Search This Blog

KOTI JEUSI - 2

 







    Simulizi : Koti Jeusi

    Sehemu Ya Pili (2)



    wakati huohuo kule kwenye kambi ya jeshi,, alionekana mkuu wa jeshi akijihami kwa kujiwekea ulinzi mkali popote aendako.... lakini moyoni alikuwa na majonzi akiamini kuwa familia yake imeangamizwa!!..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya lisaa limoja kupita,, kule porini alionekana mke wa kuu wa jeshi akizinduka fahamu zikarejea.. akastaajabu kujikuta kaketi ndani ya gari,,, akajisemea moyoni,, "huku ni wapi?  na nimefikaje huku? alipogeuza shingo yake akashtuka kuona watoto wakowa wamejilaza kwenye viti vya upande wa nyuma!! kutokana na ile sindano aliyochomwa na Bakari... ubongo wake ulifuta kumbukumbu zote akawa kama kazaliwa leo,,,hakuwatambua watoto hao kuwa ni watoto wake!  akajisemea moyoni,, "watoto hawa wanafanya nini hapa?

    wakati anajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu!!  wale watoto Wakazinduka na kupata fahamu,,, kila mmoja akastaajabu kumuona mwenzake,,, yani utadhani hawajuani wala hawajawahi kuonana!!!!  pia watoto hao walimshangaa mama yao... wakauliza,, "wewe ni nani?? 

    Mke wa mkuu wa jeshi akabaki mdomo wazi huku akiendelea kuwashangaa watoto hao,,, akakosa neno la kuongea akabaki kimya huku akijaribu kuvuta kumbukumbu huenda akakumbuka kitu chochote,,lakini alipojaribu kuvuta kumbukumbu hakukumbuka kitu chochote! akaamua kuliwasha gari hilo na kuliondoa gari pasipokujua ni wapi anaelekea!



                              **********************************



    Siku zilizidi kusonga,,, mambo yakawa magumu kwa upande wa mkuu wa jeshi,,,

    siku ya leo akiwa ndani ya ofisi yake akaonekana akiwa kwenye dimbwi zito la mawazo!  akaamua kutoka nje ya ofisi yake akazipiga hatua kulifuata gari lake... huku akilindwa na ulinzi mkali! alipofungua mlango wa gari.. akashtuka kukuta koti jeusi limewekwa juu ya kiti cha upande wa dereva!

    koti hilo linafanana na yale makoti yanayokutwa kwenye tukio la mauwaji! wakati anatahamaki,,  ikasikika simu ikiita ndani ya gari lake!  akashtuka. akajipapasa mifukonibmwake akaiona simu yake.. lakini mlio wa simu uliendelea kuita ndani ya gari. Punde si punde,, mara ghafla!!!!!!

                   

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ukasikika mlio wa risasi ukitokea nje ya kambi hiyo. ....mkuu wa jeshi akaamuru baadhi ya wanajeshi waende kutazama nini kimetokea huko nje ya uzio wa kambi ya jeshi!..

    bila kuchelewa wanajeshi hao wakatimua mbio kutoka nje ya uzio wa kambi ya jeshi huku wamebeba silaha za moto... walipofika kule nje wakashtuka kumuona afisa wa jeshi akiwa kauwawa ndani ya gari lake kapigwa risasi ya kichwa kwenye paji la uso.... huku mwili wake umefunikwa kwa koti jeusi!

    taarifa hiyo ilizidi kumuogopesha mkuu wa jeshi...

    akaamua kuandaa mpango madhubuti....akaamuru mtu yeyote atakayeonekana kavaa koti jeusi auwawe papohapo!!!

    Raia wasiokuwa na hatia waliuwawa kwa wingi,, watu wakaogopa kuvaa makoti meusi.. yakatoweka kabisa nchini.....

    hali ikawa shwari...kwa kipimdi cha mwaka mmoja.... mkuu wa jeshi akajipa matumaini kuwa miongoni mwa watu waliuwawa kwa amri aliyoitoa bila shaka muuwaji aliyekuwa akisababisha mauwaji na kufunika maiti kwa koti jeusi naye aliuwawa!!!! na ndio sababu sasahivi hakuna matukio ya mauwaji kama mwanzo.

    kumbe hakujua kuwa Muuwaji bado yupo hai! mbaya zaidi hakuna tetetsi zozote za kuinekana sura yake, hivyo hakuna aliyemfahamu!



                    **************************



    Ulande mwingine alionekana Bakari akiwa kaketi ndani ya chumba cha hotel akiandaa mpango wa kusafiri kuelekea SouthAfrica(Afrika ya kusini)  akanyanyuka kwenye kiti akafunua godoro akatoa daftari pamoja na kalamu...

    daftari hilo lilikuwa kubwa kiasi lilikuwa na picha za maafisa pamoja na viongozi wa serikarini wote aliowauwa,, ni wale wanaojihusisha na bihashara aramu ya kuuza siraha kinyume na sheria,, uingizaji wa madawa ya kevya,, pamoja na kushirikiana na majasusi....

    baada ya wikioja kupita Bakari akasafiri kuekea Afrika ya kusini.



                       ************************



    Upande mwingine alionekana mke wa Mkuu wa Jeshi akiwa katika nyumba ambayo inaonekana haijamalizika ujenzi huko bagamoyo.. aliishi hapo kwa kipindi cha mwaka mzima akiwa na wale watoto......ubongo wake haukumbuki tukio lolote hata hao watoto anawalea lakini hajui kama ni wakwake... hata jina lake halikumbuki!!!!  mwanamke huyo aitwa Johari.. alikuwa akiishi kwa kuombaomba msaada wa pesa na chakula barabarani wakati mwingine hupita kwenye maduka na kuomba msaada wa chakula!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya wiki moja kupita,, alionekana mwanaume mmoja mtanashati akitokea kwenye kiwanja cha ndege(Airport) mwanaume huyo.. akaonekana akionyesha hati ya kusafiria(passport) kisha akatoka nje kabisa ya uwanja wa ndege..

    akakodi taxi impeleke MID HOTEL buguruni.

    alipofika akalipia chumba pesa ya mwezi mzima yeye kuwepo ndani ya hotel hiyo!!! akaketi kwenye sofa kisha akafungua begi lake akatoa picha mbili.

    picha moja ilionekana anepiga na familia yake mke na watoto wake watatu... akanyanyuka na kukisogelea kioo.. akajitazama kwenye kioo hicho  kisha akaitazama ile picha ambayo kapiga peke yake.

    kumbe ni Bakari!!! alikwenda Afrika ya kusini kubadilisha muonekano wa sura yake kw akufanyiwa upasuaji na kubadilishwa ngozi ya uso wake.. akaonekana ni mtu mwingine kabisa tofauti na Bakari....

    kisha akajisemea moyoni,, "sasa nitaifanya kazi yangu kuwaangamiza wote waliosalia,,,

    kwa uhuru...akanunua sanduku la zawadi...lililokuwa limenakshiwa kwa mapambo ya kuvutia.... akaweka koti jeusi ndani yake... kisha akatoka nje hotel hiyo akakodi taxi... akamuamuru dereva aliegeshe gari hilo kando kabisa ya kambi  ya Jeshi. 

    kisha akaitazama saa yake ya mkononi.. akajisemea,," huu ndio muda wake wa kutoka,, naamisasahivi atakuwa ameshasahau pia anaamini kuwa muuwaji ameshauwawa!

    wakati anawaza hayo,, punde si punde likaonekana gari la mkuu wa jeshi likitokea ndani ya kambi ya jeshi.....

    Bakari akamuamuru dereva alifuate gari hilo kwa umbali wa mita ishirini....

    mkuu wa jeshi akaonekana akiliegesha gari lake na kuingia kwenye jengo moja la hotel... kukutana na wenzake anaoshirikiana nao kwenye bihashara haramu!

    Bakari akaahuka kutoka ndani ya taxi,, akamlila dereva huyo kisha akazipiga hatua huku kabeba mfuko mweusi uliokuwa na sanduku dogo la zawadi akalifuata gari la mkuu wa jeshi.. alipolikaribia akaangaza angaza macho yake huku na kule kisha akaingiza mkono mfukoni mwake akatoa ufunguo wa bandia.. akafungua mlango wa gari akaweka sanduku hilo kwenye kiti cha dereva kisha akafunga mlango wa gari hilo na kuondoka zake.....

    baada ya nusu saa kupita akaonekana mkuu wa jeshi.. akitokea ndani ya jengo la hotel hiyo,, akazipiga hatua kulifuata gari lake.



                   

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akastaajabu kukuta box la zawadi!akasita kulifungua box hilo, akatimua mbio akasimama kando akihisi huenda ni bomu! akatoa  simu yake akapiga simu kwenye kambi ya jeshi,,akaamuru baadhi ya wanajeshi waje haraka,,na mtambo maalumu wa kukagiua bomu....ndani ya dakika kadhaa wanajeshi wakafika eneo hilo wakakagua box hilo...lakini ikagaundulika kuwa hakuna bomu ndani yake! mkuu wa jeshi akaamuru box hilo lifunguliwe muda huo huo,,,

    bila kuchelewa amri ya mkuu wa jeshi ikatekelezwa! box likafunguliwa macho yakamtoka mkuu wa jeshi baada ya kuona zawadi ya koti jeusi.ndani box hilo!

    akajisemea moyo,,"haaaa! inamaana huyu muuwaji bado yupo hai?hili ni tatizo...



    wakati huo huo,upande mwingine alionekana mke wa mkuu wa jeshi akiwa mitaani akiomba msaada kwenye maduka yaliyopo kando ya barabara....

    kwa kmbali likaonekana basi la abiria likiingia ndani ya kituo cha mabasi ya abiria....akaonekana Bakari akishuka kutoka ndani ya basi ilo akaiwa kabeba begi dogo la mgongoni! akazipiga hatua kutoka kwenye kituo hicho cha mabasi...alipoangaza angaza macho yake akamuona mke wa mkuu wajeshi akiwa kaongozana na wale watototo wanne,,,ambao ni watototo wake wa kuwazaa mwenyewe! lakini hana kumbukumbu yoyote kuhusu watoto hao kama ni wa kwake,,,hata pia watoto hao hawana kumbukumbu kuwa huyo ni mama yao mzazi...kutokana na ile sindano waliyo chomwa,pasipo wenyewe kujijua!

    Bakari akamfuata mwanamke huyo,,alipomkaribia akamuita na kumwambia atamsaidia hivyo amchukue yeye pamoja na wale watoto wanne akaishi nao.

    mke wa mkuu wa jeshi akakubali....Bakari akawachukua na kutafuta nyumba ya kulala wageni,,,akalipia vyumba na kuwahifadhi hapo kwa muda wa wiki moja,,pia akalipia chakula,,

    yeye akarudi Dar es salaaamu kwenda kutafuta nyumba....akafanikiwa kupata,,,watu walimshangaa sana Bakari kwa sababu alikuwa na pesa lakini haaijulikani anafanya kazi gani?

    kumbe safari yake ya kwenda huko bagamoyo ilikuwa ni kwa lengo la kumtafuta mwanamke huyo pamoja na wale watoto wanne.....



    Bakari alibaki Dar es salaam kwa muda wa siku mbili akanunua nyumba akaweka kila kitu ndani ya nyumba hiyo.....na siku iliyofuata,Bakari akasafiri kurudi bagamoyo,kumfuata mke wa mkuu wa jeshi..akafika mpaka kwenye ile nyumba ya kulala wageni,,

    kesho yake safari ikaanza ya kurudi Dar es salaam.......wakafikia kwenye ile nyumba aliyonunua Bakari,,,,



            **********************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    siku zilizidi kusonga,,maisha yakaendelea,,amani ikatawala kwenye nyumba ya Bakari,,,,kutokana na ukarimu alioufanya Bakari,,,mke wa mkuu wa jeshi aitwae LINDA..akajikuta  anaanza kumpenda Bakari! akashindwa kujizuia akaamua kumuonyesha hisia zake ilimradi atambue kuwa anampenda!

    Bakari akajikuta yupo kwenye wakati mgumu,,kwa sababu yeye hayupo kimapenzi zaidi!nia na lengo lake ni kuikamilisha kazi aliyokusudia kuifanya! ya kumuangamiza mkuu wa jeshi.,

    siku zilizidi kusonga hatimae Bakari akajikuta anashawishika na penzi la Linda! akajikuta anazama kwenye dimbwi la penzi zito juu ya Linda!

    baada ya miaka miwili kupita Linda akashika ujauzito....akajifungua mtoto wa kiume,,maisha yakaendelea na amani ikatawala ndani ya nyumba lakini Linda alijitahidi kumdadisi Bakari ili Bakari amwambie kazi anayoifanya,,kumuingizia kipato,,lakini Bakari alijibu kwa kudanganya kuwa ni mfanya bihashara,,,huwa anasafiri kwenda nchi za nje kufuata bidhaa na kuzileta nchini,,kuziuza....

    kwa sababu mara kwa mara Bakari anasafiri ,,,na Bakari akimuaga Linda kuwa anasafiri,,basi kesho yake,,lazima vyombo vya habari vitangaze tukio la mauwaji,,,tena safari hii,,muuwaji alikuwa akifanya tukio la mauwaji,,,anaacha kipande kilichochanwa kwenye koti jeusi!.



                                      ****************BAADA YA MIAKA ISHIRINI KUPITA************



    Wale watoto wanne wakakuwa ,,,kwa sasa wanatimiza umri wa miaka ishirini na kadhaa..isipokuwa yule mtoto mdogo wa mwisho ndiye alikuwa anatimiza miaka ishirini kamili!

    Bakari aliwafundisha mbinu mbalimbali za kupigana na kujihami mbele ya adui,watoto hao,,ambao kwa sasa ni vijana wakubwa wakawa ni moto wa kuotea mbali!

    kwa kipindi cha miaka hiyo yote Linda hakufahamu kazi ya Bakari...hivyo aliamini kuwa Bakari ni mfanya bihashara.



    upande mwingine alionekana mkuu wa jeshi akiwa kambini akiandaa mpango wa upelelezi ,,ili wamnase muuwaji anayefanya mauwaji kwa kipindi cha miaka hiyo yote lake,,akamatwe haraka.

    mpango huo ulikuwa ni siri hakutaka kumshirikisha mwanajeshi hata mmoja!...taakatafuta mtu wa kumuangamiza muuwaji,,,akafanikiwa kumpata kijana mmoja aliyeonekana akishuka kutoka ndani ya gari..kavalia suti nyeusi na miwani nyeusi!             





    ****************

    ***************************

    ***************************************







    mwanajeshi mmoja akilifuata gari hilo akaingia na kuliwasha,,,akaliendesha kwa mwendo wa wastani ,,alipokuwa akiliingiza ndani ya geti la kambi hiyo!

    Solo akalitambua gari hilo vyema,,kuwa hajalifananisha bali ni gari la yumbani kwao,wadogo zake wanapenda kulitumia mara kwa mara!

    macho yakamtoka!akajisemea moyoni inamaana ndugu zangu wako wapi!? isije kuwa wameuwawa na mkuu wa jeshi,,kwa sababu nimesikia akisema,,"zichukuliwe maiti na kwenda kuzikwa porini!wakati anajiuliza maswali hayo ghafla wazo likamjia!akatoa simu yake katika mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa!



    Alipoitazama simu yake.. akaona namba ya Bakari,, ndeye anampigia!  Solo akaipokea simu hiyo!!  Bakari akauliza upo wapi?

    Solo akajibu kwa kudanganya kuwa mjini! kwenye mizunguko yake!

    kumbe Bakari,,anajua ni wapi Solo alipo!!  na mawasiliano yote kwenye simu ya Solo,, alikuwa anayanasa kupitia ule mtambo wake maalumu!!  GPS TRACKER! ,,Solo hakulitambua hilo.

    Bakari akakata simu..

    Punde si punde mkuu wa jesshi akampigia simu Solo na kumwambia kuwa aingie ndani ya kambi ya jeshi! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kuchelewa Solo akazipiga hatua za kikakamavu akalifuata geti la kuingilia ndani ya kambi!!!

    alipofika getini,, akajitambulisha,, kuwa yeye ni mgeni wa mkuu wa jeshi,,wale walinzi waliokuwa zamu kulinda siku hiyo.. wakapiga simu kwa mkuu wa jeshi kuthibitisha ujio wa Solo!

    mkuu wa jeshi akaamuru Solo aruhusiwe kuingia ndani ya kambi!

    wakaonekana wanajeshi wawili wakimfuata Solo na kumpeleka kwenye ofisi ya mkuu wa jeshi!!

    alipofika akauliza,, "je naweza kuoata picha inayoonyesha sura ya muuwaji,, ambaye natakiwa kumuangamiza?

    mkuu wa jeshi akasema,, "hata miminpia siifahamu sura ya muuwa huyo!  lakini naamini kuwa unaweza kumnasa na kumuangamiza! lakini muuwaji huyo,, huwa anatumia koti la naman hii kuliacha kwenye eneo la tukio baada ya kufanya mauwaji!  mkuu wa jeshi aliongea maneno hayo huku akifungua kabati na kutoa koti jeusi.. alilolikuta ndani ya gari lake siku ile!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog