Simulizi : Uko Wapi Mama?
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi siku zilisonga miaka nayo ikizidi kusogea wakati huo Kagaruki na dada yake Hamala wameshaacha shule ili kumuhudumia mama yao ambaye tayali mlemavu wa mgongo na upofu wa macho,Kiukweli maisha kwa upande wao yalikua magumu sana na hivyo Kagaruki akawa ndio kama mtu tegemezi kwa mama yake huku Hamala nae akiwa na kazi ya kumsafisha mama yake kila anapo jisaidia maana mama Kagaruki hukuwa na uwezo wa kukaa wala kusimama kwa sababu alivunjwa mgongo na yule nyoka aliyetokea kwenye kaburi la mama Nyanzala kwahiyo mama Kagaruki akawa anajisaidia ndani haja kubwa kwa ndogo.. Hapo ukatimia msemo usemao malipo ni hapa hapa duniani na kwa mungu ni hukum tu.
Huzuni juu ya huzuni nyumbani hapo kwa mama Kagaruki,na siku moja Hamala akamwambia kaka yake "Kagaruki nimemkumbuka sana dada Nyanzala sijui alienda wapi??
Kagaruki akajibu.."sio wewe tu hata mimi maana nadhani laiti kama Nyanzala angelikuwepo basi mama angejisikia faraja sana kwa sababu siku haiishi bila kumtaja Nyanzala "..Kagaruki alimjibu dada yake kwa sauti ya huzuni huku wakiwa chini ya mti wakila viazi vya kuchomwa,mara baada kumaliza kula hatimae Kagaruki alimwambia dada yake kuwa wamalizie kulima eneo ndogo lililobaki ili wawe wamemaliza kabisa kibarua walichopewa.
Lakini Hamala alikataa katukatu kurudi tena shambani huku akisema kuwa anarudi nyumbani kumwangalia mama yake...
"Hamala naomba unielewe dada tukimaliza hili eneo lililobaki tutapata hela yetu leo leo ili tuweze kununulia mahitaji ya nyumbani sawa" alisema Kagaruki akimwelekeza dada yake,ila Hamala baado alikataa huku akiondoka zake kitendo ambacho kilimuudhi Kagaruki mwishowe akampiga makofi ndipo Hamala hakuweza kukubali nae alimrudishia hivyo ikawa purugashani katika shamba la watu.
Na wakati Kagaruki na dada yake wakiwa bado wanapigana hatimae mzee mwenye shamba alikuja kwa niaba ya kukagua mwenendo wa kazi unavyokwenda lakini cha ajabu aliwakuta mtu na dada yake wakipigana huku Hamala damu zikimtoka puani kama maji,basi yule mzee mwenye shamba aliingilia kati na kisha akasema "Nyie nimewapa kazi ili mpate hela ya kumsaidia mama yenu lakini jinsi mlivyokuwa wajinga mnaanza kupigana haya ondokeni hapa pumbafu zenu"
Kwisha kusema hayo mzee huuo aliwakabidhi kiasi cha fedha kilicho lingana na eneo walilo fanya kazi Shani halafu akawatimua shambani kwake.
Baada Kagaruki na dada yake kufika nyumbani,Hatimae walimkuta mama yao hali sio shwali na hivyo bila kuchelewa Kagaruki alikimbia kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye nae alikuwa anafanya biashara ya kukodisha baiskeli,haraka sana Kagaruki alikodi baiskeli kisha akaelekea mjini kwenda kumnunulia mama yake dawa akijuwa labda mama yake kashikwa na malaria.
Kwa muda wa saa moja Kagaruki alifanikiwa kuingia mjini na baiskeli yake,hivyo moja kwa moja alielekea mahali yalipo maduka ya madawa. Baada kununu dawa alichukua baiskeli yake kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani,lakini kabla hajaumaliza mji ili aingie kijijini mara ghafla Kagaruki alifinya brek ya baada kumwona binti kama Nyanzala. Hivyo Kagaruki akawa ametulia akisubili yule binti ageauke ili amtazame usoni kama kweli ni Nyanzala au sio...Lakin mpaka yule binti anazama kwenye uchochoro flani hivi bila hata kugeuka nyuma..."daaah sijui ni yeye Nyanzala ??au nimemfananisha?
Alijiuliza mwenye Kagaruki huku mapigo ya moyo wake yakimwenda mbio.. Ila yote kwa yote aliamuwa kumwachia mungu akanyonga baiskeli yake kurudi nyumbani kwao huku akili yake yote ikimfikilia yule binti aliye mwona mjini akifanana mwendo na Nyanzala kwahiyo maswali mengi aliweza kujiuliza kuhusu yule binti..na moja ya maswali.Tetesi kwamba Nyanzala alifariki mbona kaburi lake halionekani nyumbani?Wakati mila na desturi zetu zinadai kuwa hatakama mtu kafia wapi sharti ni lazima azikwe nyumbani alikozaliwa ..Sasa leo hii iweje waseme kwamba Nyanzala alifariki wakati hata mahali alipozikwa hapaonekani??...hapana ipo siku nitakuja tena mjini ili nifanye upelelezi kuhusu Nyanzala ".....Alijisemea mwemye kutoka katika ubongo wake Kagaruki ilihali muda huo huo akawa amefika nyumbani kwao lakini cha ajabu alikuta mlango umefungwa kwa ndani, aligonga kama mala tatu kisha Hamala akafungua mlango.
"Kulikoni mbona unajifungia ndani mchana wote huu??....Kagaruki alimuuliza dada yake...nae akamjibu.."huwezi kuamini kaka,kwani muda ule ulivyokwenda mjini kumnunulia dawa mama..Alikuja mwanamke mmoja kumuulizia Nyanzala tena kibaya zaidi yule mwanamke nilipomtazama kwa umakini macho yake yalikua kama ya nyoka pia hata mikono yake kwa mbaali ilikuwa ngozi ya nyoka ingawa mwili na vingine vyote ni kama binadam" Ni maelezo ambayo yalimwacha mdomo wazi Kagaruki huku asielewe cha kufanya.
"enhee vipi uyo mama hajaacha ujumbe wowote au nia yeke alimtaka Nyanzala tu??"
Alihoji Kagaruki huku akionekana kuwa na woga flani hivi..."mmh kasema atakuja baadae usiku kuja kumpa pole mama..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kagaruki alikastaajabu kuambiwa na dada yake kwamba kuna mwanamke amekuja nyumbani kwao ikiwa sehem mbali mbali za mwili wake anafana na Nyoka,kibaya zaidi kilicho mchanganya Kagaruki ni pale alipo ambiwa kuwa mwanamke huyo atakuja usiku kumpa pole mama yao. Hapo akawa mpole akionekana kana kwamba anawaza jambo fulani,mwisho akakata ukimya huo akamtazama dada yake akasema "Dada nakuomba leo upike chakula mapema ili tuwahi kulala . Pia tafadhali endapo ukisikia mtu akibisha hodi usifungue mlango sawa dada? Kagaruki alimwambia hivyo dada yake ambae nae wakati huo alikuwa akichambua mboga za maboga kwa niaba ya chakula cha usiku. "Sawa kaka nimekuelewa.. vipi lakini dawa umepata? " Hamala alihoji. "Ndio nimepata, enhee sasa sikia hii mpya niliyotoka nayo mjini" Ghafla Hamala akastisha zoezi la kuchambuwa mboga akawa makini kumsikiliza kaka yake alichotaka kuzungumza. "Dada leo bwana kwa macho yangu nimemwona dada mmoja kafanana na Nynazala kila kitu" Hamala aliguna kusikia maneno hayo kisha akajibu" lakini kaka kweli? Au umemfananisha? "
"Kweli mimi sikudanganyi.. cha muhimu ngoja nirudishe baiskeli kwa mwenyekiti kisha nije nikupe mkasa wenyewe" " sawa kaka fanya hivyo wakati huu mimi naanda mboga.." Kagaruki alitengua stendi ya baiskeli. Moja kwa moja akaanza safari ya kuelekea kwa mwenyekiti wa kijiji ambako ndiko aliko kodi baiskeli. Lakini kabla Kagaruki hajafika mbali, mara ghafla dada yake alimuita nae Kagaruki akaitika "Kama unahela njoo na Mafuta ya kupikia " Hamala alimwambia hivyo kaka yake lakini Kagaruki akasema " sina hata senti dada yangu" kwisha kumjibu dada yake, Kagaruki akarudia kupanda baiskeli hadi kwa mwenyekiti ambapo akajikuta akitukanwa na mwenyekiti baada kupitiliza muda alio pewa.
Hatimae Kagaruki alirejea nyumbani kwao.. akamkuta dada yake akisonga ugali, Kagaruki alifurahi saana. Akasema "kweli dada yangu unamkono mwepesi yaani dakika kadhaa tayali unasonga ugali? Ila angali usipike ugali mbichi bwana" Alisema Kagaruki huku akiingizia na utani kidogo ulio mfanya Hamala kuachia kicheko. Kisha nae akajibu " Acha kunivunja mbafu kaka embu andaa maji hapo sebuleni" "sawa..mama umemchotea uji? " "ndio hilo ni jambo ambalo siwezi kulisahau" Alijibu Hamala kwa sauti ya upole. Ukweli mama Kagaruki kutokana na jinsi hali yake ilivyokuwa hakuweza kula chakula chochote kigumu. kwahiyo chakula chake kilikuwa maji na uji mwepesi. " Mama uji tayali mama" Hamala alisema hivyo baada kumpelekea uji mama yake,Mama Kagaruki aliasama mdomo wake kisha mwanae akaanza kumnywesha. Hayo ndio yakawa maisha ya mama huyo. Kwani alikuwa mtu wa kulala chali pia hata kuona mwanga au Dunia jinsi ilivyo ilishindikana kwa maana alikuwa kipofu,Hivyo mara baada Hamala kumaliza kumnywesha uji mama,yake nae na kaka yake walikaa wakaanza kula chakula wakati huo imeshatimia saa kumi na mbili jioni. "Enhee niambie sasa kaka yangu.Ulisema umemuona Nyanzala? "Ndio ila sina uhakika kama ni yeye ingawa nampa asilimia nyingi huwenda yule akawa Nyanzala" Alisema Kagaruki kwa kujiamini kabisa" "kaka kwani hujaipata habali kuwa Nyanzala alifariki?.." Hamala alijibu kwa mshangao jibu lake likiambatana na swali. "Mimi sikubaliani na hilo dada hadi nilione kaburi lake.. hivyo cha msingi ipo siku nitaenda mjini kumtafuata dada Nyanzala nimemkumbuka sana mimi" Kagaruki alimwambia dada yake huku machozi yakimtoka,Hamala alimsihi kaka yake apumguze munkali. Kagaruki akyafuta machozi kisha akainuka kuelekea chumbani kwake huku dada yake nae akielekea chumbani kwake wote wakienda kulala. Kagaruki akarudia kumkumusha Hamala,akasema"Dada usisahau.. nakuomba usifungue mlango hata kama utasikia mtu unae mfaham kagonga mlango" "sawa kaka" alijibu Hamala kisha akaingia chumbani kwake kulala.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada watoto hao kujichimbia vyumbani mwao,kweli punde si punde ilisikika sauti ya mwanamke ikimuita Hamala. Hamala alishtuka kutoka usingizi baada kusikia hiyo sauti,akajuwa tayali yule mwanamke aliye sema atakuja kumjulia hali mama yao tayali kafika. Hapo ndipo Hamala alipo nyamanza kimya huku ile sauti nayo ikiendelea kumuita mwishowe sauti hiyo aliisikia mama Hamala,hivyo nae akapasa sauti ya kumuita Hamala lakini Hamala bado hakuweza kuitikia. Wakati huo Kagaruki nae alitelemka kutoka kitandani kisha akazipiga hatua kuingia chumbani kwa mama yake. Baada kumfikia, kagaruki alimziba mdomo mama yake kisha akasema "Mama kaa kimya huyo sio binadamu wa kawaida" Mama Kagaruki alishtuka..
"kwani saa hizi saa ngapi? Alihoji mama Kagaruki. "Sijui ila saa hizi usiku wa manane" Kagaruki alimjibu hivyo mama yake kisha akamuaga kuwa anarudi chumbani kwake kulala. Lakini kabla Kagaruki hajaondoka. Mama yake alimuita " Kagaruki mwanangu" "Naam mama" "Hamala yuko wapi? "Yupo chumbani kwake kalala" alijibu Kagaruki . Mama Kagaruki akashusha pumzi kwa nguvu Kisha akasema "Muite na yeye kuna mambo nataka kuwaeleza maana mimi sio waleo wala wa kesho" Aliongeza kwa kusema hivyo mama Kagaruki maneno ambayo yaliweza kumshtua Kagaruki. Hima alizipiga hatua kuelekea chumbani kwa dada yake akamwamsha. Na kwa Sababu Hamala alikuwa macho wakati wote,haraka sana aliitika moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa mama yao ambae kiukweli hali yake ilionekana kuwa mbaya zaidi.
Baada Kagaruki na dada yake kufika chumbani kwa mama yao,Kagaruki alipapasa mahali kilipo kibiliti akakiona akawasha kibatali wakati huo huo ile sauti iliyokuwa ikimuita Hamala imeshapotea. "Mama tupo pembeni yako watoto wako" Alisema Kagaruki kwa sauti ya upole. Mama Kagaruki alirudia kushusha pumzi kwa nguvu huku kijasho kikimtoka kisha akasema. "Nampenda Nyanzala mtoto mwema kwangu hakika najutia kwanini nilimtesa bila kuwa na hatia. .Leo hii wanangu mimi sio waleo wala wakesho muda wowote nakata kauli. Nawaza mtaishije wanangu kwenye hii Dunia hali ya kuwa mkiwa yatima? Baba yenu alifariki kwa ajari ya gari,baba yenu pia mlezi ambae ni baba Nyanzala nae huko alipo sijui atarudi lini. Wanangu nawonea huruma mimi" Alisema Mama Kagaruki huku akilia kwa uchungu kilio ambacho kiliweza kuzua simanzi kwa Kagaruki na dada yake.
"Mama nisaidie chakula japo kidogo ili nipate nguvu za kunifanya niende kuleta maji mtoni" Maneno hayo yalijirudia kichwani mwa Mama Kagaruki. Maneno ya Nyanzala alipokuwa akimuomba chakula. "Usiniombe mimi chakula, kamuombe Mama yako pale nyuma ya nyumba kwenye kaburi lake. Mama Kagaruki alizidi Kulia maladufu huku akijutia kwa kile alichokuwa akimjibu Nyanzala pindi alipokuwa akidai haki yake kama mtoto.
Hivyo kilio hicho kiliweza kustisha kile alichokuwa akitaka kusema Kagaruki ambapo watoto wake walimtuliza kisha wao wakarejea kwenye vyumba vyao kulala huku kila mmoja akiwa na sikitiko ndani ya moyo wake.
Na asubuhi palipokucha,Hamala ndio alikuwa wa kwanza kuamka ambapo alishtuka kuona gamba la nyoka mlangoni kwao,Hamala akamuita kaka yake ambapo yeye alikuwa bado amelala. Kagaruki alipo sikia akiitwa tena kwa mashasha,haraka aliamka akaenda kulishudia hilo gamba la nyoka. Hakika walioigwa na butwaa lakini mwishowe wakashauliana na dada yake kuwa walichome moto hilo gamba. Kweli kagaruki alilinyunyuzia mafuta ya tataa kisha akaliwasha moto,ila wakati gamba hilo likiwa limezungukwa na moto. Upande mwingine nako kule ndani ilisikika sauti ya mama Kagaruki akilia kwa kumtaja Nyanzala mtoto ambae alimnyanyasa kadri awezavyo. Moto ulipokuwa ukizidi kukolea ndivyo mama Kagaruki nae alivyozidi kupasa sauti ya kilio.
Mama Kagaruki alisikika akipiga kelele ndani wakati huo lile gamba la nyoka nalo likizidi kuzungukwa na moto. Lakini cha ajabu lile gamba licha ya kushikwa na moto ila halikuweza kuteketea. "Mama kuna nini mama"Kagaruki alimuuliza mama yake mara tu alipo ingia ndani kwenda kujuwa kitu kinacho msibu Mama yake hadi afikie hatua ya kumtaja Nyanzala huku akilia.,ila licha ya Kagaruki kuhoji kamwe Mama yake hakusema chochote zaidi ya kuangua kilio huku akiendelea kumtaja Nyanzala. Kiukweli Mama Kagaruki alijutia sana alitamani amuone au amsikie Nyanzala Kwa mala ya pili lakini ndio hivyo Nyanzala hakuwepo tena mbele yake au pembeni yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kilio kile cha mama Kagaruki kilidumu ndani ya nusu saa wakati huo Hamala na Kagaruki nao wakiwa wameshika tama hawaelewi wamsaidieje mama yao ambae kimwonekano alionekana sio waleo wala wa kesho. Simanzi kubwa ilitanda malangoni kwakina Kagaruki ila simanzi hiyo ghafla ikakatishwa na jopo la wanakijiji walio onekana kuja nyumbani hapo wakiwa na siraha mbali