Simulizi : Chozi La Ukombozi
Sehemu Ya Nne (4)
mazy alizipiga hatua za harakaharaka kurudi ndani ya jumbamba la kifalme.....kisha akaitisha kikao.....na kusema lazima tuivamie Ghemi na tutaangamiza kila kitacho onekana hai....kisha mazy akaelekea kule gerezani alipokuwa amefungiwa mfalme wa Ghemi.....kwenye chumba kilichokuwa kimejaa maji yanayofika shingoni....alafu mlango ulikuwa juu....mfalme alibaki kasimama wima tangu siku aliyowekwa kwenye chumba hicho kwa sababu kilikuwa kimejaa maji....kutokana na baridi pamoja na wadudu waliokuwemo ndani ya maji hayo....hali ya mfalme ilianza kuwa mbaya.......punde mazy aliamuru mlinzi afungue mlango ili aweze kuongea na mfalme...."" wewe ni baba yangu na utabaki kuwa baba yangu..lakini sitokuacha hai kama hautaachia madalaka ya ufalme na kuyakabidhi mikononi mwangu.....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
kule ghemi alionekana komba akimtibu baba yake kwa dawa za kienyeji.....alichukua unga wa kijani na kuuweka kwenye maji ya moto kisha akachukua uji wa unga ule na kuuweka kwenye jelaha la baba yake... kisha akafunga kitambaa juu ya jelaha hilo.....baada ya kumaliza kifunga kitambaa hicho punde Prince mody alianza kupata nafuu akapata nguvu za kunyanyuka kitandani......alipogeuza shingo alitabasamu baada ya kumuona mwanae komba....pia komba alimtazama baba yake kisha akatabasamu ......akazipiga hatua akatoka upande wa nje......akapanda farasi wake....na kutoka nje ya lango la falme ya ghemi.....ramuh alimuita komba lakini komba hakugeuka... alitoka nje na kutokomea kusikojulikana....ramuh hakuwa na namna kwa sababu komba alikuwa tayari ameshaondoka....
**********************
upande mwingine alionekana komba akiwa juu ya farasi wake kuelekea Beha ili akamuokoe mfalme pamoja na Rubi...komba alipokaribia Beha....alishuka kwenye farasi wake kisha akamfunga katika mti. mbali kidogo na jengo la kifalme.....komba aliamua kutembea kwa miguu kuelekea kwenye falme ya beha...aliamua kufanya hivyo..aliamini kuwa wanajeshi wa beha wakimuona farasi yule itawafanya wamini kuwa komba hayupo mbali....hivyo hawatakuwa na wazo kama komba ameingia kinyemela kwenye falme ya beha....komba alizipiga hatua akaingia ndani ya jumba la kifalme kwa njia za kinyemela....alichinja mlinzi mmoja baada ya mwingine....alizipiga hatua mpaka ndani kabisa.....akiwa anatembea huku macho yake yakitazama kwa tahadhali kubwa....ghafla alisikia mtu anakohoa....komba alistuka kwa sababu mfalme wa Ghemi ndio huwa anakohoa hivyo!!!! komba akaamua kuelekea kule aliposikia sauti hiyo aliweza kuuwona mlango wa gereza alilofungiwa mfalme......komba aliunja kufuli na kufungua mlango ili amtoe mfalme.....
alijitahidi kumvuta mfalme hatimae akamtoa kunako gereza hilo la mateso......komba akamkokota mfalme mpaka kwenye chemba za kusafirisha maji machafu kuelekea baharini.....walitoka mpaka upande wa nje.....kisha komba akamficha mfalme....sehemu salama....
kisha akarudi upande wa ndani ya falme ya Beha..
aliingia ndani kabisa akaanza kumtafuta rubi....alifanikiwa kumpata rubi lakini alimkuta akiwa na hoi taabani...komba alimfungulia kamba zilizokuwa zimefungwa mikononi na miguuni..akambeba na umtoa nje kwa kupitia chemba ile ya maji machafu....
kisha akaandika ukutani kwa kutumia mshale...
maandishi yale yalisomeka hiviCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
(NITARUDI TENA KWA MARA NYINGINE)
kisha akatoka nje akamchukua mfalme pamoja na rubi""akawakokota mpaka kule alipokuwa amemfunga farasi wake.
akampandisha mfalme pamoja na rubi juu ya farasi akamwambia mfalme atangulie Ghemi......kisha komba akarudi mpaka upande wa ndani. akaiba farasi mmoja kisha akaondoka na farasi huyo kwa kupitia katikati ya lango la falme ya beha walinzi hawakuweza kumstukia komba waliamini ni mmoja kati ya wanajeshi wa beha..walinzi walifungua mlango komba akatoka na kutokomea......
Komba alionekana akimuongoza farasi kuelekea Ghemi........kwa mbali walinzi wa falme ya gemi waliweza kumuona mfalme akiwa kwenye farasi... waliweza kumuona kwa sababu ghemi ilikuwa juu ya kilima....ilipigwa mbiu (taarifa ya dharura) mbiu hiyo ilipigwa kwa kutumia tarumbeta kubwa lililotoa mlio mkubwa sana....tarumbeta lile lilikuwa maalumu hivyo watu na jeshi la ghemi lilikaa tayari kwa chochote kitakachotokea.....walinzi walifungua lango kuu punde mfalme alifika na kuingia ndani....kisha lango lile likafungwa kabla komba hajafika....
**********************
ule upande mwingine alionekana mazy akiendelea kutazama jeshi lake likifanya mazoezi...ghafla kunamlinzi mmoja alionekana akikimbia kuelekea ule upande aliokuwa amesimama mazy kisha akasema"" mtukufu mfalme...wale mateka wametoroka" Mazy alistuka kisha akazipiga hatua za harakaharaka kuelekea kule alipokuwa amemfungia mfalme.....alipofika alistahajabu kukuta mlango upo wazi alafu mflame hakuwepo...
mazy alichanganyikiwa..kisha akazipiga hatua kuelekea alipokuwa amefungwa rubi pia hakuwepo....mazy aliamua kutoka na kuelekea upande wa nje....akiwa kwenye kordo alistahajabu kuona maneno yameandikwa kwenye ukuta!!!! alipoyasoma yale maneno yalikuwa yameandikwa
NITARUDI KWA MARA NYINGINE"
mazy alichanganyikiwa"""bila shaka huyu ni komba!!!huyu mwanaharamu kawezaje kuingia humu???mazy alikasirika akachomoa upanga na kumchinja mmoja wa walinzi wake...kisha akafoka sana...mnakuwa wazembe kiasi hiki!! adui anaingia na kutoka utadhani nyumbani kwake!!! kisha akamfuata mlinzi mwingine akamchinja...wale walinzi wengine walitimua mbio baada ya kuona hivyo....
kisha mazy akatoka nje na kuitisha kikao cha dharura...
*************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ule upande mwingine alionekana komba kakaribia kabisa ghemi alipofika alifunguliwa mlango na kuingia upande wa ndani....hakutaka kuongea na mtu yeyote alishuka kwenye farasi akazipiga hatua za harakaharaka nusu akimbie...akingia ndani mpaka kwa mfalme....alipofika mfalme alifurahi sana kumuona komba....akamsgukuru na kumpongeza komba....
************
wakati huohuo mazy alikuwa akiongea na jeshi lake kuhusu mpango na mikakati ya kuivamia ghemi......kisha akasema""ndani ya mwezi huu lazima tuivamie ghemi nakuimiliki...
wanajeshi wake waliitikia kwa pamoja "NDIO MTUKUFU MFALME...kisha mazy akazipiga hatua na kurudi ndani....
*************
palipokucha mfalme wa ghemi alitisha kikao na kusema ""yatupasa tuwe na jeshi imara hivyo inabidi mfanye mazoezi kwa hali na mali ili nipate jeshi shupavu na lenye nguvu....kisha akamuita komba na kumwambia hakikisha unalinda Taifa lako nakuamini....Komba alifurahi sana kusikia maneno ya mfalme...
siku zilisonga...siku moja komba akiwa katika matembezi alimuona mtu ambae aliwahi kumuona sehemu...alipojaribu kukumbuka aliweza kumtambua mtu yule...akaanza mumfatilia kwa nyuma...yule mtu alistuka akahisi kunamtu anamfatilia...alipogeuka alimuona komba....mtu yule alianza kutimua mbio komba alimkimbiza lakini yule mtu alipanda farasi na kutokomea kusikojulikana...kumbe mtu huyo ni mmoja kati ya wanajeshi waliovamia na kuangamiza wakazi wa kisiwa Dhaho alipozaliwa komba miaka 25 iliyopita
komba alijawa na jazba alitamani arudi kwenye ngome ya kifalme akachukue farasi wake lakini alikuwa ameshachelewa....ile anageuka mara ghafla.
mara ghafla kwa mbali aliona mtu akimtazama kisha akajifunika kininja upande wa usoni...mtu yule alianza kuzioiga hatua za uwoga wa hali ya juu... kitendo hicho kilimfanya komba amtilie mashaka akaamua kumfatilia kwa nyuma...wakati komba akizipiga hatua ghafla alimparamia mtu aliyekuwa kabeba mfuko uliojaa matunda mfuko ule ulidindoka....komba alipogeuza shingo yake ili amuombe radhi ghafla...yule mtu aliyejifunika kininja sehemu ya usoni hakuonekana tena kutokana enei lile palikuwa na watu wengi sana....
komba aliangaza angaza macho huku na kule lakini hakumuina mtu huyo.....alikata tamaa na kurudi kwenye ngome ya falme ya ghemi....alipofika....aliitwa na mfalme...kisha mfalme akasema"" naomba unisamehe mjukuu wangu kwa kosa kubwa nililofanya miaka mingi iliyopita...niliamuru mama yako atoswe baharini...nisamehe sana nakusihi.....kauli ile ya mfalme ilimfanya komba awe mnyonge alimkumbuka mama yake...komba hakuongea kitu...kwa sababu aliamini mama yake baada ya kutoswa baharini aliokolewa....
pia waliomuuwa mama yake ni jeshi la falme ya Beha..na aliyempiga mshale mama yake ni Mazy amba ni baba yake mkubwa....
alimsogelea mfalme akaina ishara ya kutoa heshima kwa mfalme....mfalme alifurahi sana hakutegemea kama komba angemsamehe....kisha akasema "nifuate......
komba alimfuata mfalme kwa nyuma...waliingia kwenye chumba....... chumba hicho kilikuwa na nyaraka pamoja na ramani ya Ghemi...na hati za siri......mfalme aliaamua kumuonesha kila kitu komba....
mfalme hakuwahi kumuonesha mtu yeyote hata watoto wake....Mazy pamoja na Prince mody...hakuna mtu aliyewahi kuingia ndani ya chumba hicho isipokuwa mfalme pekee......kisha mfalme akafungua kabati lililokuwa kwenye ukuta...alitoa upanga.....uoanga huo ulikuwa wa miujiza....ulikuwa na nguvu na maajabu......kisha akamkabidhi komba uoanga ule.........
kulewa uoanga huo ni ishara kwamba ipo siku ambayo haijulikani...utakuwa mfalme......alimchukua komba na kumpeleka upande mwingine......kulikuwa na chungu...ndani ya chungu hicho kulikuwa na maji....kisha mfalme akasema"" maji haya ni ufunguo...na mlango upo baharini katikati ya mpaka wa GHEMI na BEHA..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
maji haya ukiyamwaga kwenye mpaka huo mlango utafunguka na huko ndani kuna MZIMU mzimu huo ulifungiwa humo ndani miaka elfu moja iliyo pita na falme ya BEHA....na ili kuufufua MZIMU huo ni lazima kipatikane chungu cha pili kilichokuwa na damu...chungu hicho chenye damu kilichukuliwa na marehemu mfalme wa beha..... alikihifadhi kwenye chemba ya siri ambayo hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa akifahamu chungu hicho kilipo.....
kumbe vita kati ya BEHA na GHEMI ilitokea mara kwa mara kumbe chanzo ni kugombania mpaka..na siri ya mpaka huo walikuwa wanajua wafalme pekee.......kila falme ilitaka huo mzimu uwe upande wake....na ili kuufufua mzimu huo ni lazima uwe na vyungu vyote viwili...chugu cha damu pamoja na chungu cha yale maji maalumu....
mfalme wa Ghemi aliamua kutoboa siri hiyo na kumwambia komba pekee..kwa sababu aliamini kuwa komba ndiye mkombozi pekee..
