Search This Blog

NZITA - 2

 







    Simulizi : Nzita

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    alizipokea na safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza....kwa sababu njia ya kuelekea kwa mganga huyo ilikuwa ni katikati ya misitu..hivyo iliwalazimu kuacha gari.... jasmini alikabidhi gari lake kwa mlinzi wa hotel kisha akamlipa ili alilinde gari lake kwa usalama zaidi ""walichukua makoti makubwa"" jasmin alinunua makoti yale kwa sababu Anaijuwa vyema milima hiyo kwani yeye ni mpogoro ni mzaliwa wa huko.. milima hiyo inabaridi sana........walianza kuzipiga hatua kuelekea kule inapopatikana milima ta ulugulu.... walitembea kiasi cha lisaa limoja na hatimae wakaanza kuufikia ule mlima ambao anapatikana mganga Sumbi... zanida alikuwa akistahajabu jinsi milima ile ilivyokuwa mikumbwa na mirefu....baada ya muda wa lisaa limoja walifika lile eneo ambapo anapatikana mganga sumbi... walipoanza kuingia eneo lile walistahajabu kukutana na vinyago vya kutisha pamoja na mafuvu mawili ya binadamu yakiwa yametundikwa juu ya miti miwili iliyo onekana kuwa ndio mlango wa kuingilia hapo kwa mganga sumbi.... mara ghafla... walistuka wakaogopa sana baada ya kusikia sauti huku mtu aliyekuwa akitoa sauti hiyo bila kuonekana....sauti hiyo ilisema tawile tawile (karibuni karibuni) punde mganga sumbi alijitokeza kichawi..... alijitokeza baada ya kugumdua kuwa watu wale wamekuja walikuwa ma shida nae.... pia alimkumbuka jasmin alishawahi kuwa mteja wake miaka ya nyuma...

    aliwakaribisha kisha zanida akaongea shida yake..

    mganga sumbi alimwambia kuwa tiba yako itachukuwa siku tatu hivyo atabaki hapo kuanzia siku hiyo kwa matibabu.... zanida aliogopa kwa sababu mlima ule ulikuwa na misitu yenye kuleta giza pia mazingira ya pale yalionekana kutisha sana palikuwa na vitu na vinyago vya kutisha... jasmin alimsihi kuwa asiogope... baada ya siku tatu kuisha atarudi kumfata.... kwa sababu zanida alimuamini sana jasmin alikubali kubaki hapo peke yake....

    jasmin na kijana yule waliondoka...

    ilipofika usiku majira ya saa saba usiku zanida alistahajabu sana kuona watu... pia sehemu ile palibadilika muonekano yani hapakuwa kama palivyokuwa mwanzo mara ghafla...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ghafla aliona kuna mtu anazipiga hatua kuelekea pale alipokuwa ameketi... zanida aliogopa sana na mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu mtu yule alisogea mpaka karibu kabisa na zanida"" mtu yule alikuwa na muonekano wa kutisha sana alikuwa mrefu sana pia alikuwa na jicho moja katikati ya paji lake la uso... mtu yule alipomkaribia zanida"" zanida alipoteza fahamu.... mtu yule wa kutisha alianza kuziondoa nguo za zanida mpaka akabaki utupu(uchi wa mnyama) kisha mtu yule alimuingilia kimwili zanida......mtu yule alipomaliza haja zake alinyanyuka....na kutoweka kichawi...



    **********



    Mnamo majira ya saa tano Asubuhi zanida alizinduka fahamu zikarejea"" kutokana yule mtu alikuwa na maumbile makubwa kuliko binadamu wa kawaida zanida alichanika sehemu zake za siri

    (ukeni) damu zilikuwa zikimtoka zanida alihisi maumivu makali sana....alipojitazama aliona kuwa yupo mtupu(uchi wa mnyama) zanida alianza kulia na kujutua kwa nini amekwenda huko!!! haya yote yametokana na ujinga wangu nilioufanya miaka ya nyuma laiti kama nisingechanganya masomo na mapenzi haya yote yasingenipata.. alijisemea moyoni huki akilia kwa uchungu mkubwa.... mganga yule alizipiga hatua na kuelekea pale zanida alipokuwa amelala huku akiwa uchi wa mnyama... kisha mganga sumbi akasema usisikitike kwani kilichokuwa kinakunyima amani katika maisha yako kimekwisha... sasa utapata mtoto na jina lake utamuita "NZITA" zanida alistuka kisha akauliza NZITA!!!??? jina hilo linamaana gani? ,,."" Mganga sumbi alicheka kisha akajibu NZITA" maana ya NZITA ni mtoto kutoka kuzimu.... zanida aliogopa sana inamaana mtoto nitakayezaa atatoka kuzimu kama ndivyo hivyo hapana mimi siwezi kulea mtoto wa kishetani!!! "alisema hivyo zanida mganga alinyanyuka na kuanza kuzipiga hatua kuelekea upande mwingine kisha akasema hapo ulipo yayari wewe ni mjamzito.... macho yalimtoka zanida inamaana mtoto nitakayemzaa atakuwa sio damu ya mume wangu!!! ??? alijisemea moyoni zanida huku macho yakimtoka kama fundi saa kapoteza nati....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***BAADA YA SIKU TATU KUPITA***



    mganga aliamuru zanida aondoke kwa tayari amekwishapa tiba iliyo mleta.... zanida aliongozwa na kijana msaidi wa mganga sumbi kutoka kwenye mlima huo.... kumbe wakati huo jasmin alikuwa njiani kumfuata rafiki yake ni baada ya kuambiwa kuwa baada ya siku tatu matibabu ya zanida yatakuwa yamekamilika.... walikutana njiani... kisha wakaanza kurudi wote kuelekea kule jasmin alipokuwa amelipaki gari lake....

    baada ya mwendo wa lisaa limoja hatimae walifika chini kabisa ya mlima huo... walitembea na baada ya nusu saa walifika mpaka pale jasmin alipokuwa amepaki gari""kwa kuwa giza lilikuwa limeanza kutanda waliona si vyema kusafiri usiku... waliamua kuchukua chumba cha kulala katika nyumba ya kulala wageni.... hawakuona haja ya kuchukua vyumba viwili walkamua kuchukua chumba kimoja..... kisha wakaagiza chakula kupitia muhudumu mmoja wa gest hiyo.... zanida alianza kumsimulia yale yote aliyoyaona huko mlimani kwa mganga sumbi... jasmin alimuonea huruma rafiki yake kipenzi kisha akamkumbatia kumfariji..... punde chakula walichoagiza kililetwa mlango uligongwa"""" zanida anyanyuka na kufungua mlango kisha akakipokea chakula hicho..... walianza kula..... huku wakipiga stori na kucheka....

    (kama kawaida ya matafiki wawili wakikutana)

    walipomaliza kula,,, zanida aliingia bafuni kuoga kwa sababu zilipita siku tatu bila kuoga kwa sababu kule kwa mganga hakuna bafu wala maji ya kuoga.....alipomaliza alitoka bafuni kisha jasmin akafuatia.... baada ya muda walizima taa na kuanza kuutafuta usingizi......jasmin alikuwa wa kwanza kusinzia......zanida hakuweza kupata usingizi kwa haraka kutokana alikuwa akikumbuka yale yaliyomtokea kule mlimani kwa mganga sumbi... kilichokuwa kinamchanganya zaidi akikumbuka kauli ile ya mganga sumbi kuwa tayafi yeye ni mjamzito... je mume wamgu siku akijua!!!!!???? alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu... baada ya dakika kadhaa usingizi ulianza kumnyemelea na hatimae akasinzia....

    akiwa usingizini aliota ndoto alihisi kunamtu anampapasa papasa sehemu ya mwili wake... kumbe yule mtu wa kutisha alikuwa kavutiwa sana na zanida hivyo alianza kumfatilia....kumbe haikuwa ndo ilikuwa ni kweli yule mtu anapapasa mwili wake ile anataka kumuingilia kimwili mara ghafla...



     zanida alistuka kutoka usingizini... akanyanyuka kitandani na kuwasha taa...ule mzimu ukayayuka na kitoweka kichawi zanida hakuina kilichokuwa kikiendelea..... alistahajabu akaogopa sana alipojikuta kalowana sehemu zake za siri(ukeni)

    lakini aligundua kuwa hakuingiliwa kimwili. ...zanida alimuamsha jasmin na kumwambia alivyoota... jasmin akasema hiyo ni ndoto tu lala tu. zanida alijifunika shuka na kuanza kuutafuta usingizi... baada ya dakika kadhaa alianza kusinzia...



    ********



    Palipokucha walidamka na kujiandaa kwa safari ya kurudi dar es salaam.. kisha safari ikaanza....

    mnamo majira ya saa saba za mchana waliwasili dar es salaam..... jasmin aliliendesha gari mpaka nyumbani kwa zanida walipofika zanida alishuka kisha jasmin aliondokazake kuelekea magomeni nyumbani kwake...



    Zanida aliingia jikoni kisha akaanza kuandaa chakula....na baada ya lisaa limoja chakula kilikuwa tayari.... alipakua na kuanza kula....kisha akapanda kitandani kujipumzisha,,, punde akapitiwa usingizi alipostuka ilikuwa ni saa nane za usiku...hakushangaa sana aliamini..kuwa huenda kalala masaa mengi kutokana na uchovu wa safari... aliamua kuendelea kulala..

    Asubuhi palipokucha alistahajabu akaingiwa na uwoga wa hali ya juu baada ya kujikuta tumbo lake limechomoza kama mwanamke mwenye mimba ya miezi minne(4) aliogopa sana ghafla ikasikika sauti ikimwambia usiogope zanida ndani ya tumbo lako kuna mtoto wa kike... siku ikifika utazaa na jina lake utamuita "NZITA" kisha sauti hiyo haikusikika tena... zanida aliogopa sana alitazama huku na kule kutafuta sauti ile ni wapi inatokea.. lakini hakuona mtu aliyekuwa akitoa sauti hiyo!!!!!

    MUMGU WANGU"" je mume wangu akijua kuwa ujauzito huu sio wake si ataniuwa!!? alijiuliza zanida..... ghafla simu yake ikaita alipoitazama aligundua kuwa Mumewe anampigia alipoipokea

    Nassoro alisema kuwa siku ya leo nitaingia TANZANIA marija ya saa mbili za usiku nimekuletea zawadi Mke wangu kipenzi.... wakati nassoro akiongea hivyo mawazo na akili ya zanida haikuwa makini kusikiliza kile alichokuwa anakiongea nassoro kwani zanida alikuwa akiwaza kuhusu mimba yake hiyo ya kimiujiza..... zanida aliitikia tu ok""" bila kujua nassoro kaongea nini!!! mbona kama hauna furaha mke wangu... au kunatatizo??? aliuliza nassoro"

    hapana najihisi uchovu tu mume wangu""alisema zanida......ok pole sana mke wangu nakutakia mapumziko mema,,,"""mimi najiandaa kuelekea UWANJA WA NDEGE (Airpor) kisha nassoro akakata simu......

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    zanida alihisi kuchanganyikiwa kwani hakuwahi kumwambia mumewe kuwa yeye ni mjamzito tangu mumewe aliposafi miezi mitano iliyopita alijiuliza ataanzaje kumwambia mumewe ili amuelewe... zanida aliamua kuchukua simu yake na kumpigia jasmin kisha akamsimulia kuhusu tumbo lake na ujio wa nassoro kurudi Tanzania" jasmin alistahajabu sana...aliamua kuliwasha gari na kuelekea nyumbani kwa zanida... baada ya muda jasmin alifika kisha akamwambia waende hospitol kwenye vipimo ili wakahakikishe kama kweli ilikuwa ni mimba... muda huohuo waliingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea hospitali... walikwenda mpaka hospitali ya MNAZI MOJA.. kisha zanida akafanyiwa vipimo.....zanida alistahajabu baada ya kuambiwa na daktari kuwa anaujauzito wa miezi minne(4) hakuamini ilibidi amwambie daktari ampeleke kwenye kipimo cha U-TRA SOUND

    vipimo hivyo vilionesha kuwa kuna mtoto ndani ya tumbo..... zanida alihisi kuchanganyikiwa... hata daktari alistahajabu kumuona zanida katika hali ile ya kuinesha kutokuwa na furaha juu ya ujauzito wake. ... zanida alilipia gharama za vipimo kisha wakaanza kuzipiga hatua kuelekea upande wa nje waliingia ndani ya gari....jasmin aliliwasha ghali na kuelekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwa zanida... zanida alishuka kutoka ndani ya gari kisha jasmin akaondoka zake... zanida alizipiga hatua kuelekea ndsni kwake.... alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake... ile amefungua mlango wa chumbani kwake mara ghafla...



    Mara ghafla simu yake iliita.. alipoitazama aliona jasmin anampigia... aliipokea alistuka sana baada ya kupewa taarifa kuwa ndege iliyokuwa inasafiri kutoka Amerca kuelekea Amsterdam ili abiria wapande ndege nyingine kuunganisha safari ya kwenda Africa ya mashariki... imepata hitirafu na kuangukia baharini... kwa mujibu wa taarifa hakupona mtgu hata mmoja.... nassor naye pia alikua miongoni mwa abiria waliopanda ndege hiyo.... taarifa hizo jasmin alizipata taarifa hizo kupitia radio iliyokuwa ndani ya gari lake....

    Zanida alihisi kuchanganyikiwa aliangua kilio kikubwa...alilia kwa uchungu sana Eee Mungu wangu ninamkosi gani mimi...alisema maneno hayo huku akilia...

    baadhi ya maiti hazikupatikana baharini humo... miongoni mwa maiti hizo na ya Nassoro haukupatikana pia.....



    *****BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA******



    Tumbo la zanida liliziku kukuwa.....ulikuwa ni ujauzito wa miezi saba..

    sikumoja zanida aliota ndoto""alikuwa ni usiku wa manane akiwa usingizini aliona vitu vya ajabu sana aliona yule mtu wa kutisha aliyemuingilia kimwili amekuja na kumchukuawa zanida kisha akaondokanae....walitokezea KUZIMU....kisha mtu yule wa kutisha alizipiga hatua mpaka kwenye lango kubwa... lango hilo lilifunguka kisha akatoka mtu wakutisha zaidi... mtu huyo alikuwa na mapembe mawili na jicho moja katikati ya paji lake la uso......kisha akazipiga hatua kuelekea pale alipokuwa kasimama zanida... ""zanida aliogopa na mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio.alipotaka kumshika zanida alistuka kutoka usingizini... zanida alianza kufanya maombi alisali... kisha akatoka chumbani akaelekea upande wa sebule.... zanida alistahajabu kukuta vitu vyote vya sebuleni vikielea hewani aliweza kuona hivyo kwa sababu taa ya kibarazani ilikuwa ikiwaka hivyo mwanga ulipenya mpaka sebuleni kwa kupitia dirisha.... zanida aliogopa akawasha taa haraka... ghafla vitu vile vilirudi kama vivyokuwa mwanzo.... zanida aliogopa sana.. alirudi haraka chumbani kwake... alipoingia alipanda kitandani hakuzima taa... alibaki macho mpaka kukakucha...



    ************



    Asubuhi alijiandaa na kuanza safari ya kwenda Magomeni kwa rafiki yake jasmini... alipofika alimsimulia mambo yote aliyoyaona usiku wa jana... jasmin alistahajabu sana... aliamua kumpeleka kwa mganga mwingine.... safari ilianza muda huohuo,,, waliingia ndani ya gari na kuanza safari ya kwenda kwa mganga.... walipofika zanida alieleza ukweli wa mambo kwa mganga huyo aitwae KUMBA.....kumba alisema nitakusaidia lakini kwa masharti mawili" inahitajika kafara la damu ya chimbuko lako (baba au mama) au mtoto utakayemzaa atakuwa ni wakala kutoka KUZIMU...mganga aliendelea kupiga tunguli zake ghafla akasita...kisha akasema usiku wa leo usilale pefke yako... zanida aliamua kukubali mtoto huyo atakaemzaa awe wakala wa Kuzimu...kuliko kumtoa baba au mama.... kwanza niliingiliwa kimwili na jitu la ajabu.. acha awe tu wakala kutoka kuzimu... alijisemea moyoni zanida.

    siku zilisonga..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA****



    mimba ya zanida ilifikisha miezi tisa ilibidi ahamie nyumbani kwao.... sikumoja majira ya saa sita usiku zanida alihisi maumivu makali chini ya tumbo maumivu hatimae maumivu hayo yalihamia kwenye kiuno... alimuita mama yake.... mama zanida aliingia haraka chumbani kwa zanida... (UTUUZIMA DAWA) mama zanida aligundua kuwa mwanae anasumbuliwa na uchungu.... ilikuwa ni muda muafaka wa kujifungua... baba zanida aliwasha gari na mumkeleka hospitali ya AMANA...madaktari waliokuwepo zamu walimpokea zanida haraka na kumuingiza moja kwa moja katika wodi ya wamama wajawazito.... mnamo majira ya saa tisa za usiku zanida alijifungua mtoto wa kike..baada ya mtoto kutoka mara ghafla..



    baada ya mtoto kutoka mara ghafla zanida aliishiwa nguvu na kuzimia""" zanida alichanika sehemu kubwa na uke wake kwa sababu mtoto alikuwa na ukubwa usio wa kawaida.... hata madaktari na manesi waliokuwa zamu siku hiyo,, walistahajabu sana baada ya kumuona mtoto huyo mchanga alikuwa na ukubwa usio wa kawaida walipompima kilo...alikuwa na kilo kumi na sita(16)

    zanida alitundikiwa dripu ya maji... iliyokuwa na dawa ya kusti presha....na baada ya lisaa limoja zanida alizinduka akapata fahamu... alihisi maumivu makali kwenye uke wake.. kwa sababu alishonwa.... zilipopita siku tatu zanida aliruhusiwa kwenda nyumbani.



    ******BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA*******



    mtoto wa zanida aliendelea kukuwa.....zanida alifuata masharti aliyopewa na mganga... alimpa mwanae jina la NZITA....mtoto huyo mchanga wa kike alikuwa mzuri sana.. alifanana sana na zanida

    ""Siku zililidi kwenda... Nzita alizi kukuwa.... siku moja jasmin alikwenda kumtembelea zanida... alipofika nyumbani kwa zanida alibisha hodi zanida aligundua kuwa ni jasmini baada ya kuliona gari la jasmini kupitia dirisha lake la chumbani... zanida alimuacha Nzita sebuleni akiwa amesinzia....kisha alienda kuoga... hakuwa na wasiwasi kwa kuwa mtoto alikuwa kalala.....jasmin aliendelea kugonga hodi... zanida alipaza sauti... ingia ndani mlango upo wazi.... jasmini alipoingia sebuleni alistahajabu kukuta watu wawili waliovalia mavazi meusi marefu kama kanzu.. wamemzunguka Mtoto Nzita.. ghafla watu wale walitoweka kimiujiza.....mmh!!! hivi naota au ni kweli nilikuwa naona hicho nilichokiona!!!? alijisemea moyoni jasmin... huku amesimama pale pale mlangoni... punde alikuja zanida.... vipi mbona umesimama!!!? aliuliza zanida

    hapana shosti ndio nimeingia hivyo... jasmin hakutaka kumueleza zanida kile alichokiona....



    ghafla nzita aliamka na kuanza kulia.. zanida alimnyanyua nzita na kuanza kumnyonyesha.

    huku wakipiga stori...kama ilivyo kawaida marafiki wawili wakiwa pamoja.. hasa wanawake.... walipiga stori huku wakicheka.... mnamo majira ya saa mbili isiku jasmin alimuaga zanida kuwa anarudi nyumbani kwake... """sawa shosti wacha mimi nimuogeshe nzita kisha nim-bembeleze alale...alisema hivyo zanida"""

    jasmin alitoka nje akaingia ndani ya gari lake,,, aliliwasha na kuondokazake....aagh itabidi nitafute mfanyakazi wa ndani Nzita mwanangu unanichosha sana mimi mama yako.. zanida aliongea maneno hayo huku akimuangalia mwanae usoni.... baada ya kumaliza kumuogesha nzita alimnyonyesha na baada ya dakika kadhaa nzita alisinzia... zanida aliweka neti na kumuweka nzita kunako kitanda.... kisha na yeye akaanza kuutafuta usingizi....na baada ya dakika kadhaa usingizi ulimnyemelea hatimae akasinzia kabisa..

    wakati zanida akiwa usingizini aliota kuwa kuna watu wamekuja chumbani kwake wakamchukua nzita.... watu hao walikuwa wawili.. wamefunika nyuso zao kwa kitambaa chekundu huku wamevalia mavazi meusi marefu kama kanzu.. aliona wananyanyua nzita kutoka kitandani... zanida alistuka kutoka usingizini.. alipotazama kando ya godoro alipokuwa amelala nzita alistahajabu kuona nzita akielea hewani.. zanida aliingiwa na uwoga wa hali ya juu huku mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio... alinyanyuka haraka kutoka kitandani... akawasha taa... alipotazama kitandani mara ghafla...



    alipotazama kitandani... mara ghafla alistahajabu kumuona nzita kala t usingizi...zanida alipoangaza angaza macho hakuweza kuwaona watu wale!!!!

    hivi hii ni ndoto au nilikuwa naona kweli?!! alijisemea moyoni zanida"""aliamua kurudi kitandani na kuacha taa ikiwa inawaka... alimkumbatia nzita kisha akaanza kuutafuta usingizi... punde alisinzia""



    *******BAADA YA MIAKA MITATU KUPITA*******

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nzita alizidi kukuwa... alifanana sana na mama yake.... hivyo nzita alikuwa mrembo sana.... siku moja majira ya usiku wa manane.... zanida aliamka kwa lengo la kunywa maji... kiu kilim-bana

    alistahajabu akaogopa sana baada ya kuona nzita hayupo kitandani.... zanida alinyanyuka haraka kutoka kitandani akawasha taa lakini bado hakumuona nzita....zanida alihisi kuchanganyikiwa.... jamani mwanangu!!! atakuwa kaenda wapi???? mbona huyu mtoto ananipa mawazo kila kukicha!!! ""alijisemea moyoni zanida... huku uso wake ukiomesha kujawa na wasiwasi mkubwa... alipojaribu kufungua mlango mlango ulikuwa umefungwa""" inamaana nzita kapitia sehemu gani!!!! alijiuliza bila kupata majibu.... zanida alianza kuzipiga hatua kuelekea sebuleni....alistahajabu kukuta nzita kakaa peke yake katikati ya sebule.... zanida aliogopa akaamua kuwasha taa""mara ghafla hakumuona tena nzita....zanida alistuka...kanga zilimdondoka... akarudi haraka chumbani... ile kaingia tu.. hakuamini alichokiona... alimkuta nzita yupo kitandani kalala usingizi mzito.. zanida aliogopa sana mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio....aliogopa hata kurudi kitandani.... aliamua kuketi kwenye sofa lililokuwa chumbani humo.. alibaki macho mpaka kukakucha....



    ***********





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog