Search This Blog

SUNDI - 4

 







    Simulizi : Sundi

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbigili aliendelea kuliendesha gari hilo kwa kasi akaliingiza mstuni,,,kisha akalisimakisha!!! Anita akamtazama Mbigili kwa macho ya mshangao! akauliza,,"unamaana gani kunileta huku?

    Mbigili akamtazama Anita kwa macho ya uchu,,

    Anita akawasha taa ya ndani ya gari,,Mbigili anazima akamkamata Anita na kutaka kumbaka kinguvu!,,

    Anita akasema,,"subiri,,wacha nichukue kinga ndani ya pochi yangu,,kwa nini hukusema mapema kama unahiaji kufanya hivyo na mimi? ungeniambia kuliko kunileta huku porini wakati vyumba na vitanda vipo! Anita aliongea maneno hao ili Mbigili aingie kwenye mtego.....kunq jambo ambalo anataka kulifanya Anita,,pasipo Mbigili kujua!

    Mbigili akaingia kwenye mtego,,,akatabasamu kisha akasema,,"nilihisi utanikatalia ndio maana niliamua kufanya hivi kwa sababu nakupenda...

    Anita akatabasamu huku akipapasa mwili wa Mbigili,

    Anita akasema,, vua nguo zako zote..nahitaji ubaki kama ulivyozaliwa,, nahitaji nikufanyie jambo ambalo hautanisahau maisha yako yote....

    Mbigili akafurahi sana huku akijipongeza kuwa yeye ni kidume,,kumpata Anita,,,akajisemea moyoni,"nakula uroda kiulaini,,ujanja wake wote kwisha,,kumbe nilikuwa nachelewachelewa wakati ngamia kaangalia kibla,,wacha nimuonyeshe ufundi wangu,,,anipende daima...

    wakati mbigili anajisifu moyoni.....

    Anita alikuwa akiendelea kumvua Mbigili nguo zake,,hatimae mbigili akabaki uchi wa mnyama,,,Anita akaziweka nguo za mbigili kwenye kiti alichokuwa kaketi yeye...akaendelea kumpapasa Mbigili huku akimtazama mqchoninkwa macho ya mahaba ya wizi....Mbigili akazidi kuchanganyikiwa,,akajisahau kabisa! Anita akachomoq ufunguo wa gari pasipo Mbigili kujua,,,alipohakikisha kachukua ufunguo wa gari....akasema,,"nahisi haja ndogo wacha nikajisaidie hapo nyuma ya gari...

    Mbigili hakuwa na kipingamizi kwa sababu Anita anaonyesha amemkubali asilimia mia.....Mbigili akatabasamu kisha akasema,,uwanja wako mama,,fanya haraka nakusubiri...

    kutokana na giza totoro lililokuwa limetanda ndani ya msitu huo....Anita akatumia mwanya huo huvuta taratibu pochi yake,,pia akachukua nguo za Mbigili zilizokuwa kwenye kiti alichoketi yeye...akafungua mlqngo ja kutoka nje ya gari....Mbigili hakuweza kuona tukio hilo kuokana na giza,,,akabaki ndani ya gari akiendelea kumsubiri Anita aje,, waibanjue amri ya sita!!!



    Baada ya dakika tano kupita,, Mbili akashtuka,,akaanza kuingiwa na wasiwasi..huenda anita kamtelekeza na kukimbia.......

    Mbigili akaamua kufungua mlango na kutoka nje ya gari akiwa uchi wa mnyama,,,,hakujali kwa sababu ni porini,,hivyo aliamini hakuna mtu anashuhudia!

    alipozunguka nyuma ya gari akastaajabu kutokumuona Anita....

    macho yakamtoka! akasema,,"hivi huyu mwanamke kanizidi ujanja? kumbe mimi ni bwege!

    Mbigili akaamua kurudi ndani ya gari avae nguo zake haraka,,,awashe gari na kumfuata Anita,,,

    aliamini kuwa Anita atakuwa hajafika mbali !!!!

    akawasha taa ya ndani ya gari,,akashtuka kutokuuona mkoba wa Anita,,alipotafuta nguo zake hakuziona pia...

    akajisemea moyoni,,"wacha niondoke nitampata huko mbele kwa mbele hajafika mbali..

    alipojaribu kupapasa sehemu ya kuwashia gari...akashtuka kutokuuona ufunguo wa gari!! Mbigili akazidi kuchanganyikiwa....