***************
sikumoja mazy alkagua kwenye chemba zote za falme ya Beha....mazy aliona kunachungu kimehifadhiwa alipokitoa aliona kuna damu ndani yake...pia pembeni kulikuw na karatasi....akaichukua na kuisoma.....karatasi ile ilikuwa na maelekezo kuhusu kuufufua MZIMU uliofungiwa kwenye mpaka wa Gjemi na Beha uliopita baharini.. ...mazy alistahajabu sana akawa na shauku ya kutaka kuufufua mzimu huo ili autumie kuiangamiza Ghemi... alipogeuza karatasi hiyo upande wa nyuma alistuka baada ya kuona maandishi yaliyosomeka hivi""ili kuufifua mzimu huo inabidi viwepo vyungu vyote viwili...chungu chenye damu....na chungu chenye maji....
chungu chenye maji kipo falme ya Ghemi...
mazy alipagawa akaacha kuendelea kukagua akaingia kwenye chimba chenye siri za falme ya Beha ili aone kama atapata historia ya Mzimu huo...alianza kukagua nyaraka moja baada ya nyingine.....aliona kitabu kimoja akakichukua...alipokisoma kitabu hicho uso wake na macho yake yalionekana kutazama kwa mshangao......kabla hajamaliza kusoma historia hiyo mara ghafla.. alisikia kama watu wakipigana huko upande wa nje....lakini hakujali aliendelea kusoma historia ile inayoelezea huo mzimu uliofungiwa.......alistuka baada ya kusikia mgomvi ukiendelea tena sasahivi zilisikia sauti za mapanga yakigongana...aliamua kuacha kusoma kitabu kile akatoka upanda wa nje..alistahajabu kuona wamevamiwa .....mazy alichanganyikiwa. akakimbilia upande wa ndani kabla haja fika ndani aligeuza sgingo yake alistahajabu sana....kuona wanajeshi wake wakiuwawa na kuchinjwa kama kuku...wakati anatahamaki mara ghafla alimuona komba aliingia huku akiwa juu ya farasi....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mazy alipagawa macho yalimtoka kisha akapaza sauti...mzuieni huyo mtu ni hatari.....kila mwanajesgi aliyejaribu kumzuia komba alichinjwa bila huruma.....mazy alikimbia mpaka upande wa ndani akaingia kwenye ile chemba akakichukua kile chungu kilichokuwa na damu...akatoka haraka akajifungia kwenye chumba cha siri kilichokuwa kinahifadhi nyaraka muhimu za falme ya Beha....
*************
upande wa nje vumbi lilitimka ilikuwa ni viya ya kufa na kupona....yani usipomuuwa adui uako basi anakuuwa wewe....mapigano yaliendelea....
kwa mbali alionekana komba akitoka juu ya farasi nakuanza kupambana na wanajeshi wa falme ya beha...wakati huo mazy alipoingia kwenye kile chumba ndani yake kulikuwa na mlango wa siri wa kutokezea nje kabisa ya ngome ya falme ya Beha
mazy alikichukua chungu kile chenye damu.. kisha alifungua mlango na kuingia ndani akapita njia za chini kwa chini ua aridhi....alitokezea nyuma ya jengo la kifalme akachukua farasi kisha akafungua mlango wa nyuma akatoka nje na kutokomea......lengo la mazy lilikuwa aende Ghemi akatafute kile chungu kingine kilichokuwa na maji ambayo ni ufunguo wa kufungulia mlango wa kimiujiza uliokuwa katikati ya mpaka wa Ghemi na Beha....mazy aliamua kufanya hivyo kwa sababu aliamini kule ghemi hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyebakia wote wapo vitani kwenye falme ya Beha..
*************
ule upande mwingine alionekana rubi akizipiga hatua za harakaharaka akielekea kule kwenye chumba cha siri cha falme ya ghemi...kumbe rubi alipandikizwa akili nyingine kwa njia ya kichawi na MCHAWI wa Beha aitwaeCHARO aliyekuwa akiisaidia beha kwa mambo yasiyokuwa ya halali...rubi hakutambua ni nini anakifanya......aliongozwa na akili za kichawi....punde aliingia mpaka kwenye kile chumba.....aliona chungu akazipiga hatua na kukichukua chungu kile kilichokuwa na maji ndani yake...
***************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huohuo alionekana akikaribia Falme ya ghemi.... punde alifika akamfunga farasi wake mbali kidogo...akatembea kwa miguu akaingia upande wa ndani kwa kupitia njia za siri.....alipoingia ndani aliuwa walinzi wachache waliokuwa wamebaki..kisha akaingia upande wa ndani...kabisa huku akiwa amesgikilia panga mbili..
***************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment