Simulizi : Jini Wa Daraja La Salenda
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA; Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wake wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis. SASA ENDELEA... BAADA ya kutoka kwa mganga wakiwa ndani ya gari lao walianza kujadiliana kuhusiana na maneno ya mzee Njiwa Manga. “Sasa tutafanya nini?” “Kwa nini tusiachane naye?” “Mmh! Lazima atatufanyia kitu kibaya, si umemuona ametokwa na machozi ya damu kwa hasira, anaweza kutufanya kitu kibaya.” “Sasa tufanyeje?” “Lazima tutafute njia nyingine, unajua mzee yule nimemtoa akili, shida yake ni fedha na si kutaka kujua tutafanya nini.” “Tena namshangaa anajifanya hataki fedha wakati anafanya kazi ile ili kusukuma maisha yake,” Ashura aliongezea. “Ooh! Nimekumbuka kuna sehemu moja kuna mtaalam mmoja nina imani anaweza kutusaidia. ” Tonny alisema. “Kama ni hivyo tusirudi nyumbani tupitie huko huko maana bado simuamini yule mwanamke
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
amenitisha sana, lakini Tonny asiwe kama mzee Chujio tukaumbuka?” “Namuamini ameshawahi kunifanyia mambo mengi ambayo sikuwahi kukushirikisha, y ule mzee huwa haulizi ukimueleza chochote hata kuua anafanya,tena anapenda kuua kama nini.” “Tena huyo ndiye mzuri sana, lakini tutafika salama?” Ashura alikuwa na wasiwasi. “Sifa ya yule mganga ukiwa na wazo la kwenda kwake kuanzia hapo unakuwa salama hakuna kitu cha kukuzuia.” “Tena huyo anafaa, kwa nini hukusema mapema?” “Nilimuamini babu yule baada ya kujua ana sifa ya kutatua matatizo ya majini.” “Basi tuelekee, leo hatuna kazi nyingine zaidi ya kuujua mwisho wa Balkis.” Safari ilielekea kwa mganga mwingine, njia nzima ilikuwa ni mitihani mingi kutokana na gari kuteleza bila utelezi na kuona mambo ya kutisha lakini safari iliendelea. Matukio hayo yalimtisha sana Ashura kufikia hatua ya kumuomba mwanaume wake wasitishe safari yao. “Tonny kwa nini tusirudi huoni safari yetu imejaa matukio ya kutisha tunaweza kupata ajali mbaya na kufa?” “Shuuna hivi ni vitisho vya Balkis baada ya kugundua tunakwenda kwa mganga mwenye uwezo wa kumuangamiza. Hawezi kutufanya lolote ni kuhangaika kwake kwa mfa maji tu.” “Mmh! Yaani naogopa kuna kipindi niliona mti wa ajabu umetokea ghafla barabarani, nilijua tunakufa na kufumba macho, nilipofumbua nilishangaa kuona tumevuka salama.” “Shuuna hizo ni hila za majini, ule si mti ni kiini macho tu ukiukwepa tu umeumia lazima gari litapinduka.” “Jamani! Ningekuwa mimi ningeukwepa.” “Lazima ungepinduka, barabara hii umepita mara ngapi?” “Mara nyingi tu.” “Huo mti uliwahi kuuona?” “Sijawahi kuuona.” “Basi mimi nimepasua katikati ya mti ule hakuna kitu kilichoizuia gari kupita.” “Mmh! Kweli yule mwanamke ni jini.” “Awe jini mara ngapi?” “Tukipata dawa itatusaidia sana.” “Hesabu tumemkomesha, yule bwana alisema katika dunia hii hawezi kurudisha roho ya mwanadamu tu, kwa vile ni kazi ya Mungu peke yake. Lakini chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kwa uwezo wa Mungu anakifanya kwa ukamilifu.” Baada ya kufanikiwa kuvuka vizingiti vya Balkis walifika Vingunguti walikata kushoto njia ya kuingia Jeti Rumo, waliifuata njia ile mpaka maeneo ya Kijiwe Samli. Tonny alisimamisha gari mbele ya duka moja ambapo pembeni yake kulikuwepo na vijana wakicheza drafti. “Tumefika,” Tonny alisema huku akizima injini ya gari. “Mbona yupo kwenye makazi ya watu?” Ashura aliuliza. “Siku hizi huduma zimewafuata watu, hakuna waganga wa kizamani kuwa kijijini nyumba za majani. Waganga wa siku hizi wanakwenda na wakati hata mavazi yao si kaniki na ngozi na shanga kibao.” Baada ya kufunga gari na kuliacha katika hali ya usalama aliifuata njia ya uchochoro kati ya nyumba ya duka na ya kawaida na kutokea mtaa wa pili walikata kulia kuelekea kwa mganga. “Tonny huku umepajuaje?” “Kuhangaika, unafikiri kama tungekuwa tunamtegemea mzee Chujio peke yake ingekuwaje?” “Mmh! Na kweli, ona kama alivyotutoa nishai yule mzee sijui kunguru, baada ya kifo cha mzee Chujio tungekwenda wapi?” “Atajijua mwenyewe kama anaitwa Njiwa au bundi, mzee yule kanichefua hana lolote kumbe sifa za uongo.” Tonny alimkandia mzee Njiwa Manga. Nini kitaendelea? Kweli mganga huyu ana uwezo wa kumdhibiti Balkis?ILIPOISHIA; “Mmh! Na kweli, ona kama alivyotutoa nishai yule mzee sijui Kunguru, baada ya kifo cha mzee Chujio tungekwenda wapi?” “Atajijua mwenyewe kama anaitwa Njiwa au Bundi, mzee yule kanichefua, hana lolote kumbe sifa za uongo,” Tonny alimkandia mzee Njiwa Manga. SASA ENDELEA... “Nashangaa mganga kupanga cha kumchanjia mgonjwa, mwenye tatizo ni yeye au sisi?” “Waganga wengine miyeyusho tu, tumefika,” Tonny alisema huku akiingia kwenye uzio wa nyumba moja ya kifahari. “Sweet hapa kwa mtu au kwa mganga?” “Nikueleze mara ngapi si wote wanatumia makazi ya kisasa.” “Karibuni,” walikaribishwa na dada mmoja aliyeonekana yupo kwenye meza iliyokuwa na simu ya mezani. “Asante,” walijibu kwa pamoja. “Mzee yupo?” “Yupo na wateja, mnaweza kumsubiri.” Walikaa kwenye sofa kama vile wanataka kuingia kwenye hospitali za kifahari, hali ile ilizidi kumchanganya Ashura. “Sweet, mbona sielewi, hapa ni kwa mganga au hospitali?” “Kwa mganga.” Wakiwa katika ya mazungumzo, msichana aliyekuwa mapokezi aliwashtua. “Sahamani, sasa mnaweza kwenda kuonana na mzee.” “Hakuna tatizo,” alinyanyuka na kuingia katika chumba alichokuwemo mganga. “Karibuni,” mganga aliwakaribisha. Alikuwa tofauti na waganga wengine, alikuwa yupo kwenye chumba chenye kiyoyozi na kukaa kwenye kiti cha kifahari nyuma ya meza iliyonakshiwa kwa vitu vya thamani. Moyoni Ashura aliona yule si mganga bali mjanja wa mjini anayekula fedha za watu kiujanjaujanja na si kwa huduma za kweli. Hakuamini hata siku moja kama kuna mganga wa dawa za asili hajifungi kaniki na chumba kujaa vikapu na chupa za dawa. Swali lake alipanga kumuuliza mpenzi wake baada ya kutoka mle ndani. “Ooh! Mr Tonny za siku mbili tatu?” mganga alimsalimia Tonny kuonesha wanafahamiana. “Nzuri mkubwa.” “Karibuni sana.” “Asante, nimekuja tena.” “Karibu, halafu Tonny ile kazi niliyokufanyia hakurudisha majibu.” “Nilikuwa nije kesho kukueleza, imekwenda kama ulivyonieleza.” “Umepata kile ulichotaka?” “Yaani wewe kiboko, sijawahi kuona mtu kama wewe.” “Tatizo mnakuwa hamuamini, pia nikiwaeleza malipo mnaona kama nawakamua lakini hamjui na mimi natafuta kama nyie. Mimi si mganga anayesema eti nipe sadaka wakati maisha yake yanamkimbiza mchakamchaka. Nataka kukueleza kitu kimoja Mr Tonny, nimepewa uganga ili niwasaidie watu matatizo yao, pia mimi mnipunguzie makali ya maisha. Hebu fikiria mtu nilimtengenezea dawa akaenda machimboni na kupata zaidi ya milioni hamsini, nikiomba milioni mbili mnaona nyingi. Mwingine ameshinda kesi ya ufisadi zaidi ya milioni 150, kunilipa milioni mbili zangu imekuwa shida, mtu kama huyo utamuweka kwenye kundi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/--
gani?” “Kweli ubinadamu kazi.” “Tuachane na hayo, mmh! Mna tatizo gani?” “Kuna jini mmoja anatusumbua,” Tonny alisema. “Jini! Huyo jini mmemjuaje?” Tonny alimueleza kisa kizima cha Balkis, baada ya kumsikiliza kwa makini mganga Kakakuona alisema: “Nimewaeleweni, kazi itafanyika mnavyotaka, malipo yake ni milioni mbili.” “Mbona nyingi?” Tonny alishtuka. “Nyingi? Uhai wa mzee Chujio kutokana na maelezo yenu nani kaulipa, familia yake sasa hivi inateseka kwa ajili yenu.” “Punguza kidogo.” “Haipungui, kazi ya kupambana na jini yule ni kumbwa, heri upambane na jini kisirani, siku zote majini mapole huona yameonewa na vita yake ni kubwa.” “Sawa tutalipa kwa hiyo utatufanyia kazi gani?” “Ninyi mnataka nini?” “Umuue,” alisema Ashura. “Noo, nasikia majini yana fedha, tunataka kinga ili tuipate mali yake?” “Kupata mali yake ni vigumu kwa vile inatumika kijini na si kibinadamu.” “Sasa utatusaidia vipi?” “Vyovyote lakini tofauti na hilo.” “Basi fanya kama alivyosema mwenzangu.” “Hakuna tatizo, tangulizeni milioni kesho njooni na iliyobaki ili tumalize kazi.” “Tuna laki tano tu kwenye gari.” “Leteni hizo nyingine kesho.” Wakati Tonny akienda kwenye gari Balkis alikuwa pembeni ya nyumba ya mganga, moyo wake kila dakika ulijaa hasira na kuona hakuna haja ya kuwaonea huruma. Kila alivyokuwa akimuangalia Tonny alitamani kumvaa lakini kila alipomsogelea alipoteza uwezo wake. Roho ilizidi kumuuma na kuona kama anafanya mzaha ambao ungemletea madhara mwishowe. Baada ya kurudi na mkoba wa fedha walizoombwa na mganga, Balkis aliendelea kufuatilia mazungumzo ya kina Ashura na mganga, aligundua kuwa mganga alikuwa amekubali kuwapa kinga pia mganga alikuwa na dhamira mbaya ya kuua. Ile ilimfanya akose raha na kutokwa na machozi, alipata wazo la kuwahi chini bahari kabla uchawi wa kuua haujafanywa. Lakini alikumbuka ana deni na baba yake la kuachana na Muddy, mwanaume aliyepanga kuachana naye baada ya kumpa ujauzito.... Itaendelea
Ilipoishia: ILE ilimfanya akose raha na kutokwa na machozi, alipata wazo la kuwahi chini ya bahari kabla uchawi wa kumuua haujafanywa. Lakini alikumbuka ana deni na baba yake la kuachana na Muddy mwanaume aliyepanga kuachana naye baada ya kumpa ujauzito ambao wazazi wake hawatakuwa na nguvu na kumruhusu aishi naye. Sasa endelea... ALIJIKUTA akiuapia moyo wake kuwa atapigana mpaka tone la mwisho la damu yake lakini hatarudi chini ya bahari. Akiwa amesimama pembeni ya nyumba kwenye mti wa jirani katika umbile la njiwa, alijiuliza atafanya nini ili aweze kujiokoa na hatari ile. Alishuhudia Ashura akitoa laki tano kwenye mkoba na kumpatia mganga ambaye alinyanyuka ili akachukue vifaa vya kutengengeneza dawa ya kummaliza. Balkis juu ya mtu alijikuta akipoteza uwezo wake wa kawaida baada ya kuamini wakati wowote anaweza kufanyiwa kitu kibaya. Alijua waganga wengi huwavuta majini kwa dawa na kuwamaliza, akiwa ametota kwa jasho kwenye manyoya yake kwa hofu ya kifo. Alimuona mganga akitoka uani kwake na kumwita mkewe aliyekuwa akizungumza na wanawake wenzake. “Mke wangu,” alimsikia akimwita mkewe kwa sauti ya juu kidogo. “Abee mume wangu,” alimuona mkewe aliyekuwa amevalia nguo na vito vya dhahabu kila kona kuonesha kwamba wanaishi maisha ya kifahari. “Hebu nenda dukani kaniletee ile kiboko ya majini.” “Kuna mtu ana jini nini?” Alimuuliza huku akipokea fedha. “Kuna jini mmoja anawakosesha raha wateja wangu.” “Sasa unataka kumfanya nini, unataka kumtia kwenye chupa nini?” “Namuulia mbali, unajua jini ukilifungia kwenye chupa likitoka linaweza kukumaliza. Dawa yake sasa hivi ni kulimalizia mbali, itakuwa wakijua wanakuja Kakakuona watakuwa wanakimbia wenyewe.” “Ngapi nichukue?” “Kwa vile nammaliza kazi kabisa nichukulie tano na ndimu kumi na nne na sindano kumi na nne.” “Mmh! Mbona nyingi sana leo umepania.” “Nimemuona ana kiburi, pia ana mchezo wa kutaka ushindani, nikimfunga anaweza kutoka, si unajua siku hizi watu wakikuta kitu lazima wakifungue.” Kauli ile ilimshtua Balkis ambaye aliamini siku ile ndiyo ilikuwa ni mwisho wa maisha yake, wazo la haraka lilikuwa ni kurudi kwao na kuwa tayari kukubaliana na matakwa ya baba yake ya kuachana na Muddy ili awe salama. “Mmh! Haya kazi kwenu,” mkewe mganga alisema huku akitokea mlango wa nyuma kwenda duka la dawa za asili. Balkis alimuangalia mke wa mganga na kumuona ni mweupe asiye na kinga imara ya kuzuia nguvu za majini, kutokana na kukataa kuchanjwa na mumewe. Kwa vile mumewe alimpata baada ya kuja kutibiwa kutafuta dawa ya kuolewa na kigogo mmoja na mganga akamgeuzia kibao cha kutengeneza dawa ambayo ilimfanya yule mwanamke ampende mganga badala ya mtu aliyemkusudia. Baada ya kufanikiwa kumpata, ilibidi akubaliane na mkewe ambaye hakutaka kuishi kiganga zaidi ya maisha ya kifahari ya kujirusha kwa kutembelea gari. Kutokana na uwezo wa mganga wateja wake wengi walikuwa watu wenye uwezo hivyo kumfanya asiwe na shida ya fedha ndogo ndogo. Pamoja na mkewe kutoishi kama mke wa mganga na muda wote kuvaa nguo na vito vya thamani, bado alikuwa akijua baadhi ya dawa ambazo zilikuwa zikitumiwa na mumewe. Hata pale mumewe alipokuwa safarini alielekezwa jinsi ya kuzitengeneza na kuwapa wateja lakini mumewe alipokuwa nyumbani yeye aliendelea na maisha yake ya kujiachia. Balkis aliona ile ndiyo nafasi yake ya kufanya kitu kitakachomfanya mganga asifanye lolote juu yake. Alikurupuka kutoka juu ya mti kama njiwa na kumgonga kichwani mke wa mganga ambaye alikwenda juu na aliporudi chini hakuomba hata maji. Waliokuwepo pembeni walimuona njiwa mweupe akimgonga kichwani na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Kelele na kilio cha mtu aliyeingia kwa mganga zilimshtua mganga aliyekuwa ameanza kuandaa vifaa vya kummaliza Balkis. Aliacha na kutoka na kukutana na mfanyakazi wake wa mapokezi. “Vipi?” alimuuliza baada ya kumuona amechanganyikiwa. “Mama.” “Amefanya nini?” “Ame....” “Yupo wapi?” aliuliza huku presha imempanda. “Yupo nje ya nyumba.” “Kafanya nini?” “Si...sijui.” Mara alisikia sauti za vilio vya mashoga wa mkewe ambao walikuwa wakizungumza naye muda mfupi uliopita, vilio vile vilizidi kumtisha na kumchanganya. “Jamani kuna nini?” Aliuliza tena macho yakiwa yamemtoka pima.
ILIPOISHIA; Mara alisikia sauti za vilio vya mashoga wa mkewe ambao walikuwa wakizungumza nao. Vilio vile vilizidi kumtisha na kumchanganya. “Jamani kuna nini?” aliuliza tena macho yakiwa yamemtoka pima. SASA ENDELEA... “Sauda,” walisema mashoga zake waliokuwa wakilia huku mikono ikiwa kichwani, wengine hata nguo ziliwaanguka bila kujua. “Sauda kafanya nini?” “Ame...” “Amefanya nini mbona mnanichanganya, mke wangu kafanya nini jamani?” mganga alijikuta kwenye mtihani mzito wa kujua mkewe amefanya nini kwani muda mfupi uliopita alimtuma dukani. Mara aliingia mwanamke mwingine aliyekuwa akilia huku akisema: “Haiwezekani Sauda atutoke kirahisi namna hii.” “Huu lazima uchawi haiwezekani njiwa amgonge afe,” mwingine alisema huku akijitupa chini kwa uchungu. “Jamani mke wangu kafanya nini?” pamoja na kuwasikia wakisema lakini hakuwaelewa. Mara watu waliingia na mwili wa mkewe ambaye alikuwa amekwishapoteza uhai. \“Ha! Amefanya nini?” Kakakuona alitaharuki. Alimvamia mkewe ambaye
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alikuwa amefunikwa kanga, akamfunua na kumwinamia! Hakuamini alichokiona mbele yake. “Sauda mke wangu umepatwa na nini? Kwa nini nilikutuma kwenda kuchukua dawa? Kwa nini nilikuwa na wazo baya? Maskini mke wangu nimekuponza, ulikuwa ukizungumza na wanawake wenzako, ona sasa umebadilika jina na kuitwa marehemu! Nini faida ya kazi yangu?” Mganga alilia kama mtoto mdogo huku akimgeuza mkewe ambaye alikuwa ameanza kupoa. Ashura na mwanaume wake nao walikuwa wametoka na kushuhudia tukio lile. Balkis naye hakuwa mbali, moyo ulimuuma kwa kitendo chake cha kuyachukua maisha ya kiumbe kisicho na hatia. Machozi ya damu yalimtoka. Kila mganga alipokuwa anamlilia mkewe kwa maneno ya uchungu na yeye ndivyo alivyokuwa akiumia na kulia zaidi. Ashura alipoangalia pembeni alishtuka baada ya kumuona Balkis akiwa katika kundi la watu huku naye machozi yakimtoka. Baada ya kumuona alipatwa na mshtuko mkubwa, akaanguka na kupoteza fahamu. Hali ile iliwatisha watu wote waliokuwa pale. Mganga alimwacha mkewe na kukimbilia ndani kuchukua dawa ya unga kwa ajili ya kuzuia nguvu zozote mbaya. Aliimwaga hewani lakini Balkis aliwahi kuondoka eneo lile na kwenda kukaa njiani kuwasubiri Ashura na mwanaume wake. Mganga baada ya kufanya vile bado hakuamini, aliuchukua mwili wa mkewe na kuuingiza ndani kujaribu tiba zote anazozijua akiamini atafanikiwa kumrudisha mkewe. Alikuwa amesahau kuwa hakuna mtu wala kiumbe chochote dunia chenye uwezo wa kurudisha roho ya mtu au kiumbe zaidi ya Muumba peke yake. Licha ya kuhangaika zaidi ya saa nzima kurudisha roho ya mkewe iliyopotea, bado hakufanikiwa. Hatimaye alikubaliana na ukweli kwamba mkewe amefariki. Ilibidi atoe taarifa za kifo cha mkewe kwa ndugu na jamaa, mipango ya mazishi ikaanza. Kutokana na kuchanganyikiwa na kifo cha mkewe alisahau hata kama kuna wateja aliokuwa akiwashughulikia. Ashura baada ya kupata nafuu alijikuta akichanganyikiwa kwa kuamini kabisa kifo cha mke wa mganga kimefanywa na Balkis. Wasiwasi ulizidi kumpanda na kujiuliza kama ni yeye basi hata maisha yao yalikuwa hatarini. “Tonny nimemuona Balkis?” “Wapi?” “Alikuwa kwenye kundi la watu.” “Mwongo!” “Kweli! Tena alikuwa analia machozi ya damu.” “Mungu wangu! Unataka kuniambia aliyefanya haya ni yeye?” “Inawezekana kabisa, si unakumbuka kauli aliyotoa kwa mzee Njiwa Manga kuwa kama angetusaidia angemuua mjukuu wake.” “Sasa unafikiria anaweza kutufanyia kitu kibaya?” “Hata mimi nimechanganyikiwa.” “Sasa mganga atatusaidia nini?” Tonny aliuliza huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi. “Wee! Tena nyamaza, inavyonekana sisi ndiyo chanzo cha kifo cha mkewe.” “Kwa hiyo unaniambia nini?” “Tuondoke, ikiwezekana tusirudi tena na Balkis tuachane naye,” Ashura alisema huku akitetemeka. Wakati huo watu walizidi kusogea eneo la tukio, kila mtu alikuwa akisema lake juu ya kifo cha ghafla cha mke wa Kakakuona. Wapo walioelezea jinsi walivyomuona njiwa yule akimpiga kichwani mke wa mganga na kutoweka kisha kuanguka chini na kupoteza uhai. “Kweli kabisa Balkis ndiye aliyemuua mke wa Kakakuona,” Tonny alipata uhakika. “Sasa unaona tumechokoza nyuki wakati hatuna mbio.” “Sijui tufanye nini ili Balkis atuelewe?” “Nimekueleza tuachane naye.” “Atatuelewa?” “Mmh! Kazi ipo, kama amejua tunataka kumuua unafikiri atatufanya nini?” Ashura alisema kwa sauti ya kukata tamaa. “Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, kwa nini tusiendelee kuwa hapa ili mganga atupe hata kinga ili asitudhuru?” “Tonny hebu kuwa na akili, umesikia aliyefanya vile ni Balkis mganga atatufanya nini, hiyo milioni mbili yako itarudisha roho ya mkewe?” “Mmh! Na kweli, kwa hiyo unasemaje?” Je, nini kitaendelea?
ILIPOISHIA “Hatuna jinsi “Huu si wakati wa kulaumiana tutafute njia ya kujiokoa kwa Balkis.” “Mmh! Huoni tukitafuta mganga mwingine ni sawa na kuongeza mafuta kwenye moto?” “Sasa tutafanya nini?” Tonny alionesha kuchanganyikiwa na kusahau kama wanatakiwa kuondoka eneo lile na badala ya kujilaza kwenye usukani. SASA ENDELEA... “Tonny hebu ondoa gari kama huwezi nipishe miye niendeshe.” “Ashura njoo uendeshe nina imani Balkis anajua mimi ndiye mbaya wake namba moja, hata sijui itakuwaje?” “Tonny we twende nyumbani lolote litakalotokea tuwe tayari kukabiliana nalo.” “Mmh! Haya sina jinsi yaani najuta kumfahamu Balkis.” “Lakini si tumeambiwa ni kiumbe mwenye huruma?” “Si umesema umeona akitokwa na machozi ya damu kuonesha hasira unafikiri mtu tuliyetaka kumuua atakuwa na huruma na sisi?” “Bwana wee hebu tuondoke mengine tutayajua huko huko.” Tonny alijikaza na kuwasha gari kisha waliondoka eneo la Kiwalani, Balkis aliwaona kwa mbali wakija, akiwa amejawa na hasira kutokana na kiburi walichokionesha alikosa adhabu inayowafaa kutokana na roho zao mbaya ili wasirudie tena kumfuatafuata. Adhabu aliyoipanga ilikuwa kuhakikisha kwanza anamtia aibu Ashura na mumewe kwa kumgeuza kiumbe wa ajabu asiyependwa na wanadamu au wanyama. Hakutaka kuwasumbua aliwaacha warudi mpaka nyumbani kwao ili aweze kufanya alichokikusudia. Ashura na mwanaume wake walishangaa kwenda mpaka nyumbani kwao bila kukutana na tatizo lolote, walipofika walishukuru Mungu. Baada ya kuingia ndani hata kabla hawajakaa vizuri mlango uligongwa, Tonny alikwenda kuufungua na Ashura alikwenda chumbani. Alipofungua alipatwa na mshtuko uliomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu. Ashura aliyekuwa chumbani alishitushwa na kishindo cha mtu kuanguka chini, alimwita mwanaume wake huku akitetemeka ili ajue kimetokea nini. “Toooni,” aliita kwa sauti ya juu bila kupata jibu, woga ulimwingia. Alirudia tena kumwita Tonny bila jibu lolote, alitoka chumbani huku akiwa na wasiwasi, kabla ya kufika sebuleni alisikia harufu ya manukato aliyoyazoea kuyasikia wakati Balkis akiwa karibu yake. Harufu ile ilimjulisha tayari walikuwa wamevamiwa ndani ya nyumba yao. Mlangoni alikuwepo Tonny aliyekuwa amelala chini, alianza kutetemeka. Akiwa bado katika hali hiyo, mlango uligongwa tena, alitamani kurudi chumbani kwake lakini alijikaza na kusogea hadi mlangoni na kuufungua. Alipofungua alikutana uso kwa uso na Balkis, kwa woga alioupata haja ndogo ilimtoka bila kutarajia. “Samahani Balkis,” aliomba msamaha huku akipiga magoti kwa kujua kiama kimefika. “Ya nini?” “Najua nimekukosea.” “Kosa gani?” “Unajua, naomba usituue.” “Kuua ni kazi ya Mungu peke yake si ya kiumbe chochote.” “Mbona ume..,” Ashura alisita kusema Balkis kamuua mke wa mganga Kakakuona kwa kuhofia kumzulia jambo ambalo huenda hakulitenda na kumuongezea hasira. “Nimefanya nini?” “Hujafanya kitu.” “Najua ulitaka kusema nini.” “Ha...ha...pana,” Ashura alitetemeka kwa hofu. “Kwanza mmwagie maji mwenzako azinduke, nashangaa anakuwa mwoga wakati yeye ni bingwa wa kutoa roho za watu.” “Naomba unisamehe Balkis najua kiasi gani tumekuudhi.” “Hebu fanya kwanza niliyokuagiza,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo. Ashura alikwenda jikoni na kurudi na maji kwenye bakuli. “Mmwagie kidogo kichwani.” Ashura alifanya kama alivyoelekezwa, baada ya kumwagia maji mwanaume wake alirudiwa na fahamu. Tonny alipozinduka alishtuka kujikuta yupo mbele ya Balkis. Alinyanyuka na kupiga magoti mbele ya Balkis kuomba msamaha. “Samahani Balkis najua umekuja
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kutudhuru, lakini tunakuhakikishia hatutarudia tena kukufuata,” Tonny alisema huku akitokwa na machozi. “Kabla ya kuzungumza lolote naomba Ashura aende akajisafishe, siwezi kuzungumza na mtu aliyejipaka najisi.” Ashura alikwenda bafuni kujisafisha kisha kubadili nguo na kurudi mbele ya Balkis bila kujua nini hatima yao baada ya kumchokonoa kwa muda mrefu. Baada ya kurudi alisogea kwa mwanaume wake na kuungana naye kupiga magoti. “Naomba mkae chini, magoti yenu yataniongeza hasira niwageuze kuwa manyani” Baada ya kukaa alimuuliza Ashura swali lake la awali.” “Ashura, uliuliza mbona nimemuua mke wa mganga?” “Ha...ha...pana sikumaanisha hivyo.” “Naona unataka kunichefua nikugeuze kuwa nyoka sasa hivi muuaji mkubwa, hivi mimi nikifa ninyi mtafaidika nini?” Hakuna aliyejibu kitu, wote walibakia kimya nyuso zao wamezielekezea chini kwa aibu.
. ILIPOISHIA: “Naomba ukae chini, magoti yenu yataniongeza hasira niwageuze nyani.” Baada ya kukaa alimuuliza Ashura swali lake la awali.” “Ashura ulisema mbona nimemuua mke wa mganga?” “Ha..ha..pana sikumaanisha hivyo.” “Naona anataka kunichefua nikugeuze nyoka sasa hivi muuaji mkubwa wewe, hivi mimi nikifa ninyi mtafaidika nini?” Hakuna aliyejibu kitu, wote walibakia kimya wakiwa wameangalia chini kwa aibu. SASA ENDELEA... “Kwa kweli wanadamu ni viumbe wenye kiburi kuliko kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu. Matendo yenu mabaya kuliko hata ya shetani. Shetani siku zote humvuta mtu kwenye dhambi lakini si kuua. Ninyi kila kukicha mnatoa roho za watu kwa ajili ya mali. Mmesababisha nimuue mke wa mganga bila sababu kutokana na nia yenu ya kuhakikisha nakufa. Jamani kosa langu nini, kama Hemed mliachana baada ya kumfilisi, sasa hivi umemuona mzuri?” Ashura hakujibu kitu, aliendelea kuinama na kumfanya Balkis aendelee kuzungumza kwa hasira huku machozi ya damu yakizidi kuichafua nguo aliyokuwa amevaa. “Kwa vile mmekuwa kenge msiosikia mpaka mtoke damu masikioni, sasa chagueni adhabu yoyote ila iwe mbaya kuliko zote zilizowahi kutolewa chini ya jua.” “Tunaomba utusamehe,” walisema kwa pamoja huku wakitamani kunyanyuka kwenda kumlamba miguu. “Sitawasamehe, lazima niwape adhabu kubwa sana ambayo hata mimi mtekelezaji itaniuma moyoni mwangu kwa jinsi mtakavyoteseka,” Balkis alisema kwa hasira. Wote walibakia kimya wakishindwa kujua wachague adhabu ipi, kila adhabu waliyoifikiria ilikuwa nzito kwao. Baada ya kukaa kimya, Balkis alisema huku akitembea taratibu ndani ya nyumba na kuifanya nyumba inukie vizuri: “Ashura, adhabu yako ya kwanza ni kutembea uchi mbele za watu kama tulivyokubaliana, baada hiyo itafuata nyingine ambayo nitaijua mwenyewe.” “Na wewe,” alimgeukia Tonny aliyekuwa amejikunyata kwa hofu ya maisha yake. “Tena wewe ndiye nitakayekufanya kitu kibaya, kwanza nitakugeuza nzi wa kijani maisha yako yawe chooni na jalalani, adhabu nyingine nitajua hapo baadaye.” “Ni semehe Ba..ba..lki....” “Shatap mashetani nyie,” alimkata kauli kwa sauti kali. “Nina imani mzee Njiwa Manga aliwaeleza vizuri japo mwanzo hata mimi niliwaeleza lakini mlijitia viburi, sasa kiburi chenu kitawatokea puani.” “Tusamehe hatutarudia tena.” “Hebu niambieni kosa langu nini?” aliwauliza huku akiwa amewakazia macho. “Hu..hu..na kosa.” “Sasa kwa nini mnataka kuniua?” “Tu..tu..sa..sa..mehe.” “Nina imani uwezo wangu mlikuwa hamuufahamu lakini leo ndiyo mtaujua.” “Balkis haki ya nani tunakuahidi hatutarudia tena,” walirudia kupiga magoti mbele yake. “Hivi mngefanikiwa kuniua haya magoti mngempigia nani? Kumbukeni nimepata dhambi kwa ajili ya mtu mwingine hivyo lazima nitimize nilichopanga kuwafanyia.” Wakati wakizungumza yale, Balkis alihisi mabadiliko mwilini mwake yaliyomfanya ahisi kizunguzungu kikali. Kwa haraka alishika kwenye paji la uso na kutoweka mle ndani. Ile hali ilimtisha na kuamua kwenda moja kwa moja chini ya bahari kuwahi kujisalimisha kwa wazazi wake. Wasiwasi wake ulikuwa huenda mganga ameamua kulipa kisasi baada ya mkewe kuuliwa. Akiwa amechoka alijivuta huku kizunguzungu kikizidi, akatembea kwa kujivuta huku akipepesuka lakini alipofika lango kuu la kuingilia kwenye jumba la mfalme alianguka chini na kupoteza fahamu. Vijakazi na watwana walifika na kumuokota hadi ndani ya jumba kuu akiwa hajitambui kabisa. Malkia Huleiya alishtuka kupata taarifa za kuletwa Balkis akiwa hajitambui, akiwa na kanga mkononi alikimbilia sebuleni na kumkuta Balkis akiwa amelazwa chini akiwa hajitambui. “Amefanya nini?” aliuliza kwa mshtuko. “Hatujui Malkia Mtukufu,” walijibu kwa pamoja. “Mmemkuta wapi?” “Lango kuu Malkia Mtukufu.” “Mpelekeni chumbani mara moja.” Walimbeba na kumpeleka chumbani na kumlaza kitandani, baada ya kumlaza walitoka. Malkia Huleiya alichanganyikiwa na kujiuliza mwanaye kafanywa nini na wanadamu. Alijua ile itakuwa vita na wanadamu ambao ni viumbe hatari aliokuwa akiwaogopa usiku na mchana.
“Mpelekeni chumbani mara moja.” Walimbeba na kumpeleka chumbani na kumlaza kitandani, baadaye walitoka. Malkia Huleiya alichanganyikiwa na kujiuliza mwanaye kafanywa nini na wanadamu. Alijua ile itakuwa vita na wanadamu ambao ni viumbe hatari aliokuwa akiwaogopa usiku kucha. SASA ENDELEA... ALITAKA kwenda kumwita mumewe Mfalme Barami aliyekuwa kwenye kikao na baraza lake la mawaziri lakini alipata wazo la kumfuata mganga mkuu Bunusa ili akaangalie hali ya Balkis. Alimtuma mtwana kumfuata mganga mkuu Bunusa. Bunusa alifika mara moja na kupelekwa chumba alichokuwa amelazwa Balkis ambaye muda wote alikuwa amepoteza fahamu. “Bunusa naomba msaada wako hali ya mwanangu ni mbaya sana.” “Hakuna tatizo,” Bunusa alisema huku akifungua mkoba wenye vitendea kazi. Alimshika Balkis kichwani, kifuani, tumboni na miguuni kisha alimshika kwenye paji la uso na kutulia kwa muda akipata ripoti za uchunguzi wa mwili wake. Baada ya muda alipumua pumzi nyingi kuonesha kuna jambo. Malkia Huleiya akimfuatilia kutaka kujua vipimo vile vina majibu gani. Baada ya kuvuta pumzi ndefu alimgeukia Malkia Huleiya na kumwambia: “Balkis haumwi ugonjwa wa kutisha ni hali ya kawaida.” “Bunusa, Balkis hajatokewa na hali hii toka nilipomzaa, leo atokewe na tukio la kutisha useme hana ugonjwa wa kutisha?” “Nimesema hali aliyonayo si ugonjwa, ila tatizo kubwa ni uchovu, inaoneka kafanya kazi kwa mwezi mzima bila kupumzika. Kutokana na hali aliyokuwa nayo lazima hali hii imtokee.” “Hali! Hali gani hiyo?” “Ya ujauzito.” “Unasema ana nini?” “Ana ujauzito ambao hakujua kama anao na ndiyo uliomfanya kuchoka baada ya kufanya kazi nzito.” “Mungu wangu ujauzito wa nani, wa jini au mwanadamu?” Malkia Huleiya aliuliza huku akiweka mkono wake kifuani kuzuia mshtuko. “Wa mwanadamu.” “Ooh! Mbona mwana huyu amenitafutia matatizo, baba yake nitamweleza nini anielewe.” “Ni kweli hili ni tatizo inaonesha taarifa hizi za kupata ujauzito wa mwanadamu zitakuwa na mpasuko mkubwa ndani ya familia.” “Sasa nitafanya nini? Tuutoe kabla baba yake hajajua?” “Mmh! Katika kosa lingine kubwa mtakalofanya ni kuutoa ujauzito huu, nia kubwa ya mwanao ni kubeba ujauzito na kuzaa na mwanadamu kisha arudi kwa baba yake kwa kuamini hatakuwa na jinsi tena ya kuzuia matakwa yake.” “Ooh! Sasa Bunusa utanisaidia kitu gani ili kutoleta
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mtafaruku mkubwa.” “Dawa ni kumrudisha duniani ili aendelee na maisha yake na mumeo asijue chochote.” “Tutafanyaje?” “Nitampa dawa ya kumrudisha katika hali yake kisha arudi duniani kuendelea na maisha yake.” “Lakini watwana na vijakazi wanajua alikuja, si watamwambia?” “Hao ni wa kuwaita na kuwaeleza wasizungumze chochote kuhusiana na Balkis na kutoa vitisho vikali.” “Sawa nitafanya hivyo.” Mganga mkuu Bunusa alianza kumshughulikia Balkis kwa kumnusisha dawa iliyomfanya apige chafya na kuzinduka. Balkis alijishangaa kuwa mbele ya mama yake na mganga mkuu Bunusa. “Mama,” alimwita kwa sauti ya chini. “Abee mwanangu, unaendeleaje?” “Sijambo kidogo, baba yupo wapi?” “Yupo kwenye baraza na mawaziri wake.” “Mmh! Siamini kama nipo salama, asante Bunusa nilijua ndiyo basi.” “Ndiyo basi kwa vipi?” Malkia Huleiya alimuuliza mwanaye. “Nilijua mganga niliyemuulia mke wake kaamua kunimaliza.” “Ni kweli alikuwa na wazo la kukumaliza lakini kiburi chako ndicho kilichokusaidia,” mganga Bunusa alisema. “Ni kweli alinitumia kombora?” “Walaa.” “Sasa nini kile?” “Ni kizunguzungu kikali, inaonesha umefanya kazi ngumu bila kupumzika na kusababisha uchoke sana.” “Mmh! Mbona kazi hiyo ni ndogo, nimekwishafanya nyingi zaidi ya hizo bila matatizo.” “Ni kweli, lakini sasa hali yako haikuruhusu kuusumbua mwili kwa muda mrefu.” “Hali! Hali gani?” “Ya ujauzito.” “Ujauzito?” Balkis alishtuka huku akishika mikono kifuani kwake. “Eeh, vipi hukuutegemea?” Bunusa alimuuliza. Swali lile ambalo lilikuwa zito kulijibu mbele ya mama yake, Malkia Huleiya alimgeukia mwanaye aliyekuwa bado amekaa kitandani.
Swali lile lilikuwa zito kulijibu mbele ya mama yake, Malkia Huleiya alimgeukia mwanaye aliyekuwa bado amekaa kitandani. SASA ENDELEA... “Balkis.” “Abee mama.” “Kwa nini umefanya hivi?” “Mama sina jibu lakini ndivyo nilivyoamua.” “Na vizazi vya wanawake unavyoleta vitakuwa na kazi gani?” “Kama kweli nina ujauzito kazi hiyo itakuwa imeishia hapa, siwezi kupata dhambi kila kukicha kisa niolewe na jini mwenzangu. Majini wangapi wanaishi na wanadamu maisha ya furaha, itakuwa mimi!” “Lakini kumbuka baba yako akijua una ujauzito wa mwanadamu utafia chumba cha giza.” “Na wewe mama utakubali?” “Japo siwezi kukubali lakini kumbuka kauli ya mwisho ni ya baba yako, vile vile anaweza kutufungia wote kwenye chumba cha giza.” “Kwani anajua nina ujauzito?” “Hajajua lolote, hata ujio wako hatutaki ajue. Si unajua bado una kesi ya kuachana na mwanadamu.” “Ni kweli, lakini nikitoka hapa nitarudi na mtoto.” “Ila nakuomba acha kuingia katika vita na wanadamu ili upate muda wa kupumzika ulee mimba yako, bila hivyo itatoka na kukufanya usizae tena hata ukitumia dawa za kijini,” Bunusa alimshauri Balkis. “Kabla ya kupumzika lazima niwape adhabu ambayo itakuwa fundisho kwao.” “Kweli mwanangu wamekuudhi, pamoja na huruma yako umeshindwa kuwasamehe? Kweli wamekuudhi,” mama yake naye alichangia. “Niwasamehe watu waliopanga leo kunibakiza jina, wale watu wabaya sana, lazima niwatie adabu.” “Basi ondoka ili uwahi kabla baba yako hajamaliza kikao, naona huu ndiyo muda wao wa kumaliza.” Balkis alimuaga mama yake na mganga mkuu Bunusa kisha akarudi zake duniani. *** Baada ya Balkis kuondoka, ghafla Ashura na mwanaume wake walishindwa kuelewa nini kinaendelea. Walibaki wamepiga magoti wakisubiri hukumu yao. Muda nao ulikwenda bila kuonekana Balkis. Kutokana na woga wa kumuudhi Balkis waliendelea kupiga magoti mpaka giza lilipoingia. “Tonny sasa itakuwaje?” Ashura alimuuliza mwanaume wake baada ya kuhisi miguu imekufa ganzi kwa kupiga magoti kwa muda mrefu. “Hata sijui atakuwa amekwenda wapi.” “Sasa tutateseka hivi mpaka saa ngapi?” “Lakini sisi ndiyo tuliolazimisha kupiga magoti!” Tonny alikumbuka. “Kwa hiyo tunyanyuke?” “Mmh! Hata sijui tufanye nini.” “Tutaendelea kukaa hivi mpaka saa ngapi? Bora tunyanyuke tukae ili tusubiri atakachotufanya kwani hatuna jinsi,” walijikatia tamaa ya maisha kwa kuamini adhabu watakayopewa ni kubwa sana. Ashura na mwanaume wake walinyanyuka walipokuwa wamepiga magoti na kukaa kwenye kochi kusubiri hukumu ya Balkis. Walikaa huku wakiendelea kumuomba Mungu awaepushe na kikombe kile cha adhabu ya Balkis. Usiku uliwachwea wakiwa wamekaa kwa kuogopa kuwa wakinyanyuka wanaweza kuongeza hasira za Balkis. Siku ya pili iliingia wakiwa wamekaa kwenye kochi bila kumuona wala kusikia sauti yake. Tonny kwa kujitoa muhanga alimwambia Ashura: “Shuuna sasa tutakaa hivi mpaka lini? Kwa nini tusinyanyuke tuendelee na mambo yetu? Litakalotokea hatuna jinsi.” “Mmh! Kwa nini tusisubiri, huenda ametutega ili aone tutafanya nini,” Ashura alikuwa na hofu ya kuzidi kumuudhi Balkis. “Sasa tutakaa mpaka lini hebu angalia toka jana hatujala wala kunywa chochote, kama kosa tumetenda na hayupo tayari kutusamehe tutafanya nini?” Walikubaliana kuendelea na kazi huku wakisubiri chochote watakachofanyiwa na Balkis ambaye muda wote hakuonekana. Kutokana na uchovu wa usiku na mchana, baada ya kuoga hawakuwa hata na hamu ya chakula, walipanda kitandani na usingizi mzito uliwashika. Waliamka jioni wakiwa wamechoka, baada ya chakula cha usiku walirudi kulala huku wakisubiri adhabu ya Balkis bila mafanikio. Siku ile pia ilikatika bila Balkis kuonekana, waliamua kufanya mambo yao kama kawaida huku wakiapa kutomfuatilia tena Balkis na kuamua kuishi maisha yao ya kawaida. *** Balkis baada kurudi kutoka chini ya maji alikuwa na furaha isiyo na kifani baada ya kugundua dhamira yake ya kubeba ujauzito wa mwanadamu imetimia. Alimkuta Muddy akiwa amejilaza kitandani, alipofika alimkumbatia na kumbusu kama ilivyokuwa kawaida yake kila alipoondoka na kurudi baada ya siku moja bila kuonana. Itaendelea
ILIPOISHIA; Balkis baada kurudi kutoka chini ya maji alikuwa na furaha isiyo na kifani alipogundua dhamira yake ya kubeba ujauzito wa mwanadamu imetimia. Alimkuta Muddy akiwa amejilaza kitandani, alipofika alimkumbatia na kumbusu, japo jambo lile lilikuwa ni la kawaida kila alipoondoka na kurudi baada ya kukaa siku moja bila kuonana na mpenzi wake. SASA ENDELEA... LAKINI siku ile furaha iliongezeka mara mbili kitu kilichomshtua Muddy. “Vipi mpenzi kulikoni mbona una furaha sana?” “Muddy niambie zawadi yoyote unayoitaka kwangu nikupe.” “Ya upendo.” “Muddy ya kitu kingine kwani hakuna kiumbe nitakayempenda chini ya jua kama wewe.” “Sihitaji zawadi zaidi ya hiyo.” “Basi mimi nakuchagulia zawadi ya kuyafanya maisha yako yawe kama ya peponi hata kama sipo.” “Ina maana unataka kuniacha?’ “Hapana mpenzi ni tahadhari tu, mimi ni kiumbe siwezi kuishi milele.” “Nashukuru kwa hilo.” “Nikwambie kitu?” “Niambie.” “Nina ujauzito wako.” “Utani huo!” Muddy alishtuka kusikia vile. “Ndiyo maana nimejawa na furaha isiyo na kifani na nikifanikiwa kujifungua salama nitakupa zawadi kubwa sana isiyo na mfano.” Balkis alimkumbatia Muddy kwa furaha huku akiomba ajifungue haraka kabla baba yake mfalme Barami hajatimiza dhamira yake ya kuvunja mpango wa uhusiano wake na Muddy ili aolewe na jini mwenzake. **** Balkis baada ya kupata habari njema za kupata ujauzito wa Muddy, alikuwa mwenye furaha kupita kiasi. Lakini aliamini furaha yake ingekamilika baada kuwakomesha wabaya wake. Adhabu aliyoipanga ingemfanya aishi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwa furaha mpaka muda wa kujifungua lakini hakutaka kuwaua. Wakati akipanga adhabu ya kuwapa Ashura na mwanaume wake, upande wa pili ulishangaa kuona siku zikikatika bila kusikia chochote kutoka kwa Balkis. Waliamua kufanya kazi zao kama kawaida huku wakiachana kabisa na Balkis. Ashura akiwa katikati ya mji akiendelea na mambo yake ya ununuzi wa vitu muhimu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Balkis naye alikuwa karibu yake bila mtu yeyote kumuona. Alipomkaribia aliokota udongo kidogo kisha alimpulizia mwilini. Ashura akiwa amebeba mfuko mkubwa akielekea kwenye gari alihisi kama kuna vitu vinamuwasha mwilini. Ilibidi aweke mzigo chini ili ajikune kwanza, kila muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyohisi nguo zake zikimuwasha kama vile zimemwagiwa upupu. Alianza kuvua nguo huku akipiga kelele za kuwashwa, kila mtu alishtuka na kumshangaa kumuona mwanamke akivua nguo zote na kubakia mtupu. Wasamaria wema walimsogelea na kumvisha lakini alizikataa nguo zake na kusema zinamuwasha. Ilikuwa ni kihoja Ashura aliadhirika mbele ya watu, kila alipopewa nguo na kinamama waliokuwa wameshikwa na mshangao kumuona mrembo kama yule akionekana amepandwa na mapepo. Ashura aliondoka pale na kuanza kutembea bila ya kuwa na kitu mwilini, alielekea baharini. Ilikuwa ni adhabu aliyokubaliana na Balkis kama atamfuata Muddy aliyekuwa mumewe wa zamani. Baada ya kuridhika na adhabu yake alimtokea kwa mbele akiwa na upande wa kanga. Ashura alipomuona alipiga magoti kumuomba msamaha. “Balkis najua jinsi gani tulivyokukosea lakini sasa hivi tumeachana na wewe, naomba utusamehe.” “Adhabu ya kutembea uchi nani aliichagua?” “Mimi.” “Sasa mbona hukutaka kutembea uchi baada ya kujua kabisa dhamira yako ilikuwa nini juu ya Muddy?” “Nisamehe Balkis.” “Balkis unayemuomba akusamehe angefariki ungemuomba nani msamaha?” “Najua tulikuwa na dhamira mbaya kwako lakini tumegundua makosa yetu tunakuahidi hatutakufuata tena.” “Nilikuonyeni mara ngapi, kama ningekuwa na roho mbaya hata mali ya Muddy usingechukua. Lakini nilifanya vile ili muachane na mpenzi wangu, bado hamkusikia mliendelea kunichokonoa, kuonesha sitaki kuwafanya lolote nilimuua mganga wenu lakini bado mliendelea kunitafuta. “Mzee Njiwa Manga alitukutanisha mbele yake na kukuonyeni lakini bado mliona labda utani na kufikia hatua ya kumdharau kuwa hana uwezo wa kukabiliana na mimi. Mkaamua kwenda kwa mganga mwingine kwa lengo la kuchukua mali yangu na kunimalizia. Hebu nieleze ni kiumbe gani mwenye moyo wa uvumilivu wa kiasi hicho?” “Hakuna.” “Basi adhabu yangu ya awali ya kukutembeza uchi baada ya wewe mwenyewe kutamka kwa mdomo wako imetimia kama utamfuata Muddy. Ya pili nitakugeuza mbwa atakayeishi kwa mateso mpaka hapo nitakapojifungua salama. Kama mwanangu akifariki na wewe na mumeo mtakufa.” “Ni...ni...ni..sa...sa...,” hakumaliza kusema alitemewa mate usoni na Balkis huku akisema: “Kuwa mbwa mweusi.” Ashura aligeuka mbwa mweusi, Balkis aliendelea kusema: Kazi imeanza Ashura ameshageuzwa mbwa.
. ILIPOISHIA; Ya pili nitakugeuza mbwa atakayeishi kwa mateso mpaka hapo nitakapojifungua salama. Kama mwanangu akifariki na wewe na mumeo mtakufa.” “Ni..ni..ni..sa..sa..,” hakumaliza kusema alitemewa mate usoni na Balkis huku akisema: “Kuwa mbwa mweusi.” Ashura aligeuka mbwa mweusi, Balkis aliendelea kusema: SASA ENDELEA... “Hii ni adhabu itakayokufanya uhangaike, hutapendwa na wanadamu mpaka hapo utakapotoka kifungoni na sasa namfuata mwanaume wako, naye ana adhabu kubwa kuliko hii.” Balkis baada ya kusema vile aliondoka na kumuacha Ashura kwenye umbile la mbwa asijue aende wapi. Wazo lilikuwa kuendelea kuwa pale ufukweni mpaka jioni ndiyo aende kwake. Nyumbani, Tonny alikuwa akijiandaa kwenda kwenye mihangaiko yake akiamini kabisa Balkis aliamua kuwasamehe. Alikuwa anakwenda kwenye kabati kuchukua glasi ili anywe juisi kabla ya kuondoka. Hakujua kama Balkis tayari yumo mle ndani na alikuwa na hasira za ajabu baada ya kujua Tonny ndiye aliyekuwa na kimbelembele wa kumuua. Wakati anakwenda kwenye kabati alimpulizia vitu kama matone ya maji, Tonny alishtuka lakini hakujali sana. Alipokaribia kwenye kabati alishtuka kujiona amegeuka kiumbe wa ajabu. Kilichomshangaza ilikuwa ni kujiona kwenye kioo mwili wake ukiwa umeota mizizi na kutoka damu. Tonny alishtuka na kujiangalia, akawa anashangaa kuuona mwili wake ukiota mizizi iliyoingia ardhini huku ukitoa damu. Alianza kusikia maumivu makali zaidi ya mtu aliyeng’olewa jino bila ganzi. Alijiuliza yale mateso makali yanatokana na nini na kwa nini aote mizizi mwilini kama mti lakini hakupata jibu. Balkis alimwacha apate mateso makali kwa kuongeza kumpulizia maji maji mwilini na kuufanya mwili wa Tonny utoe ufa, kila sehemu ya mwili ilipasuka, damu zilimtoka na maumivu yake yalikuwa makali sana. Kila alipopiga kelele kuomba msaada sauti yake haikutoka. Alitamani ardhi ipasuke ili immeze lakini haikuwezekana. Alishangaa kuona damu yake iliyokuwa ikitoka mwilini, kila ilipondondoka chini ilipotea, akajiuliza inakwenda wapi lakini hakupata majibu. Maumivu aliyoyasikia hakukuwa na mfano wake. Alilia mpaka machozi yalimkauka kutokana na maumivu kuongezeka ukali kila dakika kutokana na mwili wake kupasuka kila kona. Balkis alitoa adhabu ile kwa zaidi ya saa mbili kisha alijitokeza mbele yake, Tonny alipomuona alishtuka na kutamani kumlamba miguu lakini hakuweza kutembea baada ya sehemu ya mwili wake kuzama chini ya ardhi. Kila alipofumbua mdomo kuomba msamaha sauti haikutoka akawa anarusha mikono kama anaimbisha kwaya bila ujumbe wake kumfikia mlengwa. Balkis alisimama na kumtazama kwa hasira, mara machozi ya damu yalimtoka akifikiria ampe adhabu gani kubwa kuliko zote alizowahi kumpatia kiumbe aliyemchukiza. Alitamani kumchuna ngozi na kumwacha atembee na maumivu bila kufa lakini alikumbuka adhabu ya kupasua pasua mwili ilikuwa inatosha kwani maumivu yake yalitofautiana kidogo na mtu aliyechunwa ngozi bila ganzi. Tonny aliendelea kurusha mikono kuomba msaada kama mtu aliyekuwa anataka kukata roho. Aliusikia mwili wake ukiwa umekauka kama kipande cha kuni kilichopigwa na jua kwa muda mrefu. Ulimi nao ulikauka kama mti na kushindwa hata kuunyanyua. Yalikuwa mateso makali kuliko hata shetani motoni, moyoni Tonny alijiapia kama atatoka salama kwenye mateso yale mazito asingerudia tena kufanya makosa. Aliona kuokoka kwake ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano. Balkis alijikuta akiingiwa na huruma, alisogea karibu na kumshika kichwani. Dakika ileile Tonny alirudi katika hali ya kawaida lakini bado mwili wake ulimuuma kama kidonda. Tonny alipiga magoti mbele ya Balkis kuomba msamaha. “Najua tumekukosea, lakini nakuahidi hatutafanya upumbavu mwingine, tupo chini ya miguu yako, tunaomba utusamehe.” “Sawa mmekosa, hebu nielezeni kosa langu kwenu ni nini?” “Huna kosa lolote.” “Kwa nini mlidhamiria kuniua?” “Tusamehe Balkis ni shetani mbaya tu alitupitia.” “Leo unaniomba msamaha, ningekufa ungemuomba nani?” “Najua tumekukosea kwa kiasi kikubwa.” “Labda mlikuwa mnaona natania, mwenzako nimempa adhabu ya kutembea uchi mbele za watu muda si mrefu.” “Ha!” Tonny alishtuka kusikia vile. “Unashtuka nini, si alisema mbele yako akimrudia Muddy atafanya nini?” “Atatembea uchi.” “Mbona kamfuata mume wangu kupitia waganga.” “Nilikuwa sijui.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Najua tumekukosea kwa kiasi kikubwa.” “Labda mlikuwa mnaona natania, mwenzako nimempa adhabu ya kutembea uchi mbele za watu muda si mrefu.” “Ha!” Tonny alishtuka kusikia vile. “Unashtuka nini, si alisema mbele yako akimrudia Muddy atafanya nini?” “Atatembea uchi.” “Mbona kamfuata mume wangu kupitia waganga hakutembea uchi?” “Nilikuwa sijui.” SASA ENDELEA... “Utajuaje na roho yako imejaa tamaa na harufu ya damu za viumbe wasio na hatia?” “Ni kweli nilikuwa na roho mbaya lakini nimeujua ubaya wangu, nitajirekebisha.” “Kama nilivyokueleza Ashura amevua nguo mbele za watu na kupata aibu ya mwaka.” “Mungu wangu yupo wapi?” “Atakuja usiku kwa njia ya kujifichaficha.” “Kwa hiyo nguo kavua kwa hiyari yake?” “Kwani wewe adhabu uliyoipata umeipenda?” “Hata.” “Au nikuongeze?” “U...u...usifanye hivyo ni...ni...” “Baada ya tapeli mwenzako kuvua nguo mbele za watu, na kumpa adhabu ndogo aliyoichagua mwenyewe pia nimempa adhabu yangu atakayotesekanayo kwa muda mrefu.” “Ungemsamehe nina imani hawezi kurudia tena,” Tonny alimuonea huruma Ashura na kujisahau yeye. “Kwa sasa sitawasamehe lazima nitimize kile nilichokipanga kuwafanyia.” “Usituue Balkis.” “Niliapa kamwe sitawaua ili kizazi chenu kijue madhara ya ubaya ni nini?” “Sasa utatufanya nini?” “Mpenzio tayari nimeshamgeuza kuwa mbwa.” “Mungu wangu!” “Na wewe kama nilivyokueleza nitakugeuza kuwa nzi wa kijana, maisha yako yatakuwa jalalani na chooni hakuna mwanadamu atakayekupenda.” “Jamani si nitakufa?” “Hutakufa, hayo ndiyo maisha niliyowachagulia baada ya kuwabembeleza kwa muda mrefu, Lakini mmekuwa na viburi pamoja na kuwatisheni bado mkawa na masikio magumu kama kenge, nina imani adhabu ya leo itakuonesha mimi ni kiumbe wa aina gani. Kwa vile sitaki dhambi ya kuua na kisasi ni haki ya kila kiumbe, nilichokuchagulia ndicho saizi yako.” “Balkis naomba uni...sa...sa... “ Bwana wa Ashura hakumalizia kuomba msamaha alipuliziwa kitu kama unga huku Balkis akisema: “Kuanzia leo utakuwa nzi wa chooni.” Muda uleule Tonny aligeuka kuwa nzi wa kijani, ghafla mazingira ya pale nayo yakabadilika na kumfanya Tonny kuruka na kwenda moja kwa moja jalalani. Alijikuta akiishi maisha mapya ambayo yalimlazimisha kuishi chooni na kwenye majalala. Tonny pamoja na kuishi kwenye harufu kali ya mizoga na kinyesi hakuwa na jinsi kwa kuamini kuwa maeneo yale ndiyo yaliyokuwa salama kwake kwa kuogopa kuuawa na mwanadamu pale atakapokwenda ndani mwake kwa kuamini kuwa yeye ni binaadamu. Balkis baada ya kutoa adhabu ile alirudi kuilea mimba yake kwa kuamini kuwa hakukuwa tena na mwanadamu atakayemfuatilia maisha yake. Balkis alikuwa akiyafurahia maisha yake na Muddy kwa kuamini muda si mrefu wataitwa baba na mama. Baada ya kiza kuingia, Ashura aliondoka ufukweni na kurudi nyumbani akiwa katika umbile lake la mbwa. Alitembea huku akiomba Mungu afike salama nyumbani kwake, moyoni akijiuliza Tonny atamuelewa kutokana na umbile lake jipya alilokuwa nalo, alifikiria hivyo bila ya kujua kwamba mpenzi wake naye maisha yake yalikwishabadilika na kuwa kiumbe cha jalalani na chooni baada ya kugeuzwa kuwa nzi. Hakutembea umbali mrefu mvua kubwa ilianza kunyesha, alikimbilia kwenye nyumba moja iliyokuwa njiani na kujibanza upenuni. Mwenye nyumba alitoka na kumfukuza akiamini ni mbwa. Kutokana na mvua kuwa kubwa na barabara kujaa maji, Ashura alijitahidi kumwambia yule mwanadamu kuwa yeye si mbwa bali ni mwanadamu. Sauti yake ilikuwa ni ya mbwa kwa kuwa aliitoa kwa kubweka, tu hicho kilizidi kumuuzi mwenye nyumba ambaye aliingia ndani na kutoka na bakora na kumtoa mbio. Ashura hakuwa na jinsi ilibidi aingie kwenye mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha huku akiogelea kwenye maji machafu yaliyokuwa yakitoka kwenye mitaro. Aliendelea kunyeshewa na mvua kubwa iliyoambatana na radi, kuna kipindi alizama ndani ya maji na kujitahidi kuogelea ili kuendelea na safari yake. Hata alipopata sehemu ya kujibanza bado hakuona umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na kusikia baridi kali mwilini mwake iliyotokana na kulowana kwa mvua. Aliendelea na safari yake yenye mateso huku akitaka amkute Tonny nyumbani na kuomba amtambue na kukubali kuishi naye kwenye umbile lile la mbwa.
ILIPOISHIA: Alitembea ndani ya maji katika mvua kubwa ya radi, kuna kipindi alizama ndani ya maji na kujitahidi kuogelea na kuendelea na safari yake. Hata alipopata sehemu ya kujibanza bado hakuona umuhimu wa kujibanza kutokana na kusikia baridi kali kutokana na kulowa mwili wote na maji. Aliendelea na safari yake yenye mateso ya shetani motoni huku akiomba Mungu amkute Tonny nyumbani pia amtambue na kukubali kuishi naye kwenye umbile la mbwa. SASA ENDELEA... Alishangaa kutembea umbali mrefu bila kufika, alijikuta akichoka huku njaa kali na kiu ikiwa imemshika na kushindwa kujua atakula wapi. Alipofika eneo ambalo alijua ndipo kwao alishangaa kuona hakuna nyumba yao, alizunguka mpaka kuna kucha huku akiteseka na baridi kali bila mafanikio. Ashura alitamani kifo lakini kilikuwa mbali naye, alijiuliza mateso yale mpaka lini au ndiyo ya kudumu lakini hakupata jibu. Alitamani amuone Balkis mbele yake ili amueleze ya moyoni kuwa amekoma na hatarudia tena katika maisha yake. Katika hali ya kawaida aliamini kabisa Balkis hakuwa na kosa lolote, japo walitaka kumuua mateso yale yalikuwa makubwa heri angemuua akajua moja lakini si mateso ya kutengwa na jamii kwa kumchukia kila atakapokwenda kwa kujulikana mbwa kumbe mwanadamu yalikuwa makubwa sana. Wakati akiteseka vile, Tonny naye alikuwa kwenye mateso mazito pembeni ya jalala kwenye tawi la mti uliokuwa na afadhali kutokana na mvua kuwa kubwa sana. Baada ya mvua kukatika aliendelea kukaa kwenye tawi lile ambalo mvua haikufika sehemu ile kama ingefika aliamini angekufa. Lakini chini yake kulikuwa na mzoga wa mbwa aliyekufa siku mbili zilizopita na kutoa harufu kali ambayo iliongezeka baada ya kunyeshewa na mvua. Harufu ilikuwa mbaya sana lakini hakuwa na jinsi, aliendelea kuvumilia kwa kuhofia kupoteza maisha yake kutokana na eneo lote kuwa na maji ya mvua iliyokuwa inanyesha kwa nguvu. Yalikuwa mateso makubwa kutokana na adhabu ya kuvuta harufu kali ya uchafu na mizoga. Njaa na kiu ilikuwa kali pamoja, licha ya umbile la kugeuzwa nzi bado alikuwa na akili za binadamu asingeweza kula mizoga wala kinyesi. Aliamini asingefikisha siku nyingi lazima angekufa kwa njaa. Aliwaza kama Balkis angetokea mbele yake angemuomba amuue kuliko kumtesa vile, kama siku moja hali ilikuwa vile kwa mwezi mzima ingekuwaje. Majira ya saa tisa za usiku akiwa amejikunyata kwa baridi kali la usiku kucha aliamshwa usingizini. Alipofumbua macho hakuamini kumuona Balkis mbele yake, alitaka kufunua mdomo wake kumuomba msamaha, lakini angewezaje kuzungumza katika umbile kama lile la nzi. Balkis alimchukua na kwenda naye sehemu na kumtemea mate, palepale Tonny alirudi katika umbile lake la kawaida. Alikuwa amemletea chakula kitamu, alimkaribisha. “Karibu chakula, najua huwezi kula chakula cha nzi ambacho ni kinyesi na uchafu kwa vile wewe bado mwanadamu.” “Ba..ba..ba..lkis naomba u..uni..samehe,” Tonny alipiga magoti huku akitetemeka. “Tonny sikuja kusikiliza msamaha wako, ulishaomba sana siku za nyuma, nimekuletea chakula kula niondoke.” “Basi niue kabisa chakula hiki sili,” Tonny alionesha jeuri kwa Balkis. “Tonny hunijui hata kuwaletea chakula kizuri ni huruma yangu, lakini mlitakiwa mle kinyesi na uchafu.” “Nimesema sili niue kabisa,” Tonny alionesha jeuri kwa Balkis kuonesha yupo tayari kwa lolote. “Tonny usinione nakuchekea ukaniona ni bwege mwenzio, sasa hivi nitakugeuza funza maisha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
yako yawe ndani ya kinyesi usiniletee upumbavu unijue eeh! Alaa,” Balkis alibadilika na kusema kwa hasira huku macho yake yakiwaka kama taa na usiku ule yalikuwa kama tochi yenye mwanga mkali. “Ba..ba..si ni..ni.. ” “Nyamaza mpumbavu mkubwa wewe, ni kiumbe gani anayeweza kuwaletea chakula na maji baada ya kutaka kumuua zaidi ya mara mbili?” Balkis alimuuliza huku amemshikia kiuno na kitumbo chake kilionekana kwa mbali. “Na..na..te..seka Balkis harufu ni mbaya sana naomba unitafutie adhabu nyingine.” “Huwezi kunichagulia adhabu kwa vile muda wa kubembelezana ulikwisha, hebu maliza kula nataka nimpelekee na mwenzako, muda unakwenda kukipambazuka ujue hali mpaka kesho kama saa hizi.” Tonny hakuwa na jinsi, alikula chakula kile kilichokuwa kitamu ajabu, hakuwahi kula chakula kitamu kama kile, alikuwa akijiuliza Balkis ni kiumbe gani pamoja na ubaya waliomfanyia bado kawaletea chakula kitamu na maji. Moyoni aliamini huenda atamsamehe. Lakini ilikuwa tofauti na alivyodhania baada ya chakula ambacho alishiba vizuri na kunywa maji matamu, alimpulizia vitu kama unga, vilipomgusa usoni palepale aligeuka hali yake ya mwanzo ya nzi........JE NINI KITAENDELEA?
ILIPOISHIA; Lakini ilikuwa ni tofauti na alivyodhania baada ya kula chakula ambacho alishiba vizuri na kunywa maji matamu, Balkis alimpulizia vitu kama unga vilipomgusa usoni, palepale aligeuka hali yake ya mwanzo ya nzi. SASA ENDELEA ... Alitamani kuomba msamaha lakini alichelewa, alichukuliwa na kurudishwa kwenye tawi la mti na kukumbana tena na harufu kali ya uchafu wa mzoga wa mbwa aliyekuwa akinuka. Kwa harufu ile kama angekuwa katika umbile la kibinaadamu basi angetapika mpaka utumbo. Lakini bahati nzuri alikuwa kwenye umbile la nzi, aliendelea kuteseka na harufu na baridi kali. Balkis baada ya kutoka kwa Tonny alikwenda moja kwa moja kwa Ashura aliyekuwa amelala pembeni ya nyumba mbovu. Karibu yake kulikuwa na mtaro wa maji machafu lakini yeye aliichagua sehemu iliyokuwa kavu. Lakini ukali wa ubaridi ulikuwa ukimpata kisawasawa. Alijuta kwa mambo yote aliyoyafanya kwa kuwatepeli wanaume kwa ajili ya Tonny ambaye ndiye aliyemuingiza kwenye kazi ile ya kuolewa na wanaume na mwishowe kuwadhulumu kwa kuvunja uhusiano. Kitu kilichowafanya wanaume zaidi ya wawili kujiua baada ya kufilisika na wengine kupatwa na ukichaa. Aliamini hali ile ingemtokea na Muddy lakini kwa bahati ya ajabu Balkis aliyaokoa maisha yake. Alitamani Balkis atokee mbele yake amuombe msamaha lakini hakuonekana. Usingizi ulimpitia pale alipokuwa amejilaza huku akichonyotwa na njaa pamoja na kiu. Alishtuliwa kutoka usingizini na kujiona akiwa mbele ya Balkis, kama Tonny alivyotaka kuomba msamaha, naye alikuwa kama anataka kumuuma Balkis aliyemchukua na kumpeleka sehemu iliyokuwa nzuri, alimtemea mate na muda uleule alibadilika kurudia katika umbile lake la kibinadamu. Ashura baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida alipiga magoti mbele ya Balkis na kuanza kuomba msamaha. “Balkis nisamehe sana nimekosa, adhabu ya leo inatosha hali yangu ni mbaya,” alisema huku akibubujikwa na machozi. “Hii si adhabu ya siku moja ni ya muda mrefu kama nilivyokueleza muombeni Mungu nijifungue salama, kama mwanangu akifa au mimba ikitoka mjue na nyinyi maisha haya yatakuwa ya milele kwenu.” “Naomba unisamehe, sitarudia tena, niliyokutananayo leo yanatosha, ukiongeza zaidi nitakufa.” “Ashura sikufuata kuombwa msamaha, nimekuletea chakula, kula haraka kabla hapajakucha, ukichelewa utalala na njaa, kuonana na mimi tena ni mpaka kesho muda kama huu, tapeli mwenzako kanichelewesha na wewe unataka kufanya hivyo.” “Nani, Tonny?” “Eeh.” “Yupo wapi?” “Yupo jalalani.” “Anafanya nini?” “Kwani nzi makazi yake wapi?” “Mungu wangu umemgeuza kuwa nzi?” “Tena ana bahati angeendelea kuniletea ujeuri ningemgeuza kuwa funza na makazi yake yangekuwa kwenye kinyesi milele.” “Sa...sa...” “Ee...eeh! Hebu kula niondoke.” Ashura hakuwa na jinsi alikula chakula kitamu na kuamini kama Balkis ameamua kumletea chakula ambacho hakuwahi kula katika maisha yake ya kibinaadamu, lazima atakuwa amerudiwa na roho ya huruma na kumsamehe. Lakini dhana yake ilikuwa ni tofauti, baada ya kumaliza kula alirudishwa katika umbile lake la mbwa na kurudishwa alipotolewa na Balkis akatoweka. **** Siku zilikatika huku adhabu ya Ashura na mwanaume wake zikiendelea, walikuwa wakiteseka kwenye maumbile yao ya mbwa na nzi. Maisha ya Tonny yalikuwa ya jalalani na chooni japo hakuweza kula uchafu. Ashura maisha yake yote yalikuwa ni kuzurura jiji zima kutafuta sehemu iliyokuwa salama kutokana na kukimbizwa kila kukicha na watoto watukutu. Mimba ya Balkis iliendelea vizuri na baadaye alijifungua salama salmini watoto mapacha wa kike na kiume, kila mmoja alifanana na mzazi wake mmoja. Wa kike alifanana sana na mama yake na wa kiume alifanana na baba yake. Balkis alifurahi sana na kuamini dhamira yake ilitimia. Aliamua kwenda chini ya bahari na wanawe kuwatambulisha kwa wazazi wake, wakati akiwa njiani kuelekea chini ya bahari. Baba yake Mfalme Barami alikuwa na mazungumzo mazito na mkewe juu ya kukosa taarifa za Balkis. “Mke wangu hivi huyu mtoto anataka kupimana nguvu na mimi?” “Kwani tatizo ni nini?” “Hulioni? Tangu nilipomueleza aachane na yule mwanaume amepotea, haleti tena vizazi vya wanawake mwaka unakatika.” “Mume wangu jambo hili linatakiwa busara siyo kutumia nguvu.” “Kama anaona ni utani, nitamtuma Pweku mtwana mkuu akamuulie mbali huyo mwanaume wake.” “Mume wangu unatafuta vita mpya.” “Na nani?” “Siamini kama Balkis atakubali kirahisi mwanaume wake auliwe, atawamaliza watwana wako wote kwa kuwaua.” “Inamaana sasa hivi mwanao anataka kunipanda kichwani?” Walinyamaza kuzungumza baada ya kusikia kelele za chereko chereko nje, zilikuwa ni shamrashamra zilizowashangaza wote. Msafara ulikuwa ukiingia ndani, ukiongozwa na vijakazi na watwana akiwemo mtwana mkuu Pweku, sherehe kama ile hutumika kukaribisha mgeni aliyezaliwa. Balkis alionekana akiwa juu kwenye farasi mwenye matandiko ya dhahabu. Mama yake Balkis Malkia Huleiya alipowaona watoto wa Balkis, alikimbia kwenda kumpokea mwanaye na wajukuu zake kwa furaha ya ajabu. Mfalme Barami alikuwa amebaki njia panda, asielewe kilichokuwa kikiendelea mpaka wageni wale walipokuwa wakiingia ndani, hakujua watoto wale aliokuwanao Balkis walikuwa ni wa nani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ILIPOISHIA: Mama Balkis, Malkia Huleiya alipowaona watoto wa Balkis alikimbia mbio kwenda kumpokea mwanaye na wajukuu zake kwa furaha kubwa. Mfalme Barami alikuwa bado yupo njia panda, mpaka wanaingia ndani hakujua watoto aliokuwa nao Balkis ni wa nani. SASA ENDELEA... BAADA ya kuingia ndani, Balkis alijua amefanya makosa. Alipiga magoti mbele ya baba yake na kusema: “Mtukufu mfalme wa bahari, najua nitakuwa nimefanya kosa kubwa la kuzaa na binadamu, lakini sikuwa na jinsi. Nimefanya hivi kutokana na moyo wangu kuwa na hofu kuu kwa Muumba wetu. Niliamua kukaidi amri yako na kufunga ndoa na binadamu ambaye niliamini atanisaidia kupata watoto ambao ndiyo ilikuwa kiu yangu kubwa. Pia nilijua nitaepukana na dhambi ya kuvunja ndoa za watu pia kuwanyima watu haki zao za kupata watoto. Najua nimekukosea lakini uamuzi huu niliona unafaa kwa kuamini siku ya mwisho mbele ya Muumba nitahukumiwa mwenyewe kwa vile tayari najua zuri na baya. Hawa mbele yako ni wanangu wapendwa Zaaanuna na Labeiiki, kwa vile nimefanya kosa una haki ya kunifanya lolote, nipo radhi kwa adhabu yoyote ila nakuomba usiwaue wanangu.” Kauli ile ilikuwa kama mshale mkali moyoni kwa Mfalme Barami. Aligeuka bubu ghafla na kushindwa amfanye nini Balkis, mwanaye kipenzi aliyefanya kosa kubwa la kuzaa na binadamu. Lakini mke wake naye aliwahi mbele ya mume wake na kupiga magoti kumuombea msamaha mwanaye. “Mume wangu, Balkis ndiye mtoto wetu wa pekee, kama kosa amekwishafanya. Najua amekuudhi sana lakini nakuomba umsamehe mwanao. Kama adhabu naomba unipe mimi mama yake, nipo radhi kwa adhabu yoyote lakini wajukuu zangu usiwaguse.” “Kwa kweli hata sijui nifanye nini, basi tu kwa vile ni mwanangu lakini bila hivyo ningekuchemsha supu na kukunywa kwa jinsi nilivyochukia.” “Najua nimekuudhi sana baba yangu lakini niliamini kuna aliye zaidi yako ambaye si mwingine bali Muumba wetu ambaye ana uwezo wa kufanya lolote bila kuingiliwa na mtu. Ni yeye ndiye mwenye adhabu kali yenye kuumiza.” “Nimekuelewa mwanangu sina jinsi, karibu nyumbani wewe na wajukuu zangu ambao siwezi kuwafanya lolote kwa vile hawana hatia.” “Baada ya kunisamehe naomba nimlete na mkweo mbele yenu mumtambue.” “Kwa vile tayari una watoto wake hatuna la kufanya zaidi ya kukubali kumtambua.” “Na hawa watoto watakuwa wa nani?” Malkia Huleiya alimuuliza Balkis. “Ni wa kwetu wote.” “Wataishi wapi?” “Huku, duniani watakuja siku moja moja.” “Kwa hiyo hata mimi nitafurahi kucheza na wajukuu zangu,” Malkia Huleiya alionesha furaha kubwa. Ilikuwa ni furaha kubwa kusamehewa na kutambuliwa rasmi watoto wa Balkis kwa mfalme Barami. *** Balkis baada ya kupata ruhusa ya kumpeleka mume wake kwao, alijikuta akijawa na mawazo juu ya kumweleza Muddy kuwa yeye ni jini, tena anayeishi chini ya bahari. Siku zote Muddy alijua Balkis ni binadamu wa kawaida. Alirudi hadi duniani na kumkuta Muddy amejipumzisha sebuleni akisikiliza nyimbo laini kutokana na kuambukizwa na Balkis kupenda kusikiliza nyimbo za Bara Asia. “Vipi mbona umerudi peke yako, watoto wapo wapi?” Muddy alimuuliza Balkis baada ya kumuona yupo peke yake. “Nimewaacha nyumbani.” “Mke wangu, watoto wadogo kama wale umewaacha nyumbani?” “Nimekufuata wewe twende kwa wazazi wangu.” “Mmh! Itakuwaje si ulisema baba yako mkali sana?” “Ni kweli lakini kwa sasa hakuna tatizo, watoto wamemaliza kila kitu.” “Sawa tunaweza kwenda.” Siku zote Muddy alijua Balkis hakai nje ya Dar es Salaam, kabla ya kuondoka Balkis alijikuta akipata wakati mgumu kumueleza Muddy kuwa yeye ni jini, lakini mwenzake aliitambua hali ile mapema. Alimsogelea na kuzungumza naye kwa sauti iliyomtoa machozi Balkis. “Nini tena malkia na kipenzi changu?” “Muddy nina wakati mgumu wa kujieleza kwako.” “Kujieleza nini tena mpenzi wangu?” “Najua hunifahamu vizuri, nina imani ukinielewa unaweza kuniacha.” “Siwezi kukuacha, hata ungekuwa jini siwezi kukuacha nakupenda sana Balkis.” Kauli ya kusema hata kama angekuwa jini ilimshtua sana Balkis na kujiuliza anayosema ni kweli au ni kusherehesha maneno. Lakini kwa njia nyingine yalimpa nguvu ya kusema bila wasi. “Muddy unanipenda?” alimuuliza huku akimtazama kwa jicho la mahaba. “Zaidi ya kukupenda.” “Nikikueleza kitu huwezi kuniacha?” “Hata ukisema unahitaji uhai wangu, kwa mapenzi yangu mazito kwako nipo tayari na nitakufa nakupenda.” “Kweli Muddy?” “Kweli kabisa kwani bila wewe sasa hivi mimi ningekuwa nani?” “Muddy mimi si binadamu.” “Kama si mwanadamu wewe ni nani?” “Mimi ni jini.” “Nani?” Muddy alishtuka na kusogea nyuma toka alipokuwa amekaa, kitendo kile kilimfanya Balkis apige magoti mbele ya Muddy kuomba asimuache.
ILIPOISHIA “Muddy unanipenda?” Alimuuliza huku akimtazama kwa jicho la mahaba. “Zaidi ya kukupenda.” “Nikikueleza kitu huwezi kuniacha?” “Hata ukisema unahitaji uhai wangu, kwa mapenzi yangu mazito kwako nipo tayari na nitakufa nikikupenda.” “Kweli Muddy?” “Kweli kabisa, kwani bila ya wewe sasa hivi mimi ningekuwa nani?” “Muddy mimi si mwanadamu.” “Kama si mwanadamu ni nani?” “Mimi ni jini.” “Nani?” Muddy alishtuka na kusogea nyuma kutoka alipokuwa amekaa, kitendo kile kilimfanya Balkis apige magoti mbele ya Muddy na kumuomba asimuache. SASA ENDELEA... “Muddy usiniache nakupenda sana.” “Balkis unayosema ni kweli?” “Kweli mpenzi wangu mimi ni jini la chini ya bahari na baba yangu ni mfalme wa majini katika bahari hiyo. Kukubali kuwa na mimi umeokoa vizazi vya wanawake mia ambavyo nilitakiwa nivitoe ili nipate dawa ya uzazi na kuniwezesha kuolewa na jini mwenzangu.” “Balkis unayosema ni kweli?” “Ni kweli kabisa.” “Kwa nini hukunieleza mapema?” “Ujini wangu ndiyo uliokoa maisha yako na hata kuendelea kukulinda na akina Ashura waliokuwa wakiendelea kuyafuatilia maisha yetu.” “Balkis japo moyo wangu umeshtuka kusikia wewe ni jini lakini bado nitaendelea kukupenda maisha yangu yote. Sikuwahi kuamini kama jini ana roho nzuri kuliko mwanadamu, niliamini majini ni wabaya na kama ungenieleza mwanzo ningeachana na wewe. Nakuahidi kwenda mbele ya wazazi wako kujitambulisha na kuwa tayari kuishi na wewe.” Kauli hiyo ilimfanya Balkis alie machozi ya furaha na kumkumbatia Muddy. “Asante Muddy kwa kuonesha mapenzi ya kweli, nitakupenda milele.” “Nikushukuru wewe kuonesha mapenzi ya kweli kwangu pia, kulinda maisha yangu kwa nguvu zote.” “Muddy niwafanye nini akina Ashura waliopanga kukuua na kuniua mimi?” “Kwani bado wanatufuatilia?” “Walikuwa wanataka kuniua nikawawahi na kuwageuza mbwa na nzi ili niweze kujifungua salama.” “Kwa hiyo mpaka sasa bado wapo katika hali hiyo?” Muddy alishtuka. “Ndiyo.” “Wewe ulitaka kuwafanya nini?” “Lolote utakaloliamua wewe nipo tayari kulifanya kwa vile umeusikia ubaya wao.” “Naomba uwasamehe.” “Kwa kuwa umesema wewe nitawasamehe.” Naomba kabla ya kwenda kuwaona wazazi wako wawe wamerudi katika hali yao ya zamani.” Baada ya makubaliano, Balkis alitoka na kurudi na mbwa na nzi aliyekuwa juu ya mgongo wa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mbwa na kusema: “Hawa ndiyo maadui zetu.” Muddy hakuamini kuwaona mbwa na nzi na kuelezwa kuwa ni Ashura na mwanaume wake. Balkis aliwatemea mate wote wakarudi katika hali yao ya kawaida ya kibinaadamu. “Mna bahati kubwa kwa kuwa mpenzi wangu amewasamehe, japo hata mimi nilikuwa na wazo la kuwasamehe, nashukuru Mungu nimejifungua salama. Kuanzia leo nina imani kwa adhabu ndogo ambayo hailingani na dhamira yenu ya kuniua kwa kipindi cha mateso imetosha kuwafanyeni viumbe wapya. Naomba mkaendelee na maisha yenu.” “Asante Balkis, asante Muddy, tunaapa kwa mbigu na ardhi kuwa hatutathubutu hata kuua nzi, mateso tuliyoyapata yametosha. hatukufa lakini cha moto tumekiona.” “Nakutakieni maisha mapya nina imani mtakuwa viongozi wema na kuwaeleza watu kuwa ubaya haulipi na jini si mbaya ila roho mbaya ya kiumbe chochote ndiyo mbaya.” Ashura na mwanaume wake walirudi kwao na kukuta kila kitu chao kikiwa katika hali ya usalama. Balkis naye alikwenda mpaka chini ya bahari kumtambulisha mumewe Muddy. Ilikuwa sherehe kubwa ambayo haikuwahi kutokea chini ya bahari iliyobadilisha amri ya jini kuolewa na mwanadamu. Pia, Balkis alichukua nafasi ile kuwarudishia vizazi vyao wanawake wote ambao baada ya kusumbuka sana kutafuta watoto, wote walifanikiwa kupata watoto bila kujua kuwa kitendo cha Muddy kumkubali Balkis ndiyo ilikuwa tiba yao. Baada ya hapo maisha ya Muddy na Balkis yaliendelea bila watu kujua kama Balkis ni jini zaidi ya Ashura na mwanaume wake. Muddy na Balkis kila mmoja alimpenda mwenzake mapenzi ya dhati
*******MWISHOOOOOO******************
0 comments:
Post a Comment