Search This Blog

TAMBIKO - 4

 







    Simulizi : Tambiko

    Sehemu Ya Nne (4)





    katika kuanga angaza macho Conso akaona kama kunakitu kinatembea kuwafuata,,akasema,,"Baba Maliwa ebu tazama kule! nahisi kama naona kitu kinatembea kuja upande wetu!

    Shinje akageuza shingo yake kutazama..akashtuka kuona kitu kinatembea! macho yakamtoka!!! akatazama kwa umakini akagundua kuwa ni mtu,(mfu aliye hai) akanyanyuka haraka,,akasema ,,"tukimbie

    Conso akakurupuka haraka kutoka pale chini akanyanyuka na kuanza kutimua mbio....walikimbia bila ushirikiano..kila mmoja alipita njia yake!

    walikimbia umbali mrefu kiasi walipotaamaki..Shinje akajikuta yupo peke yake katika njia nyingine.... na Conso alikuwa peke yake uoande mwingine!! Shinje akaamua kuanza kumtafuta mkewe...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo Conso alionekana akiendelea kutimua mbio....akashtuka kujiona yupo uchi...kutokana na uwoga aliokuwa nao aliisahau suruali yake kule makaburini...Conso akajikuta anakuwa nyonge! akasema kwa sauti ya chini,,"aibu gani hii inayonipata mimi huku ukweni! Maliwa mwanangu tazama mama yako napata fedheha kwa ajili ya kukukomboa wewe!!! Eee Mungu nisaide..

    Conso akaendelea kuzipiga hatua huku kajiziba sehemu zake za siri kwa mikono yake,,,macho yake yalitazama kwa tahadhari...alitamani hata Dunia ilasuke atumbukie ndani yake...

    wazo likamjia kuwa arudi kule makaburini kuchukua nguo yake..kuliko fedheha na aibu kubwa itakayompata..akazipiga hatua za harakaharaka kurudi kule makaburini!



    Masaa yalizidi kusonga,,Shinje alimtafuta Conso bila mafanikio yoyote, hatimae pakaanza kukucha! na mbaramwezi ikazidi kumulika baraabara...pakawa na nuru!

    Shinje akakata tamaa akaamua kuondoka na kuelekea nyumbani kwao...

    Masaa yalizidi kusonga mpaka pakapambazuka!

    Conso akaweza kuiona njia ya kuelekea nyumbani kwa mama mkwe wake...lakini akawa na maswali mengi kichwani mwake,,kuwa atawezaje kutembea uchi!



                      **************************



    Upande mwingine alionekana mwanamke mmoja pamoja na mabinti zake wawili...mikononi mwao wakiwa wameshikilia majembe....mama huyo pamoja na mabinti zake walikuwa wanaelekea shambani....wakiwa njiani binti mmoja akamuona Conso akitimua mbio na kuingia kukifuata kichaka kwa lengo la kujificha ili asionekane..kwa sababu yupo uchi!!

    yule binti akasema,,"tazama kule yule mwanamke yupo uchi!

    wakageuza shingo zao kutaza ile sehemu waliyoelekezwa.    .wakashtuka kumuona Conso akiishirizia kichakani..wakaanza kupiga mayowe! huku wakisema,,"jamani kuna mchawi huku!!

    walipiga mayowe mfululizo..mpaka watu waliokuwa wakiishi jirani na eneo hilo wakasikia na kutoka nje ili washuhudie!

    walipofika eneo la tukio wakauliza mchawi yuko wapi?

    yule mama pamoja na mabinti zake wakasema,,"kaingia ndani ya kichaka kile!

    bila kuchelewa wanakijiji hao waliokuwa wamebeba mapanga mikononi mwao wakazipiga hatua kukifuata kichaka hicho...

    wakati huo Conso alikuwa anachunguli kule kichakani akishuhudia yote yanayotendeka...

    wanakijiji hao wakakikaribia kichaka hicho....eneo hilo lilikuwa na wanyama wakali lakini walionekana kwa nadra sana..mara nyingi walijificha kwenye mapango pamoja na kwenye mapori yenye miti mingi...

    punde si punde ,,wanakijiji hao wakavamiwa na simba,,mwenye njaa kali.



    TAHARUKI!!!!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    Simba huyo akamrukia mmoja kati ya wanakijiji hao,,akamrarua na kuanza kumla nyama,,wanakijiji hao wakaanza kutimua mbio! ndani ya sekunde kadhaa ukimya ulitawala eneo hilo.

    wakati huo  Conso alikuwa anachungulia akishuhudia yote yaliyotokea...hofu ikazidi kuongezeka mapigo yake ya moya yalikuwa yanapiga kwa kasi,,mwili wake ulikuwa unatetemeka kwa uwoga wa hali ya juu..Conso aliendelea kuchungulia akamuona simba huyo anaivuruta maiti ya mwanakijiji..na kutokomea porini!

    alipohakikisha simba huyo kaondoka akatoka ndani ya kichaka hicho akatimua mbio kurudi kule makaburini..hapakuwa na umbali,,ndani ya dakika kadhaa,,alifika akaikuta nguo yake akaichukua na kuivaa haraka haraka..akazipiga hatua kutoka nje ya eneo la makaburi....ghafla mzimu wa yule bibi ukamtokea,,Conso akapiga kelele huku anatimua mbio...alikimbia mpaka nyumbani nila kusimama..akamkuta Shinje kaketi nje ya nyumba anaongea na mama yake..Conso akapitiliza mpaka ndani ya nyumba...Shinje na mama yake wakataharuki..wakanyanyuka kumfuata Conso kule ndani ya nyumba.Shinje akauliza kulikoni?

    Conso akasema yule bibi jirani yetu..nimemuona!

    Shije akauliza umemuona wapi?

    Conso akasema,,"kanitokea kule makaburini!

    Kabla Conso hajaongea sentensi nyingine ,,mlango ukajifunga!!!mzimu wa bibi huyo ukajitokeza...kisha mzomu huo ukasema,,

    m-mefanya kosa kubwa kuweka agano na Mizimu. sitowaacha hai.

    Mama shinje akatoa kipande cha mzizi wa mti,,mzizi huo huwa ni dawa ya kufukuza mzimu kwa kuuonyesha mbele ya mzimu...

    Mzimu wa bibi huyo ukatoweka,,baada ya mama Shinje kuonyesha mzizi wa mti maalumu.



                          *************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo huo kule porini,,alionekana Maliwa akihangaika huku kalala chini,,lile umbile lake la kutisha likaanza kutoweka taratibu akabadilika na kuwa binadamu wa kawaida,,akajishangaa yupo uchi wa mnyama! akanyanyuka pale chini akaficha nyeti zake kwa mikono yake akazipiga hatua huku macho yake yakitazama huku na kule, akajiuliza,,"huku ni wapi? nimefikaje?



                   ***************************



    Upande mwingine,kule kijijini kwao Shinje wasiwasi ulizidi kulawa ndani ya nyumba..kila mmoja alikuwa na hofu kupita kiasi!

    Mama Shinje akasema yatupasa turudi kule kwenye msitu wenye mizimu ya mila zetu.

    Conso akajikuta anajuta,,kwa nini ameolewa,akajisemea moyoni,"ni bora ningeolewa na mtu mwingine..huu ukoo wa namna hii hata siuwezi,,

    Mama shinje akasema tusipoteze muda yatupasa tuondoke sasahivi...wakatoka nje ya nyumba wakazipiga hatua kuelekea kule ndani ya msitu.



    wakati huo huo.. mzimu wa yule bibi ukajitokeza kwenye milima ya Rwenzobe,,ni ule mlima ambao yupo kijana Maliwa..

    mzimu huo ukaanza kumtafuta Maliwa,,ukajitokeza mbele yake...ukayoosha mkono wake kwa lengo la kumuangamiza,,lakini  Maliwa alikuwa na nguvu za ajabu,,,nguvu hizi zilitoka kule kwenye msitu wa mizimu ya mila zao..ni baada ya lile tambiko la kuchinjwa mbuzi mweusi,,pamoja na wazaziwake kushiriki kimwili kule makaburini....

    mzimu wa yule bibi ukastaajabu,,ulipojaribu tena kumuangamiza Maliwa likatokea tetemeko la ardhi likiambatana na miale ya moto..

    moto huo ukauchoma zimu wa bibi huyo..ukaangamia na kutoweka..ikawa ndio mwisho wa mizimu huo....

    Maliwa akaingiwa na hofu akaanza kutimua mbio kutoka ndani ya mlima huo..

    alitumia lisaa limoja akawa kafika chini kabisa ya mlima huo...

    kwa mbali akaona nyumba imejitenga peke yake! kando ya nyumba hiyo kulikuwa na nguo zimeanikwa kwenye kamba..

    Maliwa akaifuata nyumba hiyo...alipofika akaangaza angaza macho yake ........akagundua kuwa hakuna mtu ndani ya nyumba hiyo..akaanua suruali na shati akavaa haraka haraka akatimua mbio kuondoka eneo hilo!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya lisaa limoja akafika nyumbani kwao akapakumbuka..alipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa! akaamua kuketi kibarazani,awasubiri wazazi wake..

    aliketi hapo mpaka giza likaingia,,posipo dalili zozote za wazazi wake kurudi nyumbani,,Maliwa akaanza kuingiwa na wasiwasi! akajisemea moyoni,,"wazazi wangu watakuwa wapi? akaamua kujilaza hapo kibarazani...



                       *****************************



    asubuhi palipokucha,,Shinje na Conso wakaamua kurudi Dar es salaam,,ni baaa ya kuambiwa na mizimu kuwa tatizo limekwisha...na mtoto wao amerudi katika hali yake ya kawaida,,Mama Shinje akawasindikiza mpaka kwenye kituo cha mabasi yanayokwenda Dar es salaam..kisha yeye akarudi nyumbani kwake.



    walisafiri kwa masaa mengi..mpaka giza likaingia..mnamo saa mbili za usiku wakawa wamewasili jijini Dar es salaam...wakakodi taxi iwapeleke mpaka nyumbani...walipofika wakaingia ndani ya nyumba yao..



    wakati huo huo alionekana Maliwa akizipiga hatua kurudi nyumbani..akitokea matembezini...alipofika nyumbani akafurahi kuona taa zinawaka upande wa ndani ya nyumba..akagundua kuwa wazazi wake wamerudi,,,akagonga hodi..Shinje akafungua mlango..akastaajabu kumuona Maliwa amekuwa kijana mkubwa..akamkaribisha ndani,,Conso akafurahi sana kumuona mwanae amerudi katika hali yake ya kawaida,,lakini alistaajabu kumuona amekuwa kijana mkubwa!



    ******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*******



    Familia ya Shinje ikaishi kwa amani na furaha,,

    Siku moja maliwa akiwa kala usingizi...akasikikia sauti ikimwambia,,muda na wakati umetimia..kisha sauti hiyo ikatoweka..

    Usiku huo huo kule chumbani kwa Shinje na Conso

    pia sauti hiyo ikasikika ikiwaambia,,muda na wakati umetimia.....inahitajika sadaka ya damu!

    hii ni shukrani kwa mizimu...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TAHARUKI!!!!!





    ************

    ******************

    ************************



    kaba hajamaliza kuongea sentensi.. Maliwa akanyanyuka haraka akamtazama mama yake kwa macho ya msisitizo kisha akamfanyia ishara kuwa akae kimya !  Conso akashtuka !  Maliwa akazipiga hatua akafungua pazia la dirishani akaona kundi kubwa la wachawi wakiwa angani wakija nyumbani kwao.. huku wakiongozwa na mkuu wa wachawi !!!! ikasikika sauti ikimwambia usiogope wala usiteteleke wewe ni shujaa. hakuna kiumbe atakaye weza kukuangamiza,,, ingiza mkono wako kwenye mfuko wa suruali, uliyoivaa kuna simbi mbili,,,

    simbi moja baki nayo wewe na nyingine mpe mama yako !

    wakati Maliwa anatahamaki,,, ghafla lile kundi la wachawi wakiwa wanaongozwa na mkuu wa wachawi,, wakajitokeza ndani ya nyumba hiyo !!wakatapakaa nyumba nzima ! mkuu wa wachawi akajifokeza kule kwenye chumba cha Conso !

    Maliwa alipojaribu kuingiza mkono wake mfukoni ili atoe simbi moja ampe mama lakini akawa ameshachelewa.. mkuu wa wachawi akanyoosha mkono wake ukatoa miale mikali ya mwanga kuelekea pale alipokuwa amesimama Maliwa !!



                                



    mwanga huo wa kichawi ukampiga Maliwa kifuani akadondoka kando! akazitoa zile simbi mbili mfukoni mwake,, kisha akairusha simbi moja pale kitandani kwa mama yake.. akasema,, "mama chukua hiyo simbi uishikilie mkononi mwako,,,

    yule mkuu wa wachawi akamfuata Conso kabla hajaokota ile simbi iliyorushwa na Maliwa pale juu ya kitanda! mkuu wa wachawi akamuwahi Conso kabla hajaolota simbi hiyo,,, akanyoosha mkono wake,, ukatokea upepo ukizunguka kwa kasi! upepo huo ukamchukua Conso akatoweka kimiujiza,, akajikuta yupo sehemu ya kutisha kupita kiasi,,, sehemu hiyo ilikuwa imezungukwa na mafuvu mengi ya vichwa vya binadamu,, pamoja na mifupa!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule nyumbani kwa Conso alionekana Maliwa akiwa anapambana na mkuu wa wachawi,  hatimae mkuu wa wachawi akazidiwa nguvu akatoweka kimiujiza,, kisha ukazuka moshi mwingi ndani ya nyumba! moshi huo ni ishara ya kuwaambia washirika wake wa chama cha kichawi kuwa kuna hali ya hatari waondoke... punde si punde lile kundi la wachawi lililokuwa limetanda ndandi ya nyumba hiyo likatoweka kimiujiza,, pia moshi huo ukatoweka kimiujiza!  Maliwa akazipiga hatua za haraka haraka kutoka chumbani!  akaelekea sebuleni kutazama kama kuna usalama.

    alipoangaza angaza mambo yake,akaona kibuyu.! kumbe kibuyu hicho kilisahaulika,

    mmoja kati ya wale wachawi, alikuwa na kibuyu ,hicho ambacho alikabidhiwa na mkuu wa wachawi kuwa wakimnasa Maliwa.....wafanye jambo la kichawi wamchukue kimiujiza na k UK muingiza ndani ya kibuyu hicho maalumu,,,

    pia ni mwiko mtu yeyote kugusa kibuyu hicho endapo sio mwanachama au mmoja kati ya wahusika wa chama hicho!  na kama kitaguswa basi wale watu wote waliowekwa kwenye lifungo cha mateso kule kuzimu watakuwa huru na watarudi duniani!



                        ********************************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog