    wakati huo huo kule nyumbani kwa Bakari aliendelea kusimulia mkasa wote,,,  Solo akaamua kubaki nyumba akiendelea kumsikiliza Bakari kwa makini,,

    baada ya lisaa limoja wanajeshi hao walifanikiwa kuipata nyumba  anayoishi Solo kwa kutumia kile kifaa maalumu kilichokuwa kinawaongoza(GPS)



    Kule ndani ya nyumba Bakari alashtuka ,,akahisi kuwa nje ya nyumba yake hakuna usalama,, akamwambia Solo kuwa,, kunahatari,, yatupasa tuondoke haraka eneo hili!

    wakatimua mbio kuingia ndani ya nyumba!! Bakari akatazama kwenye Runinga maalumu aliyoiunganisha na kamera zinazoonyesha eneo la nyumba yake upande wa nje..akawaona wanajeshi nje ya geti wakiwa wamebeba silaha za moto... akamwambia Solo sisi tuondoke,, eneo hili wacha Linda abaki.. hawatamfanya chochote, kwa sababu walengwa ni sisi!

    bila kuchelewa wakatoka haraka nje ya nyumba hiyo kupitia mlango wa siri wa njia inayopita chini kwa chini,, mpaka nje kabisa ya nyumba hiyo! Linda hakufahamu chochote kinachoendelea.

    baada ya sekunde kadhaa wale wanajeshi wakavamia na kuingia ndani ya nyumba ya Bakari,, wakakagua kila chumba hawakufanikiwa kumpata Solo,, mwanajeshi mmoja akapiga simu kwa mkuu wa jeshi akasema,, "hakuna mtu yeyote tumemkuta mwanamke tu akiwa ndani ya nyumba hii!!

    mkuu wa jeshi akasema,," mwanamke huyo apewe mateso makali mpaka aseme ni wapi Solo alipo..mimi niponnjiani nakuja  huko muda mchache ujao..

    wale wanajeshi wakaanza kumpiga Linda kila sehemu ya mwili wake,, pamoja na mateke ya tumboni,, Linda akasema,, "mimi sijui chochote,, kuhusu maswali mnayoniuliza,, wale wanajeshi wakaendelea kumpiga mateke kila sehemu ya mwili wake... mwanajeshi mmoja akaingiwa na hasira baada ya kuhisi huenda Linda anadanganya!  akampiga teke la usoni Linda akadondoka chini akatulia tuli!!

    Punde si Punde mkuu wa jeshi akawa amefika akaingia mpaka ndani ya nyumba hiyo!  alipomtazama mwanamke huyo akagundua kuwa ni mama wa watoto wake!! macho yakamtoka!

    akamsogelea na kuanza kumtikisa... kisha akanyanyuka na kuanza kufoka akiuliza ni nani aliyempiga mwanamke huyo..

    mwanajeshi mmoja akajibu,, "samahani mkuu, ulitoa amri ateswe mpaka aseme ukweli...

    mkuu wa jeshi akachomoa bastola na kufatua risasi ikaenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa mwanajeshi huyo akafa papo hapo!

    kisha kampiga risasi wanajeshi mwingine akafa papohapo!

    wale wanajeshi wengine wakatimua mbio na kutokomea kusikojulikana!  mkuu wa jeshi akajikuta anatokwa na machozi akiamini Linda amekufa!  wakati anatahamaki mara ghafla simu yake ikaita,, alipoitazama akagundua kuwa ni namba ya simu yake ndogo,, anayopenda kuacha ndani ya gari lake!







    Akasita kuipokea hofu ikatanda juu yake!  akatoka nje ya nyumba ya Bakari,, akazipiga hatua huku macho yake yakitazama. kwa tahadhari,, akalifuata gari lake,, huku kashikilia bastola tayari kwa lolote litakalotokea mbele yake! alipolikaribia gari lake akakuta koti jeusi limewekwa ndani ya gari lake!  pia ile simu yake ndogo ilikuwemo ndani ya gari hilo,, lakini hapakuwepo na mtu yeyote!



    Wakati huohuo kule nje ya nyumba alionekana Bakari na Solo wakibeba maiti za wanajeshi na kuziingiza ndani ya gari,, ni wale wanajeshi walitimua mbio kuokoa uhai wao kutoka mikononi mwa mkuu wa jeshi,,ni baada ya kumuona mkuu wa jeshi akiwapiga risasi wanajeshi wenzao wawili na kupoteza uhai papo hapo!

    walipotoka nje ya nyumba hiyo wakakutana na Solo pamoja na Bakari wakiwa wamesimama nje ya uzio wa nyumba hiyo.. Bakari na Solo wakawadhibiti wanajeshi hao na kuwauwa kimyakimya!  kisha wakazibeba maiti hizo na kuziingiza ndani ya gari mojawapo lililokuwa li. eegeshwa nje ya uzio,,  ni miongoni mwa magari waliyokujanayo wanajeshi hao,, huku gari moja likiwa ndani ya uzio, CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bakari na Solo wakaondoka eneo hilo na kurudi kwenye ile chemba ya njia ya siri inayotokea ndani ya nyumba kuelekea nje kabisa ya nyumba hiyo!



    punde si punde akaonekana mkuu wa jeshi akiliendesha gari lake kutoka kwenye geti.. alipofika upande wa nje ya uzio akastaajabu kuona wanajeshi wake wameketi ndani ya gari juku wamefumba macho!!  akaamuakushuka kutoka ndani ya gari lake akazipiga hatua kulifuata lile gari la wale wanajeshi wake!  akashtuka kuona wameuwawa!! hofu ikazidi kuongezeka,, akahisi kuchanganyikiwa akatimua mbio. kurudi ndani ya gari lake!  akaliwasha haraka na kuondoka zake na kuzitelekeza maiti za wanajeshi hao!



           

                               ************************



     Upande mwingine kule kwenye chemba, alionekana Bakari akiwa anazipiga hatua kuelekea ndani ya nyumba!  akashtuka kumkuta mkewe kalala chini huku damu zinamtoka puani na mdomoni! pumde si punde Solo akafika!!  Bakari akamtazama linda kwa makini,,akagundua bado anapumua!  akafanya jitihada za kuokoa maisha ya Linda kwa kukandamiza kifua chake mfululizo,, kusaidia mapigo ya moyo ya Linda yasisimame!  ghafla Linda akageuza shingo yake akafumbua macho,,



    Bakari akamwambia Solo!  muda tayari,, ebu chungulia kama wale wanajeshi wameondoka!

    Solo akastaajabu!!! kisja akasema,, "tumewauwa wataondoka vipi wakati tayari ni wafu?

    Bakari akasema,, "hapana hawajafa wamepoteza fahamu,, niligonga mishipa ya fahamu kwenye shingo zao!  hivyo wahajafa wamepoteza fahamu na baada ya dakika kadhaa lazima wazinduke! hii ni mbinu maalumu ya upiganaji! na ukitaka kujua sehemu hizo,  ni lazima ufundishwe huwezi kujua pasipo mafunzo!

    Solo akabaki mdomo wazi,, yeye aliamini kuwa wanajeshi hao wamekufa!



    Wakati huohuo kule upande wa nje wakaonekana wale wanajeshi wakipqta fahamu,, kila mmoja kwa muda wake!  wakastaajabu kukikuta wamo ndani ya gari lao! mmoja kati ya wanajeshi hao akaliwasha gari na kuliondosha kwa kasi ya ajabu kuelekea kambini ,,wakiwa njiani wanajeshi wote wakazinduka na kupata fahamu!  mmoja kati ya wanajeshi hao akasema,, "jamani mmeona wenzetu wawili wameuwawa mbele ya macho yetu kwa kupigwa risasi na mkuu wetu!  nyinyi hamuogopi? kama. nuinyi mnarudi kambini,, naomba mimi mnishushe hapahapa,, siitaki tena kazi hii ya kijinga!

    wale wanajeshi wengine wakatazamana nyuso zao,, wakaungana na wazo la mwenzao,, walipofika eneo la kambi ya jeshi,, wakalitelekeza gari hilo,, na kutokomea kusikojulikana!



    baada ya dakika kadhaa kupita,,,akaonekana mwanajeshi mmoja akimwambia mkuu wa jeshi kuwa gari la jeshi limetelekezwa nje ya kambi,, na hakuna mwanajeshi hata mmoja ndani yake!  mkuu wa jeshi akatoka ndani ya ofisi yake akaongozana na mwanajeshi huyo mpaka nje ya kambi!!  walipofika,, macjo yakamtoka mkuu wa jeshi,, baada ya kugundua kuwa gari jilo ni lile lililokuwa na maiti za wanajeshi waliouwawa masaa machache yaliyopota! akajisemea moyoni,, "nani kalileta hapa gari hili?  je maiti za wale wanajeshi zimepelekwa wapi?

    mkuu wa jeshi alijiuliza mazwali jayo pasipokupata majibu,, akajikuta anacheka peke yake ,,wakati huohio anali,,,akawa kama mtu mwenye ugonjwa wa akili? akatimua mbio kurudi ndani ya kambi!  jamno jilo lilimshtua yule mwanajeshi aliyetoa taarifa hiyo ya gari la jeshi kitelekezwa nje ya kambi! akabaki anamshangaa mkuu wa jeshi anavyotimua mbio! 



                 **************************



    Upande mwingine kule nyumnani kwa Bakari,, aliomekana Linda akiwa amepata nafuu ,lakini alikuwa anasema anahisi maumivu makali,,mwilini mwake!

    Bakari akaamua kumpeleka hospitali,,, wakaonhozana na Solo. kuingia ndani ya gari! 

    walipofika hospitali,, Limda akafanuiwa bipimo vya Picha(X-RAY)

    vipimo vikaonyesha kuwa baadhi ya misuli yq mwili wa Linda kuna damu umevia na imeganda,, jivyo atalazimika kulazwa kwa ajili ya matibabu maalumu!

    ilipofika majira ya saa moja za usiku,, Solo akanqki hospitali akimuuguza Linda,,

    Bakari akaondoka na kuifuata ile nyumba anauoitumia mkuu wa jeshi kwa kuficha silaha na madawa ya kulevya,,, akachoma moto nyumba hiyo na kiondoka zake,, kurudi kule hospitali.. .

    Taarifa hizo zikamfikia mkuu wa jeshi akahisi ,,akapata mshtuko waoyo akapoteza fahamu!  akakimnizwa haraka hospitali..

    kumbe hospitali,, anayopelekwa mkuu wa jeshi,, ndiyo ile hospitali aliyolazwa Linda!

    baada ya dakika kadhaa kupita mkuu wa jeshi akaletwa hapo hospitalini ,,wakati wanampeleka kwenye wodi Solo akamuona mkuu wa jeshi! kisha akajisemea moyoni,, "kajileta kwenye mdomo wa simba,, hakika hatoliona jua la kesho! Solo akafatilia kwa ukaribu akaiona wodi aliyoingizwa mkuu wa jeshi!

    ilipofika majira ya saa nne za usiku,, jali ya Linda ikabadilika akawa joi akasjindwa kupumua,, akakimnizwa haraka kwenye chumba maalumu cha usaidizi wa hewa safi kwa mtu asiyeweza kupumua mwenyewe, (I.C.U) lakini wakawa wamechelewa,,Linda akapoteza maisha!







    Mkuu wa jeshi akafanyiwa huduma ya kwanza kupandisha msukumo wa. damu mwilini!  baada ya masaa kadhaa kupita fahamu zikarejea! akastaajabu kuona yupo hospitol!  alipogeuza shingo yake hakuona mtu yeoyote kuwemo ndani ya wodi hiyo! punde si punde akaingia daktari ndani ya wodi,, akakuta mkuu wa jeshi ameshapata fahamu!  akasema,, " pole sana Mheshimiwa,unajisikiaje hali yako kwa sasa?

    mkuu wa jeshi akajibu,, "naendelea vyema,,nilioatwa na nini?  mbona nipo hapa?

    daktari akajibu,, "ulipata mshtuko,, ukapoteza fahamu!

    mkuu wa jeshi,, akajaribu kuvuta kumbukumbu,, akakumbuka kuwa alipoteza fahamu baada ya kupata taarifa hiyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine!  alionekana Solo na Bakari wakifanya maandalizi ya kumzika Linda! 

    kiukweli kifo hicho kiliwasikitisha sana,,,lakini kichwani mwa Solo alikuwa akiwaza jinsi ya kwenda kumuangamiza mkuu wa jeshi!

    Bakari akasema,, "kila kitu kipo tayari,, sasa yatupasa twende mochwari kuchukua maiti ya Linda kwa ajili ya kuzika!

    wakakubaliana na safari ya kuelekea kule hospitali kuchukua maiti ya Linda ikaanza.



    Wakati huohuo kule hospitali,, alionekana mkuu wa jeshi akimsisitiza daktari,, amruhusu aende nyumbani kwa sababu anajisikia nafuu.

    daktari akamruhusu aende nyumbani kwa ajili ya mapumziko!



                     ******************************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog