Simulizi : Chozi La Ukombozi
Sehemu Ya Tano (5)
wakati huohuo kule kwenye falme ya beha alionekana komba akiendelea kuwafyeka shingo wanajeshi wa mazy kisha akaingia upande wa ndanialipokaguakagua aligundua hakuna mtu mule ndani ya jumba la kifalme...akaanza kumtafuta mazy.. ghafla aliona mlango akautilia mashaka akaukayaga kwa kurusha teke mlango ukafunguka....akaingia ndani alistahajabu kukuta mlango mwingine upo wazi alipochungulia aligunsua kuwa mazy katoroka kupitia mlango huo...naye akapita hapohapo katika mlango huo....mpaka akatikezea upande wa nje...alijikuta yupo nyuma ya jengo la falme ya beha...akaanza kutimua mbio kulizunguka jengo hilo...akapanda farasi wake na kutoka upande wa nje ili arudi ghemi aliamini mazy atakuwa kaelekea ghemi hivyo mfalme atakuwa hatarini...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
vita iliendelea...alionekana prince mody akipambana baraabara aliwachinja wanajeshi wa mazy kama kuku....damu zilitapakaaa kila eneo..
************
upande mwingine alionekana komba akiwa juu ya farasi kuelekea ghemi alipokaribia alistahajabu kukuta farasi amefungwa...alafu hakuna mtu....mazy alishuka kwenye farasi kisha akaanza kuitimua mbio kuelekea upande wa ndani..
wakati huohuo mazy aliweza kumuona rubi kabeba kile chungu kilichokuwa na maji ndani yake rubi alimkabidhi mazy kile chungu...mazy alikipokea ghafla akamchinja rubi akadondoka chini na kupoteza maisha papohapo...kisha akatoka haraka akapitia ile njia ya siri aliyoitumia kuingia ndani.....akatoka nje kabisa ya ngome ya falme ya ghemi.....
wakati mazy anatoka komba ndio alikuwa anaingia..komba alihuzunika sana kukuta walinzi wameuwawa kikatili...akaingia ndani ya jengi la kifalme alistahajabu kumkuta rubi kauwawa...komba alikimbia akaingia chumba cha siri...alipotazama pale kilipokuwepo chungu....hakukiona.....""mungu wangu...bila shaka huyu ni mazy....komba alijisemea moyoni kisha akatimua mbio kutoka nje.. alipotoka nje ya geti kwa mbali aliona mtu akikimbia huku akiwa juu ya farasi.....aliweza kumuona kwa sababu ghemi ilikuwa kwenye kilima.....hivyo mazy alikuwa upande wa chini.....komba alikimbia haraka mpaka kwenye farasi wake akapanda na kuanza kumfatilia mazy..
upande mwingine alionekana mazy akimuongoza farasi kuelekea kwempaka uliokuwa baharini...mazy alikuwa na shauku ya kuufufua ule mzimu uliofungiwa miaka elfumoja iliyopita.. alipogeuka nyuma alimuina komba akimfuatilia kwa nyuma........mazy alimpiva farasi wake ili aongeze kasi ya kukimbia....alipoukaribia mpaka alishuka kutoka kwenye farasi akavichukua vile vyungu viwili akaanza kukimbia kuelekea baharini ili amwage ile damu pamoja na yale maji yaliyokuwa ndani ya chungu ..kabla hajaanza kuingia baharini komba alifika lakinj alikuwa ameshachelewa........mazy alimwaga baharini ile damu pamoja na yale maji......punde bahari ilibadirika rangi maji yakawa na rangi nyeusi.....likatokea tetemeko kubwa la aridhi
wakati wanatahamaki mara ghafla.....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
uliibuka ule MZIMU kutoka chini ya bahari katika ule mlango wa kimiujiza aliofungiwa...MZIMU ule ulitisha sana ulikuwa na macho matatu moja likiwa katikaki ya paji la uso na mawili yakiwa kisogoni....komna alistahajabu sana......mazy akaingiwa na uwoga wa hali ya juu kisha akaanza kutimua mbio kuelekea kule alipokuwepo farasi wake......komba naye ilibidi atimue mbio alikimbia akapanda juu ya farasi....mazy alikimbia na kutokomea kusikojulikana.....
punde ule mzimu ulitoka baharini na kuja nchi kavu....mzimu ule ulikuwa kama hewa..ulikuwa na uwezo wa kusambaa kama moshi kisha ukajikusanya na kuunganika...mzimu huo ulielekea Kwenye falme ya beha.....
punde mzimu huo ulifika na kuaza uuwa wanajeshi wa falme ya Ghemi huku ukiwaacha wanajeshi wa falme ya Beha......prince mody alipo ona mambo yamekuwa magumu aliamua kutimua mbio kurudi ghemi......
wanajeshi wa Falme ya ghemi waliuwawa wote hakubaki hata mmoja aliyebaki hai.....mazy alistahajabu sana kisha akajisemea moyoni"" inamaana mzimu huu upo upande wetu!!!!!?? mazy alianza uingiwa na ujasiri akaufuata Mzimu....alipoukaribia alistahajabu mzimu huo ulimtazama tu....kisha mazy akasema"" nataka twende ghemi tukauangushe utawala wa baba yangu...ghafla mzimu ule ulianza kupiga hatua na kuifuata njia iliyokuwa unaelekea ghemi.mazy alishangaa sanaakajisemea moyoni.
""."kumbe mzimu huu unasikiliza na kutii amri yangu... sasa dinia yote ni yangu....
******************
upande mwingine alionekana komba akiingia kwenye lango kuu la falme ya Ghemi..pumde prince mody alifika wakaingia ndani kuangalia je mfalme yupo salama,,,,,walipoingia kwenye maficho maalumu kwa ajili ya mfalme....walimkuta mfalme yupo hai....lakini alionekana kuwa katika hali ya mawazo mazito...
*****************
kule beha mazy pamoja na jeshi lake walipanda juu ya farasi na kuianza safari ya kwenda kuangusha utawala wa mfalme wa ghemi....
wakati huohuo mfalme wa ghemi alimchukua komba mpaka kwenye chumba cha siri kisha akachukua ule upanga maalumu aliomkabidhi komba....na kusema""" upanga huu ni upanga wa ajabu unauwezo wa kipekee.....upanga huu umetumiwa na kizazi cha wafalme wa Ghemi waliotawala Ghemi miaka efu moja iliyopita....nakuamini mjukuu wangu.....utautumia upanga huu kuangamiza kila kitu cha ajabu hata kisicho onekana (invisible)
*******************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ule upande mwingine...mazy pamoja na jeshi lake likiambatana na ule Mzimu....waliikaribia Ghemi walianza kuuwa wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa ngome ya kifalme..
ghafla komba alihisi kunahatari upande wa nje..alipotoka alikuta jeshi kubwa la mazy likiangamiza raia wasiokuwa na hatia....komba alitimua mbio kurudi upande wa ndani akachukua ule upanga kisha akamrudisha mfalme mafichoni...komba na baba yake walitoka upande wa nje....ghafla yalianza kurushwa majabali ya mawe makubwa kwenye ngome ya kifalme....
majabali hayo yalirushwa kwa kutumia pitalo iliyotengenezwa kwa magogo ya miti mikubwa...
majabali hayo yalibomoa baadhi ya kuta za ngome ya kifalme na kuingia ndani.....jeshi la mazy liliendelea kurusha majabali hayo mpaka lango kuu la falme ya Ghemi likang'oka na kudondoka...
lilikuwa ni jeshi la watu wawili baba na mwana...komba aliuchomoa ule upanga na kuushikilia baraabara.. pia prince mody alichomoa upanga....punde jeshi la Beha lilivamia na vita ikaanza upya.....palitimka vumbi vita ilikuwa ni zaidi ya vita zilizopita...komba aliingiwa na nguvi za ajabu baada ya kuushika upanga ule...aliwafyeka shingo kama kuku akishirikiana na baba yake....mpaka akawamaliza wanajeshi wote waliokuwa wameingia upande wa ndani...mazy alistahajabu sana...alichanganyiwa sana hakuamini alichokuwa anakiona machoni mwake...kisha akaamuru jeshi la awamu ya pili...likaingia ndani ya ngome ya kifalme....komba aliwafyeka shingo zao mpaka wote wakisha....komba alionekana kutapakaa damu mpaka sura ikabadilika utadhani kaoga damu..alipogeuka nyuma alistuka kumuona baba yake yupo chini.....ile anataka umfuata baba yake mara ghafla.....
aliona jeshi kubwa likija kwa mara nyingine tena....komba alimnyanyua baba yake na kumbeka akamkimbiza upande wa ndani kwenye maficho ya siri kwa ajili ya mfalme....kisha akatoka nje haraka...punde jeshi lile lilivamia akaanza kupambana nao...aliwafyeka shingo zao....mpaka wakaisha wote.....mazy aliendelea kuchanganyikiwa alijiuliza komba ni mtu wa namna gani!!!!! alishangazwa sana na kitendo cha kimba kupambana na wanajeshi zaidi ya elfu moja....yeye akiwa peke yake na kuwauwa wote....mazy alipo ona amebaki na wanajeshi wachache kama saba hivi aliamua ku-uamuru MZIMU umuangamize komba.....punde mzimu ule ulianza kumfuata komba...... kwa sababu ulionekana kutisha komba alikimbia na kuingia upande wa ndani kisha akapanda juu kabisa ya jengo la kifalme....akachukua upinde na mshale akaurusha mshale ukaunda moja kwa moja mpaka kifuani mwa Mzimu ule.....komba alistahajabu mshale ulidunda na kudondoka chini.... mzimu ule ulianza kuangusha nguzo zilizokuwa zimesgikilia jengo la kifalme komba alishuka mpaka upande wa chini akatoka nje ili mzimu ule uache kuvunja nguzo na kubomoa jengo....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
komba aliamua kufanya hivyo ili kuokoa maisha ya mfalme pamoja na baba yake wasifuangukiwe na kuta za jengo hilo zilizojengwa kwa mawe makubwa...komba alipotoka upande wa nje.alipaza sauti na kusema"" nipo hapa njoo upamnane na mimi.....ule mzimu uliacha kuendelea kuvunja nguzo hizo...na kuanza kumfuata komba alipomkaribia alimpiga kofi komba..kofi hilo zito na lenye nguvu...lilimfanya komba adondokee mbali kabisa.....komba alipotua chini upanga ulimponyoka na kuangukia kando....
komba alihisi maumivu makali yakiambatana na kizunguzungu...punde ule mzimu ulimfuata komba pale alipokuwa amedondoka komba....mzimu ukanyanyua mguu ili umkanyage komba afe....punde komba alichoropoka haraka akauokota upanga wake.....kishaakanza kupimbana na mzimu huo.... wakiwa wanapambana komba alimkata kwenye mkono mkono ulianza kupukutika ukawa moshi na kusambaa...... komba aligungua kumbe upanga huo unanguvu za ajabu...akaanza kumkata kila eneo la mwili wa mzimu huo...uliyayuka na kuwa moshi...kisha ukatoweka...ikawa mwisho wa mzimu huo...hautaamka kamwe.....wale wanajeshi saba waliobakia walistahajabu sana walimuigopa komba waliamua kutimua mbio na kumuacha mazy......walikimbia na kutokomea kusikojulikana........mazy alianza kuingiwa na wasiwasi akapanda juu ya farasi ili akimbie... kabla hajapanda alionekana prince mody akirusha mshale ukamlenga kaka yake..... mshale huo ulikuwa na sumu kali ya nyoka aitwae koboko(COBRA) mazy alianza kuishiwa nguvu hatimae akadondoka na kupoteza maisha....wananchi wa Ghemi walifurahi sana walimshukuru sana komba kwa kulisaidia taifa lao...kisha komba akaingia upande wa ndani alimuona babu yake akitoka mafichoni....alimkumbatia komba kisha akasema
""hakika wewe ni shujaa umekuwa
CHOZI LA UKOMBOZI nakushukuru sana pia nakupongeza kwa kulikomboa Taifa...
kesho yake mfalme aliitisha kikao kisha akamtawaza komba kuwa MFALME MPYA WA GHEMI...wananchi walifurahi sana...komba aliliongoza taifa kwa hekma na busara..wananchi waliishi kwa furaha na amani....baada ya miaka mitatu kupita Mzee ramuh aliyekuwa mlezi wa komba aliugua na kupoteza maisha komba alisikitika sana...RAMUH alizikwa kwa heshma zote katika makaburi ya watu wa heshma wa tawala ya falme ya Ghemi...maisha yaliendelea
komba alipata mchumba aitwae RAHMA akamuoa na baada ya miezi saba MALKIA RAHMA alipata ujauzito na ulipofika wakati wa kujifungua alizaa mapacha mtoto wa kike na wa kiume
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mtoto wa kike .komba alimpa jina la mama yake mzi akamuita NINO...na mtoto wa kiume alimpa jina la mlezi wake aliyemlea kuanzia utoto mpaka umri wa utu uzima alimuita RAMUH.....Ghemi ilikuwa na amani tangu miaka hiyo hapakuwahi kitokea vita mpaka leo hii....
***MWISHO****
0 comments:
Post a Comment