    Upande mwingine alionekana Anita akiendelea kutimua mbio,,kutoka nje ya pori hilo,,akafanikiwa kuipata barabara ya rami....akasimamisha bodaboda,,akaikodi impeleke nyumbani...alipofika akatoa taarifa kwa baba yake kuwa dereva wake(Mbigili)alitaka kumbaka...

    Anita akasimulia tukio zima,,mpaka alivyofanikiwa kumtoroka Mbigili.

    Kitendo hichi kilimchukiza sana Baba Anita...akaamua kwenda kutoa taarifa katika vyombo vya dora.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Upande mwingine kule mstuni,,,alionekana Mbigili akitafakari nini cha kufanya aweze kutoka ndani ya msitu huo,,mbaya zaidi yupo uchi wa mnyama.

    akaingiwa na wazo,,,akaamua kuondoka eneo hilo akiwa uchi wa mnyama!! akiamini huenda Anita ameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dora hivyo

    atakuwa matatani,

    Mbigili akalitelekeza gari hilo huko mstuni..akaanza kutimua mbio...akafanikiwa kutoka nje ya msitu huo......akaamua kujifanya kichaa,,kwa sababu alikuwa hajabaa nguo...akaanza kuokota makopo na kuyaweka kwenye mfuko,,akazipiga hatua huku akiongea peke yake....ilimradi akikutana na watu wajue kuwa ni kichaa!

    Mbigili akatembea umbali mrefu......wazo likamjia akajisemea moyoni,,"wacha niingie mitaani kwenye makazi ya watu,,huenda nikapata nguo za kuvaa,,,hata nikikuta nguo zimeanikwa kwenye kamba ni halali yangu!

    alijisemea maneno hayo,,huku akiendelea kuzioiga hatu...

    hatimae akaingia katika mtaa mmoja,,,,wakati huo ilikuwa ni nyakati za usiku wa saa nne hivi...

    kwa mbali akaona nyumba moa ikiwa na nguo zilizoanikwa nje kwenye kamba,,,akaamua kuifuata nyumba hiyo,



    Upande mwingine,,alionekana mwanaume mmoja akiongea na simu,,kisha akakata simu hiyo,,kumbe ni kdugu wa Anita,,alikuwa anaongea na baba Anita katika simu,,,akisimuliwa kilichomkuta Anita,,,,Mwanaume huyo ni mdogo wake baba Anita.....akasikitika sana,,,akamsimulia mkewe,,

    mkewe akastaajabu sana akasema,,"Mbigili huyu huyu? mbona anaonekana ni mtu anayejiheshimu,,,kapatwa na pepo gani?

    kwa sababu binadamu mwenye akili timamu hawezi kufanya jambo hilo?

    wakiwa katika maongezi,,,mumewe akasema wacha nitoke nje nikahakikishe kama nilifunga milango ya gari langu kwa sababu sina uhakika......alisema maneno hayo huku akizipiga hatua kuufuata mlango wa kutokea nje ya nyumba,,,alipoufungua mlango akahisi kama kamuona mtu!!!

    alipotazama kwa makini akaona mtu anaanua nguo zilizokuwa zimeanikwa kwenye kamba!!!!

    PATASHIKA!!!!!!!!





    mwanaume huyo akasita,,akaendelea kutazama kwa makini aone mtu huyo,,, atafanya nini baada ya kuanua nguo....

    akaona anava nguo hizo,,,kisha akaondoka zake,,wakati Mbigili nazipiga hatua,,ikaonekana pikipiki ikikatiza kando ya nyumba hiyo....kwa sababu ilikuwa inamulika kwa taa kali,,,Mbigili akaonekana vyema,,,

    yule mwanaume akamtambua vyema Mbigili,,,akapaza sauti,,we Mbigili,,

    Mbigili akashtuka kusikia sauti inaita jina lake,,akaamua kutimua mbio na kutokomea kusikojulikana!



    Siku zilizidi kusonga...maisha ya mbigili yakawa matatani,,,,akawa analala nje,,,wakati mwingine akakosa chakula,,

    wakati huo maaskari waliendelea kumtafuta kwa tuhuma za kujaribu kubaka.

    Mbigili akaamua kufanya kazi ya kubeba mizigo katika vituo vya mabasi,,,,angalau apate pesa ya chakula pia pesa nyingine awe anatuza ipatikane nauli ya kurudi Tanzania.....alifanya kazi hiyo ndani ya wiki mbili mfululizo,,,lakini pesa aliyokuwa anaipata ni ndogo,,,haitoshi kutunza,,,wakati mwingine alikosa pesa kabisa,,,maisha ya Mbigili yakawa magumu kupita kiasi....



    akaona kazi hiyo bado haimpatii kipato cha kutosha,,,akaamua kutafuta kazi ya upishi katika migahawa....akafanikiwa kupata kazi katika mgahawa mmoja,,,uliopo nje kidogo ya mji...

    akaanza kazi siku hiyo hiyo,,,lakini mmiliki wa mgahawa huo akaona kuwa Mbigili hajui kupika chakula kizuri,,,kwa sababu wateja waliozoea kula chakula katika mgahawa huo,,walilalamika,,kuwa chakula kinachopikwa sikuhizi tau katika mgahawa huo,,sio kitamu tofauti na siku za nyuma...akaamua kumsimamisha kazi Mbigili..

    Mbigili akasikitika sana kwa sababu alikuwa na malengo yake,,,akilipwa mshahara autunze aweze kupata nauli ya kurudi Tanzania...

    baada ya siku tatu kupita ,,Mbigili akaamua kurudi kule kwenye ule mgahawa alikosimamishwa kazi,,,akamsihi sana mmiliki wa mgahawa huo,,anagalau amuhurumie awe anaosha vyombo,,upande wa jikoni...

    ombi lake likakubaliwa,,,na kazi ikaendelea.



    upande mwingine,, alionekana baba yake Anita kukata tamaa ya kumpata Mbigili...

    siku ya leo, akaonekana akitokea ndani ya jengo la ofisi yake...akazipiga hatua kulifuata gari lake.....akaingia na kuliwasha akaondoka zake....

    akiwa njiani akahisi njaa,,akaamua kutafuta mgahawa safi,,angalau ale chochote kupoza njaa.....akafanikiwa kuona mgahawa ulioonekana kuwa na mazingira safi.....akaliegesha gari lake na kushuka kutoka ndani ya gari...akazioiga hatua kuufuata mgahawa huo..



    wakati huo ilikuwa ni nyakati za jioni ya saa kumi na mbili(12)

    akaonekana Mbigili akiwa ndani ya jiko la mgahawa huo,,akifuta vyombo,,alivyoviosha mudamchache uliopita......

    baada ya dakika kadhaa akawa amemaliza kufuta vyombo hiyo..na kuvipanga katika kabati la vyombo....kisha akatazama saa ya ukutani,,akaona muda wa kazi umekwisha,,,,akazipiga hatua kutooa ulande wa jikoni,,akaelekea sehemu wanayoketi wateja,,kwa sababu ndipo upo mlango wa kutoka nje ya mgahawa huo.....

    Wakati huo huo alionekana baba Anita akiwa anaendelea kula chakula alichokiagiza......aliponyanyua uso wake akashtuka,,,akahisi kama kamuonq mtu anayemfahamu,,lakini alipojaribu kutazama kwa makini,,hakumuona mtu huyo..

    kumbe Mbigili alipomuona baba Anita,,akarudi haraka kuufuata mlango wa jikoni....

    Baba Anita akaendelea kuangaza angaza macho yake ule upande wa jikoni..



    Wakati huo huo akaonekana muhudumu akitokea ndani ya jiko hilo,,ghafla Mbigili akamparamia muhudumu huyo aliyekuwa ameshikilia sahani ya chakula kikamwagika chini...

    taflani hiyo pamoja na mvunjiko wa sahani,,,ikawatanya wateja wote wageuze shingo zao kutazama nininkinaendelea.....

    katika angaza angaza ya baba Anita akamuona Mbigili!!!

    macho yakamtoka,,akanyanyuka haraka akazioiga hatua kuelekea upande huo wa jikoni!!!!

    mmiliki wa mgahawa huo naye akaona taflani hiyo,,akaamua kuzipiga hatua kuelekea upande wa jikoni,,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akastaajabu kumuona mteja anafungua mlango wa jikoni,,,,akapaza sauti,,"we mzee huko ni jikoni,,haruhusiwi mtu yoyote kuingia,,isipokuwa wahudumu pekee...

    aliongea maneno hayo akimwambia baba Anita!

    Baba Anita akageuza shingo yake akasema,,"mtu aliyeingia humu ni muarifu....nimemtafuta siku nyingi,,na leo nimefanikiwa kumuona,,,

    Wakati baba Anita anaendelea kusimulia,,mara ghafla! zikasikika sauti za majibishano ndani ya jiko hilo...pinde si punde,,,zikasikika kelele za wapishi waliokuwemo ndani ya jiko hilo,,wakisema tafadhali usitudhuru!

    majibishano hayo yalisikika vyema upande wa nje ya jiko hilo,,pale kwenye eneo la mlango..

    mmilikinwa mgahawa huo akaanza kuingiwa na wasiwasi..alipojaribu kufungua mlango wa jiko hilo,,,ulikuwa umefungwa kwa ndani...litndo hicho kikaongeza hofu kwa mmiliki wa mgahawa huo,,akaanza kuyaamini maneno ya baba Anita..

    akaamua kufanya jitihada za kuvunja mlango huo!!

    PATASHIKA!!!!



    Wakati huohuo,ke ndani ya chumba cha jiko alionekana,Mbigili akiwa kashikilia visu viwili,,,akiwaamuu wahudumu na waposhi walale chini kwenye sakafu.....

    Mbigili akatafakari nini cha kufanya,,ghafla wazo likamjia,,akaamua kupitia dirishani na kutimua mbio kutoka eneo la mgahawa huo...

    baada ya dakika kadhaa,,,mmiliki wa mgahawa huo akafanikiwa kuuvunja mlango huo,,akaingia ndani ya chumba cha jiko,,akiwa kaongozana na baba Anita! wakastaajabu kuona wapishi pamoja na baadi ya wahudumu,,wakiwa wamelala chini! walipoangazaangaza macho yao,,hawakuweza kumuona Mbigili,

    mmiliki wa mgahawa huo akauliza,, "Mbigiliko wapi?

    wakajibu kapitia hapo dirishani...



    Baba Anita akatimua mbio kutoka nje ya mgahawa huo,,ghafla akajikwaa kwenye,,,kwenye mpira uliokuwa chini kwenye sakafu...mpira huo ulikuwa unatokea kwemlnye mtungi wa gesi kuelekea kwenye majiko yaliyokuwa yanawaka...

    mpira huo ukachomoka kwenye mtungi,,na gesi ikaanza kuvuja,,punde si punde ukatokea mripuko mkubwa,,,mgahawa huo ukqanza kuwaka moto!!!

    Watu wengi waliokuwa wanakula chqkula katika mgahawa huo wakajeruhuwa! baadhi yao wakafa kwa sababu moto ulikuwa mkubwa....

    miongoni mwa watu waliopoteza maisha,,ni mmiliki wa mgahawa huo pamoja na Baba Anita,,na wale wote waliokuwemo ndani ya jiko hilo!!!! hakupona hata mmoja!



    Upande mwingine akaonekana Mbigili akiendelea kutimua mbio,,

    alikimbia pasipokujua ni wapi anaelekea,,,

    giza lilizidi kutanda,,,,Mbigili akaamua kuifuata njia iliyokuwa inaelekea porini kwa kuhofia usalama wa maisha yake!



    Hakuna aliyefahamu chanzo cha moto huo,,kwa sababu wale wote walioshuhudia tukio kule jikoni,,walikufa wote,,hivyo hapakuwepo na ushahidi.....

    Taarifa za kifo cha baba Anita zikafika katika familia yake...

    Anita akasikitika sana,,akalia kwa uchungu akaamua kumpigia simu mpenzi wake aliyeko Tanzania kumpa taarifa ya msiba wa baba yake!

    kumbe Anita ni mchumba wa Apolo,,,

    baada ya kupata taarifa hiyo,,,aporo akafanya utaratibu wa  safari,,kesho yake aende nchini Kenya,,kushiriki mazishi ya baba Anita....



                 *******************



    Asubuhi palipokucha akaonekana,,Apolo akijiandaa,,kisha akaelekea uwanja wa ndege.....tayari kwa safari ya kuelekea nchini Kenya.

    baada ya kufika huko,,akakodi taxi mpaka nyumbani kwao Anita...

    akakuta taratibu za mazishi zikiendelea...

    ilipofika majira ya saa kumi za jioni,,,wakaelekea makaburini kumzika baba Anita...

    Apolo alilazimika kubaki huko kwa muda wa wiki moja kumfariji mchumba wake.....

    Anita akaomba warudi wote nchini Tanzania,,angalau akapoteze mawazo...

    Apolo hakuwa na kipingamizi,,,akakubali ombi la mchumba wake.

    wakaondoka wote kuelekea Tanzania..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Mbigili,,akiishi kwa kujificha,,,hali hiyo ilimfanya aishi kama mkimbizi kwenye nchi ya watu..hata chakula akawa anapata kwa tabu,,,mara nyingi hasa nyakati za mchana,,alilazimika kujificha kwenye mitaro mikubwa,,,,aliyoifanya kama makazi yake,,yeye huonekana nyakati za uwiku tu....

    Mbigili akaanza kuwa mchafu kupindukia,,,kadri siku zilivyozidi kusonga,,,hali ya afya yake ikaanza kudhohofika kutokana na kukosa lishe,,,

    ukimtazama kwa harakaharaka,,,alionekana kama kichaa,,kutokana na mava,i yake kuwa machafu,,na kutoa harufu mbaya,,

    Mbigili akaanza kujutia,,,kwa ujinga wake yeye mwenyewe wa kutaka mali kwa njia isiyokuwa ya halali...

    Kule nyumbani kwa mdogo wangu nilikuwa naishi vizuri pasipo bugza yoyote,,nilikuwa napata ninachokihitaji,,,mdogo wangu alininunulia gari nzuri ya kutembelea,,,,tamaa zangu zimeniponza,,sasahivi sina hata Shilingi! Mama yangu kafa kwa ujinga wangu mwenyewe,,,laiti kama ningemuwahisha hospitali mapema,,, huenda mpaka leo hii angekuwa hai..

    Mbigili alijisemea maneno hayo kwa uchungu huku akitokwa na machozi,,

    Siku ya leo njaa ilikuwa kali kuoita kiasi,,,kwa sababu siku nzima hakufanikiwa kulata chakula.....

    alipofika majira ya saa mbili za usiku,,,akaonekana Mbigili akitokea ndani ya mtaro mkubwa wa maji machafu....mtaro huo ulikuwa mkavu kwa sababu kilikuwa ni kipindi cha kiangazi.....

    katika pitapita za Mbigili akastaajabu kuona moja ya magari ya kampuni ya mdogo wake Apolo.....

    gari hilo aina ya SCANIA lilikuwa linapakia mizigo,,tayari kwa siku ya kesho kuianza safari ya kutokea kenya kuelekea nchini Tanzania,,

    Mbigili alipoangaza angaza kwa makini,,akaona hakuna hata muhusika wa gari hilo kuonekana maeneo hayo....akaamua kufungua mlango wa nyumba ya gari hilo,,akajificha kwenye mizigo!! akiamini hata wakimuona atajitetea kuwa hilo ni gari la mdogo wake!

    Mbigili alikaa humo usiku kucha,,,

    kesho yake majira ya saa moja za asubuhi...safari ikaanza...dereva na wahusika wawili wa gari hilo,,hawakutambua kuwa kunamtu kaingia kinyemera ndani ya gari hilo!



    Upande mwingine kule nyumbani kwa Apolo alionekana,,Anita akiwa chumbani kajipumzisha na Apolo,,,

    Apolo akamsimulia historia ya maisha yake,,,mpaka siku mama yake anafariki....akaongezea kwa kusema,,"tumebaki wawili tu mimi na kaka yangu,,lakini sijui kaka yangu alipo!!!

    aliongea maneno hayo huku akinyanyuka kitandani na kuzipiga hatua,,akafungua kabati,,akachukua baadhi ya picha alizopiga na Mbigili,,akampa Anita azitazame..

    wakati Anita anatazama picha hizo,,ghafla akashtuka!!!!

    akasema,,"MBIGILI!

    Apolo akastaajabu! akauliza kwa mshangao,,"MBIGILI ni nini?

    kabla Anita hajaanza kusimulia,  ghafla simu ya Apolo ikaita!

    alipoitazama akaona mmoja kati ya madereva wa kampuni yake,,anampigia simu!

    TAHARUKI!!!!!!





    apolo akaipokea simu hiyo,,,akashtusha na taarifa,,ambayo inaeleza kuwa kakutwa mtu ukimtazama kwa harakaharaka unaweza kuhisi kuwa ni kichaa ndani ya moja kati ya magari ya kampuni ya Apolo,,,

    dereva huyo aliongezea kwa kusema,,kuwa mtu huyo anadai anaitwa Mbigili...

    Apolo akashtuka!!! akauliza Mbigili ndio nini? Mbona simfahamu mtu mwenye jina hilo? mtoeni ndani ya gari aondoke zake...

    Apolo aliongea maneno hayo kisha akakata simu!



    Yule derva akaamua kumuondoa Mbigili kutoka ndani ya gari hilo,,huku akisisitiza kuwa bosi amesema hakufahamu!

    Mbigili hakuwa na ujanja,, hakuona haja ya kujaza umati wa watu,,,akihofia huenda watu wakamuona na kumtambua kuwa anahusika na tukio la mauwaji kule kwenye mgahawa...akaamua kutoka ndani ya gari hilo na kutokomea kusikojulikana!



    wakati huohuo kule nyumbani kwa Apolo,,,maongezi yaliendelea,,Anita akamuuliza Apolo,,"nimesikia umetamka jina Mbigili,,,unamaaniwha ndio huyu niliyemuona kwenye picha?

    Apolo akasema huyu kwenye picha ni kaka yangu,,na jina lake anaitwa JUMBE,,itakuwa umemfananisha haitwi Mbigili!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Anita akabaki mdomo wazi huku akimtazama Apolo,,,,ghafla wazo likamjia,,,akakumbuka kuwa aliwahi kupiga picha na Mbigili,,,na kuirusha kwenye mtandao wa kijamii wa facebook!!

    akachukua simu yake kisha akafungua akaunti yake ya Facebook,akaitafuta picha hiyo,,,,akafanikiwa kuiona,,akaamua kumuonyesha Apolo,,

    Apolo akastaajabu kumuona kaka yake kwenye picha moja akiwa na Anita!

    macho yakamtoka akasema,,huyu ni kaka yangu,,inamaana sikuizi kabadilisha jina? mbona hiki ni kizungumkuti!

    unamaanisha yupo kenya?

    Anita akasema,,"ndio alikuwa anaishi kenya lakini kwa sasa sijui wapi alipo,,,,aliwahi kuwa dereva wangu,,,,lakini sikumoja.......

    Anita akasita kuendelea kusimulia,,chozi likamdondoka!!

    Apolo akazidi kuchanganyikiwa,,akauliza,,"unalia nini kipenzi?

    Anita hakujibu kitu,,akaendelea kuli mfululizo!

    Apolo akachukua simu yake na kumpigia yule dereva!

    akamwambia kuwa,,,safari ihairishwe,,,ahakikishe anamtafuta Mbigili popote alipo mpaka ampate,,,,

    Dereva huyo akashangazwa na maneno hayo! akauliza,,"bosi ulisema humfahamu mtu yule nikamfukuza kama ulivyoniagiza,,na ameshaondokazake sasa mimi nitampata wapi?

    Apolo akasema,,"fanya uwezavyo umpate mtu huyo hakikisha unampata na unakujanae huku tanzania,,,kwa kufanya hivyo nitakuongezea mshahara mara kumi ya mshahara wako!

    Dereva huyo akashtuka,,,akapigwa na bumbuwazi!

    hakuamini kile alichokisikia katika masikio yake,,akatabasamu kisha akajisemea moyoni,,"mwaka huu lazima nijenge nyumba,,yani kumkamata kichaa,,ni  kazi rahisi sana,,,lakini kwa nini bosi anasisitiza nisirudi pasipokumpata yule kichaa?

    akaliegesha hilo kando ya barabara,,akakodi bodaboda na kuanza kumtafuta Mbigili kona zote za mitaa...



    Upande mwingine alionekana Mbigili akiingia ndani ya mtaro ambao aliufanya kama makazi yake!



    Dereva huyo alimtafuta pasipo mafanikio yoyote,,baada ya masaa mengi kupita,,,hqtimae giza likaanza kuingia!!! dereva huyo akaamua kukodi chumba cha kulala katika nyumba ya kualala wageni,,akajipumzisha usiku huo,,,



    Upande mwingine alionekana Mbigili akitoka ndani ya mtaro huo,,akazipiga hatua kwenda kutafuta chakula kutokana na njaa kali aliyokuwanayo,,,

    katika pitapita zake akastaajabu kuliona lile gari likiwa limeegeshwa kando ya barabara,,,akajisemea moyoni,,"inamaana bado hajasafiri mpaka muda huu,,,wacha nijaribu kuongeanae nimueleze kilichonitokea huenda akanielewa! lakini kwa nini Apolo ananikana anasema hanijui??

    wakati anawaza hayo yote ghafla wazo likamjia,,akakumbuka kuwa jina la Mbigili....Apolo halifahamu!,,''mmh! bila shaka ndio sababu amesema hanifahamu,,,wacha nisubiri hapa hapa mpaka dereva huyu atakaporudi...

    Mbigili akaamua kuketi kando ya gari hilo,,

    Alibaki hapo kwa masaa mengi pasipokuona dalili zozote za dereva huyo kuja hapo katika hilo gari,,,njaa ikamzidia akaamua kuondoka kwenda kutafuta chakula maeneo ya karibu na hapo..



    Wakati huo huo,,alionekana ye dereva,,akitoka ndani ya nyumba hiyo ya wageni,,,akajisemea moyoni,,"wacha nikalitoe gari pale kando ya barabara,,nikaliegeshe sehemu yenye usalama,,kunamzigo wa mamilioni ndani yake!

    baada ya dakika kadhaa akafika eneo hilo,,akaingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake!



    Wakati gari linaondoka,, ndio muda ambao Mbigili alikuwa anarudi pale lilipokuwa limeegeshwa gari hilo,,,alipofika akastaajabu kutokulikuta gari hilo! alipoangaza angaza macho yake akafanikiwa kuliona likiishilizia kwenye kona,,,akaanza kutimua mbio kulifuata gari hilo!

    wakati anakimbia akamuona Baba yake mdogo na Anita,,akiwa kasimama kando ya barabara akisubiri magari yapungue avuke barabara,,Mbigili akasita kukimbia,,Baba yake mdogo na Anita akageuza shingo yake kutazama upande wa kushoto,,wakakutanisha macho na MBIGILI!!!!

    TAHARUKI!!!!!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    lakini Baba yake mdogo na Anita hakumuona Mbigili,,kwa sababu Mbigili alikuwa kachakaa anaonekana kama kichaa! hata muonekano wa sura yake umepotea kabisa!

    pia giza lilichangia Mbigili kutokutambulika!

    Mbigili akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana,



    wakati huo huo,upande mwigine akaonekana yule dereva akiwa tayari ameshaliegesha gari,,,akazipiga hatua kurudi kule kwenye nyumba ya kulala wagen...

    baada ya dakika kadhaa akawa amefika,,akaingia ndani ya chumba alichokikodi,,,akajilaza kitandani...lakini akili na mawazo yake yote yote,,aliwaza namana ya kumpata Mbigili....



           **************************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog