Search This Blog

TAREHE 9 SEPTEMBER - 4







    Simulizi : Tarehe 9 September

    Sehemu Ya Nne (4) 





    Zack akazidi kuchanganyikiwa,, akasema,, "huyo ni mke wangu lakini bado hatujafunga ndoa kuhalalisha,

    wakili akadakia na kumuuliza Zack,, "je? wazazi au walezi wa mwanamke huyo wanajua kuwa wewe unaishi na binti yao?

    Zack akasema hapana!

    wakili akatabasamu kisha akasema,, "ni kosa la jinai kuishi na mwanamke au kumfanya mkeo pasipo wazazi au walezi wake kujua,,, je?  kipindi unampiga alafu akufa,,ungewaeleza nini wazazi au walezi wake!?

    wakili huyo akazipiga hatua na kumtazama Hakimu, kisha akasema, Mh:Hakimu nimemaliza maswali, naomba mshtakiwa ajibu maswali,

    Hakimu akabaki mdomo wazi!!  kwa sababu faili la kesi ya Zack limeandikwa tofauti na ushahidi alioutoa wakili!

    Hakimu akaamua kuhairisha kesi na kuirusha tarehe, kesi hiyo isikilizwe siku nyingine!

    kiwha akasema,, anahitajika mtendewa aje hapa mahakamani siku hiyo kutoa ushahidi wake! kwa sababu bado yupo hai, hivyo ataeleza mbele ya mahakama kilichotokea,,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shirima akakasirika sana,, akajisemea moyoni,, mambo yameanza kuwa magumu,, endapo Shamy akija kutoa ushahidi,, atamtetea huyu, kwa sababu Shamy anampenda sana huyu bwege..

    Zack akarudishwa maabusu,, kusubiri siku ya kesi yake kusomwa tena.



                             *****************************************



    Siku zilizidi kusonga,, hatimae Shamy akapata nafuu,, akaruhusiwa arudi nyumbani..

    siku hiyo Shirima alimchukua Shamy akampeleka nyumbani,, walipofika,, Shirima akasema,, "nimemfungulia kesi yupo maabusu,, huyu kijana si mwema kwako angekuuwa,, ebu fikiria je?  asingekuja mtu hata mmoja kutoa msaada,, ingekuwaje?

    Maneno hayo ya Shirima yakaanza kumuingia Shamy,, akajikuta anaanza kumchukia Zack,, Shirima akasema,, "siku ya kesi itabidi useme kuwa alitaka kukuchoma kisu,, na huwa anakutishia mara kwa mara kukuuwa!

    Shamy akasema,, "sawa hakuna shida,, hata hivyo kweli angeniuwa kama majirani wasingekuja kutoa msaada,, nimeanza kuamini maneno yako Zack si mtu mwema kwangu!



    siku zilizidi kusonga,, hatimae tarehe ya kusomwa kesi ya Zack ikawadia...

    Shirima na Shamy wakaongozana mpaka mahakamani!

    Zack akapandishwa Kizimbani,, na kuanza kusomewa mashtaka,,, kisha akaitwa muhusikia aliyefanyiwa tukio ambaye ni Shamy mwenyewe....

    Shamy akapanda kizimbani kutoa ushahidi...







    Baada ya Shamy kupandishwa kizimbani akamtazama Zack kwa macho ya huruma.

    Shamy akasema ni kweli alinipiga nahisi ni kwa sababu ya hasira tu yule wakili muongo akadakia na kusema, "mheshimiwa hakimu mwanamke huyu atakuwa kaingiwa na uwoga baada ya kunusurika kuuawa hivyo anashindwa kunyosha maelezo.mimi kama wakili wa upande wake nitasimama badala yake, "Siku chache zilizopita mshitakiwa alimpiga mwanamke huyu pamoja na kumtishia kumuua pili, mshitakiwa huyu huyu miaka kadhaa iliyopita alifanya tukio la ujambazi akiwa na wenzake kwa kupola dhahabu ambazo ni mali ya Shirima.  Hakimu akauliza mbona sijawahi kuona jalada la kesi hiyo hapa mahakamani?  yule wakili aliyelipwa na Shirima ili atoe ushahidi wa uongo akasema, "ielelezo na ushahidi upo.Baada ya wakili huyo kusema hayo yote Shamy alishtuka dhamira yake ikamsuta.

    Shamy akasema, "Mheshimiwa hakimu kiukweli zack nimeishi nae miaka mingi na tangu nimjue sijawahi kumuona akijihusisha na vitendo vya ujambazi na pia hana tabia hiyo. Hakimu akashtuka akajisemea moyoni, "bila shaka hapa kuna namna na kuna siri nzito inayoendelea inaonyesha wazi kuwa kijana huyu amasingiziwa.

    Hakimu akasema, "mshitakiwa anaonekana hana makosa kesi hiyo ya ujambazi haina vielelezo vyenye ushahidi kuwa mshitakiwa anahusika kutokana na  sheria inavyosema mshitakiwa akalipa fidia ya kumpiga na kumjeruhi mwanamke huyu,kisha ataachiwa huru. shirima alikasirika kupita kiasi akaona mpango wake umegonga mwamba...



    Baada ya siku tatu zack akamlipa Shamy fidia,,, mbele ya mahakama... Zack akaamua kuondoka nyumbani kwa Shamy na kutafuta chumba cha kupanga..

    Shamy akaanza kupata wakati mgumu,, kwa sababu alikuwa anampenda sana Zack,, akaamua kumtafuta na kumuomba msamaha,, Zack pia hakuwa na namna kwa sababu alikuwa anampenda sana Shamy, akaamua kurudi kwa shamy,, na maisha yakaendelea.



    Siku zilizidi kusonga,, Shamy akaanza kuwa anamkwepa Shirima,, akaamua kubadilisha namba ya simu,,, hata akiwa kazini akawa hakai ofisini mara kwa mara akawa anazungukia wodi za wagonjwa ili Shirima asipate muda wa kuongea nae!

    kitendo hicho kilimfanya Shirima azidi kumchukia Zack! akaamua akaamua kufanya mpango wa kumuangamiza Zack..



    Siku moja Zack alikwenda kazini kwa Shamy,, ni baada ya Shamy kumuiga Zack kwa lengo la kumpa bahasha fulani iliyokuwa na nyaraka ndani yake,, nyaraka hiyo ilitakiwa ipelekwe almashauri.. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zack alipofika akaliegesha gari lake akimsubiri, Shamy alete bahasha hiyo,,, punde si punde, likaonekana gari likiingia na kuegeshwa,, kisha akashuka Shirima,,, wakati anashuka kunapicha zikadondoka amba, o Shirima hakuziona,, akazipiga hatua kulifuata jengo la hospitali,,

    Zack alimuona Shirima pia aliona Shirima kadondosha picha mbili! Zack akaamua kuzipiga hatua lulifuata gari la Shirima pale lilipokuwa limeegeshwa,,, akaziokota picha hizo mbili,,alipozitazama,, akashtuka sana,, macho yakamtoka baada ya kuona picha hizo! ni picha za mama yake,, picha moja ilikuwa ya mama yake akiwa peke yake,, na ile nyingine,alionekana mama yake,, pamoja na Shirima! picha hiyo ilionekana ya kizamani,,,

    Zack akahisi kuchanganyikiwa akajisemea moyoni,, "kwani mtu huyu ni nani?  mbona kapiga picha na marehemu mama yangu!!!?

    Zack akazichukua picha hizo akaziweka mfukoni mwake,kisha akazipiga hatua kurudi ndani ya gari lake,,

    baada ya dakika kadhaa kupita alionekana Shamy,, akitokea ndani ya jengo la hospitali akielekea sehemu ya kuegesha magari,,, akaliona gari la Zack,, akalifuata na kumkabidhi ile bahasha. kisha Zack Ada ndoka zake..



    Siku zilizidi kusonga hatimae,, Shirima akaamua aende kwa mganga ili amuangamize,  Zack....

    Shirima akaenda kwa mganga,, ni yule mganga Manyenye..... alipofika akaeleza shida yake,, Manyenye akasema,, "chukua hiki kisu,, andika hapo chini jina lako kamili,,pamoja na ubini wako.. kisha andika jina la huyo adui yako.

    Shirima akafanya kama alivyoagizwa na mganga Manyenye...alipomaliza,,  akaonekana Manyenye akinyanyuka na kunyunyizia dawa kwenye majina ya Shirima pamoja na ubini wake,, kisha akanyunyizia dawa kwenye jina la adui wa Shirima ambaye ni Zack.

    Manyenye akashtuka na kusema!  mbona umefikia maamuzi magumu kiasi hiki?? ni kweli umekusudia kufanya jambo hili? Shirima akasema,, "ndio nimekusudia, haka kakijana kashenzi sana kanasababisha mimi nisipendwe na mwanamke ninayempenda.. kwa sababu ni wapenzi,, na wanampango wa kuoana...

    Manyenye akasema,, "inamaana unataka kumchukuwa mchumba wa mwanao?

    Macho yakamtoka Shirima akauliza kwa mshangao,, "mwanangu kivipi?

    Manyenye akasema,, "hilo jina la adui yako uliloliandika hapo chini,,, linaonyesha linashahabiana na uzawa wa damu yako.. ndio maana nikakuuliza kuwa umekusudia kufanya jambo hili!!!!"





    Shirima akasema,, "akasema ndio nimekusudia...

    Manyenye akamtazama Shirima kwa macho ya mshangao, kisha akasema,, "simama kisha sogelea hiyo meza,, Shirima akafanya kama alivyoagizwa na mganga Manyenye.

    alipoikaribia meza hiyo,, likajitokeza boga la kimiujiza! pale juu ya meza. shirima akaingiwa na hofu,, tangu azaliwe hajawahi kuona muujiza wa namna hiyo...

    Mganga Manyenye akasema,, "chukua hicho kosu kilichopo kando ya boga hilo kisha dunga kwa kuvu boga hilo kwa kutumia hicho kisu... baada ya kufanya hivyo tayari utakuwa umemuuwa adui yako!

    Shirima akanyanyua kisu hicho huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu! jasho lilimtoka Shirima huku mwili wake ukitetemeka!

    kabla hajanyanyua kisu hicho,, ukasikika mngurumo mkubwa kupita kiasi,, mngurumo huo uliambatana na upepo mkali uliovuma kwa kasi.. Mganga Manyenye akaanza kuhisi harufu ya hatari,, pia Shirima akaogopa akakitupa kile kisu chini...

    Manyenye akachukua kibuyu kimoja chenye rangi nyekundu,,akamkabdhi Shirima kisha akasema,, shikilia kibuyu hicho ni kinga ya kukulinda wewe,,, muda si mrefu kunavita kali itatokea hapa,, bila kufanya hivyo hauwezi kutoka ndani ya nyumba hii ukiwa hai, Shirima hakutaka haga kugusa kibuyu hicho akatimua mbio akatoka ndani ya nyumba hiyo iliyoezekwa kwa nyasi kavu,, yenye vyumba mia moja(100) ndani yake.. lakini ukiitazama upande wa nje inaonekana ni ndogo kupita kiasi...akatimua mbio hakutaka kabisa kushuhudia vita aliyoambiwa kuwa itatokea muda mchache ujao... kumbe mganga Manyenye aliwahi kumuuwa mtu,, kichawi! mtu huyo alikuwa katolea kwenye ukoo wenye mizimu mikali,,hivyo mizimu hiyo ilikuja kulipiza kisasi kwa kumuangamiza mganga Manyenye,, ukawa ndio mwisho wa mganga huyo.

    hivyo ikawa pona pona ya uhai wa Zack,, inamaana Shirima angekidunga kisu kile kwenye lile boga basi Zack angekufa sekunde hiyohiyo..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shirima alionekana akitimua mbio na kuingia ndani ya gari lake akaliondoa kwa mwendo wa kasi ya ajabu,, akatoka kabisa eneo hilo,, akaelekea nyumbani kwake.

    alipofika aka akaliegesha gari lake kisha akaingia ndani ya nyumba yake... akapitiliza moja kwa moja chumbani kwake,, akajilaza kitandani...

    baada ya sekunde kadhaa akanyanyuka na kulifungua lile begi lake dogo analoweka vitu vyake vya muhimu... akatoa picha nyingi za mama Zack,, akaanza kuzitazama.....



    *************************************

    Wakati huo huo alionekana Zack akiingia ndani ya nyumba anayoishi yeye na mchumba wake Shamy! akaketi kitandani huku akiwa na mawazo mazito... alijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu,,, akanyanyuka na kuzichukua zile picha alizoziokota kando ya gari la Shirima,, akazitazama picha hizo kwa dakika nyingi sana..

    punde si punde ukasikika mngurumo wa gari likiegeshwa nje ya nyumba,, kumbe ni Shamy ndiye aliyeliegesha gari hilo, akashuka na kuzipiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. akapitiliza na kuingia chumbani.. akamkuta Zack akiwa kashikilia picha mbili,,, Shamy akamsogelea Zack kisha akamsalimia,, "habari yako kipenzi changu.

    Zack hakujibu salamu ya Shamy! alibaki kimya,,, hata kipindi Shamy anaingia chumbani Zack hakumuona kutokana na mqwazo mazito kuhusu hizo picha alizokuwa akizitazama!

    Shamy akachukua picha moja kutoka mikononi mwa Zack.. alipoitazama akashtuka,, akasema picha ya Shirima umeipata wapi?

    Zack hakujibu kitu chochote!!. Shamy akauliza tena,, "nakuiza mpenzi!

    Zack akashtuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo akastaajabu kumuona Shamy! kisha akamuuliza,, "umefika hapa muda gani?

    Shamy hakujibu swali la Zack.

    Shamy akasema,, "nimekuuliza hii picha ya Shirima umeitoa wapi?

    Zack akasema nimeziokota kule kwenye hospitali unayofanyia kazi,, kando ya gari la Shirima,, wakati anashuka kutoka ndani ya gari picha hizi zilidondoka.. nikaziokota.. lakini cha kushangaza nilipozitazama,, nikamuona marehemu mama yangu kwenye picha hizo!

    Shamy akashtuka,, akakumbuka,, kuwa kuna siku Shirima alimwambia kuwa,, alizaa na mke wa bosi wake!

    bosi wake alipogundua kuwa ameshirikiana kimwili na mkewe,, ndipo Shirima akahama mji ili kulinda usalama wa uhai wake!

    pia alisema hakuwahi kumuona mtoto huyo,, wala hajui mama wa mtoto huyo kama yupo hai au kafa!

    Shamy akahisi kuchanganyikiwa,, akasema,, "inamaana wewe ni mtoto wa Shirima!!!?

    Zack akashtuka kusikia hivyo akauliza,, "kwa nini umesema hivyo?

    ndipo Shamy akaanza kusimulia kile alichokisema Shirima,,

    Shamy aliendelea kusimulia kisha akauliza,, "huyu mwanamke kwenye picha ni mama yako?

    Zack akajibu,,"ndiyo ni mama yangu!

    Shamy akasema,, "shirima ni baab yako wa damu... inamaana yule baba yako uliyeniambia alimtelekeza mama yako kipindi anamimba changa.. ndiyo huyu Shirima?

    Zack akajibu hapana sio huyu,, yani hapa nahisi kuchanganyikia nashindwa kufahamu ukweli ni upi? naomba mimi na wewe tuongozane unipeleke nyumbani kwa Shirima nikajaribu kumdadisi ili nijue ukweli, baba yangu wa damu ni yupi?

    Shamy akasikitika sana akamtazama Zack kwa macho ya huruma! kisha akasema,, "sawa hakuna shaka,, twende sasahivi...

    bila kuchelewa,, wakaondoka muda huo huo,,na safari ya kuelekea nyumbani kwa Shirima ikaanza.



    ****************************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo huo kule nyumbani kwa Shirima,,alionekana bado akiwa amejilaza kitandani huku,, akitafakari nini cha kufanya,, ghafla akakumbuka maneno ya mganga Manyenye,, alimwambia kuwa adui yake ambaye anataka kumuangamiza kwa kuondoa uhai wake.. ni uzawa wa damu yake!! wazo likamjia akashtuka,,macho yakamtoka,, akaongea kwa sauti ya chini chini,, "mbona sielewi? yawezekana mtoto wangu ninayemtafuta miaka yote hiyo, ndio huyo Zack.

    mbona hii ni kasheshe!!! Shirima akaanza kujihisi kushindwa kupata hewa kutokana na mshtuko wa moyo! akizipiga hatua za haraka akaelekea sebuleni!! hali yake ikazidi kuwa mbaya zaidi akahisi kuishiwa nguvu,,akajitahidi kuufuata mlango ili atoke nje ya nyumba angalau apate hewa,, alipoukaribia mlango akadondoka chini akatulia tuli.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog