Simulizi : Jina La Urithi
Sehemu Ya Tano (5)
upande mwingine ulionekana mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula, mzimu huo ulikuwa ndani ya umbile la mtoto Laula....ukitazama kwa harakaharaka huwezi kutambua kuwa kunamzimu ndani ya mwili wa mtoto .
Laula akazipiga hatua na kuingia katikati ya mji..
wakati huohuo kule kijijini ,,mvua iliendelea kunyesha,,wanakijiji waliendelea kuhofia maisha yao,,,ilinyesha mfululizo takribani dakika tano mfululizo...ghafla ikaacha kunyesha,,ukimya ukatawala kila mmoja alimtazama mwenzake usoni kwa macho ya uwoga
Jogolo pia hakuamini kilichotokea. akajisemea moyoni,,"laiti kama mvua isingenyesha ningekuwa marehemu sasahivi!
Jogolo aliongea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu....Jogolo akasema,,"kunajambo nataka niwaeleze,,,dawa hii tayari imeshaharibika...kwa sababu imenyeshewa na mvua,,hivyo kunajambo mbadala lahitajika lifanyike haraka iwezekanavyo.
wanakijiji waliendelea kubaki kimya,,hakuna aliyethubutu hata kufungua mdomo wake kuongea jambo ama kuuliza swali lolote.
Jogolo akasema,,"usiku wa leo nitafanya jambo fulani,,lakini jambo hilo litafanyika makaburini,,ni lazima kaburi la muanzilishi wa ukoo wa Laula lifukuliwe.
Wakati huo huo upande mwingine alionekana Laula akizipiga hatua kuifuata barabara ya vumbi,,,barabara hiyo ilikuwa na kilima kiasi....alitembea mfululizo kwa mwendo wa saa nzima,,,ghafla akaona njia panda! akaangaza macho yake kuzitazama njia hizo mbili.....akaamua kuifuata njia moja akazipiga hatua kadhaa kisha akatoweka kimiujiza!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilipofika nyakati za usiku wa manane...akaonekana Jogolo akiwa makaburini,,tayari kuianza kazi ya kufukua kabuti la muanzilishi wa ukoo wa Laula..
bila kuchelewa akaanza kulifukua kaburi hilo....na baada ya dakika kadhaa akawa amemaliza kulifukua na kutoa udongo wote ndani ya kaburi hilo,,,akafanikiwa kuona baadhi ya mifupa ya muanzilishi wa ukoo wa Laula...akachukua fuvu la kichwa pamoja na mfupa mmoja wa uti wa mgongo..kisha akatoka ndani ya kaburi hilo kimiujiza...na kaburi likajifukia lenyewe...
Jogolo akatoweka kimiujiza,,akajitokeza kule kijijini....mbiu ikapigwa,,wanqkijiji wote wakatoka kwenye majumba yao,,wakakusanyika sehemu moja....
Jogo akasema uwashwe moto mkubwa kwa ajili ya kuianza kazi ya kuangamiza ule mzimu....
ndani ya dakika kadhaa zikakusanywa kuni nyingi,,na moto ukawashwa....
Jogolo akausogelea moto huo akiwa kashikilia lile fuvu pamoja na mfupa wa uti wa mgongo....akavirusha ndani ya moto huo,,,kisha akachukua kisu akajitoboa kwenye mkono wake,,akanyunyizia damu yake kwenye moto huo,,kisha akazipiga hatua kadhaa kurudi nyuma.
ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa....wakisubiri kuona nini kitandelea....
punde si punde,,,ule moto ukazimika,,giza totoro likatawala! wanakijiji wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,kwa mbali ukaonekana mwanga ukitokea upande mwingine kuja ule upande walipokuwa wamekusanyika wanakijiji....wakati wanatahamaki mara ghafla. akaanza kudondoka mwanakijiji mmoja baada ya mwingine...jambo hilo lilizua taharuki!!! wanakijiji wakaanza kupiga kelele....Jogolo akafungua mdomo wake kufanya jambo flani,,,huenda ikasaidia......kisha akachukua mchanga na kuuweka mdomoni....akatema mchanga huo na kuurusha ule upande unapotokea ule mwanga!!! mara ghafla!!!''
PATASHIKA!
Ule mwanga ukatoweka kimiujiza!mganga Jogolo akashtuka,,,hata wanakijiji wote wakaingiwa na hofu kupita kiasi....kila mmoja alitimua mbio na kupita njia yake,,,akabaki mganga peke yake akiwa kasimama hapo hapo.
punde si punde ule mzimu ukajitokeza kimiujiza,,,sauti ikasikika ikitokea kinywani mwa mzimu ikisema,,,hakuna atakayebaki hai....mimi ndiye Laula,,,,
wakati sauti hiyo ikiendelea kusikika masikioni mwa mganga,,ghafla wazo likamjia mganga,,akajisemea moyoni,,yanipasa nifanye jambo haraka iwezekanavyo.
akatoweka kimiujiza na kujitokeza kule makaburini katika kaburi la muanzilishi wa ukoo wa Laula...akastaajabu kukuta kaburi hilo limepasuka na hakuna hata chembe ya mabaki ya maiti ya Laula
upande mwingine kule kijijini walionekana wanakijiji wakiendelea kutimua mbio na kutokomea kabisa kuingia kijiji cha jirani....baada ya dakika kadhaa kupita ukimya ulitawala katika kijiji hicho,,,hapakuonekana dalili ya mtu yoyote kuonekana akirandaranda katika kijiji hicho......
kwa mbali ukaonekana ule mzimu ukijitokeza tena kwa mara ya pili katika anga la kijiji hicho....ghafla kijiji kikabadilika na kuwa mapango ya kutisha! utadhani hapakuwahi kuwepo kijiji hapo mwanzo!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huo huo kule makaburini alionekana mganga akijaribu kufanya jambo kuurudisha mzimu ndani ya kaburi,,na usiendelee kufanya madhara....
akaonekana akinyoosha mkono wake ukajitokeza moto wenye rangi nyingi ,,,moto huo ulidumu mikononi mwa mganga ndani ya dakika kadhaa kisha ukatoweka kimiujiza!mganga akainua uso wake kutazama juu ya anga ,,,punde si punde ukaonekana mkuki ukiwa umefungwa kitambaa chekundu,mkuki huo ulishuka moja kwa moja mpaka kando ya mganga! akauchukua na kuurusha juu kwa nguvu zake zote,
wakati huohuo kule kijijini ulionekana ule mzimu bado ukiwa umesimama katikati ya kijiji ambacho kwa sasa kinaonekana ni mapango ya kutisha
ule mkuki uliorushwa na mganga ukaenda moja kwa moja mpaka kwenye paji la uso la mzimu huo,,ikasikika sauti ya mngurumo wa kutisha ghafla ukazuka moshi mkubwa na mzimu ukateketea kwa moto huo,,
baada ya sekunde kadhaa kikaonekana kivuli kikiruka angani na kutokomea kabisa,,punde si punde mtoto Laula akaonekana kalala chini akiwa uchi wa mnyama,,wakati huo alikuwa kapoteza fahamu!
kule makaburini alionekana mganga Jogolo akiwa akainamisha uso wake chini huku mikono yake ikiwa imeshika macho yake huku akipiga kelele kwa sauti kali,,,kando yake likaonekana kaburi la Laula likijifunga taratibu,,mganga Jogolo aliendelea kupiga kelele mfululizo,,akiashilia maumivu makali kwenye macho yake!
maumivu hayo yaliendelea kuongezeka sasahivi akaanza kuhisi mwili wake unaishiwa nguvu! akadondoka chini,, povu lililochanganyikana na damu likaanza kumtoka mdomoni! baada ya sekunde kadhaa kupita akapoteza maisha...
upande mwingine kule kijijini yale mapango ya kutisha yakatoweka kimiujiza na nyumba zikarudi kama mwanzo zilivyokuwa,,
Kwa mbali akaonekana mtoto Laula akizinduka,,ni baada ya fahamu kurejea! akashtuka kujikuta kalala chini,,akiwa uchi wa mnyama! alipojaribu kuvuta kumbukumbu,,,hakuweza kukumbuka kitu chochote,,hata jina lake hakulifahamu,,,akabaki anajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu....lakini alipojaribu kuangaza angaza macho yake akahisi hiyo sehemu alishawahi kuiona,,lakini hakumbuki ni wapi!
akanyanyuka huku mikono yake ikiwa imeziba vyema nyeti zake....akazioiga hatua za haraka haraka,,,kwa mbali akaona nguo zimeanikwa nje,juu ya kamba! akazifuata akachukua pasiporuhusa,,akavaa nguo hizo na kutimua mbio,,,akajikuta katokezea kwenye barabara kubwa,,akaifuata barabara hiyo.....alitembea kwa masaa mengi mfululizo hatimae jua likazama! hakukata tamaa aliendelea kutembea,,, kwa mbali akaona nyumba nyingi,,,akaamua kuelekea upande huo.....akajikuta ametokezea mjini....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************
Baada ya siku saba kupita,,wanakijiji waliamua kurudi katika kijiji chao,lakini bado walikuwa na hofu kubwa! kila mwanakijiji alirudi katika nyumba yake na maisha yakaendelea,,
Upande mwingine kule mjini,,alionekana mtoto Laula akiwa kaketi kando ya gereji ya kutengenezea magari mabovu... akaonekana mwanaume mmoja wa makamo akimfuata Laula na kuanza kumuhoji,,"hujambo kijana?
Laula akasema,, "sijambo.
yule mwanaume akauliza,,''unafanya nini hapa? nimekuona umeketi kwa masaa mengi mfululizo,,
Laula hakujibu kitu,,akabaki kimya,,
yule mwanaume akauliza unaitwa nani?
Laula akabaki kimya,, huku macho yake yakimtazama mwanaume huyo!
kisha akajibu,,"sikumbuki jina langu!
yule mwanaume akamtazama Laula kwa macho ya mshangao! akaingiwa na huruma kwa sababu Laula alionesha sura ya majonzi..akaamua kutoa noti ya shilingi elfu mbili akamkabidhi Laula kisha akasema,,nenda katafute chakula!
Laula akaipokea noti hiyo...yule mwanaume akaondoka zake...
Kumbe wakati anwtoa pesa mfukuni,,alidondosha karatasi ndogo iliyokunjwa,,karatasi hiyo ilikuwa na kumbukumbu ya pesa ambazo anatakiwa alipwe yule mwanaume! pasipokuwa na karatasi hiyo basi atapoteza haki yake ya malipo!
Laula akaokota karatasi hiyo na kuiweka mfukoni! akaondoka zake kwenda kutafuata chakula kisha akarudi kando ya gereji hiyo.....ilipofika nyakati za jioni,,akamuona yule fundi akiwa anatoka gereji huku machozi yakimtoka,,Laula akaamua kumfuata mwanaume huyo akamuuliza mbona unalia?
yule mwanaume akamtazama Laula kwa macho ya majonzi kisha akajibu,,nimepoteza kitu muhimu sana na sijui nitakipata wapi!
kabla hajaongea neno lingine,,,,Laula akasema,,"niliamua kurudi hapa muda wote nakusubiri,,nikupe karatasi uliyoidondosha wakati unanipa pesa!
Laula aliongea maneno hayo huku akiingiza mkono wake mfukoni akaitoa karatasi na kumkabidhi mwanaume huyo.....
yule mwanaume akafurahi sana,,akasema,,asante sana, mimi ni fundi wa kutengeneza magari unaonaje nikikufundisha ufundi?
Laula akakubali kisha akasema,,"mimi sina mahala pa kuishi...yule mwanaume akaamua kumchukua Laula na kuishinae nyumbani kwake...akaamua kumpa jina akamuita ASANTE.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****BAADA YA MIAKA KUMI KUPITA****
asante akawa fundi hodari,,,hatimae akafungua gereji yake mwenyewe,,akawa na maisha mazuri mpaka leo.
_____ MWISHO________
0 comments:
Post a Comment