Search This Blog

SHUHUDA - 5







      Simulizi : Shuhuda

      Sehemu Ya Tano (5)



      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      ule upande wa pili wakati huohuo kamishna alipigiwa simu kutoka makao makuu....kamishna aliambiwa kuwa leo ndio siku anayotakiwa karimu ili apelekwe kwenye kazi ya upelelezi hivyo atafuatwa na muwakilishi/ mwenyeji wake.....kamishna alichanganyikiwa alijiuliza je huyo muwakilishi akifika itakuwaje atamjibu nini!!!!!

      alichukua simu yake akampigia peter peter alipokea simu kisha kamishna akasema unaweza kuniaaidia nimpate karimu....peter alistuka akahisi kamishna anataka kumzunguka....akaamua kukata simu....kamisha alishangazwa kwa kitendo hicho cha peter kukata simu.....""inamaana huyu mwanaharamu anataka kunizunguka!!! alisema peter kisha akaamuru karimu achukuliwe apelekwe mafichoni tofauti na hapo nyumbani kwa peter....kwa sababu alikuwa ameshaingiwa na wasiwasi na kamishna huenda anataka kumzunguka..."""polisi sio mtu wa kumuamini kwa sababu muda na wakati wowote anakugeuka kama hakujuii...peter alijisemea moyoni....kisha akawapa maelekezo majasusi wanne ni wapi Karimu apelekwe....



      *****************

      feisal hakuweza kumtabua baba yake kwa sababu ni miaka mingi imepita alimuacha feisal akiwa na miaka mitatu.....lakini huwezi amini damu ni nzito kuliko maji....kipindi wanambeba karimu kumuingiza ndani ya gari.zile ndevu na sharubu za bandia zilichomoka na kudondoka chini hivyo sura ya karimu ilionekana...feisal alipo ona hivyo kumbukumbu ilimjia akamkamtambua kuwa huyo ni baba yake....

      (watoto chini ya umri wa miaka sita wanauwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu kwa miaka isiyopungua 60)

      feisal alipaza sauti akaita""BABA............

      sauti ile iliweza kupenya masikioni mwa karimu aliitambua sauti hiyo ni ya feisal..akafumbua mcho lakini bado kizunguzungu kilitawala kichwani mwake... wale majasusi walipomuingiza ndani ya gari.............gari liliwashwa na safari ikaanza ya kwenda kumpeleka karimu kule mafichoni......kipindi wanatoka...dakikachache kupita kamisha alifika nyumbani kwa peter lakini alistahajabu alianza kufyatuliwa risasi mfululizo akageza gari na kuliendesha kwa kasi kuondoka eneo hilo...

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      *************



      wale majasusi wanne walionekana wakiliingiza gari kule kwenye kile kiwanda ambacho hakifanyi kazi kumbe karimu alizinduka na kupata fahamu muda mrefu tangu kule nyumbani kwa peter..lakini aliendeleakufumba macho ili wasimstukie.....punde wale majasusi walishuka kutoka ndani ya gari wakambeba karimu kwende kumficha huko upande wa juu...wakiwa wamembeba mara ghafla..





      karimu alichoropoka akaanza kurusha ngumi na mateke mfululizo..aliwapiga watu majasusi wale mpaka wakauwawa kwa kipigo kizito....karimj alipohakikisha hakuna hata mmoja anayeweza kuamka pale chini....karimu alizipiga hatua za harakaharaka akaingia nda ya lile gari....ambalo majasusi wale walilitumia kumleta hapo.....akaliwasha na kuianza safari kuelekea nyumbani kwake...aisee karimu ni mtu hatari sana alipofika nyumbani kwake aliingia mpaka ndani.....akapanda juu la dari akatoa bunduki matata.....bunduki hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi mia moja..huku ikiwana mkanda mwingine wa nje ukiwa na risasi mia tano pamoja na mabomu mawili moja la kutegesha na jingine la kurusha kwa mkonk(grunet) ....kisha akatoka upande wa nje na kuingia ndani ya gari.



      ***************



      ule upande mwingine alionekana mwanamke akishuka kutoka ndani ya gari lililofika na kusimama nje ya makao makuu ya jesgi la polisi pale stesheni...mwanamke yule alikuwa kavalia koti la suti nyeusi na sketi fupi yenye rangi nyekundu....mwanamke huyo alikuwa ni miwakilishi kutoka USALAMA WA TAIFA...alikuwa katumwa kufatilia taafifa za karimu lwa nini hajarepot siku ya jana ambayk alikuaa anatakiwa aende kupewa kazi ya kumfatilia na kumchunguza gaidi hatari aliyekuwa akilisumbua na kulitilisa jiji kwa matukio ya kijambazi na mauwaji ya kikatili.. gaido huyo alikuwa hajlikani wala jakuna mtu aliyekuwa akiitambua sura yake....mwanamke yule alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya kamishna....alikaribishwa....kisha akaoa bahasha iliyokuwa na barua ndani yake na kumkabidhi kamishna...kamishna alipoifungua bahasha ile alichanganyikiwa baada ya kumaliza kuisoma barua iliyokuwemo ndani ya bahasha hiyo..

      barua hiyo ilisomeka hivi.....KUTOKANA NA UTOVU WA NIDHAMU..KUSHINDWA KUTOA TAARIFA NA KUMUAMURU KARIMU AJE MAKAO MAKUU...ILI AIFANYE KAZI YA KULITUMIKIA AIFA KUMCHUNGUZA NA KUMTIA MBALONI GAIDI ANAYE ISUMBUA NCHI......HUVYO KUANZIA LEO UMESHUSHWA CHEO KUTOKA KWENYE CHEO CHA KAMISHNA NA KUWA SAJENTI... macho yalimtoka kamishna.. kisha yule mwanamke alitoka nje na kuondoka zake......



      kumbe kamishna ndiye GAIDI MKUU aliyehusika na ujambazi pamoja mauwajI yote hayo yaliyopita na ambayo yanaendelea alikuwa akimiumia peter kama pazia la kumziba maovu yake ili asijulikane...hata yale madawa ya kulevya pamoja na Siraha nzito zilizoingizwa nchini kimagendo ueye ndiye muhusika mkuu.....hivyo peter alikuwa ni kibaraka wa Kamishna...hata jana yake peter alimgeuka kamishna baada ya kuona mambo yamekuwa magumu..

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      *****************



      upande mwingine alionekana peter akichukua unga wa madawa ya kulevya kiasi na kuuweka juu ya meza ya kioo kisha akaanza kunusa unga ule..

      wakati huohuo karimu alikuwa jirani kabisa kukaribia kuifikia nyumba ya peter.......baada ya dakika kadhaa karimua alifika... akalipaki gari mbali kidogo kando ya barabara...kisha akachukua ile bunduki pamoja na mkanda wake uliojaa risasi...akaanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya peter alipofika getini alitegesha bomu hilo maalumu kwa kuvunja chuma cha pua... kisha akaliseti lilipuke baada ya dakika tano...kwa sababu ilikuwa jioni giza lilianza kunyemelea...karimu alikimbia na kusimamaupande wa pili...

      wakati huohuo peter alionekana kutoka nje ya jumba lake la kifahari..ksha akaingia ndani ya gari pamoja na feisal akaliwasha na kuelekea getini ili afunguliwe atoke upande wa nje...alipolikaribia geti...mara ghafla bom lililipuka...

      kutokana na mlipuko mkubwa........mlipuko huo ulisababisha geti kung'oka likaruka kuelekea upande wa ndani......peter alistuka sana macho yalimtoka baada ya kuonabaadhi ya walinzi wake waliokuwa pale getini walipoteza maisha papohapo kutokana na mlipuko ule..moshi mkubwa ulitanda hewani na kulizunguka geti wakati anatahamaki mara ghafla karimu alianza kufyatua risasi mfululizo huku akizipiga hatua za taratibu kuingia upande wa ndani.... peter alitimua mbio kuelekea upande wa mdani huku akimuacha feisal ndani ya gari....feisal alimuina baba yake akapaza sauti""BABAAA....... karimu alistuka kusikia sauti hiyo aliitambua kuwa ni ua geisal....karimu alikimbia kuelekea kwenye gari hilo feisal alifungua mlango wa gari na kutoka nje akakumbatiana na mtoto wake...

      wakati huohuo peter alitoka nje huku ameshikilia bunduki alimuona vyema karimu amekumbatiana na mwanae.....peter akafyatua risasi kuelekea ule upande waliokuwepo karimu na feisal........risasi ile ilikwenda moja kwa moja...karimu alikuwa bdo kamkumbatia feisal mara ghafla...



      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      ghafla karimu alistushwa na mlio walisasi iliyowakosa na kupiga kwenye bodi la gari....karimu alimvuta haraka feisal na kumficha upande wa pili wa gari.....punde akafyatua risasi mfululizo kuelekea ule upande aliokuwepo peter...

      peter aliamua utimua mbio kuelekea uoande wa ndani....wakati anakimbia.....karimu alifyatua risasi iliyokwenda moja kwa moja kwenye mgongo wa peter akadondoka chini.....akaanza kutambaa kuifuata bunduki yake iliyodondoka kando baadaya kupigwa risasi.......kabla hajaifikia karimu alimuwahi kisha akaachia teke kali kwenye kidevu cha peter teke hilo aina ya (katafunua) lilimfanya peter agisi kizunguzungu...karimu hakutaka kupoteza muda alifyatua risasi iliyokwenda moja kwa moja kwenye kichwa cha peter akapoteza maisha papohapo....



      karimu alirudi haraka pale alipokuwa amemficha feisal akamchukua na kuanza kuondoka eneo hilo...mara ghafla kalimu alisita kutembea akaamua kurudi na kuingia mdani kabisa kunako nyumba ya peter.....akaanza kupekuapekua....aliona kompyuta akaiwasha....alipojaribu kutazama mafail...aliona picha za kamishna pamoja na video za matukio ya kijambazi yakiambatana na mauwaji ya kikatili aliyoyafanya kamishna....kafimu alistahajabu sana ""inamaana kamishna ndiye muhusika namba moja???karimu aliamua kutuma picha na video hizo zilizomuonesha vyema kamishna kwenye bihashara haramu na mauwaji....akazituma kwenye barua pepe(Email) ya makao makuu ya jeshi la polisi...akajitambulisha kuwa yeye ni karimu....kisha akaongozana na feisal mpaka upande wa nje mpaka pale alipokuwa amelipaki gari...wakaingia ndani ya gari na kutokomea kusikojulikana...



      ******************

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      upande mwingine kule makao makuu..alionekana mtu anayehusika na kitengo cha mawasiliano ya simu pamoja na barua pepe(Email) za Hapo makao makuu akiifungua barua pepe(Email) iliyoingia mduda mchache uliopita. alipoifungua alistahajabu kuona picha na video zikimuonesha kamishna akifanya bihashara haramu pamoja na mauwaji ya kikatili.. mtu yule alistika...mara ghafla kamishna aliingia kwenye chumba hicho cha mawasiliano....mtu yule alistuka ajaifunga ile barua pepe haraka ili kamishna asione kinachoendelea....kisha kamishna akaamuru kuwa simu yake iondolewe kwenye itambo ya mawasiliani ya moja kwa moja(DISCONECT) mtu yule hakutii amri kwa sababu kamishna hakuwa na cheo tena hivyo alisema ""nitaondoa endapo nitapata ruhusa kutika kwa MKUU....jamishna alichanganyikiwa akatoka nje na kuelekea kule alipokuwa amelipaki gari lake....alipofika alistahajabu kuona namba za gari lake zimebadilishwa na kiwekwa namba za kawaida(PLATE NUMBER) hakumuuliza mtu yoyote akaingia ndani ya gari na kuondoka zake.. alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa peter ili akamuangamize peter kabla hajakamatwa na kutoa siri..kamishna alipofika nyumbani kwa peter alistahajabu kukuta maganda ya risasi yametapakaa upande wa nje alafu geti limeng'oka....aliingia haraka moaka uoande wa ndani alipofika alishtuka kumuona peer akiwa chini amekufa. ......kamishna alianza kuingiwa na wasiwasi kisha akajisemea moyoni """ bila shaka huyu ni karimu ndiye aliyemuuwa peter sijui itakuaje kama peter ametoa siri.....akaingia upande wa ndani ili aangalie kama kunakitu kinachomuhusu akichome moto......alipoingia upande wa ndani alistahajabu kuina kompyuta ikiwa inawaka (ON) alipotazama aliziona zile picha alizopigwa akiwa katika bihashara zake haramu pia aliziona video zilizomuonesha akifanya mauwaji ya kikatili....akimuuwa boss wake KANALI Minja....punde Emaili iliingia alipoifungua aliona inatoka makao makuu""ikisema tunashukuru kwa taarifa zako tumezipata na tunazidanyia kazi.....macho yalimtika kamishna baada ya kuona zile picha na video zake...zimetumwa makao makuu........

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      *************



      kule makao makuu alionekana yule mtu anayehusika na kitengo cha mawasiliano akisikiliza mawasiliano ya simu za kamishna alizopiga na alizopigiwa..akawaita wakuu wake wa kazi na kuwasikilizisha walistahajabu kusikia kamishna akipanga mipango ya mauwaji tangu tito alivyouwawa akiwa sero(mahabusu)pia walisikia mipango yote aliyokuwa akiipanga na kumtuma peter akafuate mizigo bandarini ikiwa na madawa ya kulevya ndani yake. kisha wakaitafuta simu ya peter kwa kutumia (GPRS TRAKING)ili wabaini yupo maeneo gani....punde karimu aliingia makao makuu yajeshi la polisi...akaomba kuonana naka mkuu wa kitengo cha upelelezi...punde kwa mbali alimuona akija upande wake.....mkuu wa kitengo cha upelelezi alipofika kabla karimu hajaongea kitu alipewa mkono wa pongezi...kisha wakaongozana mpak ofisini kwake...

      karimu akapewa kazi ya kumkamata kamishna popote alipo..bila kuchelewa karimu aliingia ndani ya gari na kuondoka zake kwenda kumtafuta kamishna...huku akiwa ameongozana na gari tano za polisi

      wakati huo kamishna alionekana akitoka nje ya nyumba ya peter kisha akaingia ndani ya gari lake na kuondoka zake alipoingia barabara kuu alistuka kuona gari za polisi akaamua kugeuza gari ili arudi alipotoka...ghafla alimuona karimu nyuma yake akiwa kalizibia njia gari lake....punde mapolisi walilizunguka gari la kamishna...

      aliamua kuinua mikono juu.ishara ya kusalimu amri....mapolisi walisogea ili wamtoe kamishna ndani ya gari......walipomkaribia kumbe kamishna alikuwa na bomu ndani ya gari akalilipua bomu hilo...mlipuko mkubwa ukatokea...baadhi ya polisi waliokuwa karibu na gari la kamishna walipoteza maisha papohapo mlipuko ule ulikwenda mpaka kwenye gari la karimu ukalirusha gari la karimu kando karimu alijeruhiwa upande wa kichwani akapoteza fahamu...punde wale mapolisi waliobakia walilifuata gari la karimuwalipomtazama waligundua bado yupo hai kwasababu mapigo yake ya mouo walikuwa yanapiga...wakamtoa kisha wakamuingiza ndani ya gari moja la polisi kumbiza hospitali....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      karimu alifanyiwa huduma ya kwanza kisha matibabu yakaendea.. baada ya masaa kadhaa kupita karimu alizinduka na kupata fahamu alistahajabu kujikuta hospitali..alipogeuza shingo alimuona mkuu wa kitengo cha upelelezi akiwa na feisal..

      baada ya wiki moja karimu alipata nafuu akarudishwa kazini....siku iliyofuata karimu alipandishwa cheo na kuwa SIR MEJA...



      ***MWISHO***



0 comments:

Post a Comment

Blog