Search This Blog

TAMBIKO - 3

 







    Simulizi : Tambiko

    Sehemu Ya Tatu (3)







    Asubuhi palipokucha....mganga akasema ,,"waweza kwenda nyumbani itamkuta mwanao akiwa katika hali uake ya kwaida...Conso akanyanyuka na kuzipiga hatua kurudi nyumbani kwake...



    alipotoka nje ya eneo la mganga huyo....mganga akacheka kisha akajibadilisha na kurudi katika umbile lake...ni yule babu mchawi...akazipiga hatua kadhaa akabadilika kuwa pakaweusi akatoweka kimiujiza.. 

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************************



    baada ya masaa matatu kupita Conso alifika nyumbani kwake..akamkuta mumewe yupo myumbani anamsubiri...Shinje alipomuona mkewe akamuuliza kwa shauku ya kutaka kujua kilichojili kwa mganga..Conso akaona aibu kumwambia Shinje..akaamua kudanganya kwa kusema,,"nilikwenda kuchimba mizizi ya dawa na yule mganga..Shinje akasema ,,"pole sana mke wangu..sasa mganga kasemaje?

    Conso akajibu,,"amesema Maliwa atarudi katika hali yake ya kawaida..

    wakasikia mtu anagonga hodi kwenye geti  la nyumba yao...Conso akatoka nje akaenda kutazama ni nani anayegonga geti..alipofungua akamuona ye babu jirani yao..Conso akasema ,,"karibu

    Babu huyo akasema,,"nimekuja kuwajulia hali vipi mtoto wenu anaendeleaje?

    Comso akajibu ,,"mpaka sasa hatujamuona na hatujui ni wapi kaelekea...babu huyo akasikitika kinafki..wakati yeye anajua kila kitu,,yeye mdio chanzo cha matatizo hayo yote..pia yeye ndiye amemuingilia kimwili Conso...kwa kujibadilisha umbile na kujifanya yeye ni mganga!



    ********************



    Siku zilisonga,,lakini Conso na Shinje hawakumuona mtoto wao..wala kusikia tetesi zake!!..kitendo hicho kiliwanyima furaha...



    wakati huo huo alionekana Maliwa akitokomea kwenye milima na kwenda kujificha huko...kwa sababu kila binadamu aliekutana nae alitimua mbio kwa kudhani kuwa Maliwa ni jini..kutokana na muonekano wa kichwa chake kuonekana kama ndege anayefanana na kuku...Maliwa akaanza kuishi kwa shida na mates makubwa...kadri siku zilivyozidi kusonga...Maliwa akaanza kula matunda na vyakula vinavyopendwa na ndege!!



    siku silizidi kusonga hatimae miaka mingi ikapita..

    Maliwa akawa mwanaume mkubwa kupita kiasi..hakuna nguo iliyoweza kumtosha..mikono yake ikawa na misiri minene..pia miguu yake ikawa mirefu kuliko miguu ya binadamu wa kawaida...hata wanyama waliokuwa ndani ya pori linalopatikana kwenye milima aliyokimbilia Maliwa wakawa wanamuogopa..kila wakimuona wanatimua mbio...kadri miaka ilivyozidi kusonga ndivyo Maliwa alizidi kuwa kiumbe wa kutisha zaidi..Zikasikika tetesi kuwa ndani ya Milima ya RWENZOBE kuna kiumbe wa kutisha...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Taarifa hizo zilienea jiji zima watu wakaanza kuingiwa na hofu..

    Shinje na Conso pia wakaipata taarifa hiyo...Shinje akasema bila shaka huyu ni Maliwa,,Itabidi twende kijijini kwa mama tukamueleze jambo hili...Conso hakuwa na kipingamizi akakubali wazo la mumewe...



                        *************************



    Upande mwingine alionekana yule mzee mchawi.akiwa ndani ya nyumba yake..ni baada ya miaka mingi kupita sasavhivi ni mzee kikongwe!

    akiwa hajiwezi...

    mzimu wa mkewe ukajitokeza chumbani kwake..

    babu huyo kikongwe..akashtuka kumuona mkewe akiwa amejifunika sanda nyeupe huku uso wake ukionekana kuwa na rangi nyeupe kama kapakw unga! mzimu huo ukasema,,"hasira hasara,ulisababisha mauti yangu..lakini mimi pia sintokuacha ukiwa hai...babu huyo akajikongoja akafunua godoro la kwenye kitanda chake ili atoe irizi ambayo ni kinga yake...lakini akawa amechelewa! bmzimu wa mkewe ukamuangamiza kwa kumnyonga shingo yake mpaka akafa!

    kisha mzimu wa bibi huyo ukatoweka kimiujiza.



                       *************************



    Kule kwenye milima ya Rwenzobe,,alionekana Maliwa akiwa aketi juu ya mti mkubwa akitazama upande wa chini..ghafla mzimu wa yule bibi ukajitokeza!! Maliwa akashtuka akajirusha kutoka juu ya mti mpaka chini...akaanza kutimua mbio.

    kutokana na ukubwa wa mwili wake..hakuweza kukimbia kwa kasi kwa sababu miti ilimzonga kila pande...akaanza kung'oa mti huku anakimbia..alipogeuza shingo yake hakuweza kumuona tena yule bibi...



    Siku zilisonga hatimae safari ya Shinje na Conso ikawadia..wakapanda basi na kuelekea kijijini kwa mama yake Shinje!!

    safari ilikuwa ndefu sana,lakini walifika salama..

    mama Shinje akawapokea kwa furaha....kwa sababu ilikuwa niajira ya usiku akawaandalia sehemu ya kulala...Shinje akaona si vyema kumueleza mama yake jambo hilo kwa usiku huo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                        ************************



    Asubuhi palipokucha,Shinje akamueleza mama yake kuhusu Maliwa..Mama Shinje akashtuka akasema,,"bila shaka kunajambo baya linaloendelea si bure,kuna mkono wa mtu mbaya!

    lakini mbona hamkunifahamisha kwa kipindi cha miaka yote hiyo?

    Shinje na Conso wakatazamana nyuso zao..Comso akasema ,,"samahani mama tulihofia unaweza kupata mshtuko kwa taarifa hizi!! lakini leo imebidi tukujulishe.

    Mama Shinje akasema,,"itabidi lifanyike jambo la kimila...lakini ni mlolongo mrefu sana wenye mapito ya kutisha..

    Conso akaingiwa na hofu akauliza,,"mapito ya kutisha? mapito gani hayo?

    Shinje akadakia na kusema,,"punguza wasiwasi mke wangu tatizo lako wewe hauna subira!!!

    amini kila kitu kitakuwa sawa.



    Mama Shinje akasema,,"muongozane na mimi.

    Shinje na Conso wakanyanyuka kutoka kwenye mkeka wakamfuata mama Shinje....walitembea mpaka kwenyemsitu ambao unasadikika kuwa na mizimu yote ya kimila.....walipofika Mama Shinje akasema,,"mti ule ndio mti wa kufanya matambiko ya kueleza shida zetu..ili kupata ufumbuzi...mizimu hii si ya kudhuri watu bali ni imani ya mila zetu...lakini kunamasharti kabla ya kuukaribia mti huo...yawapasa muwe watulivu...msinyooshe mikono yenu kusonta kitu chochote mkionacho ndani ya msitu huu ni mwiko.

    wakaendelea kuzipiga hatua,,walipoukaribia mti huo..Mama shinje akainama ishara ya kutoa heshma kwa mizimu kisha akaanza kuelezea tatizo......

    Ukasikika mngurumo mkubwa pia ikasikika sauti ikiongea....binadamu wote si wema...kijana Maliwa amefungwa kichawi..lakini bado hamjachelewa..inahitajika kafala la mbuzi mweusi. achinje na dumu yake imwagwe hapa chini ya mti..kisha baba ma mama wa mtoto huyo wanatakiwa wakafanye mapenzi juu ya kaburi !!nyakati za usiku wa manane ...kwa ajili ya tambiko la kumrudisha kijana Maliwa kenye hali yake ya kawaida.

    masharti hayo ya mizimu yaliwashtua Shinje na Conso....lakini wakabaki katika hali ya utulivu kama walivyoambiwa na mama yao.



    **************************



    ilipofika majira ya usiku..Conso ma Mumewe wakazipiga hatua kuelekea makaburini...giza lilikuwa totoro...kutokana na mapori madogo madogo kijinini hapo....wanyama pori walikuwa wakirandaranda nyakati za usiku kutafuta mawindo!!

    wakati Conso na Shinje wakiwa njiani wakakutana na Fisi mkubwa kupita kiasi...Fisi huyo akaanza kuwafuata...Shinje akajaribu kumfukuza fisi huyo lakini akastaajabu fisi huyo hata hakutishika...wakaanza kuingiwa na wasi wasi...punde si punde Fisi wengine wanne wakaongezeka...ghafla wakazungukwa na kundk kubwa la Fisi.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Conso akaingiwa na hofu kubwa..na wasiwasi ukaongezeka!! akataka kutimua mbio..Shinje akamzuia.....Fisi wakaanza kusogea taratibu kuwafuata! Shinje akajikaza akaingiwa na ujasiri.akainama akapapasa chini akaokota mawe..na kurusha jiwe moja kubwa kiasi..likampiga Fisi mmoja akalia kwa sauti kali kutokana na maumivu aliyoyapata! akatimua mbio..lile kundi la fisi pia wakatua mbio baada ya kuona mmoja wao anakimbia huku akilia..sauti ile waliitambua kuwa mmoja wao kaumia...ndio maana wakatimua mbio!

    wakati huo Conso alikuwa kajificha nyuma ya mgongo wa Shinje!

    Conso akasema,,"Tuondoke turudi nyumbani!

    Shinje akasema,,"haiwezekani unakumbuka masharti ya mizimu?

    baada ya Shinje kuomgea kauli hiyo,Conso akakubali..lakini alikuwa na hofu kubwa kitokana na giza lililokuwa limetanda usiku huo!

    Wakazipiga hatua kuendelea na safari ya kuelekea makaburini..walitembea mwendo wa dakika kadhaa wakawa wamefika....walipoangaza angaza macho yao palionekana kutisha....zilisikika sauti za wadudu waliao usiku..pamoja na kelele za vyura!! Shinje akamshika Conso mkono...wakalifuata kaburi moja lililokuwa mwanzoni mwa eneo la makaburi! Shinje akaongea kwa saiti ya chini,,"tusipoteze muda ebu tufanye haraka..

    wakatConso alikuwa na hofu kubwa macho yake yaliangaza angaza kutazama huku na kule!

    akavua suruali yake harakaharaka...

    punde si punde...akajitokeza mfu aliyeonekana kuharibika mwili wake kwa kuliwa na wadudu aina ya funza...maiti hiyo ikazipiga hatua kuwafuata pale chini walipokuwa wamelala...



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog