Simulizi : Siku 100 Za Mateso Ya Kuzimu
Sehemu Ya Tano (5)
*******
“Ta, ta, ta,” ilikuwa ni sauti ya mlio wa mshale wa saa ya ukutani. Ni ndani ya chumba tulivu, chumba kikubwa chenye fenicha chache tu ambazo ungeweza kuzihesabu.
Sofa la mtu mmoja lilikuwa ukingoni mwa kitanda. Meza ndogo ambayo ilikuwa sentimita cheche mbele ya sofa lile la thamani. Kama macho yako yangepata bahati ya kuona mandhali yachumba, kamwe usingekosa kuona kijokofu kidogo kilichojazwa matunda ya kila aina yakingoja mlaji.
Sambamba na hayo, ndani ya chumba kile nadhifu, chumba chenye utulivu wa hali ya juu, katika kitanda kulikuwa na mtu aliyekuwa mahututi. Mtu yule alikuwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya wiki.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa akipata matibabu maalumu ndani ya chumba kile, ni wazi uangalizi wake na matibabu aliyokuwa akipatiwa ilikuwa ni ya kipekee.
“Ta, ta ta,” sauti ya mlio wa saa iliendelea kujongea bila kuchoka huku ukiacha kasauti kadogo kakisambaa mule ndani.
Katika hali ile ya upweke, mara mlango wa chumba kile ulisukumwa, akangia mtu aliyekuwa amevalia koti jeupe na miwani, shingoni alikuwa amening’iniza kipimo kitumikacho kupima presha.
Mtu yule hakuwa peke yake, aliongozana na msichana mrembo ambaye kimtizamo tu, alikuwa ni nesi. Walipofika kwenye kitanda alichokuwa amelala mgonjwa wote walimtizama kwa masikitiko.
Daktari alimsogelea na kumpima mapigo ya moyo kwa kutumia kile kifaa alichokuwa amevaa shingoni.
“Si wa leo, wala kesho huyu” yule dokta alimwambia nesi baada ya kusikiliza mapigo yake ya moyo.
“Doktaa!!” nesi aliita akionekana kubaini kitu cha kushangaza kwa mgonjwa yule.
“Nini?”
“Hebu cheki”
“Nini?”
“Vidole vyake”
“Vina nini?”
“We’ angalia mwenyewe”nesi alisema akimwoneshea daktari vidole vya mgonjwa yule.
Dokta alitupa macho kwenye mkono wa mtu yule, aliona vidole vya mikono ya mgonjwa wake vyote vikicheza kwa zamu, vilikuwa vikicheza taratibu lakini kwa zamu.
“Anakaribia kupata fahamu nini?”nesi alihoji.
“Lakini vipimo vinaonesha bado, ni kweli atapata fahamu lakini si leo wala kesho”dokta akajibu
“Sasa vipi hivi vidole, ni ishara gani hii”
“Sijajua”
“Halafu nimebaini kitu” nesi yule akaendelea kusema.
“Kipi?”
“Vidole vyake vinacheza kwa kufuatisha milindimo ya sauti ya mshale wa saa ya ukutani”
“Kweli!”
“Kabisa,we mfuatilie” daktari yule alipofuatilia namna mtu yule alivyokuwa akivipigapiga taratibu vidole vyake pale kitandani, alikuwa akienda sambamba na sauti ya mshale wa saa ya ukutani.
“Ta, ta,ta,” sauti ya mshale wa saa ilisikika ukigonga kila nukta, ndivyo vidole vya mtu yule alivyokuwa akivibamiza polepole kwa zamu.
“Maajabu haya” dokta aliongea akiwa amekodolea macho kioja kile.
“Hebu fanya kitu kimoja…” dokta alinena huku akingaza macho kweye saa ile iliyokuwa kwenye ukuta wa chumba.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Toa betri za hiyo saa ili iacha kufanya kazi, tuone nini kitatokea”
Nesi yule alifanya kama alivyoelezwa, mshale wa saa ile iliacha kutembea baada ya kuondolewa betri. Mtu yule naye akaacha kuchezesha vidole vyake.
Wauguzi wale wawili walizidi kustajabishwa, wakiwa katika tafakuri, katika hali isiyo tarajiwa, Amosi Mikidadi alifungua macho yake kivivu.
Daktari na nesi wake walipatwa na taharuki ya aina yake, walibaki wamebung’aa kwa tukio hilo la kipuuzi kuwahi kutokea katika taaluma yao ya uganga.
“Jesus Christ!!!...Umeamka” Dokta alibweka huku akivua miwani yake na kufikinya macho yake ambayo alihisi yanamdanganya.
“Ni…ni..ko wapi hapa?” Amosi aliongea huku akimangamanga macho huku na kule ndani ya chumba.
“Hapa ni hospitali ya Muhimbili, upo katika uangalizi maalumu wa kimatibabu” dokta yule alisema harakaharaka huku akimsogelea pale kitandani ili amweke vizuri.
“Muhimbili!!!” Amosi aliuliza kwa mshangao. Dokta na nesi walitikisa kichwa kumkubalia.
Akawa kama anafikiria kitu fulani kichwani mwake, lakini akaonekana ni kama kulikuwa kuna kumbukumbu inayokuja kichwani mwake na kupotea.
“Tangu lini?” akendelea kuwahoji wale watu wawili.
“Relax Amosi, kila kitu utafahamu taratibu, ni mapema sana, kujibu maswali yako kwa sasa ”dokta alisema.
Amosi akavuta pumzi nyingi kwa ndani halafu akazitoa nje kwa mkupuo, kifua chake kikapanda juu na kushuka chini pindi alipovuta pumzi na kuzitoa nje.
Kila kitukwenye maisha yake kilikuwa ni michoro isiyokuwa na maana yoyote!!!!!
AMOSI alilala chali huku akijaribu kuvuta kumbukumbu, hata hivyo, kumbukumbu zilikuwa zinakuja kwa vipandevipande kama ndoto aliyoota akiwa usingizini na kusahaulika.
Daktari pamoja na nesi wake, waliendelea kumpa huduma baada ya fahamu kumrudia kimaajabu.
Baada ya kuweka kila kitu sawa, walisimama kando ya kitanda na kumwangalia. Kile kioja cha kuchezesha vidole vyake kwa kufuatisha milindimo ya saa ya ukutani, hakikuwepo tena.
Masaa machache badaye taarifa za Amosi kupata fahamu zilikuwa zimesambaa kila kona ya dunia, kila mtu alikuwa na hamu ya kusikia manusura huyo wa ndege iliyokuwa imepotea, ataeleza kitu gani.
Familia ya Amosi, pia ilikua ni moja ya watu waliokuwa wamezipata taarifa za mpendwa wao kupata fahamu baada ya kuzimia kwa muda mrefu.
Kiba akiwa na wadogo zake wawili, walipozipata taarifa hizo walifunga safari hadi Hospitali ya Muhimbili.
“Tunasikia ameamka?” lilikuwa swali la kwanza kwa daktari baada ya kuwasili Muhimbili.
“Ndio, kwakweli imekuwa ajabu sana”
“Kwanini?”
“Hatukutarajia angeweza kupata fahamu katika kipindi hiki”
“Mungu ni mkubwa, tunahitaji kumwona”
“Kumwona sio tatizo, lakini kwa mustakabali afya yake katika ubongo, ni vizuri kwa leo mngemuacha akapumzika”
“Kwani ubongo wake umefanyaje?”
“Haujafanya chochote, isipokuwa anaonekana anatatizo la kupoteza kumbukumbu, sasa kwakuwa mgonjwa mwenyewe ndio kwanza katoka kwenye koma ni vizuri mkamwacha.
“Kitendo cha kuwa naye, kitazalisha maswali mengi ya hapa na pale, kati yenu na yeye, kitu ambacho hakitakuwa kizuri kwake kwa kuwa bado anahitaji kupumzisha akili yake.” Dokta alisema.
Kiba na nduguze hawakuwa na namna ilibidi wakubaliane na ushauri ule wa kidaktari. Walimwacha Amosi apumzike.
Siku iliyofuatia, waliruhusiwa kuonana na Amosi katika chumba kile maalumu alichokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Ilikuwa ni furaha kwa ndugu wale kuona Amosi akiwa hai, wote walikizunguka kitanda na kumkumbatia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tumekusubiri kwa muda mrefu amosi, hatimaye Mungu amekurejeshea rasmi duniani” Kiba alisema.
Amosi alitabasamu huku akiwangalia nduguze kwa jicho la faraja.
“Ahsante Kiba, tangu lini mpo Dar?”
“Tuna wiki na ushee sasa, maana tupo hapa tangu ulipoletwa na watu wa usalama”
“Unataka kuniambia nina wiki nzima niko kitandani?” Amosi aliuliza kwa mshangao.
“Ndio una wiki na zaidi”
“Nataka kujua hao watu wa usalama walijuaje kwamba nilikuwa chini ya shimo kule kwa bastard”
“Kwani ulikuwa kwenye shimo…Bastard ndio nani?” Amosi naye aliuliza.
Bahati mbaya kabla hajajibiwa mlango wa chumba kile ulisukumwa wakaingia wanaume wanne waliokuwa wamevalia suti nadhifu watano akiwa ni daktari aliyekuwa akitoa matibabu kwa Amosi.
“Jamani hawa ni maofisa usalama, wanaomba radhi kidogo wanahitaji kuongea na mgonjwa” Daktari alitoa maelezo.
Kiba na wadogo zake ikabidi wawapishe wale watu walitambulishwa kwao kama maofisa usalama.
Baada ya watu wote kutoka nje, ndani wakabaki wale maofisa wane.
“Pole Amosi” mtu mmoja miongoni mwa wale alianzisha mazungumzo.
“Mimi naitwa, Inspekta Kojo, huyu ni Stanley ni CIA, yule ni Geogre na huyo karibu yako hapo anaitwa Anicet ni ofisa kutoka shirika la ndege la umoja wa mataifa..
Tuko hapa kutaka kufahamu ni kitu gani kilitokea siku ya March 28 mwaka huu majira ya kati ya saa moja jioni ukiwa ndani ya Panasonic Airlines,” yule mtu aliyejitambulisha kwa jina la Inspekta Kojo alianzisha mazungumzo moja kwa moja.
“Samahani?” Amosi alisema.
“Bila samahani,” wote waliitikia kwa pamoja.
“Kwani huu ni mwaka gani?” Amosi akauliza.
Baada ya swali hilo, wale maofisa wote waliamtizama mtu yule kwa mashaka. Mashaka yao yalitokana na mambo mawili, kwanza walihisi huenda jamaa alikuwa bado kumbukumbu zake hazijakaa sawa tofuati na walivyo elezwa na daktari, pili alikuwa na tatizo la kiakili.
“Anicet hebu mwite doktari” badala ya kujibu Inspekta Kojo alimpa amri mwenziye.
Muda mfupi badaye daktari aliingia mule ndani.
“Ulisema mgonjwa kumbukumbu zake ziko sawa?” Stanely alimuuliza daktari punde baada ya kuingia ndani.
“Ndio, kwani vpi?”
“Mgonjwa hafamu huu ni mwaka gani!” Inpekta Kojo alisema, lakini kabla dokta hajatia neno Amosi aliyekuwa kimya akiwafuatilia wale watu naye akadakia:
“Siyo kwamba sifahamu, isipokuwa nilitaka kuona kama bado nipo kuzimu ama laa!”
“Kuzimu!!” Wakauliza tena kwa pamoja.
“Ndio” Amosi akajibu.
Tabasamu jepesi likawatoka wale makamanda, daktari akabaki kando akiwangalia watu wale.
“Kuzimu ulikokuwa ilikuwa ni mwaka gani?” Inspekta Kojo akamuuliza kimasikhara.
“1960”
Maofisa wale wote wakacheka.
“Amosi”
“Naam”
“Tuko kazini, tuweke utani kando, dunia nzima inasubiri maelezo yako juu ya nini kilitokea hadi ndege ya Panasonic Airlines ikapotea”
“Sina utani na ninyi wazee, huko ilikuwa ni mwaka 1960”
“Haupo kuzimu, upo duniani, tena kwenye ulimwengu ambao huu ni mwaka 2017”
“Sawa”
“Nini kilitokea siku hiyo?” Inspekta Kojo akauliza akiwa amemkazia jicho Amosi.
“Baada ya maiti ya mama yangu kupakiwa kwenye ndege, mimi pia niliingia ndani ya ndege ya Panasonic….” Amosi alianza kusimulia.
“Muda machache baada ya ndege kupaa, kitu ninachokikumbuka nilipitiwa na usingizi, wakati huo tulikuwa umbali mrefu kutoka ardhini.
“Nikiwa katika usingizi, nikawa nahisi kama kuna mtetemo fulani…. sauti ya mhudumu wa ndege ikatuahasa abiria tusiwe na wasiwasi kwani tunapita katika anga ambalo linatheruji.” Alisema. Akapiga kimya kidogo, akawatizama wale jamaa ambao walikuwa makini kumsikiliza, kisha akaendelea
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“MHUDUMU wa ndege alitangaza kuna hali mbaya ya hewa katika anga tulilokuwa tukikatisha, akasema marubani walikuwa wakifanya kazi yao kwa umakini mkubwa mno, hivyo tusiwe na wasiwasi.
“Safari ikaendelea. Baada ya kama dakika sita ama saba, ile hali ikarudi, ndege ikawa ‘inavibrate’ safari hii ilikuwa ikitetemeka kwa nguvu zaidi ya ile ya awali. Halafu ikawa inayumba kulia na kushoto, hofu ikatanda, watu wakaanza kupiga kelele. Wengine wakawa wanasali sala zao za mwisho.
“Ghafla, ndege ile ikameguka vipande viwili, mimi na wenzangu tulijikuta tukimwagwa katika anga kama mchele, sikukumbuka tena kilicho endelea hadi nilipojikuta katika msitu nikiwa na maumivu makali” Amosi aliwambia wale maofisa usalama.
Watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza.
“Nini kilifuata baada ya hapo?” ofisa mwingine akamuuliza huku akimwangalia Amosi kwa makini.
“Sehemu tuliyokuwa tumeangukia, ilikuwa ni kuzimu” Amosi alisema kisha akapiga kimya kama mwenye kufikiria vitu fulani.
“Nini!” maofisa wale wakauliza kwa pamoja kama vile hawakusikia vizuri kile alichosema kijana yule.
“Nasema hivi, mahali tulipokuwa tumeangukia, ilikuwa ni kuzimu! Na nimeishi huko katika mateso makubwa kwa kwa siku zaidi ya 100!”
“Unamaanisha nini kusema hivyo?” Ofisa mwingine akauliza kwa kiherehere.
Amosi alivuta pumzi nyingi kwa ndani kisha akazitoa nyingi kwa mkupuo, kisha akaanza kusimulia kila kitu.
Alieleza tangu siku ya kwanza alipojikuta ameangukia katika msitu, baada ya kupoteza fahamu, akaeleza namna alivyokutana na wenzake, mauzauza mbalimbali aliyokutana nayo akiwa na wenzake hadi kuuawa.
Lakini pia, alieleza namna alivyoishi kwenye mji ambao huko ni mwaka 1960 ambapo pia, kulikuwa na mauzauza yaliyoivuruga akili yake.
Kadhalika, alisimulia kisa cha bastard ambaye alimpa kazi ya kumtafuta mtu aitwaye Soninapa na kumkabidhi ujumbe ambao hadi wakati huo hakujua uko wapi na ulikuwa ikihusu nini.
“Mambo unayoyaleza ni kama hadithi ya kipuuzi tu, hadithi isiyokuwa na maana yoyote kwenye akili ya mtu makini” kamanda mmoja miongoni mwa wale, alibwata kwa ukali akiwa amemkazia jicho Amosi.
“Dunia nzima inangoja maelezo ya msingi kutoka kwako, sasa sijui kwanini unakuja na hizi riwaya za kipuuzi namna hii kijana?” mwingine naye akafoka.
“Mnataka kusema ninawadanganya haya niwalezayo?” Amosi akauliza akiwa amewatumbulia macho watu wale.
“Ndio”
“Naongopa…?”
“Yes, unaongopa…”
“Huu ni ujinga” mwingine akadakia,
“Huwezi kutueleza eti umeishi siku 100 ‘some where’ ilihali tangu tukio la ndege kupotea leo ni siku ya 14 tu, hizo siku 100 unazosema umeishi…sijui, wapi huko!...zimetoka wapi?”
“Na unasema mara ya mwisho ulikuwa katika shimo ukizungumza na huyo mtu uliyemtaja anaitwa Bastard…sijui upuuzi gani…kisha ukapoteza fahamu, mbona timu yetu ya waokozi haikukuta shimoni?”
“Kadhalika, unatuongopea eti kuna kijiji huko ulikokuwa kinaitwa Guem, na unasema ni mwaka 1960 mbona sehemu uliyokutwa upo, eneo lote la kisiwa hakuna kijiji wala makazi ya watu?”
Jamaa walimuuliza maswali kwa kumshambulia mithili ya watu wanaomsuta mtu mzandiki.
“Ninachowaleza ni kweli ninyi!” Amosi akabwata kwa sauti huku akiwa amewakodolea macho ya mshangao wale maofisa.
“Ukweli gani?” mmoja akamuuliza kwa kebehi.
“Kwamba ulikuwa kuzimu kwa siku 100!” mwingine akamdhihaki
“Haki ya Mungu nawaapieni”
“Amosi” ofisa mmoja miongoni mwa wale akamwita kwa sauti tulivu.
“Naam”
“Unajua kama ukishindwa kueleza sababu ya ndege ya Panasonic kupotea na mahali ilipokuwa kwa wiki nzima, utaingia kwenye tatizo”
“Kivipi sasa?”
“Utahusishwa na masuala ya ugaidi,”
“Khaa!…kwahiyo ninyi mnataka niwaeleze ukweli upi?”
“Hatutaki kukuchagulia cha kusema, isipokuwa tunachotaka kwako ni ukweli”
“Ukweli ndio huo nilio waeleza”
“Kwamba ulikuwa kuzimu?”
“Ndio”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa siku 100?”
“Kabisa”
“Kamanda Anicet mfunge pingu” kiongozi wao alitoa amri.
Amosi akabaki ameduwaa kama teja wa madawa ya kulevya.
“Jiandae kwa mashtaka ya ugaidi”kamanda yule akaongeza nakuondoka mule wodini kwa hasira.
“Niacheni!!!” Amosi alipiga kelele wakati anafungwa pingu akiwa kitandani.
*****
“Siamini unachonieleza dokta”
“Niamini Amosi”
“ Mambo yote yaliyotokea yalikuwa ni ndoto!!!!”
“Kabisa”
“Kwahiyo hakuna kitu kinaichoitwa Bastard?”
“Ndio”
“Hapana dokta, mimi sio punguani, mambo yote ninayo yaeleza nimeyaishi sasa vpi iwe ni ndoto”
“Hebu na wewe niambie ni wakati gani na lini umeishi siku 100 huko unakokusema wewe ulikuwa? Kwa taarifa yako tangu tukio la ajali ya ndege litokee leo ni siku ya 14, siku saba zimetumika kukutafuta, na siku saba zingine umezimetumia ukiwa kitandani!”
Yalikuwa ni maongezo baina ya Amosi na daktari bingwa wa saikorojia na magonjwa ya akili Zulfa Hussein. Ambaye alikuwa akitoa matibabu kwa Amosi baada ya kudhaniwa huenda afya ya akili yake haikuwa sawa kutokana na hadithi alizokuwa akizitoa juu ya mahali alikokuwa.
“Nakuhakikishia kuna mahali nimeishi dokta” Amosi alisema kwa sauti ya kukata tamaa huku akimwangalia daktari yule wa kike.
“Na mimi pia nakuhakikishia hakuna mahali ulikokuwa, hayo yote unayodhani yaliyotokea kwenye maisha yako, ilikuwa ni ndoto inayopita kichwani mwako ukiwa umelala!” dokta alimwambia.
Kadiri alivyoendelea kuhakikishiwa kwamba maisha aliyoishi mahali fulani kwa siku takribani 100, ilikuwa ni ndoto alizidi kuchanganyikiwa ziaidi.
*****
HOSPITALI YA MILEMBE DODOMA
Kiasi cha miezi mitatu ilikuwa imepita tangu amosi apate msaada, baada ya kupotea katika ndege ya abiria ya Panasonic Airlines…
Hapakuwepo na mtu mwingine yeyote miongoni mwa abiria aliyepatikana. Jina la amosi lilikuwa likipamba vichwa mbalimbali vya habari karibu dunia nzima.
Kutokana na upekee wake, Kila mtu alizungumza lake vile alivyoweza, vyombo vya habari viliandika kila kukicha.
Ushuhuda aliokuwa akiutoa Amosi, kwamba aliishi kwa siku 100 mahali fulani kuzimu, ulimfanya kila mtu aliyemsikiliza kuamini kwamba, kijana huyo mwenye bahati ya aina yake maishani, alikuwa amekumbwa na wazimu.
Hali hiyo, ilitosha kupelekwa katika Hospitali ya Milembe maalumu kwa watu wenye matatizo ya kiakili.
Alikuwa akipatiwa matibabu chini ya dakatri bingwa wa matatizo ya akili ‘Brain disorders’ Dokta Zulfa Hussein.
Siku hiyo ya Jumatano, dokta Zulfa Hussein alikuwa akitoa ripoti kwa maofis wa CIA na wale wa usalama wa taifa, juu ya tatizo lililokuwa likimsumbua Amosi.
Matokeo ya taarifa hiyo yalirejesha ombwe la huzuni kwa maofisa wale.
Akijivuania taaluma yake ya udaktari, mwanamke yule, mwenye uso mwembamba na pua iliyochongoka, sanjari na macho yake makubwa ya duara yakifanya mwonekanao wake ufanane kabisa na ule wa mwanamke aliyeshinda taji la urembo. Alijiweka sawa kitini mbele ya maofisa wale. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa utulivu kama mtangazaji wa taarifa ya habari katika runinga, akaanza kueleza uchunguzi wake kwa Amosi.
“Amosi anasumbuliwa na ugonjwa uitwao ‘Amnesia’ mmewahi kuusikia popote?” Dokta Zulfaa aliwauliza katika namna ya kujivunia elimu yake huku akiwatizama kwa zamu.
Wakatisa kichwa kumkatalia.
“Huu ni ugonjwa ambao kwa Lugha ya Kingereza unajulikana ‘…a without a memory’ au kwa tafsiri ya Lugha ya Kiswahili ni ‘…bila ya kumbukumbu’
“Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ni maradhi yanayo sababishwa na hitilafu katika ubongo, magonjwa sugu na maumivu ya kisaikorojia.
“Kitu muhimu cha kufahamu ni kwamba, amnesia inaweza kukufanya ukapoteza kumbukumbu zote na usikumbuke chochote maishani au ukapoteza kumbukumbu lakini zikarudi polepole. Jambo hili mara nyingi hutegemeana na ukubwa wa tatizo lako,” Dokta alisema, Akapiga kimya akawatizama wanausalama wale, akaona wako makini kumsikiliza. Akaendelea.
“Omosi anasumbuliwa na ‘reotrograde amnesia’ ambapo aina hii husababishwa na msongo wa mawazo uliopitiliza, nadhani hali hii imetokana na matukio ambayo inaoesha kweli mtu huyu ameyaishi mahali fulani.”
“Mungu wangu!!” ofisa mmoja alihamaki.
“Kwahiyo ndio kusema hawezi kurejewa tena na kumbukumbu?” mwingine akadakia.
“Hapana, kwa huyu mtu iko tofauti kidogo,” dokta Zulfa Hussein alisema, watu wote mule ndani wakapiga kimya kumsikiliza.
“Tofauti aliyonayo kijana huyu, ambayo hata mimi binafsi inanichanyanga ni kwamba, yeye anazo kumbukumbu nyingi tu za maisha yake ya nyuma, yanii maisha kabla ya kupotea na ndege.
“Lakini, kumbukumbu hizo zinapotea kwa kasi mno, kitu pekee kilichonata kwenye ubongo wake ni maisha anayodai aliishi kuzimu kwa siku 100!.
“Sijakuelewa hapo” ofisa mmoja alisema.
“Nasema hivi, mtu huyu anapoteza kumbukumbu kwa kasi ya ajabu na kabakiwa na matukio anayoyajua mwenyewe.”
“Duh, kwahiyo suluhu ni nini hapo?”
“Nisema mara ngapi kwamba hiyo ni ‘reotrograde amnesia’….ugonjwa huo hauna tiba, atakuwa wa hivyohivyo maisha yake yote duniani” dokta Zulfa alisema kwa msisitizo.
Maofisa wale walichoka, jitihada za kupata ukweli juu ya ndege iliyopotea zilififia kama sio kufa kabisa!.
*****
Hali ya Amosi ilizidi kuwa mbaya kila kuchwapo, mwonekano wa mwendawazimu ndio taswira iliyokuwa ikionekana kwa mtu huyo.
Alipenda kuwa peke yake, na alizungumza mwenyewe, maneno yake mengi alikuwa akijielezea mwenyewe maisha aliyoishi kuzimu kwa siku 100!
Alitamani aingie kwenye nyoyo za watu na awaeleze ukweli kwamba alipitia maisha fulani, lakini hilo lilibaki kuwa tamanio tu. Hakuweza.
Hapakuwa na aliyemwamini, madakti walimhakikishia madai aliyokuwa akiyaeleza ilikuwa ni ndoto aliyoota akiwa amelala usingizini.
Kila mtu alimpuuza kwa kumwona na kiumbe aliyedata.
Hata ndugu zake wa karibu, pia walimtizama katika mazamo huo. ‘Mwendawazimu’. Hapakuwa na mtu hata mmoja aliyemwamini.
Sasa kila kitu kwenye maisha yake, ilikuwa ni michoro isiyokuwa na maana yoyote. Hakuwa na yeyote wa kumsikiliza, Amosi aliishi kwa tabu katika siku za ujana wake, alichomwa sindano na kupewa madawa makali ambayo madaktari walidai ni msaada kwakwe kutokana na kuwa na maradhi ya ‘Amnesia’…”
Kutokana na kutoaminika, madawa hayo ambayo aliambiwa yanafanya kazi ya kupumzisha ubongo wake, yalimfanya asahau mambo mengi ya nyuma.
Dunia alianza kuiona chungu. Alijiona anatendewa unyama na watu wake wenyewe. Kwa zaidi ya miezi sita akiwa hospitali ya Milembe, hakuwa na chochote alichokuwa akikikumbuka zaidi ya siku 100 za maisha ya kuzimu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
“Maiti…maiti…maiti!!” mtu mmoja alikuwa akipiga kelele kwa nguvu huku akitimua mbio. Ni ndani ya Hospitali ya Milembe.
Wauguzi walijaribu kumzuia mtu huyo ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagonjwa wa akili waliokuwa wakipata matibabu katika hospitali ile ya taifa.
Mtu huyo, usoni alionekana kuwa ni mwenye hofu kubwa na taharuki ya aina yake.
“Ni nini?” muuguzi mmoja alimuuliza.
“Maiti!! mtu kajiua!”
“Wapi?”
“Kule, kwenye chumba kile” aliosonta kwenye chumba alichokuwa akiishi Amosi.
“Unasema kweli?”
“Haki ya mungu ni kweli kama akili yangu haijanidanganya”
Upesi waaguzi wale waliekea kwenye chumba alichokuwa akishi Amosi. hawakuamini walikutana nacho nacho.
Mwili wa Amosi alikuwa anang’inia katika kenchi. Alikuwa amejinyonga kwa kutumia mashuka ya kujivunika.
****
SEHEMU YA MWISHO
Wauguzi walichanganyikiwa kwa kile walichokuwa wakikiona mbele yao! Taharuki kubwa zaidi ya ile ya awali ikazuka Hospitali ya Milembe. Masaa matatu badaye habari juu ya kifo cha Amosi zilienea kila mahali.
Kifo cha mtu huyo kilisambaa katika kila pembe ya duania kwa kasi ya ajabu, hilo lilikuwa ni tukio lililoleta mijadala mingi.
Kuna waliohusisha tukio la kifo cha Amosi na ujasusi, Wengine waliihusisha Jumuiya ya Freemason, wachache waliamini yalikuwa ni mapenzi ya Mungu.
“Kifo cha Amosi kimetokana na ‘Fractius’…yanii hasira katika msongo wa mawazo, na hii ni kutokana na ujumbe aliouacha kabla ya kujiua” alisema Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Abdulahim Ally.
Alikuwa ameshikilia karatasi za ripoti ya ‘postmoterm’ ya mwili wa Amosi iliyofanyika katika Hospitali ya mkoa wa Dodoma. Mbele yake walikuwa wameketi mawaziri kadhaa wa serikali, akiwemo waziri wa afya, waziri mambo ya ndani , IGP wa jeshi la polisi, sanjari na maofisa wengine wa jeshi wa ngazi za juu.
Alimeza funda la mate kisha akaendelea kuzungumza:
“Pamoja na hayo yote, bado uchunguzi wa kina unaonesha kijana Amosi Mikidadi, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ‘Anemsia’ ambayo licha kupoteza kumbukumbu, lakini maradhi hayo yalimsababishia tatizo la kurukwa na akili!.” Aliongea kisha akachukua karatasi nyingine na kuendelea kusoma:
“Mazingira ambayo mwili wa kijana huyu ulikutwa ukiwa mfu, ulipatikana ujumbe ambao ulikuwa kwenye kipande cha karatasi, ujumbe huo uliandikwa kwa maandishi makubwa ulisomeaka ‘SONINAPAC” alisema, akawatizama tena wale vigogo waliokuwa wakimsikiliza kwa kina.
“Neno hili baaada ya timu yetu kulifanyia uchunguzi wa kina tumebaini halina maana yoyote zaidi ya kwamba, neno hilo ‘soninapac’ ukiligeuza kuanzia mwisho kuja mwanzo unapata neno PANASONIC!”
“Panasonic ndio jina la ndege ambayo ilipotea! Hapa hatupati maana yoyote, japokuwa marehemu kabla ya kifo chake aliwahi kueleza hadithi ya kuishi siku 100 huko kuzimu, kisa ambacho sote tunakubaliana ilikuwa ni ndoto aliyokuwa anaoota akiwa amelalala anapatiwa matibabu.
“Hivyo basi, mapendekezo ya kurugenzi ya usalama wa taifa tunaona kuwa ni vema sakatala hili liwe ‘close but unsoved’…..” alimaliza kutoa maelezo.
Viongozi wote waliokuwa pale walitikisa vichwa kukubaliiana na maelezo, pamoja na mapendekezo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
WIKI MBILI BADAYE
Amosi alizikwa nyumbani kwao Nyamalembo mkoani Geita, ilikuwa ni huzini kubwa kwa familia, marafiki na jamaa wa karibu.
Baaada ya mazishi watu waliketi matanga kwa wiki mbili wakiimba tenzi za rohoni, pamoja na kumfanyia ibada ili roho yake ilazwe mahali pema peponi.
“Mungu ametoa, ndiye ametwaa, kwaheri Amosi, kwaheri mpendwa, rohoyako ilazwe mahali pema peponi…”
“Emeeeni!” watu wote waliitikia kwa sauti.
Hadithi ya Amosi ikabaki kuwa ndoto!.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment