Search This Blog

UTAJIRI WA DAMU - 4

 





    Simulizi : Utajiri Wa Damu

    Sehemu Ya Nne (4)



    "Mzee Mitimingi hapa umeletwa mbele yangu kwa sababu ya vitu viwili, kiganja cha mkono na ngozi za chui, basi. Unaelewa hili?"

    "Naelewa." Akajibu.

    "Bila kukutwa na vitu hivyo wala usingehojiwa hapa. Je, kile kiganja ni cha nani?" alihoji mtu yule ambaye ni askari wa upelelezi.

    Mzee Mitimingi alipata kigugumizi cha kujibu swali akawa anang'aang'aa macho tu.

    SASA TIRIRIKA NAYO..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya chumba kile cha mahojiano kulikuwa na baridi kali kutokana na kuwa na kiyoyozi, lakini nadhani iliongezeka mwilini mwangu kutokana na woga wa



    kesi inayotukabili.

    Nilikuwa najiuliza kwamba inawezekana kabisa tukaunganishwa na kesi ya mauaji ikiwa kama kuna maiti iliwahi kuokotwa ikiwa haina kiganja.

    Naamini kabisa kuwa woga wangu wa kuhojiwa na polisi haukumzidi mzee Mitimingi ambaye alikuwa akitetemeka waziwazi.

    Licha ya mwili wake kutetemeka lakini pia meno yake niliyasikia yakigongana na nikahisi kwamba anaweza kuanguka kwa presha.

    Yule askari aliyeletwa atuhoji alikuwa akitembeatembea katika chumba kile kana kwamba hakuwa na kazi ya kufanya.

    Baadaye alirudia kumuuliza mzee Mitimingi swali lilelile.

    "Kile kiganja ni cha nani?"

    Mzee Mitimingi hakujibu akawa anazidi kutetemeka. Nilishitukia akizabwa kibao cha shavuni.

    "Mzee sema, nitakuumiza na sitaki kabisa kupoteza wakati hapa. Niambie kile kiganja ni cha nani?"

    "Mimi nililetewa tu mheshimiwa."

    Baada ya jibu hilo alikula konzi ya nguvu kichwani, akawa anamwagika jasho.

    "Sitaki majibu nusunusu, sema aliyekuletea."

    "Nililetewa na mganga wa kienyeji."

    "Mzee nadhani unataka kuleta mchezo. Huyo mganga hana jina siyo?"

    "Anaitwa Mwapacha."

    "Anaishi wapi au mtaa gani?"

    "Anaishi Mtaa wa Kamchape, jirani na grosari."

    "Alikuambia kiganja kile ni cha kazi gani?"

    "Alisema kitanifanya niwe tajiri sana."

    "Je, tangu akuletee kiganja hicho umetajirika."

    "Sikutajirika kwa ajili ya kiganja nilikuwa nimeshakuwa tajiri ila alisema utajiri utaongezeka mara dufu."

    "Uliongezeka?"

    "Ahh wapi!!"

    "Alikuambia sababu za wewe kutotajirika zaidi?"

    "Alisema angenipa sababu hivi karibuni."

    "Kiganja kile ni cha nani?"

    "Sijui, kwa sababu aliniambia nimtafutie kiganja nikasema hiyo kazi sitaweza, akasema ataifanya yeye."

    "Je, vipi kuhusu ngozi ya chui?"

    "Hii nililetewa na mwindaji mmoja anayeishi Mtandi."

    "Mtandi?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndiyo, Kijiji cha Mtandi."

    "Nakifahamu."

    "Unafanya biashara haramu ya ngozi za chui wewe mzee?"

    "Hapana, sifanyi."

    "Sasa wewe ngozi ya chui kuwa ndani ya nyumba yako maana yake ni nini""

    "Hapana, hii ngozi siyo yangu…"

    "Siyo yako wakati imekutwa ndani ya nyumba yako? Au kuna mtu aliiweka, kama yupo, nitajie."

    "Mle ndani niliiweka mimi…"

    "Ndiyo maana nikasema umekutwa na ngozi ya chui maana hata wahenga walisema anayekutwa na ngozi ndiye mwizi wa ng'ombe, hujawahi kusikia msemo huo



    mzee Mitimingi?"

    "Nimewahi."

    "Basi hili ni lako. Au unamjua huyo mtu aliyekuletea anakaa wapi."

    "Ni yule yule mganga wa kienyeji aliyeniletea kiganja cha mtu."

    "Khaa! Huyu mtu ana matatizo kweli, kakuletea kiganja, akaleta na ngozi ya chui, hii nayo alisema ni ya kazi gani?"

    "Alisema zote hizo zinahusiana na uganga wake wa kunizidishia utajiri."

    "Jamani duniani kuna mambo, mzee utajiri wote ulionao unakubali kuwa na vitu vya ajabu nyumbani kwako, tena siyo vya ajabu bali ni vya hatari kwa maisha



    yako."

    "Kweli kijana wangu, nimekosea sana. Mnisamehe."

    "Hili siyo jambo dogo tena, hukusoma kwenye gazeti la Uwazi?"

    "Sijasoma."

    Yule askari alitoa gazeti na kumuonesha mzee Mitimingi. Kichwa cha habari kilikuwa kikisomeka kwa wino uliokolea, ‘Tajiri akamatwa na kiganja,



    ngozi ya chui na nywele za watoto.'

    "Mzee habari ikishatoka kwenye gazeti kama hivi ni sawa na moto wa petroli, kuuzima ni kazi nzito,"alisema yule askari aliyekuwa akihoji.

    "Sasa niambie zile nywele ambazo tulizikuta ndani ni za nani?"

    "Mwenye nywele simjui, nazo nililetewa."

    "Uliletewa na yule yule mganga?"

    "Hapana, alileta ni Che Che

    "Unababaika nini?"

    Nilianza kutetemeka kwa kuona kuwa akinitaja basi nitakuwa nimekwisha.

    Kwa kuwa nilikuwa nipo jirani na mzee huyo nilisogeza mguu wangu na kumkanyaga, kumkataza asinitaje.

    Aliniangalia huku akibubujikwa na machozi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Alizileta yule mganga."



    Baadaye yule askari alichukua redio call yake na kuzungumza:



    "Roja, namba kumi na saba hapa, naomba askari wawili afande." Baada ya kusema hayo



    alipunguza sauti ya redio yake hivyo sikusikia jibu alilopewa na badala yake nikaona askari wawili



    wanaume wakiingia.



    "Tumekuja afande."

    "Mchukueni huyo mzee Mitimingi akawaoneshe alipo mganga wake. Mkimkuta mkamateni mleteni hapa."

    Alitoa amri na dakika ileile mzee Mitimingi alifungwa pingu na kutoka na askari wale.

    Mle ndani ya chumba cha mahojiano tulibaki mimi na yule askari tu na hakuwa ananiangalia usoni.

    Nilikumbuka usemi wa wahenga kuwa ukitaka kumuua nyani usimuangalia usoni. Nilijikaza nisionekane natetemeka lakini ukweli ni kwamba nilikuwa



    natetemeka.

    "Msichana taja jina lako."Alianza kunihoji huku akiwa ameketi kwenye kiti kilichokuwa mbele yangu tofauti na wakati anamhoji mzee Mitimingi kwani wakati



    ule alikuwa akirandaranda chumbani kama vile alikuwa akitafuta kitu.

    "Naitwa Cheprisca."

    "Uliona nilivyomchapa makofi yule mzee. Sitaki majibu nusunusu, jibu kikamilifu ndiyo tutaelewana," alinionya yule askari.

    "Jina langu ni Chepriska Nahatani."

    "Kwani wewe baba yako Mchina."

    "Hata kidogo baba yangu ni Mmakua."

    "Mimi najua Nahatani ni Wajapani na nilivyokuona u mweupe na macho ya Kichina nikadhani baba yako ni Mchina."

    "Hapana afande."

    "Hebu niambie huyu mzee ni baba yako ki vipi?"

    "Mzee Mitimingi siyo baba yangu wa damu ni baba yangu kwa kuwa ana undugu na baba yangu mzazi."

    "Undugu wao ukoje?"

    "Wamezaliwa kwa mama mkubwa na mdogo lakini mzee Mitimingi ni mdogo kwa baba yangu."

    "Ilikuwaje akakuchukua wewe kuishi naye?"

    "Alikuja kwa baba na kuniomba akasema anataka niwe mhasibu wa kampuni yake hasa kwa kuwa mimi nilikuwa nimesomea DSA, kule Kurasini."

    "Uliwahi kugundua kuwa baba yako anajihusisha na mambo ya kishirikina?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sikujua lolote. Mimi kazi yangu ilikuwa ni kukusanya fedha zinazoletwa na madereva wa malori na mabasi yake kisha kuzipeleka benki."

    "Hujawahi kuona kiganja katika nyumba yenu?"

    Swali hilo lilifanya moyo huo upige paa, nilijiuliza kwamba labda siku ile nilipokiona kwenye jokofu kuna askari aliniona na ndiyo maana wakaja kutukamata.



    Hata hivyo, nilijisemea kimoyomoyo kuwa itakuwa ni ujinga kukiri jambo zito kama hilo.

    "Kwa kweli sijawahi. Kwanza sikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwake. Ki ukweli sijawahi kuingia chumbani kwa baba."

    "Unajua chochote kuhusu mbwa mtu?"

    "Ninachokumbuka ni kwamba aliniambia nisilikaribie banda la mbwa kwa sababu alisema ni mkali sana hasa kwa wanawake na mbaya zaidi alinitisha akasema



    amemchanjia kuuma watu, hivyo anilipiga marufuku hata kwenda kumuona."

    "Ina maana wewe hujawahi kumuona huyo mbwa mtu anayesemwa?"

    "Siku moja kabla ya polisi hawajatukamata nilimuona mbwa yule, nilimuuliza akasema atanipa mkasa wote kuhusiana na mbwa yule na kuniambia sababu za



    kuwa na sura kama ya mtu."

    "Alikusimulia mkasa huo?"

    "Hakuwahi kusimulia kwani tulikamatwa siku ambayo ilikuwa nipate simulizi yake."

    "Kuna habari kuwa ulikuwa unashiriki kumletea mzee Mitimingi vitu vya kichawi, niambie kuna ukweli wowote hapo?"

    "Hakuna ukweli. Nani kakuambia?"

    "Wewe kazi yako ni kujibu maswali yangu na siyo kuniuliza, jibu ndiyo au siyo."

    "Hapana."

    Baada ya mahojiano hayo niliangalia kwa nyuma kumbe alikuwepo yule askari wa kike ambaye alifanya ukaguzi pale nyumbani kwa mzee Mitimingi aliniambia



    niinuke, nikatii kisha yule polisi wa kike akanifunga pingu.

    "Kamfungie mahabusu." Alitoa amri na yule askari wa kike akawa ananipeleka kwenye mahabusu ya wanawake.

    Nilishangaa baada ya kutoka kwenye chumba kile nje nilikuta umati wa watu ulijazana kumuangalia yule mbwa mtu.





    Yule askari wa kike alinichukuwa na kunipeleka mahabusu ambako alinifungia lakini kila kitu kilichokuwa kinatokea nje nikawa nakisikia.

    “Huyu jamani siyo mbwa, huyu ni binadamu amefanyiwa mambo ya kishirikina na kugeuzwa mtu,” nilimsikia mtu mmoja akisema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni kweli kabisa afande. Ni lazima huyu mzee Mitimingi na binti yake Chepriska wanalijua hili.”

    “Chepriska yupi tena huyo?”

    “Si kale kabinti kadogo ulikokaona kanaingizwa mahabusu sasa hivi!”

    Moyo ulinipiga paa kwa kuona kuwa wanaozungumza hapo nje wananihusisha na mbwa mtu wakati kiukweli sikujua chochote. Niligundua kuwa



    wanaozungumza ni askari kwa sababu nilimsikia mmoja akimuita mwenzake afande nikajua kwamba ni lazima watanihoji na kuniadhibu ili niwaambie ukweli



    kuhusu mbwa mtu huyo ambaye hakika wataniua kama wangenilazimisha niwape habari kwa kuwa sikujua kitu.

    Baada ya muda nilisikia mngurumo wa gari nikajua kuwa hilo ni gari la polisi aina ya ‘defenda’ kwa sababu nilisikia askari wakiamuru watu kushuka.

    “Shuka mmoja mmoja na kila anayeshuka achuchumae na mkae kwa mstari.”

    “Mzee Mitimingi pia chuchumaa nyuma ya huyo mganga wako.”

    Maelezo hayo yalinifanya nijue kuwa safari ya mzee Mitimingi na askari makachero kwenda kumsaka mganga wa kienyeji imefanikiwa kwa kumnasa sangoma



    huyo.

    Haukupita muda nilisikia askari wakiwaelekeza waliowaleta kuingia katika ofisi ya wapelelezi.

    “Kila anayeingia ndani akae chini.” Ilikuwa ni amri ya askari wa kiume na alisema kwa sauti kali ya juu kuonesha kuwa ilikuwa ni amri.

    Chumba cha mahojiano cha askari wa upelelezi kilikuwa siyo mbali sana na mahabusu ya wanawake kwa hiyo kama pana ukimya kiliwezesha anayefungiwa



    humo kusikia kila kitu.

    “Wewe mzee unaitwa nani?”

    “Naitwa Antonia Mpepechere.”

    “Kabila lako na umri wako.”

    “Mmakonde. Nina miaka 65.”

    “Kazi yako ipi?”

    “Mganga wa kienyeji.”

    “Huyu mzee Mitimingi anasema kuwa wewe ni mganga wake, je taarifa hiyo ni kweli au siyo kweli?”

    “Taarifa hiyo ni kweli kabisa.”

    “Umewahi kumpelekea huyu mzee kiganja cha mtu?”

    “Ndiyo.”

    “Ulikipata wapi?”

    “Nilikipata barabarani, njia kuu ya kuelekea Morogoro.”

    “Ulikipataje?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mara baada ya ajali moja ya basi kutokea sijui ni lini, lakini iliua sana, nilikiokota kiganja cha mkono, nikakichukua kwa kuona kuwa kitanifaa kwa kazi yangu.”

    “Kazi gani mzee, hukujua kuwa unatenda kosa la jinai?”

    “Sikuona kama ni kosa, niliona kitanifaa siku zijazo lakini siku ileile akaja huyu mzee kutaka dawa ya utajiri nikamuagiza atafute kiganja cha mtu akasema hiyo



    kazi hataiweza, basi nikampa kile nilichokiokota ajalini kwa kulipia. Sikwenda popote kumkata mtu hata ukihoji watu wa kijiji hiki, hakuna ambaye amekatwa



    kiganja.”

    Nilijua kuwa huyo anayejitetea ni yule mganga wa kienyeji wa mzee Mitimingi lakini nikamuona hana akili ya kujitetea kwa sababu kuwa na kiganja tena cha



    binadamu ni kosa la jinai. Ni bora kingekuwa kiganja ya nyani japokuwa hilo pia angebanwa na watu wa Tanapa.

    “Lakini mzee hujui kuwa kiganja cha mtu ni haramu kuwa nacho?”

    Kimyaa.

    “Sasa tuachane na kiganja, tuambie kuhusu ngozi ya chui ambayo ulimpelekea mzee Mitimingi, ni kweli kwamba wewe ndiye ulimpelekea?”

    “Ndiyo.”

    “Ulipata wapi ngozi ile?”

    “Nililetewa na watu.”

    “Tunajua kuwa uliletewa na watu, tunachota utufahamishe watu hao ni akina nani?”

    “Siwajui. Mimi walikuja nyumbani kwangu na kuniambia kuwa wana ngozi ya chui, nikainunua, sijui walitokea wapi na hivi sasa nimeingiwa na wazo kuwa



    inawezekana ndiyo walioleta taarifa kwenu. Kwa maana kuwa inawezekana wamenizunguka.”

    “Sasa tuambie kuhusu huyu mbwa mtu. Je, ni wewe ambaye umemgeuza mtu na kuwa katika hali ile?”

    “Mimi sijamgeuza isipokuwa mzee Mitimingi nilimpa dawa yenye masharti sasa kwa vyovyote inawezekana yeye hakufuata masharti ndiyo maana yamemkuta ya



    kumkuta.”

    “Lakini unajua wewe mzee una matatizo sana, huoni kuwa kumgeuza mtu mbwa ni kosa? Licha ya kuwa ni kosa hujui kuwa huo ni unyama?”

    “Kwa kweli mimi sijamgeuza huyo mtu isipokuwa masharti yamemfanya awe vile?”

    “Kwani masharti hayo ni ya nani? Siyo wewe uliyeyaweka?”

    Kimyaa.

    “Unatakiwa umrejeshee ubinadamu wake. Utaweza kumgeuza?”

    “Mhhhh ina…ina…ina….” yule mganga alishikwa na kigugumizi na kushindwa kuzungumza, akawa anameza mate huku jasho likimtoka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    Baada ya mahojiano ya muda mrefu mzee yule mganga wa kienyeji alilazimishwa na polisi kumrudishia ubinadamu wake mbwa mtu yule.

    "Itabidi mniachie ili nikaifanye kazi hiyo nyumbani kwenye banda langu la uganga."

    "Ukweli ni kwamba hutaachiwa isipokuwa utapelekwa kwako na polisi na utakuwa huru kufanya uganga wako,"alisema afisa wa polisi.

    "Sawa nakubali. Baada ya hapo je?" alihoji mganga huyo huku akiwa anatoka jasho.

    "Kitakachofuata utafahamishwa, elewa kwamba sasa hivi upo chini ya dola."

    "Lakini itabidi na mzee Mitimingi tufuatane," akasema.

    "Kwa nini? Kwani yeye ndiye aliyemgeuza mtu yule kuwa mbwa?"

    "Yeye hakumgeuza lakini ndiye aliyekiuka masharti ya uganga."

    "Sawa. Tutamfungulia na mtafuatana naye, kuna lingine?"

    "Lipo." Akaitikia mganga yule haraka huku akimuangalia yule askari aliyekuwa akimhoji.

    "Lipi hilo mzee?"

    "Gharama."

    "Gharama za nini?"

    "Gharama za kumrejeshea umbile la kibinadamu. Kuna vitu vitahitajika, nani atalipa?"

    "Sisi hayo hatuyajui, tunachotaka mtu huyu uliyemgeuza mbwa anakuwa binadamu."

    "Sawa, sijakataa sasa nani atalipia gharama ya vitu vya kuchanganya ili awe binadamu?"

    "Kwani kunahitajika nini na nini?"

    "Vipo vitu vingi kama vile mkia wa kondoo, pembe za ng'ombe mbili, mtungi mkubwa mmoja, kitambaa chekundu mita sita, mbwa mzima mmoja, vibuyu



    vitatu, mchanga wa baharini au maji ya bahari na kadhalika."

    Baada ya kutaja masharti hayo yule askari alimuangalia kisha kutikisa kichwa.

    "Ina maana hivyo vyote ni lazima vipatikane? Fanya shotikati."

    "Hakuna shotikati katika mambo haya ya uganga. Leteni vitu , turejeshe ubinadamu wake."

    "Ukipewa fedha utaweza kuvitafuta vitu hivyo?"

    "Penye fedha hakuna lisilowezekana."

    "Kama shilingi ngapi kwa vifaa vyote hivyo?"

    "Shilingi laki nne."

    "Sawa."

    Baada ya mahojiano hayo askari yule aliamuru mzee Mitimingi aletwe pale ofisini kwake na baada ya dakika chache alikuwa tayari amesimama mbele ya afande



    huyo.

    "Mzee Mitimingi hapa una msala. Ni lazima mtu huyu uliyemgeuza mbwa ajirudie hali yake na kuwa mwanadamu."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Mzee Mitimingi hakujibu chochote akawa anatetemeka.

    ***

    Mbele ya nyumba ya mganga huyo Mtaa wa Mtandi kulikuwa kumejaa watu wengi waliokuwa na shauku ya kuona kwa macho yao mbwa mtu akigeuzwa na



    kuwa binadamu.

    Kulikuwa na polisi wa kumwaga ambao walikuwa na bunduki za rasharasha pamoja na mabomu ya machozi pia kulikuwa na askari kanzu pamoja na mbwa wa



    polisi wote hao walikuwepo kulinda usalama wa mganga kwa sababu haijajulikana huyu aliyegeuzwa mbwa ni nani.

    Mbwa wa polisi walibweka sana baada ya kumuona mbwa mtu akishushwa katika gari la polisi aina ya difenda.

    Bila shaka walikuwa wakimshangaa mwenzao kwa jinsi alivyokuwa anafanana na binadamu hasa macho, pua na mdomo.

    Lakini cha kushangaza zaidi mbwa mtu huyo aliwasononesha watu wengi kwa jinsi alivyokuwa akitiririkwa na machozi kama binadamu na mkia wake akiwa



    ameufyata.

    Lakini mzee Mitimingi alipokuwa anashushwa na watu kujua kuwa ndiye aliyesababisha hayo yote alianza kuzomewa na umati uliofurika nje ya nyumba hiyo ya



    sangoma.

    "Mchawi huyoooo, Mchawi huyooo, utajiri wake kumbe ni wa damuu, chawi hilooo," yalikuwa ni maneno ya baadhi ya watu waliokuwa wakimzomea.

    Baada ya muda uliwashwa moto katika jiko moja kubwa la mkaa na ukawekwa mkia wa kondoo ambao ulisaidia kukoleza moto na kuwa mkubwa.

    Watu waliokuwa wanazomea walikaa kimya ili kushuhudia kitakachotokea na baada ya dakika chache wakamuona mganga wa kienyeji akitoka katika banda la



    uganga huku akiwa amevaa lile tambaa la rangi nyekundu tupu na mkononi alikuwa ameshika usinga.

    Alikwenda moja kwa moja kwenye moto na kutoa kipande cha mkia wa kondoo uliokuwa unababuka. Aliuweka kwenye chungu cheusi na kukatakata vipande



    kisha akamuendea mbwa mtu na kumlisha mkia huo huku akisema maneno ambayo wengi tulikuwa hatuyaelewi maana yake.

    "N-dyeke mwilha, nthathueke ntu (Kula mkia ugeuka kuwa mtu)" ni maneno ambayo alikuwa akiimba mzee huyo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Umati wa watu uliminyana kila mmoja akitaka kuona kitakachotokea kwa mbwa mtu ambaye alikuwa akila mkia wa kondoo huku akilia.

    Alikuwa akitiririkwa na machozi kama binadamu hasa ikizingatiwa kuwa macho yake yalifanana kabisa na ya binadaamu.



    Kutokana na watu kumzunguka mbwa mtu huyo, polisi iliwabidi wafanye kazi ya ziada kuwatawanya na baadaye sangoma akaamua kumchukua na kumuingiza katika chumba chake cha uganga.

    Watu hawakuridhika na uamuzi huo kwani walikimbilia dirishani kuchungulia ili waone kinachoendelea ndani, hata hivyo, waligonga mwamba baada ya sangoma kufunga madirisha yote, ndani nilikuwepo mimi Chepriscar, mzee Mitimingi, mbwa mtu na wasaidizi wa mganga.

    Haukupita muda mrefu yalianza kusikika manyanga yakipingwa huku nyimbo zikiimbwa na sangoma pamoja na wasaidizi wake. Polisi na watu wengine walikaa nje na kushuhudia moshi wa ubani ukitoka kupitia kwenye nyufa za madirisha.

    Baada ya dakika thelathini mganga huku akiwa amejifunika kitambaa cha rangi nyekundu alitoka nje ya ile nyumba na kuanza kutangaza:

    “Ndugu zangu, kazi imekamilika, mbwa mtu amegeuka binadamu na baada ya dakika chache nitamtoa nje mumuone,”

    “Mtoe sasa hivi,” “Mtoeeeee,” “Mtoeeeeeee”, zilikuwa ni kelele za watu waliokuwa wameongezeka baada ya habari hiyo kusambaa mji mzima.

    “Ndugu zangu, tuache apumzike na anapewa dawa ili akili zake ziwe sawasawa….. Msiwe na shaka atatoka na mtamuona,” alizidi kuwasihi, niliogopa nikawa na hofu kuwa wanaweza kuvamia na kuingia ndani kwa nguvu.

    Baadaye aliingia ndani na baada ya nusu saa alitoka mmoja wa wasaidizi wake na kumchukua mkuu wa wale polisi wakaingia ndani, alipoingia aliniangalia kama vile alitaka kusema na dakika kumi baadaye walitoka sangoma, kamanda na mtu anayetajwa kuwa aligeuzwa mbwa.

    Umati ulishangaa huku wengine wakipiga kelele ambazo hazikuwa zikieleweka walitaka nini kwani wapo waliokuwa wakisema; “Azungumzeeee,” wengine wakawa wanasema; “Mpeni kipaza sauti.”

    Hii ni kutokana na mkuu wa polisi kutumia kipaza sauti cha kiganjani mara kwa mara alipotaka kuwaambia jambo.

    ***

    Tulikuwa tukishushwa kituo cha polisi kutoka kwenye gari ‘difenda’ ambalo lilikuwa na askari wenye silaha, watu walikuwa wengi kituoni kushuhudia tukio hilo japokuwa walikuwa wakisogezwa mbali na askari.

    Alianza kushuka sangoma, akafuatia mzee Mitimingi kisha mbwa mtu ambaye sasa alikuwa binadamu na alivikwa kile kitambaa cha rangi nyekundu na shati alilopewa na sangoma, nikamalizia mimi.

    “Wewe Chepriska, mfuate huyo kamanda wa kike akupeleke mahabusu ya wanawake,” alisema yule mkuu wa polisi.

    **

    Ilikuwa ni Jumatatu, saa mbili asubuhu nilishitukia yule askari wa kike akifungua geti la chuma la chumba cha mahabusu.

    “Cheprisca jiandae, tunawapeleka mahakamani,” alisema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa kosa gani?” nilimuuliza.

    “Utajua hukohuko,” aliniambia huku akitoa pingu kwenye mkanda wake.

    Nilifungwa pingu hiyo na kupelekwa nje ambako niliingizwa kwenye difenda. Baada ya dakika chache waliingizwa mzee Mitimingi na yule sangoma, lakini yule mbwa mtu ambaye sasa ni binadamu sikumuona, nadhani aliachiwa.

    Baadhi ya ndugu zangu walikuwepo na ndugu wa Sangoma pia walijaa tele pale. Dada yangu mmoja aliniambia nisiwe na wasiwasi kwa sababu wamenitafutia Wakili Mabere Marando ambaye nitamkuta mahakamani.

    Nilifarijika sana kusikia hivyo lakini nikajua pia kuwa kwa upande wa mzee Mitimingi alitafutiwa wakili aitwaye Dk. Ngali Maita. Ni sangoma tu ambaye sikusikia ndugu zake wakimfahamisha kuwa atakutana na wakili wake huko kortini.



    Tulifikishwa katika Mahakama ya Mtandi mapema sana na kweli mimi nilimkuta Marando ambaye alinichukua nikiwa chini ya ulinzi hadi kwenye chumba kimoja cha mawakili mahakamani hapo.

    “Wewe ndiye Chepriska bila shaka,” alisema.

    “Ndiyo.”

    “ Kwa kuwa sijakusikiliza. Hapa leo kila utakachoulizwa utakataa na sisi tutaomba kesi kuahirishwa, baada ya hapo tutajua la kufanya,” aliniambia Marando.

    Baadaye tuliingia katika mahakama ya wazi ambayo ilikuwa imefurika watu waliotaka kujua nini kitatokea. Mle mahakamani niliona watu wengi wakiwa na Gazeti la Uwazi ambalo lilikuwa lina picha zetu ukurasa wa mbele huku mbwa mtu akiwa ndiye picha kubwa.

    “Kooooooooooorti,” zilikuwana kelele za askari wakati hakimu anaingia mahakamani.

    Tulisomewa mashtaka ya kumgeuza mtu kuwa mbwa na kukutwa na kiganja cha mtu na ngozi ya chui. Wote tulikataa. Kesi iliahirishwa mpaka baada ya wiki mbili, tuliwekewa dhamana.

    **

    Siku ya kesi ilifika shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri alikuwa yule mtu aliyegeuzwa kuwa mbwa. Alipanda kizimbani kutoa ushahidi wake nasi watatu, sangoma, mzee Mitimingi na mimi Chepriska tulikuwa katika kizimba cha washtakiwa.

    Mwendesha mashtaka Zombi Kwale ndiye aliyekuwa akimuongoza kutoa ushahidi wake.

    “Ieleze mahakama, unaitwa nani na dini yako ni ipi na una umri gani?” aliuza mwendesha mashtaka.

    “Naitwa Mavata Mpwanyera. Nina miaka 28, Mmakua na Mkristo.”

    “Iambie mahakama wale washtakiwa unawafahamu?”

    Mavata mbwa mtu: Namfahamu, mzee Mitimingi na sangoma yaani mganga ambaye anaitwa Ntimwi.

    Wakili Kwale: Ieleze mahakama, unawafahamuje?

    Mavata mbwa mtu: Namfahamu mzee Mitimingi kwa sababu ndiye aliyenigeuza kuwa mbwa mtu na mganga Ntimwi alikuwa akinipa dawa kupeleka kwa huyo mzee.

    Wakili Kwale: Ilikuwaje mpaka akakugeuza mbwa mtu?

    Mavata mbwa mtu: “Alikuwa ananituma mara kwa mara kwa mganga Ntimwi na nikawa nampelekea. Siku hiyo nilikwenda kwa sangoma Ntimwi akanipa dawa na kunieleza kwamba jinsi ya kutumia amemuelekeza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwa njia ya simu. Nilipofika kwake baada ya kumpa dawa aliniambia nikae kwa muda mle ndani. Baadaye alileta chai tukanywa. Chai ile ilinishangaza kwa sababu chini yake nilikuta kuna vijiti kama kumi na mbili.”

    Wakili Kwale: Baada ya kuona hivyo vijiti, nini kiliendelea?

    Mavata mbwa mtu: Nilimuuliza mzee Mitimingi, kwa nini hii chai ina miti kumi na mbili?

    “Alianza kunifokea kwamba siyo kazi yangu kujua, akasema kwa kuwa nimevunja miiko, sasa nitakiona cha moto. Pale pale nikaanza kuhisi mwili kufa ganzi na kuona ngozi yangu ikianza kubadilika na kuwa kama ya mbwa. Nilianza kulia huku nikiishiwa nguvu na haraka haraka akachukua kitambaa na kunifunga mdomo.”

    Wakili Kwale: Baada ya kukufunga mdomo, ilikuwaje? Hakukuwa na mtu mwingine ndani ya nyumba hiyo?

    Mavata mbwa mtu: “Hakukuwa na mtu na tangu nimfahamu huyu mzee Mitimingi sijawahi kumuona mtu pale isipokuwa mlinzi tu.

    Wakili Kwale: Baada ya hapo ilikuwaje?

    Mavata mbwa mtu:Niliendelea kubadilika na kuota mkia, nililia sana kwa sababu sikuwa na la kufanya baadaye nikaona mikono na miguu inanyauka na kugeuka kama ya mbwa, ndani ya dakika kumi nikawa mbwa.

    Wasikilizaji: Looooooohhhhh…. mkatili jamani….

    Askari polisi: Jamani, hapa ni mahakamani, utulivu unatakiwa, ohoooo.

    Wakili Kwale: Baada ya kugeuka mbwa, ulikuwa ukijitambua?

    Mavata mbwa mtu: Ndiyo nilikuwa najitambua, akili za kibinadamu hazikuniondoka na ndiyo maana nilikuwa nikilia sana. Baadaye alichukua mnyororo na kunifunga shingoni akawa ananiburuza kunipeleka kwenye banda uani.

    Wakili Kwale: Wakati anakupeleka kwenye banda kulikuwa na mtu yeyote anaona?

    Mavata mbwa mtu: Ndiyo, alimuita mlinzi akamuambi kuwa amemleta mbwa na itakuwa marufuku kwake kwenda kumpa chakula au kumfungulia kibandani. Nililia sana kwa kujua kuwa sasa nitakufa kwa njaa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog