Search This Blog

SUNDI - 5

 







    Simulizi : Sundi

    Sehemu Ya Tano (5)





    asubuhi palipokucha akadamka mapema ,,,akaingia mitaani kumtafuta Mbigili,,lakini kila mtaa aliojaribu kutembelea hakufanikiwa kumpata Mbigili..

    aliendelea kumtafuta kwa masaa mengi pasipomafanikio yoyote ya kumpata Mbigili,,akaamua kurudi kule kwenye nyumba ya kulala wageni..

    wakati huohuo Mbigili alikuwa mule ndani ya mtaro anamolala sikuzote!

    masaa yalizidi kusonga hatimae giza likaanza kuingia,,

    Mbigili akatoka ndani ya mtaro huo kwenda kutafuta chakula...

    katika pitapita zake,,akapita ule mtaa,ilipokuwepo ile nyumba ya kulala wageni,,

    wakati huo huo akaonekana yule dereva akitokea ndani ya nyumba hiyo kuja upande wa nje....

    alipofika nje,,,kwa mbali akamuona Mbigili anakatiza eneo hilo,,akaamua kupaza sauti kumuita Mbigili,,,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbigili akashtuka kusikia mtu akimuita! akaamua kutimua mbio,,kwa kuhofia huenda ni yule baba yake mdogo na Anita...anataka kumkamata

    alikimbia na kutokomea kusikojulikana!

    yule dereva akaifuata ile njia ambayo mbigili kakimbilia!lakini hakufanikiwa kumuona Mbigili!

    akajisemea moyoni,,"anamaanisha nini kukikimbia! nikifanya uzembe nitakosa dau aliloniahidi bosi Apolo...dereva huyo hakukata tamaa akaamua kuingia mitaani kumtafuta huku akitembea kwa miguu!



    wakati huohuo alionekana Mbigili akiwa mtaani,,,akaizipiga hatua za harakaharaka pasipokujua ni wapi anaelekea!,,

    baada ya dakika kadhaa kupita akatokezea mtaa mwingine,,kumbe ndipo alipo dereva huyo,,,akakutana uso kwa uso na Mbigili!akataka kutimua mbio! dereva akasema,," usikimbie,,ninahabari njema kutoka kwa mdogo wako Apolo..

    Mbigili akaanza kuingiwa na amani baada ya kusikia maneno hayo!akazipiga hatua kumfuata dereva huyo,,,wakaamua kuelekea kwenye ile nyumba ya kulala wageni..

    wakiwa njiani Mbigili alikuwa anaongea mfululizo,,akimdadisi dereva huyo kujua Apolo kaongea nini...

    Dereva akasema,,"amesema amekutafuta kwa miaka kadhaa na hajui ni wapi ulipo! hivyo amesema ,,nihakikishe narudi na wewe Tanzania,,hataki uendelee kuishi huku!

    dereva huyo aliongea maneno hayo huku akimtazama Mbigili kwa macho ya huruma,,,kisha akauliza,,"mbona wewe upo katika hali hii wakati mdogo wako anapesa ni bilionea mkubwa kule Tanzania!

    Mbigili akajibu kwa kudanganya,,akasema nilifungwa gerezani,,hivyo ninasiku chache tangu nimetoka,,na hakuna mtu yeyote aliyekuwa anajua...

    dereva huyo akampigia simu Apolo ili ampe taarifa kuwa amempata Mbigili,,



    upande mwingine kule nyumbani kwa Apolo akafurahi sana kusikia taarifa hiyo...akamwambia Anita kuwa kaka yake kapatikana,,,lakini Anita hakuwa na furaha kila muda alikumbuka lile tukio la Mbigili kujaribu kumbaka,,mbaya zaidi kumbe ni kaka wa Apolo ambaye ni mchumba wake,,,

    Jambo hilo,,lilimfanya akose furaha tangu ile siku aliyoambiwa kuwa Mbigili ni kaka wa Apolo....

    Apolo hakujali kuhusu zile taarifa za kutaka kumbaka Anita,,,yeye anachohitaji,,,kaka yake aishi kwa amani...na si kama chokoraa.



                          ****************************



    Asubuhi palipokucha,,Mbigili pamoja na yule dereva wakaianza safari ya kutoka kenya kurudi Tanzania....

    walipofika mpakani,,dereva akashuka na kwenda kufanya taratibu za kulipia mzigo alioubeba kwenye gari pamoja na watu waliokuwemo ndani ya gari,,,ni yeye na Mbiligi.

    alipomaliza kulipia mzigo ,,,akaambiwa ataje idadi ya watu na majina ya waliokuwemo ndani ya gari hilo..

    akataja jina lake,,,ikaandikwa risiti moja,,,alipotaja jina la Mbigili...yule muhusika akashtuka! akasita kuendelea kuandika,,,akasema,,"subiri kwa dakika kadhaa,,,aliongea maneno hayo huku akitoka nje,,,akaongea na simu,,

    punde si punde wakaonekana maaskari wakija eneo hilo wakasiamama mbele ya dereva huyo!

    kwa mbali mbigili aliona jambo hilo,,akagundua kuwa kuna hali ya hatari,,akashuka kutoka ndani ya gari,,,akajificha chini ya uvungu wa gari hilo!11

    yule dereva akastaajabu kuona kazungukwa na maaskari! alipoangaza angaza macho yake,,akaona,tangazo likiambatana na picha ya Mbigili,,tangazo hilo lilikuwa limebandikwa ukutani....macho yakamtoka!!!!!!



    wale maaskari wakaanza kumuhoji dereva huyo kuhusu habari za Mbigili!!

    dereva huyo akadanganya,,"nimekosea jina namaanisha mbido,,ni mfanyakazi mwenzangu katika kqmpuni ninayofanyia kazi.

    aliongea maneno hayo ya uwongo huku akijiamini kwa asilimia mia!

    wale maaskari wakatazamana kisha wakaondoka zao...risiti ikaandikwa Mbido..akapewa dereva huyo akazipiga hatua kulifuata gari....alipolikaribia akastaajabu kutokumuona Mbigili mule ndani ya gari!! akajisemea moyoni,, "ni bora amelitambua hilo mapema,,amejificha,,je? atakuwa ameenda wapi?

    bila shaka huyu ni mtu hatari sana,anatafutwa na maaskari,,pia kila kona naona matangazo yameambatana na picha yake!

    lakini pasipokumfikisha kwa bosi Apolo naukosa utajiri hivi hivi..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    derava huyo akafungua mlango akaingia ndani ya gari na kuliwasha gari hilo,,tayari kwa kuondoka!



    Upande mwingine kule nyumbani kwa Apolo,,,alionekana Anita,,akiwa kashikilia picha ambayo Apolo akiwa pamoja na Mbigili!! kwa sababu alikuwa anampenda sana Apolo,,akaamua kumsamehe Mbigili,,kwa ukatiri aliotaka kumfanyia kuleporini!

    akazipiga hatua kuifuata kabati akafungua droo ndogo akairudisha picha hiyo!



    Wakati huohuo,,alionekana Apolo akiwa katika ofisi yake...akachukua simu yake na kumpigia yule dereva,,lakini simu hiyo iliita pasipokupokelewa!

    kumbe wakati dereva huyo anaongea na we maaskari,,Mbigili aliona simu ya dereva huyo ikiwa katika droo ya gari hilo,,akaamua kuichukua na kutoka kinyemera ndani ya gari hilo akajificha chini ya uvungu wa gari hilo!

    Mbigili aliisikia simu hiyo inaita katika mfuko wake wa suruali,,lakini alishindwa kuipokea kwa sababu,,alikuwa kashikilia vyuma vilivyokuwa chini ya gari hilo,,hivyo akawa ananing'inia!



    dereva alizidi kuzipanga gia hatimae wakatoka kwenye mpaka wa kenya na kuingia eneo la Tanzania,,

    Mbigili aliendelea kushikilia vyuma hivyo kwa nguvu zake zote!

    gari liliendelea na safari huku dereva akizidi kuzipanga gia, likaenda kwa mwendo wa kasi!



    Ke chini ya gari simu iliendelea kuita ndani ya mfuko wa Mbigili,,lakini bado hakuweza kuipokea kwa sababu gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi,,,



    kwa mbali wakaonekana maaskari wa usalama wa barabarani(Trafk police)wakalisimamisha gari hilo kwa lengo la kuangalia vibari na ukaguzi mdogo!

    dereva huyo akasimamisha gari hilo!

    dereva akapunguza mwendo na kuliegesha gari hilo kushoto kando ya barabara!

    bila kuchelewa wale maaskari wakaanza kulikagua gari hilo...



    wakati huo huo,,Upande mwingine alionekana Apolo,,akiwa amejawa na jazba,,akasema,,"huyu dereva anamaana gani kutopokea simu yangu? amepatwa na tatizo gani?

    Apolo alijiuliza maswali hayo pasipo kulata majibu! akaamua kupiga tena simu,,



    Upande mwingine akaonekana Mbigili akiwa bado yupo kule chini ya gari!! akaachia mikono yake akachungulia,,akashtuka kuona maaskari!! wakiwa kando ya gari hilo wakilizunguka.

    akajisemea moyoni,,"sijui ninamkosi gani!! mbonq jambo likiisha linazuka lingine!? nisipokuwa makini nitaingia matatani!

    alijisemea maneno hayo huku akijivuta na kushikilia vyuma asionekane!,,punde si punde simu ikaita mfululizo!!!!!

    Mbigili akaingiwa na wasiwasi,,kwa sababu simu hiyo ilikuwa inatoa mlio kwa sauti kubwa!!!

    ghafla akaonekana askari mmoja akizioiga hatua kuja upande wa nyuma ya gari alipokaribia kwenye sehemu ya Magiudumu ya nyuma,,,akajikwaa kwenye kipande cha jiwe lililokuwa limeingia ardhini na kuchomoza kiasi upande wa juu ya ardhi,,kitabu alichokuwa amekishikilia kikadondoka chini!!! jirani kabisa na sehemu aliyokuwa amejificha Mbigili,,,

    Mbigili akashtuka!! alipokitazama kile kitabu akaona karatasi moja inamaandishi,,alafu kunapicha yake katika karatasi hiyo!

    hofu ikazidi kuongezeka! wakati anatahamaki, akamuona askari huyo aliyedondosha kitabu hicho anainama kwa lengo la kukiokota kitabu hicho!!!!ghafla ukasikika mlio wa simu inaita!!!!





    Kumbe mlio huo ulikuwa ni wa simu ya askari huyo!! akasita kuokota kitabu hicho,,akaingiza mkono wake katioa mfuko wa suruali aliyokuwa kaivaa,,akatoa simu na kuipokea,,

    Mbigili akapata nafasi ya kujisogeza kando kidogo na kujificha vyema,,



    baada ya sekunde kadhaa kupita,,ukaonekana mkono wa askari huyo akiokota kitabu,,na kuzipiga hatua kurudi upande wa mbele ya gari,,

    punde si punde gari likaruhusiwa liendelee na safari,,,

    wakati huo Mbigili alikuwa na hofu ya hali ya juu,,,alipoona gari linaondoka,,akaplshusha pumzi,,huku akiendelea kushikilia vyuma vilivyokuwa chini ya gari!



    ******************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine,,alionekana Apolo,,akiwa ndani ya gari lake,,akiliendesha kwa kasi,,, hatimae akafika nyumbani kwake,,

    akamkuta Anita akiwa tayari kaandaa chakula cha jioni,,,lakini Apolo alionekana kutokuwa na furaha,,,jambo hilo lilimstaajasha Anita,,,akauliza,,"mbona unaonekana kama hauna furaha?

    Apolo akamtazama Anita kisha akabaki kimya pasipo kujibu kitu chochote! akazipiga hatua kuelekea chumbani..

    Anita akabaki mdomo wazi!! akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu!

    "Bila sha kunajambo ambalo halijakaa sawa! huyu sio Apolo ninaemfahamu siku zote....au kakasirika baada ya kumwambia kuwa Mbigili alitaka kunibaka?

    Anita akajikuta anatokwa na machozi,,amjue nini cha kufanya!

    akaamua kuzipiga hatua kukifuata chumba chao cha kulala! akafungua mlango na kuingia upande wa ndani,,,akamkuta Apolo akiwa kasimama kando ya dirisha huku simu yake akiwa kaishikilia kwenye sikio,,,,ghafla.akairusha simu ukutani,,,na kuanza kufoka akiongea peke yake....akageuza shingo yake akakutanisha macho na Anita,,,,

    Anita akaingiwa na hofu! kwa sababu uso wa Apolo ulionesha kujawa na hasira!!!!

    Apolo akazipiga hatua na kutoka nje ya chumba hicho...huku akijisemea moyoni,,"yani huyu dereva anafikia hatua ya kunidharau mimi bosi wake,,nimepiga simu siku nzima,,, lakini hapokei,,,na sasahivi simu yake haipatikani hewani!



    Kule chumbani akaonekana Anita,,akiwa kaketi kitandani,,,ghafla akanyanyuka na kulifuata kabati,,akaanza kutoa nguo zake,,na kuziweka ndani ya begi,,,alipomaliza,,,,akachukua kalamu na karatasi,,akaandika ujumbe mzito,,,huku akijilaumu kwa nini alimwambia Apolo kuhusu Mbigili!

    alipomaliza kuandika ujumbe huo mzito...akachukua begi lake na kulivuruta kutoka nje ya chumba hicho!!!akaendelea kuzipiga hatua,,akatoka nje kabisa ya nyumba hiyo,,,akaangaza macho yake,,hakuliona gari la Apolo,,akagundua kuwa Apolo ameondoka! mbaya zaidi Apolo hakuongea jambo lolote na Anita,,hivyo Anita alikuwa katika wakati mgumu,,,akihisi huenda Apolo ameamua kumuacha,,

    Anita akalifuata geti na kutoka nje ya eneo la nyumba ya Apolo!!

    baada ya mwendo wa dakika kadhaa,,akatokezea barabara kuuu,,,akakodi taxi..impeleke kwenye hotel yoyote iliyopo karibu na uwanja wa ndege!!!



    baada ya nusu saa kupita Apolo akarudi nyumbani,,,akastaajabu kuona begi la Anita halipo ndani ya chumba hicho....akaingiwa na wasiwasi,,,akafungua kabati,,hakuona nguo hata moja ya Anita,,

    wakati anatahamaki,,akaona karatasi yenye maandishi,,ikiwa juu ya kitanda,,akaichukua karatasi hiyo na kuanza kuisoma!

    Ujumbe ulisomeka hivi,;

    nachukua nafasi hii,,kukwambia kuwa,,najua unahasira kuhusu kaka yako,,juu ya kitendo cha kutaka kunibaka!!!

    lakini sina budi kukutaarifu kuwa,,nimeamua kuondoka nyumbani kwako kwa sababu, unaonyesha huna Upndo thena kwangu! imefikia hatua nakuongelesha unaishia kunitazama kama kinyago,,na kunionyesha sura ya hasira!!!

    kwa sasa naelekea katika hotel yoyote iliyopo jirani na uwanja wa ndege,,ili kesho nirudi kwetu Kenya...kwa heri APOLO.

    macho yakamtoka Apolo baada ya kuwoma ujumbe huo...akahisi kuchanganyikiwa akatimua mbio akatoka nje ya nyumba akaingia ndani ya gari na kuliondosha kwa kasi kwenda kumtafuta Anita.



    Wakati huo huo,,alionekana Mbigili,,,bado akiwa ke chini ya gari,,,alitamani kutoka lakini alishindwa kwa sababu gari lilikuwa katika mwendo wa kasi,,,,Mbigili akahisi mikono yake inaishiwa nguvu,,kwa sababu kaning'inia kwa masaa mengi mfululizo..

    akajitahidi lakini akashindwa akajikuta anaachilia mikono yake,,,akadondoka chini ya gari hilo!...





    kwa bahati nzuri,,akadondokea katikati,,,katika sehemu ambayo hayakanyagi magurudumu ya gari hilo,,ikawa ndio ponapona yake.akasimama haraka,,,akaanza kupunga mkono,,ishara ya kutaka dereva huyo asimamishe gari,,,,

    Mbigili alifanya hivyo huku akipiga mayowe kwa saui kali,,



    yule dereva akahisi kaona mtu akiwa kasimama katikati ya barabara upande wa nyuma! alipotazama kwa makini kupitia kioo cha pembeni ya gari hilo,,akamuona mtu huyo akiendelea kupunga mkono wake huku akitimua mbio kulifuata gari hilo

    kwa nyuma!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akamtambua mtu huyo kuwa ni Mbigili! akaamua kupunguza mwendo na kuliegesha gari kando ya barabara!

    Punde si punde akaonekana Mbigili,,akiwa kalikaribia gari hilo!

    akafungua mlango na kuingia ndani ya gari!

    Dereva huyo akastaajabu sana akauliza kwa mshangao!,,"ulikuwa wapi? na umefikaje fikaje eneo hili!!?

    Mbigili akasema,,"nilijificha chini ya gari kwa kuning'inia lakini mikono ilichoka,,nilishindwa kutoka chini ya gari kwa sababu ulikuwa unaendewha gari kwa mwendo wa kasi....hata hivyo ni bahati kutoka nikiwa salama!

    tuachane na hayo ukiona duka lolote  simamisha gari!

    dereva huyo hakuongea jambo lolote ,,,aliendelea kumtazama Mbigili kwa macho ya mshangao!

    baada ya sekunde kadhaa kupita,,,dereva huyo akaliwasha gari na safari ikaendelea,,,

    kabla hawajafika mbali,,Mbigili akaona duka kando ya barabara akasema,,"simamisha gari, pia naomba shilingi Mia tano(500)

    Dereva huyo akadhani huenda Mbigili ni mvutaji wa sigara hivyo anahitaji pesa hiyo akanunue sigara! akatoa noti ya shilingi elfu mbili akamkabidhi Mbigili,,

    bila kuchelewa,, Mbigili akaipokea noti hiyo kisha akafungua mlango wa gari na kutoka nje!

    akazipiga hatua kulifuata duka...akanunua nyembe tatu kisha akarudi kwenye gari!

    akaanza kuyoa nywele zake pamoja na ndevu,,,baada ya dakika kadhaa akawa amemaliza kujinyoa kipara na ndevu zote!

    akabadika kabisa,,,ule muonekano wa Mbigili ukatoweka akawa na sura tofauti...akajitazama katika kioo cha gari akatabasamu,,kisha akajisemea moyoni,,"hakuna atakayenijua kwa urahisi!!!

    safari iliendelea hatimae wakaingia jijini Dar es salaam,,

    dereva akaliendesha gari hilo mpaka nyumbani kwa Apolo,,

    walipofika akaliegesha nje ya geti kisha akashuka kutoka ndani ya gari huku akiwa kaongozana na Mbigili....

    geti lilikuwa wazi,,wakaingia mpaka ndani ya uzio wa nyumba hiyo....pia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ulikuwa wazi!!

    wakazipiga hatua kuufuata mlango huo! wakaingia ndani ya nyumba wakiamini kunamtu ndani ya nyumba.

    Dereva akajipapasa mifukoni mwake,,kwa lengo la kutoa simu ampigie Apolo,,amtaarifu kuwa amemleta Mbigili...

    ghafla Mbigili akasema,,"ninayo simu yako...niliichukua ndani ya gari kabla hatujatoka mpakani, lakini imezimika..

    Mbigili aliongea maneno hayo huku akimpa simu dereva.

    Mbigili akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea upande wa vyumbani...akaita lakini hakuna mtu aliyeitikia.

    Dereva akaamua kumuaga Mbigili na kuondoka zake..

    masaa yalizidi kusonga,,lakini Apolo hakurudi nyumbani,,,

    Mbigili akaamua kukifuata chumba cha mdogo wake Apolo,,akafungua mlango na kuingia ndani,,,alipoangaza macho yake akaona kadi ya benki,,ambayo anaitumia Apolo kuhifadhi fedha zote za kampuni yake,,,

    Mbigili akaingiwa na tamaa akamua kuichukua kadi hiyo,,,akaiweka mfukoni mwake...kisha akatoka haraka ndani ya chumba hicho! akaelekea sebuleni akaketi kwenye sofa!

    Baada ya lisaa limoja akaonekana akiliegesha gari lake ndani ya uzio wa nyumba yake,,akashuka na kuzipiga hatua kuingia ndani ya nyumba!

    Alipofungua mlango akashtuka kumuona Mbigili!!! akamtambua ingawa Mbigili alikuwa anaonekana muonekano tofauti!

    Apolo akafurahi sana kumuona kaka yake kwa mara nyingine tena,,ni baada ya kupotezana kwa miaka kadhaa!!

    wakasalimiana kwa furaha!

    Apolo hakuona haja ya kumuuliza maswali kaka yake,,,,akasema,,"wacha nikapumzike,,,tutaongea kesho...

    Mbigili akajisemea moyoni,,"natamani pakuche mapema,,,lazima nihamishe pesa zote katika akaunti ya Apolo,,,huu neio utajiri wangu!! hakuna haja ya kumuuwa..

    Mbigili akazipiga hatua na kuingia chumbani kupumzika!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi lalipokucha,,Mbigili akadamka mapema,,,akaondoka zake,,,akaelekea katika benki anayoitumia Apolo kuhifadhi pesa zote za kampuni yake.

    Mbigili akahamisha pesa hizo na kuzituma katika akaunti ya Anita kule Kenya!kisha akarudi nyumbani pasipo Apolo kufahamu chochote! Mbigili aliamua kufanya hivyo,,akiamini Anita atamsamehe na kumpenda,,,hivyo itakuwa rahisi kummiliki,

    Mbigili alikuwa hajui chochote kuhusu mahusiano ya Apolo na Anita,,na hakufahamu kuwa Anita alikuwa anaishi katika nyumba hiyo na aliondoka siku ya jana kabla yeye hajafika hapo!



    Apolo akadamka akapiga simu ya Anita lakini haikupatikana hewani,,,,hivyo akaamini kuwa Anita ameshaondoka kurudi Kenya!

    kutokana na Msimamo wa Anita,,Apolo hakuwa na namna,,,akatafakari njia nyingine ya kumbembeleza Anita arudi!



    wakati huo huo alionekana Anita,,akiingia katika benki huko kenya kwa lengo la kuto kiasi cha fedha katika akaunti yake ya benki..

    akastaajabu kukuta akaunti yake inamabilioni ya pesa...alipojaribu kufatilia akaona pesa hizo zimetumwa kutoka katika akaunti ya Apolo!!!!!

    macho yakamtoka Anita! akaona ni kama ndoto,, akaamua kumpigia simu Apolo lakini kila akipiga simu haipatikani hewani.

    alijaribu kwa siku kadhaa lakini simu ya Apolo haikupatikana!



    siku zilizidi kusonga,,Apolo hakufahamu chochote kuwa pesa zake zote zimehamishwa kutoka katika Akaunti yake!

    siku ya leo akaamua kwenda benki kutuma pesa katika kampuni ya magari huko china,,kwa lengo la kuagiza magari kumi mapya..kwa ajili ya kampuni yake!!

    lakini akaambiwa akaunti yake haina hata shilingi!

    alipofatilia,,akagundua pesa hizo zimehamishiwa katika akaunti ya Anita!!

    macho yakamtoka!!!akahisi kuchanganyikiwa!! akajisemea moyoni,,"ANITA umeamua kuniibia pesa zote! siamini,,

    lakini kila akivuta kumbukumbu,,,hakuna mtu anayejua namba ya siri ya akaunti yake zaidi ya kaka yake Mbigili!!

    lakini kinachomtatiza zaidi,,pesa hizo zimehamishwa Baada ya Anita kuondoka,,,na kilichomfanya amtilie mashaka Anita,,kwa nini Anita aliondoka na kuacha ujumbe,,kwa nini asingemsubiri arudi ili amuage!!

    "Bila shaka Anita ndiye kaiba pesa hizo" alijisemea Apolo!



    akarudi nyumbani huku akiwa kama kachanganyikiwa!!

    Mbigili akajifanya hajui kilichotokea,,akabaki kimya huku akimuuliza Apolo maswali ya kizushi...



    Kesho yake,,majira ya saa mbili za usiku,!!! alionekana Apolo akiwa na Mbigili wameketi sebuleni,,Apolo alimsimulia kaka yake kuhusu upotevu wa pesa katika akauti yake ya benki.hafla geti likagongwa!

    Apolo akaamua kutoka nje ya nyumba kwenda kutazama ni nani anayegonga geti! alipofungua geti akamuona Anita!

    Apolo akashtuka akabaki kimya huku akimtazama Anita kwa macho ya msisitizo!



    kule ndani ya nyumba akaonekana Mbigili naye akitoka na kuelekea upande wa nje ya nyumba,,alipoangaza macho yake akashtuka kumuona Anita akiwa na Apolo! pale getini...macho yakamtoka!!!akahisi kuchanganyikiwa!!! kutokana na mshtuko,,akili za Mbigili zikaruka,,akawa kichaa ghafla akaanza kucheka peke yake akavua nguo zote,, akatimua mbio na kutoka nje ya uzio wa nyumba hiyo,,,kabla hajafika mbali akagongwa na pikipiki,,,akafa papohapo!

    Apolo na Anita walishuhudia jambo hilo,,,kikweli ulikuwa ni msiba mkubwa kwa Apolo...

    Aniita akamuuliza Apolo,,"mbona umenitumia pesa nyingi kiasi hiki!

    Apolo akashtuka,,,akaingiwa na wazo akasema,,"sasa nimefahamu ukweli wa jambo hili,,,huyu ni JUMBE ndiye kafanya hivi,,,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kesho yake taratibu za mazishi zikafanyika Mbigili akazikwa!kisha Apolo akamsimulia Anita kilichotokea,,kuhusu pesa hizo kuhqmishwa katika akaunti yake.

    Anita akarudisha fedha hizo katika akaunti ya Apolo,,,na baada ya mwezi mmoja kupita wakafunga ndoa...

    Apolo na Anita wakaishi kwa amani, wakabahatika kupata watoto wawili...na misha ya Apolo na Anita yakawa mfano wa kuigwa.



                         *******MWISHO**********



0 comments:

Post a Comment

Blog