mbali. Kagaruki akatoka ndani baada kusikia fujo nje. Akataharuki kuona wanakijiji wakiwa na mapanga na mikuki huku baadhi yao wakisema "kijijini kwetu hatutaki wachawi" "ndio ukingundulika kuwa wewe ni mchawi adhabu ni moja tu lazima uchomwe moto" Yalikuwa maneno ambayo yalimshtua sana Kagaruki akaogopa sana akajuwa kuwa tayali kimenuka, Kagaruki alimuita dada yake ili atoke ndani waweze kujitetetea wote. Wakati huo huo wanakijiji hao walionekana kuwa na hasira kali walikuwa tayali wamesha ikalibia nyumba yakina Kagaruki. "Unaona sasa? Hilo si gamba Nyoka? Aaah sasa huu uchawi wao umetosha hapa kijijini kwetu" Alisema mmoja wa wanakijiji waliokuwepo pale. Wakati huo Kagaruki na dada yake wakijaribu kujitetea bila mafanikio ya kusikilizwa. Hivyo punde si punde mzee mmoja aliye fahamika kwa jina moja aliitwa Katabi,aliwaamulu vijana wake waingie ndani ya nyumba ya baba Nyanzala wakakague vitu ambavyo yeye alihisi vimo ndani. Kweli wale vijana waliingia ndani wakatazama kila kona ya nyumba hadi uvunguni,hatimae wakafanikiwa kuapata tunguli ambalo lilikuwa limefunikwa kwa kitamba chekundu.moja kwa moja vijana hao wakatoka nalo ndani. . wanakijiji waliokuwepo pale walistaajabu kuona kitu kile,hata Kagaruki na dada yake wakajikuta wakipigwa na butwa "Ndio maaana huyo mama hakuwa na hata lepe la huruma kwa mtoto wa mwanamke mwenzake kumbe mchawi bwana" alisema hivyo balozi wa nyumba kumi. Hapo hapo yule mzee Katabi akakohoa kidogo kisha akasema "hili pekee ndilo lililozidisha matatizo kwa yule mtoto alie fiwa na mama yake,kwani kwa kutumia tunguli hili ilimfanya baba wa mtoto kutojali kile mtoto asemacho hatakama kipo kwenye ukweli" Alisema yule mzee Katabi huku akiwa ameshikilia tunguli lilitoka ndani ya nyumba ya mama Kagaruki. Na wakati akisema hayo. Upande mwingine wanakijiji walionekana kuwa na ham ya kufanya maangamizi kwa kuichoma moto nyumba ya yakina Kagaruki,na hivyo baada yule Katabi kuongea kwa kirefu zaidi hatimae alulitipa lile tunguli ambapo nalo lilipo tua chini alitokea ndege mweusi akiwa na uzi mweusi mguuni,ndege huyo akaruka na kutoweka zake. Kitendo hicho kilizidi kuzua taharuki,lakini yote kwa yote waligeuka upande mwingine,kwa sauti kali kagaruki akaulizwa "Mama yako yuko wapi" Kagaruki akajibu kwa woga "yupo ndani hali yake sio nzuri" jibu hilo liliwapa nguvu wale wanakijiji kwa kuchukuwa hatua ya kuchoma moto nyumba hali ya kuwa mama kagaruki akiwa ndani.
"Mamaaaaa...mamaaaaaah!" Mayowe yalisikika kutoka kwa Kagaruki na dada yake wakimlilia mama yao huku moto nao ukizidi kutanda kwenye nyumba,mama Kagaruki alishtuka baada kuhisi joto likiongezeka,na punde si punde kipande cha fito chenye moto kilimdondokea kwenye mwili wake hivyo akajuwa tayali nyumba imeshika moto. Hapo sasa akipiga mayowe akiwaita wanae,Kagaruki baada kusikia sauti ya mama yake alitaka kujitosa kwenye moto ili kumuokoa mama yake lakini akazuiwa na mmoja ya wanakijiji. Kwahiyo hadi nyumba yote inateketea Kagaruki aliitazama huku akiishia kulia tu. Mama Kagaruki na roho yake mbaya akawa amekufa na ukatili wake kwa Nyanzala pia dhambi ya kumpa mume wake limbwata akiwa na lengo la kumteka kifikra,ilihali muda huo huo mama Kagaruki anakufa gamba lile la nyoka nalo lilitoweka kimaajabu.
Maisha yakabaki ya Kagaruki na dada yake ambae ni Hamala,ambao nao walitimuliwa kijijini baada ndugu zake baba Maria kuja kuunza kiwanja ambacho kilikuwa na nyumba ya kina Nyanzala. Kumbe marehem baba Maria alimkatia uwanja baba Nyanzala kama ujirani mwema kwani baba Nyanzala alikuwa akiishi shambani kwake na sio kijijini,kwahiyo kitendo kile cha Baba Nyanzala kumuua baba Maria kiliwakera wanandugu wa baba Maria hadi ikafikia hatua ya kuuza eneo lili alilopewa baba Nyazala.
Kagaruki na Hamala wakakimbilia mjini,ambapo huko walianza kuingia katika shunghuli ya kuomba omba huku Kagaruki akitamani japo siku moja akatune na yule binti aliye muona kwa mbaaali akiwa kafanana na Nyanzala.
******
Siku zilisonga miezi nayo ikisogea. Hakika maisha ni kama karata. Ikimbukwe kuwa watoto hao hao Kagaruki na Hamala ndio walikuwa wakimuona Nyanzala kama takataka na hivyo Leo hii nao wanalionja joto la jiwe baada kufiwa na mama yao mzazi ambae ndio alikuwa kikwanzo kwa kigoli Nyanzala. Kiukweli Kagaruki na Hamala walihangaika sana katika jua kali wakiomba walau fedha ya kununulia chakula ili wapoze njaa kitu ambacho ilizidi kuwakondesha. Na siku moja asubuhi mapema Hamala alimueleza kaka yake kuwa anahisi homa na kweli punde si punde Hamala akaanza kutapika matapishi ya njano wakati huo Kagaruki akiwa hana hata shilling mia mfukoni hivyo akawaza atamsaidiaje dada yake? Na hatimae akaamua kutimua mbio kuelekea mtaani kutafuta kibarua chochote ili apate fedha ya kumnunulia dada yake dawa kwa Maana hali ya Hamala haikuwa nzuri hata kidogo,lakini wakati Kagaruki akiwa katika heka heka ya kutaka kuvuka barabara,mara ghafla akagongwa na gari.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kagaruki alipelekwa hospitali baada kugongwa na gari. Wakati huo Hamala nae kule alipo achwa na kaka yake,hali ilizidi kuwa mbaya akaona kama kaka yake kamuacha kwenye mataa na ndipo alipo amuwa kujikongoja kutoka maskani walipokuwa wakilaza mbavu zao,moja kwa moja akajivuta mpaka kando kando ya barabara ambako napo alishindwa kuendelea na safari akaanguka chini kwani hakuwa na nguvu za kusonga mbele kwa wakati ule. Hamala alilalama huku akiomba msaada kwa watembea kwa miguu,hatimae mama mmoja msamalia aliweza kumsaidi kwa kumpeleka nyumbani kwake kuishi nae,na kwa bahati nzuri mama yule hakuwa na mtoto hata mmoja licha ya kuwa na mwanaume pamoja na mali nyingi za kutosha. Hivyo mama yule msamalia aliweza kumpa uhuru Hamala ajisikie kama yupo nyumbani kwao wakati huo tayali amesha pelekwa kwenye matibabu kwahiyo akawa yupo kwenye dozi. Siku ya kwanza iliisha ikafuata siku ya pili hadi ya tatu ambapo Hamala akaanza kumkumbuka kaka yake kipenzi Kagaruki,chakula akawa hali kama inavyotakiwa kwani muda wote alikuwa akimuwaza kaka yake huku sintofahamu ikiwa ndio imetawaala kichwani mwake akishindwa kutambua hali aliyonayo Kaka yake kama ni mzima ama la!
Na wakati Hamala akiwa kwenye hali hiyo,Upande mwingine ilionekana gari ndogo aina ya RAV4,gari hiyo ilionekana ikielekea eneo la hospital na punde si punde ikaegesha eneo maalum la kuegeshea magari ya watu walioleta au kuja kuwaona wagonjwa wao. Na mara baada gari lile kuegeshwa ,ghafla kunako gari hilo alishuka binti wa makamo ambae alionekana mrembo kupita kiasi nae hakuwa peke yake bali alikuwa na msichana mwingine ambae yeye alikuwa mkubwa kupita huyo binti aliyetangulia kushuka kwenye gari. Hivyo mabinti hao walizipiga hatua kuingia hospitalini wakajieleza mbele ya wauguzi kumbe wao ndio walio mgonga Kagaruki kwahiyo walifika hospitalini hapo kwa niaba ya kughalamia ghalama zote kwa mgonjwa Kagaruki ambae kiukweli hali yake ilikuwa mbaya sana. Lakini katika mabinti hao wawili mmoja ambae ndio mdogo alishtuka akajikuta akipigwa na butwaa baada kumtazama Kagaruki. kwa mshangao akasema "Huyu mvulana kama namkumbuka" alisema binti huyo ambae hakuwa mwingine bali ni Nyanzala binti ambae ilisemekana amefariki kumbe Nyanzala hakufa bali baada kupoteza fahamu kwa sababu kutoka damu nyingi sehem ya siri alipo unguzwa na mama yake wa kambo,alipelekwa hospital akaongezwa damu akapata faham. Alipo pata faham mwanakijiji mmoja alidokeza kwa kuwaambia watu waliokuwa maeneo ya hospital kuwa mtoto Nyanzala mahali anapoishi hana amani hata kidogo.Mwanakijiji huyo aliongeza kwa kusema "nibora nyie watu wamjini mumsaidie huyu mtoto kwa kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kuliko huyo mtoto arudishwe kwa mama yake wa kambo"Kweli kutokana na kitendo kile cha kinyama alicho tendewa Nyanzala wengi waliumia sana ambapo alijitokeza mama mmoja kumsaidi Nyanzala. Mama huyo alikuwa na mtoto mmoja wa kike ambae ndio huyo aliyekuja na Nyanzala Hospital kumuona kagaruki baada kumgonga na gari.
Hakika Nyanzala alizidi kuvuta kumbukumbu na mwishowe kumbukumbu ilimjia akaamini kuwa yule ni Kagaruki mtoto wa mama yake wa kambo.. kiukweli Nyanzala alilia saana,hali iliyomfanya yule binti aliekuja nae hospital kumshangaa "Nyanzala unalia nini mdogo wangu? Alihoji yule binti ambae alifahamika kwa jina Pendo. Lakini Nyanzala hakusema chochote zaidi ya kujifuta machozi. Pendo baada kuona hali ile kwa Nyanzala,alifungua pochi yake akafungua akatoa kiasi cha fedha akamkabidhi muuguzi. Kisha akamwambia Nyanzala waondoke mule hospital. Nyanzala alikubali kuondoka klakini alimwachia ujumbe muuguzi kuwa asimruhusu Kagaruki kuondoka hadi pale atakapo rudi tena kumuona.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Baada ya siku nne hali ya kagaruki kidogo ilianza kuimalika,hivyo alipo pata faham alikumbuka kuwa ana dada yake na pia mara ya mwisho alimuacha akiwa na homa kali. Hapo Kagaruki kwanza akijiuliza kafikaje fikaje pale hospital? alipokumbuka kwamba aligongwa na gari akaona sasa haina haja ya kuendelea kukaa hospital, hima aliafanya m pango wa kutoroka pale hospital kweli alifanikiwa japo kwa bahati nasibu kwani wakati alipokuwa akitoroka hakuna muuguzi aliyekuwa kwenye wodi yake.
Mwendo wa polepole Kagaruki alizipiga hatua kuelekea kule alipo muacha dada yake akiugulia homa. Laikini kagaruki hakumkuta kwani Hamala tayali alikuwa ameshapata msaada kutoka kwa mama msamalia. Kagaruki alilia sana kumkosa dada yake akajiona hana bahati katika dunia, wakati huo huo upande wa pili Nyanzala alirejea hospital kumuona tena kagaruki ili waweze kuzungumza japo mambo mawili matatu ikiwemo kuulizia hali ya kijijini tangu wapotezane,Nyanzala akajikuta akishtuka baada kuambiwa kuwa mgonjwa wake katoroka. Kiukweli Nyanzala aliumia sana lakini hakuwa na lakufanya zaidi kuingia ndani ya gari kisha kuondoka zake.
Japo Nyanzala maisha aliyokuwa akiishi ni mtu baki,lakini yalikuwa maisha matamu alikuwa na uhuru wa kufanya chochote chema tofauti na jinsi alivyokuwa akiishi na mama yake wa kambo hapo awali. Ila licha yakuwa katika hali hiyo, Nyanzala bado moyo wake ulionekana kushiba majeraha ya mateso aliyoyapata kutoka kwa mama yake wa kambo. Hatakama akiwa na furaha ila ghafla furaha ile inatoweka kila akumbukapo Yale yaliyowahi kukatisha Elimu yake. Kwingineko Kagaruki alikuwa akihaha kumuulizia dada yake
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wapi ulipo dada yangu? Alijiuliza Kagaruki huku akipiga hatua kuelekea mahali asipo pajuwa kwa muda ule ambao tayali ilikuwa saa za jioni muda ambao mji unakuwa umechangamka. Na wakati Kagaruki akitembea hana hilo wala lile hatimae aliingia kwenye moja ya uchochoro ambako huko alikutana na kundi la vibaka wakivuta bange. Kagaruki aliogopa sana akataka kukimbia lakini ghafla akajikuta tayali kazungukwa na vibaka. Vibaka wale walimkagua Kagaruki kila kona ya mwili wake wakidhania kuwa huwenda Kagaruki ana pesa ili wapate kumtapeli lakini kagaruki hakuwa na hata shilling mia mfukoni mwake.. Vibaka wale baada kuona kagaruki hana pesa,waluchukuwa uamuzi wa kumvutisha bange Kagaruki. Kagaruki alitaka kukataa lakini wale vibaka wakamtishia kumchoma kisu. Hali ambayo ilimuogopesha sana Kagaruki ikabadi avute japo kwa shida. Na wakati akivutishwa bange mara ghafla walivamiwa na kundi la sungusungu. Na moja kwa moja vibaka hao akiwemo na Kagaruki walifikishwa kituo cha police,ambapo taarifa hiyo ya kukamatwa kwa hao vibaka ilirushwa mubashara katika kituo cha ITV.. Hivyo wakati taarifa hiyo ikiwa mubashara,Hamala nae alikuwa makini mno kufuatilia taarifa ya habari kwahiyo akabahatika kumuona Kaka yake akiwa katika wale vibaka. Hamala alifurahi sana haraka kumwona kaka yake,haraka sana akamwambia mlezi wake kuhusu taarifa hiyo,na kwakuwa mlezi huyo alimpenda saana Hamala akamwambia "Usijali Hamala kesho tutaenda kituoni kumtoa! " Hamala alifurahi kuambiwa hivyo hata chakula siku hiyo alikila kwa furaha ya hali ya juu.
Kesho yake asubuhi mama huyo msamalia akiambataba na Hamala walielekea kituo cha police. Hatimae kagaruki akawa amekombolewa,furaha isiyo kifani ilitawala kwa watoto wale Kagaruki pamoja na Hamala. Wakati huo Nyanzala nae akiwa na Pendo walionekana kuja palepale kituoni kwa niaba ya kumkomboa Kagaruki kwani wao pia walimuona kwenye taarifa ya habari baada kukamatwa na police kwa tuhuma za ukabaji. Hatimae Nyanzala akabahatika kuwaona wote wawili Kagaruki na Hamala. Kama ilivyo ada Nyanzala alidondosha machozi huku akisema "Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.. Hamala unanikumbuka? Je, Kagaruki unanikumbuka? Mimi Nyanzala nilikuwa kijakazi chenu katika imaya ya Baba yangu..Mlininyima chakula mkitegemea nile nini? Mama yenu akanikataza kwenda shule akitegemea nini katika maisha yangu? " Alisema Nyanzala kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni..Hamala na Kagaruki walishtuka kusikia maneno yale wote wakaatazama wasiamini kama kweli yule ni Nyanzala. Hakika walidondosha machozi na punde wakamuomba msamaha Nyanzala. Nyanzala akasema "nimeumbwa na moyo wa chuma nilisha wasamehe kitambo,hata yule alienifanya dunia niione chungu nimemsamehe" alisema Nyanzala huku akilia na mwishowe alipanda kwenye gari na Pendo kisha wakondoka zao wakiwaacha Kagaruki na Hamala wakilia kwa simanzi nzito ..lakini nao mwishowe walipanda gari ya yule mama msamalia alie jitolea kumsaidia Hamala kisha wakondoka eneo lile la police. Lakini wakati Kagaruki na Hamala pia yule mama msamalia walipo kuwa njiani wakirejea nyumbani,ghafla walipata ajari baada gari Yao kugongana uso kwa uso na Roli. Katika ajari hiyo hakupona mtu yoyote. Hivyo Hamala na kaka yake wakaaga dunia huku wakiwa na huzuni kubwa moyoni mwao.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment