Search This Blog

MERISA JINI MWITU - 2

 







    Simulizi : Merisa Jini Mwitu

    Sehemu Ya Pili (2)





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sasa weunafikiri nani anataka hii aibu impate maana mtoto ndo wewe nakuamka kwako ndo saa nne kama hivi nisipo jitoa sindo nitaonekana na mimi sina mana kama wewe "



    "mmmh mama.."



    "nini kwani uongo?"



    "basi yaishe usije mwambia Geb tuu"wakati bado naongea na mama simu iliita hakuwa mwingine ila ni Geb" hello Geb"



    "mmh anna umeamka je mpenzi?"



    "namshukuru mungu Geb"



    "ooooh ok basi sikia nimetoka ofisini hivi nimepewa  wiki nzima ya kurelux "



    "waow!!! na nyumbani unakuja saa ngapi ?"



    "mmmh mida ya saa saba hivi nitakuwa hapo nikila chakula ulichokipika wewe mke wangu mtarajiwa" tuliongea mengi utani haukukosekana na hatimaye geb alifika nyumbani na jutitambulisha mbele ya wazazi wangu na kuelezea lengo na nia yake  kwangu sio mimi pekee niliye kampenda na kujisalimisha kwake pasi na hofu yoyote hata baba na mama yangu walimpenda sana Geb alikuwa mcheshi kiasi kwa muda mfupi alikuwa mwenyeji kwa wazazi wangu na akawa part muhimu katika familia hasa kwa siku ile iliyokuwa maarumu na special sana kwangu,Hatimaye siku iliishaikisindikizwa na kuzama kwa jua ,kutanda kwa kiza na kuchomoza kwa mwezi angani ndipo Geb alipoomba kurejea kwake nasi tukabaki nyumbani huku baba akimsindikiza Geb kwa gari mpaka kwake naye kurejea nyumbani. siku hii ilipambwa na furaha na ndelemo nyingi sana hasa kwa wazazi wangu kwani walikwisha amini Geb alikuwa ndio mume au mwanaume sahihi kwa mtoto wao anna.



    Siku zilisogea na kabla hata ya wiki aliyopewa Geb kuisha ili aweze kuanza safari yake ya kuelekea Cannada ,Siku moja jioni nikiwa natoka zangu chuo wakati naingia ndani simu yangu ya mkononi iliita hakuwa mwingine ila ni Geb nilipokea simu na kuiweka sikioni kabla sijasema chochote aliyepiga simu aliniwahi kuongea

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " anna mpenzi toka nje utakuta Gari jeusi hapo naomba uingie nikueleze kitu najua umchovu na mihangaiko ya leo ila tafadhali kama unanipenda kweli nakuomba ufanye hivyo laa sivyo utakuwa umenipoteza nakuomba ufanye hivyo mpenzi"siku bahatika kusema chochote na simu ilikatwa nanilipokuwa na jaribu kupiga simu tena haikupatikana nilihakiki mara mbili ni kweli ilikuwa namba ya geb nilitua mizigo yangu yote pale pale na kutoka nje kweli nililiona gari jeusi niliingiwa na hofu kubwa ila sikuwa najinsi maana ni kweli sikuwa radhi kumpoteza Geb nililikabiri na kugonga kioo cha dereva ambaye sura yake kwangu haikuwa ngeni ila sikukumbuka niliwahi kumuona wapi naye hakunisemesha alinielekeza kwa ishara kuwa nipite mlango wa nyuma kufungua nilimkuta Geb amejiinamia ile kufungamlango iliniweze muuliza vizur geb kakubwa na ninigari lilianza kuondoka na Geb aliinua kichwa na kunitazama



    "asante anna nina imani ni kwa upendo wako tuu kwangu umeamua kujitoa ila bado kunamoja naomba pia unisaidie" aliongea kwa upole mithiri ya mtu mwenye huzuni sana



    "kitu gani hiko Geb?" niliuliza kwa shauku la kutaka kufanya chochote asemacho, alijiinu kidogo na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa kidogo chekundu kilikuwa na maneno ila kwa jinsi Geb alivyokawa amekishika ilikuwa ngumu sana kujua kimeandika nini



    "naomba nikuzibe macho mpaka tutakapo fika mwisho wa safari nitakifungua "roho ilisita na kukataa kabisa ila sikuwa na namna maaana nikweli nilikuwa nina nia na lengo la kujitoa kwa ajili yake Geb alinifunga kitambaa na baada ya nusu saa nilisikia sauti yaGeb akimuelekeza yule kijana sehemu na namna ya kupark gari. mwisho nikasikia gari ikiwa imezimwa mara milango ikafunguliwa na kushikwa mkono nakukokotwa taratibu mara nikawa nasikiasauti za baruti pamoja na watu wakiwa na shangwe kama wapo katika hafla ila bado nilihisi masikio yana nidanganya baada ya hatua kadhaa nikahisi kusimama maana aliyekuwa amenishika  mkono na yeye alikuwa amesimama mara mtu alikuja nyuma yangu na kuuangaliza uso wangu juu kisha kunifungua kile kitambaa aaah sikuamininilichokiona angali paliandikwa happy engagement day anna and Geb wakati bado sijakaa sawa niliona



    Geb akipiga goti na kuingiza mkono mfukoni na kuitoa pete ndogo ya gold"anna ni kwa ajili yako mpenzi naomba ulilinde penzi langu kufatiwa na pete hii ikiwa kama ishara ya kuwa upondani ya himaya yangu haikuwa furaha pekee ila isiyo na kifani kila aliyekuwepo pale alikuwa akipeperusha bendera ya amani na upendo kati ya Geb na anna, Geb aliandaa hafla fupi kwa ajili yangu ambapo alinizawadia kidani cha dhahabu na cheki ya pesa kwa ada ya chuo na matumizi madogo madogo mpaka namaliza chuo.Ilikuwa hafla ndefu  kiasi ilipotimu saa sita niliomba kurudi nyumbani na Geb akanichua na gari moja kwa moja mpaka nyumbani.

    *****************************

    "mama anna huyu mtoto mpaka saizi usiku huu bado tu ajarudi kutoka chuo"aliongea baba huku akiwa mwenye hofu na wasi wasi mkubwa juu yangu



    "labda tumpigie simu mume wangu"mama alitoa wazo na hatimaye lilichukuliwa kama lilivyo bila ya kujadiliwa baba alichukua simu yake ya mkononi na kunipigia mara simu iliita pae walipoketi kutazama palikuwapo na vitu vyangu vyote vya chuo walizidi kupatwa na hofu zaidi juu yangu



    .....................************....................







    mara nikiwa na Geb simu yake ya mkononi iliita kuangalia alikuwa baba angu akimpigia akapokea kumsikiliza bila shaka walikuwa na hofu zidi yangu walitaka kumtaarifu geb pia juu ya kutokuwepo kwangu nyumbani iliwaweze jua watafanya nini."hallow baba shikamoo?" Geb alianza kumsalimia baba baada ya kuitikia tuu salamu yake sikujuanini alimuuliza geb mara nikasikia geb akisema "samahani baba ni mimi ndo nilikuwa nimekujamchukua hapo nyumbani wakati ndo anarudi tuu kutoka chuo na saizi nipo naye na mrejesha nyumbani niwieni radhi katika hilo wazazi wangu



     " sikujua kitu gani alijibiwa maana alikaa kimya kwa muda kuisikiliza simu ile mwisho akajibu sawa baba nimekuelewa na simu ikakatwa akanitazama usoni na kuniambia mzee MAGESA anamtaka mwanaye ,akakanyaga mafuta na kuongeza mwendo mwisho tukafika nyumbani kutahamaki wote walikuwa wamelala hivyo Geb akaamua kurudi nyumbani na kuniacha nikiingia ndani. nyumba nzimailikuwa kimya nilipita mpaka chumbani kwangu na kujitupa kitandani kushtuka mlango wachumba changu unagongwa ilikuwa tayari asubuhi na mama ndio aliyekuwa akigonga mlango akapita mpaka ndani baada ya kumruhusu aingie ndani



    "shikamoo mama?" nilimsalimia nikiwa bado nimelala



    "marahaba ,ndo nini anna hivi kutuweka kiroho juu jaman au kukubaliwa kuolewa ndo unajiona unaweza kufanya chochote unachojisikia sio?" aliitikia na kuniambatanishia swali niligundua mama alikuwa na hasira kwa nilichokifanya jana yake



    "hapana mama?"



    "ila nini ?"aliniuliza tena baada ya kumjibukisha akaendelea tena



    "anna nimekulea katika malezi ya tofauti sana usije nitia aibu ukubwani mama baba ako ajapenda kabisa kitendo chako cha jana umetupa wasiwasi kweli"



    "smahani mama sitorudia tena." nilimuwahi mama angu kabla ajaondoka



    "mimi nishakusamehe ila langu kubwa usije ukaiachia sana eti kisa ndo ushaaidiwa kuolewa na sisi wazazi wako tushakubali maana wanaume hawa awatabiliki wanabadilika kama mvua za masika zikiamua kunyesha zina nyesha tuu hata kama dalili zake za mawingu hazipo na kinyume chake ni sahihi zaidi" nilimuelewa vyema mama angu na nilijutia kwa jana yake kuondoka bila kuwaambia nimekwenda wapi ilasikuwa na jinsi .



    Siku hii ndo siku ambayo Geb alikuwa akiitajika kuianza safari yake ya kuelekea CANNADA kunako MERISA NATIONAL PARK laiti ningalijua ningemkataza na kumzuia Geb asindoke tanzania maana ndo mfarakano wa kwanza katika safari yangu ya mapenzi na Geb ila ningelijua huja baada ya kuwa yameshatokea nilimuaga geb ambaye alikuja nyumbani kwa ajili ya kuchukua baraka za wazazi katika safari yake nilimsihi sana asije nisahau baada ya kukutana na wasichana warembo zaidi yangu maana mbali na uzuri niliokawa nao ila sikuwamwenye kujiamini kwani niliamini kauli isemwayo na walimwengu kuwa uzuri wa mtu upo machoni mwa mtu ila mama yangu alininyima kabisa nafasi ya kuamini kuwa nilikuwa na mvuto kwa asilimia zote na kiasi yoyote anionaye anatamani kuwa na mimi na kwa wasichana kutamani kuwa kama mimi ila nimshukuru sana mama yangu maana alinijengea dhati thabiti kwa Geb.



    Geb alikaa nyumbani karbu nusu saa nzima akipewa wosia na wazazi wangu kisha akaondoka sikuwa na nguvu hata za kumsindikiza hivyo ilimbidi aende mwenyewe mpaka airport.kwa muda wa masaa saba walikuwa wamekwishafika CANNADA na kuelekea moja moja kunako hotel ambayo walipaswa kulala siku ile kabla ya kuanza safari yao yakuelekea katika mbuga isiyo na wanyama kwa ajili ya kutarii maajabu yaliyopo huko maana ni msituusifikao CANNADA nzima kwa maajabu ,uzuri na vituko vilivyomo ndani yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili Geb aliamka mapema na wenzake Dav,John,mary na janeth pia na kujiweka sawa kwa ajili ya kupewa muongozaji wa safari yao na kupewa maelekezo kwa ujumla kabla ya kuianza safari yao ambayo ingewezakuchukua takribani wiki mbili hadi tatu mpaka kumaliza ziara yao. waliwasili mapokezi muda wa saa tatu asubuhi baada ya kunywa chai na kuhakikisha kila mtu yuko tayari kwa ajili ya safari ile ambayo siyakutumia gari ,walikabidhiwa muongozaji amaye alijitambulisha kwa jina la MIKE alianza kwakuwaelezea historia fupi juu yambuga ile



    "mnamo mwaka 1975 mbuga hii ilipogunduliwa na kuanza kutunzwa kama hifadhi iliitwa THE CANNADA MAGIC GARDEN ambapo bado mambo mengi hayakugundulika na kuipa sifa zaidi hifadhi hii ya ajabu watu wengi walipenda kuitembelea hifadhi ile ambayo wala haikuwa na kiumbe hai au mnyama aliye weza kuishi ndani ile hifadhi zaidi ya watarii na ni kwa muda maalumu na kuondoka zao " aliyaongea hayo muongozaji huku akiwa tayari amewapatia kipeperushi kilichoandikwa MERISA NATIONAL PARK geb aliuliza



    "na kwanini merisa ?" muongozaji aliendelea



    "imeitwa merisa kunako mti ndani ya msitu huu uliona umbo la mwanamke mrembo na dhani ukiangalia hapo juu ya kipeperushi kunapicha ya mti unaiyona na ndo mti uitwao merisa na ndo kubwa ambalo watu huwa wanakuja kuangalia katika hifadhii. wote waliangalia kunako kipeperushi  na kuutazama vyema mti ule.wote waliridhishwa na jibu lile nahakutokea mwenye swali mwingine safari ilianza rasmi kwa ajili ya kutarii kulikuwa na vituo kila baada ya hatua kazaa ambapo watalii waliopita huko mwanzo walikuwa wakiweka kambi katika maeneo hayo kwa siku ya kwanza msitu ulikuwa umetulia kupita kiasi kulikuwa na ukimya wa namna yake ilipoingia jioni waliwekakambi mahali na kuwasha moto na kutengwa mahema matatu ambalo moja alilala mary na janeth na pili alilala dav,mike na john na lingine alilala Geb na mizigo yote wakati bado awajaingia kulala walikaa wakiota moto nje ya hema moja wapo huku mike akiendelea kuwaeleza mawili matatu juu ya msitu hule.kiukweli mike hakuwa mwenyeji sana japo alikwisha anza kuyaelewa mazingira baada ya kuwepo pale kwa muda wa miaka miwili sasa ila bado hakutosha kuwa na uzoefu mkubwa  juu ya msitu ule



    "kunako kambi tatu mbeleni tuuone mti huo ambao umejawa na maajabu kupita kiasi ambao kilaifikapo saa sita usiku katikamacho ya yule mwanamke aliyejiegemeza katika mti uleuitwao merisa huwaka mithiriya balbu nyeupe na humulika usawa wa kjiji na karibu ya hivyo hupaswi kuwasha moto kwa miiko ya maeneo yale inavyosema



    " geb alidakia "kwani ukiwasha moto nikitu gani kinatokea?"



    "kwa hapo sijawahi shuhudia maana mimi pia cna muda mwingi tangu nianze kazi hapa na sijawahi kupewa historia juu ya kilichowahi kutokea baada ya kufanya hivyo sasa cjui"alijielezea mike



    "hivi mnaonaje tukajaribu ilikuona kitakacho tokea"lilikuwa niwazo 

    kutoka kwa geb



    "hapana si vyema kufanya hivyo kwa kuwa tumeshaambiwa tusifanye hvyo mimi sioni umuhimu maana lisije zuka balaa hapa bure watu tukaanzakutafutana" yalikuwa maneno ya janeth,wote walicheka baada ya kumsikia janethakitoa mawazo yake.



    "acha uwoga wewe mwanamke jiamini"aliongea Dav akimtaka janeth ajiamini na awe na moyo mkunjufu juu ya wazo la Geb lakini haikuwa hivyo kwa upande wa janeth moyo wake ulikataa kabisa kuafiki jambo lile mwisho muongozaji ilibidi atoe hitimisho.



    "sikilizeni ndugu sio mimi wala nyinyi sote niwageni atuwezi kujua kwa nini tulipewa miiko hii tafadhali tusijaribu kuivunjaa maana hatujui ni lipi litatokeana ni vipi tulikabili baada ya sisi kukiuka miiko tuliyopewa miminaona ni vyema tungeendelea tuu na mambo yetu mti tutaupita tuuu na kuangalia maajabu menginemakubwa yaliyopo ndani ya msitu huu"



               ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,********,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,





    wote walikubaliana na kila mmoja aliingia anakostahiki kwaajili yakujipumzisha Geb alikuwa pekeyake chumbani kwake akiwaza mengi hasa alipenda kufanya jaribio la kuwasha moto siku atakapo ukaribia mti ule wenye taswira ya mtu  alimkumbuka anna pia ambaye alimuacha tanzania muda mfupi tuu maana haikutimia hata wiki tangu aondoke tanzania.hatimaye akapitiwa na usingizi mzito kutokana na uchovu wa mihangaiko ya siku hiyo nzima na kama ulivyomwili wabinadamu huitaji kupumzika pale tuu uingiapo usiku maana imekuwa kama kanuni na sheria katika maumbile yetu maana ni ngumu kupinga kutosinzia kwa muda wa masaa ishirini na nne na ndivyo ilivyotokea kwa geb alilala pasipo kutaraji na akiwa bado ajaamua juu ya kile alichokuwa akikiwaza.



    ********************************************

    Haikuwa rahisi kwangu niliyaona mengi katika macho yangu roho iliniuma sana ila sikuwa na jinsi ila kumuacha geb akatafute pesa ilituje kuwa na familia bora na watotowetu wasijepata tabu na matatizo madogo dogo.hakuna ambaye hakutambua kama furaha yangu ilitoeka ghafra haikuwa chuoni wala nyumbani sikutamani kusoma tena japo tulikuwa karibu na mitihani ila sikujali hilomara nyingi nilikuwa nikienda tuu chuo ila sio kwa lengo la kusoma na hata sikuwa nikisoma nilitamani geb arudi ila ilikuwa ngumu sana .

    Siku zilisogea hatimaye nikazoea na kuendelea kujisomea kama kawaida siku za mitihani ziliwadia na nikafanya mitihani yangu vizuri bila kikwazo chochote na kutulia nyumbani nikisubiri matokeo.

    wiki sasa ilipita na safari ya kina geb ilikuwa ndo kwanza inakaribia nusu ilikufikia ukingoni siku hii waliweka kambi tena sehemu kwa ajili ya kujipumzisha walipotaka kuwasha  moto  mike aliwakataza



    "hapana msifanye hivyo zimebaki hatua chache tuu tuufikie huo mti wa ajabu na kunako kutimu saa sita kamili usiku mutaona msitu ukibadilika na giza kutoeka na kuwa kama mchana " sio siri kila mtu alifurahishwa na kwa kuona tayari watakuwa maweifikia nusu ya safari hiyo maana walijua fika mti huo upo katikati ya msitu ule hakuna aliyekubali kulala pasi na shuhudia maajabu ya msitu ule kila mmoja alikuwa  radhi kukesha ajionee maajabu yaliyokawepo ndani ya msitu ule stori za hapa na pale zilizuka utani kwa sana ilimradi tuu wasiweze kupitiwa na usingizi huku kilammoja akiwa makini na saa yake ilikukaa tayari pale itakapo karibia saa sita kamili mara Dav aliitazama saa yake na kusema zimebaki dakika mbili kutimu saa sita kamili kila mmoja alihakiki kupitia saa yake na kuungana na Dav kuwa alikuwa sahihi .



    Wote walikaa kimya kusubiri mpaka dakika mbili zilipopita na kutimu saa sita kamili mwanga ulianza kuangaza poli zima na kufanya wajione ilikuwa mchana uliofunikwa na giza zito na sasa giza lile liliondolewa ulikuwamwanga mkali kweli uliokuwa tayari hata kuumiza macho ya watu ila walipewa miwani ya kukinga macho yao kabla hawaja dhurika  na walipoona mwanga unazidi kuwa mkali walivaa miwani ile ili wasijepoteza nuru za macho yao. Ilikuwa ajabu sana kwao wote na hikuwahi kutokea kukutana na ajabu kama ilewaliweza kukutana na miti yenye matunda mfano wa umbo la mwanamke mti wenye matunda mfano wa maumbile ya kiume ila mtiule ulikuwa na maajabu zaidi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hivi mike ni muda gani tunaweza kuufikia mtihuu kutoka hapa tulipo" aliuliza geb kama ilivyokawaida yake ya kuhoji kila jambo



    " inategemea na jitihada zetu ila na zani kesho tutaweza kukaribia kabisa kuuona mti huo" mike alijibu swali la geb kwa ufasaha zaidi japohakuikizi haja ya geb maana geb alitamani kufika katika mti hule mapema zaidi maana nafsi ilishamtuma kufanya jambo. walikaa kwa muda huku wakielezana ya hapa na pale mwisho mike aliaga nakwenda kulala akabaki Geb na Dav  hali ya kuwa wote wakiwa wamelala



    "unajua mimi natamani sana kuonakitakacho tokea baada ya kuwasha moto "aliongea Geb kwa sauti ya chini akiwa kama ana mnong'ong'oneza dav



    "mmh! Geb mi naona tuache tuu yasije yaka tutokea puani" aliongea dav na yeye akaingia ndani ambako alimkuta john akiwa amekwisha lala ajielewi kabisa na yeye akajiweka pembeni yake na kuvuta shuka wala haikuchukua muda mrefu tayari na yeye alikuwa katika sayari mpya ya kuijenga kesho yake.

    huku nyuma geb alikusanya majani kiasi na vijivipande vya miti na kuviweka pamoja kisha akatazama kushoto na kulia kama kuna yoyote aliyekuwa akimtazama juu ya kile alichokuwa anakifanya ila hakubaini uwepo wa yeyote mahali pale ndipo alipo chukua kiberiti na kuwasha moto na kuusubiri mpaka utakapo zima, haikutokea dalili mbaya yoyote wala baya kwa upande wake na hata alipojaribu kuangaza huku na kule bado kulikuwa shwari. ndipo alipoamua na yeye kuiuka na kuingia ndani kujilaza .Ghafra alihisi usingizi mzito sana baada ya muda alijikuta katika himaya tofauti ilikuwahimaya ya kifalme ambapo Geb hakuweza kujua kuwa niwapi pale au ni himaya ipi ile alizungukwa na watu wenye sura mbaya na za kutisha bila shaka mara akasikia sauti ikitoka kwa mwangwi



    "mleteni hapa mbele yangu" aliinuliwa geb ktoka pale alipokawa na kupelekwa mpaka kule ilikotokea sauti ile akiwa anaburuzwa, naam ilikuwani himaya ya kifalme sasa geb alithibitisha zile   fikra za akili yake alikuwepo mzee mmoja aliyekalia kiti cha thamani kubwa na hata mavazi yake yalikuwa na thamani kiasi geb alimtambua vyema kuwa ndiye mfalme pembeni yake alikuwapo mwanamke mzuri mwenye asili ya kiarabu Geb aliweza kumgundua pia kuwa bila shaka ndiye malikia wa himaya ile ila bado alikuwa ajaelewa haswakilichomfanya apelekwe kule haswa kilikuwa nikitu gani.

    Ghafrah mfalme alitoa hukumu ya kumtoa uhai Geb kwa kumuingiza katika miamba moto iliyopo chini ya ardhi punde ikasikika sauti ya mtoto wakike



    "hapana baba adhabu hiyo hailingani na uzitowa kosa alilolifanya hata hivyo huyu ni binadamu yupo tofauti xana na sisi ambao siku zote tumezaliwa,tumekulia na tunaishi katika himaya hii"







    "kimya mwanaharamu wewe"alikatishwa na sauti nzito ya mfalme iliyojawa na ghadhabu pamoja na hasira baada ya kumsikiliza binti yake kwa mudamrefu bila kuweza kutia neno ndani yake bila shaka kilichosemwa kilikuwa na ukweli ila mfalme hakutaka kabisa kuingiliwa katika himaya yake na hasa upande wa maamuzi .Ndipo mfalme alipo patwa na hasira na kuamuru vijakazi wake kuwa kusanya wote wawili na kuwa weka pamoja na kesho yake kutupwa katikamiamba moto huko chini ya ardhi. Ilifanyika kama mfalme alivyosema na hatimaye asubuhi ilifika hakuna aliyemsemesha mwenziwe tangu usiku ule mpka kunapochomoza jua walipo kuja kuchukuliwa na kupelekwa kunako miamba moto aridhini ambapo yule msichana alipewa heshima yake bado akiwa kama mtoto wa mfalme hakuwepo aliye amini kama mfalme angeweza kumfanyia vile binti yake tena wa pekee ila pia hakuwepo aliyeweza kufahamu ukweli juu ya binti yule zaidi ya mfalme na mkewe pekee.



    wakati wapo njiani binti alijaribu kumuuliza mfuasi wake ambaye alimlea tangu yungali mdogo mpaka pale alipofikia kama inawezekana kweli yeye kutupwa miamba moto na baba yake mzazi maana tayari akilini mwake lilikuja wazo jipya kuwa uwenda hakuwa baba yake mzazi. Japo alielezwa mengi juu ya matukio mbali mbali ya baba ake tena ya kutisha na mengi yalijawaukatili na uonevu ijspo kuwa walikuwa wakimkosea mfalme ila aliwapa adhabu kali na nzito tofauti kabisa na uzito wa kosa lenyewe. mara Geb akashitu kumbe ilikuwa ndoto mbele yake alikuwa mike aliyekuwa akimtikisa mguu kwa muda wa kama dakika ishirini bila mafanikio yoyote ghafra geb alifumbua macho



    "kulikoni mshikaji mbona unalala hivyo kama haupo kazini bwana" aliongea mike huku akinyanyuka



    "daaah sijui hata nimekubwa na nini kwani umeniamsha muda sana ?"



    "nusu saa sasa nipo na wewe hapa tunapigizana kerere tuu wala au amki "



    "Daaah samahani bhna sijui hata nilikubwa na nini uwenda ni uchovu tuu" aliongea Geb ilikumuweka sawa muongozaji wa safari ile .Baada ya muda walijiandaa na safari kuanza upya ilikuu karibia mti huo wa maajabu .



         ******************************

    Hatimaye nilimaliza vizurimitihani yangu na kufanya  sherehe kubwa ya mahafari kwa pale chuoni nanyumbani pia nilifanyiwa sherehe ya kupongezwa juu ya kumaliza kwangu elimu ya chuo kikuu sasa nilikaa nyumbani nikisubiri majibu iliniweze kujishikiza popote nitakapo bahatika siku zote hizo nilikuwa nikiwasiliana na Geb kwa mjia ya Email na kumjuza mambo mbali mbaliyaliyokawa yanatokea huku upande wa pili wa shilingi hata majibu ya mitihani yalivyotoka na kuonyesha nimefaulu vizuri pia siku acha kumjulisha maana sasa nilianza kumuona Geb ni zaidi ya kila kitu kwangu na upendo wangu uliongezeka mara dufu kilanilipokuwa nikifikiria kuwa ndoa yetu ipo karibu zaidi ili nasi tuweze kuwa mwili mmoja.

    Sasa zilibaki takribani wiki mbili Geb arudi na ulishatimu mwezi mmoja na wiki mbilitangu geb aondoke. Siku hii baba na mama waliniita na kutaka tuongee baadhi ya mambo,



    "Abee mama" niliitika nikiwa wima



    "pita uketi tuna maongezi mafupi na wewe" alisema mama huku akinionyesha pakuketi kwa mkono naminilifatiza kama vile mkono wake ulivyo onyesha nikaketi na kuwa tazama " anna mama?" aliniita baba



    "Abee baba"



    "unajua zimebaki siku chache tuu mchumba wako Geb aweze kurejea tanzania na wewe tayari umekwisha maliza kusoma sasa nimikakati gani ambayo mko nayo mpaka sasa juu ya ndoa yenu pindi atakapo rudi?"aliongea baba akitaka kujua nini kinaendelea maana ulipita ukumya mwingi tangu nilipo wasiliana na Geb wakati wakumueleza juu ya ufaulu wangu chuoni " mara ya mwisho nilimueleza juu ya matokeo ya chuo ambapo yeye pia aligusia suala la maandalizi ya harusi ila bado sijaenda kuchukua pesa ilituweze kujua tuna fanyaje "

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo ndipo ilipo kawafuraha ya mama angu maana aliwaogopa sana vijana wa kileo aliwaza uwenda geb akawa miongoni mwao kuwa ashatambulishwa kwetu sasa anakimbia nyumba na kutafuta mwingine ila kwa Geb haikuwa hivyo maana alikuwa nizaidi ya mwanaume muaminifu kwangu, Tulipanga kwenda kuchukua pesa na kuanza maandalizi ya harusi kukicha niliiyandaa harusi yetu katika kichwa changu nilitamani sana Geb arudi ilituipambe harusi yetu ila bado halikuwa tatizo maana baba na mama walikuwa bega kwa bega na mimi na tuka andaa kila kitu kikawa sawa tukawa tuna msubiri Geb pekee aweze kurudi ili vikao vya harusi viweze kufanyika .



    ***************************



    siku hii Geb alikuwa mkimya sana akiitafakali ndoto yake ambayo aliota amepelekwa katika falme za majini mwituhakuelewa kabisa yaliyotokea nandoto ile haikumuingia akilini kuwa ilikuwa ni ndoto tuu za kawaida kama ndoto nyingine akilini mwake alisema lazima kuna kitu hapa aiweze kani nikaota ndoto kama hii wakati anayawaza haya akujuakumbe alikuwa akiongea kwa sauti kabisa kiasi wenzake waliweza kugundua kuwa Geb hakuwa sawa



    " una nini ?"aliuliza janeth huku akimshika bega Geb



    "am,,, am,,,amna"alijibu huku akibaba ika huku akiwatazama wenzie mmoja baada ya mwingine



    "tuambie umeota ndoto gani mbaya"aliuliza mike

    sasa Geb alishindwa kabisa kujitetea na kukaa kimya kila mmoja alimshawishi katika aina yake ila Geb alikuwa mzito sana kuielezea ndoto ile maana kwake ilimjia kama nikweli yale yaitokea kwa upande wake baada ya kuona wamemaliza muda mwingi kumuuliza kuhusu ilo na jibu halikupatikana sasa waliamua kuendelea na safari ambapo baada ya hatua kadhaa mike alisimama na kuwa geukia wenzie na kuwa ambia



    "tumeshafika sasa kunako mti wa maajabu kila mmoja alikuwa tayari kusikiliza huku wakiangaza huku na huku iliwaweze kuuona mti ule wa maajabu  baada ya kupewa maelekezo ya namna za kuufikia mti huo walitoa camera zao kwa ajili ya picha na kusongea mbele kidogo ambako waliweza kuuona mti hule kiurahisi zaidi hatimaye waliuona kila mtu aliusogereana kutaka kupiga picha pembeni yake ilipofika hatua ya Geb kutaka kupiga picha alitaka kwanza kuushika mtiule ambao katika mikono yake kulichuruzika maji mfano wa chemichemi iliyo hai aridhini alisogea akapitisha mkono wake katika shavu la ule mti wenye tawira ya mwanamke Ghafra ilitokea sura ya yule msichana aliyemuona akiwa ndotoni akitabasamu na kupotea alisita kufanya hivyo akarudi nyuma akatazama kama kuna yoyote aliyemuona kati ya ule msafara hakuwepo akafanya vile tena mauza uza hayakuacha kumtokea walipiga picha na kuifurahia safari yao napo walikuwa wamefika nusu ya safari yao na maajabu yaliyokawa yamebakia katika msitu ule yalikuwa machache na lile ndo lilikuwa kubwa ,



    "mti huu hutumika kutengenezea dawa za magonjwa mbali mbali ikiwa kama kuotesha meno na mengineyo na dawa zake huwa gharama sana na hakuna nchi waliyoweza kuzitengeneza dawa hizo kwa kutumia mti huu zaidi ya India peke yake  napo alikuja mwanachemiammoja ndo alipogundua ponyo la mti huu ila ajabu jingine katika mti huu ni kwamba hauna miche kusema uchukue ukapande pengine au kusema ukate kipande ukakipande sehemu kingine maana hakitoota kamwe" alifafanua mike baada ya watalii wake kutulia kwa purukushani za kupiga picha za hapa na pale



    "Oooh kwa hiyo huu ni mti pekee duniani kote ?" aliuliza janeth akiwa na shauku kubwa la kutaka kujua



    "ndio na kwa upande wangu sijawahi kusikia kama kunamti kama huu na kama upo basi bado aujajulikana ila huu mti ni wakipekee sana "alijibu mike kwa msisitizo  na janeth alimuelewa vizuri sana Mike



    "na vipi kuhusu hiyo hospitali tunaweza kuiyona ?" aliuliza Geb huku kichwa chake kikiwa bado hakija kaa sawa



    "ndio tena nilisahau kuwaambia tripe za kuenda katika hiyo hospitali inakuwa kama zawadi kutoka kwetu na kutibiwa huko pia inakuwa juu yetu na hata kuhusu safari yako na gharama zote zitakazo husu safari pia tutahusikanazo



    "kwa umahili wa mike katika kuongea nidhahirialikuwa na rafudhi nzuri upangiliaji wa maneno na kaulizilizo njema kiasi mtu kuhamasika wote waliweza kumuelewa baada yamapumziko mafupi waliendelea na safari na hatimaye giza likaingia kwa mahesabu ya guider mike walikuwa hawachukui wiki watakuwa washa maliza ziara yao. Giza lilitanda na usiku uliandamana kwakishindo kulivamia jua na kuliondoa kabisa kaika usowa dunia nakuwa fanya watu kuangaika kwa vijitochi ili wasiweze kupatwa na madhara maana bado walikuwa karibu na ule msitu hivyo hawakupaswa kabisa kuwasha moto mahali pale maana ilikuwa hatari kwao  wakati wamekaa wanajadili la hapa na pale mara Geb alisikia sauti ya mwanamke akilia na kumtaja jina lake



    "Geeb Geb njoo unisaidie Geb?" Geb aliinuka na kuisikiliza sauti inatokea wapi



    "Jamani tumsaidieni " aliongea Geb huku akiwa na hofu kubwa sana wote waliinuka na kumtuliza Geb



    " kulikoni Geb mbona hatukuelewi?" aliuliza mary bado Geb alirudia kauli yake na kuanza kukimbia kuelekea kusiko julikana walimfatisha na kumkamata na kumtuliza tena chini



    "kulikoni Geb ?"aliuliza Dav sasa  Geb alikuwa yupo sawa naakili zake zilikuwa zimerudi kama kawaida aliwatazama mmoja badala ya mwingine alitamani kusema jambo alishindwa walimuomba awaeleze kinacho mtatiza ila bado lilikuwa tatizo Geb hakuweza kusema chochote, Mwisho story ilibadilika na Geb alikuwa wa kwanza kulala ila cha ajabu siku hiyo japo walikuwa bado wapo karibu na ule mti ila mwanga ule ambao huwa unawaka kila ifikapo saa sita usiku kwa siku hii haukutokea tena jambo ili lilimpa sana hofu mike kulingana na uzoefu wake pia katika msitu haikuwahi kutokea kabisa wakati anatafakari jambo hilo akakumbuka kauli aliyo ambiwa na geb mchana wa siku ile baada tu ya kuanza safari upya kuelekea mbele kidogo na mti ule wa maajabu



    " mike unauhakika kabisa msitu huu hauna vioja vya majini ?" swali ambalo mike halikumuingia akilini kwa muda ule ila sasa lilijirejea kichwani mwake ikiwa kama msisitizo wakati huo kila mtu alikuwa  amekwisha lala alitamani kwenda kumuamsha Geb walijadili ilaiikuwa ngumu kwa hilo kwani Geb alikwisha lala zamani wakati bado anatafakari alipitiwa na usingizi.



    Yapata saa nane na nusu usiku Geb anaisikiasauti kama ile aliyokaisikia mara ya kwanza ikimuita na kulalama kuomba msaada kutoka kwa Geb, Geb alianza kupagawa tena ila hakutaka kumuamsha mtu mara hii sauti ile ya mtt wakike ilimuumiza sana kwani mwanamke yule alionekana kuna kitu kilikuwa kikimuumiza sana naaliitajia msaada kutoka kwa Geb,Geb aliinuka na kutembea kwa kunyata mpaka katika hema walilolala mike, Dav na John kisha kwa mary na Janeth alipo hakikisha wamelala wote ndipo alipoanza kunyata taratibu ili asijekuamka yoyote na kujua kama alikuwa akiondoka kinyemela







    Aliifata sauti ile bila mafanikio yoyote baada ya kuona amepoteza muda mwingi sana katika poli lile alirudi kulala asubuh waliendelea na safari ilikuweza kukamilisha mzunguko wa kwenda na kuanza kurudi walikotoka alifanya hvyo mara tatu kila usiku ulipoingia na kuisikia sauti ile katika msitu ule huku ikimuita kwa jina lake na kumtaka msaada siku moja wakiwa wapo katika pita pita za utalii wao Geb alikuwa nyumakabisa na mike alimuuliza tena tena mike



    "mike unauhakika kabisa msitu huu hauna vioja vya majini ?"swali ambalo lilizidi mtia shaka mike na kunza kuwaza uwenda kukawa nakitu cha ajabu ambacho Geb kilikuwa kikimsumbua kiasi anakosa amani ilahakuelewa moja kwa moja aliendelea kutafakari swali lile ila bado hakupata jibu usiku uliwadia kamailivyo ada watu hukaa nje na kuongea mawili matatu kisha kila mmoja kuingia katika hema lake na kulala ilipotimu saasita usiku sasa ilikuwa kama kawaida kwa Geb alishitushwa usingizini nasauti ya msichana yule yule aliyekuwa akimuita siku zote na kumuomba msaada leo Geb alisema liwalo na liwe lazima aonane na yule msichana alitoka nje Geb nakuangaza macho katika pembe zote za mahali pale kisha katuliza akili kusikiliza vizuri sauti ilipotokea akarudi ndani ya hema na kuvaa koti kubwa ilikujikinga na baridi ndani hakuwa amevalia chochote akaanza ifata ile sauti taratibu mpaka ikafika mahali sasa sauti ile ilimuonyesha ilitoka mahali karibu kabisa na pale alipo akasimama nakutazama kushoto na kulia ghafra aligongana macho na msichana mrembo mwenye uzuri wa rangi macho ya makubwa na meupe nywere ndefu mpka mgongoni alionekana na asili ya kighana alikuwa uchi wanyama hakuwa na nguo hata moja na alitetemeka sana kwa baridi Geb alishitushwa na hali ya kumkuta msichana yule mahali pale akiwa uchi alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog