Search This Blog

SHUHUDA - 3







    Simulizi : Shuhuda

    Sehemu Ya Tatu (3)







    punde karimu aliingia nyumbani kwake lakini alionekana kutokuwa na furaha...ali ile ilimfanya mke wa karimu kuwa mnyonge sana kwani kila siku zinavyozidi kwenda karimu alizidi kuwa mtu mwenye mawazo mazito yaliyoichanganya akili yake....karimu alikuwa anachelewa kurudi nyumbani pia akirudi muda mwingi anakuwa akiangalia na kuperuzi peruzi katika laptop yake....hivyo hakuweza kupata muda wa kuwa karibu na familia yake........

    karimu hakuweza kula chakula cha usiku.....siku hiyo.....alipofika kwake aliingia moja kwa moja bafuni....alipomaliza kuoga alichukuwa laptop yake na kuanza kuchunguza shughuri za peter...pia alichunguza anashirikiana na nani????? hakuweza kufanikiwa kupata chochote ambacho kingeweza kumsaidia katika upelelezi wake.......alihisi usingizi akazima laptop yake na kupanda kitandani akaanza kuutafuta usingizi.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    asubuhi palipokucha alidamka lakini hali ya mtoto wake haikuwa nzuri hivyo aliamua kumpeleka hospitali......alimchukuwa mtoto wake...akaongozana na mkewe wakaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea hospitali.....kabla hawajafika mbali walipishana na gari moja aina ya BMW...karimu alihisi mule ndani ya gari hilo kamuona mtu mmoja aliyemuona jana alipolisimamisha gari alilolitilia mashaka.....kutokana na hali ya mwanae kuwa mgojwa hakulijali gari lile aliendelea kuzipanga gia kuelekea hospitali...



    ************



    ule upande mwingine walionekana wale vijana wa kazi wa peter wakishuka kutoka ndani ya gari...kisha wakazipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya karimu walivamia na kuingia ndani...lakini hawakukuta mtu.....waliamua kuondoka....kipindi wanatoka mmoja kati ya wale majasusi aliparamia meza na kudondosha tuzo ya karimu iliyokuwa imewekwa mezani kama pambo...kwa sababu tuzo ile ilikuwa imenakshiwa kwa kioo ilivunjika.......majasusi wale hawakujali walitoka ulande wa nje wakaingia ndani ya gari na kutokomea......



    *************



    kule hospitali"" mtoto wa karimu alifanyiwa vipimo ikagundulika alikuwa anasumbuliwa na maralia....hivyo alipewa dawa za kumeza akaruhusiwa arudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko......karimu na mkewe pamoja na mtoto wao wa pekee waliingia ndani ya gari na kuianza safari ya kurudi nyumbani...baada ya nusu saa walifika nyumbani.....karimu alilipaki gari kisha wakashuka kutoka ndani ya gari na kuelekea upande wa ndani......karimu alipofunfua mlango alihisi kuwa kunamtu kaingia nyumbani kwake....baada ya kuona ile tuzo yake imedondoka chini na kuvunjika.....aliamini hivyo kwani si rahisi tuzo hiyi kudondoka kwa sababu ilikuwa katikati ya meza na meza ilikuwa pana.....karimu alitoa haraka bastola kisha akaanza kunyata kuelekea upande wa vyumbani.....alistahajabu kukuta milango yote ipo wazi wakati yeye aliacha milango imedungwa......wakati akitahamaki mara ghafla simu yake ikaita

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    simu yake iliita...aliipokea huku anafungua geti..alipoingia upande wa ndani alistuka kukuta mkewe kauwawa kwa kuchomwa visu vingi mwilini...karimu alikata simu ile kisha alipiga hatua za harakaharaka mpaka pale chini alipokuwa ameanguka mkewe...alisikitika sana alihisi kutokwa na machozi...karimu alikumbuka kifo cha yule daktari....yaonekana muuwaji aliyemuuwa yule daktari..ndiye muuwaji aliyemuuwa mke wangu""

    kisha karimu akakimbia na kuelekea upande wa ndani akamuita mtoto wake...Feisal"



    feisal aliitambua sauti ya baba yake...akatoka haraka ndani ya kabati...na kuelekea upande wa sebuleni.... karimu alimshukuru mungu kuumkuta mwanae akiwa hai....kisha akatoka nje...akachukua simu yake na kupiga namba ya dharura....baada ya dakika kadhaa gari la kubeba wagojwa lilikuja....likiongozana na gari la polisi.....walipofika waliichukua maiti ya mke wa karimu na kiiweka ndani ya gari ili kupelekwa mochwari.....punde kamishna alifika.....karimu alimweleze kamishna..

    lakini alistahajabu kusikia kamishna akiamuru kuwa karimu akamatwe.......amri ilitekelezwa karimu akakamatwa na kupelekwa kituo cha polisi...akawekwa sero hata bila kuandika maelezo..

    kesho yake asubuhi alipelekwa mahakamani na kusomewa staka la mauwaji...karimu alipojaribu kujitetea na kueleza alichokikuta"" ilionekana kuwa karimu ni muongo.....anajaribu kuidanganya mahakama......kisha hakimu akaamuru kesi ihairishwe irushwe tarehe kuanzia siku hiyo,, tarehe 31/12/2017 mpaka tarehe 3/2/2017....kisha akamuru karimu arudishwe maabusu bila dhamana.....karimu alisikitika sana mda wote alikuwa akimkumbuka mkewe...na kumfikiria mwanae Feisal......maskini mwanangu sijui yupokwenye hali gani.......

    kamishna alimchukua feisal na kumlea kwa sababu baba yake alikuwa jela....



    ****************



    ule upande mwingine alionekana peter akiongea na simu huku uso wake ukionekana kuwa na furaha ya hali ya juu....kumbe alikuwa anaongea na kamishna juu ya mpango wao kukamilika..

    waliendelea kufanya bihashara haramu....uingizaji wa madawa ya kulevya na siraha za moto ziliingiza nchini kiolela....ujambazi ulishamiri....

    perer alikuwa ni Gaidi hatari mwenye mtandao mkubwa. alikuwa na vijana wa kazi zaidi ya elfu moja...walikuwa wakifanya kazi ya kuvamia na kupora pesa na mali.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA******



    karimu alipelekwa mahakamani.....hakimu alimuhukumu karimu kifungo cha maisha gerezani......karimu alistahajabu aljjiuliza ""kwa nini apewi wakili!!!! na kwanini apewi nafasi ya kujitetea...bila shaka kutakuwa na mtu wa karibu anayenizunguka....karimu alijisemea moyoni.

    karimu alipelekwa gerezani na kuanza kutumikia kifungo.......

    alisikitika sana lakini hakuwa na namna yakufanya aliamua kumuachia Mungu...



    ilipofika majira ya usiku..alionekana peter akishuka kutoka ndani ya gari....kisha akachukuwa box lililokuwa na bunduki ndani yake.... akamkabidhi mtu aliyekuwa anahitaji bunduki hizo....kisha mtu yule alitoa mabunda matani yanoti za shilingi elfu kumi kumi na kumkabidgi peter.....bihashara ilikwisha peter na vijana wake waliingia ndani ya gari na kuindoka zao.....

    walikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Peter.....



    ************



    asubuhi palipokucha.....kamishna alionekana yumo ndani ya gari akielekea kazini....lakini alikuwa akifikiria kuhusu mtoto wa karimu....

    aliamua kupanga mpango wa kumsomesha..na kumlea kama mwanae....



    Baada ya miaka kumi kupita.....karimu aliamua kuandaa mpango wa kutoroka gerezani ili akachunguze ni nani aliyehusika na mauwaji ya mkewe....""lazima alipe damu ya mke wangu. alijisemea moyoni....

    siku moja wafungwa walitolewa nje kwa ajili ya mapumziko.....karimu aliingia jikoni kinyemera akaiba kisu na kiberiti....kisha akanyata na kumpiga kabari mpaka kumuuwa askari yule aliyekuwa analinda upande wa nje,,,, na kuchukuwa bastora kisa akazitoa sisasi zote na kurudisha bastora ikiwa tupu kiunoni mwa askari yule.....kisha akamvuruta na kumtumbukiza ndani ya shimo la kupitisha maji machafu....kisha akakata upande wa juu wa risasi na kutoa unga wa baruti iliyokua ndani....kisha akaikusanya unga huo wa baruti na kuchana kipande cha nguo kisha akufunga...akaanza kuzipiga atua kuelekea kwenye choo kilichokuwa upande wa nje....akawasha kiberiti na kuchoma kile kipande cha nguo.....kisha akatoka haraka.....baada ya dakika moja ile baruti ililipuka askari wakilimbia kuelekea ule upande ambao ulisikika mlio mkubwa kama risasi......

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    karimu alipo ona askari wote wamezubaa alikimbia na kurudi ule upande wa jikoni kisha akachukua mavazi ya wapishi akavaa pamoja na kofia akutoka nje...alizipiga hatua mpaka getini...alifunguliwa geti bila kustukiwa.....akatoka nje kabisa....



    karimu akaona kuna gari likitokea upande wa ndani ya geti la kamishna kisha likatokomea kusikojulikana.....baada ya sekunde kadhaa karimu aliamua kunyata mpaka kwenye gari la peter......kisha akapandikiza kifaa maalumu...kifaa hicho kitaonesha gari hilo popote litakapokwenda..

    (GPRS LOCATE FINDER) baada ya kupandikiza kifaa hicho chini ya gari hilo aliamua kutoweka eneo hilo haraka sana....

    baada ya nusu saa peter alitoka nje ya nyumba ya kamishna na kuingia ndani ya gari lake na kuondaka..



    **************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog