Search This Blog

BAHARI YA HINDI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Bahari Ya Hindi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilionekana gari moja aina ya Mark II (old model) ya kizamani,ikipaki nje ya geti la kuingilia bandarini....wakashuka watu wawili,,Mwanaume mmoja na mwanamke mmoja,,watu hao walikuwa wanafanya kazi sehemu moja,katika kituo cha Habari,,,yule mwanaume alifahamika kwa jina la TOBI na yule mwanamke anaitwa RODA....ghafla!!! ukasikika mlio mkali wa honi ya meli,,honi hiyo ikiashiria kuwa muda umekwisha,,meli inataka kung'oa nanga...wakakimbia haraka kuingia ndani ya geti...lakini Tobi alizuiliwa kuingia ndani ya meli...kwa sababu alikuwa amesahau tiketi nyumbani kwake,,hakuwa na ujanja akalazimika kubaki ili afanye mpango wa kukata tiketi katika meli nyingine...



    Roda alisikitika sana,,lakini hakuwa na namna...akaingia ndani ya meli,,huku akimuacha Tobi hapo bandarini...baada ya dakika mbili kupita Meli ikang'oa nanga,, na safari ikaanza,,,wakati huo ilikuwa ni majira ya saa mbili za asubuhi,,Meli hiyo ilikuwa anatokea Mombasa kuelekea Zanzibar...Safari hiyo ya Roda na Tobi walikuwa waende Zanzibar kukusanya na kuandika habari kuhusu watawala wa kale(wakoloni)

    lakini Roda akalazimika kusafiri peke yake!!! bila Tobi.

    meli ilizidi kuchana mawimbi na baada ya mwendo wa masaa matatu kupita..meli hiyo ikapata hitirafu,,injini zote mbili zikashindwa kuendelea kufanya kazi,,hivyo meli hiyo ikazimika na kubaki ikielea juu ya maji yenye kina kirefu sana...chenye urefu wa mita sabini kwenda chini!! nahodha wa meli hiyo..akatangaza kwa kutumia kipaza sauti(MIC) sauti ya nahodha huyo ikasikika kwenye spika zilizokuwa zimewekwa kila kona,,, ndani ya meli hiyo!

    nahodha alisema hivi,,"Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza hivi punde!!!..hivyo muwe wavumilivu,,wakati mabaharia na mafundi wakiwa wanatengeneza meli hii....



    ***********************



    wakati huohuo,,wakaonekana mabaharia watano(mafundi wa meli) wakiingia kwenye milango inayotokezea kwenye chemba ya kwenda upande wa injini za meli hiyo....wakaanza kutafuta  chanzo cha injini hizo kushindwa kufanya kazi!!!

    walitumia masaa mawili mfululizo kutafuta chanzo ni nini!!...punde si punde...mmoja kati ya mabaharia hao,,akagundua kuwa kuna kifaa kimepasuka inatakiwa kichomwe na kuunganishwa kwa moto wa gesi...bila kuchelewa mabaharia wengine wakaleta mtungi wa gesi haraka na kazi ikaanza..wakachoma kifaa hicho kwa kuunganisha na kile kipande kilichopasuka....waliifanya kazi hiyo kwa lisaa limoja wakawa wamemaliza......pamoja na yale masaa mawili yakawa masaa matatu yametimia.



    Baharia mmoja akatoka kwenye chemba hiyo na kwenda kutoa taarifa kwa Nahodha kuwa tayari kazi imekwisha,,hivyo awashe mitambo safari iendelee...lakini yule Nahodha kila akijaribu kuwasha mitambo...haikuwaka,,, bado ilionekana kuwa kunatatizo katika upande wa injini..

    yule baharia akashuka kule chini ilipokuwepo injini kwa kupitia ule mlango wa chemba..kwenda kuwajulisha wenzake kuwa bado kunatatizo



    *************************



    Upande wa juu ya meli..alionekana Roda akiwa amesinzia kwenye kile kiti alichokuwa ameketi!! akastuka kutoka usingizini...akaangaza angaza macho yake huku na kule..akaona abiria wenzake wakiwa wamesinzia!! huku wengine wakiwa macho wazi...ukimya ulitawala ndani ya meli hiyo!!!.haikusikika hata sauti ya mtu akiongea na jirani yake!



    Roda akainua mkono wake na kutazama saa aliyokuwa kaivaa mkononi mwake....akastahajabu!!! ilikuwa yapata saa kumi kasoro za jioni..akastuka akajisemea moyoni,,inamaana tangu muda ule mpaka sasa meli haijaondoka!!!? Roda akaanza kuingiwa na wasi wasi...

    kule nje,,,Upepo ulivuma kwa kasi..

    upepo huo ulisababisha maji ya bahari kutengeneza mawimbi makubwa sana..yakawa yanapiga kwenye ubavu wa meli hiyo..ikawa inayumbayumba huku ikielea.

    abiria wote waliokuwemo ndani ya Meli hiyo wakaanza kuingiwa na hofu......ukimya ukazidi kutawala

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea chooni kujisaidia...

    akiwa anatembea,,kabla hajaufikia mlango wa choo,,kuna wimbi kubwa lililokuja kwa kasi na kupiga ubavuni mwa meli hiyo ikayumba kupita kiasi!!,, nusu Roda adondoke akawahi kushikilia kingo za korido ya meli hiyo..mkononi mwake alikuwa kashikilia kifaa kidodo chenye ukubwa sawa na simu ya kawaida!!(TAPE RECORDER) kifaa hicho kilimponyoka kutoka mkononi na kutumbukia kwenye ile chemba ya kuelekea kule chini,,zilipo inji za meli hiyo....kikadondoka  chini zaidi...



    *******************



    Upande mwingine kule kwenye chumba cha Nahodha wa meli hiyo,Nahodha huyo alionekana kuingiwa na wasiwasi!!! akajiuliza,,"mbona mpaka sasa hivi sijapokea taarifa yoyote kutoka kwa mabaharia(mafundi wa meli) kuna tatizo gani???

    Nahodha huyo alijiuliza maswali bila kupata jibu...akaendelea kuwa mvumilivu,,kusubiri taarifa kutoka kwa mabaharia waliokuwa wakitengeneza injini za meli hiyo......



    **********************



    Upande mwingine alionekana Roda akijilaumu sana..akajisemea moyoni,,"siwezi kukiacha kifaa hicho(TAPE RECORDER)..ndicho kinatunza kumbukumbu ya kazi zangu za uandishi wa habari...isitoshe..kunahabari imo ndani yake na habari hiyo ni muhimu sana...



    Roda akaamua kusukuma  mlango wa chemba hiyo..akashuka upande wa chini kwa kutumia ngazi iliyokuwemo ndani ya chemba hiyo...alipofika upande wa chini akafanikiwa kukiona kifaa chake(TAPE RECORDER)....kabla hajakiokota akasikia vishindo vya mtu akikimbia kuja upande wake!!! akashtuka.....ghafla akasikia sauti ya mtu akilia kwa sauti kali,,ghafla sauti hiyo ikanyamaza....Roda akaamua kuchungulia aone nini kimetokea.....akashtuka!! macho yakamtoka baada ya kuona wale mabaharia watano wakiwa wameuwawa kikatiri huku damu nyingi zikitoka mwilini mwao!!! Roda akaingiwa na hofu kubwa..akatimua mbio kuifuata chemba ili atoke na kurudi kule upande wa juu..ghafla akahisi kaona kitu kimepita mbele yake kama upepo!!.lakini hakukitambua kuwa ni kitu gani!! wakati anatahamaki,,,,,,ghafla akaguswa begani.........





    Alipogeuka hakuona mtu,,hofu ikazidi kuongezeka,,akajikuta anatamani apige kelele,,lakini akawa anaogopa,,endapo kelele hizo zitasikika,,wahusika wa meli hiyo wakija na kukuta wale mabaharia wameuwawa...basi yeye atakuwa hatiani...akaingia kwenye chemba,,ili apande ngazi atokezee uoande wa juu....akaanza kupanda gazi harakaharaka..alipokanyaga ngazi ya mwisho ili atokezee upande wa juu ghafla mlango ukajifunga!! akashtuka akaachia mikono yake akadondoka chini na kupoteza fahamu!



    ***********************



    kule juu ya meli katika chumba cha Nahodha, alionekana Nahodha akizioiga hatua kuifuata chemba ya kushuka chini kule kwenye injini za meli hiyo,,,aliamua kwenda huko baada ya kuona ni masaa mawili mfululizo hajapata taarifa yoyote,,kutoka kwa mabaharia,,alipoufikia mlango wa chemba hiyo,,akastaajabu kukuta mlago huo umefungwa kwa ndani!!!,,,

    kutokana na uzoefu wa kuendesha meli hiyo miaka mingi,,alikuwa anazijua chemba zote za meli hiyo.....akaamua kuelekea kwenye chemba nyingine inayotikezea kule chini ya meli kwenye injini.



    Wakati huo abiria wote waliokuwa wamepanda meli hiyo,,walionekana kuwa na hofo na wasiwasi juu ya safari yao,,walijiuliza mpaka mda huu bado wapo katikati ya bahari,,alafu hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wahusika wa meli hiyo,,kuhusu maendeleo ya matengenezo ya meli hiyo!

    nje ya meli,,Mawimbi makubwa ya maji yaliendelea kupiga kwenye ubacu wa meli hiyo..na kusabavisha mtikisiko mkubwa na meli hiyo kuyumbayumba kila wakati!! masaa yalizidi kusonga na giza likaanda kutanda  kuizunguka bahari...



    **************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    uoande mwingine alionekana nahodha wa meli hiyo akizioiga hatua,,hatimae kaifikia chemba nyingine,itakayoitumia kuelekea kule kwenye injini za meli hiyo,,,akafungua mlango,,akawasha swichi za taa zinazomulika huko chini ya meli..akaanza kuzipiga hatua kuzifuata injini zilipo.. ghafla akasikia sauti ya mlango ukijifunga,akashtuka!!!

    akaangaza angaza macho yake lakini hakuona mtu aliyefunga mlango huo...hakujali,,akahisi huenda kwa sababu meli inayumbishwa na mawimbi,,ndio sababu mlangu umjifunga,,akaendelea kuzipiga hatua,,alipokaribia kwenye sehemu zilipokuwepo injini za meli hiyo..akashtuka! macho yakamtoka!! baada ya kuona mabaharia wote wameuwawa huku wakionekana kitapakaa damu mwili mzima!! akatoa bastora iliyokuwa kwenye pochi ndogo iliyofungwa kwa mkanda kiunoni mwake...akaiweka tayari kupambana na chochote kitakachojitokeza mbele yake. ghafla taa zikaanza kuzima na kuwaka,bila kuonekana mtu anayefanya hivyo!!!



    ****************************



    kule upande wa juu ya mwili,,bado walionekana abiria wa meli hiyo,, kuwa katika hali ya wasiwasi,,na hofu kubwa kuliko,,,ukimya ulitawala,,zilisikika tu kelele za mawimbi yakigpiga kwenye ubavu wa meli na kusambaa...ghafla taa zikazimika,baada ya sekunde kadhaa zikawaka,,abiria wakaanza kupiga mayowe na kelele,,wakiomba wapate taarifa kuhusu maendeleo ya meli hiyo,,kutoka kwa wahusika!!!

    ghafla taa zikazimika!!! hazikuwaka tena,,giza lilitawala,,na kila abiria alibaki kimya akiMuomba mungu , kwa imani yake..



    Nje ya meli upepo uliendelea kuvuma kwa kasi,,huku mawimbi makubwa yakiendelea,,kuizonga bahari!! vingu kubwa likatanda,,,,hatimae mvua kubwa ikaanza kunyesha....



    ***************************



    Kule chini ya meli, zilipo injini za meli hiyo,,alionekana Nahodha wa meli hiyo,,,akiwa ameshikilia bastola huku macho yake yakitazama kwa tahadhali!

    wakati huohuo alionekana Roda akiwa bado kalala pale chini baada ya kudondoka kutoka juu ya ngazi..

    Roda akaanza kupata fahamu,,akafumbua macho,,

    akashtuka kuona giza nene limetanda!!! akanyanyuka haraka,,akaanza kubahatisha nzia kwa kupiga hatua huku katanguliza mikono yake yote miwili mbele huku akipapasa papasa aendako,,,ghafla akagusa makalio ya Nahodha!!

    Nahodha akashtuka akajikura anafyatua risasi ovyo ovyo bila kumuona mtu anayemshambulia..

    Roda alipiga kelele huku kachuchumaa,,,akaziba masikio yake kwa kutumia viganja vyake vya mikono...

    Nahodha huyo aitwae YUVE,,akapaza sauti na kusema,,"WEWE NI NANI?? JITAMBULISHE HARAKA KABLA SIJATENGANISHA ROHO NA KIWILIWILI CHAKO!



    Yuve aliuliza swali hilo huku akiwa na uwoga wa hali ya juu...

    ikasikika sauti ya Roda ikisema,,usiniuwe kaka yangu!! naomba msaada wako unitoe huku niweze kurudi kule juu ya meli,, kwenye kiti changu.

    Yuve akasema kwa sauti ya msisitizo,,"nataka uniambie wewe ni nani? na umeingiaje huku kwenye chumba cha injini!!! na ulikuwa na lengo gani??

    Roda alishindwa kujibu chochote,,ghafka ikasikika sauti ya kitu kikijigonga kwenye nguzo moja iliyopo  eneo hilo....

    Yuve akazidi kuchanganyikiwa....jwa sababu alikuwa haoni mtu yeyote,,bali alisikia sauti tu,,kutikana na giza totoro lililokuwa limetanda humo baada ya taa kuzimwa na mtu asiyejulikana.....

    wakati Yuve bado yupo katika hali ya mshangao!!!

    ghafla zikasikika sauti za abiria kule juu ya meli wakipiga mayowe ya kuomba msaada!!

    Roda akasema,,"kaka upo wapi naomba unisaidie kunitoa huku,,,Roda aliongea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi,,na hofu kubwa kutanda juu yake,,kwa sababu alikuwa hamuoni mtu anayeingea nae, kutikana na giza nene ndani ya chumba hicho maalumu kwa injini za meli hiyo..

    Yuve alizidi kuchanganyikiwa akajikuta anatetemeka mwili mzima kutokana na uwoga wa hali ya juu! akazipiga hatua kwa kutumia hisia na uzoefu kuufuata mlango wa kutokezea kwenye chemba ya kufika uoande wa juu ya meli..ghafla taa zikawaka,,na mwanga ukamulika kila kona ya chemba hiyo....Yuve akaangaza angaza macho yake huku na kule akamuona Roda,,akastaajabu sana akamuuliza,,huku ulikuja kutafuta nini???

    Yuve aliuliza huku bado akiwa na mashaka na Roda.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akajibu,,"nimekuja kufata kifaa changu kilidondija huku chini wakati nataka kuingia chooni(TOILET)! Yuve akashtuka akauliza kwa mshangao!! kifaa chako?? kifaa kipi hicho??

    kabla Roda hajajibu taa zikazimika,,na giza likatanda!! baada ya sekunde kadhaa taa zikajiwasha bila kuonekana mtu anayewasha taa hizo....walipotahamaki..wakamuona mtoto mdogo wa kiume kasimama katikati yao huku akiwa amevalia mavazi meupe yanayo ng'aa,,mtoto huyo alionekana kuwa na umri kati ya miaka minne(4) au mitano(5) akaachama mdomo wake,,machi yake yakabadilika na kuwa kama ya mnyama paka! meno mawili ya juu na chini uakawa marefu kama ya mbwa..kucha zake za mikononi zikaanza kurefuka akazipiga hatua kumfuata Roda...





    Roda akapiga mayowe kwa uoga wa hali ya juu..hofu kubwa ilitanda juu yake,,Yubv akafyatua pqrisasi mbili kumlenga yule mtoto kichwani. risasi zikaingia ndani ya kichwa cha mtotoq huyo...akageuza shingo yake kumtazama Yuve..mtoto huyo akapindisha shingo yake kushoto kulia,,huku akiendelea kumtazama Yuve.punde si punde Yuve akahisi kukabwa shingoni na kitu kisichoonekana....akaanza kushindwa kuvuta pumzi wala kutoa pumzi..akaachilia bastola baada ya dakikamoja kupita akadondoka chini na kupoteza maisha...Roda akatimua mbio akajificha chini ya injini moja ya meli hiyo!



    akawa anachungulia ili aone mtoto huyo atafanya nini baada ya hapo!! yule mtoto akageuza shingo yake na kutazama ule upande ilipokuwepo injini ya meli hiyo..

    Roda akashtuka,,akiamini kuwa yeye ndiye anayefuata kuuwawa!! akajiziba mdomo kwa kutumia kiganja cha mkino wake mmoja...ili asipige kelele ikasikika kwa mtoto huyo....

    Roda aliendelea kuchungulia akimtazama mtoto huyo..ghafla mtoto huyo akatoweka kimiujiza,,na kutokomea kusikojulikana...



    *************************



    kule juu ya meli Abiria waliendelea kupiga mayowe ya kuomba msaada,,baada ya kuona abiria mmoja mmoja anauwawa na mtu asiyeonekana kwa macho....huku taa zikizimika na kujiwasha pasipo mtu yeyote kuonekana akifanya kitendo hicho!!! ghafla taa zikawaka na mwanga ukaangaza kila kona ndani ya meli hiyo.

    Abiria wote wakanyamaza,,na ukimya ukatawala...

    Wakati huo meli ilikuwa inayumba yumba, kutokana na mawimbi makubwa yaliyokuwa yanapiga ubavuni mwa meli hiyo..



    ******************************



    upande mwingine,, chini ya bahari,kilionekana kiumbe kisichokuwa na mfano kikija upande wa juu ya bahari,,kiumbe hicho kilionekana kutisha sana,,ghafla kikatoweka,,kikajitokeza ndani ya meli hiyo!!! kule juu sehemu ya abiria.

    Abiria wote wakaingiwa na hofu baada ya kumuona kiumbe huyo,,wakaanza kupiga mayowe,,ghafla taa zikazimika!!! giza likatawala kupita kiasi,,baada ya sekunde kadhaa,,ukasikika mngurumo wa injini za meli,,na meli ikawaka,,,taa zote zikawaka,, na kuangaza kila kona ndani ya meli hiyo,,meli ikaanza kuondoka,,



    Roda akashtuka kutoka usingizini...akaangaza angaza macho yake huku na kule akaona abiria wote wameketi huku wengine wamesinzia...akajisemea moyoni..MUNGU WANGU..hii ndoto ina maana gani? sijawahi kuota mdoto ya kutisha kiasi hiki!!! akajipapasa mifukobi mwake kuangalia kifaa chake kinachomrahisishia kazi...katika shughuri zake za uandishi wa habari..

    akakiona kimo ndani ya mfuko wa koti alilokuwa amelivaa...akatazama upande wa nje kwa kupitia moja ya  dirisha la meli hiyo..akaona meli inaendelea na safari..



    Kumbe mambo yale yote yaliyotokea ilikuwa ni mdoto aliyoiota baada ya kuketi na kupitiwa usingizi ndani ya meli hiyo...

    akahisi kiu,,akanyanyuka na kuufuata  mgahawa uliokuwemo ndani ya meli hiyo maalumu kwa abiria...akanunua maji pia akaagiza chakula akaanza kula huku akichezea simu yake..

    alipo angaza macho yake,,kwa mbali akamuona mtoto mdogo wa kiume...mtoto huyo alifanana kila kitu,mpaka mavazi na yule mtoto aliyemuona kwenye ndoto....Roda akashtuka akajisemea moyoni,,"mmh! mbona nimeanza kuingiwa na wasiwasi!!! akanyanyuka haraka,,akazioiga hatua kumfuata mtoto huyo...akamuona anaelekea kwenye kiti kilichokuwa wazi,,na kando yake kulikuwa na Bibi kizee mmoja,, akamuona mtoto huyo akiongea na huyo Bibi  huku wakicheka na kufurahi,,mkononi alionekana kushikilia sahani iliyokuwa na chipsi kuku pamoja na chupa ya maji ikiwa nusu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akajisemea moyoni,"bila shaka huyo ni Bibi yake...au itakuwa nilimuona huyu mtoto kavla sijasinzia na ndio maana nimeota na kumfananisha!!

    Roda hakujali,akaamua kurudi kule ndani ya mgahawa ili aendelee kula chakula chake,,,alipoikaribia meza aliyokuwepo mwanzo akastaajabu..kutokuiona sahani iliyokuwa na chakula chake alichoagiza,,pia ile chupa ya maji aliyoiacha ikiwa na maji nusu haikuwepo!!!...akajisemea moyoni,,"jamani niliacha hapa juu ya meza hii sahani ikiwa na chipsi kuku. nani atakuwa kachukua chakula changu????

    wazo likamjia akajisemea moyon,,"huenda wahudumu wa mgahawa huu wamekiifadhi baada ya kuona nimeondoka,,wacha mikawaulize.

    akazipiga hatua kumfuata muhudumu mmojawapo kati ya wahudumu wa mgahawa huo akauliza,,"chakula changi nilikiacha kwenye meza ilepale!! nani kakitoa wakati mimi bado sijamaliza kula!!! yule muhudumu akaonekana kumshangaa Roda!!! kisha akasema,,"kwa kweli mimi sifahamu chochote kuhusu chakula chako...

    kaba hajamaliza kuongea sentensi hiyo..ghafla meli ikazimika...na baada ya sekunde kadhaa Nahodha akatangaza kwa kutumia kilaza sauti,,akisema,,"abiria wote tunaomba muwe wavumilivu,,mele imepata hitirafu..na muda si mrefu mafundi(mabaharia) wataitengeneza haraka iwezekanavyo....

    Roda akashtuka!! akazipiga hatua kutoka ndani ya mgahawa huo...alipoangaza macho yake kwenye kile kiti alichokuwa ameketi yule Bibi kizee pamoja na yule mtoto hakuwaona tena....



    Roda akaingiwa na wasiwasi....akazipiga hatua za haraka haraka akapanda ngazi kuelekea kwenye chumba maalumu cha Nahodha anayeiongoza meli hiyo...alipofika akafungua mlango wa chumba hicho bila ruhusa,,akaingia kwa pupa mlaka upande wa ndani!! Nahodha akashtuka akauliza kwa mshangao kulikoni? hiki ni chumba maalumu kwa ajili ya mtu anayeingoza meli ikiwa safarini,,haruhusiwi mtu yeyote kuingia bila ruhusa au kibali...kwani ,ulikuwa na shida gani?

    Roda akauliza,,"Jina lako unaitwa nani?

    Nahodha akamtazama Roda kwa macho ya mshangao,,akasita kwa sekunde kadhaa kisha akajibu,,"Mimi naitwa Sam.

    Roda akauliza kwa mshangao Yuve ni nani?

    Nahodha akasema,,"hakuna muhusika wa meli hii anayeitwa Yuve!!! labla jina lingine...

    Punde si punde akaingia mmoja kati ya mabaharia  ambaye ni fundi wa Meli hiyo...akamwambia Sam,,"kuna paipu moja imepasuka kule kwenye injini ya upande wa kushoto...

    Sam akasema,,"fanyeni uwezekano wa kuiziba ili tuendelee na safari.



    yule baharia akafungua mlango na kutoka nje,,akaelekea kwenye chemba za kushuka kule chini zilipokuwepo injini za meli hiyo..

    Roda akagisi kuchanganyikiwa akamtazama Sam ambaye ni nahodha wa Meli hiyo,,akataka kusema neno lakini akasita akafungua mlango na kutoka ndani ya chumba hicho. akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea sehemu ya abiria... kwa mbali akamuona yule mtoto wa kiume akiishilizia kwenye korido ya kuelekea kwenye vyoo vya Meli hiyo..Roda akaamua kumfuata mtoto huyo angalau amchunguze,,

    lakini Roda alipoifikia korido hiyo akaona mguu mmoja wa mtoto huyo ukiishilizia kuelekea katika chumba cha choo. 

    Roda akazipiga hatua za kunyatia kumfuata aone mtoto huyo anafanya nini!!!! alipokikaribia kwenye choo hicho.....akashtuka!! akahisi kuna mtu anamfatilia kwa nyuma....Roda akageuza shingo yake haraka ili atazame ni nani aliopo nyuma yake!! akamuona yule bibi kizee akiishilizia kwenye kina ya korido kuelekea kule sehemu ya abiria.....Rose akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,,"kwa nini kila nikiangaza macho yangu  namuona yule mtoto akiwa anaishilizia kukatisha kona...hata huyu bibi yake pia,,mmh!! bila shaka kuna jambo ambalo si la kawaida!!! Roda akaamua kuchungulia kwenye kile choo alichoingia yule mtoto... alipotazama kwa makini hakuona mtu ndani ya choo hicho!!

    akashtuka akajisemea moyoni,,"au sio chumba hiki!!? lakini mbona niliona anaingia humu?



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog